Skip to main content
Printable page generated Sunday, 28 Nov 2021, 12:35
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Printable page generated Sunday, 28 Nov 2021, 12:35

4. Tumia Patografu

Kipindi cha 4 cha Somo Tumia Patografu

Utangulizi

Sababu tano kuu za vifo vya wajawazito katika nchi zinazoendelea ni shinikizo la juu la damu, kutokwa na damu, maambukizi, matatizo ya leba, na utoaji wa mimba kwa njia isiyo salama. Wakati uchungu wa leba unapochukua muda mrefu, uvujaji damu, maambukizi, na matatizo ya leba ina uwezekano mkubwa. Hasa, kutokwa kwa damu na sepsisi baada ya kuzaliwa kwa mtoto (maambukizi) ni ya kawaida sana wakati leba inapodumu zaidi ya masaa 18-24. Matatizo ya leba ni matokeo ya moja kwa moja ya leba isiyo ya kawaida kwa muda mrefu. Kipindi cha 9 cha Somo kinatoa maelezo kuhusu leba ya muda mrefu isiyo ya kawaida. Unaweza kuepukana na matatizo haya. Tumia chati ambayo inaitwa patografu kutambua mwendeleo usio wa kawaida wa leba ya muda mrefu ambayo inaweza kuwa na matatizo. Pia inakutahadharisha kwa ishara ya tatizo la fetasi

Katika Kipindi hiki cha somo, utajifunza jinsi ya kutumia patografu. Utajifunza jinsi ya kusoma kile ambacho patografu inayokueleza kuhusu leba. Utajifunza hatua unayopaswa kuchukua wakati taarifa unayoandika kutoka kwa patografu inahitilafiana na ya kawaida. Leba ikiendelea vizuri, taarifa iliyo kwa patografu inakuhakikishia pamoja na kwamba mama na mtoto wana afya njema.

Malengo ya Somola Kipindi cha 4 cha Somo

Baada ya Kipindi hiki cha somo, unaweza:

4.1 Kueleza na kutumia kwa ufasaha maneno yote muhimu yaliyo kwa herufi nzito. (Swali la Kujitathmini 4.1 na 4.3)

4.2 Kuelezea umuhimu na matumizi ya patografu katika ufuatiliaji wa maendeleo ya leba. (Swali la Kujitathmini 4.1 na 4.2)

4.3 Kuelezea sehemu za patografu na muda sahihi wa vipindi vya kuandika uchunguzi wako na vipimo. (Swali la Kujitathmini 4.1 na 4.3)

4.4 Kuelezea viashiria katika patografu vinavyoonyesha maendeleo mazuri ya leba, na dalili ya hali njema ya fetasi pamoja na ya mama. (Swali la Kujitathmini 4.3)

4.5 Kutambua viashiria katika patografu kwa rufaa ya haraka hospitalini wakati wa leba. (Swali la Kujitathmini 4.3)

4.1 Kwa nini patografu ni muhimu

Patografu ni grafu inayoonyesha maendeleo ya leba, na hali ya fetasi na ya mama wakati wa leba. Ndio chombo bora zaidi cha kukusaidia kufahamu kama leba inaendelea kwa njia ya kawaida au la. Iwapo itaonyesha dalili ya tatizo la fatesi ama vipimo muhimu vya uzima wa mama zinahitilafiana na vya kawaida, patografu itakuonya. Utafiti unaonyesha kwamba matatizo kwa kina mama na fetasi kutokana na leba ya muda mrefu ulikuwa wa kiwango cha chini wakati mhudumu wa kuzalisha alipotumia patografu. Tumia patografu kila wakati unapomhudumia mama aliye katika leba nyumbani mwake au katika kituo cha afya.

Katika moduli hii vikao vya somo vinaelezea sababu kuu za kufuatilia kwa makini mama aliye katika leba. Kumbuka kwamba leba ambayo inaendelea vyema inahitaji usaidizi wako mdogo kuliko ile inayoendelea kwa njia kawaida. Unapotumia patografu kuandika taarifa wakati wa leba, utajua kwa haraka wakati kuna shida. Patografu inaweza kukusaidia kuamua wakati wa kumpa mama rufaa ya kwenda kwa kituo cha afya kilicho karibu au hospitalini kwa utathmini zaidi na kuchukua hatua.

4.2 Sehemu za patografu

Patografu ni chati yako ya mama aliye katika leba (Mchoro 4.1). Juu ya chati, andika jina na umri wa mama na hali ya "gravida" na "para". Andika kituo chake cha afya au nambari yake ya usajili ya hospitali. Andika tarehe na saa uliyoanza kumhudumia wakati wa kuzaa. Andika wakati membreni za fetasi zilipopasuka.

 • Je, kuna tofauti gani kati ya mwanamke ambaye ni multigravida na yule ambaye ni multipara?

 • Multigravida ni mwanamke ambaye amepata mimba angalau mara moja kabla ya mimba iliyoko. Multipara ni mwanamke ambaye amezaa hapo awali watoto walio na uhai angalau mara mbili kabla ya sasa.

  Mwisho wa jibu

Iwapo utatumia chati nyingine, unaweza kuandika taarifa zingine nyuma ya patografu. Andika historia ya uzazi ya mwanamke na ya matibabu aliyoyapata pamoja na ya sasa. Andika taarifa kutokana na ukaguzi wa mwili na hatua zozote ulizoanzisha. (Pamoja na dawa, maelezo ya kuzaa, na rufaa.)

4.2.1 Sehemu za grafu ya patografu

Tumia sehemu za grafu ya patografu kuandika taarifa muhimu ya fetusi au ya mama. Mchoro 4.1 unaonyesha patografu. Patografu ina sehemu hizi:

 • Chini ya maelezo ya utambulisho ya mgonjwa, andika Kiwango cha Mpigo wa Moyo wa Fetasi mwanzoni na kisha kila baada ya dakika 30. Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetusi inajumlisha kutoka 80 hadi 200 wa mdundo kwa dakika.
 • Chini ya kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi, safu mbili hukaribiana. Safu ya kwanza ni amnioni, ambalo ni neno la tiba maji ya amnioni. Kama membreni ya fetasi imepasuka, andika rangi ya amnioni ya awali na kila baada ya masaa 4.
 • Safu iliyo chini ya amnioni ni ufinyanzi. Ufinyanzi huelezea kiasi mifupa ya fuvu la kichwa cha fetusi hupishana wakati kichwa kinaingia kwa njia ya uzazi. Tathmini kiwango cha ufinyanzi mwanzoni na kila baada ya saa 4
Mchoro 4.1 Patografu kina nafasi ya juu ya maelezo ya kutambulisha mgonjwa na sehemu ya grafu chini.
 • Kwa Ufinyanzi, chati iliyopachikwa jina seviksi (sentimita) (Weka X). Andika taarifa kuhusu utanzi wa seviksi, ambacho ni kipenyo cha seviksi ya mama kwa sentimita. Pia andika kuteremka kwa Kichwa (Weka O), ambayo ni umbali gani chini njia ya uzazi na kichwa cha mtoto kimeendelea. Nakili vipimo hivi kama X au O, mwanzoni na kila baada ya saa 4. Katika safu mbili chini ya sehemu hii ya patografu, andika saa. Andika idadi ya saa ambayo umefuatilia leba.
 • Katika sehemu inayofuata, andika mikazo ya uterasi kwa dakika 10 mwanzo na kila dakika 30.
 • Katika safu mbili zifuatazo, andika taarifa kuhusu utoaji wa oksitosini wakati wa leba na kiasi kilichotolewa. (Ni daktari tu ndiye anayetoa oksitosini wakati wa leba. Utajifunza utoaji oksitosini baada ya mtoto kuzaliwa iwapo mama ana hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa)
 • Eneo linalofuata ni la dawa na viowevu vya mishipa alivyopewa mama
 • Karibu na chini ya patografu, andika vipimo muhimu vya mama. Chati ni ya mdundo wa moyo na shinikizo la damu na ni kutoka 60 hadi 180. Chini ya safu hii, andika Joto (halijoto) ya mama kwa sentigredi.
 • Chini kabisa, andika hali ya mkojo: kiasi cha protini na asetoni kwa mama. Umejifunza jinsi ya kutumia vijiti vya kupima uwepo wa protini kwa mkojo (alibumini) wakati wa utunzaji katika ujauzito.

Utajifunza jinsi ya kupatiana tiba ya viowevu ndani ya mshipa kwa wanawake ambao wanatokwa na damu nyingi katika Kipindi cha 22 cha Somo la Moduli ya Utunzaji katika ujauzito.

 • Je, rangi ya amnioni inaonyesha nini?

 • Damu nyekundu katika amnioni ni onyo kwamba mama anavuja damu ndani. Mekoniamu ya rangi ya kijani katika amnioni ni ishara ya tatizo kwa mtoto. (Mekoniamu ni kinyesi cha kwanza cha fetusi.)

  Mwisho wa jibu

4.2.2 Mistari ya Tahadhari na Hatua

Katika sehemu ya upanuzi wa seviksi na kuteremka kwa kichwa cha fetasi, angalia mistari miwili zilizohanamu zilizoandikwa Tahadhari na Hatua. Mstari wa tahadhari huanzia sentimita 4 za upanuzi wa seviksi na kuendelea hanamu kwenda juu. Wakati tahadhari huendelea kwa kiwango cha sentimita 1 kwa saa na huacha wakati upanuzi unatarajiwa kukamilika (sentimita10). Mstari wa hatua huwa sambamba na ule wa Tahadhari, na ni saa 4 upande wa kulia wa mstari wa Tahadhari. Hii mistari miwili hukuonya ili uchukue hatua za haraka iwapo leba haiendelei kwa kawaida.

Ikiwa alama zinazoonyesha upanuzi wa seviksi zikiwa zimevuka mstari wa Tahadhari, mpe mama rufaa ya kituo cha afya au hospitali. Hizi alama zinaonyesha kuwa seviksi inatanuka polepole mno. (Mstari wa Hatua ni kwa ajili ya uamuzi katika kituo cha afya.)

4.3 Nakili na ueleze maendeleo ya leba

Wakati wa leba inayoendelea kwa kawaida, seviksi hupanuka angalau sentimita 1 kwa saa moja wakati leba imeingia hatua ya kwanza iliyoimarika. Utajifunza taarifa hii katika Kipindi cha 1 cha Somo.

Isipokuwa ukigundua matatizo kwa mama au fetasi, hesabu mpigo wa moyo wa fetasi kila dakika 30 kwa dakika moja kamili. Hesabu mkazo wa uterusi kwa dakika 10.

Mwanzo, pima uke kutathmini mambo haya:

 • Kiwango cha sevikisi kupatana na kichwa cha fetasi (Rejelea mchoro 1.1) na upanuzi wa seviksi
 • Sehemu ya fetasi inayotangulia
 • Hali ya membreni ya fetasi (imeshikana au imepasuka ) na amnioni
 • Ukubwa wa pelvisi ya mama ili kubaini kama ukingo ni mkubwa kutosha motto kupita.

Kisha baada ya, kila saa 4, angalia mabadiliko katika mambo haya:

 • Upanuzi wa seviksi
 • Ukuaji wa edema kwa seviksi. (Seviksi nyembamba inaweza kuvimba ikiwa mama ataanza kumsukuma mapema zaidi. Seviksi inaweza kuvimba ikiwa leba itachukua muda mrefu na seviksi haijatanuka sana.)
 • Kama unaweza kutambua hali ya fetasi,
 • Namna kichwa cha fetasi kimeteremka
 • Ukuaji wa ufinyanzi na kaputi (Kipindi cha 2)
 • Rangi ya amnioni (ikiwa membreni ya fetasi tayari imepasuka).

Andika matokeo ya uchunguzi wako kwa patografu kwa vipindi vilivyopendekezwa wakati leba inapoendelea. Alama zinakuonyesha kama kila kitu kinaendelea vizuri au ikiwa vipimo vinasababisha wasiwasi. Unapoandika kwa patografu, hakikisha unafanya mambo haya:

 • Tumia fomumoja ya patografu kwa kila mama aliye katika leba. (Unaweza kufikiri kuwa leba ya ukweli imeanza na uandike kwa patografu, lakini baadaye utambue kwamba ilikuwa bandia. Unaweza kumtuma mama nyumbani au umshauri kuendelea na shughuli zake za kawaida za kila siku. Wakati leba umedhibitishwa, tumia patografu mpya).
 • Andika kwenye patografu wakati leba iko katika hatua ya kwanza iliyoimarika (Seviksi imetanuka sentimita 4 na juu zaidi).
 • Andika wazi, ili kila anayefahamu kuhusu patografu anaweza kuelewa na kueleza alama zako.
 • Kama ni lazima umpatie mama rufaa kwa kituo cha afya cha ngazi ya juu, tuma patografu na barua yako ya rufaa. Andika maelezeo yako ya patografu katika hiyo barua.
 • Bila kurejelea sehemu za awali, andika kwa haraka vipimo vya patografu vilivyo lazima ili kufuatilia miendo ya leba.

 • Linganisha orodha yako na patografu katika mchoro 4.1. Kama huna uhakika hata kidogo kuhusu vipimo vyovyote, basi soma tena Sehemu za 4.2 na 4.3.

  Mwisho wa jibu

4.4 Kupanuka kwa seviksi

Kama ulivyo soma katika Kipindi cha 1, hatua ya kwanza ya leba imegawanywa katika awamu iliyofishe na ya leba iliyoimarika. Awamu fishe hudumu hadi seviksi itanuke sentimita 4 na iwe imepatana na kichwa cha fetasi (Mchoro 1.1). Awamu fishe hudumu hadi saa 8, ingawa kwa kawaida huwa fupi zaidi. Tathmini afya ya mama na fetasi na uandike matokeo yote. Hata hivyo, usiandike habari hii kwa patografu hadi leba iimarike.

Kipimo cha ukeni hufanywa kwa takriban kila baada ya saa 4 hadi mtoto azaliwe. Awamu iliyomarika huanza wakati seviksi hupanuka sentimita 4. Awamu iliyoimarika hukamilika wakati upanuzi umekamilika, yaani, sentimita 10. Seviksi hupanuka sentimita 1 kwa saa moja wakati wa awamu iliyoimarika. (Seviksi utapanuka upesi katika akina mama waliowahi kuwa wajawazito mara mbili au zaidi).

Katika sehemu ya upanuzi wa seviksi kwa patografu, chini upande wa kushoto, kuna nambari 0-10. Kila namba/mraba inawakilisha upanuzi wa sentimita 1. Chini ya sehemu hii kuna miraba 24, kila moja inawakilisha saa 1. Baada ya kila saa 4, pima uke na ukadirie jinsi seviksi inatanuka. Andika alama X kwa patografu kwa nambari hiyo. Angalia seviksi ya wanawake waliowahi kuzaa mara mmoja au zaidi mara nyingi zaidi kuliko kila baada ya saa 4 wakati leba umeimarika zaidi. Mara nyingi wao huendelea haraka kuliko wanawake ambao wanazaa kwa mara ya kwanza.

 • Kwa mfano katika mchoro 4.2, ni tofauti gani katika upanuzi wa seviksi imerekodiwa kwa kipindi na muda gani?

  Mchoro 4.2 Mfano wa jinsi ya kunakili upanuzi wa seviksi (zilizoandikwa na alama za X) na kuteremka kwa kichwa cha fetasi (zilizoandikwa na alama za 0) kwa patografu.
 • Seviksi ilikuwa imepanuka sentimita 5 saa 1 baada ya kuanza ufuatiliaji wa uchunguzi wa kuzaa. Baada ya saa zingine 4, seviksi ya mama ilikuwa imepanuka kikamilifu sentimita10.

  Mwisho wa jibu

Kama uchunguzi wa kuzaa kutaendelea vizuri, alama ya upanuzi wa seviksi hubaki juu au upande wa kushoto wa mstari wa Tahadhari.

Ikiwa membreni imepasuka na mama hana leba, usipime uke kwa vidole. Huwezi kutambua leba na unaweza kuanzisha maambukizi. (Kupasuka kwa mapema wa membreni, umeelezwa katika Kipindi 17 cha Somo la Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito)

4.5 Kushuka kwa kichwa cha fetasi

Leba kunapoendelea vizuri, kichwa cha fetasi hushuka kadiri seviksi inavyopanuka. Andika kushuka huko kwa sehemu hiyo ya patografu, lakini tumia O kama ishara. Kukadiria maendeleo ya kushuka kwa fetasi, tathmini pahali kichwa cha fetasi kimefika kwenye pelvisi (Mchoro 4.3). Pima uke kwa vidole vilivyo na glavu. Hisi sehemu inayotangulia kwa fuvu ya fetasi ukilinganisha na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu katika ukingo wa pelvisi ya mama.

Mchoro 4.3 Tathmini pahali pa kichwa cha fetasi kwa kupima uke, ukilinganisha na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu katika ukingo wa pelvisi ya mama. (Chanzo: Shirika la Afya Duniani, 2008, Midwifery Education Module: Managing Prolonged and Obstructed Labour, Mchoro 7.28, ukurasa 132)

Mchoro 4.3 kinaonyesha kuwa stesheni 0 ni wakati kichwa cha fetasi kiko katika kiwango kimoja na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiumu. Iwapo kichwa kiko juu ya njia ya uzazi kupita sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiumu, alama hupewa nambari ya kutoa. Katika alama -4 au -3 kichwa cha fetasi bado kina "elea" na hakijaingia kwenye pelvisi. Katika alama ya -2 au -1, kichwa kiko karibu na sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu.

Iwapo kichwa cha fetasi kiko chini ya njia ya uzazi kupita sehemu nyembamba ya mfupa wa iskiamu, alama hupewa nambari ya kuongeza. Katika amala +1 na hata zaidi katika alama +2, sehemu ya kichwa cha mtoto huwa hutoka wakati wa mikazo. Katika alama ya +3, kichwa kinatokea kwa uke ya mama, kumaanisha kinaonekana katika ufunguzi wa uke hata kati ya mikazo. Seviksi sasa inapaswa kuwa imepanuka kikamilifu.

Ni tatizo kuweka alama mbalimbali ya uteremkaji wa fetasi kwa patografu. Alama ya upanuzi wa seviksi na kushuka chini kwa kichwa huwa na kipimo cha 0-10 katika mizani. Kwa kawaida, thamani ya 0 hadi 5 hutumiwa kunakili kiwango cha kushuka chini kwa fetasi. Jedwali 4.1 linaoonyesha jinsi ya kubadilisha alama ya kichwa cha fetasi (Mchoro 4.3) ili kuweka alama kwa patografu kwa kuandika O. (Kumbuka, kuweka alama ya kwenda chini kwa fetasi na alama za O na upanuzi wa seviksi na alama za X, ili zote mbili hazichanganywe).

Kichwa cha mtoto kinapotokea kwa uke ya mama (alama ya +3), unaweza kukosa wakati wa kuandika O kwenye patografu!

Jedwali 4.1 Alama ya kichwa cha fetasi (inayoamuliwa na kupima uke) na alama ya kushuka kwa fetasi kwa patografu.

Alama ya kichwa cha fetasi (Mchoro 4.3)Alama kwa patografu
–4 or –35
–2 or –14
03
+12
+21
+30
 • Nini maana ya crowning na inakueleza nini?

 • Crowning inamaanisha kwamba sehemu inayotangulia kwa fuvu ya fetasi inaonekana kati ya mikazo. Wakati kichwa cha mtoto kinapotokea kwa uke wa mama, seviksi inatanuka kikamilifu.

  Mwisho wa jibu

4.6 Tathmini ufinyanzi na utengenezaji wa kaputi

Mchoro 4.4 Mishono na utosi katika fuvu ya mtoto mchanga.

Mifupa tano zisizoungana na fuvu ya fetasi huunganishwa na mishono, ambazo hupindika wakati wa kuzaa. Maeneo mawili yaliyo makubwa na nyororo huitwa utosi (Mchoro 4.4). Msongamano katika mishono na utosi inaruhusu mifupa ya fuvu kupishana ikiwa mikazo inalazimisha kichwa chini kwa njia ya uzazi. Kupishana kwa mifupa ya fuvu ya fetasi huitwa ufinyanzi. Kichwa cha mtoto kinaweza kuonekana kimechongoka au kunyooka wakati anazaliwa (Mchoro 4.5).

Mchoro 4.5 Mabadiliko ya kawaida katika ufinyanzi wa fuvu ya mtoto mchanga, ambayo kwa kawaida hupotea katika siku 1-3 baada ya kuzaliwa.

Baadhi za fuvu ya mtoto huwa na sehemu iliyovimba iitwayo kaputi katika eneo lililokuwa limefinywa kwa seviksi wakati wa leba na kuzaa (Mchoro 4.6). Kaputi huwa kawaida hata wakati wa leba inayoendelea kikawaida. Kaputi ambayo inaendelea katikati ni ya kawaida. Kaputi inayotokezea kwa upande mmoja si ya kawaida. Hisi ukichunguza ufinyanzi au kaputi mtoto anaposonga chini katika njia ya uzazi. Ukigundua mojawapo, hakikisha kwamba ufunguzi wa pelvisi ni mkubwa kutosha mtoto kupitia. Pelvisi ndogo huwa kawaida kwa wanawake waliokuwa wana utapiamlo wakiwa watoto. Pelvisi ndogo ni kisababishi cha mara kwa mara ya leba ya muda mrefu na matatizo.

Mchoro 4.6 Kaputi ya fuvu ya fetasi huwa ya kawaida ikitokea katikati, lakini si kawaida ikitokea upande mmoja.

Uvimbe katika upande mmoja wa kichwa cha mtoto mchanga ni ishara hatari. Mpe mtoto rufaa ya haraka hospitalini. Damu au viowevu vingine vinaweza kukua katika fuvu la mtoto.

4.6.1 Kunakili ufinyazi kwenyepatografu

Ili kutambua ufinyanzi, kwanza papasa mistari ya mshono kwenye kichwa cha fetasi. (Kwa maelezo, angalia Mchoro 1.4 katika Kipindi cha1.) Fanya uamuzi hali hizi zikihusika. Mifupa ya fuvu zilizo na uwezekano mkubwa zaidi kupishana ni mifupa ya parieto. Mifupa hii huunganishwa na mshono wa sagita, na huwa na utosi wa mbele na wa nyuma hadi mbele na nyuma.

 • Mishono zilizokaribu: Mifupa ya fuvu zilizokaribiana hugusana, lakini haipishani. Ufinyanzi huu huitwa awamu ya 1 ya ufinyanzi (+1).
 • Mishono zilizopishana lakini zinaweza kurudi: Utahisi kwamba mfupa moja wa fuvu unapishana na mwingine. Wakati unaposukuma mfupa uliopishana kwa utaratibu, hurudi kwa urahisi. Ufinyanzi huu huitwa awamu ya 2 ya ufinyanzi (+2).
 • Mishono zilizopishana na zisizorudi: Utahisi kwamba mfupa moja wa fuvu unapishana na nyingine. Unapojaribu kusukuma mfupa uliopishana, hairudi nyuma. Ufinyanzi huu huitwa awamu ya 3 ya ufinyanzi (+3). Iwapo utapata +3 ya ufinyanzi na maendeleo duni ya leba, hatari ya matatizo ya leba huongezeka.

Iwapo utatambua dalili za matatizo ya leba, mpe mama rufaa ya haraka kwa kituo cha afya. Kipindi cha 9 cha Somo kinatoa maelezo zaidi.

Kuandika awamu ya ufinyanzi kwa patografu, tumia vipimo kutoka 0 (hakuna ufinyanzi) hadi +3, na uyaandike kwa mistari ya mraba:

0        Mifupa zinatenganishwa na mishono zinaweza kuhisiwa kwa urahisi.

+1     Mifupa zinagusana tu.

+2     Mifupa zinapishana lakini zinaweza kutenganishwa kwa urahisi kwa kufinya kwa kidole.

+3     Mifupa zinapishana lakini haziwezi kutenganishwa kwa urahisi kwa kufinya kwa kidole.

Patografu haina nafasi maalum ya kuandika kuhusu kaputi. Hata hivyo, kila wakati unapopima uke, tafuta kaputi. Kama ufinyanzi, andika awamu ya kaputi kama 0, +1, + 2 au +3. Kaputi +1 ni ndogo na +3 ni kubwa. Unaweza kuandika awamu ya kaputi nyuma ya patografu au kwa rekodi ya afya ya mama.

 • Je, ikiwa unatathmini awamu ya ufinyanzi wa fuvu ya fetasi. Ni matokeo gani itakayo kufanya umpe mwanamke ambaye yuko katika leba rufaa ya haraka, na ni kwa nini?

 • Iwapo utapata ufinyanzi ulio +3 na leba inamwendeleo duni, inaweza kumaanisha kwamba uterasi ina matatizo.

  Mwisho wa jibu

4.7 Mikazo ya uterasi

Mikazo mizuri ya uterasi ni muhimu kwa maendeleo mazuri ya leba (Kipindi cha 2). Kwa kawaida, mikazo huwa nyingi na hudumu kadiri leba inavyoendelea. Weka alama ya mikazo kila dakika 30 kwenye patografu katika alama yao, ambayo iko chini ya safu ya saa na wakati. Katika alama hii andika "Mkazo kwa dakika 10" na kipimo kimehesabiwe kutoka 1 hadi 5. Kila mraba unawakilisha mkazo mmoja. Ikiwa mikazo miwili itahisiwa katika dakika 10, weka alama kwenye miraba miwili.

Katika kila mraba, onyesha muda wa kila mkazo na ishara katika mchoro 4.7.

Mchoro 4.7 Utusitusi tofauti ambao utakaochora kwa mraba wa partografu unaonyesha nguvu na muda wa mikazo.

4.8 Tathmini na unakili afya ya fetasi

Unajuaje kuwa fetasi yuko katika afya nzuri wakati wa leba na kuzaa? Tathmini hali ya fetasi kwa njia mbili:

 • Hesabu mpigo wa moyo wa fetasi kila baada ya dakika 30.
 • Kama membreni ya fetasi imepasuka, angalia rangi ya amnioni.

4.8.1 Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kama daliliya tatizo la fetasi

Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi wakati mimba imetimiza muda wa kuzaliwa (wiki 37 na zaidi) iko kati ya midundo 120-160 kwa dakika. Hesabu mpigo wa moyo wa fetasi wakati wowote katika leba. Ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo kiko chini ya midundo 120 au zaidi ya 160 kwa dakika, hesabu mara nyingi mpaka utulie katika kiwango cha kawaida. Ni kawaida kwa mpigo wa moyo wa fetasi kuwa nje na kisha kurejea hali yake. Hata hivyo, matatizo ya fetasi wakati wa leba na kuzaa zinaweza kuonyeshwa kwa njia hizi:

 • Mpigo wa moyo wa fetasi kinabaki chini ya mipigo 120 kila dakika kwa dakika 10 au zaidi. (Madaktari huita bradikadia ya fetasiilioendelea.)
 • Mpigo wa moyo wa fetasi ikiwa zaidi ya 160 kila dakika kwa dakika 10 au zaidi. (Madaktari huita takikadia ya fetasiilioendelea).

4.8.2 Visababishi vya tatizo la fetasi

Hali nyingi huathiri afya ya fetasi wakati wa leba na wa kuzaa. Lazima fetasi iwe na plasenta inayofanya kazi vizuri na virutubisho na oksijeni kutoka kwa damu ya mama mjamzito. Ulijifunza jambo hili katika Kipindi cha 5 cha Somo ya Moduli ya Utunzaji katika ujauzito. Ikiwa damu ya mama au plasenta haifanyi kazi vizuri, fetasi yuko katika hatari ya asifiksia. Fetasi aliye na asifiksia huwa na mpigo wa moyo ulio wa kiwango kilicho mbali na ya kawaida. Hali nyingine zinazoweza kuathiroi afya ya fetasi zinaweza kuonyeshwa na kiwango cha mpigo wa moyo usiokuwa sawa. Hali hizi zimeonyeshwa katika Kisanduku 4.1.

Ulijifunza kuhusu hitilafu za shinikizo la damu wakati wa mimba, anemia ya wajawazito, na kuachilia kwa plasenta katika Vikao vya 18, 19, na 21 vya Somo la Moduli ya Utunzaji katika ujauzito, Sehemu ya 2.

Kisanduku 4.1 Sababu zinazopelekea mpigo wa moyo wa fetasi kutokuwa wa kawaida

Damu kutoka kwa plasenta hadi kwa fetasi hupungua, hali inayotokea mambo haya yanapofanyika:

 • Hitilafu ya shinikizo la damu katika ujauzito.
 • Mama akiwa na anemia.
 • Upungufu wa kiasi cha damu ya mama, ambayo huwa ni haipovolemia. Hutokea kutokana na upungufu wa damu, au upungufu wa viowevu mwilini kupitia kutapika na kuhara.
 • Haipoksia ya mama, ambayo ni ukosefu wa oksijeni. Hutokea mama akiwa na ugonjwa wa moyo au wa mapafu, au akiishi katika mwinuko wa juu sana.
 • Plasenta iliyo "nzee."
 • Amnioni inakuwa kiasi kidogo, na kuzuia fetasi kusonga kwa urahisi. Mwili wa mtoto unaweza kufinya kambakitovu kwa ukuta wa uterasi.
 • Kambakitovu inafinywa. Hutokea ikija chini ya njia ya uzazi kabla ya fetasi, au ikizunguka shingoni mwa mtoto.
 • Plasenta ikitengana na ukuta wa uteresi mapema, ambayo ni kuachilia kwa plasenta.

Hesabu kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kila dakika 30 na uweke alama kwenye patografu. Patografu inaweza kusaidia kugundua mkwepuko wowote mbali na ya kawaida. Ukigundua kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi wowote usio wa kawaida, usisubiri dakika 30 zingine. Pima kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi mara nyingi iwezekanavyo. Iwapo huo mpigo usio wa kiwango cha kawaida utaendelea kwa zaidi ya dakika 10, mpe mama aliye katika leba rufaa haraka.

4.8.3 Nakili kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kwenye patografu

Kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi huandikwa juu ya patografu. Katika kipindi cha kwanza cha leba, pima kila baada ya dakika 30 ikiwa kila kiwango kiko sawa. Katika kipindi cha pili, pima kila baada ya dakika 5. Hesabu kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi nyakati hizi:

 • Mara nyingi iwezekanavyo kwa muda wa dakika kama 10 na uamue la kufanya baada ya hapo.
 • Hesabu kila baada ya dakika 5 iwapo amnioni inamekoniumu iliyo na rangi ya kijani au nyeusi. (Patografu huita kiowevu hiki Liquor.)
 • Wakati wowote membreni ya fetasi itapasuka.
 • Wakati mwingine kambakitovu hutokea na inafinywa, au kuachilia kwa plasenta hutokea wakati amnioni inatoka.

Kwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi, kila mraba kwa patografu inawakilisha dakika 30. Wakati kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ni cha kawaida na amnioni haina rangi au ina rangi kidogo ya damu, andika matokeo kwenye patografu (Mchoro 4.8). Unapohesabu kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kwa vipindi vya chini ya dakika 30, tumia upande wa nyuma wa patografu kuandika kila kipimo. Tayarisha safu ya wakati na kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi.

Mchoro 4.8 Mfano wa kiwango cha kawaida cha kiwago cha mpigo wa moyo wa fetasi kama imenakiliwa kwenye patografu kwa vipindi vya dakika 30.

4.8.4 Amnioni kama dalili ya tatizo la fetasi

Dalili nyingine ya tatizo la fetasi ambayo tayari imetajwa ni amnioni iliyo na mekoniamu (rangi ya kijani au amnioni nyeusi). Amnioni iliyo na mekoniamu kidogo sio lazima iwe ni ishara ya shida kwa fetasi, isipokuwa iwe pamoja na uendelevu wa mabadiliko ya kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi usio wa kawaida.

Uchunguzi ufuatao hufanywa wakati wa kila kipimo cha uke na kunakiliwa kwenye patografu, chini baada tu ya pahali kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ulionakiliwa.

Ikiwa membreni ya fetasi haijapasuka, andika herufi 'I' ('iliyo kamilika’).

Iwapo membreni imepasuka na:

 • Hakuna amnioni, andika 'A' (ikiwa 'hakuna')
 • Amnioni ni dhahiri, andika 'C' (ikiwa ni'dhahiri')
 • Amnioni ina damu, nakili 'B'
 • Amnioni ina mekoniumu, rekodi 'M1' ikiwa kidogo, 'M2' ikiwa nene kidogo na 'M3' kwa amnioni nzito sana iliyo kama supu (Kisanduku 4.2).
Jedwali 4.2 Kadiri ya kiasi cha mekoniamu

Mpe mama aliye katika leba rufaa kwa kituo cha afya cha gazi ya juu mapema iwezekanavyo ukiona mambo haya:

 • Amnioni M1 katika kipindi cha kwanza cha leba kwa awamu fiche, hata ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi uko kawaida.
 • Amnioni M2 katika kipindi cha kwanza cha leba kwa awamu iliyo imarika, hata ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ni cha kawaida.
 • Amnioni M3 katika kipindi chochote cha leba, isipokuwa leba ikiendelea haraka.

4.9 Tathmini hali ya afya ya mama

Wakati wa leba na kuzaa, baada ya utathmini wako kamilifu wa mwanzo, afya ya mama hufuatiwa na upimaji wa ishara muhimu za mama: shinikizo la damu, mpigo wa moyo, joto, na kiasi cha mkojo. Shinikizo la damu hupimwa kila baada ya saa 4. Mpigo wa moyo hunakiliwa baada ya kila dakika 30. Joto, hunakiliwa kila baada saa 2. Kiasi cha mkojo hunakiliwa kila wakati mama akikojoa. Ukitambua mwendeleo wa mabadiliko usio kawaida kwa vipimo hivi vyote, mpe mama rufaa kwa kituo cha afya cha gazi ya juu.

Muhtasari wa Kipindi cha 4

Katika Kipindi cha 4, umejifunza mambo haya:

 1. Patografu ni chombo muhimu kinacho kusaidia kugundua mwendeleo wa leba usio wa kawaida, tatizo la fetasi, na ishara za mama kuwa katika matatizo.
 2. Patografu hufuatilia utambulisho wa mama, kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi, rangi ya amnioni, na ufinyanzi wa kichwa cha fetasi. Patografu pia hufuatilia upanuzi wa seviksi, uteremkaji wa fetasi, mikazo ya uterasi, na kama oksitosini au viowevu vya mishipa vilitolewa. Patografu pia hufuatilia ishara muhimu ya mama na kiasi cha mkojo.
 3. Anza kuandika kwenye patografu wakati leba iko katika kipindi cha kwanza, awamu iliyoimarika (upanuzi wa sentimita 4 au zaidi).
 4. Kutathmini maendeleo ya leba, kufuatilia upanuzi wa seviksi, uteremkaji wa kichwa cha fetasi, na mikazo ya uterasi. Katika kipindi cha kwanza awamu iliyoimarika, mwendeleo mzuri ni upanuzi wa seviksi wa sentimita 1 kwa saa na uteremkaji wa kichwa cha fetasi wa sentimita1 kwa saa 4.
 5. Iwapo kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi na mikazo ya uterasi kiko katika kiwango cha kawaida, vitathmini kila baada ya dakika 30 na uviandike kwenye patografu. Kila baada ya saa 4, tathmini upanuzi wa seviksi, uteremkaji wa kichwa cha fetasi, rangi ya amnioni (ikiwa membreni imepasuka), na awamu ya ufinyazi au kaputi.
 6. Kama membreni inapasuka na amnioni inatoka wakati wa kipindi chochote cha leba, pima uke mara moja kwa vidole vilivyo na glavu.
 7. Mpe mama rufaa kwa kituo cha afya au hospitali ishara ya upanuzi wa seviksi ikipita mstari wa Tahadhari kwenye patografu.
 8. Ukitambua ufinyazi wa kichwa cha fetasi wa +3 na maendeleo duni ya leba, leba ina matatizo. Mpe mama rufaa haraka.
 9. Mpe mama rufaa haraka ikiwa kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi kiko chini ya midundo 120 au zaidi ya 160 kwa zaidi ya dakika 10. Mpe mama rufaa ila tu leba ikiendelee haraka.
 10. Hata kukiwa na kiwango cha kawaida cha mpigo wa moyo wa fetasi, toa rufaa ukiona amnioni ya aina hii,ila tu leba ikiendlea haraka:
  • Amnioni ilio na mekoniamu kidogo katika kipindi cha kwanza awamu fishe ya leba
  • Amnioni ilio na mekoniamu nyingi katika kipindi cha kwanza cha awamu ya leba iliyoimarika.
  • Amnioni nzito katika kipindi chochote cha leba

Swali la Kujitathmini la Kipindi cha 4

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, jibu maswali haya kutathmini uliyojifunza. Unaweza kuangalia majibu yako kwenye vidokezo kuhusu Swali la Kujitathmini vilivyo mwishoni mwa Moduli ya huduma ya leba na kuzaa.

Soma Uchunguzi Kifani 4.1 na ujibu maswali.

Uchunguzi maalum 4.1 Kisa cha Bekelech

Bekelech ni mama mwenye gravida5 na para4. Mimba ya sasa imefikia umri wa ujauzito wa wiki 40 na siku 4. Unapofika kwa nyumba yake, unampata akiwa katika leba.Wakati wa utathmini wako wa kwanza, alikuwa na mikazo ya uterusi 4 kila dakika 10, kila moja ikidumu kwa sekunde 35-40. Ulipima uke wake na kichwa cha fetasi kilikuwa katika alama ya -3 na seviksi ilikuwa imepanuka sentimita 5. Mpigo wa moyo wa fetasi ilihesabiwa kuwa midundo 144 kwa dakika.

Maswali ya Kujitathmini 4.1 (Malengo ya Somo la 4.1, 4.2, na 4.3)

 1. Ina maana gani kusema Bekelech ni mama mwenye ‘gravida 5 na para 4’?
 2. Unawezaje kueleza umri wa ujauzito wa mtoto?
 3. Amefika kipindi gani cha leba na kichwa cha mtoto kimeingia kwenye pelvisi?
 4. Mpigo wa moyo wa fetasi kiwango cha kawaida au la?
 5. Ungefanya nini ili kufuatilia mwendeleo wa leba hii?
 6. Ni mara gapi ungepima uke wa Bekelech na kwa nini?
Answer
 1. Kama mama gravida 5, para 4, Bekelech amekuwa na mimba 5 na moja haikuzaliwa ikiwa hai.
 2. Kwa wiki 40 na siku 4, mimba imetimiza muda wa kuzaliwa.
 3. Seviksi ya Bekelech imepanuka sentimita 5 na ana mikazo ya uterusi 4 kila dakika 10 kila moja inadumu sekunde 35-40. Bekelech ameingia katika kipindi cha kwanza cha awamu ya leba iliyoimarika. Katika alama ya -3, Kichwa cha fetasi bado hakijateremka kwa pelvisi.
 4. Mpigo wa moyo wa fetasi uko kwa kiwango cha kawaida kati ya midudo 120-160 kwa dakika.
 5. Leba iko katika awamu iliyoimarika na seviksi imepanuka zaidi ya sentimita 4. Una fuatilia kwa utaratibu mwendeleo wa leba yake mara moja, ishara zake muhimu na viashiria vya tatizo la fetasi. Andika vipimo hivi kwenye patografu (Mchoro 4.1 na Sehemu 4.2.1)
 6. Unaamua kupima uke wake mara nyingi zaidi kuliko saa 4 za kawaida. Leba hii inaweza kuendelea haraka kwa sababu Bekelech ni mama aliye multigravida na multipara. Kuwa mwangalifu kwa ishara za matatizo yoyote, kwa sababu Bekelech tayari alipoteza mtoto mmoja kabla ya kuzaliwa.

Mwisho wa jibu

Maswaliya Kujitathmini 4.2 (Malengo ya Somo la 4.2)

Toa sababu mbili za kutumia patografu

Answer

Tumia patografu kwa sababu hizi mbili muhimu:

 1. Ikitumika kwa usahihi, inaweza kukusaidia kutambua leba ikiendelea kwa kawaida, na ikiwa lazima umpe mama rufaa ya hospitali. Leba ikiendelea vizuri, habari iliyo kwenye patografu inakuonyesha wewe na mama kwamba yeye na mtoto wake wako katika afya nzuri.
 2. Utafiti umeonyesha kwamba matatizo katika fetasi wakati wa leba ya muda mrefu ziko chini wakati mhudumu wa kuzalisha anapotumia patografu kufuatilia mwendeleo wa leba.

Mwisho wa jibu

Maswaliya Kujitathmini 4.3 (Malengo ya Somo la 4.1, 4.3, 4.4 na 4.5)

 1. Ni viashiria vipi vya mwendeleo mzuri wa leba utaonakili kwenye patografu?
 2. Ni viashiria vipi vya afya bora ya fetasi utakaonakili kwenye patografu?
 3. Ni kwa mara ngapi utapima ishara muhimu za mama na kunakili kwenye patografu wakati wa leba inayoendelea vizuri?
 4. Ni viashiria vipi kuu vya kuhitaji rufaa kwa mara moja?
Answer

1. Mwendeleo mzuri wa leba unaonyeshwa na mambo haya:

 • wakati seviksi inapopanuka kwa kiwango sawa au upande wa kushoto wa mstari wa Tahadhari kwenye patografu
 • ushahidi kuwa fetasi anateremka vile seviksi inatanuka
 • mikazo ya uterasi zinazoendelea kuongezeka kwa muda na idadi kila dakika 10

2. Hali ya afya bora kwa fetasi inaonyeshwa na mambo haya:

 • mpigo wa moyo wa fetasi wa kiwango cha midundo kati ya 120-160 kwa dakika (isipokuwa tofauti kidogo inayodumu chini ya dakika 10)
 • ufinyanzi (upishani wa mifupa ya kichwa ya fetasi) usiyo zidi +2
 • amnioni nyeupe au iliyobadilika kidogo (C au M1)

3. Wakati wa leba inayoendelea vizuri, pima vitu hivi vya mama na uviandike kwenye patografu:

 • shinikizo la damu (kila baada ya saa 4)
 • mdundo wa moyo (kila baada ya dakika 30)
 • joto (kila baada ya saa 2
 • mkojo (kila anapokojoa)

4. Toa rufaa mara moja utakapoona moja kati ya vitu hivi:

 • upanuzi wa seviksi wa polepole ( kwa upande wa kulia wa mstari wa Tahadhari kwenye patografu)
 • mwendeleo duni wa leba kukiwa na ufinyanzi wa kichwa cha fetasi wa +3
 • kiwango cha mpigo wa moyo wa fetasi ukiendelea kuwa chini ya midudo 120 au zaidi ya 160 kwa dakika
 • amnioni ilio na mekoniamu, ikitegemea kipindi cha leba, hata ikiwa mpigo wa moyo wa fetasi uko kwa kiwango cha kawaida. Toa rufaa ukiona :
  • Amnioni M1 wakati wa kipindi cha kwanza cha awamu ya leba fishe
  • Amnioni M2 wakati wa mwanzo wa kipindi cha kwanza cha awamu ya leba ilio imarika
  • Amnioni M3 wakati wowote wa leba isipokuwa leba ikiendelea haraka Mwisho wa jibu