Kichwa:● Kichwa cha fetasi kikubwa (kikubwa kwa hicho fetasi)● Hidrosefalasi (kukusanyika kwa maji ndani ya kichwa, inayosababisha uvimbe wa fuvu)Kitangulizi na mkao:● Paji la uso, uso, bega ● Uendelefu wa kukaa vibaya kwa fetasiMimba ya mapacha:● Mapacha waliofungiana (kufungiana kwa shingo)● Mapacha walioshikana (walioshikana na kutumia baadhi ya viungo pamoja) | Mifupa ya pelvisi:● Upungufu (kwa sababu ya utapia mlo)● Iliyoumbuka (kwa sababu ya jeraha au polio)Tishu nyororo:● Uvimbe kwenye pelvisi● Maambukizi ya virusi kwenye uterasi au fumbatio● Kovu (kutokana na ukeketaji) |