Mara tu mtoto anapozaliwa, lazima mkunga amchunguze mtoto huyo mchanga haraka ili kuamua ikiwa anahitaji usaidizi wa kupumua. Ni sharti utambue dalili za jumla za hatari kwa mtoto huyo kwa sekunde chache. Kumshughulikia mtoto kwa haraka huzuia matatizo mabaya au hata kifo iwapo mtoto huyo hapati oksijeni ya kutosha. Watoto wengi hupumua wenyewe mara tu wanapozaliwa. Unahitaji tu kuzifuata hatua za utunzaji wa kimsingi wa mtoto mchanga zilizotolewa katika Kipindi cha 5 cha Somo. Utazisoma kwa kina katika Moduli ya Utunzaji wa baada ya ujauzito. Hatua hizi zimeelezewa tena katika Moduli ya Udhibiti Changani wa Maradhi ya Watoto wachanga na ya Utotoni.
Kipindi hiki cha somo kinaangazia watoto wachanga wasioweza kupumua vizuri. Utajifunza jinsi ya kuwahaisha na kuwasaidia kupumua kikawaida. Pia, utajifunza jinsi ya kutofautisha kati ya mtoto mwenye afya na yule aliye na asifiksia kwa kadiri au kwa kiwango kikubwa. Asifiksia humaanisha kukosa oksijeni kutokana na matatizo katika kupumua. Pia utajifunza kuhusu hatua mwafaka utakazochukua. Kipindi hiki cha somo ni maalum, kwani habari nyingi zinatolewa kwa njia ya michoro (Mchoro).
Baada ya Kipindi hiki cha somo, utaweza:
7.1 Kufafanua na kutumia kwa usahihi maneno yote muhimu yaliyo katika herufi nzito. (Swali la kujitathmini 7.2)
7.2 Kutoa kwa muhtasari dalili za asifiksia ya watoto wachanga zinazoashiria kuwa unapaswa kuanza uhaishaji (uhaisho) wa mtoto mchanga. (Swali la kujitathmini 7.1)
7.3 Kueleza jinsi ya kutumia mbinu za wastani za uhaisho kuwasaidia watoto wachanga kupumua. (Maswali ya kujitathmini 7.1 na 7.2)
7.4 Kutambua vifaa unavyopaswa kuwa navyo ili kumhaisha mtoto mchanga na jinsi ya kuvitumia ifaavyo. (Swali la kujitathmini 7.3)
7.5 Kueleza vitu usivyotakiwa kufanya unapomtathmini mtoto kwa matatizo ya kupumua. (Swali la kujitathmini 7.4)
7.6 Kutoa muhtasari wa hatari kuu za kiafya na huduma muhimu kwa watoto wachanga. (Swali la kujitathmini 7.5)
Sehemu hii inaanza kwa muhtasari wa kile kinachofanyika iwapo ni sharti mtoto apumue kivyake. Ni lazima mtoto mchanga apitie na azoee mabadiliko kutoka kwa maisha ya ndani ya uterasi ya mama hadi ya nje.
Kwa kawaida, mtoto mwenye afya hupumua mwenyewe mara tu baada ya kuzaliwa (Picha 7.1). Iwapo kupumua kulianza kwenyewe na mtoto anapumua bila kusaidiwa, mambo haya ni kweli:
Je, unachunguza vipi hali njema ya mtoto wakati wa leba na kuzaa?
Fetasi yenye afya ina midundo ya moyo kati ya 120 na 160 kwa dakika. Membreni za fetasi zinapopasuka, kiowevu cha amnioni kinachovuja kutoka ukeni mwa mama huyo ni angavu. Kiowevu hakina rangi nyekundu ya damu au rangi ya kijani au nyeusi ya mekoniamu. (Mekoniamu ni kinyesi cha kwanza cha mtoto.)
Mwisho wa jibu.
Umechunguza mdundo wa moyo wa fetasi mara kwa mara katika kipindi chote cha leba. Uliyaandika matokeo kwenye patografu jinsi ulivyojifunza katika Kipindi cha 4 cha somo. Ulimpa mama rufaa iwapo mtoto ambaye hajazaliwa alionyesha dalili za kuathirika. Kwa hivyo, usishughulikie uzazi wa mtoto aliye na asifiksia. Hata hivyo, matatizo katika uzazi yanaweza kutokea bila kutarajiwa au unaweza kuitwa kumhudumia mwanamke aliye katika kipindi cha pili cha leba. Kwa hivyo, ni lazima ujue jinsi ya kumhaisha mtoto mchanga iwapo utashughulikia uzazi wa mtotot aliye na asifiksia.
Jinsi ulivyojifunza katika Kipindi cha 4 cha somo, asifiksia ni uhaba wa oksijeni. Asifiksia kwenye uterasi husababishwa wakati ambapo damu ya mama haina oksijeni ya kutosha. Asifiksia kwenye uterasi pia husababishwa na tatizo kwenye plasenta. Asifiksia kwenye uterasi inaweza kusababisha mambo haya:
Mbadilishano wa gesi hutendeka kwa kila pumzi. Oksijeni kutoka kwa hewa iliyovutwa ndani hufyonzwa ndani ya damu inapopita kwenye mapafu. Dioksidi ya kaboni hutolewa kwenye damu hadi kwenye hewa inayotolewa nje.
Hata hivyo, asifiksia ya mtoto mchanga husababishwa na mambo matatu:
Mtoto asiyeweza kupumua vyema hawezi kuishi kivyake nje ya mwili wa mama yake. Uhashaji wa mtoto mchanga humsaidia aweze kupumua mwenyewe na kupeleka oksijeni kwenye ogani na tishu zake. Ni lazima ubongo upate oksijeni haraka au uharibike. Unaweza kuhitaji kumhaisha mtoto aliye na anemia kali kutokana na kupoteza damu wakati wa leba na kuzaa. Huenda uhitaji kumhaisha mtoto anayeendelea kuwa na sinosisi hata kama anapumua vizuri. Sinosisi ni ugeukaji wa rangi ya midomo na ngozi kuwa samawati. Sinosisi hutokea wakati ambapo damu haina oksijeni ya kutosha (Picha 7.2).
Ili kuepuka matatizo ya mara moja na ya muda mrefu ya asifiksia, lazima umsaidie mtoto yeyote mchanga asiyeweza kupumua vizuri.
Jifunze hizi aina tatu za uhaishaji wa mtoto mchanga.
Upitishaji wa hewa safi: Tumia mfuko wa ambu unaotumika kwa mkono (Picha 7.3). Iweke barakoa kwenye pua na mdomo wa mtoto na usukume hewa kwenye mapafu ya mtoto huyo. (Wakati mwingine wataalamu wa afya hutumia neno “uwekaji mfuko wa ambu” kumaanisha upitishaji wa hewa safi.)
Kabla ya kuanza aina yoyote ya uhaishaji, chunguza mambo haya:
Watoto walio na asifiksia kiasi au kali wanahitaji huduma makini ya uhaishaji. Jifunze jinsi ya kutambua kiwango cha asifiksia kwa mtoto mchanga. Tathmini kama mtoto yuko hai au amefariki katika sekunde 5 baada ya kuzaliwa. Iwapo yuko hai, kadiri kiwango cha asifiksia. Huenda mtoto aliye na asifiksia kali asipumue kabisa. Hasongezi mikono wala miguu yake. Rangi ya ngozi yake ni samawati sana au nyeupe sana. Mtoto asiyeweza kupumua au anayetweta ili kupata hewa anahitaji huduma ya dharura. Mtoto anayepumua chini ya pumzi 30 kwa dakika pia anahitaji huduma ya dharura. Mtoto asipopumua punde tu baada ya kuzaliwa, ubongo wake unaweza kuharibika au kufariki. Ukiwahaisha watoto vizuri na kwa haraka, wengi wao wanaweza kuongoka.
Jedwali 7.1 linaorodhesha mambo utakayochunguza ili kutathmini kiwango cha asifiksia kwa mtoto mchanga. Pia, tazama picha za watoto wachanga walio na viwango tofauti vya asifiksia (Picha 7.1, 7.2 na 7.5).
Mtoto mchanga anayetweta anaweza tu kuvuta pumzi chache na kwa ugumu. Mitweto mikubwa kati ya kila pumzi pia ni tatizo. Mtoto mchanga anayetweta, kwa kawaida huwa karibu kufariki.
Dalili | Hakuna asifiksia | Asifiksia ndogo | Asifiksia kiasi | Asifiksia kali |
---|---|---|---|---|
Mpigo wa moyo | Zaidi ya mipigo 100 kwa dakika | Zaidi ya mipigo 100 kwa dakika | Zaidi ya mipigo 60 kwa dakika | Chini ya mipigo 60 kwa dakika |
Rangi ya ngozi | Waridi | Buluu kidogo | Buluu wastani | Buluu sana |
Mkondo wa kupumua | Kulia | Kulia | Kupumua lakini sio sana | Kutopumua wala kutweta |
Kusonga kwa miguu na mikono | Inasonga vizuri | Kusonga kidhaifu | Kutosonga | Kutosonga |
Kuchafuliwa na mekoniamu | La | La | Labda | Kawaida |
Uhaishaji | Hakuna haja | Mwitiko wa haraka | Mwitiko mzuri | Anachukua muda mrefu kuitika |
Tathmini kiwango cha asifiksia chini ya sekunde 5. Fanya hivyo haraka lakini usiwe na hofu.
Lazima utoe huduma ya kumhaisha mtoto katika muda wa dakika moja baada ya kuzaliwa. Kwa hivyo, ni rahisi kukadiria mpigo wa moyo kuliko kuhesabu. Ni rahisi na haraka kutazama mkondo wa pumzi zake kuliko kuhesabu kiwango cha pumzi. Jedwali 7.2 linaorodhesha dalili zinazoonyesha kilicho na kisicho cha kawaida baada ya kuzaliwa.
Ishara | Ugunduzi wa kawaida | Ugunduzi usio wa kawaida |
---|---|---|
Rangi | Yafaa kuwa waridi | Buluu au yenye sinosisi (ukosefu wa oksijeni ya kutosha) Nyeupe, (weupe) anemia Umanjano |
Pumzi | Pumzi 40-60 kwa dakika | Hakuna pumzi Kiwango cha kupumua ni chini ya 30 kwa dakika Mitweto (pumzi chache mno na zenye ugumu) |
Kiwango cha mpigo wa moyo | Mipigo 120-160 kwa dakika | Hakuna mpigo wa moyo Mpigo wa moyo ni chini ya 100 kwa dakika |
Siha ya misuli | Mikono na miguu ya mtoto aliyezaliwa baada ya kutimiza umri kamili wa ujauzito imeyojikunja kidogo | Kujikunja duni kwa miguu na mikono, dhaifu (Picha 7.2), inayoashiria asifiksia kali inayoathiri ubongo |
Matendohiari | Mtoto huhisi na kuitika kidole kinapowekwa kwenye kaakaa la kinywa chake | Mtoto hahisi wala kuitika unapoligusa kaakaa la kinywa chake. |
“Chini ya” inaweza kubadilishwa na alama <, kwa mfano < 30 kwa dakika. “Zaidi ya” inaweza kubadilishwa na alama >, kwa mfano > 30 kwa dakika.
Kabla ya kwenda kuzalisha, hakikisha una vifaa utakavyohitaji katika kuhaisha na kumpa mtoto mchanga huduma ya haraka. Sehemu hii inaeleza hatua utakazochukua baada ya kutathmini kiwango cha asifiksia.
Jedwali 7.3 linatoa muhtasari wa mambo utakayofanya ukiona dalili za asifiksia katika sekunde 5 za kwanza baada ya mtoto kuzaliwa. Habari zaidi zimetolewa baada ya maelezo haya ya jumla.
Mtoto mchanga anafanya nini | Tathmini | Kitendo |
---|---|---|
Analia na kusongesha miguu na mikono | Labda mtoto ni mwenye afya | Uhaishaji hauhitajiki |
Anapumua kidhaifu, hasongeshi mikono wala miguu, ana sinosisi kiasi | Labda ana asifiksia kiasi | Pitisha hewa safi ukisita Kadiria kiwango cha mpigo wa moyo |
Halii, hapumui, hatweti wala kusongesha mikono na miguu. Mikono na miguu ni dhaifu. Ana sinosisi au mwili wake una mekoniamu | Labda asifiksia kali | Ita msaidizi (jamaa au mtu mwingine). Tumia sirinji ya balbu. Fyonza kwenye kinywa, pua na maeneo ya koromeo chini ya sekunde 5. Pitisha hewa ukisita |
Halii, hapumui, hatweti wala kusongesha mikono na miguu. Mikono na miguu ni dhaifu. Ana sinosisi au mwili wake una mekoniamu | Kiwango cha mpigo moyo ni zaidi ya 60 kwa dakika | |
Halii, hapumui, hatweti wala kusongesha mikono na miguu. Mikono na miguu ni dhaifu. Ana sinosisi au mwili wake una mekoniamu | Kiwango cha mpigo moyo ni chini ya 60 kwa dakika | Tekeleza vitendo vyote vilivyo kwenye jedwali hili na pia uusinge moyo (Picha 7.4). |
Mpigo wa moyo wa apeksi ni jina la mpigo wa moyo unaosikika kwa moyo kwenye upande wa kushoto wa kifua kwa kutumia stethoskopu (Picha 7.6). Unaitwa “wa apeksi” kwa sababu utausikia moja kwa moja kutoka juu ya moyo.
Je, idadi ya mipigo ya moyo kwa kila dakika inayopimiwa kwenye sehemu zingine mbali na moyo huitwaje?
Huitawa mpwito wa ateri.
Mwisho wa jibu
Njia nyingine ya kuhesabu mipigo ya moyo wa mtoto mchanga ni kuhisi mpwito mwanzoni mwa kiungamwana (Mchoro 7.6).
Fanya shughuli hizi kwa watoto wote wachanga bila kuzingatia kiwango cha asifiksia:
Chunguza kila picha kwa makini. Soma muhtasari na maelezo yazo.
Mlalishe mtoto mahali penye joto mbali na vitu. Tumia taa yenye joto au vifaa vingine vya kupasha joto juu ya kichwa ikiwa vipo. Kisha, mpashe mtoto joto (Mchoro 7.8).
Mweke mtoto karibu sana na mama kiasi kwamba ngozi zao zinagusana kisha uwafunike na blanketi lenye joto. Funika kichwa cha mtoto na kofia au shali yenye joto.
Ikiwa sirinji aina ya balbu ipo:
Fyonza kwenye kinywa kwanza, kisha pua (Mchoro 7.9).
Usifyonze kwa kina kwa sirinji aina ya balbu! Ufyonzaji wa kina unaweza kupunguza kiwango cha mpigo wa moyo (bradikadia).
Ondoa vinyeso kwenye kinywa na pua kwa kitambaa safi kikavu.
Usimchochee kwa vitendo hivi.
Aina hizi za kuchochea ni hatari na zinaweza kumjeruhi mtoto huyu mchanga.
Mlalishe chali mtoto huyu mchanga huku shingo lake likiwa limenyooshwa kidogo jinsi ilivyoonyeshwa kwenye picha ya kwanza katika mchoro 7.11. Fyonza kinywa na pua kwa sirinji aina ya balbu. Kufyonza hufungua njia ya hewa (Picha 7.9).
Ikiwa mpigo wa moyo wa apeksi ni zaidi ya mipigo 60 kwa dakika:
Ikiwa mpigo wa moyo wa apeksi ni chini ya mipigo 60 kwa dakika:
Hesabu kwa sauti: “pumzi-mbili-tatu” huku ukipitisha hewa safi (Mchoro 7.14). Finya mfuko huku ukisema “pumzi” na uachilie shinikizo kwa mfuko huku ukisema “mbili-tatu”. Hesabu hii hukusaidia kupitisha hewa safi ukitumia wizani kwa kiwango kinachofaa kwa mapafu ya watoto wachanga.
Kiasi cha hewa unayoingiza na kutoa ndani ya mapafu ni sawa na takriban pumzi 40 kwa dakika. Tumia shinikizo la kutosha ili kutimiza mwinuko na mshuko mpole kwa kifua cha mtoto. Pumzi chache za kwanza zinaweza kuhitaji shinikizo la juu. Shinikizo litakuwa jingi sana iwapo mtoto ataonekana kupua kwa nguvu sana.
Dalili bora ya upitishaji mzuri wa hewa na ubora wa hali ya mtoto ni ongezeko katika kiwango cha mpigo wa moyo hadi mipigo 100 kwa dakika.
Je, ni mabadiliko yapi mengine utakayotarajia kuona kwa mtoto unapompa hewa ikiwa uhaishaji unaendelea vizuri?
Utatarajia kuona ngozi ya mtoto ikibadilika kutoka rangi ya samawati au buluu hafifu sana hadi rangi bora ya waridi. Mtoto anaanza kusonga kidogo, anaanza kukunja mikono na miguu yake na haonekani mdhaifu sana.
Mwisho wa jibu
Je, unapoacha kumpa hewa safi kwa muda, mtoto huyo anaweza kupumua au kulia bila kusaidiwa? Dalili hizi ni nzuri. Watoto wengi hupata nafuu haraka sana baada ya muda mfupi wa kupewa hewa safi. Hata hivyo, endelea kumchunguza mtoto hadi utakapohakikisha kuwa anapumua vizuri mwenyewe.
Ikiwa mtoto anabaki mdhaifu au anapumua kwa kusita baada ya dakika 30 za kupewa hewa safi, mpe mama na mtoto rufaa haraka. Wape rufaa waende katika kituo cha afya au hospitali ambapo watoto wasiopumua vizuri husaidiwa. Enda nao na umpe mtoto hewa safi safarini hadi mtakapofika. Hakikisha mtoto ana joto wakati wote. Watoto wachanga hupoteza joto kwa urahisi. Mtoto asiyepumua vizuri mwenyewe anaweza kupata baridi nyingi na afariki. Mchoro 7.15 Inatoa muhtasari wa hatua katika uhaishaji wa mtoto mchanga ulizosoma katika sehemu ya 7.4.
Sehemu ya mwisho ya Kipindi hiki cha somo inakukumbusha kuhusu utunzaji muhimu wa mtoto mchanga. Toa utunzaji huu kwa watoto wote pasipo kujali iwapo wana dalili za asifiksia. Kiungamwana kinapokatwa, mabadiliko mengi ya kifisiolojia mwilini mwa mtoto humsaidia kuzoea maisha ya nje ya mwili wa mama yake. Ni vigumu sana kumudu nje kuliko ndani ya uterasi ambapo ni salama. Toa utunzaji wa kimsingi kwa mtoto mchanga ili kumsaidia kujikinga dhidi ya hatari za kiafya zilizoorodheshwa katika Kisanduku 7.1.
Watoto wachanga huhitaji utunzaji ili kuzuia matatizo haya:
Magonjwa yanayozuilika kwa chanjo yamejadiliwa kwa kina katika Moduli ya Magonjwa ya kuambukiza, Vikao vya 3 na 4 vya Somo.
Uzuiaji wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto umeelezewa katika Moduli ya Utunzaji katika ujauzito, Kipindi cha 17 cha Somo. Dawa na utaratibu wa uzuiaji wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto umeelezewa katika Moduli ya Magonjwa ya kuambukiza, Kipindi cha 27 cha Somo.
Kwa kuzingatia hatari za kiafya zilizo kwenye Kisanduku 7.1, wape watoto wote utunzaji huu muhimu:
Ratiba ya uchanjaji ya chanjo zote zilizo kwenye Moduli ya Uchanjaji.
Utajifunza yote kuhusu unyonyeshaji katika Moduli yaUtunzaji baada ya kuzaa. Unyonyeshaji na VVU vimeelezewa katika Moduli ya Magonjwa ya kuambukiza, Kipindi cha 27 cha Somo.
Katika Kipindi cha 7, umejifunza mambo haya:
Kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, jibu maswali haya ili utathmini kujifunza kwako. Linganisha majibu yako na Muhtasari juu ya Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.
Kwanza soma Uchunguzi Kifani 7.1 kisha ujibu maswali yanayofuata.
Atsede, mwanamke wa umri wa miaka 25, aliletwa katika Kituo chako cha Afya. Alikuwa katika leba nyumbani kwake kwa muda wa saa 38. Muda tu baada ya kufika kwako, akazaa mtoto mvulana aliyetimiza umri kamili wa ujauzito. Ulimtathmini na kugundua haya: hakujaribu kupumua, hakusongesha miguu wala mikono yake, mwili wake wote ulikuwa umefunikwa na mekoniamu yenye kiowevu cha amnioni, bado hakujaribu kupumua ulipompanguza na kumpa mguso wa kumsisimua.
Mwisho wa jibu
Orodhesha vifaa vya kimsingi unavyopaswa kuwa navyo ili kumhaisha mtoto mchanga asiyeweza kupumua.
Unahitaji vifaa hivi vya kimsingi kwa kumhaisha mtoto mchanga asiyeweza kupumua:
Mwisho wa jibu
Je,ni kauli ipi isiyo sahihi? Eleza kisicho sahihi kwa kila kauli.
A si sahihi. Mtoto mchanga akilia mara tu baada ya kuzaliwa huwa ishara kuwa asifiksia haijatokea au haikutokea kabla ya kuzaliwa.
B si sahihi. Sinosisi inamaanisha kuwa ngozi ina rangi ya samawati kutokana na upungufu wa oksijeni (asifiksia).
C ni sahihi. Mpigo wa moyo wa apeksi unaweza kugunduliwa kwa kusikiliza kifua cha mtoto kwa stethoskopu.
D si sahihi. Mbadilishano wa gesi mapafuni hutendeka dioksidi ya kaboni inapotolewa nje huku oksijeni ikiingizwa.
E si sahihi. Sindano ya vitamini K kwa watoto wachanga ni ya kuzuia kutokwa na damu. Lihamu ya tetrasiklini inayopakwa machoni huzuia maambukizi ya macho.
F ni sahihi. Kiwango kilichopendekezwa cha kuwapa watoto hewa safi ni pumzi 40 kwa dakika.
Mwisho wa jibu
Je, njia zilizopendekezwa za kumsisimua mtoto mchanga ni zipi? Je, ni njia zipi zilizo hatari na zisizoruhusiwa?
Ni njia mbili tu zilizopendekezwa kumsisimua mtoto kwa upole:
Hizo njia zingine zote ni hatari. Usizitumie.
Mwisho wa jibu
Kisanduku7.1 ni muhtasari wa baadhi ya hatari za kiafya zinazotokea sana kwa watoto wachanga na utunzaji muhimu wa mara moja kwa uzuiaji wa matatizo hayo. Baadhi ya majedwali yameachwa na mapengo ili uyakamilishe.
Hatari ya kiafya kwa mtoto mchanga | Utunzaji muhimu wa mara moja kwa Mtoto mchanga |
---|---|
Maambukizi ya macho | |
Damu kutoka yenyewe | |
Hipothemia | |
Hipoglisimia |
Kisanduku 7.1 lililokamilishwa ndilo hili.
Hatari ya kiafya kwa mtoto mchanga | Utunzaji muhimu wa mara moja kwa Mtoto mchanga |
---|---|
Maambukizi ya macho | Weka lihamu ya tetrasiklini |
Damu kutoka yenyewe | Dunga sindano ya miligramu 1 ya vitamini K kwenye msuli |
Hipothemia | Mgusano wa ngozi kwa ngozi na mama, blanketi, na kofia |
Hipoglisimia | Unyonyeshaji wa mapema au chakula mbadala cha kutosha |
Mwisho wa jibu