Ruka hadi kwa yaliyomo
Printable page generated Alhamisi, 14 Nov 2024, 23:27
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Alhamisi, 14 Nov 2024, 23:27

Namba ya moduli 3: Kuangalia sanaa

Sehemu ya 1: Kuchunguza Kazi za Sanaa zionekanazo

Swali Lengwa muhimu: Unachunguzaje sanaa za maonyesho na wanafunzi wako?

Maneno muhimu: sanaa; vinyago; maonyesho; ughushi; ujuzi wa kufikiria; ufundi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umejijengea ujuzi wa kuendesha shughuli za darasani na majadiliano yanayohusu eneo la sanaa zinazoonekana;
  • Umejenga uelewa wa wanafunzi juu ya sanaa zinazoonekana ambazo zinatengenezwa na kutumika katika jamii;
  • Umefanya kazi ya sanaa kwa vitendo na wanafunzi wako.

Utangulizi

Baadhi ya sehemu zinazofurahisha sana katika urithi wa jamii ni sanaa zake na ufundi wa jadi. Jinsi hivi vitu vya mapambo na vya kila siku, vinavyotengenezwa na kupambwa, na muziki na michezo inayotolewa, vinatoa mwelekeo wa thamani halisi na mahitaji ya jamii.

Sehemu hii itakuonyesha jinsi ya kuwahusisha wanafunzi wako na kazi za sanaa zionekanazo zinazowazunguka na jinsi ya kutumia hizi sanaa kuamsha ubunifu darasani kwako.Kazi yako ni kuwasaidia wanfunzia kuelewa kuwa kazi za sanaa hufanya mazingira yavutie. Vilevile,utahitaji kujenga uelewa kuwa sanaa ni njia ya mawasiliano na ni njia ya kueneza utamaduni.

Somo la 1

Uchunguzi wa sanaa na ughushi na jinsi vinavyotengenezwa unaweza kutoa mwanga kwa wanafunzi juu ya utamaduni wao na historia ya jamii. Pia, inakupa wewe, mwalimu, nafasi ya kubuni vizuri masomo kwa vitendo, kwa sababu kuna vitu vingi sana vya kusisimua na kazi za sanaa ambazo zinaweza kuletwa darasani kuamsha utashi, pamoja na kutoa mawazo kwa kazi za sanaa za wanafunzi.

Alama ambazo zinapatikana kwenye sanaa, mara nying zinahusiana na uadilifu na dini za jamii husika. Kwahiyo, ni muhinu kuwahimiza wanafunzi wako kuipenda sanaa-kuhifadhi urithi wao wa utamaduni na wasaidie waimaanishe katika mazingira yao. Hii ndiyo sababu tunawafundisha wanafunzi kuhusu sanaa.

Uchunguzi kifani ya 1: Kufikiria juu ya ughushi wa mahali hapo

Siku moja kabla ya somo la kwanza juu ya sanaa za asili, Bi. Kabalimu, kutoka mkoa wa Tanga Tanzania, aliwaambia wanafunzi wake watengeneze orodha ya ughushi unaotengenezwa katika jamii yao,iwe zamani au sasa. Walikuwa waongee na wazazi wao au majirani ili kupata hizi habari. Ili kuwafanya waanze kufikiria, aliwaonyesha baadhi ya mifano

ya ughushi, kama vile kikapu cha kusukwa kizuri cha Kimakonde na shanga za kuvaa shingoni za Kimasai.

Siku iliyofuata, wanafunzi waliteta orodha-Bi. Kabalimu alipitia kila moja na kuirudisha (angalia Nyenzo rejea ya muhimu 1: Kazi ya nyumbani ya kuorodhesha ughushi wa mahali hapo ). Alianza somo kwa kuwaambia wanafunzi wataje majina ya ughushi waliyojifunza, ambayo aliyaandika ubaoni. Yalikuwemo majina ya uchongaji, upakaji rangi na

michoro mbalimbali, silaha, vifaa vya nyumbani na vishirikishi. Bi. Kabalimu aliligawa darasa katika makundi madogo (angalia Nyenzo rejea ya muhimu: Kutumia makundi darasani kwako ) na kulipa kila kundi majina ya vitu viwili vya sanaa na maswali yafuatayo:

Elezea matumizi ya hivyo vitu.

Ni ujuzi gani unahitajika kutengeneza vitu hivyo? Ujuzi huu unafahamika kwa watu wengi?

Jinsi gani vitu hivi vinaweza kutunzwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya vizazi vijavyo?

Baada ya dakika 15, kila kundi liliwasilisha majibu yake kwa darasa zima. Bi. Kabalimu alitengeneza muhtasari kwenye makaratasi makubwa, na kwa kufanya hivyo, alijumuisha mawazo ya wanafunzi katika vipengele mbalimbali. Alitambua kuwa ilikuwa ni muhimu kuyajumuisha mawazo kulingana na jinsi yalivyopangwa.

Hizi karatasi zilibandikwa kwenye ubao wa matangazo wa darasa na kuachwa kwa muda wa juma moja ili wanafunzi wajifunze. Sio tu kwamba wanafunzi walikuwa wanajifunza kuhusu ughushi kwenye jamii yao, pia walikuwa wanapewa nafasi ya kujenga uwezo wa kufikiri.

Shughuli ya 1: Kuchangia mazwazo na kutengeneza sanaa za jadi na ughushi

Unaweza kuangalia katika mchoro Nyenzo rejea muhimu 2: makundi ya kuandaa aina za kazi za mikono na ughushi kukusaidia kupangilia somo hili

Kwenye majadiliano darasani, waambie wanafunzi wafikirie juu ya vitu vya sanaa asilia na ughushi wanavyovifahamu. Anza kwa kutoa mifano.

Jinsi wanafunzi wanavyotoa mawazo, yaandike ubaoni katika vipengele mbalimbali (angalia Nyenzo rejea muhimu 2).

Chunguza kila kifaa kilichosemwa kuwa ni sanaa ya uchongaji na liambie darasa lijadili ujuzi unaotakiwa ili kutengeneza hivyo vifaa, ni vipi na wapi vilitengenezwa, na ni jinsi gani vinasafishwa na kuhifadhiwa.

Fanya hivyo na kwa vipengele vingine, kwa vitu vingi kadri muda utakavyoruhusu.

Maliza somo kwa kuwaambia wanafunzi juu ya kipindi kingine cha sanaa, ambapo watachora picha au kutengeneza baadhi ya vitu. Tafuta sehemu ambapo vitu hivi vitaweza kuonyeshwa kulingana na vipengele vyake. Baadae vinaweza kuwa ni sehemu ya maonyesho ya shule.

Somo la 2

Vinyago vya jadi vya Kiafrika vilifikiriwa kuwa ni vitu vya muhimu sana kwa sababu vilifanya kazi muhimu ya mizimu katika imani za Kiafrika. Kusudi la kwanza la kutengeneza vinyago vya Kiafrika lilikuwa ni kwa ajili ya sherehe maalumu au shughuli muhimu za kijamii. Si kama Ulaya Magharibi amabako vinyago vilichukuliwa kama njia ya “kuuwakisha” mzimu, vinyago vya Kiafrika vilieleweka kuwa pale ambako mzimu “uliumbwa”.

Kwa maneno mengine, pale ambapo mtu anavaa kinyago, pamoja na vazi ambalo limefunika kuanzia kichwani hadi miguuni, mtu huyo kwa kweli “anakuwa” ni mfano wa mzimu amabao umekusudiwa kuwakilishwa, ukipewa uhai kwa kupitia ishara, sauti, shughuli mbalimbali na hata hali yao ya kupagawa.

Katika Uchunguzi kifani 2 , mwalimu hutumia kazi za vikundi kuwawezesha wanafunzi wake kufikiri na kuwaruhusu kubadilishana mawazo juu ya madhumuni ya vinyago tofauti. Katika shughuli 2, wanafunzi wako watatengeneza vinyago vyao wenyewe, wakiwa wametafakari maswali kama yale yaliyoulizwa kwenye uchunguzi kifani.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuchunguza alama na maana kwenye vinyago vya jadi vya Kiafrika

Bi. Sungi ni mwalimu wa sanaa katika shule ya Ihanja, mkoa wa Singida. Ameamua kufanya uchunguzi wa vinyago vya jadi vya Kiafrika akiwa na mitazamo mitatu akilini mwake:

Kuangalia juu ya uzoefu na matumizi ya kazi za sanaa Afrika nzima. Kuchunguza jinsi alama zilizo kwenye kazi ya sanaa zinavyopeleka maana halisi katika mtazamo wa kiutamaduni.

Kuwasaidia wanafunzi wake kutengeneza vinyago vyao wenyewe. Anapanga kutumia kama vipindi viwili vinavyofuatana vya somo la sanaa ili kufikia malengo yake.

Bi. Sungi anaanza kwa kuwaonyesha wanafunzi wake vitabu vya picha na majarida yaliyo na picha za vinyago vya jadi kutoka eneo lote la Afrika, kusini mwa jangwa la sahara. (Angalia Nyenzo rejea muhimu 3: Kinyago cha Afrika kwa mfano.)

Analiambia darasa, likiwa katika makundi, kuchunguza baadhi ya vitabu kwa pamoja na kupata matumizi ya kawaida ya vinyago katika maisha ya kijamii kwenye mazingira tofauti ya kiutamaduni. Kila kundi linaandaa orodha ya matambiko na kazi za kiutamaduni za vinyago vya Kiafrika.

Kwa kutumia Nyenzo rejea muhimu 4: Andalio la somo la vinyago vya Afrika ya Mashariki , Bi. Sungi anaendelea kuonyesha vinyago maalumu kutoka Afrika Mashariki, ambavyo ni vya mitindo mingi sana ikiendana na matambiko na ishara ya uwezo. Anakazia kwenye alama muhimu za vinyago. Baadaye anawapa wanafunzi wake muda wa kutengeneza vinyago vyao wenyewe.

Shughuli ya 2: Kutengeneza vinyago vinavyowakilisha hisia na ujumbe wa jamii

Kabla ya somo, kusanya pamoja vitabu vya picha na majarida yenye vinyago vya Kiafrika kutoka sehemu mbalimbali na, ikiwezekana, baadhi ya mifano ya vinyago halisi vya mahali hapo.

Waambie wanafunzi waziangalie nyenzo rejea muhimu ulizozikusanya kupata mwelekeo wa vinyago vyao wenyewe.

Wanavyopangilia vinyago vyao, wanafunzi wanahitaji kufikiria ni ujumbe gani wanataka vinyago vyao vibebe. Wakumbushe kuwa wanatakiwa kufikiria juu ya:

Alama za usoni; alama wanazoweza kutumia; jinsi ya kuteka hisia; rangi.

Waambie wapangilie vinyago vyao katika vipande vidogo vya karatasi/kadi kwanza, kabla ya kutengeneza picha kubwa au mfano wa vinyago kutokana na kadi hizo hizo.

Itabidi uwape vipindi vya sanaa kadhaa kwa ajili ya kazi hii. Onyesha vinyago vyilivyokamilika ili wote waone na alika madarasa mengine yaje yaone.

Somo la 3

Kutengeneza ughushi wao wenyewe ni muhimu kwa wanafunzi wako na watataka kushirikisha mafanikio yao kwa watu wengine. Katika sehemu hii, tunashauri kuwe na maonyesho shuleni ya ughushi na vitu vingine ambavyo vimetengenezwa na wanafunzi kama njia ya kuendeleza na kuhifadhi fahari ya wanafunzi wako katika urithi wao wa utamaduni. Ughushi kutoka kwenye jamii ya hapo ambao hauwezi kubebeka au haupatikani unaweza kuonyeshwa kwa kutumia picha zilizokatwa kutoka magazetini na vyanzo vingine.

Uchunguzi kifani 3 unaonyesha jinsi darasa moja, likifanya kazi kwa makundi, lilivyojihusisha kwenye hatua zote za maonyesho, kutoka

kwenye kuyaandaa hadi kuongea na wageni. Kwenye Shughuli muhimu , wanafunzi wako wataandaa onyesho ambalo wageni watatembelea bila wenyeji, hivyo kazi ya kuweka alama zinazojieleza na za kuvutia ni muhimu sana.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuonyesha ughushi shuleni siku isiyo ya masomo

Siku ambazo si za masomo za shule ya msingi ya Ilemela kwa kawaida hufanyika kuelekea mwishoni mwa mwaka wa shule. Bwana Koku, amabaye ni mwalimu wa sanaa wa wanafunzi wa drasa la nne, aliiambia kamati ya maandalizi ya siku hiyo kuweka sehemu kwenye chumba cha maonyesho ili darasa lake lionyeshe ughushi waliotengeneza darasani au waliokusanya kutoka vyanzo mbalimbali katika jamii. Ombi lake lilikubalika.

Katika kipindi cha maandalizi, Bwana Koku aliliongoza darasa lake kuandaa maonyesho. Aliwagawa wanafunzi katika makundi manne. Kundi la kwanza lilitakiwa kukusanya na kuweka utambulisho kwenye michoro yote, picha na vitu ambavyo vilitambulika kama vifaa vya nyumbani. Kundi la pili lilipewa kazi kwa upande wa vifaa vya muziki, kundi la tatu lilipewa kazi kwenye sehemu ya usonara na kundi la nne lilipewa upande wa uchongaji.

Shughuli zote hizo zilichukua vipindi viwili. Katika kipindi cha tatu, kulikuwa na kuelezea makusanyo hayo darasani kama ambavyo mtu angeweza kuelezea kwa wageni. Siku ilipowadia, darasa lilionyesha vitu vikiwa vimepangwa katika makundi manne, na wanafunzi wanne wakitoa maelezo kwa wazazi na wanajamii wengine waliotembelea meza ya maonyesho ya darasa.

Mwisho wa siku, meza ya ughushi ilizawadiwa kikombe cha kuwa meza bora kwenye chumba cha maonyesho.

Shughuli muhimu: Kuandaa maonyesho ya ughushi

Waambie wanafunzi wako walete darasani michoro, ughushi, vinyago, vyungu na vikapu iwe kutoka nyumbani au walivyotengeneza wakati wa vipindi vya sanaa.

Andaa kadi tano. Kwa kila kadi, andika moja ya maneno yafuatayo: wachoraji, wachongaji, wafinyanzi, mafundi seremala, wasusi. Ligawe darasa lako katika makundi matano na toa kadi moja kwa kila kundi.

Waambie kila kundi wachague vitu walivyoleta vinavyoendana na majina ya kadi zao na waviweke sehemu tofauti.

Baada ya hapo, yaambie makundi yalinganishe vitu. Majadiliano yatakayoendelea hapa ni muhimu kujenga uwezo wa wanafunzi wa kutofautisha na uwezo wa kufikiri; na pia yatasaidia kutambua mambo ya msingi wanayotaka kuyajumuisha kwenye utambulisho wa vitu.

Waambie kila kundi liandike jina na utambulisho wenye maelezo kwa kila kitu kwenye kundi lao.

Waambie kila kundi, wapange vitu vyao kwa ajili ya watu kuangalia, wakati wanafunzi wengine wakijifanya kuwa ni wageni. Waambie “wageni” watoe maoni yao ni jinsi gani makundi yangeweza kuboresha utambulisho wao.

Andaa labels za mwisho na lipe darasa lako muda wa kuandaa maonyesho.

Andaa orodha ya wanafunzi watakaojifanya wamekuja kutembelea maonyesho. Hii inaweza kufanyika muda wa mapumziko au muda wa chakula cha mchana tu.

Baada ya maonyesho,jadili na wanafunzi wako juu ya walichopata kutokana na uzoefu kwa misingi ya uelewa wa ughushi na kujihusisha kwao kwenye tukio kama hilo.

Nyenzo-rejea ya 1: Kazi ya nyumbani ya kuorodhesha kazi za ughushi za mahali hapo

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Jabali 6B, 02.10.2005, Majina ya Ughushi

Ngoma
GitaaHili ni gitaa ulilotengeneza?
Kijiko cha mti
ChupaFikiria tene. Hii chupa kweli ilitengenezwa katika jamii yako?
Chungu cha udongo 

Vizuri sana

Mchoro wa tingatingaHii ni nini?
Gari la kuchezea watotoMoja ya hiki kifaa kinatengenezwa kijijini kwako?
mkeka uliosukwa kwa mikono
 

Umfanya vizuri Jabali. Hapa umekusanya orodha nzuri ya ughushi. Hakikisha unaelewa ni zipi

zinatengenezwa katika jamii yako.

Nyenzo-rejea ya 2: Kazi ya nyumbani ya kuorodhesha kazi za ughushi za mahali hapo

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Nyenzo-rejea ya 3: Kinyago cha kiafrika

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Chanzo halisi: Cable, M. The African Kings. New York: Select Books

Nyenzo-rejea ya 4: Andalio la somo kuhusu vinyago vya Afrika ya Mashariki

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Chanzo halisi: Masks of the World, Website

Kwa jumla kuna aina tatu za vinyago; vya usoni, vya kichwani (ambavyo kama jina linavyooyesha vinavaliwa kichwani), na vya mwilini, ambavyo hufunika sehemu kubwa ya mwili wa mchezaji na vinategemewa kubadili mwonekano wake kutoka kwa watu wanaomfahamu. Vinyago vya mwilini wakati mwingine hufunika mwili tu na huvaliwa pamoja na vya usoni au vya kichwani.

Vinyago vyote huwakilisha mizimu au wazee waliokufa,na vilikuwa vikitumika sana kwenye sherehe za jando kama muonesho wa mwendelezo, hofu na uadilifu. Vilevile vilitumika kwenye ngoma na matukio ya sikukuu, kwa mfano sharehe za mavuno.

Vinyago vya kichwani (mapiko; umoja lipiko) vinafahamika sana kwa mfanano wake. Vingi vina nywele halisi za mwanadamu zilizonyolewa vizuri, nyuso nzuri na midomo ya wazi isiyokuwa na meno, masikio makubwa au vizibo vya mdomo. Vinatumika katika mchezo wa mapiko na michezo mingine. Japo kuwa vichwa vya wanaume na wanawake wote vinaweza kutumika, ni mara chache sana kuona vichwa vya wanawake. Mchezaji hupumua na kuona kupitia tundu dogo lililoko mdomoni.

Mapiko si jina linapewa kwa vinyago (kwa kawaida vya kichwani) tu, bali pia ni jina la ngoma, jina la nguvu inayotisha, na vilevile ni jina la moja kati ya hatua za unyago wa wanaume, wakati mhusika anapoingizwa kwenye siri za Mapiko. Vinyago vyenyewe vimetengenezwa katika sehemu ya siri porini inayojulikana kama Mpolo, ambayo wanawake wanakatazwa kupafikia. Pale vinapokuwa havitumiki, vinyago huwekwa

Mpolo, na kijadi vilichomwa moto vilipovunjika au kubadilishwa na vingine vipya.

Matokeo

Wanafunzi watajenga tathmini mbalimbali za vinyago na watatengeneza vinyago;+

Vifaa

karatasi ya kuchorea

kadi

penseli

udongo

karatasi katika rangi anuwai

kalamu za rangi

rangi ya bango

shanga, magamba n.k

mkasi

gundi

1.     Kusanya baadhi ya picha za vinyago za kuwaonyesha wanafunzi wako.

2.     Jadili taswira za vinyago na uashiria wake.

3.     Waambie wanafunzi watengeneze mchoro wa mwanzo wa kinyago.

4.     Wafuatishie michoro kwenye kadi halafu wachore vinyago vyao. Waambie wanafunzi kuwa wanaweza kubadili baadhi ya vitu kwenye nyuso za vinyago vyao. Mfuatisho ni mwongozo tu wa mahali pa kuweka macho na mdomo endapo wangependa kuvivaa vinyago vyao.

5.     Paka vinyago rangi na viache vikauke.

6.     Toa vinyago na andaa vitu ambavyo vitaambatana navyo kama nywele na mkanda wa kukishikilia kichwani.

7.     Wape wanafunzi muda wa kupamba vinyago vyao.

Sehemu ya 2: Kuandaa Shughuli za Sanaa kwa Vitendo

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kuuliza maswali kuhusu na kutengeneza sanaa ya mahali hapo?

Maneno muhimu: ustadi; utafiti; mawasilisho; vitendo; utamaduni

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umepata ni nini wanafunzi tayari wanajua juu ya ufundi wa mahali hapo;
  • Umewapanga wanafunzi wako katika makundi madogo kufanya shughuli za kiutafiti;
  • Umeandaa shughuli za vitendo ili kuwasaidia wanafunzi watengeneze na kutathimini vifaa vyao vya ufundi.

Utangulizi

Wanafunzi wengi tayari watakuwa na uelewa juu ya ufundi wa mahali hapo na baadhi yao wanaweza wakawa na ujuzi mkubwa wa kutengeneza baadhi ya hivyo vifaa. Wigo wa ufundi mahali hapo unaweza kujumuisha vitu kama utungaji shanga, ufinyanzi, uchongaji, uchoraji na uhunzi.

Ni muhimu kutambua wanafunzi wanachokifahamu kwanza, na kutumia huo ufahamu kama msingi wa kupangilia shughuli kuzunguka ufundi wa mahali hapo. Katika sehemu hii, utawahimiza wanafunzi kuchangia mawazo na kujenga uelewa wao juu ya thamani na matumizi ya huu ufundi wa jadi. Njia mojawapo muhimu ni kuwaruhusu wanafunzi kutengeneze zana zao wenyewe; hii hutoa nafasi kwao kupangilia na kutathimini kazi zao.

Somo la 1

Ufundi wa jadi wa jamii utakuwa na maana zaidi kwa wanafunzi wako kama utawahusisha katika kufanya baadhi ya hizi kazi za ufundi. Sehemu hii inaibua kile wanafunzi wako wanachoelewa juu ya ufundi wa mahali hapo pamoja na watu wanaotengeneza zana hizo katika mazingira ya vitendo. Inakupa wewe nafasi ya kujenga ujuzi wa kuuliza maswali, na inakuonyesha njia ya kuwasaidia wanafunzi wako kuuliza maswali yao wenyewe.

Uchoraji ni njia moja ambayo jamii nyingi zinaweza kurekodi matukuio ambayo yametokea. Vilevile ni njia ambayo hutumia kufikiria sana, hivyo ni nzuri kwa wanafunzi kuelezea mawazo na hisia zao.

Uchunguzi Kifani 1 unaelezea jinsi mwalimu mmoja alivyowahimiza wanafunzi wake kupaka rangi na kuchora. Katika Shughuli 1, unatumia majadiliano ya vikundi vidogo kuibua nini wanafunzi wanaelewa juu ya ufundi wa mahali hapo, matumizi yake na jinsi zinavyotengezwa. Hii inaweza kuwa ni hatua ya mwanzo ya kufanya utafiti zaidi juu ya ufundi katika shughuli itakayofuata.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuangalia michoro

Bi Moyosola kutoka kusini-magharibi mwa Nigeria alikuwa anafundisha upakaji rangi. Alitaka kulihimiza darasa lake kupaka rangi na kuchora. Aliamua kuanza kwa kuwaambia wanafunzi wake watazame baadhi ya picha zilizochorwa na wachoraji wa kisasa wa Nigeria kutoka katika eneo lao.

Alikuwa na nakala moja kwa kila picha aliyoaibandika ubaoni. Aliwaambia wanafunzi watazame hizo picha na waseme ni kitu gani walikipenda na kipi hawakukipenda. Aliwauliza kama mmoja kati yao aliwahi kupaka rangi au kuchora, na kama ndivyo, alipaka rangi au kuchora nini na lini. Wengi hawakuweza kuwa na karatasi na kalamu, lakini walisema huchora picha mchangani nje ya nyumba wanazoishi. Walisikitika kwa kuwa picha hizi hazikuweza kudumu.

Bi Moyosola aliwaambia wanafunzi wake wafikirie kitu ambacho wangependa kupaka rangi au kuchora. Aliwapa karatasi na penseli, na kuruhusu vipindi viwili vya sanaa wavitumie kwa kuchora na kupaka rangi. Wengi walichora picha zao wenyewe na wengine walifuatishia zile picha za kisasa za Nigeria.

Bi Moyosola alizionyesha hizi picha ili kila mmoja achangie mawazo.

Shughuli ya 1: Kuuliza maswali juu ya ufundi wa mahali hapo

Kusanya baadhi ya mifano ya ufundi wa mahali hapo. Ungeweza kutumia mifano hiyo hiyo kwa makundi yako yote, au mfano tofauti kwa kila kundi.

Pangilia darsa lako katika makundi madogo ya wanafunzi wanne/watano.

Waambie kila kundi wajadili kitu wanachofahamu katika ufundi wa aina moja. Waambie waanze kwa kujibu maswali yafuatayo (yaandike maswali haya ubaoni).

Ni kitu gani? Kinatumikaje?

Kilitumikaje siku za nyuma? Kinatengenezwaje?

Wape wanafunzi dakika 10–15 kujadili haya maswali na kufikiria swali moja zaidi la kuuliza kuhusu ufundi. Ungeweza kuwaambia wanafunzi wakubwa wachore na kuandika mawazo yao kwenye mchoro.

Halafu, waulize baadhi ya majibu yao. Unaweza kukuta kuwa hawakujibu maswali yote, hivyo waeleze kuwa wataenda kufanya utafiti ili kukusanya habari zaidi katika Shughuli 2.

Somo la 2

Kuujadili ufundi wa mahali hapo au silaha za asili au mavazi inahamasisha sana kwa wanafunzi walio wengi kwa kuwa wanaweza kuona uhalisia wa vitu hivi katika maisha yao.Wanafunzi wanapovutiwa, inakuwa pia ni rahisi kwako kusimamia tabia zao. Kwenye Uchunguzi kifani 2, kuvutiwa huku kunasababishwa na mgeni. Unamfahamu mtu yeyote ambaye ana muda wa kutembelea darasa lako? Umewauliza wanafunzi kama kuna mtu yeyote wanamfahamu?

Vilevile kama unatumia zaidi njia shirikishi kama vile, kuwagawa wanafunzi wawili wawili au katika makundi, wanafunzi wanaweza kuelewa zaidi kwa kufanya kazi pamoja. Katika Shughuli 2, wanafunzi wanafanya kazi wawili wawili kutafuta majibu ya maswali yao wenyewe. Hii nayo pia inawapa motisha sana wanafunzi.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuangalia historia ya zana asilia za kilimo

Bwana Msane aliwataka wanafunzi wake kutafuta habari zaidi kuhusu zana za asili zinazotumika kwa kilimo. Aliamua kuwapa nafasi ya kuangalia picha na ughushi, na kuandika juu ya walichokiona. Lakini kwanza,alilishangaza darasa lake. Alikuwa amemuomba mwanajamii mmoja ambaye alikuwa na mkusanyiko wa zana za asili kuzileta baadhi yake darasani.

Wanafunzi waliufurahia huo ugeni na waliweza kukusanya habari nyingi kuhusu zana za asili na kuongezea katika utafiti wao. Koleo la zamani ambalo lilikuwa la babu yake na mgeni liliwasisimua sana wanafunzi hasa kwa sababu ya umri wake mkubwa.

Baada ya ugeni, Bwana Msane aliligawa darasa lake katika makundi madogo na kuwapa kila kundi picha –baadhi ya makundi yalichangia picha moja kwa kuwa hakuwa na picha nyingine za kuwapa.Aliwaeleza kuwa walitakiwa kuzijadili hizo picha na baadae kuandika habari fupi kuhusu kila zana ya kwenye picha ilivyokuwa ikitumika.

Alieleza kuwa wangeweza kutumia karatasi ya maswali na kufikiria juu ya kitu gani cha kuandikia (angalia Nyenzo rejea ya muhimu 1: maswali ya utafiti kuhusu zana za asili ). Wanafunzi walitumia muhtasari wao kutoka kwa mgeni na pia kutoka kwenye baadhi ya vitabu ambavyo Bwana Msane alikuwa anavyo. Walifanya kazi pamoja kwenye makundi yao na kuandika. Mwishoni, kila kundi lilitoa lilichoandika kwa darasa zima.

Shughuli ya 2: Kutafiti ufundi wa mahali hapo

Waambie wanafunzi, wawili wawili, wachague ni zana zipi wanataka kuzitafiti zaidi.

Kila kundi la wanafunzi wawili wawili linaweza kuchagua kati ya kutafuta maelezo kwenye vitabu au kumhoji mtu katika jamii yao, ikiwa ni hatua ya kuanzia.

Halafu, waambie wafikirie aina ya maswali wanayouliza ili yawaongoze wapate maelezo sahihi, kama vile: “Nini matumizi ya asili ya hili bakuli?” Jadili baadhi ya majibu na muamue kwa pamoja kama yanatoa mwelekeo kuhusiana na lengo la utafiti. Kila kundi la wanafunzi wawili lichague maswali yake.

Kila kundi lifanye utafiti kwa kutumia maswalli yake, na njia yao ya utafiti waliyochagua. Kwa wale ambao watatumia vitabu kama vyanzo vya habari, utahitaji kutoa vitabu au makala kutoka vitabuni au magazetini, na wengine uwape muda wa kufanya mahojiano.

Kama wanapata tatizo la kupata habari kwa kutumia njia moja, wanaweza kutumia njia nyingine vilevile. Wape muda wa kutosha kwa ajili ya utafiti na waongoze wanapopata ugumu.

Waambie kila kundi watengeneze bango ili kuonyesha majibu yao

Tathmini kazi ya wanafunzi wako kwa kutumia Nyenzo rejea ya muhimu 2: Karatasi ya kutathimini mawasilisho ya utafiti .

Somo la 3

Unapojifunza mada ya vitendo kama kazi za ufundi, ni muhimu wanafunzi wako wakapata nafasi ya kutumia vifaa vya kujitengenezea wenyewe au walau waone mtu akivitumia kutengeneza vitu vya ufundi.

Uchunguzi kifani 3 unaonyesha jinsi mwalimu mmoja alivyokusanya udongo wa mfinyanzi kutoka pembeni mwa mto ili wanafunzi wake waweze kutengeneza vyungu vya udongo wao wenyewe. Kwa kuwapa vifaa na kuangalia nini wanachoweza kufanya, wanafunzi wanapata mwanga mzuri wa ujuzi wanaohitaji. Kama una uhakika wa upatikanaji wa vifaa,

waandalie wanafunzi wako watengeneze stadi zao wenyewe.Hizi zinaweza baadae kuonyeshwa kwa wanafunzi wengine au kwa wazazi. Kwa wanafunzi wakubwa, wahimize wathamanishe kazi zao-nini walichohisi kimeenda vizuri? Nini wangeweza kuboresha hapo baadae?

Shughuli muhimu inaelezea jinsi ya kuandaa maonyesho ya ufundi. Hii ni njia nyingine ya kuwahamasisha wanafunzi na kuwawezesha kuelewa vizuri uwezo wa ufundi wa mahali hapo.

Uchunguzi kifani ya 3: Kutengeneza vyungu

Bi. Kapunga alikuwa anafundisha somo juu ya vyungu vya asili. Alianza kwa kuwataka wanafunzi watoe uzoefu wao juu ya vyungu vya asili na vifaa vingine. Wanafunzi walikuwa na uelewa mzuri juu ya matumizi ya vifaa hivyo wakati wa mavuno na wakati wa sherehe za ndoa na za kidini. Wanafunzi vilevile waliongelea juu ya vyungu tofauti wanavyovifahamu, kama vile vya kuhifadhia mapambo. Wakati wanaongea hayo, Bi. Kapunga alitengeneza orodha ya vyungu vya asili ubaoni.

Bi. Kapunga alikuwa ameleta baadhi ya vyungu ambavyo alivipata kwa watu katika jamii anayoishi. Aliwaambia wanafunzi nao wapeleke vyungu walivyokuwa navyo nyumbani ili waweze kuangali maumbo n.k. Baadae, aliwaonyesha jinsi ya kutengeneza chungu kidogo kutokana na udongo aliokuja nao kutoka mtoni. Aliwapa kila kundi la wanafunzi wawili udongo kidogo watengeneze chungu na kukipamba kwa njia yoyote ile waliyoipenda.

Aliwahimiza waangalie mitindo ya asili, na kutoka hapo ndipo wajenge mitazamo yao wenyewe. Vyungu vya wanafunzi viliachwa ili vikauke pembeni mwa darasa ambapo kila mmoja angeweza kuviona. Bi. Kapunga alifurahishwa sana na kazi ya wanafunzi.

Nyenzo rejea muhimu 3: Kutengeneza vyungu inatoa taarifa za msingi.

Shughuli muhimu

Wanafunzi wako wanapokuwa wamemaliza kufanya utafiti juu ya zana waliyoichagua, mualike mtaalamu mmoja wa mahali hapo aje awaonyeshe jinsi zana hizo zinavyotengenezwa, kwa mfano, utungaji shanga au uchongaji, ndipo wanafunzi wanaweza kutambua zaidi ni kwa nini na kwa jinsi gani wanafanya ufundi.

Halafu, waulize wanafunzi wako ni kwa jinsi gani wangependa kuwasilisha utafiti wao na wangependa wafanye hivyo kwa nani. Lipangilie darasa lako katika makundi ambayo yanapendezwa na ufundi wa aina moja au unaofanana ili wajadili mawazo yao.

Jadili baadhi ya mawazo yao.

Kubaliana nao kuhusu tarehe na sehemu kwa ajili ya hili.

Toa muda wa kutosha kwa kila kundi kuandaa kitabu chake, bango, onyesho, uthibitisho wa jinsi ya kutengeneza zana au mawasilisho kwa kutumia mdomo.

Wafanye majaribio ya tukio na waambie kila kundi liwasilishe kazi zake

Siku yenyewe, darasa au shule nyingine, au wazazi wanaalikwa kuja na kuona kazi za wanafunzi. Kila kundi linasimama na kazi zake na kuelezea kwa wageni. Maelezo kwa mdomo yanafuata baada ya kuwa watu wameona zana zilizoonyeshwa.n.k.

Nyenzo-rejea ya 1: Maswali ya utafiti juu ya vifaa vya jadi na kazi zake

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Angalia picha hii kwa makini. Fikiria juu ya mambo yote unayoyaona kwenye picha hii.

Imenakiliwa kutoka: Verizon 827, Website

1.     Ni vifaa gani unaviona kwenye picha?

2.     Ni nani anavitumia?

3.     Huyo anayevitumia, anavitumia kwa ajili gani?

Imenakiliwa kutoka: IFAD, Website

1.     Ni zana gani unaziona kwenye picha?

2.     Nani anazitumia?

3.     Huyo anayezitumia, anazitumia kwa ajili gani?

Nyenzo rejea 2: Tathimini ya mawasilisho ya utafiti

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Jina la mwanafunzi:                                            

Tarehe:        

Darasa:           

Kipindi cha maonyesho mwanafunzil:Alifani Kiwa venaAlifaniKiwaAnahitaji msaada
Alionyesha kifaa halisi cha ustadi, mchoro, au mfano wa picha.
Alikipa hicho kifaa jina.
Alijibu swali la utafiti.

Maoni ya mrejesho:                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                            

Mwalimu:                                

Nyenzo rejea 3: Kutengenza vyungu

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Mfano wa kutumia gurudumu la ufinyanzi

Udongo wa mfinyanzi unaweza kutengenezwa vyombo kutokana na sifa zake za pekee. Muundo wa udongo wa mfinyanzi una tabia ya ‘plastiki’ unayoufanya utengenezwe katika maumbo mbalimbali. Vifaa hivi vikiwekwa kwenye joto la kutosha vinabadilika kuwa katika hali ya mwamba mgumu, na hivyo kuwa vya kudumu. Udongo wa mfinyanzi unatokana na vitu asilia vinavyopatikana ardhini, kwa maana hiyo, unapatikana duniani kote, chini ya miguu yetu. Udongo wa mfinyazi uliwahi kutumiwa karibu na tamaduni zote, na kwa matokeo ya pekee kabisa. Vyungu vinaweza kutenengezwa kwa kutumia mikono na udongo uliochanganywa na maji.

Mfinyazi, anauandaa udongo kwa mikono yake. Vidole vinatumika kutengeneza sehemu ya chini ya chungu, halafu zinafuatia kuta katika umbo la silinda. Halafu mfinyanzi taratibu hutengeneza umbo analolitaka, kwa kutumia ncha za vidole vyake, kadiri gurudumu linavyozidi kuzunguka. Pindi kazi itakapokuwa tayari, gurudumu lililoko kwenye chungu huondolewa. Mchakato huu hurudiwa kwa ajili ya kutengeneza chungu kingine.

Wakati chungu kinapokuwa kimekauka, kinaweza kusawazishwa. Vishikio vinawekwa kwenye hatua hii. Baadhi ya aina ya mapambo yanaweza kuongezwa.

Pindi vyungu vinapokuwa vimekauka kabisa, vinaweza kuchomwa kwenye tanuru. Hii hutoa vyombo vigumu na vyepesi.

Kila chungu kinatumbukizwa moja kwa moja kwenye ndoo yenye malai kwa ajili ya kung’arishwa.

Pindi tanuru linapojaa, mlango wake unafungwa. Moto unaachwa uendelee kwa masaa 18. Vyungu vinaungua taratibu hadi joto linafikia nyuzi 1,250 °C. Katika hatua anuwai wakati moto unawaka, tanuru linaishiwa hewa ya oksijeni. Hali hii husababisha oksijeni iondolewe kwenye udongo wa mfinyanzi na ving’arisho, kitendo ambacho hupelekea mng’aro zaidi

Mfano wa kutumia mfinyo kwenye kutengeneza chungu

Kwa kuufinya udongo, unaweza kutengeneza vitu kama wanyama au bakuli, chungu, kikombe n.k. Wakati aina hii ya ufinyanzi inaonekana kuwa ya msingi, unaweza kuelewa tabia za udongo unaofanyia kazi pamoja na kujua mipaka yake (Unakunjika kirahisi? Unakauka haraka? n.k)

Kutengeneza bakuli, chungu au kikombe, anza na fundo la udongo. Kandamizia kidole gumba chako katikati, halafu finya kuta zake kwa juu.

Geuza chungu wakati unafinyanga. Hii itakusaidia kuweka unene wa kuta unaofanana.

Taratibu weka sehemu ya chini kwenye uso wa kitu ulio sawa ili kutengeneza usawa katika sehemu ya chini ya chungu.

Mfano wa chungu cha jadi – chungu cha kutunzia bangili cha Kiafrika

Chungu hiki cha jadi kuhifadhia bangili.

Imenakiliwa kutoka: Hoboken Pottery, Website and JH Pottery, Website.

Sehemu ya 3: Kutumia ngoma kujifunza

Swali Lengwa muhimu: Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia ngoma kukuza ujifunzaji na ustawi wa mtu?

Maneno muhimu: Ngoma , Utamaduni, Mila, Mabadiliko

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umegundua njia za kuonyesha namna mila ya ngoma za kiafrika zinavyoweza kueleza mahitaji ya jamii na maadili yake;
  • Umewasaidia Wanafunzi wako kuelewa asili ya mabadiliko ya mila kupitia ngoma ya kufaa;
  • Umeielezea mila ya ngoma ili kuboresha ujifunzaji na makadirio, na kujenga ustawi wa mwanafunzi.

Utangulizi

Sanaa kwa ujumla ni sehemu muhimu ya utamaduni wa watu na ngoma ina nguvu na kipimo tosha cha tamaduni nyingi. Ngoma ni sehemu ya kila sura ya maisha ya Kiafrika. Aina nyingi za ngoma zenye asili ya Afrika, ingawa zina mizizi katika wakati uliopita, zimebadilika au zimepotea; hivyo kuhamasisha utashi katika ngoma kutazilinda zile ambazo bado zinatumika.

Sehemu hii itakusaidia kujenga njia za kutumia ngoma darasani. Inachunguza mila na tamaduni za ngoma katika Africa, pamoja na njia mpya unavyoweza kutumia ngoma katika mtaala.

Somo la 1

Kuwasaidia wanafunzi wako watambue thamani ya ngoma za kimila za Kiafrika ni sehemu muhimu ya kufundisha sanaa. Kujifunza kuhusu sanaa mara nyingi kumejikita katika masimulizi ya zamani.

Pia, sanaa inawawezesha watu kuelezea maana katika maisha yao ya kila siku na kuwasaidia kujenga hisia za kujitambua na kujithamini.

Uchunguzi Kifani 1 na shughuli 1 itakusaidia kuzingatia pamoja na wanafunzi wako namna mila zinavyobadilika na kutoweka, na mdahalo iwapo hili ni jambo zuri au baya.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuchunguza Wavenda na domba

Bi. Sylvia Msane anafundisha katika shule ya msingi Sebokeng, mji ulioko kusini mwa jiji la Johannesburg Afrika Kusini.

Sylvia ameolewa na mwanaume mwenye asili ya Kizulu na wanaongea kiingereza na Kizulu nyumbani. Hata hivyo, mababa wamama yake wanatoka venda. Sylivia anahusisha kwamba wanafunzi wake kama walivyo vijana katika Afrika kusini, wanajua kidogo kuhusu vyanzo vya kimila. Sylvia anafikiria msemo uliorithishwa kwake ‘Umuntu ngu muntu nga bantu’ ‘Mtu ni mtu kwa sababu ya watu wengine’

Ameamua kuwaambia wanafunzi wake hadithi ambazo bibi yake alimhadithia alipokuwa mtoto kuhusu watu wa Venda (angalia nyenzo rejea muhimu 1: Hadithi za ngoma za Wavenda). Baada ya kuwaeleza namna watu wa venda walivyokuja kuishi kaskazini mwa Afrika ya Kusini, anawaonyesha nguo za kimila za kivenda na picha ya mabinti wakicheza domba. Mwanafunzi mmoja anauliza wanachofanya hao wanawake. Sylvia anafafanua kuwa hawa wanawake ni kama wamemaliza kufundwa/jando na wanacheza kama nyoka.Anawaeleza hadithi nyingine kuelezea umuhimu wa nyoka huyu na wanagundua namna ya ngoma ya domba inavyosherekea uwezo wa kuzaa wa mabinti (angalia nyenzo rejea muhimu 1). Mwanafunzi mwingine alimuuliza kama alifundwa katika njia hii na anaelezea kuwa hakufanyiwa hivyo. Maisha ya watu na vipaumbele vimebadilika na mila nyingi tokea zamani zimekufa. Wanajadili iwapo ni vizuri au vibaya kwa hili lililotokea.

Nyenzo rejea ya muhimu 2 : Mila za kienyeji inakueleza kuhusu mitindo ya ngoma katika Tanzania.

Shughuli ya 1: Kuchunguza ngoma za asili za Kiafrika hapo zamani.

Chunguza kutoka darasani mwako, wanafunzi wenzio au wanajamii kama kuna wachonga ngoma za asili katika eneo.

Muulize mwalimu mkuu kama unaweza kumwalika mtu. Wasiliana na mtu na mwalike aje azungumze na darasa lako juu ya ngoma za asili na utoe mfano wa ngoma moja au mbili.Waambiwe waje na nguo wanazovaa.

Andaa darasa lako kwa ajili ya ugeni (angalia nyenzo ya muhimu: kwa kutumia jumuiya/mazingira kama nyenzo rejea ). Fikiria kuhusus maswali ambayo wanafunzi wanaweza kutaka kuuliza.

Andaa darasa lenye nafasi kwa mgeni kukaa na kucheza ili wanafunzi wote waone.

Mkaribishe na kumtambulisha mgeni.Mgeni aongee na kucheza kwa takribani nusu saa.

Wahimize wanafunzi wako kumuuliza mgeni maswali.

Baada yaugeni, jadili na wanafunzi wako walivyojifunza kuhusu ngoma. Nani wameipenda? Nani wanapenda kufanya zaidi/Kuendelea? Fikiria cha kufanya baadaye.Labda mgeni atarudi kuwafundisha baadhi ya ngoma?

Somo la 2

Kucheza ngoma darasani kunafaa kwa kazi za mtaala, kwani unagundua mawazo ndani ya ngoma, umuhimu wa mavazi (maalumu) na kujifunza namna ya kucheza ngoma.

Ngoma ni shughuli halisi na inaweza kufanywa kama sehemu ya elimu ya viungo au inaweza kutumika kugundua mawazo katika maeneo ya masomo mengine kama vile fasihi na sayansi.

Katika uchunguzi kifani 2 na shughuli 2 za ngoma inatumika kuwasaidia wanafunzi kuonyesha kile wanachojua juu ya mada au kuhadithia hadithi.

Uchunguzi kifani ya 2: Kufanya kazi kwenye makundi ili kutengeneza mpangilio wa ngoma.

Bibi Msane amekuwa akifanya kazi na darasa lake namna ubongo anavyotuma ujumbe mwilini. Anaamua kutumia mada hii katika masomo yake ya PE ambapo anafanya mfululizo wa masomo juu ya ngoma.

Bibi Msane anawaambia wanafunzi wake kuwa atawagawanya katika makundi ya watu kati ya sita na kumi. Kundi linatakiwa kufikiri njia za kuonyesha namna ujumbe unavyokwenda kutoka kwenye ubongo mpaka kwenye sehemu ya mwili kuiambia ijongee na ujumbe mwingine kurudi

kwenye ubongo kujenga au kusimamisha mjongeo. Anawapa muda wa kufikiri juu ya hili na anawazungukia kuwasaidia wanapozungumza.

Baada ya dakika 15, anapendekeza wanavyofikiri namna ya kucheza ngoma na kuanza kufanya kwa vitendo.Anawatahadharisha/anawakumbusha kuwa waeneze ujumbe/mawazo yao kwa myumbo bila maneno.

Baada ya kufanya kwa vitendo kila kundi linaonyesha namna lilivyofanya baada ya kila tukio/Sehemu ya darasa iliyobaki wanatakiwa kubuni kinachotokea na wanaweza kuuliza maswali.

Anaamua kuwapa muda wa kujenga mawazo yao na kuyaonyesha kwa darasa juma linalofuata, kundi moja mwishoni mwa kila siku.

Bibi Msane anagundua kuwa kila mmoja amefurahia na anafikiri kwamba wanafunzi wake pia wanafahamu umuhimu wa ngoma kama nyenzo ya kujieleza na kama njia ya kuwasiliana.

Shughuli ya 2: Kutumia ngoma kutoka zamani mpaka sasa kuwasiliana.

Kumuulizia kila mwanafunzi kutafiti ngoma ambayo mzazi ndugu au mtu wa makamo alikuwa akicheza au bado anafanya. Siyo lazima iwe ngoma ya asili.

Watambue

Ngoma inatoka wapi?

Kwa nini ngoma ilichezwa na ilikuwa na lengo gani? Ilichezwa wapi?

Namna ilivyochezwa?

Wape nafasi ya kufanya hivyo na kuadika namna ya kucheza ngoma (angalia pia nyenzo muhimu rejea: kutafiti darasani )

Kinachofuata, kwa kutumia moja ya ngoma za asili kama msingi, waulize wanafunzi wako kuorodhesha inachokusudia (ngoma) kuonyesha)

Sasa waambie wanafunzi wako kuandaa ngoma zao wenyewe kwa kutumia mbinu yoyote wanayopenda, kueleza mawazo yanayofanana. Haya yanaweza kuwa yanahusu.

Kufikia utu uzima; Kuzaliwa kwa mtoto; Mavuno mazuri

Wape nafasi ya kutenda na kushiriki katika ngoma zao

Wakumbushe wanafunzi wako kuwa wanatakiwa kuonyesha hisia zao; kama vile furaha, dukuduku, mshtuko, huzuni pamoja na miili yao na nyuso wanapocheza.

Jadili hisia hizi na wape muda wa kufanya mazoezi tena. Shiriki nao utendaji tena na jadili namna walivyoboresha.

Somo la 3

Ngoma inaweza kuwa na mvuto kwa mtu binafsi lakini pia imejikita kwenye uchezaji wa kikundi na kuwaruhusu wanafunzi wako wakue katika

kujiamini na kujithamini.. Hii ni muhimu kwani inaweza kuinua mtazamo wao juu ya kujifunza na mafanikio yao.

Kama mwalimu, ni muhimu katika nafasi ya vitendo kutambua watu katika kundi na mafanikio yao, pamoja na mafanikio ya pamoja ya kundi.

Uchunguzi kifani 3 na shughuli muhimu 3 inapendekeza njia za kutoa mrejesho kwa wanafunzi wako utakaowasaidia kujiandaa kucheza mbele ya hadhira. Utagundua pia namna rika linavyoweza kupima na kupeana mwisho nyuma ili kujenga uelewa wao na kuboresha kazi zao.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuandaa na kutoa burudani ya ngoma kwa mafanikio.

Bibi Msane anasikia kutoka kwa mmoja wa washiriki kwamba shule itakuwa na siku ya wazi mwishoni mwa muhula. Wazazi na watu kutoka kwenye jumuiya wataalikwa kuhudhuria. Bibi Msane amevutiwa na shauku ya wanafunzi wake kutokana na kazi ya kucheza ngoma waliyokuwa wakifanya na anaamua kuwasaidia kutengeneza/kuendeleza ngoma walizotengeneza darasani ili zichezwe kwenye ‘Siku ya Wazazi’ (Open Day).

Anawahimiza kufanya mazoezi wakati wa chakula cha mchana na kutenga muda wakati wa masomo ya elimu ya viungo. Juma moja kabla ya ‘siku ya wazazi’, wanacheza wenyewe kwa wenyewe na kutoa mrejesho juu ya ubora wa ngoma na njia za kuboresha. Anatumia mfululizo wa maswali kuwasaidia kufikiri juu ya kuboresha uchezaji wao (angalia nyenzo rejea 3: Kuboresha ngoma yetu ). Wanafanya mazoezi na kukamilisha ngoma yao. ‘Siku ya wazazi’, kila mtu alishangaa namna wanafunzi wa Bibi Msane walivyofikisha mawazo kuhusu namna akili inavyofanya kazi kwa kutumia ngoma. Hatimaye, bibi Msane anawaambia kutafakari uzoefu walioupata; hii inampa mrejesho wa kufaa juu ya mchakato wa kujifunza, pia kuwasaidia wanafunzi wake kufikiri juu ya kile walichopata (angalia nyenzo rejea 4: Tafakari juu ya ngoma).

Shughuli muhimu: Kujiandaa kucheza

Kabla ya somo la kwanza, soma nyenzo rejea 3 na 4

Waeleze wanafunzi wako kuwa watacheza ngoma jioni inayofuata kwa wazazi na kwamba mwalimu mkuu anaalika wanajamii pia waje.

Kabla hujaanza hakikisha kuwa wanafunzi wako wanajua mahitaji ya kuwa waangalifu. Wape maelezo ya kina namna utakavyokuwa unawasimamisha wanapocheza na watahadharishe kuwa wanapaswa kujua walipo wanadarasa wenzao.

Panga darasa lako latika makundi.Kiambie kila kikundi kuandaa ngoma kulingana na mada walizokuwa wanasoma. (Unaweza kuamua au waruhusu wanafunzi wapigie kura kutoka kwenye orodha.

Yape makundi muda wa kufanya mazoezi.

Ruhusu kila kikundi kucheza mbele ya darasa. Wahamasishe wanafunzi wako kupeana yanayofaa yatakaowasaidia kuboresha michezo yao.

Wasaidie wanavikundi wanapofikiria namna ya kuboresha na kuziremba ngoma zao ili ziwe tayari kuchezwa mbele ya hadhira

Jadili mavazi na vivaa vya ngoma na uviandae

Andaa ratiba

Cheza

Jadili pamoja namna ilivyoenda. Wamejifunza nini kuhusu ngoma? Wamejifunza nini juu ya mada?

Nyenzo-rejea ya 1: Hadithi za ngoma ya Venda

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Hadithi ya ngoma takatifu ya Venda

Hapo zamani za kale, miungu ya mababu iitwayo Mwari iliwapa watu wa Venda ngoma yao takatifu ikiitwa ngoma Lungundu. Katika siku hizi za kale, mababu wa venda waliishi Zimbambwe. Siku moja walipokea ujumbe wa kimungu kwamba wanatakiwa kuchukua ngoma yao takatifu, Ngoma Lugundu, na waelekee kusini.

Ngoma hii ilikuwa kubwa na nzito na ilipaswa kubebwa na wanaume wengi. Ili watunze nguvu za ngoma, ilitakiwa isiguse chini/ardhi.Ikipigwa na mfalme inaweza kusababisha ukungu, mvua ya mawe, mvua, radi au miale ya radi. Kwa muda fulani Mungu mkuu Mwari anaipiga yeye mwenyewe. Wakati huu ngoma ingeonekana kama inajipiga yenyewe. Maadui walikimbia kwa hofu, walizimia au kufa waliposikia midundo yake yenye nguvu.

Nguvu hizi zilisaidia kuwalinda hawa mababu wa Venda wakati wa hii safari na mwishowe walifika wanapoishi leo hii kaskazini mwa Afrika kusini. Hapa kuna ziwa linaloitwa funduzi ambalo ni takatifu kwa wavenda.

Miaka mingi iliyopita, shujaa wa wavenda, aitwaye Thoyo ya Ndou, alipotelea katika ziwa hili akiwa amebeba ngoma hiyo. Watu wengi wanafikiri kuwa haijawahi kuonekana tangia wakati huo, lakini wengine wanaamini kuwa imelindwa na kufichwa katika pango.Thoyo ya Ndou, au mkuu wa Tembo, alikuwa anatamaniwa kwa sababu aliwaunganisha watu wa Venda na kulikuwa na amani na ustawi. Tangu alipopotea, wengi wanasema kuwa kumekuwa na kutoelewana mafarakano/migongano katika familia ya kifalme ya Venda.

Chanzo halisi: Catalogue: Ten Years of Collecting (1979–89), Standard Bank Foundation Collection of African Art, Editors: Hammond-Tooke & Nettleton, 1989

Nyoka/Joka (Chatu)

Katika jimbo la Limpopo kuna ziwa zuri liitwalo Fundulizi.Watu wa Venda wanalichukulia kuwa muhimu sana, eneo lililotakaswa, kwani wanaamini kuwa kuna joka kubwa jeupe linaloishi chini ya Fundudzi. Joka hili ni Mungu wa mtuba. Kwa maneno mangine anahakikisha kuwa watu wana afya nzuri na wana watoto wengi.

Hapo zamani, Mungu huyu aliishi nchi kavu.Alikuwa na ngozi nzuri; na alioa wanawake wanadamu wawili; mmoja mzee na mwingine kijana. Ilitokea kuwa alikuwa akiwatembelea hawa wake zake wawili kila siku usiku sana. Alitembelea vibanda vyao walipokuwa wametingwa na kazi za shamba. Hivyo hawakuwahi kumuona mume wao au kujua alikuwa anafananaje.

Siku moja, mke mdogo aliingiwa na tashwishwi na kuamua kurudi toka shambani mapema na kuchungulia dirishani. Alitishika alipoona kuwa mume wake alikuwa ni joka nene na kupiga kelele. Joka lilikimbia na kuingia ziwani. Tokea hapo kulikuwa na ukame na njaa juu ya ardhi. Wanyama walikufa na hakukuwa na maji ya kutosha kwa ajili ya mazao.

Hakuna anayejua kilichosababisha balaa hili na wazee walikutana ili kujadiliana juu ya tatizo hilo. Hatimaye, mke mdogo alikiri kuhusika kwa yale yaliyotokea. Walimwomba awasaidie kurudisha rutuba kwenye ardhi. Siku moja alichukua mtungi wenye pombe na kuelekea ziwani. Wanaume walipiga filimbi zao ili kumtia ujasiri. Alitembea kwenye kina kirefu hadi maji yalipofunika kichwa chake, na hakuonekana tena.

Baada ya hili, mvua ilirudi na ukame ukakoma. Mpaka leo, wafalme wa Venda na waganga wa kienyeji/jadi huenda kwenye ziwa Fundudzi na kumwaga pombe majini. Wanaamini kuwa kama pombe itazama, ni dalili za furaha ya Mungu Nyoka na kukubali kwake zawadi yao. Katika mila ya Venda, vijana kuhudhuria shule maalumu ya jando.Hii huwaandaa kwa majukumu yao kama waume na wake ndani ya jamii. Vijana hujifunza ngoma ya domba wanapohudhuria dombani au shule ya jadi. Kabla ya domba haijaanza, kiongozi wa ngoma anaita: ‘Tharu ya mahbidighami!’ (‘Joka linajikunjua’). Wanapocheza ngoma, hutengeneza mstari mrefu kama ‘ nyoka’ kwa kuzunguka moto.

Nyenzo-rejea ya 2: Mila za kienyeji: Mbinu za kuchezangoma katika Tanzania

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Kimila/ kiasili, makabila katika Tanzania walitumia muziki na ngoma kuashiria tukio maalumu kama vile uvunaji, sherehe za jando na harusi. Ngoma, moja ya vifaa muhimu vya muziki, hutumika pia kama njia ya mawasiliano. Kila kabila ya makabila 120 ya Tanzanaia wana ngoma yao au mbinu yao ya uchezaji. Kwa mfano, wanapocheza Wamakonde hutikisa viuno vyao katika msisimko wa sindimba; wakati Wasukuma hutumia nyoka kama vile chatu katika ngoma yao ya Bugobogobo” Wazaramo wanarukaruka katika mdundiko, wakati wanapocheza ngoma ya asili kama vile ‘mitamba yalagala kumchuzi’ .

Wamasai wana ngoma ya kuruka inayoendana na mdundo wa kuguna wa sauti zao nzito.

Chanzo halisi: Tanzanian Culture, Website

Kama unaweza kupata mtandao unaweza kuwaonyesha wanafunzi wako mikanda ya video ya ngoma za asili, kwa mfano:

http://www.youtube.com/ watch?v=9ifeNAP-AXM Ni mkanda wa video wa ngoma za asili mkoani mwanza

Nyenzo rejea 3: Kuboresha ngoma zetu

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Tumia maswali yafuatayo kuongoza mjadala juu ya ngoma ya kila kundi. Kumbuka kuwa hulazimiki kufuata maswali haya katika mapangilio fulani.

Ubunifu;

Unaweza kubuni tofauti/mabadiliko yaliyomo ndani ya ngoma yako ili uwasilishe mawazo yako?

Unaweza, kwa mfano, kubadilli uelekeo kutumia sehemu tofauti za nafasi, kutumia sehemu tofauti za mwili au kubadilisha eneo kati ya wacheza ngoma?

Kufanya kazi pamoja

Kuna njia tofauti za kufanya kazi pamoja katika ngoma ya kundi. Angalia baadhi ya tofauti zifuatazo:_

Kufanya kazi kwenye kundi kubwa m.f wawiliwawili; Kuangaliana, kucheza jirani, kugeukiana na kuegemeana; Kutofautisha umbali kati ya wachezaji;

Kubuni mtazamo wa mmoja au wachezaji zaidi katika muda fulani; Kuruhusu mchezaji mmoja aongoze na wengine wafuate.

Nafasi ya kuchezea

Je, Unahitaji kujibana kwenye ngoma ili utimize nafasi ya kuchezea? Ni namna gani utajipanga kwenye nafasi ili uanze?

Ni namna gani utajipanga kwenye nafasi utakapomaliza?

Ni namna gani utajipanga kwenye nafasi wakati wa kucheza? Utayari wa hadhira

Ni rahisi kwa hadhira kuwaona wacheza ngoma katika kundi?

Unaweza kujibana ngoma ili hadhira ione vizuri

Mambo mengine ya kufikiria

Kuna mtu yeyote ndani ya kundi lako anayehitaji kuungwa mkono au msaada?

Unaweza kuiboresha       kwa kuvaa kofia ile ile, rangi fulani n.k?

Nyenzo rejea 4: Kutafakari juu ya ngoma

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Unaweza kutumia haya maswali hapa kuwasaidia wanafunzi wako kurudi nyuma kwenye uzoefu wao. Waambie wasome na kutafakari juu ya maswali haya kwa uangalifu na kuyajibu kwa uaminifu na undani.

  1. Andika maneno matatu au zaidi kueleze jinsi ulivyojisikia wakati wa hatua zifuatazo:-
    • a.Ulivyotoa ngoma yako kwa darasa b).Kushuhudia wengine wakicheza
    • b.Kushuhudia wengine wakicheza
    • c.Kuicheza ngoma yako mbele ya hadhira
  2. Ni nini ulichofurahia zaidi juu ya masomo hayo? Kwa nini?
  3. Ni nini ulikiona kama changamoto juu ya masomo hayo? Kwa nini?
  4. Unafikiri ni jambo gani la mafanikio juu ya ngoma yako? Kwa nini?
  5. Unafikiri kuna njia za kuboresha ngoma yako? Kama ndivyo namna gani?
  6. Ni uigizaji/uchezaji gain mwingine uliopenda? Kwa nini?
  7. Umejifunza kitu chochote kipya kuhusu wewe mwenyewe?
  8. Umejifunza nini kutoka kwa michezo mingine/nyingine?

Sehemu ya 4: Kutumia muziki darasani

Swali Lengwa muhimu: Kuna mbinu gani tofauti ambazo zinatumika kutengeneza muziki darasani?

Maneno muhimu: muziki; wimbo wa kusifu; kazi ya kikundi;jamii; vifaa; utamaduni

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umetumia mazingira na jamii kama nyenzo za kujifunzia;
  • Umepanga shughuli za muziki kwa vitendo;
  • Umewahusisha wanafunzi kutengeneza muziki wao, kwa akutumia muziki wa tamaduni na desturi mabalimbali.

Utangulizi

Muziki ni sehemu muhimu ya maisha na tamaduni za watu. Uelewa wa nafasi ya muziki na namna ya kuufanya muziki uwasaidie wanafunzi kujitambua na kujiamini ni muhimu. 

Msisitizo katika sehemu hii ni kugundua sauti mabalimbali na kufanya kazi pamoja. Katika shughuli zote hizi, wahamasishe wanafunzi wako kusikiliza kwa umakini,kuuliza maswali na kujaribu.

Somo la 1

Mazingira ni nyenzo ya thamani katika kugundua sauti na namna vifaa tofauti vinavyoweza kutoa sauti.

Madhumuni ya sehemu hii ni kupanua uelewa wa wanafunzi wako na uzoefu wa aina mbalimbali za sauti, na kuona namna wao wenyewe na mazingira yao ya karibu yalivyo nyenzo za muziki. Uchunguzi kifani 1 na shughuli 1 vinaonyesha namna sauti katika maisha yetu ya kila siku zilivyo mwanzo mzuri wa mada hii.

Shughuli hizi zingeweza kupanuliwa kwa kuwaambia wanafunzi watengeneze zana zao wenyewe kutokana na vifaa vya kawaida* (makopo, chupa n.k) au unaweza ukabahatika kuwapata wanafunzi wanoweza kupiga zana au kuimba. Wapangie namna watakavyoonyesha ujuzi wao darasani.

Angalia Nyenzo rejea 1: Kugundua sauti ili kupata taarifa za msingi na moduli ya SAYANSI 3, Sehemu ya 2 kwa taarifa zaidi juu ya sauti na vifaa vya muziki.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutengeneza ramani akilini kuunganisha vifaa na sauti

Katika darasa lake la msingi la Soweto, Afrika ya Kusini, Bi Simelane anagundua wavulana wawili wakigonga dawati. Anasikiliza kwa makini jinsi wanavyotengeneza mapigo kwa kutumia dawati kama ngoma. Halafu wanagonga makasha yao ya penseli. Bi Simelane anafuatilia kwa makini muziki wao, na anawaambia wanadarasa wafumbe macho yao na

kusikiliza. ‘Wanatengeneza muziki? Kwa jinsi gani?’ ‘Unaweza kusikia

sauti gani tofauti?’ Wanafunzi wanavutiwa kutumia madawati yao, kalamu zao na makasha ya penseli kutengeneza sauti. Anawaacha wagundue sauti tofauti wanazoweza kutengeneza kwenye madawati yao kwa kutumia vifaa vinavyowazunguka. Wanasikiliziana sauti na kutoa maoni ya jinsi zinavyotengenezwa.

Bi Simelane anawaambia wanafunzi wapendekeze zana zinazotengeneza sauti akilini mwao na kuzirekodi ubaoni. Anawahimiza kufikiria juu ya uhusiano kati ya vifaa na sauti. ‘Ni aina gani ya sauti tunaisikia tunapogonganisha chupa na kijiko? Au kupuliza mdomo wa chupa ulio wazi?’ ‘Ni sauti gani zinatengenezwa na ngoma za ukubwa tofauti?’

‘Tunailezeaje sauti?’ anaongezea mawazo yao kwenye ramani ya akilini mwao.

Anaridhishwa na majibu yao na anaona huu kama ni mwanzo wa wanafunzi kutengeneza zana zao kwa kutumia vifaa vilivyo kwenye maznagira ya kawaida. (Angalia Nyenzo rejea 2: Kutengeneza zana ).Mwishoni mwa somo, anawaambia waende nyumbani na kukusanya vifaa vingi tofauti kadri watakavyoweza na kuvileta shuleni kuongezea kwa vile vilivyokwisha kusanywa. Juma lijayo watatengeneza na kuonyesha zana hizi.

Shughuli ya 1: Kusikiliza sauti

Kabla ya somo, soma Nyenzo rejea 3: Kusikiliza sauti katika maisha ya kila siku.

Waambie wanafunzi wako wakae kimya na kusikiliza sauti wanazoweza kuzisikia darasani.

Katika makundi, au darasa zima likiwa limekuzunguka, wachangie mawazo juu ya sauti zote wanazoweza kusikia kwenye karatasi kubwa au ubaoni. (angalia Nyenzo rejea muhimu: Kutumia ramani za akilini na chemsha bongo kugundua mawazo .)

Baadaye, panga makundi madogo ya wanafunzi (nne/tano) kwenda nje kwa muachano na kutembea kwenye viwanja vya shule. Wasimame katika maeneo manne na kusikiliza kwa makini chochote wanachoweza kusikia. Wachukue kalamu au penseli na vitabu vyao au karatasi kwa ajili hii.

Kila kundi wachukue dondoo kwa kila sauti mpya wanayosikia na mahali walipoisikia, na wajaribu kuainisha ni nini kinatengeneza hizo sauti na kwa namna gani zinatengenezwa.

Wanaporudi darasani, waambie kila kundi wachore ramani zao za kufikirika juu ya sauti walizosikiliza.

Haya yanapoisha, yaonyeshwe ili wote waone na kujadili mawazo yao namna sauti zinavyotengenezwa.

Somo la 2: Kufanya kazi katika vikundi ili kutunga ushairi wa wasifu yaani utenzi

Utenzi na uimbaji ni uzoefu muhimu wa Kiafrika, wa kale na wa sasa. Majina ya Kiafrika huambatanisha nafsi yako na wapi utokako. Huwataarifu watu kuhusu uzoefu wako, furaha na mapambano yako, na jinsi ulivyo, ili watu wakutambuwe. Watu hutunga nyimbo zao wenyewe za sifa. Watunzi wa mashairi huburudisha kwa kuonyeshwa kwenye sherehe, ada za asili na sikukuu ili kutoa wasifu wa mtu au kikundi. Nyimbo za sifa na utenzi zimekuwa sanaa staarabu, ambayo hufanywa na tamaduni nyingi kwa kupitia muziki, dansi na uimbaji.

Utawasaidia wanafunzi kufanya utafiti na kubuni tenzi zao wenyewe au nyimbo, ukilenga mawasiliano ya kujitambulisha na urithi wa ukoo. Hii itawasaidia wanafunzi wako kupata uhusiano baina yao wenyewe na uzoefu wa muziki.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia mashairi ya kusifu kujenga uelewa wa muziki

Ndugu Mtui ni mwalimu wa muziki, sanaa na utamaduni ambaye amekulia Kilimanjaro. Anafundisha shule ya msingi iliyoko mjini, ambako wanafunzi wake wanawakilisha, tamaduni, dini na lugha mbalimbali. Anapiga wimbo wa kichaga wa zamani kwenye gitaa lake anapokuwa anafikiria juu ya somo lake la muziki la mwezi ujao. Atajengaje dhamira ya utambulisho kwa kutumia muziki? Anapoimba, muziki unamrudisha nyuma wakati wa utoto wake, nyumba yao, wazazi na mababu na mabibi. Anakumbuka alivyokuwa anasikia nyimbo za kutaja majina na kujisifu kama mtoto. Anaukumbuka wimbo wake wa majigambo unaoelezea kuzaliwa kwake na ukoo wake. Kumbukumbu zake zinatengeneza mwanzo wa wazo lake kwa darasa lake.

Ndugu Mtui anakusanya baadhi ya mashairi ya kusifu na nyimbo na kuvitungia maswali. Anasikiliza muundo wa nyimbo za kuita na kujibu na anaziunganisha na mchezo wa kujigamba uliozoeleka ambao wanafunzi wake wanaucheza kiwanjani. Anapanga kufundisha somo juu ya mashairi ya kusifu kwa kuanzia kwenye nyimbo zilizozoeleka. Halafu anawahimiza wanafunzi wake kutengeneza na kuimba nyimbo na mashairi ya kusifu rafiki zao. Angalia Nyenzo rejea 4: Kuimba kwa kusifu kwa habari zaidi za kina.

Shughuli ya 2: Nyimbo na mashairi ya kusifu

Kabla ya shughuli hii, tazama Nyenzo rejea 5: Nyimbo za kusifu za mwanafunzi.

Imba wimbo wa kusifu unaofahamu darasani kwako au mwambie mwanafunzi aimbe darasani. Waeleze wanafunzi namna muundo wa wimbo unavyofanya kazi na washirikishe kutoa majibu.

Imba wimbo tena wakati wanafunzi wakitunza mdundo kwa kupiga makofi, kugonga madawati au kutumia zana.

Ongea nao juu ya wazo la nyimbo za kusifu, nani wanaziimba na kwa nini

Imba nao shairi la kusifu, ukifuatilia mapigo ya maneno na kuwasilisha hisia za shairi kwa sauti yako. Ongeza sauti za vifaa zitakazoongeza hisia za shairi kama inawezezekana.

Halafu, ligawe darasa katika makundi ya wanafunzi sita. Waambie kila kundi wafanye kazi watatu watatu na waandike shairi lao la kusifu. Kila wanafunzi watatu waimbe shairi lao kwa wenzao watatu kisha waeleze maana na hisia zilizopo kwenye shairi. Kwa pamoja, kundi zima linachagua kiitikio na kujaribu kuimba mashairi yao mawili. Wanaweza kuongeza sauti nyingine kama wanapenda.

Baada ya siku chache zijazo, waambie kila kundi liimbe shairi lake la kusifu kwa darasa zima.

Somo la 3

Upigaji muziki ni aina ya mawasiliano: vyombo na sauti 'huzungumza', kuwasilisha hisia, mawazo na fikra. Muziki huakisi na kujenga utamaduni, na daima huwa na vuguvugu – linalobadilika na kuendelea. Barani Afrika, muziki ni muhimu kwa kujenga mshikamano wa kijamii (umoja) na unaweza kuwa muhimu darasani.

Katika sehemu hii, utaendeleza vitendo vilivyopita kwa kuandaa maonyesho ya darasa zima. Jinsi ulivyokipanga kitendo ndivyo hivyo kitakavyochangia katika maarifa ya ushirikiano na usikilizaji wa wanafunzi.

Uchunguzi kifani ya 3: Thamani ya kuandaa muziki wa kikundi

Uchu wa Goodluck ni kutengeneza muziki katika kikundi. Hisia anazopata akiwa anapiga marimba, au anapoimba katika kwaya ni maalumu kwa mshikamano. Anataka kuwashirikisha wanafunzi wake hisia hizi; wapate uzoefu wa namna inavyokuwa kutengeneza muziki wa pamoja wakati kila mmoja anamsikiliza mwenzake kwa umakini.

Goodluck anasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma iliyoko katikati mwa Tanzania, na kutembelea Shule ya Msingi Umoja iliyoko mbalil na mjini. Anamtembelea mwalimu wa sanaa na utamaduni. Anapofika, anakuta kuna sherehe. Makundi ya wavulana wadogo yanapiga filimbi na ngoma wakati wa maandalizi.Kwenye uwanja wa vumbi, Goodluck anasikiliza na kuliona kundi la watoto 50wakisogea na kufanya muziki kwa pamoja-kila mmoja akichangia, akitazama na kusikiliza wanapoeleza hadithi ya ngoma.

Akivutiwa na wapiga filimbi na ngoma, aliamua kuwa wanafunzi wake Dar es Salaam wanahitaji kupata uzoefu wa jinsi gani ilivyo ‘kuwa mmoja’ kwa kutumia muziki. Baada ya kuongea na waalimu na kujifunza zaidi juu ya umuhimu wa muziki kiutamaduni na ngoma ya Mheme, anarudi nyumbani kuandaa somo ambapo wanafunzi wake watatengeneza muziki kwa pamoja.

Nyenzo rejea 6: Kutengeneza muziki inaonyesha ni jinsi gani zana za muziki zinaweza kutengenezwa kwa ajili ya wanafunzi wako kuzitumia.

Shughuli muhimu: Kutengeneza muziki

Waulize wanafunze kama mmoja kati yao anapiga kifaa cha muziki. Kama wanapiga, waambie wavilete shuleni.

Siku inayofuata, waambie wanafunzi walioleta vifaa wavionyeshe na kuvipiga darasani.

Waulize wanafunzi wako kama wanajua nyimbo au mashairi ya majigambo. Kama wanajua, waambie wakuambie maneno, na yaandike ubaoni.

Mwambie mwanafunzi aimbe ushairi/wimbo halafu waambie wanafunzi darasani waungane nawe utakapoimba ushairi/wimbo tena.

Rudia hadi darasa litakapoimba barabara.

Sasa, waambie wale wanaopiga vifaa nao waungane na wenzao. Fanyia mazoezi wimbo mzima hadi kila mmoja atakapofurahi na waimbe kwa darasa lingine au ‘siku ya wazazi’.

Nyenzo-rejea ya 1: Kugundua sauti

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Shughuli A: Maswali ya kimuziki kuhusu sauti

Anza kwa kuchunguza sayansi ya sauti na wanafunzi. Gundua haya maswali na wanafunzi wako kwa kutengeneza sauti mbalimbali, katika njia tofauti, kwa kutumia vitu vinavyokuzunguka: dawati, sakafu, kalamu, chupa, ubao au dirisha. Kumbuka, kuongelea juu ya sauti lazima

kuendane na uzoefu tulionao juu ya sauti.

Sauti ni nini?

Nini kitokee ili sisi tusikie sauti? Sauti inasafirije kutufikia sisi?

Nini kinafanya kitu kuwa kifaa cha muziki?

Tunaweza kutumia mwili wetu kama kifaa cha muziki? Kwanini unafikiri kuwa watu wanatumia vifaa vya muziki

kutengeneza muziki? Inatimiza malengo gani?

Unafahamu vifaa gani vya muziki? Unaweza ukaviainisha katika makundi?

Ni kigezo gain ulitumia kuainisha hivyo vifaa?

Shughuli B: Muunganiko wa kisayansi – jinsi gani sauti inasafiri

Umewahi kuona”wimbi la Kimeksiko” (‘Mexcan Wave’) kwenye tukio kubwa la kimichezo? Sauti husafiri kwenye njia sawa na mwendo wa wimbi la Kimeksiko; molekyuli za hewa, kama watu katika mkusanyiko, zinakwenda mbele na kurudi nyuma, zikiungana na kutengeneza wimbi. Molekyuli mojamoja hazisafiri kutoka eneo moja kwenda jingine: molekyuli hutetemeka, kila moja kwenye nafasi yake, isipokuwa

kunapokuwa na kitu kingine karibu na molekyuli zinasogea. Hizi molekyuli zinazotetemeka zinavuta molekyuli nyingine, hivyo basi zinatoka kwenye sehemu zao.

Sauti inaweza kusafiri kwenye hewa kitu chochote kilichotengenezwa kwa molekyuli kama maji, chuma au mti. Sauti husafiri kwa kasi tofauti kutegemeana na kitu inamosafiria.

Shughuli C: Kutengeneza wimbi la sauti

Tengeneza mstari wa wanafunzi kumi waliosimama kwa kufuatana. Upande mmoja, mwambie mwanafunzi mmoja apige chombo cha muziki kama mbiu na mwingine alama kubwa inayosema SAUTI. Upande mwingine, mwabie mwanafunzi abebe picha kubwa ya SIKIO. Wanafunzi wengine kwenye mstari wawe na alama ya HEWA.

Mwambie mwenye mbiu aipige. Mwanafunzi wa kwanza.anayumba mbele na nyuma kwa kutumia mwili wake (huku miguu ikiwa imesimama ardhini); mwanafunzi anayefuata naye anayumba baada ya kuhisi uwepo wa mtetemo wa mwanafunzi wa kwanza, na hivyo hivyo kwa mstari mzima.Mwnafunzi wa mwisho anashikilia alama ya KUSIKIA anapohisi myumbo wa mwanafunzi anayemfuata.

Chanzo halisi: Stomp Online Lessons, Website

Nyenzo-rejea ya 2: Kutengeneza zana

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

‘Zamani za kale, kabla vitu vya kutengenezwa na binadamu kuwepo,watu katika jamii za asili ya Afrika walitengeneza zana za muziki kulingana na vifaa vilivyokuwa karibu yao…Katika jamii za vijijini walitengeneza pinde kutokana na miti, njuga kutokana na matunda au magamba ya kokuni yaliyojazwa mbegu au mawe, na ngoma kutokana na ngozi za wanyama na miti’

(Traditional Music of South Africa by Laurie Levine, 2005)

Orodha ya vifaa vya kutengenezea zana

Tengeneza mkusanyiko wa vitengeneza sauti, kwa kutumia aina zifuatazo kama mwongozo.

Vifaa vya miti. Vifaa vya chuma.

Vifaa vyenye mashimo.

Nyuso zinazoweza kukwanguliwa. Nyuso zinazoweza kugongwa.

Vitu vinavyoweza kutundikwa. Vitu vinavyoweza kutikiswa.

Vifaa vinavyoweza kunyonyolewa. Vyombo kwa ajili ya ngoma:

Chupa ndogo za glasi au chupa ya plastiki, vikombe, viberiti, masanduku ya unga wa kusafishia, ubao wa kubania karatasi au

mabomba ya plastiki, makopo ya kahawa, makopo ya vinywaji baridi, chupa za plastiki za vinywaji.

Vipande bapa vya Makasha ya kutengenezea sinia la sauti.

Chupa za glasi za ukubwa na maumbo mbalimbali (zijaze maji na uzigonge kwa kifaa cha chuma).

Vitu ya kujaza kwenye vitikisio na vigoma

Mawe, mbegu, mchele, maharage, misumari, mchanga,shanga, vifuniko vya chupa, vizibo vya chupa, vitoboleo vya karatasi, mawe.

Vifaa kwa ajili ya gitaa:

Masanduku ya viatu, madebe makuukuu, tepe zinazovutika, vipande bapa vya miti, nyaya nyembamba au mishipi ya kuvulia samaki.

Vifaa vya kutengeneza zana zinazoweza kutoa sauti zaidi ya moja: Birika kuukuu, vyombo vya jikoni, visu, kifuniko cha habu ya gari,

mbuzi ya kukunia nazi, brashi ya kupangusia nguo, chujio,

Vifaa vya chuma vya kuning’iniza kutoka kwenye stendi, kining’inizio chaa chuma au cha mti

Misumari ya chuma iliyofungwa pamoja, boliti kubwa ya chuma, vipande vya chuma vikuukuu, kiatu cha farasi kikuu, na bomba la shaba.

Vipigaji:

Kisu kikuu, msumari mrefu, fimbo imara ya mti, mswaki, rula na, kijiti. Vifaa zaidi:

Maganda ya mbegu au vibuyu vikavu, gazeti, nyaya za kuning’inizia makoti, povu, uzi na nyaya za chuma za ukubwa na uimara tofauti, fimbo za miti au matofali na mifuko ya plastiki.

Nyenzo rejea 3: Kusikiliza sauti katika maisha ya kila siku

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Shughuli hii inawahimiza wanafunzi kusikiliza sauti zinazowazunguka. Unaweza kuitumia kama mradi wa darasa au mradi wa ‘utafiti wa sauti’ nyumbani.

Msako wa sauti

Waambie wanafunzi wafanye kazi katika makundi ya watu wawili wawili kutambua na kurekodi sauti zifuatazo kwa kutumia maneno, alama au michoro. Msako unaweza ukafanyika nyumbani, mitaani au shuleni.

Malengo ni kutumia masikio yao, na sio macho yao! Waambie watambue:

Sauti ya muziki;

Sauti ya kukarahisha;

Sauti ya juu kabisa wanayoweza; Sauti fupi na kali;

Sauti zinazowafanya wajisikie kutulia na kuburudika; Sauti endelevu;

Sauti yenye mpangilio unaoeleweka;

Sauti inayowafanya watake kujongea au kucheza; Sauti ya vitisho

sauti ndogo sana;

sauti ambayo iko mbali sana;

sauti ambayo iko karibu;

sauti ya kimdundo; sauti ya mlio wa njuga sauti yenye mkwaruzo; Sauti nzito.

Kwa kuanzia, tumieni sauti chache kati ya hizi wewe na wanafunzi wako, kwa kuchagua zilizo rahisi (kama sauti nzito), halafu ongeza orodha kila wanapoelewa zoezi. Waache watengeneze maelezo ya sauti wenyewe na wajaribu kutengeneza sauti ambazo zinafanana na maelezo yao.

Nyenzo rejea 4: Kusifu uimbaji

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Mada za uimbaji wa kusifu zinaweza kuwa kati ya rasmi na zisizo rasmi. Kwa vile zinashawishi, zinasisimua, zinachokoza na kupendezesha suala linalosifiwa, kila kitu ni sawa/haki. Mbinu rahisi kabisa za kusifu na za kawaida mara nyingi zinaleta usikivu wa sura sahihi ya mtu anayehusika. Mwimbaji anaweza kuelezea juu ya uzuri wao au ujeuri wao, umbo lao (urefu, ufupi, wembamba au upana) au rangi ya ngozi zao.

Hapa kuna baadhi ya mifano ya hizi aina rahisi za kusifu:

E wo geele ya ya – Tazama mmiliki wa hiki kichwa cha kifaa cha kuwindia wanyama.

E wa woo – Njoo uone (hii ingefuatiwa na majina ya mtu majisifu ya muonekano wao).

Kwa undani, mwimbaji wa kusifu anaweza akachukua mafanikio ya mtu au familia yake ya karibu. Iwe biashara, siasa au mafanikio ya kimila, yanaweza yakasifiwa moja kwa moja.

Bibi ire ko se f’owo ra oti daju – Huwezi kununua uzaliwe kwenye ukuu. Ki a bi ni ko to ka tuntun ara eni bi – Kuzaliwa kwenye ukuu hakuna

maana ukilinganisha na ulichokifanya ulipopewa nafasi…….(weka jina la

mtu hapa) 

Au wanaweza kusifiwa kwa kuelezea sifa zao za jumla, za majina ya familia zao au miji yao.

Kwa undani zaidi, waimbaji wa kusifu huchukua kwenye mila na desturi za jamii fulani, historia ya maneno na ushairi kupandisha hadhi ya mtu ambaye anawamwagia fedha. Hii inafanyika ufahamu wa majina ya familia, miji au mikoa, na historia za kabila. Kwa mfano, katika Wayoruba wa Nigeria, kila mtu, familia na mji ana kile kinachotambulika kama ‘Oriki’ au mashairi ya kusifu. Mashairi haya ya kusifu yanasema vitu rahisi lakini vya maana sana juu ya watu na vitu vilivyowafunga kijamii (kwa mfano kifamilia, kimiji, na kikabila).

Mwimbaji mkuu wa kusifu ana uelewa na mtazamo mzuri wa jamii kuchukua haya na kutoa mchanganyiko wa simulizi ambazo zinabadilika mara kwa mara na zinaburudisha, kusifu na kuchekesha,ambazo zinahusisha hadhira inayoangalia onyesho na kusubiri nafasi yao ya kummwagia mtu fedha ili wasifiwe mbele ya macho ya halaiki. Mwimbaji wa kusifu anatakiwa mara kwa mara aitathmini hadhira na kuliongoza kundi / kwa mwelekeo wowote ule linakoelekea kuchemka, hadhira itajihusisha na fedha zitamwagika.

Mfano mzuri wa wimbo wa kupokezana kutoka Tanzania ni ‘Twendeni

Tukajenge Taifa’. Twendeni tukajenge Taifa Twendeni tukajenge Taifa... Twendeni tukajenge Taifa!

Nyerere maua mama popote chanua... Nyerere maua mama popote chanua!

Chanzo halisi: E. Songoyi, ‘Memories of National Services Songs’, 2004, unpublished.

Nyenzo rejea 5: Nyimbo za kusifu za mwanafunzi

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

Gracie – Wimbo wa kusifu

Imba shairi hili na waambie wanafunzi wako wabuni kiitikio kinachoendana na mwito.Chagua vifaa au sauti zinazooana na maneno: juu, iliyojikita, miito, chachu, miongozo na mwezi.

Mwito:

Gracie

Anayeishi kwenye jangwa kuu

Amejikita katika amani

Anaita roho za ngedere na simba Anachachua pamoja na kereng’ende Anaongoza kalamu

Mwezi ukazama

Mstari 1. Gracie (jina langu).

Mstari 2. Anayeishi kwenye jangwa kuu (nilizaliwa na kulelewa hapa

Bend ambalo ni jangwa kuu).

Mstari 3. Amejikita katika amani (babu zangu Mfalme Joseph wa kabila la

Nez Perce alifahamika kwa tabia yake ya amani).

Mstari 4. Anaita roho za ngedere na simba (wanyama wangu wanaowakilisha mizimu ni ngedere na simba. Ngedere huonyesha hulka yangu ya utotoni na simba huonyesha nguvu, ufahari na ukatili).

Mstari 5. Anachachua pamoja na kereng’ende (Kereng’ende anawakilisha mawazo yangu, mapenzi na ndoto).

Mstari 6. Anaongoza kalamu (Napenda kuchora na haya ni mapenzi yangu).

Mstari 7. Mwezi ukazama (Wakati wa usiku ndipo ninapopata faraja, nyota hunipa matumaini na mwezi ndio naweza kuuamini katika matatizo yangu).

Kuandaa shairi la kusifu au wimbo (maelekezo kwa mwanafunzi)

Anza na jina lako.

Rejea kwenye kitu kinachoelezea wapi na namna ulivyozaliwa

Ongea kitu chochote juu ya urithi wa familia yako;asili ya familia yako. Taja kitu, mnyama, kitu asilia ambacho ni cha maana au maalumu

kwako.

Ongea kitu kukuhusu wewe: unapenda nini, unataka nini na ndoto zako.

Andaa shairi kati ya mistari mitano na minane. Shairi liwe fupi, kila neno libebe picha, (kila neno liwe na maana nyingi, likitueleza mambo mengi).

Chagua maneno yako kwa uangalifu. Tumia kifaa chako kuboresha hisia na maana ya shairi lako. Chagua lini na ni vipi utaitengeneza sauti. Fikiri kwa makini kuhusu namna utakavyotumia sauti yako kujieleza.

Unaweza kuona zaidi nyimbo za kusifu za mwanafunzi katika tovuti ifuatayo: http://web.cocc.edu/ catagucci/ ambako yaliyopo hapo ya juu ndiko yalikonakiliwa.

Nyenzo rejea 6: Kutengeneza muziki

Taarifa za msingi/welewa wa somo wa mwalimu utangulizi

A. Kutengeneza na kupiga filimbi za Tshikona

Kutengeneza kundi la wapiga filimbi

(kutoka Talking Drum, April 1999, Sandra Bonnett, p. 17–18)

Wapiga filimbi ni makundi maalumu ya muziki kwa sababu kila mtu anapiga nota moja tu-lakini, zinawekwa pamoja, mara nyingi katika njia za kutatanisha, zinatengeneza muziki wa kustaajabisha. Wavha Venda, Watswana na Wabapedi wanafahamika kwa makundi yao ya wapiga filimbi za mitete, ambazo zinasemekana kwenda sambamba na ngoma kama Venda Tshikona na Bapedi Dinaka. Filimbi zimetengenezwa kwa matete (sehemu za vijijini) au filimbi za chuma (sehemu za mijini au kwenye machimbo ya madini). Filimbi zinatofautiana kwa ukubwa kutoka

sentimeta 20 hadi mita moja kwa urefu, ikitoa nota kuanzia za juu hadi za chini.

Shughuli hii imeelemea kwenye muziki kiTshikona na filimbi iliyochezwa na Wavenda wanaoishi kaskazini kabisa mwa Afrika ya Kusini (Jimbo la Limpopo). Filimbi za kiTshikona ni ndefu zikiwa na urefu wa kutofautiana, kila moja ikitoa nota tofauti. Unaweza kutengeneza filimbi zako kwa kutuma mabomba ya plastiki kama vile yale ya kupitishia nyaya za umeme, vipande vya mabomba ya plastiki, mabomba ya umwagiliaji (kipenyo cha mm 12-15). Tengeneza filimbi za urefu uliotofautiana ili uwe na nota tofauti. Vile vile ungeweza kutumia chupa za ukubwa mbalimbali na kupuliza kwa juu ili kutoa sauti.

Jinsi ya kupiga filimbi

1.     Weka sehemu ya wazi ya kifaa kwenye midomo ya chini.

2.     Shikilia filimbi kati ya vidole vyako, kidole cha shahada na kidole gumba.

3.     Weka vidole vilivyobaki kuzunguka eneo la katikati la kifaa.

4.     Anza kupuliza taratibu juu ya shimo hadi hapo nota itakapotokea.

5.     Jaribisha kwa kuziba sehemu ya chini ya filimbi kwa mkono wako.

B. Kutengeneza muziki wa kidemokrasia

Wagawe wanafunzi katika makundi ya watu kumi na jaribisha filimbi za mitete, ili waweze kusikilizana kwa umakini. Tengeneza nafasi katika mapigo yako ili wanafunzi waweze kujaza nafasi hizo. Halafu ongeza na mbinu za kucheza. Huna haja ya kucheza muda wote. Pokezaneni.

Unganisha- kujaza nafasi

Wazo la kuunganisha ni la msingi kwa muziki wa kiafrika. Unapojiunganisha na sauti unakuwa unajaza nafasi katika muziki (ukimya) kwa kutumia sauti. Kwa maneno mengine unasubiri hadi upate

nafasi ya kutoa sauti yako. Huu ni ujuzi muhimu unaofundisha wajifunzaji kusikiliza kwa makini, achianeni na kuweni makini. Huu ni msingi wa kutengeneza muziki wa kikundi kama picha za sauti.

C. Kutumia chupa kutengeneza filimbi za muziki wa makundi.

Kama ulitengeneza chupa za muziki badala ya filimbi, zituni chupa zako ili kuwe na namba sawa ya chupa zilizokuwa zimewekwa kwenye sauti A, E, G and D (kuanzia ya juu hadi ya chini). Utahitaji kitunio au kinanda ili kukagua tuni zako na kurekebisha maji kwenye chupa yako.

Wagawe wanafunzi wako katika makundi mawili. Hapa kuna mpangilio wa muziki kwa kila kundi uliogawanywa katika mapigo 8. Jaribisha kwanza kwa kupiga makofi kwenye namba zilizokolezwa wino, wakati mtu mwingine akipiga ngoma ya besi kuhifadhi mapigo. Utunze huo mdundo wa ngoma katika hali yake ya taratibu. Halafu puliza kwenye chupa yako katika muda sahihi, ukitunza mapigo kwa kutumia ngoma (lazima ujue ni nota gain ngoma yako inasikika!)

Kundi A

Chupa zote za A katika kundi la ‘lahani’ zinapuliza kwenye namba 1 na 5;

chupa zote za G zinapuliza kwenye namba 2 na 6, n.k.

Kundi A

Hesabu/Idadi ya nota

A12345678
G12345678
E12345678
D12345678

Kundi B

Hesabu/Idadi ya nota

A12345678
E12345678
D12345678

Weka makundi yote mawili pamoja, sikiliza kwa umakini kwenye ngoma ili ujue ni mdundo gani wa kupiga. Muziki utakaopatikana unatakiwa uwe wa kuvutia. Ukishafanyia mazoezi, tengeneza muziki wako, kwa kucheza nota hizo kwa mapigo tofauti.

(Kazi ya Sandra Bonnett, 1997. In Talking Drum April 1999)

D. Nyenzo katika jamii na bendi

Kwa ajili ya mwalimu:

Endelezeni mradi huu kwa kuunda kabendi, kwa kutumia vifaa vilivyotengenezwa na wanafunzi. Hakikisha kuwa kila kundi lina vifaa kadhaa. Jenga dhamira ya utambulisho wa kundi na aina ya nyimbo za kusifu ili kila kundi litengeneze shairi kwa kutumia vifaa, ikiwasilisha jambo kuwahusu wao wenyewe. Kutengeneza nyimbo za makundi kunahitaji muda kama mchakato wa kujifunza namna ya kutengeneza muziki kwa pamoja unavyojengeka. Shirikiana pamoja na mwalimu na shule yako rafiki. Andaa mchezo wa pamoja ambapo kila kundi linacheza nyimbo zake na kuonyesha vifaa walivyotengeneza.

Tafuta nini kinatokea kimuziki katika jamii yako. Kunaweza kuwa na wanamuziki wazuri ambao wangeweza kuja na kuimba kwa wanafunzi wako, na kushiriki nao katika shughuli za muziki na utamaduni. Tumia jamii kama nyenzo ya kujifunzia.

Kwa ajili ya wanafunzi: Mawazo ya mradi wa utafiti

Tafuta mwanamuziki anayeishi kaitka eneo lako na umhoji. Muulize:

Kifaa chako ni nini?

Ni aina gani ya muziki unaimba?

Muziki unamaanisha nini kwenye maisha yako? Wapi na vipi ulijifunza kuimba?

Tafiti aina mbalimbali za makundi ya muziki: kwaya, bendi, muziki wa pop/rock/kizazikipya/ngoma za asili na aina nyingine ya makundi.

Tafuta:

Ni nini kinachofanya kila kwaya au bendi iwe ya kipekee? Wanacheza muziki gani?

Wanatumia vifaa gani?

Muziki wao umerekodiwa? Kama ndiyo walirekodi vipi?

Ni akina nani waliohusika katika kutoa wimbo au albamu iliyorekodiwa? Wanafanya nini?

Ni hatua gani muhimu za kuchukua ili kuunda kundi la muziki lenye mafanikio?

Mazoezi ya mwisho yanafanyaje kazi?Ni namna gani kikundi au kwaya inafanya mazoezi?Wapi?Kwa muda gani?

Ni namna gani bendi au kwaya inavyojiimarisha yenyewe na matamasha yao?

Kutengeneza bendi yangu mwenyewe

Kwa kutumia taarifa ambazo umekusanya unda kundi na baadhi ya rafiki zako na tumia vifaa vyako kutengeneza kibendi chako mwenyewe. Ipe bendi hiyo jina. Fikiri kuhusu aina ya muziki ambao ungependa kuucheza. Tengeneza sauti zako mwenyewe. Endelea kubuni vifaa. Endelea kusikiliza na kugundua sauti za kuvutia ambazo unaweza kutengeneza na ziweke pamoja ili utengeneze muziki wako mwenyewe.

Kuona jinsi wanafunzi wengine walivyounda vibendi vyao, nenda www.soundhouse.co.uk/ mixedup/

Sehemu ya 5: Sanaa ya kuhadithia hadithi

Swali Lengwa muhimu: Kwa jinsi gani unaweza kuwasaidia wanafunzi wazikubali/hadithi na kujijengea ujuzi wa kuhadithia hadithi?

Maneno muhimu: hadithi jamii, kuhadithia hadithi, kuandika, utamaduni kazi ya kikundi.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Umepanga na kusimamia kazi za madarasa ili kusimamia tathimini ya hadithi na kuhadithia;
  • Umetumia mawasiliano ya ndani na rasilimali iliyojenga ufahamu wako juu ya utamaduni wa kuhadithia;
  • Umebuni na kutumia mbinu/mkakati wa kuwasaidia wanafunzi kuandika hadithi zao.

Utangulizi

Hadithi zimekuwa sehemu muhimu ya historia ya binadamu kwa karne ya sasa. Siku za nyuma, hadithi maranyingi zilitoa ujumbe muhimu. Waskilizaji wangecheka, kulia na wakati mwingine kuimba pamoja na mtoa hadithi.

Ni uwezo wa kubeba ujumbe unaozipa hadithi thamani kwako, kama mwalimu. Shughuli, uchunguzi kifani na nyenzo rejea katika sehemu hii zinalenga kukusaidia wewe kutumia utajiri huu wa kurithi ili uwajengee wanafunzi wako ujuzi wa sanaa ya kuandika, kuhadithia na kusimulia/ghani hadithi. Hii itawajengea hisia za kujitambua na kuwapa uelewa kuhusu urithi wao wa kitamaduni.

Somo la 1

Hadithi inaweza kusemwa, kuandikwa, kusomwa na kusimuliwa. Inaweza kuwa hadithi ya kweli au ya kutunga. Mara nyingi hadithi zina ujumbe

ndani yake juu ya taratibu za jamii, namna ya kuishi maisha yetu na namna ya kuwajali wangine.

Wewe na wanafunzi wako yawezekana mmeshawahi kuhadithia au kusikia hadithi. Yawezekana pia mmeshaandika baadhi. Sehemu hii itakusaidia kuwajengea wanafunzi wako uelewa wa sanaa ya kuhadithia hadithi na kwamba kuhadithia hadithi kumejikita ndani ya utamaduni wa jamii yenu.

Unaweza kuwa na bahati kwa kumfahamu mtu ndani ya utamaduni wa jamii yenu. Unaweza kuwa na bahati kwa kumfahamu mtu ndani ya jamii yenu mwenye ujuzi wa kuhadithia na ukaweza kuja kuhadithia hadithi darasani kwako (angalia nyenzo rejea muhimu; kutumia jamii/mazingira ya asili kama nyenzo rejea ). Au, katika uchunguzi kifani 1 , unaweza kumtembelea wahadithiaji na kuwarekodi kwenye kanda ili uitumie darasani kwako. Shughuli 1 inapendekeza njia za kuwaandaa wanafunzi kushirikishana hadithi wazipendazo.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutumia watu wa kawaida kujifunza umuhimu wa kiutamataduni wa hadithi.

Bibi Biyela anafundisha katika Shule ya Msingi Furaha nchini Tanzania. Anajiandaa kwa mada yake unayofuata, ambayo ni ‘Hadithi’. Anapitia vitabu na nyenzo rejea za tovuti juu ya uhadithiaji wa hadithi, uandishi na usomaji. Anajifunza kuwa kuhadithia hadithi kuna umuhimu wa ndani wa kiutamaduni, na anatafuta baadhi ya njia za kufikisha umuhimu huu kwa wanafunzi wake.

Amesikia habari za ajuza/kikongwe mmoja, Bibi Koku, anayeishi jirani ni maarufu kwa uhadidhiaji. Mchana mmoja, anaamua kumtembelea Bibi

Koku na akamuuliza kama atakuwa tayari kuhadithia hadithi wanafunzi wa mwalimu Biyela. wa darasa la nne. Kikongwe huyu anakubali lakini anasema ‘jioni tu’. Anasisitiza kuwa watu wanaohadithia hadithi mchana wanakaribisha njaa katika jamii yao naye hayuko tayari kufanya hivyo.

Haraka, suala hili linakuwa jambo la kuvitia kwa Bibi Biyela-Ana uhakika litavuta usikivu wa wanafunzi wake na kuwapa uelewa zaidi wa utamaduni wa kuhadithia hadithi.

Kwa hiyo anapanga kuleta chombo cha kurekodi/kinasa sauti ili amrekodi Ma’Koku akihadithia hadithi, pamoja na kuongelea miiko ya kuhadithia mchana. Anajitahidi na kuhakikisha kuwa kikongwe huyu anaongelea suala hili namna ambayo wanafunzi wake wataelewa. Inavyoonekena, Ma’Koku ametatua tatizo lake kwa kuhadithia kinachowatokea watu wanaohadithia hadithi mchana.

Siku ya somo, Bi Biyela anakagua kinasa sauti chake na anahakikisha kuwa kote kote kiko sawa. Anatoa utangulizi wa somo, anawauliza wanafunzi kama wamewahi kusikia hadithi zilizotolewa na watu. Watoto wanahamasika -wanamsikiliza Ma’Koku akihadithia hadithi.

Baadaye, Bibi Biyela anaendesha majadiliano kuhusu kwa nini Ma’Koku hakuja kuwahadithia hadithi shuleni asubuhi ile. Anashangazwa na ukweli kwamba wanafunzi wengi wanaijua desturi ya kutohadithia mchana. Kufikia mwishoni wa kipindi, walikuwa wamejenga uelewea mkubwa wa mila na miiko inyohusiana/ambatana na suala hili.

Shughuli ya 1: Kuchagua hadithi murua/inayopendwa

Kabla ya somo, muulize kila mwanafunzi kuamua hadithi fupi aipendayo ili ashirikishe wenzake darasani.

Liandae darasa katika makudi madogo madogo ya watu kati ya wane hadi sita. Mtake kila mwanafunzi kuwahadithia hadithi yake kwenye kundi lake. Kabla hawajaanza, sisitiza kuwa kila mmoja apate nafasi ya kuhadithia pia wasikilize hadithi za mwenzao.

Baada ya hapo, waambie kila kundi kuchagua hadithi moja kutoka kwenye makundi yao. Hizi wataziwasilisha darasani. Kama ukigundua kuwa kuna kundi lolote linapata shida ya kukubaliana, ingilia kati kuwasaidia wachague hadithi.

Wape nafasi vikundi wajiandae. Ikiwezekana, andaa, mavazi, zana, midoli, vifaa vya muziki, n.k. au waambie wanafunzi wavilete, ili kufanikisha hadithi zao na kuwasaidia kufikisha ujumbe/maana.

Kila kundi liwasilishe hadithi yao kwa darasa zima na kufafanua kwa nini wanaipenda.

Hatimaye, jadiliana na darasa lako sehemu muhimu za hadithi, mwanzo? Hadithi yenyewe, mtiririko wa visa, mandhari, wahusika na mwisho/tamati.

Ulishangazwa na hadithi ambazo wanafunzi wako walichangua? Ni vizuri kiasi gani wanafunzi wako walifanya kazi pamoja katika makundi madogo? Je, unahitaji kupanga makundi tofauti kazi ijayo?

Somo la 2

Mila nyingi na imani zinaenezwa kupitia hadithi. Katika sehemu hii, tunashauri namna ya kujenga uelewa wa wanafunzi juu ya umuhimu wa hadithi katika urithisha/eneza mila hizi na kutoa ujumbe jinsi/namna watu wanavyopaswa kuishi.

Inavutia/sisimua kwa wanafunzi wasikiliza wataalamu wa hadithi akihadithia hadithi zao. Katika uchunguzi kifani 2 , mwalimu anaandaa ziara kwenda kwa mwadithiaji. Katika shughuli 2, unatumia mbinu ya kuchangia mawazo kuchunguza ufahamu wa wanafunzi wako juu ya ngano/kisa cha asili na kugundua njia za kuziweka hadithi hizi pamoja (angalia nyenzo rejea muhimu: Kutumia ramani kifani na kuchangia mawazo kugundua mawazo).

Uchunguzi kifani ya 2: Kuwapeleka wanafunzi kumtembele/kuzuru msimuliaji hadithi.

Bwana Bakari ni mwalimu wa masomo ya sayansi ya jamii na sanaa katika shule moja umasaini. Bwana Bakari alimtembelea kiongozi wake wa kijiji Mzee Sokoine, na kumuuliza iwapo awalete wanafunzi wa darasa la sita(6) nyumbani kwake. Pia alimuuliza kiongozi huyo kama atawaeleza ngano wanafunzi. Hili lilikubaliwa.

Siku moja kabla ya siku ya mapatano, ndugu Bakari aliliambia darasa kuwa atawapeleka nje ya shule kutembelea boma ya Mzee Sokoine ili wasikilize ngano za wamasai. Ili kuwaandaa wanafunzi wake, aliandaa mjadala mfupi juu ya uzoefu wao juu ya hadithi na nini wanafikiri watapata kesho yake na kuwatengenezea ramani ya kufikirika ya mawazo yao ubaoni.

Ngano/kisa alichosimulia mzee Sokoine kiko katika Nyenzo rejea 1: sauti ya kiwavi. Ngano hiyo ilikuwa na ujumbe muhimu na masomo ya kujifunza. Mwalimu Bakari, alivyosikiliza hadithi, alikuwa tayari anaandaa maswali atakayouliza darasani juu ya hadithi ili kutoa mafundisho haya. Kwa vile Mzee Sokoine alikuwa Mzee wa kuheshimiwa, aliweza kuwavutia watoto juu ya utajiri wa ukoo/jadi unaoambatishwa na hadithi za mila za kimasai ambazo zilitolewa kwa muda mrefu na maana zake ili kuziimarisha kutoka kizazi hadi kizazi nyingine. Ndugu Bakari aligundua kuwa alifanya maamuzi ya busara kwa kuwapeleka wanafunzi kwenye boma, badala ya kuwaeleza hadithi yeye mwenyewe.

Shughuli ya 2: Kutengeneza Ngano za Kiasili

Kabla ya somo, kusanya masimulizi yaliyoandkiwa na ya mdomo ya hadithi za kimila kadri utakuvyoweza. (Angalia Nyenzo rejea 2 : Hadithi na hekaya/ngano kutoka Afrika kwa ajili ya tovuti na soma Nyenzo rejea muhimu: kutumia teknolojia mpya.

Waambie

Mwanafunzi kujadiliana kuhusu ngano za asili kama ambavyo wanakumbuka kuzisikia.

Kisha, gawanya darasa lako katika makundi ya wanafunzi wanne wanne. Litake kila kundi kuchagua hadithi iliyoainishwa wakati wa kujadiliana na kuiandika kwa kirefu wakiweka wakiweka na michoro.

Toa maelekezo, kama

Jina la ngano?

Ngano hiyo inatoka jamii/ukoo gani? Ngano hiyo inatoa ujumbe gani?

Ni somo/mafundisho gani yanaweza kupatikana kwenye ngano?

Nani huhadithia hadithi?

Ni hadhira gani imelengwa na kwa nini hadhira hii imelengwa? Ni muda/wakati gani ngano husimuliwa? Kwa nini?

Ni muda gani kwa siku ngano husimuliwa? Kwa nini?

Hadithi zilizotolewa zinaweza kutenenezwa na kutumika kama vijitabu vya rejea shuleni. Inawezekana kuzichapisha na kutumika katika jamii au zaidi ya hapo.

Somo la 3

Kuwa na uelewa mzuri wa ngano za asili ni msingi mzuri kwa wanafunzi wako kubuni hadithi zao. Kusikiliza hadithi zilizohadithiwa kwa kuigizwa na kutumia maneno zinawafanya kujiamini na kuwa tayari kushiriki katika kuandika na kuzalisha/kutoa ngano zilizobuniwa vyema.

Lengo la sehemu hii ni kutumia nyenzo rejea za kawaida ili kuwajengea wanafunzi wako ujuzi wa kuandika hadithi na mashairi yao. Utaweza pia kujenga ujuzi wa kupanga shughuli za ujifunzaji unaowashirikisha wanafunzi.

Katika Uchunguzi kifani 3 mwalimu anatumia kipindi cha radio kuhamasisha wanafunzi kuhusu hadithi. Shughuli muhimu picha zinatumika kama kichocheo. Kwa watoto wadogo zaidi wanaweza kuchora picha kama hadithi zao. Ni muhimu kila mwanafunzi kuweza kutoa hadithi bila kuhangaika na kuandika maneno kwa usahii au kwa mwandiko mzuri.

Uchunguzi kifani ya 3: Kujifunza kutoka kwa mtaalam wa kuhadithia hadithi

Huku akisikiliza radio, Bi Sala, Mwalimu wa mafunzo ya jamii, alisikia kuwa Ijumaa inayofuata kutakuwa na programu/kipindi ambacho msimuliaji hadithi maarufu na mwandishi atahojiwa.

Bahati nzuri, programm/kipindi kilipangwa kwa muda mwafaka, wakati wa kawaida wa shule. Hivyo Bi Sala alikuja shuleni na radio yake. Amejiandaa pia kurekodi kipindi hicho.

Kabla ya kipindi hicho kuanza, alijadiliana na wanafunzi wake walichokijua juu ya mwandishi, na walitegemea nini kutokana na maongezi atakayotoa wakati atakapokuwa anahojiwa.

Wakati wa kipindi, mwandishi alieleza juu ya muundo wa hadithi, dhamira/wazo kuu, wahusika na mandhari. Alitoa ushauri juu ya mchakato wa unadishi. Pia alizungumzia juu ya kilichomvuta na mawazo yake aliyapata wapi. Baada ya kipindi, Bi Sala aliuliza maswali yafuatayo ili kuchochea mjadala kwa wanafunzi wake:

Unaweza kujifunza nini kutoka kwa mwandishi huyu yanayoweza kukufanya uwe mwandishi mzuri?

Kipi kinamkuchochea? Je kuna mambo katika maisha au jamii yako unayotoka kuandikia?

Uandishi mzuri/maandishi mazuri yana muundo na habari zipi? Aliuliza swali la mwisho mwishoni mwa kipindi kwa sababu alitaka

kichochewe na mambo makubwa.

Mwishoni mwa somo, alisema kuwa kwenye uandishi wa ubunifu utakaofuata, utawataka wanafunzi kujaribu mbinu zilizopendekezwa na mhadithiaji. Ataangalia ushahidi kama wamezingatia masuala haya na kwa uangalifu atatoa mrejesho.

Shughuli muhimu: Kuandika na kusimulia hadithi

Wape wanafunzi kichokoo ili kupata mawazo juu ya maisha, Jamii au Jamii pana. Angalia Nyenzo rejea 3: Picha za hadithi kwa ajili ya taswira zinazofanyakazi vizuri, lakini unaweza kuchagua kitu kingine cha kufanana/aina hiyo.

Tumia Nyenzo rejea 4: kutumia picha kama kuchokoo cha kuandika hadithi ili ikuongoze, jadili picha ambayo darasa limechagua.

Waambie wanafunzi waandike hadithi zao wenyewe. Wahamisishe kuongeze mawazo yao na matukio/ wanapoandika. Kwa mfano: Nini kilitokea kabla kilichosababisha picha itokee na nini kitafuata?

Siku inayofuata, wanafunzi walisomeane hadithi zao katika makundi madogo madogo na kila kundi linamchagua mtu mmoja wa kusomea darasa zima. Wasisitize umuhimu wa kutumia sauti na ‘vichocheo’ kama inawezekana ili viwasaidie.

Unaweza kuziweka hadithi zote kwenye vitabu vya darasa

Nyenzo-rejea ya 1: Sauti ya kiwavi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Hapo zamani za kale, kiwavi kilitambaa hadi ndani ya nyumba ya sungura, wakati sungura akiwa hayupo, na kukaa kwa raha zake. Sungura aliporudi, aligundua alama mpya ardhini pangoni mwake. Aliita

‘Nani yuko ndani ya nyumba yangu? Kiwavi akalipuka kwa sauti kubwa, “Ni mimi! Ndiyo, ni mimi ninaye sagasaga kifaru hadi ardhini na kukanyaga tembo kwenye vumbi”.

Sungura akanyong’onyea na kulia akisema, ‘kiumbe mdogo kama mimi atamfanya nini kiumbe anayesagasaga kifaru na kukanyaga kanyaga tembo?’

Punde alikutana na mbweha na kumuuliza/kumwomba aongee na kiumbe huyo wa kutisha aliyejitwalia mji wake (sungura) ili amshawishi kuoondoka. Mbeha alikubali, na walipolifikia eneo alibweka kwa nguvu na kusema ‘Nani yuko ndani ya nyumba ya rafiki yangu Sungura?’

Kiwavi akajibu kwa sauti iliyotetemesha nchi, ‘Ni mimi! Ndiyo, mimi ninaye sagasaga kifaru hadi ardhini na kukanyagakanyaga tembo mavumbini!’ Alivyosikia haya, mbweha akafikiri ‘kwa vyovyote siwezi kufanya chochote juu ya kuimbe hicho,’ akaondoka mbiombio.

Sungura akamleta chui, na kumwomba amsaidie. Chui akamhakikishia kuwa hakutakuwa na tatizo. Alipofika kwenye tukio, chui alikwaruza kwa kucha zake na kusema, ‘Nani yuko ndani ya nyumba ya rafiki yangu sungura?’ Kiwavi alimjibu katika hali aliyowajibu wawili waliopita. Chui alihadharishwa na kufikiri, ‘kama kusagasaga kifaru na kukanyagakanyaga tembo, sitaki hata kufikiri atakachonifanya!’

Kilichofuata sungura akamwona kifaru. ‘Bila shaka, ni mnyama mwenye kutisha,’ kifaru alijigamba. Kifaru alitembea kwenda kwenye pango la sungura, alipokoroma na kuparura ardhi kwa miguuyake mizito.

Lakini kifaru alipouliza aliyeko ndani na kusikia sauti ya kutisha ya kiwavi, akafikiri ‘Nini, anasema anaweza kunisagasaga ardhini?’ Na kifaru akatoweka, akitokomea msituni.

Akiwa amekata tamaa, Sungura akamjaribu tembo kwa kumwomba masaada wake. Lakini kama wengine, aliposikia maneno ya kiwavi tembo akajua kuwa hakuwa anatamani kukanyagwakanyagwa kama mavumbi, akaondoka zake.

Kwa kusikitishwa na hoja hii, Sungura alimwomba chura aliyekuwa anapita kama anaweza kumsaidia na kumfanya kiumbe aliyowatisha wanyama wote aondoke nyumbani mwake. Chura alikwenda kwenye mlango wa pango na kuuliza aliyekuwa ndani. Alipokea jibu lilelile walilopewa wengine. Kisha chura alisogea karibu na kupiga kelele, ‘Mimi niliye na nguvu kuliko wote, nimekuja hatimaye. Mimi husagasaga wale wasagao vifaru! Mimi huwakanyagakanyaga tembo!’

Kiwavi aliposikia hayo kule ndani alitetemeka. Alihisi kivuli cha chura kikisogea na kufikiri, ‘Hata hivyo mimi ni kiwavi tu! Na kiwavi akajificha kwenye tundu lililokuwa kwenye pembe ili asionekane. Wanyama waliokusanyika karibu na nyumba ya sungura walimkamata na kumtoa nje. ‘Nani, wewe?’ Wote walipiga kelele kwa kutoamini.

‘Siwezi kufikiri kukaa ndani ya pango hilo!’ Kiwavi aliyasema pua akawa amebinua juu, ‘mwangwi wake anatisha kwa kiumbe mungwana kama mimi!’ Alivyo ondoka zake, wanyama wengine wakacheka kwa matatizo/usumbufu aliowasababishia.

Nyenzo-rejea ya 2: Hadithi na hekaya kutoka Afrika

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Tovuti hapa chini imekupa zaidi ya hadithi 50 na ngano katoka Afrika http://www.gateway-africa.com/ stories/

Kama hii hapa chini

Radi na mwale wa radi

Hapo zamani za kale radi na mwale waliishi hapa duniani pamoja na watu. Radi alikuwa kondoo jike na mwale ulikuwa mtoto kondoo dume. Hakuna mnyama aliyekuwa maarufu kwa watu, kwani pale mtu alipomkosea mwale, angepaa kwa ghadhabu na kuanza kuunguza chochote alichokutana nacho. Hii ilihusisha vibanda, vihenge na hata miti

mikubwa. Wakati mwingine angeharibu mazao shambani kwa moto wake na muda mwingi aliua watu waliopita kwenye anga zake. Radi alipojua kuwa wanae alikuwa na tabia ya aina hii, aliinua sauti na kumpigia kelele na zilikuwa kilele kweli kweli. Kiuhalisia, majirani walikuwa wamehuzunishwa, kwanza kwa hasara, iliyosababishwa na mwale na kwa sauti zisizovumilika zilizotoka kwa mama yake zilizokuwa zinafuatia upasukaji wake. Wanakijiji walilalamika kwa mfalme matukio mengi hadi pale alipowaagiza wote wawili kuishi kwenye mpaka wa kijiji na kuwaambia kuwa wasjie wakachanganyika tena na watu. Hata hivyo, hii haikusaidia kwani mwale aliendelea kuwaona wanakijiji walipokuwa wakitembea kijijini/Mitaani hivyo kupata urahisi wa kuendelea kukwaruzana/kuzozana nao.

Mfalme akawatumia ujumbe tena aliwaambia ‘Nimewapa fursa nyingi kuishi maisha mazuri, lakini naona kuwa haijafaa chochote. Kuanzia sasa na kuendelea, mwende mbali na kijiji chetu, mkaishi kwenye pori. Hatutaki kuona sura zenu hapa tena.’ Radi na mwale iliwabidi watii mfalme na kukubali kufuata hukumu yake. Hivyo waliondoka kijijini, wakiwa na hasira na wakazi wake. Bado kulikuwa na matatizo makubwa kwa hifadhi za wanakijiji, kwani mwale alikasirika kwa kufukuzwa kiasi

kwamba aliwasha moto kwenye pori lote, na kwa vile ilikuwa wakati wa kiangazi, hali hii ilikuwa mbaya zaidi.

Moto aliambaa kwenye mashamba madogo ya watu na wakati mwingine kwenye nyumba zao, sasa walikuwa kwenye mashaka tena. Mara nyingi walisikia sauti ya kondoo jike (mama wa kondoo dume) akimwita mwanae akimuonya aache lakini kwa vile aliyafanya baada ya tukio, haikuleta tofuati yoyote. Mfalme aliwaita washauri wake ili wamshauri. Baada ya mdahalo mkubwa, wakapata mpango. Kwa nini tusiwafukuze radi na mwale jumla watoke duniani, na kuwasukumia kuishi angani? Hivyo mfalme akaafiki. Radi na mwale walitupwa/sukumwa angani ambapo

watu walitumainia kuwa hawasabisha madhara tena.                                                                Lakini mambo hayakwenda kama walivyotarajia; hata hivyo mwale bado anaonyesha hasira yake mara kwa mara na hawezi kuacha kutupa moto duniani anapokasirika. Unaweza kumsikia mama yake akimkemea kwa sauti yake ya kutisha.

Imepatikana katika chanzo: Gateway Africa, Website

Nyenzo-rejea ya 3: Picha za hadithi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi.

Chanzo asilia: Arthus-Bertrand, Y. 2004. 365 Jours. Editions de la Martiniēre: Paris

Nyenzo rejea 4: Kutumia picha kama kichokoo cha kuandika hadithi

Nyenzo ya Mwalimu kwa kupanga au kubadili nyenzo ili zitumike na wanafunzi

Picha zinaweza kuwa kichokoo kizuri cha uandishi wenye ubunifu kabla wanafunzi hawajaandika hadithi au ushairi wao. Unaweza kuijadili picha iliyochaguliwa na darasa zima au uwe na makala nyingi za sura hiyo hiyo au sura tofauti ili wanafunzi wajadiliane katika makundi yao. Kama una darasa kubwa unahitaji kuwa na sura nyingi au ufanye kazi na nusu darasa kwa wakati mmoja wakati wengine wakifanya kazi nyingine.

Maswali yafuatayo yanaweza kutumika pamoja na picha yoyote ili kuchokoa mawazo na ubunifu. Unaweza kuandika maswali ubaoni na kuyajadili na darasa zima au lipe kila kundi maswali yake na waambie watoe majibu ndani ya muda mfupi/dakika chache. Baadhi ya maswali hayatafaa kwa kila picha. Itabidi uchague yale yanazoendena na malengo au waambie wanafunzi kuibua maswali juu ya picha.

1.       Unafikiri kinatokea nini kwenye picha hii?

2.       Unafikiri inaitwaje?

3.       Nini kinakuvutia kwenye picha hii? Kwa nini?

4.       Unapenda nini kwenye picha hii?

5.       Hujapendezwa na nini kwenye picha hii?

6.       Kuna hadithi gani kwenye picha hii?

7.       Nini/kipi kilisababisha picha hii ipakwe rangi/picha hii ichukuliwe?

8.       Unafikiri nini kitatokea baadaye?

Nakili majibu ya wanafunzi ubaoni ili wayatumie ukiwapa kazi ya kuandika hadithi; lakini wahamasishe kuwa wabunifu na kutumia mawazo yao.

Wahamasishe kufikiri kilichotokea hapo kabla ya picha na ikiwezekana waanzie hadithi yao pale.