Ruka hadi kwa yaliyomo
Printable page generated Jumapili, 1 Des 2024, 18:34
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Jumapili, 1 Des 2024, 18:34

Namba ya moduli 2: Utafiti wa Kihistoria

Sehemu ya 1: Utafiti wa historia ya familia

Swali Lengwa muhimu: Namna gani unaweza kupanga shughuli vikundi vidogo vidogo darasani kukuza ufanyaji kazi pamoja na kujenga kujiamini?

Maneno muhimu: familia: historia: kujiamini: utafiti: kundi dogo la kazi: majadiliano.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umepanga kazi zako kusaidia wanafunza kujielewa wenyewe na uhusiano wao na familia nyingine;
  • umetumia makundi madogo ya majadiliano kujenga kujiamini wanafunzi wakiwa wanatafiti historia za familia zao.

Utangulizi

Ufundishaji mzuri huanza kwa kuwahamasisha wanafunzi kutafiti mambo ambayo wanayafahamu.Kihistoria, hii ina maana kutumia maisha yao na ya familia zao kama chanzo cha utafiti. Ujuzi uliotumika kutafiti historia ya familia, unaweza kutumika kutafiti masuala mapana zaidi ya kihistoria.

Sisi wote tuna historia,iliyoanza mara baada ya kuzaliwa.Hii inajumuisha uzoefu wetu na watu wote tunaohusiana nao.

Katika sehemu hii,unaanza kutafiti hali za familia za wanafunzi wako, kazi na majukumu yao katika famlilia zao. Utaangalia pia kwa upana familia kubwazenye misingi ya kiukoo. Kadili unavyotafiti sehemu hii unatakiwa kuwa makini na uzoefu tofauti wa familia au miundo mingine ambayo wanafunzi wako wanaiishi.

Somo la 1

Uanapotafiti familia ni muhimu kujua kwanza uelewa wa wanafunzi juu ya maana familia na kuwaonesha mipangilio tofauti ya familia. Kujua utofauti huu kunawasaidia wanafunzi kujisikia vizuri wanapotambua namna ambavyo familia zinaweza kutofautiana. Uchunguzi kifani 1 na shunguli 1 tunangali njia mbali mbali za kufanya hili.

Katika Uchunguzi kifani,mwalimu huwahamasisha wanafunzi kufanya kazi katika makundi madogo (rejea nyenzo muhimu: Utumiaji wa kazi za makundi katika darasa lako) na kukumbuka sheria walizokubaliana kufuata kwenye majadiliano ya vikundi.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia kundi dogo kutafiti familia yangu.

Bwana Nguzo, mwalimu wa Maarifa ya Jamii katika shule ya msingi Muhimu Tanzania alitaka wanafunzi wake wa darasa la tatu kujifunza kuhusu familia na kazi za familia mbalimbali.

Aliunda makundi ya wanafunzi wasiozidi sita. Aliwaweka wanafunzi pamoja ambao sio kawaida yao kufanya kazi pamoja. 

Katika makundi wanafunzi walijibu maswali yafuatayo,ambayo ambayo mwalimu aliaandika ubaoni:

Jina lako nani?

Baba na mama yako ni nani? Taja majina yao

Babu na bibi yako ni nani? Taja majina yao

Una dada na kaka wangapi? Taja majina yao. Ni wakubwa au wadogo kuliko wewe?

Una binamu wangapi? Taja majina yao

Wakati wa majadiliano,Bwana Nguzo alikwenda kila kundi kuahakikisha kuwa wanafunzi wote walipewa nafasi ya kutoa mawazo. Baaada ya dakika

10 hadi 15,aliyataka makundi kushirikishana na darasa nini wametafiti kuhusu familia mbalimbali. Nini mfanano kati ya familia hizo? Nini totauti?(kwa wanafunzi wadogo au wasiojiamini huwauliza maswali zaidi, mfano: Nani alikuwa na kaka wengi?)

Pia aliyataka makundi kuzingatia swali hili.

Nini kinamfanya mtu awe dada ,kaka shangazi yako,n.k?

Baada ya dakika 10,mwanafunzi mmoja kutoka kila kundi huwasilisha majibu ya maswali la 6 darasani. Nguzo huandaa jedwali kubwa la mahusiano kusaidia kuongoza mjadala (Angalia Nyenzo rejea 1 jedwali la uhusiano )

Bwana Nguzo na wanafunzi wanajua kuwa ingawa kuna maneno katika lugha zao yanayoelezea kuhusu binamu, baba mdogo/mkubwa na mama mdogo/mkubwa, mahusiano haya kwa kawaida hujulikana kama, kaka au dada, baba na mama. Kunautofauti kati ya kaka wa baba na kaka wa mama pia dada wa mama na dada wa baba. Mfano: Kaka wa mama ni mjomba lakini kaka wa baba ni baba mdogo/mkubwa; dada wa baba ni Shangazi lakini dada wa mama ni mama mdogo/mkubwa. Mwalimu Nguzo anagundua kwamba kufundisha wanafunzi kuhusu uhusiano wa kifamilia unaweza kuwachanganya wanafunzi wadogo.

Shughuli ya 1: Mimi ni nani?

Kabla ya kipindi, andaa jedwali la mahusiano (angalia Nyenzo rejea 1 )

Watake wanafunzi kufanya kazi katika makundi ya watatu au wane. Mwanafunzi mmoja ajitolee kuorodhesha watu wote anaowafahamu katika familia yake na kujaza habari zao kwenye jedwali la mahusiano (unaweza kumchagua mwanafunzi wewe mwenyewe)

Wanafunzi wanaweza kuhitaji kuchora picha za ndugu zao kwenye jedwali

Shirikishana majedwali haya na darasa lote

Jadili utofauti katika familia na sisitiza jinsi utofauti huo ulivyo mzuri

Mwishoni mwa kipindi, onesha jedwali la uhusiano kwenye ukuta wa darasa

Somo la 2

Tunapo jifunza mambo ya kale, ni muhimu kusaidia wanafunzi kuelewa kupita kwa wakati na jinsi vitu vinavyobadilika kutoka kizazi hadi kizazi.

Kubuni njia ambazo wanafunzi wanazitumia kujifunza historia za familia zao kunawasaidia kuhusianisha matukio pamoja na kuyaweka kwenye mtiririko mzuri. Nyenzo rejea 2: jedwali jingine la uhusiano linaonesha ukoo ambao utawasaidia wanafunzi kuona uhusiano kati ya wanafamilia mfano binamu yao ni mtoto wa dada au kaka wa mama au baba yao,

Uchunguzi kifani ya 2: Historia za familia

Juma Bhalo anapanga kufundisha wanafunzi wa darasa la tano kuhusu uhusiano wa kifamilia kwa kipindi fulani

Anakakata vipande kadhaa vya picha kutoka kwenye magazeti ya watu wa nyakati tofauti, wakifanya shughuli tofaut,:i mfano harusi, siku ya bonanza la shule, na kuandika namba nyuma ya kila picha. Aliwaambia wanafunzi wake kuwa picha zinawakilisha matukio tofauti kwa maisha ya mtu mmoja na kuwataka wanafunzi katika makundi ya watu sita kupanga picha kulingana na umri wake. Anawapa dakikia 15 kujadili mpangilio wao.

Halafu anawataka kila kundi kutoa mrejesho. Anawataka kueleza kwa nini walichagua mpangilio fulani na kuandika dondoo za picha zilizo wasaidia kupanga matukio. Wanajadiliana matukio muhimu yaliyoonyeshwa kwenye picha na Mwalimu Juma anawaambia wametengeneza kalenda ya matukio ya maisha.

Shughuli ya 2: Wanafunzi watengeneze kalenda zao za matukio

Nyenzo rejea 3: Kalenda yangu inaweza kuwa mwanzo kwa darasa kutengeneza kalenda yao ya matukio.

Kwanza, jadili umuhimu wa kujijua asili yako na wanafamilia wengine

Elezea maana ya kalenda ya matukio

Onyesha mfano kwa kutengeneza kalenda ya matukio yako mwenyewe (sio lazima utumie maisha yako halisi-unaweza ukatumia uhalisia wa maisha ya mtu fulani unaye mfahamu). Kuonyesha mfano ni njia muafaka ya kuwasaidia wanafunzi

kujifunza ujuzi mpya. Chora kalenda hii ubaoni waone na zungumzia nini unafanya au uwe umeiandaa kwenye karatasi kubwa. Kumbuka kutumia vipimo sahihi- mwaka uwakilishe na umbali fulani. (wanafunzi wako wanapotengeneza kalenda zao, watumie sentimeta za mraba 5 au umbali wa mkono kama hawana rula.

Watake wanafunzi kuandika vitu muhimu wanavyokummbuka kuhusu maisha yao. Pia wape muda wa kuwauliza wazazi/walezi kuhusu walipotembea kwa mara ya kwanza n.k.

Watake kunakiri taarifa yoyote wanayohitaji kuiweka katika kalenda ya matukio

Wasaidie wakati wanatengeneza kalenda zao. Unaweza kuwahamasisha kuandika matukio makubwa ambayo yamewatokea, na katika rangi tofauti.( au katika mabano chini ya mstari) matukio makubwa ambayo yalitokea katika familia zao( mfano dada mkubwa kwenda chuo, baba kununua shamba n.k)

Onyesha kalenda zao darasani

Wanafunzi wanaomaliza mapema wanaweza kuombwa kufikiri na kuchora kalenda ya muda ujao. Nini yatakuwa matukio makubwa wakati wana umri wa miaka 20,25,40 n.k?

Somo la 3

Kusaidia wanafunzi kukuza ufahamu wao wa mambo ya zamani na sasa kunachukua muda, na inahusisha kuwapa kazi mbalimbali ambapo wanatakiwa kuona, kuuliza maswali na kufanya maamuzi kuhusu kile wanacho chunguza.

Wanawezaje kukuza ujuzi kuwasaidia kufikiri kuhusu namna vitu vinavyobadilika kulingana na muda? Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu unatumia mazingira ya kawaida kupanua ufahamu wa wanafunzi wako kuhusu muda unaopita na vitu vinavyobadilika.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutembelea mzee wa mahali

Mbwana Kato, Bibi Sime na Dada Benda waliandaa pamoja mafunzo ya jamii. Hawakufundisha wote mada moja kwa wakati mmoja, lakini iliwasaidia kushirikishana mawazo.

Wote walisoma Nyenzo muhimu: matumizi ya mazingira ya jamii/ mahali kama nyenzo. Walipanga kwenda pamoja na wanafunzi kutembelea wazee katika jamii kuongea nao kuhusu namna kijiji kilivyobadilika tangu walipokuwa watoto. Waliamua kugawa darasa katika makundi na kila kundi lingeandaa maswali ya kumuuliza mzee. Kila kundi lingeuliza maswali kwenye eneo tofauti kama michezo waliyocheza, chakula walicho kula,nyumba walizoishi n.k.

Shughuli muhimu: Matumizi ya vyanzo mbalimbali kuchunguza maisha ya zamani

Wape wanafunzi nafasi ya kutoa mawazo yao. Watake kufikiria jinsi wanavyoweza kuchunguza namna maisha yalivyobadilika katika familia zao, kijijini au katika jamii kwa kipindi fulani. Wangetumia nyenzo gani kuchunguza hilo?

Wanaweza kuwa na mawazo kama: kutumia uchunguzi na kumbukumbu zao kufikiri kuhusu nini kimebadilika katika maisha yao; kuuliza wazazi wao; kuzungumza na wazee wengine; kuongea na watu wenye mamlaka ( kama wafalme); kuangalia ramani za zamani; kutumia makumbusho (kama yapo); kusoma vitabu vinavyohusu eneo husika n.k.

Watake wanafunzi kukusanya hadithi kutoka kwenye familia zao kuhusu namna maisha yalivyobadilika kwa vizazi vichache vilivyopita, namna maisha ya kila siku yalivyokuwa. Zipi ni hadithi za zamani za familia zao? Je familia inachapisho lolote? Picha, barua.n.k zinazovyoonesha maisha yalikuwaje?

Wanafunzi washirikishane hadithi zao kwa kila mmoja darasani na tumia hadithi zao kama msingi wa mawasilisho –hii itajumuisha picha zinazoonyesha maisha yalivvokuwa,kazi zilizofanyika kwa maisha ya zamani maandishi yanayohusu hadithi za familia na nyaraka nyingine.na hadithi za kufikirika mfano: elezea siku moja katika maisha ya bibi yako wakati akiwa kijana.

Nyenzo-rejea ya 1: Jedwali la mahusiano/ukoo

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Jedwali la ukoo linaonyesha kila mtu anavyohusiana na wengine na wanafamilia au jamii. Tamaduni tofauti zina namna tofauti za kuelezea uhusiano wao.

Lifuatalo ni jedwali la mahusiano ya ukoo kwa Tanzania.

Nyenzo-rejea 2: Jedwali jingine la ukoo

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Nyenzo-rejea 3: Kalenda ya matukio yangu

Nyenzo za mwalimu kwa kuandaa au kubadili kwa matumizi ya wanafunzi

Sehemu ya 2: Kutafiti namna tulivyoishi zamani

Swali Lengwa muhimu: Je, namna gani unaweza kukuza ujuzi wa kufikiri katika historia kwa wanafunzi?

Maneno muhimu: ushahidi: historia: ujuzi wa kufikiri: mahojiano: maswali,:uchunguzi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umetumia mapokeo na nyaraka,kukuza ujuzi wa kufikiri wa wanafunzi wako katika historia;
  • Umepanga na kufanya shughuli zinazo saidia wanafunzi kukusanya na kutumia ushahidi wa mapokeo kutafiti kuhusu matukio ya yaliyopita..

Utangulizi

Tunaposoma historia kama sehemu ya mafunzo ya jamii, tunaweka msisitizo katika vyanzo vya ushahidi vinavyoweza kutufundisha mambo ya kale.

Kuna njia kuu mbili za kupata ushahidi wa kale-kutafuta na kuchanganua nyaraka ambazo huweka kumbukumbu ya kile kilichotokea na kutumia mapokeo. Mapokeo ni makusanyo ya hadithi za watu kuhusu tukio fulani.

Katika sehemu hii, utahamasisha wanafunzi wako kutafiti nyaraka na kufanya mahojiano kwa lengo la kujenga uelewa wa kule walikotoka. Ni muhimu kuhamasisha wanafunzi kuuliza maswali na kusikiliza mawazo ya wenzao; hivyo wanakuza ujuzi katika kupembua ushahidi na kupata picha halisi.

Somo la 1

Kufundisha historia sio tu kunahusisha ukweli juu ya matukio ya kihistoria bali pia maendeleo ya ujuzi wa wanafunzi katika nyanja ya historia. Kama mwalimu, unatakiwa kuwapa wanafunzi wako nafasi ya kukuza na kufanyia mazoezi ujuzi huu. Aina ya matukio unayotafiti na wanafunzi wako yatategemea umri wao. Kwa watoto wadogo, utatoa mwongozo zaidi katika kuwasaidia kutafuta na kuelewa nini kilitokea.

Katika sehemu hii, wanafunzi watafanya mahojiano pamoja na waliowazidi umri katika familia zao au yeyote katika jamii. Lengo la mahojiano ni kutafuta namna wanavyotofautiana kimaisha, ukilinganisha na watu wa kale. Kwa kuwaonyesha wanafunzi namna ya kufanya mahojiano, unaweza saidia kukuza ujuzi muhimu-kuwa tayari kuona thamani ya historia simulizi na kuwa tayari kusikiliza. ( Rejea nyenzo 1: Historia simulizi ; kufahamu zaidi juu ya nyenzo hii muhimu)

Uchunguzi kifani 1 unaonesha namna mwalimu mmoja alivyowaelekeza wanafunzi wake wazo la kutumia historia simulizi kutafiti juu ya mambo ya kale. Soma hii na wanafunzi wako kabla ya kujaribu shughuli 1.

Uchunguzi kifani ya 1: Historia simulizi za familia

Kila mtu anahistoria yake. Bibi Eunice Shikongo, mwalimu wa darasa la tano katika shule ya Sheetheni nje ya Windhoek Namibia, hutaka wanafunzi wake kutafiti historia za familia zao kwa kumhoji mmoja wa wanafamilia.

Kwanza, hujadili maana ya ushahidi wa mapokeo kwa kuwahamasisha wanafunzi kushirikishana vitu walivyojifunza kutoka kwa wazazi wao. Huwauliza: Je, kile mlichojifunza kimeandikwa? Wengi wanakubali kuwa vitu walivyojifunza kwa njia hii havijaandikwa, lakini wameyapata kwa njia ya mdomo. Bibi Shikongo kisha huelezea kwamba, kwa kufanya mahojiano, wanafunzi watakusanya ushahidi wa mapokeo kuhusu zamani ilivyokuwa na watajua jinsi chanzo hiki kinavyoweza kuwa muhimu kuelezea mambo ya kale.

Huwasaidia kukusanya maswali muhimu watakayotumia kuwahoji wanafamilia zao (Angalia Nyenzo rejea 2: maswali yanayoweza kutumika katika mahojiano ). Halafu wanafunzi huongeza maswali yao kabla yakufanya mahojiano majumbani kwao.

Siku inayofuata, wanashirikishana matokeo ya utafiti na wanafunzi wenzao. Bibi Shikongo uandika muhtasari wa utafiti wao kwenye ubao kwa kichwa cha habari ‘Kale’. halafu, huwataka kujibu maswali yaleyale kuhusu maisha yao, na kuandika muhtasari wa maelezo yao chini ya kichwa cha habari cha habari, ‘Sasa’.

Huwataka kufikiri kuhusu namna maisha yao yanavyotofautiana na ya ndugu zao wa zamani. Halafu huwataka wanafunzi wawili wawili, kulinganisha Kale’ na ‘Sasa’

Wanafunzi wa umri mdogo huandika sentensi mbili/tatu kwa kutumia maneno ya ubaoni. Wanafunzi wakubwa huandika aya fupi.

Shughuli ya 1: Mahojiano ya ana kwa ana kuhusu utoto

Kwanza panga wanafunzi wawili wawili. Halafu, waambie wafikirie baadhi ya maswali wanayoweza kuuliza watu wazima kuhusu utoto wao. Wape wanafunzi muda wa kufikiri juu ya maswali yao na waambie muda watakaotumia katika zoezi

hili-yaweza kuwa siku mbili au tatu. Kama una wanafunzi wa umri mdogo, mnaweza kufanya pamoja kutengeneza maswali matatu au manne ambayo watakumbuka na kuweza kuuliza nyumbani.

Wakisha uliza maswali nyumbani, watake wanafunzi kushirikishana mawazo na wenzao.

Halafu, watake kila kundi la wanafunzi wawili kuungana na kundi lingine ili kushirikishana kile walichokipata.

Sasa waulize kila kundi la wanafunzi wanne kumalizia jedwali kuonyesha jinsi maisha yanavyoweza kubadilika.

Jadili na darasa lote namna maisha yalivyobadilika tangu wazazi wao na/au babu au watu wengine wa zamani walipokuwa watoto.

Uliza maswali yanayo wahamasisha kufikiri kwa nini mabadiliko haya yametokea.( Nyenzo muhimu: matumizi ya maswali kusaidia kufikiri inaweza kusaidia kufikiri aina gani ya maswali unahitaji kuuliza kuwahamasisha wanafunzi. Unaweza kuandika haya kabla ya kipindi kukukumbusha katika hatua hii.)

Tengeneza orodha ya mabadiliko ubaoni

Somo la 2

Kama ulivyoweza kutumia historia simulizi kujua maisha ya kale, unaweza pia pamoja na wanafunzi wako kutumia kumbukumbu zilizoandikwa

Katika sehemu hii, tunaangalia namna jozi tofauti za kumbkumbu zinavyoweza kusaidia kujenga uelewa wao wa mambo ya kale. Katika shughuli 2 na shughuli muhimu , wanafunzi hutafiti kumbukumbu zilizoandikwa juu ya mambo ya kale na kufanya mahojiano ya ana kwa ana na wanajamii. Namna unavyoweza kutunga na kukusanya pamoja nyenzo ni sehemu ya jukumu lako. Ushauri unavyoweza kufanya kazi hii umetolewa.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia nyaraka kutafiti matukio yaliyopita.

Bwana Murungi ni mwalimu wa darasa la 6 katika Shule ya msingi Mkiwa, sehemu ya Marangu,

Tanzania. Siku ya kuhadhimisha uhuru wa Tanzania inakaribia na anataka wanafunzi wake kufikiri kuhusu historia ya Tanzania.

Alipeleka darasa lake maktaba ambako walisoma kuhusu matukio. Magazeti mawili, The Daily News na The Express , yamekwisha kuchapisha kuhusu uhuru na huwasomea wanafunzi sehemu ya machapisho kuamsha ari ya kutaka kujua. Vitinyi hivi vina historia ya maisha ya baadhi ya watu husika. Aligawa darasa lake katika makundi na kuwataka kila kundi kuchukua mmoja kati ya watu hawa na kujifunza habari zake,halafu kuandika historia ya yule mtu katika bango, kwa maonyesho katika ukumbi wa shule. Bango lazima lijumuishe namna walivyojihusisha na nini kimewatokea.

Wanafunzi wa Bwana Mrungi kisha walipanga kuonyesha matokeo ya utafiti wao kwa shule nzima. Mabango yao yalibandikwa kuzunguka ukumbi na baadhi ya wanafunzi walisimulia kwenye mkusanyiko wa shule nzima.

Nyenzo rejea 3: Uhuru wa Tanzania inatoa taarifa za msingi

Shughuli ya 2: Kujifunza tarehe muhimu katika historia.

Shughuli hii inategemea kutembelea sehemu za makumbusho, yaani makumbusho ya kitaifa ya Dares Salaam, lakini unaweza kutumia sehemu nyingine. (kama haiwezekani kutembelea makumbusho, unaweza kukusanya pamoja baadhi ya machapisho kwenye magazeti, picha na vitabu kusaidia wanafunzi wako kujitafutia wenyewe kuhusu tukio.

Chagua tukio fulani la kihistoria unalotaka wanafunzi wako walitafiti wakati wa kutembelea makumbusho (au darasani kama una nyenzo husika), mfano, harakati za ukombozi/uhuru. Ni muhimu kuzingatia ufahamu wa wanafunzi wako juu ya tukio fulani, hasahasa kama wanatembelea makumbusho yanayoonyesha matukio ya miaka mingi iliyopita.

Gawanya wanafunzi kwenye makundi, ukiwapa kila kikundi mada tofauti ya kuzingatia juu ya tukio la kihistoria 

Jadili aina ya maswali wanayoweza kuhitaji kutafutia majibu wakati wakisoma na kuangalia maonyesho (kama ni kwenye makumbusho) au nyenzo (kama ni shuleni).

Darasani, watake wanafunzi kwenye makundi yao kuandika juu ya utafiti wao katika mabango makubwa. Yaweke mabango darasani au ukumbini kwa wote kuona.

Somo la 3

Sehemu hii inalenga kupanua mawazo yako namna ya kusaidia wanafunzi kutumia historia simulizi kama nyenzo ya kujifunzia juu ya mambo ya kale. Utawahamasisha kufikiri kiundani juu ya ukweli na uhalisia wa ushahidi huu, na kulinganisha ushahidi wa mapokeo ya matukio ya kihistoria pamoja na ushahidi wa maandishi kwa tukio hilohilo. Kutafiti ufanano na utofauti katika aina mbili za ushahidi kunatoa nafasi nzuri kwa wanafunzi kujifunza.

Uchunguzi kifani ya 3: Kukusanya ushahidi wa mapokeo

Bi Paka Ngowa hufundisha historia darasa la Sita kwenye shule ndogo nje kidogo ya Dares Salaam, Tanzania. Familia nyingi katika eneo hilo zilihusika kwenye matukio yaliyopelekea kupatikana kwa uhuru wa Tanzania. Bi Ngowa amewaarika shuleni wageni wawili walioshiriki katika harakati za kupata uhuru ili kuelezea juu ya uzoefu wao. (angalia

nyenzo rejea muhimu: kutumia jamii/mazingira husik a kama nyenzo zitakazo kusaidia kuandaa na kupanga ujio huo) Watakuja kwa siku mfululizo kwa vile hawajuani na wana mitazamo tofauti juu ya uhuru wa Tanzania.

Bi ngowa huwatahadharisha wanafunzi kwamba watu hawa wawili kwa sasa ni wazee sana, na kumbukumbu zao sio nzuri muda wote. Kabla ya wageni kufika, wanafunzi huandaa baadhi ya maswali muhimu wanayotaka kuuliza kwa wazee hao. Kwa siku mbili, wageni hufika na kusimulia hadithi zao. Wanapoondoka, Bi Ngowa na wanafunzi hujadili ufanano na tofauti kati ya hadithi mbili. Pia hujadili sababu zilizopelekea kutofautiana.

Mwalimu huorodhesha dondoo muhimu zilizojitokeza kwenye hadithi zao. Pia huelezea kwamba ingawa historia simulizi inaweza kufanya wanafunzi waelewe vizuri uhuru wa Tanzania, lakini mara nyingine wasimuliaji hawawezi kuwa sahihi na hadithi za watu tofauti huweza kutofautiana. Bi Ngowa anaamini kuwa wanafunzi wake wamejifunza kipindi muhimu katika matumizi na matatizo ya historia simulizi.

Shughuli muhimu: Kulinganisha mahojiano na nyaraka zilizoandikwa

Pamoja na wanafunzi wako, taja tukio muhimu la kihistoria (kama mapigano ya kikabila, au uasi) yaliyotokea. Kama unaweza, tafuta nyaraka zilizoandika juu ya hilo.

Katika kuandaa shughuli hii, unahitaji kujua (kama mwalimu) kuhusu kile jamii yako inachofahamu juu ya uasi au tukio husika. Kumbukumbu hizi ni hadithi simulizi iliyorithiwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Watambue baadhi ya watu muhimu ambao wanafunzi wako wanaweza kuzungumza nao nyumbani au wanaweza kuja shuleni.

Peleka wanafunzi wako nje kwenye makundi kwa mahojiano/usaili na wazee hawa. Watake wanafunzi kuorodhesha dondoo muhimu kumi zilizotolewa na kila mhojiwa/msailiwa (Hakikisha wanafunzi wanakwenda kimakundi tu na wako salama muda wote.)

Mkirudi darasani, watake wanafunzi kuelezea matokeo muhimu ya utafiti.

Watake kila kundi kubuni chati/bango la tukio husika, ikijumuisha matukio muhimu na kutumia baadhi ya maelezo ya wageni kutoa hisia ya kile kilichokuwepo.

Onyesha hii darasani.

Jadili pamoja na wanafunzi wako kama wanafikiri wanaushahidi wa kutosha juu ya nini kilitokea kutoka kwa watu walio zungumza nao. Kama hakuna, namna gani wanaweza kutafiti zaidi?

Nyenzo-rejea ya 1: Historia simulizi

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Wote tunahadithi za kusimulia, hadithi kuhusu maisha yetu na matukio muhimu yaliyotokea. Tunatoa uzoefu wetu na kuunganisha kumbukumbu zetu kufanya ziwe hadithi. Hadithi hizi zinaweza kuturuhusu kujenga picha halisi juu ya nini kilitokea kama zitaunganishwa na kumbukumbu za watu wengine katika tukio moja.

Jamii yako itakuwa chanzo muhimu kwa utafiti wa nini kilitokea kwa tukio husika au nini kinahisiwa kuwepo pale miaka 20 iliyopita. Wanafunzi wako wanaweza kutafiti vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Wanigeria au vita vya Biafra au matukio mengine.

Nini maana ya historia simulizi?

Historia simulizi siyo uwongo au uvumi lakini ni historia ya kweli ya watu wanaozungumziwa kutokana na mitazamo yao kadili wanavyoikumbuka. Inahusu mpangilio mzuri wa ukusanyaji wa hadithi juu ya uzoefu wa

watu. Kumbukumbu hizi za kila siku zina umuhimu kihistoria. Zinatusaidia kuelewa maisha jinsi yalivyo. Kama hatukusanyi na kuzitunza kumbukumbu hizo, siku moja zitapotea moja kwa moja.

Hadithi zako na hadithi za watu wanaokuzunguka ni za pekee na zinaweza kukupa taarifa muhimu.

Kwa sababu tunaishi kwa miaka kadhaa tunaweza kuwa na kumbukumbu za kipindi tu cha maisha. Hii

hufanya wanahistoria wawe na wasiwasi kwamba wanaweza kupoteza kumbukumbu muhimu na mitazamo juu ya matukio. Kukusanya hadithi hizi husaidia wanafunzi wako kukuza hisia za kujitambua wao wenyewe na namna gani wanajiweka katika hadithi ya mazingira yao.

Namna gani unakusanya hadithi za watu?

Unapokuwa umeamua ni tukio au shughuli gani unataka kuichunguza, unahitaji kutafuta watu waliohusika na kuwaomba kama wapo tayari kukusimulia hadithi zao.

Wasiliana nao kupanga muda na waambie nini unataka kuzungumzia na nini utafanya.

Unahitaji kunukuu wanachokisema. Unaweza kufanya hivyo kwa kuandika kwa mkono au ikiwezekana kwa kuchukua mkanda wa video au kurekodi sauti.

Baada ya kukusanya habari au ushahidi wao, ni muhimu kulinganisha na kutofautisha mitazamo ya watu tofauti kwenye tukio hilohilo, ili kuweza kugundua ukweli kutoka tafsiri za watu mbalimbali walizonazo juu ya tukio hilo. Unaweza kuwaomba wanafunzi wako katika makundi kufanya mahojiano na watu mbalinbali na halafu kuandika ufupisho wa utafiti wao ili kushirikishana au kushirikiana na wanafunzi wengine. Kitabu kinaweza kutengenezwa kuhusu utafiti wa wanafunzi juu ya tukio Fulani.

Imenukuliwa kutoka Do History, Website

Nyenzo-rejea ya 2: Maswali yanayoweza kutumika kwenye mahojiano

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Chini, ni baadhi ya maswali ya kutumia na wageni kutafiti juu ya matukio yaliyopita au namna walivyofanya vitu wakati uliopita. Maeneo unayoweza kutafiti yanajumuisha:

  • kuzalisha chakula
  • mavazi ya kale
  • tiba za asili
  • kujenga nyumba
  • Elimu

Jozi hizi tatu za masawali ya mwanzo yatakusaidia kuwapa wanafunzi msaada wa kufikiri juu ya maswali yao.

(1) matukio ya kihistoria.

  • Matukio gani ya kihistoria yalitokea wakati wa udogo wako?
  • Ulivaa nini wakati unaenda kwenye sherehe au harusi?
  • Nitukio gani unalikumbuka zaidi?
  • Unakumbuka nini juu ya hilo?
  • Nini kilitokea? Nisimulie ilivyokuwa.
  • Nani mwingine alikuwa na wewe?
  • Naweza kuongea nao juu ya hadithi hii?

(2) Michezo

  • Ni michezo gani ulicheza wakati wa utoto wako?
  • Namna gani ulicheza michezo hiyo?
  • Nani alikufundisha kucheza michezo hiyo?
  • Lini ulicheza michezo hiyo?
  • Ulichezea wapi michezo hiyo?
  • Ni shughuli gani nyingine ulizifurahia?

(3) Kuzalisha chakula

  • Mboga na matunda gani ulizalisha?
  • Namna gani ulizalisha?
  • Ulizalishia wapi?
  • Ulitumia zana gani?
  • Mboga ziligharimu kiasi gani wakati huo?
  • Ulinunua wapi? Mboga gani ulinunua?
  • Chakula gani kingine ulikula?
  • Je unaendelea kula chakula hicho?

Nyenzo-rejea ya 3: Uhuru wa Tanzania

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Tanganyika ilipata uhuru kamili tarehe 9 Desemba 1961 baada ya Nyerere kuwa Waziri Mkuu mapema mwaka huo. Hatukumwaga damu. Huu ulikuwa mfano mzuri wa kile kinachofanywa na umoja na mshikamano na pia ulikuwa mwanzo mzuri kwa taifa. Uhuru wa Zanzibar haukuja kirahisi, ingawa walikuwa chini ya Waingereza, Waarabu walitawala kikamilifu na wao pia walihitaji uhuru. Ukijumuisha kutokubaliana kati ya Waasia,Waafrika na Waarabu wenyewe, utakuwa huna njia nyingine zaidi ya mapinduzi-na ndicho hicho kilichotokea. Baada ya miaka miwili ya kukosa utulivu-na katika jitihada za kuongeza mchakato wa kujitawala- PAFM( Pan African Freedom Movement) kwa Africka Mashariki, Kati na Afrika Kusini viliunganisha vyama vya upinzani na mwaka 1963 mwezi wa Sita, uhuru ulipatikana.

Uhuru kamili wa Zanzibar kutoka kwa Waingereza ulitolewa tarehe 10

Desemba 1963. kulifuata kutoridhika, na Januari 1964 baada ya vurugu na vita vya wenywewe, Sultani na serikali yake walifukuzwa. Msukumo mkubwa wa mapinduzi ulitoka chama muhimu cha UMMA, chini ya uongozi wa Abdul Rahman Mohammed,kwa kushirikiana na John Okello wa Kenya. Tarehe 11 Januari 1964 walitwaa Zanzibar Mjini na kutangaza serikali mpya ya Mapinduzi ya Zanzibar. Tarehe 26 Aprili 1964 Zanzibar, Pemba,na Tanganyika ziliungana kufanya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Kama sehemu ya katiba, serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ingebaki na uhuru na Raisi wake angekuwa Makamu wa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Tanzania ilipopata uhuru wake, ilikuwa masikini na nchi ya mwisho kimaendeleo kwa Afrika Mashariki. Nyerere alikuwa na wasiwasi kuwa wale waliokuwa madarakani wangejitajirisha wenyewe kwa gharama za watu masikini waishio vijijini na kuzuia hilo, alifanya Tanzania iwe na mfumo wa chama kimoja na siasa ya ujamaa. Hili halikuwafurahisha viongozi wa Magharibi. Nyerere alizungumzia upinzani dhidi ya utawala uliojitangazia uhuru Rhodesia, alipata upinzani kutoka kwa Waingereza ambao walikata misaada yote kwa Tanzania. Msaada wa Nyerere kwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini, Msumbiji na Angola pia uliiongezea Tanzania maadui hasahasa alipowaruhusu ANC na FRELIMO kufanya shughuli zao Tanzania.

Tanzania pia ilivamiwa na Idi Amin –kiongozi wa Uganda maarufu kwa utawala wake wa mauaji-wakati Nyerere alipowahifadhi baadhi ya Waganda pamoja na Milton Obote na Yoweri Mseveni. Amin alivamia kaskazini magharibi mwa Tanzania Oktoba 1978 na kulilipua Bukoba na Musoma. Mwaka 1979, Nyerere aliweka pamoja jeshi dogo la Tanzania na kujibu kwa kuvamia Uganda na kumwondoa Amin madarakani. Moja kwa moja kitendo hicho kililaaniwa na viongozi wengine wa Afrika-mbali kwamba Amin alikuwa mchokozi. Pia vita hiyo ilishusha uchumi wa Tanzania kwa vile hakukuwa na fidia-iwe kutoka Magharibi au sehemu nyingine ya Afrika.

Wakati huohuo, Zanzibar, mambo yalikuwa hayajatulia. Zanzibar hawakukubali kuungana na Tanganyika matokeo vurugu ziliendelea. Abeid Karume, raisi wa kwanza wa Zanzibar aliuwawa mwaka 1972 na nafasi yake ilichukuliwa na Abdu Jumbe. Miaka michache baadae katika harakati kutuliza vurugu kutokana na kuungana kwa Tanzania bara na Zanzibar, Nyerere aliamuru kuundwa nchi ya chama kimoja kilichoitwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Muungano uliridhiwa Aprili 1977 na ingawa leo kuna chaguzi za vyama vingi, CCM imebaki chama chenye nguvu katika siasa za Tanzania.

Imetolewa kutoka Absolute Tanzania, Website

Sehemu ya 3: Kutumia njia tofauti za ushahidi katika historia

Swali Lengwa muhimu: Kwa jinsi gani unaweza kutumia ‘ramani ya mawazo’ na ziara za mafunzo kukuza ujuzi wa kihistoria.

Maneno muhimu: ujuzi wa kihistoria; Mawazo; ziara za mafunzo; utafiti, historia; ramani.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia ramani ya picha kusaidia wanafunzi kuona umuhimu wa mazingira asili katika makazi ya watu (rejea pia moduli 1, sehemu ya 2);
  • Umetumia utafiti wa kundi dogo,ikijumuisha ziara maalumu,kukuza uelewa wa wanafunzi juu ya jamii za kale za Kiafrika.

Utangulizi

Mbali na kuangalia ushahidi wa mapokeo na maandishi wanafunzi wanaweza pia kujifunza kuhusu mambo ya kale kutoka vyanzo vingine kwa mfani ramani.

Katika sehemu hii,utaunda vipindi na shughuli zitakazo wasaidia wanafunzi kuelewa sababu zilizopelekea kujitokeza kwa falme shupavu za kiafrika siku hizo.Hii inakuwezesha kujua undani wa aina za ushahidi na nyenzo unazoweza kutumia.

Inajumuisha

Kutumia ramani na nyaraka nyingine kuchunguza sababu katika mazingira halisi zilizopelekea kuwepo kwa aina Fulani ya makazi na falme.

Kutafiti umuhimu wa shughuli za ufugaji na kilimo katika kubadilisha maisha ya kiafrika na utamaduni.

Kuwapa mwanga wanafunzi kwa vitu halisi vilivyobakia katika mazingira yanayowazunguka ambavyo vitawasaidia kuchunguza namna kale ilivyokuwa.

Somo la 1

Kwa kuangalia mazingira ya kawaida na muundo wa nchi inawezekana kufiria sababu zilizofanya jamii kukaa mahali Fulani.

Zimbabwe kuu ni mfano mzuri. Kama mwalimu wa mafunzo ya jamii nimuhimu kuelewa kifani kama hiki, ambacho kinakupa ujuzi wa kuhusianisha mawazo haya na falme tofauti za Kiafrika pamoja na mazingira yako halisi. Kutumia ziara za mafunzo kama ziara kwenye eneo fulani huwezesha kujionea wenyewe kwanini sehemu moja ilichaguliwa kwa makazi na kwanini baadhi ya maendeleo yamedumu kwa muda mrefu kuliko mengine.

Makazi mengi yapo pale kwa sababu mazingira yana baadhi ya mahitaji muhimu kama vile maji au miti, na/au eneo linatoa ulinzi kutoka vitu fulani au dhidi ya maadui. Vijiji na miji mara nyingi hupatikana jirani na mito au misitu ambayo hutoa maji na miti ya ujenzi na kuni. Kwa kuangalia kwa ukaribu mazingira ya shule yako au nyumbani kwa wanafunzi, utawasaidia kuelewa jinsi makazi yalivyoanzishwa.

Ramani za zamani zitaonyesha jinsi eneo lilivyobadilika muda hadi muda (hii inaweza kuwa mwendelezo wa shughuli za matembezi kutoka moduli 2, Sehemu 1).

Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza maeneo ya utamaduni.

Sekai Chiwamdamira hufundisha darasa la sita katika shule ya msingi Musvingo Zimbabwe. Shule yake iko karibu na eneo la utamaduni la Zimbabwe kuu. Anafahamu kuwa wanafunzi wake wengi pindi waendapo shuleni hupita karibu na eneo hili maarufu lililozungukwa na kuta za mawe. Lakini haelewi kama wanajua kwa nini lipo pale. Sekai hutaka kuwasaidia wanafunzi kutambua kwamba ardhi na rasilimali zake za asili zilichangia katika uamuzi wa watu kuishi katika Zimbabwe Kuu.

Alianza kipindi kwa kuelezea jinsi Zimbabwe kuu ilivyokuwa na nguvu katika falme za kiafrika ambayo ilikuwepo miaka ya 1300-1450 ( rejea nyenzo 1: Zimbabwe kuu ). Huwataka wanafunzi kufikiria kwa nini watawala wa falme hii walichagua kuishi katika miinuko ya Zimbabwe kuliko eneo lingine katika Afrika. Ramani ni nyenzo yake muhimu kwa majadiliano haya ( rejea nyenzo 2: ramani ya picha ya Zimbabwe kuu

). Huonesha uwepo wa dhahabu pembe za ndovu, mbungo, uwepo wa maji na njia za kibiashara kwenye ramani: huwataka wanafunzi wake kupendekeza namna kila moja ilivyochochea watu kujenga makazi hapo yalipo. Kadili wanafunzi wanavyotoa mapendekezo yao, Sekai huchora picha ya mawazo ubaoni

Sekai ameridhishwa na kiwango cha kufikiri na majadiliano kilichoonyeshwa.

Shughuli ya 1: Kutumia ramani kupata taarifa kuhusu Zimbabwe kuu

Kabla ya kipindi, nakiri ramani na maswali kutoka nyenzo ya 2

kwenye ubao au andaa nakala kwa kila kikundi.

Kwanza, elezea kile kinachowakilishwa na ufunguo ubaoni. Halafu, gawanya darasa katika makundi na kitake kila kikundi kupambanua ufunguo kuhusiana na ramani ya Zimbabwe kuu. Kubali kila kitu kinachowakilishwa na ufunguo.

Uliza wanafunzi wako kwanini wanafikiri waliishi hapa kwanza. Unaweza kutumia maswali kutoka nyenzo ya 2 kama msaada kuanza majadiliano.

Kadili unavyofanya, zunguka zunguka katika makundi kutoa msaada pale unapohitajika kwa kuuliza maswali yanayowaongoza.

Baada ya dakika 15, kitake kila kikundi kuorodhesha mawazo yao

Baada ya hapo, watake kupanga mawazo yao kulingana na umuhimu wake.

Andika mawazo yao ubaoni

Mwisho, waambie wanafunzi kupigia kura sababu tatu wanazofikiri ni muhimu.

Kwa watoto wadogo, unaweza kuangalia katika vitu katika mazingira yao na watake wafikiri kwanini binadamu walishi hapa.

Somo la 2

Zamani, ng’ombe walitazamwa kama rasilimali muhimu, na wakulima wengi na jamii bado hutazama ng’ombe katika mtazamo huu.

Lengo la shughuli ya 2 ni kwa wanafunzi kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika jamii za Kiafrika kwa kutumia jamii husika kama chanzo cha taarifa. Hapo wanafunzi watagundua kiasi gani jamii za wakulima zimebadilika.

Uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 , tumia akili na mwongozo kusaidia wanafunzi juu ya shughuli hii kadili wanavyoshirikiana katika makundi.

Uchunguzi kifani ya 2: Shughuli za kilimo Arusha

Kuna wakulima wengi wanaoishi Arusha na wengi wa wanafunzi mashuleni ni watoto wa wakulima.Wema pamoja na wanaunzi wake wanataka kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika maisha na utamaduni wa wakulima wa zamani walioishi Tanzania.

Wema huanza kipindi chake kwa kuelezea jukumu muhimu la ng’ombe katika jamii za Kiafrika siku hizo. Huchora ramani ubaoni ambayo husisitiza umuhimu wa ng’ombe na namna ng’ombe walivyotumika. ( Nyenzo rejea muhimu: Kutumia picha ya mawazo na majadiliano na

Nyenzo 3: ufahamu kuhusu ufugaji ng’ombe kukusaidia kuwauliza maswali wanafunzi). Wanafunzi wajadili mawazo hayo

Katika kipindi kijacho, mtu mzima na wanafunzi katika makundi watakwenda kuwauliza maswali wakulima. Wema amewasiliana nao kujua ambaye yupo tayari kuongea na wanafunzi. wanafunzi walikuwa na maswali rahisi mawili ya kuwauliza wakulima

Kwanini ng’ombe ni muhimu kwako? Nini matumizi ya ng’ombe?

Darasani, wanafunzi hushirikishana utafiti wao na Wema huorodhesha majibu yao ubaoni. Wanajadiliana juu ya kile kilichobadilika kulingana na wakati.

Shughuli ya 2: Kilimo cha zamani na sasa.

Kabla ya kipindi, soma nyenzo 4: Ng’ombe katika maisha ya kitamaduni-Wamasai.

Elezea kwa wanafunzi umuhimu wa ng’ombe kwa watu wanaoishi Tanzania

Wakiwa katika makundi , watake kuorodhesha sababu zilizopelekea wafuge ngombe

Kwa kazi ya nyumbani, waombe kutafiti kutoka kwa wazee wa jamii zao namna ufugaji ulivyobadilika.

Katika kipindi kinachofuata, waombe wanafunzi kunakiri na halafu kujaza mwongozo katika Nyenzo 5: Umuhimu wa ng’ombe –zamani na sasa kudondoa mawazo yao.

Shirikishana na wanafunzi wote majibu ya kila kundi na weka mwongozo ukutani kwa siku kadhaa ili wanafunzi waweze kujikumbusha.

Somo la 3

Njia mojawapo ya kujua jinsi jamii ya kale ilivyoishi ni kuchunguza majengo, kazi za sanaa, sanamu na alama za muda mrefu zinazopatikana sehemu fulani.

Katika sehemu hii, wanafunzi waende ziara kwenye maeneo ya kihistoria. Kama hili haliwezekani kwa darasa lako, inawezekana kufanya jambo linalofanana na hilo darasani kwa kutumia nyaraka mbalimbali, picha na kazi za sanaa. Wanafunzi wanaweza kuelewa jinsi ya kutafiti hili na kujaza baadhi ya nafasi wenyewe kuhusiana na nini kilitokea.

Uchunguzi kifani ya 3: Uandaaji wa ziara ya mafunzo

Jasmin ameshafanya uchunguzi na wanafunzi wake wa darasa la tano kuwa huenda mwanzo wa binadamu ni Afrika Mashariki. Sasa anawataka kufikiri jinsi tunavyojua juu ya hili, kwa vile shule yake ipo jirani na makummbusho ya Olduvai Gorge yaliyo Ngorongoro, huandaa ziara ya mafunzo. Hutaka wanafunzi kuchunguza kazi za sanaa na picha, na kufikiri jinsi wanahistoria walivyotumia taarifa kuongeza uelewa wetu juu ya mabadiliko ya mwanadamu.

Ziarani, wanafunzi wachukue dondoo za taarifa kwenye chati na picha. Pia wanaelezea na kuchora baadhi ya kazi za sanaa na alama ambazo zipo Olduvai Gorge.

Shuleni, hujadili vitu vyote walivyoona na kusikia na kuviorodhesha ubaoni. Jasmine huwaomba kupanga tafiti zao chini ya vichwa tofauti vya habari juu ya aina za majengo waliyoona. Halafu wanafunzi hujadili wanachofikiri kuhusu matumizi ya majengo, kwa kuzingatia mwonekano wake na kazi za sanaa na sanamu zilizomo. Jasmin husaidia kujaza nafasi kwa kuelezea maana ya baadhi ya kazi za sanaa na sanamu. Mawazo hutolewa na wanafunzi wengine wanaalikwa kuona kazi yao.

Rejea Nyenzo muhimu: matumizi ya mazingira ya asili/jamii husika kama nyenzo muhimu

Shughuli muhimu: Kutafiti historia ya mahali

Kabla hujaanza shughuli hii, kusanya taarifa za kutosha kadili unavyoweza kuhusu jamii ya mahali kama ilivyokuwa. Unaweza kuwa na machapisho ya magazeti, dondoo za mazungumzo na wazee katika jamii hiyo, majina ya watu waliotayari kuongea na wanafunzi wako.

Panga wanafunzi kwenye makundi. Elezea kuwa watatafiti kuhusu historia ya kijiji kwa kutumia nyenzo mbalimbali. Kila kundi litashughulika na kipengele kimojawapo, kwa mfano duka, kanisa au shule.

Angalia nyenzo ulizonazo, kabla hujaenda kuongea na watu. Wape wanafunzi muda wakuandaa maswali na halafu wapangie

siku ya kwenda kuuliza maswali kuhusu kipengele chao.

Warudipo shuleni, kila kundi liamue namna ya kuwasilisha utafiti wao darasani.

Shirikishana utafiti

Unaweza kutoa kitabu cha kazi zao kuhusu historia ya eneo husika.

Nyenzo-rejea ya 1: Zimbabwe kuu

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Zimbabwe kuu au nyumba ya mawe, ni jina lililotolewa kwa mamia ya ngome za mawe zilizozunguka kilomita za mraba 500 ndani ya Zimbabwe ya sasa, ambayo imeitwa kutokana na ngome hizo.

Ngome zinaweza kugawanywa katika makundi matatu tofauti yanajulikana kama Mwinuko Changamano, Bonde Changamano na eneo maarufu lililozungushiwa ukuta. Kiasi cha majengo 300 yapo katika eneo hili lililiozungushiwa ukuta. Aina za majengo ya mawe yanayopatikana katika eneo hili yanaonyesha hali ya uzalendo. Majengo mazuri zaidi yalikuwa kwa ajili ya wafalme na yalijengwa mbali na mji. Inaaminika kuwa ilifanywa hivyo kukwepa ugonjwa wa malale (ugonjwa wa kusinzia).

Mifano michache iliyopo inaonyesha kuwa Zimbabwe kuu pia ilikuwa kituo cha kibiashara, kazi za sanaa zinaonyesha kuwa mji uliunganishwa kibiashara na China. Sarafu kutoka Arabia, shanga na vitu vingine visivyo vya asili vimepatikana katika ardhi ya Zimbabwe.

Hakuna anayejua kwanini eneo hili hatimaye liliachwa. Labda ilisababishwa na ukame, magonjwa au inaweza kuwa kuanguka kwa biashara ya dhahabu iliyowalazimu watu walioishi Zimbabwe kuu kwenda sehemu nyingine. Ngome za Zimbabwe kuu ni shemu zilizochukuliwa na UNESCO tangu 1986.

Imenukuliwa kutoka: Zimbabwe Wikipedia, Website

Nyenzo-rejea ya 2: Ramani ya picha ya Zimbabwe kuu

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Tafuta Zimbabwe kuu

1. Tafuta miinuko ya Zimbabwe. Unafikiri ni kwanini waanzilishi wa

Zimbabwe kuu waliamua kuanzisha makazi juu ya miinuko?

2. Rasilimali gani za asili zilipatikana hapo na eneo linalozunguka

Zimbabwe kuu?

3. Kwanini rasilimali hizi zilikuwa muhimu?

4. Ni sababu zipi nyingine za kimazingira zilizochangia katika uamuzi wa kuweka makazi juu ya miinuko? 

Chanzo: dyer, c., nisbet, j., friedman, m., johannesson, b., jacobs, m., roberts, b. & seleti, y. (2005). looking into the past: source-based history for grade 10. cape town: maskew miller longman. isbn 0 636 06045 4.

Nyenzo-rejea ya 3: Ufahamu juu ya ufugaji ngo’mbe

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Nyenzo-rejea ya 4: Ng’ombe na utamaduni wa maisha ya Wamasai.

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Maisha ya kabila la wamasai waishio Kenya na Tanzania yanahusu ng’ombe wao ambao ni chanzo kikuu cha chakula na uchumi wao. Wanaamini kuwa Mungu aliwapa ng’ombe wakuchunga na majukumu ya kijamii na hadhi yao inapatikana na mahusiano yao na ng’ombe.

Madaraja ya Wamasai hutegemea kiasi cha ng’ombe ilichonacho familia, hivyo ng’ombe ni mara chache huchinjwa; huachwa wazaliane kama ishara ya utajiri na huuzwa au kununuliwa kulipa deni. Mara nyingine askari wa kimasai huandaliwa kimakundi kwa lengo la kuiba au kunyang’anya ng’ombe.

Mazingira yao ya kuchungia ngombe yanaanzia katikati ya Kenya hadi katikati ya Tanzania. Vijana wakiume wanahusika kuchunga ng’ombe na kawaida huishi kwenye kambi ndogondogo, wakihama mara kwa mara kutafuta maji na malisho mazuri. Kwa vile wanahamahama, Wamasai hujenga nyumba za muda kwa kinyesi cha ng’mbe na matope. Mchanganyiko huu hukauka haraka na jua na ni mgumu kama saruji na hautoi harufu. Nyumba hujengwa kwa mduara; usiku ng’ombe wote huwekwa katikati ili kuwaepusha na wanyama wakali.

Maziwa ya ng’ombe pamoja na damu ni chakula cha kila siku kwa wamasai ambao hawali matunda wala nafaka. Mara moja kwa mwezi damu huchukuliwa kwa wanyama hai kwa kuchoma mkuki shingoni.

Damu hii huchanganywa na maziwa kwenye kibuyu kilichooshwa kwa mkojo kuzuia yasiharibike.

Imenukuliwa kutoka: University of Iowa, Website

Nyenzo-rejea ya 5: Umuhimu wa ng’ombe-zamani na sasa.

Kwa matumizi ya wanafunzi

Umuhimu wa ng’ombe zamaniUmuhimu wa ng’ombe sasa
Ng’ombe walikuwa muhimu kwa:Ng’ombe ni muhimu kwa:

Sehemu ya 4: Ufahamu wa Chati ya kalenda ya matukio

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia kalenda ya matukio ya kihistoria na nyenzo nyingine kukuza ufahamu wa chanzo na matokeo?

Maneno muhimu: Chati ya wakati na matukio, mabadiliko ya kihistoria; mpangilio wa matukio ya kihistoria; historia; vyanzo vya kihistoria; mdahalo

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia kalenda ya matukio kuonyesha mabadiliko ya kihistoria kipindi hadi kipindi;
  • umewasaidia wanafunzi kutambua matukio muhimu katika mchakato fulani wa kihistoria;
  • umewahamasisha wanafunzi kuiangalia historia sio kama mtiririko wa tarehe za kujifunza lakini ni mchakato wa kutafiti;
  • Umetumia nyenzo mbalimbali kusaidia wanafunzi kujifunza kwamba tukio moja linaweza kuwa ni matokeo ya sababu nyingi.

Utangulizi

Unapokuza ufahamu wa muda uliopita na unaoendelea kupita, ni muhimu kuwa na uwezo wa kupanga matukio katika mpangilio fulani kulingana na yalivyokuwa yanatokea.

Mara nyingi wanafunzi huhangaikia kujua dhana ya muda. Katika sehemu hii kitu cha kwanza utawasaidia wanafunzi wako kugawanya muda katika vipindi ambavyo ni rahisi kuelewa; mara wakiweza kufanya hili, kufikiri kuhusu mtiririko wa matukio na kwa nini ni muhimu. (kwa wanafunzi wadogo hili linaweza kurahisishwa kwa utawasaidia namna ya kupanga kazi fulani wanazozifanya, ukiwaelekeza kwenye shughuli ngumu kadili ufahamu wao unavyoongezeka). Utawasaidia wanafunzi wako kutambua matukio muhimu katika kipindi fulani. Hili litawaongoza wanafunzi wadogo na wakubwa kwenye uchambuzi wa chanzo na matokeo yake, na kujua kuwa kuna sababu zaidi ya moja katika tukio fulani.

Somo la 1

Kutafiti kipindi fulani cha kihistoria, na kujaribu kupanga matukio kwa mtirirko kadili yalivyotokea kutasaidia wanafunzi kuanza kuona uhusiano kati ya matukio na baadhi ya sababu za matukio. Kujua chanzo cha mabadiliko katika nchi na jamii zetu, inaweza kutusaidia kuishi maisha bora.

Kusudio la sehemu hii ni kutafuta namna matumizi ya kalenda ya matukio ya kihistoria yanavyoweza kuwa ni njia muhimu katika kugawanya vipindi ili kujua ni kipindi gani tunahusika nacho. Hili ni muhimu hasa pale tunapofundisha historia kwa sababu ni lazima wanafunzi kujua mabadiliko kutegemeana na muda.

Wanafunzi wanahitaji kusaidiwa kuchambua na kupanga matukio kutoka utotoni. Kadili wanavyokua na kuishi wanaweza kurejea shughuli kama hizi kwa kutumia mchanganyiko zaidi wa matukio.

(Sehemu ya 1 katika moduli hii imetumia kalenda ya matukio kutafiti historia ya familia. Inafaa kuangalia sehemu hiyo kama bado hujapitia, hasa kama unafanya kazi na wanafunzi wenye umri mdogo)

Uchunguzi kifani ya 1: Mpangilio wa matukio

Tetha Rugenza, ambaye hufundisha historia katika shule ndogo Rwanda, anataka kuwaonyesha wanafunzi wa darasala 4 jinsi ya kugawanya muda katika vipindi vidogo vidogo. Ili kufanya hili, huandaa kipindi ambapo wanafunzi na yeye mwenyewe hujifunza namna ya kutengeneza kalenda ya matukio na kuigawanya katika vipindi.

Rugenza huamua kutumia mfano wa Rwanda. Huchora kalenda ya matukio ya historia ya Rwanda ubaoni. Kuwasaidia wanafunzi kuelewa dhana ya vipindi, hugawanya historia ya Rwanda katika vipindi vya kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na wakati wa uhuru.

Huandika orodha ya matukio muhimu pamoja na tarehe yalipotokea kwenye vipande tofauti vya karatasi na kuweka mezani. Kila tukio, analowaelezea wanafunzi lipo katika kipindi fulani. Huwataka wanafunzi wake kupanga matukio kulingana na vipindi yalipotokea.

Huanza na tukio moja na huruhusu mwanafunzi kuchukua tukio la pili na kubandika sehemu husika kwenye kalenda ya matukio. Wanafunzi wengine huhakikisha kama tukio limewekwa katika sehemu sahihi. Kupitia majadiliano, huwasaidia wanafunzi kama hawana uhakika na mahali tukio linapotakiwa kuwekwa. Huwataka wanafunzi kufikiri kama kuna matukio mengine ya kitaifa yanayoweza kuwekwa kwenye kalenda ya matukio nayo pia huyapanga katika mtiririko unaofaa.

Shughuli ya 1: Uchoraji wa kalenda ya matukio

Waambie wanafunzi kuwa wanatakiwa kutengeneza kalenda ya matukio ya shule kwa pamoja.

Anza kipindi kwa kuwataka wanafunzi wako kuandika matukio muhimu yaliyotokea shuleni katika mwaka husika.

Watake wanafunzi kutoa tarehe ya kila tukio kama wanaweza au watafute tarehe hizo.

Watake wanafunzi kupanga matukio haya kutoka mwanzo hadi mwisho wa mwaka wa shule.

Wasaidie wanafunzi kufanya uamuzi kuhusu ukubwa wa kalenda za matulio wanaoutaka na kutengezeza kipimo inavyotakiwa.

Watake wanafunzi kuonyesha mwezi kwa usahihi kulingana na vipimo walivyochagua na kuandika tarehe za matukio kushoto mwa kalenda- matukio ya miaka ya zamani yaanzie chini nay a tarehe za karibuni yawe juu.

Katika upande wa kulia wa kalenda ya matukio, watake wanafunzi waandike maelezo mafupi ya tukio husika dhidi ya kila tarehe.

Weka wazi hiyo kalenda ili wote waione. (kama huna nyenzo za kutosha kwa kila mwanafunzi kufanya peke yake, basi kazi hii inaweza kufanywa katika makundi ya wanafunzi wasiozidi watano.) Darasa zima wajadili kama kuna matukio ya shule yaliyoweza kutokea wakati wowote katika mwaka. Je kuna yale yanayotokea katika kipindi fulani? Kwa nini? (kwa mfano, kwa nini mitihani ya kumaliza mwaka haiwezi kufanywa mwanzoni mwa muhula?

Zamani, ng’ombe walitazamwa kama rasilimali muhimu, na wakulima wengi na jamii bado hutazama ng’ombe katika mtazamo huu.

Somo la 2

Lengo la shughuli ya 2 ni kwa wanafunzi kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika jamii za Kiafrika kwa kutumia jamii husika kama chanzo cha taarifa. Hapo wanafunzi watagundua kiasi gani jamii za wakulima zimebadilika.

Uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 , tumia akili na mwongozo kusaidia wanafunzi juu ya shughuli hii kadili wanavyoshirikiana katika makundi.

Uchunguzi kifani ya 2: Shughuli za kilimo Arusha

Kuna wakulima wengi wanaoishi Arusha na wengi wa wanafunzi mashuleni ni watoto wa wakulima.Wema pamoja na wanaunzi wake wanataka kuchunguza umuhimu wa ng’ombe katika maisha na utamaduni wa wakulima wa zamani walioishi Tanzania.

Wema huanza kipindi chake kwa kuelezea jukumu muhimu la ng’ombe katika jamii za Kiafrika siku hizo. Huchora ramani ubaoni ambayo husisitiza umuhimu wa ng’ombe na namna ng’ombe walivyotumika. ( Nyenzo rejea muhimu: Kutumia picha ya mawazo na majadiliano na

Nyenzo 3: ufahamu kuhusu ufugaji ng’ombe kukusaidia kuwauliza maswali wanafunzi). Wanafunzi wajadili mawazo hayo

Katika kipindi kijacho, mtu mzima na wanafunzi katika makundi watakwenda kuwauliza maswali wakulima. Wema amewasiliana nao kujua ambaye yupo tayari kuongea na wanafunzi. 

Wanafunzi walikuwa na maswali rahisi mawili ya kuwauliza wakulima

Kwanini ng’ombe ni muhimu kwako? Nini matumizi ya ng’ombe?

Darasani, wanafunzi hushirikishana utafiti wao na Wema huorodhesha majibu yao ubaoni. Wanajadiliana juu ya kile kilichobadilika kulingana na wakati.

Shughuli ya 2: Kilimo cha zamani na sasa.

Kabla ya kipindi, soma nyenzo 4: Ng’ombe katika maisha ya kitamaduni-Wamasai.

Elezea kwa wanafunzi umuhimu wa ng’ombe kwa watu wanaoishi Tanzania

Wakiwa katika makundi , watake kuorodhesha sababu zilizopelekea wafuge ngombe

Kwa kazi ya nyumbani, waombe kutafiti kutoka kwa wazee wa jamii zao namna ufugaji ulivyobadilika.

Katika kipindi kinachofuata, waombe wanafunzi kunakiri na halafu kujaza mwongozo katika Nyenzo 5: Umuhimu wa ng’ombe –zamani na sasa kudondoa mawazo yao.

Shirikishana na wanafunzi wote majibu ya kila kundi na weka mwongozo ukutani kwa siku kadhaa ili wanafunzi waweze kujikumbusha.

Somo la 3

Njia mojawapo ya kujua jinsi jamii ya kale ilivyoishi ni kuchunguza majengo, kazi za sanaa, sanamu na alama za muda mrefu zinazopatikana sehemu fulani.

Katika sehemu hii, wanafunzi waende ziara kwenye maeneo ya kihistoria. Kama hili haliwezekani kwa darasa lako, inawezekana kufanya jambo linalofanana na hilo darasani kwa kutumia nyaraka mbalimbali, picha na kazi za sanaa. Wanafunzi wanaweza kuelewa jinsi ya kutafiti hili na kujaza baadhi ya nafasi wenyewe kuhusiana na nini kilitokea.

Uchunguzi kifani ya 3: Uandaaji wa ziara ya mafunzo

Jasmin ameshafanya uchunguzi na wanafunzi wake wa darasa la tano kuwa huenda mwanzo wa binadamu ni Afrika Mashariki. Sasa anawataka kufikiri jinsi tunavyojua juu ya hili, kwa vile shule yake ipo jirani na makummbusho ya Olduvai Gorge yaliyo Ngorongoro, huandaa ziara ya mafunzo. Hutaka wanafunzi kuchunguza kazi za sanaa na picha, na kufikiri jinsi wanahistoria walivyotumia taarifa kuongeza uelewa wetu juu ya mabadiliko ya mwanadamu.

Ziarani, wanafunzi wachukue dondoo za taarifa kwenye chati na picha. Pia wanaelezea na kuchora baadhi ya kazi za sanaa na alama ambazo zipo Olduvai Gorge.

Shuleni, hujadili vitu vyote walivyoona na kusikia na kuviorodhesha ubaoni. Jasmine huwaomba kupanga tafiti zao chini ya vichwa tofauti vya habari juu ya aina za majengo waliyoona. Halafu wanafunzi hujadili wanachofikiri kuhusu matumizi ya majengo, kwa kuzingatia mwonekano wake na kazi za sanaa na sanamu zilizomo. Jasmin husaidia kujaza nafasi kwa kuelezea maana ya baadhi ya kazi za sanaa na sanamu. Mawazo hutolewa na wanafunzi wengine wanaalikwa kuona kazi yao.

Rejea Nyenzo muhimu: matumizi ya mazingira ya asili/jamii husika kama nyenzo muhimu

Shughuli muhimu: Kutafiti historia ya mahali

Kabla hujaanza shughuli hii, kusanya taarifa za kutosha kadili unavyoweza kuhusu jamii ya mahali kama ilivyokuwa. Unaweza kuwa na machapisho ya magazeti, dondoo za mazungumzo na wazee katika jamii hiyo, majina ya watu waliotayari kuongea na wanafunzi wako.

Panga wanafunzi kwenye makundi. Elezea kuwa watatafiti kuhusu historia ya kijiji kwa kutumia nyenzo mbalimbali. Kila kundi litashughulika na kipengele kimojawapo, kwa mfano duka, kanisa au shule.

Angalia nyenzo ulizonazo, kabla hujaenda kuongea na watu.

Wape wanafunzi muda wakuandaa maswali na halafu wapangie siku ya kwenda kuuliza maswali kuhusu kipengele chao.

Warudipo shuleni, kila kundi liamue namna ya kuwasilisha utafiti wao darasani.

Shirikishana utafiti

Unaweza kutoa kitabu cha kazi zao kuhusu historia ya eneo husika.

Nyenzo-rejea ya 1: Zimbabwe kuu

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Zimbabwe kuu au nyumba ya mawe, ni jina lililotolewa kwa mamia ya ngome za mawe zilizozunguka kilomita za mraba 500 ndani ya Zimbabwe ya sasa, ambayo imeitwa kutokana na ngome hizo.

Ngome zinaweza kugawanywa katika makundi matatu tofauti yanajulikana kama Mwinuko Changamano, Bonde Changamano na eneo maarufu lililozungushiwa ukuta. Kiasi cha majengo 300 yapo katika eneo hili lililiozungushiwa ukuta. Aina za majengo ya mawe yanayopatikana katika eneo hili yanaonyesha hali ya uzalendo. Majengo mazuri zaidi yalikuwa kwa ajili ya wafalme na yalijengwa mbali na mji. Inaaminika kuwa ilifanywa hivyo kukwepa ugonjwa wa malale (ugonjwa wa kusinzia). Mifano michache iliyopo inaonyesha kuwa Zimbabwe kuu pia ilikuwa kituo cha kibiashara, kazi za sanaa zinaonyesha kuwa mji uliunganishwa kibiashara na China. Sarafu kutoka Arabia, shanga na vitu vingine visivyo vya asili vimepatikana katika ardhi ya Zimbabwe.

Hakuna anayejua kwanini eneo hili hatimaye liliachwa. Labda ilisababishwa na ukame, magonjwa au inaweza kuwa kuanguka kwa biashara ya dhahabu iliyowalazimu watu walioishi Zimbabwe kuu kwenda sehemu nyingine.

Ngome za Zimbabwe kuu ni shemu zilizochukuliwa na UNESCO tangu

1986.

Imenukuliwa kutoka: Zimbabwe Wikipedia, Website

Nyenzo 2: Jedwali la Kalenda ya matukio ya Kiafrika

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Nigeria   

Uhuru

(63)

Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010
Ghana 

uhuru

 

(57)

Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010

uhuru
Sudan(57)
Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010
Kenya 

uhuru

 

(63)

Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010
Rwanda
Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010
   

Afrika

Kusini

Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010
Matukio ya Dunia
Tarehe194019451950195519601965197019751980198519901995200020052010

Nyenzo-rejea ya 3: Matukio muhimu kuelekea uhuru

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

1957Ghana inakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kupata uhuru chini ya Kwame Nkrumah kupitia mikutano kama ile ya Ghandi, migomo, kuwalazimisha Waingereza kutoa uhuru
1958Chinua Achebe(Nigeria): Things Fall Apart, kilicho andikwa kwa ‘Kingereza cha Kiafrika’ kinachunguzia madhara ya utamaduni wa Magharibi kwa tamaduni za asili.
1958Mkutano wa mataifa yote ya Afrika: suluhisho la ubepari na ukolini, Accra, 5-13 Desemba 1958
1954–1962Makoloni ya Kifaransa (mataifa ya Kiafrika yanayo zungumza Kifaransa) yanakataa kuendelea kutawaliwa hata kama wanatambua kuwa uchumi na tamaduni zao bado zinategemea Ufaransa-isipokuwa Algeria iliyokua na walowezi wapatao millioni 1. Vita vya kikabila nchini Algeria viliendelea hadi ulipopatikana uhuru mwaka 1962, miaka sita baadae baadaye Moroko na Tunisia kupata uhuru.
1958Makaburu wenye asili ya Kidachi walipata uhuru kutoka kwa Waingereza Afrika Kusini.
1964Nelson Mandela, katika hukumu ya uhaini na viongozi wenzake wa ANC mbele ya Mahakama Kuu ya
Pretoria, anatoa hotuba kali kabla hajafungwa kwa muda wa miaka 25 katika gereza lililo kisiwani Robben.
1960–1961Zaire (koloni la zamani la Ubelgiji) linapata uhuru kutoka kwa Wabelgiji mwaka 1960. Halafu katika mji wa Elisabethville( sasa Lubumbashi ), kiongozi mzalendo Patrice Lumumba aliuwawa mwaka 1961, na kanali Joseph Desere Mobuto (30) ambaye alikuja kuwa raisi. (Bill Berkeley, ‘Zaire: An African Horror Story’, The Atlantic Monthly, August 1993; rpt. Atlantic Online)
1962Algeria inapata uhuru kutoka kwa Wafaransa, zaidi ya walowezi 900,000 wanaihama nchi mpya.
1963Kenya inatangaza uhuru kutoka kwa Waingereza
1963 

Mkataba wa umoja wa nchi huru za Afrika, 25 Mei

1963

Mid-60sNchi nyingi za Afrika zinapata uhuru na kipindi cha ukoloni kinaisha. Vile vile utawala wa uchumi na utamaduni wa magharibi na uchu wa mali na madaraka vinaongeza matatizo yanayozikumba nchi huru za Kiafrika.
1965Rodesia: kutangazwa kwa utawala wa watu wachache
1966Bechuanaland inapata uhuru na kuwa Botswana
1970s 

Wareno wanapoteza makoloni ya Afrika, pamoja na

Angola na Msumbiji

1976Cheikh Anta Diop( Senegal , 1923-1986), moja wa
wanataaluma wa Afrika wa karne ya 20, anatoa kitabu, Afrika chanzo cha Ustaarabu kuondoa uvumi (kuhusu historia ya Afrika) tulio jifunza na kusahihisha kwa kizazi kijacho.
1980Zimbabwe ( zamani Rodesia ya Kusini inapata uhuru kutoka kwa walowezi wa kizungu baada ya miaka kadhaa ya uadui
1970s–1980sWatawala wachache wa Kizungu Afrika Kusini wanasisitiza kuendeleza ubaguzi na mfumo usio na usawa wa ubaguzi wa rangi kupelekea vurugu, uadui, migomo na mauaji kutawala.
1986 

Mnigeria mwandishi wa tamthilia za fasihi Wole

Soyinka anatuzwa zawadi ya Nobel 1986.

1988Mmisri mwandishi wa hadithi na hadithi fupi Nahfouz anatuzwa zawadi ya Nobel 1988, mwandishi wa kwanza kushinda akiwa Kiarabu ndiyo lugha yake ya asili(ya kwanza)
 

1994

       

1996

 

Wahutu waliua Watusi wapatao 1,000,000, huku wakiogopa serikali ya Kitusi kulipa kisasi zaidi ya wahutu millioni 1 walihama Rwanda kwa mkupuo na kuvuta hisia dunia nzima.

    

Wakimizi wa Kihutu kama 500,000 walirudi Rwanda kutoka Zaire kuepuka vita nchini zaire

2001 

Baada ya miaka 38 ya uwepo,OAU (http://

oau.oua.org) inageuzwa kuwa Umoja wa Afrika (AU)

Kalenda-Nchi za Afrika katika mpangilio wao wa kupata uhuru

Imenukuliwa kutoka: Decolonization of Africa, Wikipedia, Website

Sehemu ya 5: Kutumia kazi za sanaa kujifunza mambo ya kale

Swali Lengwa muhimu: unawezaje kutumia kazi za sanaa na ushahidi mwingine kutafita historia ya mahali fulani na ya kitaifa?

Maneno muhimu: kazi za sanaa; ushahidi; kazi za makundi; historia ya mahali; mazingira; kuuliza

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia kazi za sanaa kusaidia wanafunzi kuibua maswali juu ya mambo ya kale na kuifahamu historia yao;
  • umeandaa vipindi vinavyowafanya wanafunzi kujitambua wao kwa kufikiri na kujihusianisha na historia ya taifa lao;
  • Umetumia wataalamu wa ndani na mazingira ya mahali hapo katika kipindi chako kuamsha hamasa ya wanafunzi ya kutaka kujua historia yao.

Utangulizi

Kujifahamu wewe ni nani na kujitambua kunaimarishwa kama una uelewa mpana juu ya utambulisho wako na unaweza kuona nafasi yako katika maisha kwa ujumla. Kujifunza kilichotokea zamani kunaweza kuchangia hili. Kupitia kazi za sehemu hii,utawahamasisha wanafunzi wako kufikiria jinsi walivyosehemu ya historia hiyo. Kwa kutumia kazi za makundi, kualika wageni darasani na kazi za mikono, kuchunguza kazi za sanaa kutawafanya wanafunzi kushirikishana mawazo na kukuza ujuzi wao katika historia.

Somo la 1

Kutumia kazi za sanaa au kuangalia picha zao ni njia yakuwafanya wawe wasikivu kwa dhana halisi ya historia na tafsiri yake. Kitu kinachoweza kukusaidia katika kazi hii ni kukusanya nyenzo kama zilivyo na kadili unavyoweza. Daima inawezekana kutafuta vyombo vya zamani na kazi za sanaa kutoka nyumbani na sokoni.

Sehemu hii itakusaidia kupanga shughuli kwa wanafunzi wako kufikiri jinsi vitu tunavyotumia katika maisha yetu ya kila siku vilivyobadilika. Kwa mfano, vitu tunavyotumia kupikia sasa na tulivyotumia zamani tunaweza kupata picha namna gani watu waliishi. Tunaweza kulinganisha vyombo na kutokana na ulinganisho huo, kubuni juu ya maisha yalivyokuwa zamani kwa kutumia kazi za sanaa kama hizo. Hili litawahamasisha wanafunzi kujitafakari nafasi yao katika jamii yao na historia yake.

Uchunguzi kifani ya 1: Uchunguzi wa vitu

Bwana Ndomba, mwalimu wa darasa la 5 mjini Mbinga, Tanzania ameamua kutumia kazi za sanaa zilizotumika kwa kilimo katika somo lake kuamusha udadisi wa wanafunzi na kuwahamasisha kufikiri kihistoria.

Hupanga darasa katika makundi, na kuwapa kila kundi kazi halisi za sanaa au picha mojawapo. Huwataka kuangalia picha au vitu kwa undani na kuandika kadili wanavyoweza juu ya vitu au picha hizo. Wanafunzi wake hufanya vizuri,kwa kuwa hupenda majadiliano, na inaeleweka kwa Ndomba kuwa wanavutiwa na wanafurahia kudadisi juu ya kazi za sanaa.( rejea Nyenzo muhimu: utumiaji wa kazi za makundi darasani )

Baada ya dakika chache, hulitaka kila kundi kubadilishana picha au kazi za sanaa zao na kundi jingine na kufanya tena zoezi lile. Wanapo maliza huamuru makundi mawili kuungana na kushirikishana mawazo yao juu ya picha na kazi za sanaa. Wanafikiri nini juu ya kazi hizo za sanaa?

Zimetengenezwa kwa kutumia nini? Zimetengenezwaje? Wanakubaliana kuandika dondoo tano kwa kila kazi ya sanaa, na kila kundi hushughulika na picha au kazi moja ya sanaa.

Bwana Ndomba huweka kazi za sanaa mezani na dondoo zake tano na kuweka mahali wazi kwa siku kadhaa ili wote waone.

Mwishoni mwa juma, hutaka kila kundi kuandika kwenye upande mmoja wa karatasi juu ya kile walicho na uhakika nacho, na kwa upande mwingine wa karatasi waandike vitu ambavyo hawana uhakika navyo pamoja na maswali yoyote wanayoweza kuwa nayo. Kwake, sio muhimu wakubaliane juu ya kitu, lakini anataka majadiliano yaliyochangamka juu ya yanayodhaniwa kuwa ni matumizi yake na umri wa kitu hicho.

Shughuli ya 1: Kuwa mtaalamu wa historia wa kutumia kazi za sanaa.

Rejea nyenzo 1 : kutumia kazi za sanaa darasani kabla ya kuanza kipindi.

Waamuru wanafunzi kuleta vitu vyovyote vya kitamaduni walivyonavyo majumbani. Waambie unataka kitu kilicho cha zamani kadili inavyo wezekana, labda kilichotumiwa na babu zao au nyuma yao. Lakini wasisitize kuvitunza kwa uangalifu visiharibiwe. Kuwe na meza tayari kwa kuviweka pindi wanafunzi watakapoleta siku ya pili.

Waeleze wanafunzi wako kuwa watakuwa wataalamu wa kuunganisha pamoja ushahidi na taarifa nyingi iwezekanavyo kuhusu vitu vyao.

Watake katika jozi waangalie kazi za sanaa zote na kuziita majina na kuorodhesha katika daftari zao. Kwa kuangalia na kushika, watake kuandika wanachofikiri kimetumika kuzitengeneza, jinsi kilivyotengenezwa na matumizi yake. Unaweza kuwapa karatasi kwa matumizi hayo.

Angalia kazi za sanaa kama darasa kwa zamu na jadili mawazo juu ya sanaa hizo. Kubaliana na wazo lililotolewa na wengi na mtake aliyeleta hicho kitu aeleze anajua nini juu yake. Au wapeleke nyumbani na baadhi ya maswali ya kuuliza na kuleta majibu kwa lengo la kushirikishana na wengine siku inayofuata.

Somo la 2

Moja ya malengo ya kufundisha historia kwa wanafunzi wako ni kuwawezesha kujielewa na kujigundua na kuelewa utambulisho wa jamii zao. Kama mwalimu wa mafunzo ya jamii, hata kama wa shule za msingi unatakiwa kutafuta njia zinazovutia za kuwasaidia wanafunzi kujua ya kale na historia yao. Kwa kuzingatia namna utamaduni wao, shughuli za kila siku na vitu vitumikavyo vilivyobadilika husaidia kujenga utambulisho huu.

Uchunguzi kifani ya 2: Mafunzo ya mavazi ya asili

Bibi Ndonga amewaalika wazee wawili kutoka katika jamii kuja darasani wakiwa na mavazi yao ya asili na kuzungumza kuhusu nini kimebadilika kwenye mavazi ya asili tangu utoto wao.

Kabla ya ziara, Bibi Ndonga husoma Nyenzo muhimu: matumizi ya jamii/mazingira ya mahali kama nyenzo muhimu; na pamoja na wanafunzi wake, huandaa ziara hiyo. Mara wakikubaliana kuhusu muda na tarehe, wanafunzi huandaa maswali ya kuwauliza wageni juu ya kile kilichobadilika kulingana na wakati.

Siku ya ziara, darasa linapangwa na baadhi kwenda kuwakaribisha wageni. Darasa limesisimuka lakini lina aibuaibu kwa wageni. Hata hivyo, wageni wamefurahishwa kuja na kuongea. Pia na kwamba kila mmoja alitulia na kukawa na mjadala mzito juu ya mavazi waliyovaa na umuhimu wa kila kipande cha nguo hizo. Pia wageni walileta baadhi ya mavazi ya asili waliyotumia wazazi wao ili watoto wayaone.

Baada ya wageni kuondoka, Bibi Ndonga anawauliza wanafunzi kuhusu kitu kipya walichojifunza na anashangazwa na kuridhishwa kwa namna wanavyo kumbuka na kulipenda tukio hilo.

Shughuli ya 2: Uchunguzi wa utaalam/ujuzi wa asili

Shughuli hii inalenga kuweka mwongozo, kama mwalimu, unaweza kutumia kufanyia mjadala darasani kuhusu dhana yoyote ya mafunzo ya jamii au historia. Kwa maana hiyo, tunaangalia kazi za sanaa na matumizi yake ya asili.

Waandalie wanafunzi wako ziara ya kumtembelea fundi asilia au waalike shule kuongea na wanafunzi kuhusu ufundi wao wa sasa na namna ulivyokuwa siku za nyuma.

Kabla ya ziara utahitaji kupanga tarehe na muda na nini unataka kuongelea, ili wageni wajiandae nini cha kuleta.

Halafu, pamoja na wanafunzi wako amua ni vitu gani wanataka kuvijua na maswali gani wanataka kuuliza kuhusu kazi za sanaa ambazo wageni wanaweza kuwaonyesha au kuviona wakati wa ziara yao. Inawezekana wageni wakafanya maonesho mbele ya darasa.

Siku ya ziara, waambie wanafunzi wafurahie ziara na kuwaheshimu wakubwa.

Katika kipindi kinachofuata, jadili matokeo ya utafiti na watake wanafunzi katika makundi ya watu wanne kuchagua kitu kimoja kukichora na kuandika wanachokiweza kuhusiana nacho kutokana na kumbukumbu na dondoo walizochukua.(rejea nyenzo muhimu : Matumizi ya kazi za makundi darasani.)

Watake wanafunzi kuweka kazi zao ukutani ili wote wazione na kusoma

Unaweza kuandaa kipindi cha ufundi pamoja na wageni ili wanafunzi waweze kufanya kwa vitendo.

Somo la 3

Daima, historia inaweka usawa kati mawazo au maoni ya watu binafsi dhidi ushahidi halisia. Unapojifunza kazi za sanaa badala ya ushahidi simulizi na maandishi uwiano uleule hujitokeza. Kuna vitu halisi ambavyo vinaweza kuongelewa kwa mfano chungu yaani umbo lake, kimetengenezwa kwa kutumia nini, n.k. kitu kama matumizi yake inaweza kuwa ni udadisi tu kuzingatia matumizi yake kwa sasa. Kwa kuangalia chungu kwa umakini unapochunguza michoro ya zamani na upigwaji wa rangi na kuzungumza na wengine tunaweza kujenga picha fulani kuhusu matumizi ya chungu siku za nyuma.

Sehemu hii inatafiti njia za kusaidia wanafunzi kudadisi fikira na uelewa wao kuhusu kazi za sanaa.

Uchunguzi kifani ya 3: Tafsiri ya matukio ya kihistoria kwa kutumia herufi zikiwa kama kazi za sanaa.

Bibi Marwa kutoka Shinyanga huamua kutumia kitabu cha herufi juu ya namna watoto wanavyokumbuka uasi wa Soweto mwaka 1976. Amepanga kutumia kitabu cha Mbwa Wawili na Uhuru kama kitabu cha kiada kwa ajili ya kipindi. Anachukua baadhi ya barua fupi kuhusu uzoefu wa watoto kuhusu uasi huo. Baada ya kujifunza hili kwa uangalifu, Bibi Marwa anatambua kuwa barua zile zilikuwa ni maoni ya watu binafsi na alifikiri kuwa ni vizuri kulinganisha maoni hayo na ushahidi halisi wa kihistoria wakati wa kipindi. Kwa hiyo Bibi Marwa alikusanya na kupanga nyaraka na vitabu vya historia vinavyochunguza migogoro ya Kitongoijo cha Soweto katika miaka ya 1970. Alitengeneza majumuisho ya mawazo muhimu ya kutumia darasani.

Kwanza, aliwataka kila kundi kusoma barua zilizochaguliwa na watoto ndani ya kitabu cha Mbwa Wawili na uhuru na kuwataka kuangalia jedwali la matukio muhimu na mawazo yaliyowasilishwa na wanahistoria. Je, wanaona ufanano au utofauti katika maelezo ya tukio moja? Wanajadili kama maoni binafsi katika kitabu yanashadidiwa na ushahidi halisi wa kihistoria uliowekwa na wanahistoria.

Wanakubaliana kuwa zote zinawiana kitabu ni mtazamo wa watoto na unaweza kutofautiana kutokana na imani zao, lakini jedwali linabakia kuwa na ukweli.

Mwishoni, Bibi Marwa hutoa majumuisho ya utofauti kati ya ushahidi wa maoni binafsi na ushahidi halisi katika kujifunza ya kale.

Shughuli muhimu: Maonyesho ya baadhi ya historia yetu

Watake wanafunzi wako kuleta vitu vya zamani walivyo navyo majumbani-kama mavazi ya asili, vyombo vya kupikia, kazi za miti, vinyago, shanga, vyungu n.k

Kumbuka kwamba kwa wanafunzi wako vitu vya miaka ya 20 au

30 tu vitaonekana kama vya zamani sana. Sehemu muhimu ya zoezi hili ni kwa wao kukusanya ushahidi juu ya kazi za sanaa na kwa kuangalia vitu vingi vya zamani, kukuza baadhi ya mawazo ya jinsi maisha ya zamani yalivyokuwa. Kama unaweza hakikisha kuwa umekusanya baadhi ya vitu ili uweze kuonyesha kwa wale ambao hawana uwezo wa kuleta chochote.

Watake wanafunzi wako katika jozi kutengeneza ukurasa ( rejea nyenzo 2: kazi zangu za kisanaa ) kuonyesha pamoja na kazi za sanaa.

maonesho yakiwa tayari, waalike wanafunzi wengine kutembelea maonesho yako. Unaweza kuwaalika hata wazazi na jamii inayowazunguka kuja kuona maonesho. Unaweza kupata mawazo mengine kutoka kwa waalikwa kuhusu baadhi ya kazi zako za sanaa.

Nyenzo-rejea ya 1: Matumizi ya kazi za sanaa darasani

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Nafasi ya kushika kazi halisi za sanaa ni uzoefu pekee. Kwa sababu ambazo hakuna mwenye uhakika nazo, kitendo cha kushika kitu ambacho dhahiri kina historia na hadithi yake, huhamasisha kila mmoja. Bila shaka wanafunzi watakuwa wadadisi juu ya kazi za sanaa na hii itapelekea kuwa na mjadala mzuri.

Kushika kazi ya sanaa huwafanya wanafunzi kutumia hisia zao kukuza udadisi na ujuzi wa kutatua matatizo, kuimarisha uelewa wao wa wakati ule na kuwajali watu wa kale.

Nini lengo la kipindi cha kazi za sanaa?

Vipindi vya kazi za sanaa vinaweza kutumika kwa:

  • kuwapa motisha wanafunzi mwanzoni mwa mada;
  • kuwavutia na kuvuta usikivu wa wanafunzi
  • kupanua ufahamu wao juu ya mada wanayojifunza
  • kuwapelekea kujifunza kiundani na kwa mapana zaidi
  • Kusimama kama daraja kati ya baadhi ya masomo tofauti na vitu vinavyozungumziwa
  • Kupembua ukuaji wa ufahamu wa wanafunzi mwishoni mwa kipindi. Maswali gani niulize wakati wa kipindi cha kazi za sanaa?

Aina ya maswali unayouliza yatategemea ni kazi gani ya sanaa unatumia. Maswali ya hapa chini yatakusaidia kupata majibu ya kazi za sanaa.

Maswali kuhusu tabia za wazi za kitu

  • Inaonekanaje? Hisia, harufu na sauti yake?
  • Ni kikubwa kiasi gani?
  • Kina umbo gani?
  • kina rangi gani?
  • Kina uzito gani?
  • Je kina alama yoyote inayotuonyesha namna kilivyotengenezwa, kilivyo tumiwa au kutunzwa?
  • Kimetengenezwa kwa kutumia nini?
  • Ni cha kawaida au chakipekee?
  • Ni kizima au sehemu ya kitu chote?
  • Je kipo katika hali nzuri au kimechakaa?
  • Je, kimebadilishwa kimeigwa, kimerekebishwa au kimegeuzwa?

Maswali kuhusu ubunifu na matengenezo ya kitu

  • Kimetengenezwa kwa vifaa gani?
  • Kwanini vifaa hivyo vilichaguliwa?
  • Je vifaa tofauti vingetumika?
  • Kinavutia kukiangalia?
  • Kinaweza kuwa kilitengenezwa lini na wapi?
  • kilitengenezwa kwa mkono au kwa mashine?
  • Nani anaweza kuwa alitengeneza?
  • Kimetengenezwa katika kipande kimoja au vipande tofauti?
  • Kinaweza kuvunjwa vipande vipande?
  • Kimeunganishwaje?
  • Kinawezaje kufanya kazi?
  • Kimerembwa au kawaida?
  • Kuna alama zozote/taswira kwenye kitu?
  • Hivi vinatuambia nini kuhusu watu waliokitengeneza au wanaokimiliki na wakati tunapojifunza?

Maswali kuhusu umuhimu na thamani ya kitu 

  • Kifaa hicho kilileta utofauti gani katika maisha ya watu?
  • Kilikuwa na umuhimu gani: watu waliokitengeneza au waliokimiliki; watu wa leo?
  • Kinatuambia nini kuhusu watu waliokimiliki?
  • Kimetengenezwa kwa wingi, mara chache au kwa upekee?
  • Ni muhimu kiuchumi/kihistoria/kiutamaduni?
  • Ni kwa namna gani ni muhimu leo?

Maswali kuhusu kazi ya kifaa

  • Ni nini?
  • Kwa nini kilitengenezwa?
  • Jinsi gani kinaweza kuwa kilitengenezwa?
  • Nani anadhaniwa kukitumia?
  • Ujuzi gani ulihitajika kukitumia?
  • Kingeweza kutumiwaje?
  • Wapi kinadhaniwa kutumiwa?
  • Je kinadhaniwa kutumiwa na vitu vingine?
  • Matumizi yake yamebadilika?

Kufundisha kwa kutumia vitu-baadhi ya mbinu

Baadhi ya mbinu zilizoelezewa hapo chini zinaweza kutumiwa na wanafunzi wakati wa kusoma nyaraka, machapisho na rangi. kichokoo kinachoonekana

Vitu vinaweza kutumika kuanzisha majadiliano mwanzoni mwa kipindi. Vitu hivyohivyo vinaweza kutumika kurejea walichojifunza wanafunzi na kuona kama moja ya mawazo na ufahamu wao umebadilika kutokana na kipindi hicho.

utafiti wa kihistoria

Uchaguzi wa vitu unaweza kutumika na wanafunzi kwa mazoezi ya utafiti kihistoria-kupata taarifa kutoka vyanzo. Wape muda wanafunzi kuona vitu kwa umakini kabla ya kutafiti baadhi ya maswali yafuatayo:

  • Kimetengenezwa kwa kutumia nini?
  • Vifaa au mbinu gani zilihitajika kukitengeneza?
  • Nani anadhaniwa kukitengeneza?
  • Je kulihitajika ujuzi wa kipekee kukitengeneza?
  • Kimerembwa? Namna gani?
  • Nani anadhaniwa kukitumia?
  • Kilikuwa ni kwa matumizi gani?
  • Je kilifanya kazi au kilitumika kwa njia nyingine?
  • Kinauzito au ukubwa kiasi gani?
  • Ni cha muhimu au kitu adimu? 

Kulinganisha na kuvihusianisha vitu

Tumia vitu viwili au taswira kwa pamoja na watake wanafunzi kulinganisha, kutafiti ufanano na utofauti kati ya vitu na taswira. Tumia makundi ya vitu na ongelea uhusiano kati yao.

Uwakilishi na ufasiri

Baadhi ya kazi ya sanaa zinaweza kuonyesha ushahidi wa mtazamo fulani. Nani alitengeneza kitu hicho na kwa malengo gani? Ni kitu halisi au propaganda tu? Kinatupa habari yote? Kinatuambia nini?

Shughuli nyingine zitumiazo vitu ni

Shughuli za utabiri-waonyeshe wanafunzi kifaa na watake kufikiria kipindi gani cha kihistoria kinahusiana na kifaa hicho.

Uchunguzi kifani-wanafunzi wanaweza kutumia kitu kimoja au vingi kujenga uchunguzi kifani, kwa mfano maisha ya Afrika Mashariki kabla ya kuja Waarabu.

Makundi-wanafunzi wanaweza kukusanya vitu katika jozi zinazokuwa na vitu fulani vinavyofanana (kama vifaa fulani, nchi vinakotoka, namna vilivyotumika). Wanafunzi wanaweza kufikiria namna ya kutengeneza makumbusho kwa kuweka vitu katika makundi na kwa namna tofauti.

Uandishi wa kichwa cha habari-wanafunzi wanaweza kuandika vichwa vyao vya habari au alama za maonyesho, au kutoka mtazamo wa kisasa au kama walikuwa wanandika kwa muda huohuo wakati kitu kinatengenezwa.

Hisia zenye ufahamu-wanafunzi wanaweza kuorodhesha sifa zinazoelezea namna wanavyojisikia kuhusu kitu, wakionyesha ufahamu na kuguswa juu ya vitu husika.

Majibu ya ubunifu-wanafunzi wanaweza kuitikia vitu kupitia ubunifu, tamthilia au sanaa za maonyesho.

Ni masomo gani yanaweza kusaidiwa na matumizi ya kazi za sanaa?

kujifunza kutokana na vitu ni msaada kwa somo katika mitaala mbalimbali

  • Historia: ufahamu wa mtiririko, hisia na ujuzi wa msingi
  • Sayansi: tabia za vitu, uchunguzi, kulinganisha, mchanganuo, na ujuzi wa kudadisi.
  • Kingereza: kuuliza na kujibu maswali, nyenzo za muktadha.
  • Tamthilia: nyenzo chokoo, kujenga hisia
  • Sanaa na ubunifu: nyenzo chokoo, nyenzo za muktadha

Nyenzo-rejea ya 2: Sanaa zangu

Matumizi ya wanafunzi

Jina la mwanafunzi

Kazi ya sanaa yangu

Sanna hii imeundwa kutokana na

Sanaa hii ilitumika kwa

Hivi ndivyo sanaa hii ilivyotumika

Hivi ndivyo sanaa ya zamani inavyodhaniwa kuwa