Skip to main content
Printable page generated Thursday, 28 March 2024, 9:23 PM
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Thursday, 28 March 2024, 9:23 PM

3. Puperiamu isiyo ya Kawaida

Kipindi cha 3 Puperiamu isiyo ya Kawaida

Utangulizi

Kama ulivyojifunza katika Kipindi cha 2, puperiamu huendelea vizuri kwa wanawake wengi. Puperiamu ni muda wa angalau wiki 6 baada ya kuzaa, ambapo mawazo hurejea kwa hali ya isiyo ya ujauzito. Hata hivyo, wakati mwingine wanawake hupata matatizo ya kiafya ambazo unapaswa kuyatilia maanani. Unaweza kushughulikia baadhi ya matatizo haya mwenyewe, lakini unaweza kurufaa mengine hospitalini au kwa kituo cha afya kwa utathmini zaidi na matibabu. Maambukizi ni miongoni mwa matatizo maarufu ya puperiamu na kisababishi kikuu cha vifo vya wajawazito Kusini mwa Jangwa la Afrika. Joto jingi mwilini ni dalili kuu na antibiotiki ni tiba kuu. Hatua bora zaidi ya kuzuia maambukizi ni kudumisha usafi na elimusiha wakati wa kuzaa.

Neno ‘postpartum’ linamaanisha ‘baada ya kuzaa na mahusiko yake’.

Matatizo mengine ya kawaida ni kuchelewa kuvuja damu baada ya kuzaa, maambukizi kwa mfumo wa mkojo, shinikizo la juu la damu, na matatizo ya akilini. Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu matatizo yasiyo ya kawaida ambayo yanaweza kutokea wakati wa puperiamu, na mojawapo ya tatizo lisilo la kawaida linalotisha maisha – mvilio ndani ya mshipa wa damu (damu kuganda ndani ya mishipa ambayo huzuia mtiririko wa damu).

Malengo ya Somo la Kipindi cha 3

Baada ya kipindi hiki, utaweza:

3.1 Kufafanua na kutumia kwa usahihi maneno yote muhimu yaliyochapishwa kwa herufi nzito. (Swali la Kujitathmini 3.1)

3.2 Kuelezea visababishi vya kuvuja damu iliyochelewa baada ya kuzaa. (Swali la Kujitathmini 3.1)

3.3 Kujadili aina za kawaida za maambukizi ya puperiamu na hatari zake. (Swali la Kujitathmini 3.2)

3.4 Kutambua dalili hatari za mvilio ndani ya mshipa wa damu. (Swali la Kujitathmini 3.3)

3.5 Kufafanua nakala ya kliniki ya puperiamu isiyo ya kawaida, ikiwa ni pamoja na matatizo akilini baada ya kuzaa. (Swali la Kujitathmini 3.1 na 3.4)

3.1 Kuvuja damu baada ya kuzaa

Vipindi vya 3 na 11 vya somo la Moduli ya Utunzaji wa Leba na Kuzaa vilielezea kwamba kutokwa na damu baada ya kuzaa inayohatarisha maisha hutokana na upotezaji wa angalau mililita 500 ya damu kutoka uterasi au ukeni. Kipindi hatari cha kupata uvujaji wa damu baada ya kuzaa ni katika vipindi vya tatu na nne vya leba.

  • Je, vipindi vya tatu na nne vya leba ni nini?

  • Kipindi cha tatu ni utoaji wa plasenta na tando za fetasi; kipindi cha nne ni masaa manne yanayofuatilia.

    Mwisho wa jibu

Mchoro 3.1 Uterasi inapaswa kujikaza vyema masaa 4-6 baada ya kuzaa.

Karibu vifo 90% inayosababishwa na utokaji wa damu hutokea kati ya masaa manne baada ya kuzaa. Katika masaa manne hadi sita ya kwanza, hakikisha kwamba uterasi imekazwa vyema (Mchoro 3.1) na hakuna upotezaji wa damu nyingi. Hata hivyo, mwanamke anaweza kutokwa na damu wakati wowote wa puperiamu, kwa kijumla katika wiki ya kwanza, lakini hata hadi wiki sita baada ya kuzaa. Aina hii ya kuvuja damu inajulikana kama hatua ya mwisho ya kutokwa na damu iliyochelewa baada ya kuzaa.

Kuwepo kwa anemia au hali ya moyo inaweza kuhatarisha maisha ya mama hata kama upungufu wa damu ni chini ya mililita 500. Kwa kawaida mwanamke ambaye ana utapiamlo hana uwezo wa kukabiliana na upotezaji wa damu kuliko mwanamke ambaye analishe bora.

3.1.1 Visababishi vya kuvuja damu iliyochelewa baada ya kuzaa

Kwa kawaida kutokwa na damu husababishwa na mikazo duni ya uterasi baada ya kuzaa, ambayo hushindwa kufunga kapilari iliyoraruka mahali ambapo plasenta ilivutwa nje. Iwapo uterasi haipungui kwa unene wake wa kawaida, inaweza kuwa ni kwa sababu ya maambukizi, au uzuiaji wa kipande cha plasenta, ambayo baadaye huraruka na kuwachana na kuta ya uterasi na kusababisha uvujaji damu. Kisanduku 3.1 linaeleza kwa muhtasari sababu za kawaida za kutokwa na damu uliochelewa baada ya kuzaa.

Ikiwa kawaida kuna uvujaji wa damu nyingi ukeni, au unashuku kuwa kuna uvujaji wa damu nyingi ndani ya mwili, rufaa mama hospitalini au kwa kituo cha afya iliyoko karibu yenye huduma ya kuongeza damu mwilini.

Kisanduku 3.1 Visababishi vya kutokwa na damu iliyochelewa baada ya kuzaa
  • Maambukizi ya ukuta wa endometria: Endometritisi imeelezwa katika Sehemu ya 3.2.1. Wakati eneo la plasenta bado halijapona, maambukizi katika uterasi inaweza kusababisha kapilari katika eneo la plasenta zianze kutokwa na damu tena.
  • Uterasi yenye mikazo duni: Uterasi inaweza kukosa mikazo yanayotarajiwa kwa sababu ya maambukizi, vipande vya plasenta vilivyobaki, au kwa sababu isiyojulikana. Kama hivyo, uvujaji damu unaweza kuanza tena.
  • Plasenta iliyobaki: Mabaki ya tishu ya plasenta au tando za fetasi yaliyobaki katika uterasi ndizo visababishi vya kawaida vya kutokwa kwa damu iliyochelewa baada ya kuzaa.
  • Kutengana kwa sehemu ya plasenta: Kuna uwezekano kwamba sehemu ya plasenta iliyopona hutengana na kufungua kapilari ya damu tena.
  • Ujauzito isiyo kuwa ya kawaida: Ingawa sio kawaida kwa mwanamke kupata ujauzito isiyo kuwa ya kawaida, matokeo yake inaweza kuwa na matatizo ya kutisha maisha; kumea kasi kwa kwa tishu kama zabibu katika uterasi inaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi.

3.1.2 Rufaa kabla ya kudhibiti uvujaji damu baada ya kuzaa

Kumbuka kwamba kiasi chochote cha damu kinachotoka ukeni baada ya masaa 24 (ya wakati huo au nyekundu sana) inaweza kuwa imesababishwa na mojawapo ya yale yalioorodheshwa katika Kisanduku 3.1, au zingine zisizotajwa. Hivyo basi, unapaswa kurufaa wanawake wanaovuja damu hospitalini bila kujali kiasi cha damu kinachotoka. Kumbuka pia kuongezwa damu pekee ndiyo njia inayoweza kuokoa maisha ya mama, Ikiwa anavuja damu sana.

Udhibiti ulioelezwa kwa kina zaidi kuhusu kutokwa na damu baada ya kuzaa ulifunzwa katika Kipindi cha 11 cha Moduli ya Utunzaji wa Leba na kuzaa na kimeelezwa katika Kipindi cha 22 cha Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito, kama vile katika tajriba yako.

  • Je, vipindi hivi vya masomo vimekufunza nini kabla ya kurufaa wanawake wanaovuja damu baada ya kuzaa?

  • Mchoro 3.2 Mdungiye 10 IU ya oxytocin (au umpatie mikrogramu 400 za misoprostol) kabla kurufaa mwanamke anayevuja damu baada ya kuzaa.

    Weka laini dawa ya kudungia mshipa, na umwanzishe na tiba ya kumwingiza dawa ndani ya mshipa kwa kutumia Ringer’s Lactate au Saline ya kawaida, ukitumia ml 1,000 (lita-1) ya mfuko na kiwango cha mtiririko kilichowekwa kitiririke haraka iwezekanavyo.

    Mwisho wa jibu

Kama tiba ya kabla rufaa, pia mpe dozi ya pili ya misoprostol (mikrogramu 400 mdomoni au kupitia rektamu), au 10 IU oxytocin kwa sindano ya ndani ya misuli (Mchoro 3.2).

3.2 Sepsisi inayosababishwa na uzazi na joto jingi mwilini

Sepsisi inayosababishwa na uzazi inahusu maambukizi yoyote ya bakteria ambayo huenea katika mfumo wa uzazi wa mwanamke baada ya kuzaa. Baadhi ya wanawake wako hatarini zaidi dhidi ya sepsisi inayosababishwa na uzazi, kwa mfano wanawake ambao wana anemia na/au wana utapiamlo. Joto jingi (joto lililo juu mwilini) kwa mama wakati wa kipindi cha baada ya kuzaa ni dalili hatari ya kijumla. Anahisi baridi kwa ghafla na kutetemeka, kufuatia kuhisi joto na kutokwa na jasho. Joto jingi mwilini baada ya kuzaa inaweza kuwa imesababishwa na sepsisi inayosababishwa na uzazi, lakini pia inaweza kusababishwa na:

Maambukizi haya yote yaliyoelezwa katika Moduli ya Magonjwa ya Kuambukizana.

  • Maambukizi kwa mfumo wa mkojo
  • Maambukizi kwa jeraha
  • Mastitisi au jipu kwa matiti
  • Maambukizi zisizohusiana na mimba au kuzaa, kama vile VVU, malaria, homa ya matumbo, pepopunda, meninjitisi, nimonia, na kadhalika

Katika hali nyingi, ili kuzuia maambukizi kwa mama baada ya kuzaa tekeleza uzalishaji kwa njia safi na iliyo salama, kuchanja wajawazito dhidi ya pepopunda, na kutoa matibabu kabla ya maambukizi. Katika maeneo ya endemiki ya malaria, usisahau kutoa vyandarua vilivyotibiwa na dawa ya kudumu ya kuua wadudu (Vyandarua vilivyotibiwa kukinga wadudu, Picha 3.3) wakati wa ziara yako ya nyumbani, ikiwa hawakupewa hapo awali. Pia washauri kina mama jinsi ya kuzitumia mara kwa mara kila wakati. Hakikisha kwamba mama na mtoto wake wanalala chini ya chandarua kila wakati.

Picha 3.3 Mama huyu amepewa chandarua kilichotibiwa watumie na mtoto wake wanapolala. (Picha: Hazina ya Dharura ya Watoto ya Umoja wa Mataifa)

3.2.1 Endometritisi

Endometritisi ni mchakato wa maambukizi inayoshirikisha ukuta wa ndani ya uterasi (endometria). Kwa kawaida inasababishwa na bakteria kupanda juu kutoka ukeni, au bakteria iliyohamishwa kutoka kwa rektamu na mkundu hadi mfumo wa uzazi. Sababu zinazojulikana na zinazoweza kuzuiwa zinazochangia hatari ya endometrisi ni pamoja na:

Kupasuka kwa Tando Kabla ya Wakati ni mada ya Kipindi cha 17 cha Moduli ya Utunzaji katika ujauzito.

  • Leba ya muda mrefu: Hatari hii inaweza kudhibitiwa kwa kurufaa wanawake walio katika leba iliyochukuwa muda mrefu.
  • Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati na iliyochukuwa muda mrefu: Hatari ni kubwa iwapo Kupasuka kwa Tando kabla ya imetokea muda mrefu Kabla mtoto hajazaliwa. Unaweza kupunguza hatari kwa kurufaa haraka.
  • Uchunguzi wa mara kwa mara wa ukeni: Unaweza kuepukana na hatari hii kwa kukosa kutekeleza uchunguzi wa ndani isiyohitajika.
  • Hali duni ya elimusiha na usafi wakati wa kuzalisha: Kwa mfano, kuingiza mkono mchafu ukeni, au kutumia vyombo vilivyo na vimelea, vinaweza kusambaza maambukizi.
  • Maambukizi yaliokuwa: Maambukizi ukeni na uterasi kutokana na magonjwa ya zinaa au kwa mfumo wa mkojo.
  • Mabaki ya plasenta au tando za fetasi: Seli zilizokufa katika tishu hizi huchangia kuongezeka kwa bakteria.
  • Kutoa plasenta kwa kutumia mikono: Kambakitovi ikikatika ukivuta polepole ili kusaidia kutoa plasenta, inaweza kubakia na mwanamke huweza kuvuja damu nyingi. Katika hali hizi, utalazimika kutoa kwa kuingiza vidole ndani ya pengo la endometria, kutambua plasenta, na kuitoa vipande vipande au mzima. zaidi ya hatari kwa mama kutokana na kuvuja damu, kuna hatari pia za maambukizi za endomeria.
Mchoro 3.4 Maumivu kwa fumbatio yanaweza kuwa dalili ya endometritisi.
  • Anemia: Hatari inayojulikana ya endometiritisi na aina zingine za maambukizi ya pupera, anemia inaweza kusababishwa na upungufu wa damu wakati wa ujauzito, leba, au kuzaa, au kwa matatizo ya lishe.
  • Jeraha la kuzalisha: (kwa mfano, kwa kutumia koleo, au kwa operesheni ya kisu)
  • Kutokwa na damu iliyochelewa baada ya kuzaa.

Magonjwa ya zinaa yameelezwa katika Kipindi cha 31 katika Moduli ya Magonjwa Ambukizi; Maambukizi kwa mfumo wa mkojo yamejadiliwa katika Kipindi cha 18 cha Moduli ya Utunzaji katika ujauzito

Dalili za endomentritisi

Mwanamke aliye na endometritisi kwa kawaida huwa na homa ya Sentigredi 38° au zaidi, mpigo wa kasi wa mshipa, na maumivu (maumivu unapoguswa) unapogusa fumbatio (Mchoro 3.4). Baadhi ya wanawake wanaweza kupata mchozo iliyoganda inayoonekana kama maziwa ya rangi ya manjano iliyo na harufu mbaya kutoka ukeni, ambapo wengine huwa na mchozo kiasi kisichokuwa na harufu. Kwa ufupi, kumkagua mama kwa maambukizi ya uterasi, muulize kama ana:

  • Historia ya joto jingi mwilini au iwapo anahisi joto. Mpime joto lake na ikiwa ni sawa au zaidi ya Sentigredi 38, basi ana joto jingi mwilini.
  • Maumivu katika sehemu ya chini ya fumbatio.
  • Harufu mbaya, mchozo unaoonekana kama maziwa yalio ganda kutoka ukeni.

Iwapo mama ana mojawapo ya matokeo yaliyotajwa hapo awali, uchukulie kwamba ana endometritisi na umpatie rufaa ya haraka hospitalini au kwa kituo cha afya kilichokaribu.

Iwapo utashuku mama wakati wa puperiamu kuwa ana endometritisi unapofanya ziara yako, ni muhimu kumrufaa haraka kwa matibabu zaidi. Ikiwa ana shinikizo la chini la damu (diastoli chini ya mililita 60 ya zebaki), unaweza kuanza uamishaji wa Saline ya kawaidakwa mishipa. Mweke alale chali miguu yake yakiwa yameinuka kwa kuweka mito chini ya magoti yake (mtindo wa mstuko), kabla ya kumpeleka kwa kituo cha afya.

  • Ni hatari zipi za ukuaji wa endometritisi, unaweza kutekeleza, wewe binafsi?

  • Kuhakikisha viwango vya juu vya elimusiha na usafi wakati wa kuzaa; na kujiepusha, iwezekanavyo, na urudiaji wa uchunguzi ukeni mwa mama.

    Mwisho wa jibu

3.2.2 Maambukizi kwa mfumo wa mkojo

Sababu nyingine ya kawaida ya maumivu na joto jingi mwilini wakati wa puperiamu ni maambukizi ya mfumo wa mkojo. Mwanamke mwenye Maambukizi ya Mfumo wa Mkojo hulalamika mkojo hutoka kila mara, anahisi akichomeka anapokojoa, na hamu ya kukojoa mara kwa mara. Unapofinya fumbatio lake juu ya pelvisi, anahisi uchungu. Mwanamke huyu anahitaji rufaa ili atibiwe na antibiotiki.

Maambukizi ya Mfumo wa Mkojo ni kawaida wakati wa ujauzito na puperiamu kwa sababu ya:

  • Kufungwa kwa mkojo kwa ajili ya kizuizi kwa mfumo wa mkojo katika baadhi ya wajawazito wakati wa kipindi cha mwisho cha ujauzito.
  • Msongamano wa mifupa na jeraha kwa urethra wakati wa leba na wa kuzaa, ambayo huongeza hatari ya bakteria kutoka kwa mfumo wa kuzalisha na rektamu kwenda juu na kuingia ndani ya kibofu na kutoka hapo hadi kwa figo.

3.2.3 Mastitisi ya pupera

Mchoro 3.5 Uchungu wa matiti inaweza kuwa dalili ya mastitisi.

Mastitisi ni inflamesheni yenye uchungu wa matiti kutokana na maambukizi ya bakteria (Mchoro 3.5). Bakteria ambayo mara nyingi husababisha mastitisi, au jipu iliokali zaidi, huitwa Staphylococcus aureus. Chanzo kikuu cha bakteria hizi ni mtoto ambaye ananyonya. Mastitisi huweza kuwa wakati wa kunyonyesha kuliko wakati matiti hayatoi maziwa. Mara nyingi hutokea wakati maziwa hubaki kwa matiti kwa muda mrefu (kutokamua yote) kwa sababu mtoto hanyonyi vizuri, au kutoka kwa mipasuko ya chuchu.

  • Je, chuchu iliyopasuka inawezaje kuwa hatari kwa mastitisi?

  • Maumivu kutokana na chuchu iliyopasuka inaweza kumfanya mama asitishe unyonyeshaji, hivyo maziwa mengi hubaki kwa matiti yake. Zaidi ya hayo, bakteria kutoka kwa mdomo wa mtoto au kutoka kwa ngozi ya mama zinaweza kuingia ndani ya matiti kupitia mipasuko ya chuchu.

    Mwisho wa jibu

Maambukizi ya matiti yasiyotunzwa, yenye upinzani, au yaliyorejea huweza kusababisha ukuaji wa jipu, mkusanyiko wa usaha ndani ya matiti. Usaha ni kiowevu kilichoshikana cha rangi ya manjano-nyeupe katika tishu iliyoambukizwa na ina bakteria, seli nyeupe za damu, mabaki yaliyoundwa na seli, na tishu zinazokufa. Wanawake walio na mastitisi mara kwa mara hupata maumivu, joto jingi mwilini, kuhisi baridi, na maumivu ya misuli mwili mzima. Titi huonekana nyekundu, lenye joto, na lina uchungu mno likiguswa. Wakati uchunguzi unaonyesha mkusanyiko mgumu uliofunikwa na uwekundu, maumivu unapoguswa, kuna uwezekano kuwa titi lina jipu.

Iwapo utatekeleza utambuzi wa mastitisi au jipu la titi, dhibiti uchungu kwa kutumia paracetamol, ukishikilia matiti na sidilia au kitu chochote kinachoweza kufungwa kwa kifua. Pia rufaa mwanamke kwa kituo cha afya na/au hospitali iliyoko karibu kwa matibabu ya antibiotiki.

Rufaa mwanamke aliye na mastitisi au jipu kwa matiti.

Utakapomshauri mwanamke aliye na maambukizi kwa matiti, usimshauri KAMWE awache kumnyonyesha mtoto kwa matiti yaliyo ambukizwa. Kuruhusu mtoto kunyonya husaidia kupunguza tatizo na maumivu. Hivyo, mshawishi anyonyeshe ila tu usaha unatoka kutoka kwa chuchu. Hata hivyo, kunyonyesha hairuhusiwi ikiwa sababu ya maambukizi inashukiwa kuwa ni kifua kikuu, ambayo inahusishwa na ushahidi wa maradhi ya muda mrefu na kupona (kovu) na maambukizi mapya katika titi hilo.

3.2.4 Maambukizi kwa kidonda

Maambukizi kwa kidonda wakati wa puperiamu kwa kawaida uathiri tishu ya msamba iliyokatika, maambukizi kwa episiotomi (mkato wenyewe hutekelezwa ili kuongeza uwazi wa uke ili mtoto aweze kupitia), au kidonda kufuatia upasuaji kwa fumbatio baada ya kuzaa kwa njia upasuaji inayotekelezwa kwa kituo cha afya.

Kwa ujumla, maambukizi kwa kidonda huwa wazi katika siku ya tatu au ya nne baada ya kuzaa na utambuliwa kwa erithema (wekundu katika eneo lililoambukizwa), na ugumu wa tishu iliyo juu ya eneo lililoathirika, ambayo hupata joto na huwa chungu inapoguswa. Usaha wa rangi ya manjano unaweza kutiririka kutoka kwa kidonda, na mama anaweza pia kuwa na joto jingi mwilini.

Mchoro 3.6 Kidonda kilichoambukizwa kwa msamba kinaweza kutibiwa kwa kuosha na maji vuguvugu yaliyo na chumvi, au kufinywa ili kutoa usaha.

Matibabu ya kidonda kwa msamba kilicho na maambukizi ni pamoja na kuondoa maumivu na paracetamol na kuosha eneo hilo na maji vuguvugu ambayo yametiwa chumvi kijiko kimoja katika kila lita ya maji. Kama kuna usaha kutoka kwa kidonda kwenye msamba, utoe kwa kufinya eneo hilo na kitambaa kilichowekwa katika maji vuguvugu yenye chumvi (Mchoro 3.6).

Ikiwa mama pia ana joto jingi mwilini na anahisi baridi, na unadhani kuna usaha ambayo haitoki nje ya kidonda, rufaa kwa kituo cha afya cha gazi ya juu ili aweze kutibiwa na antibiotiki. Ikiwa ana jipu, inaweza kutolewa kwa njia ya upasuaji. Wengi hupona haraka wakati usaha inatolewa kwa njia ya upasuaji na kutumia antibiotiki. Kwa kijumla antibiotiki hutumika hadi wakati mama hana joto jingi mwilini kwa masaa 24-48. Maambukizi ya kidonda kwenye fumbatio kwa kijumla hutibiwa katika hospitali, hivyo rufaa kina mama kwenye kituo cha afya cha gazi ya juu.

3.3 Uchunguzi wa shinikizo la juu la damu baada ya kuzaa

Shinikizo la diastoli la damu hupimwa wakati moyo umepumzika katikati ya mipigo ya moyo.

Ishara bainifu ya Shinikizo la juu la damu ya ujauzito ni Shinikizo la juu la damu, kwa kawaida shinikizo la juu ya diastoli ya zaidi milimita90 ya zebaki. Ulijifunza jinsi ya kupima shinikizo la damu ya mama katika Moduli ya Utunzaji katika ujauzito, Kipindi cha 9, na kuhusu matatizo ya damu ya ujauzito katika Kipindi cha 19. Hapa tutashughulika na Shinikizo la juu la damu inayoanza au kurudi wakati wa puperiamu. Ili kuchunguza haya, uliza mama kuhusu dalili zifuatazo:

  • Maumivu ya kichwa, pamoja na au bila matatizo ya kuona (kutoona vizuri), na wakati mwingine kichefuchefu na kutapika.
  • Mtukutiko kali zaidi (eklampsia). Hakikisha kwamba unajua istilahi ya mtukutiko inayotumika pale. Inaweza kuelezwa kama isiyo kuwa ya kawaida na isiyoweza kuzuilika zilizoambatana, kwa mikono na miguu, na au bila kupoteza fahamu.
  • Kuvimba kwa (edema) mikono na miguu, au hata uso.
  • Maumivu makali katika sehemu ya juu ya fumbatio.

Pima mkojo kwa kutumia kijiti cha kutumbukiza (kama ulivyofunzwa katika Kipindi cha 9 katika Moduli ya Utunzaji katika ujauzito). Mkojo ukipimwa na kijiti cha kutumbukiza kubaini kuwepo kwa protini, mama aliye na Shinikizo la juu la damu anaweza kuonyesha kuwepo kwa protini. Kuwepo kwa protini huonyeshwa juu ya kijiti cha kutumbukiza kutoka +1 hadi +3 na zaidi. Iwapo mojawapo ya uchunguzi uliyotajwa hapo awali uko, shuku Shinikizo la juu la damu iliyosababishwa na ujauzito. Rufaa mama haraka kwenye kituo cha afya kilicho karibu. Kumbuka kwamba shinikizo la damu baada ya kuzaa inaweza kuwa kwa mama yeyote, hata kwa yule ambaye alikuwa na shinikizo la damu la kawaida na hakuwa na dalili yoyote wakati wa ujauzito, leba, na kuzaa.

3.4 Mvilio ndani ya mshipa wa damu

Mvilio ndani ya mshipa wa damu- damu huganda, karibu kila mara katika moja ya mishipa ya ndani ya miguuni - ni tatizo nadra wakati wa puperiamu. Hata hivyo, wakati hutokea, inaweza kusababisha kifo kwa haraka kama ganda la damu litatoka kwa mshipa ya mguu na kuelekea kwa moyo, mapafu, au ubongo, na kuzuia damu muhimu kwa mshipa ya damu.

Uwezekano wa ukuaji wa mvilio ndani ya mshipa wa damu ni kawaida sana wakati wa ujauzito kuliko katika hali isiyo ya ujauzito, na uongezeka zaidi wakati wa puperiamu. Sababu hasa za damu kuganda katika mishipa ya ndani miguuni (mvilio) haijulikani. Hata hivyo, hatari huwa kubwa zaidi wakati mama anakaa muda mwingi kitandani na hafanyi chochote kwa siku kadhaa baada ya kuzaa. Katika sehemu nyingi za Afrika, desturi za nyumbani ni kuwa kina mama, baada ya kuzaa, hawapaswi kujishughulisha na chochote ila tu kukaa kitandani na kutembea tu kwenda chooni. Hivyo ni muhimu utambue dalili na ishara za mvilio ndani ya mshipa wa damu, tekeleza utambuzi na kurufaa mama hospitalini haraka iwezekanavyo. Kisanduku 3.2 linaonyesha dalili na ishara za kawaida za mvilio ndani ya mshipa wa damu.

Kisanduku 3.2 Dalili na ishara za mvilio ndani ya mshipa wa damu

  • Maumivu katika mguu mmoja tu: kawaida hutokea kwa ghafla, ikiwa na uchungu inayoendelea na aina ya maumivu.
  • Uchungu unapogusa: eneo hilo ni uchungu unapogusa mahali hapo.
  • Uvimbe: mguu ulioathirika huwa mkubwa na tofauti kubwa zaidi wa sentimita 2 wa mduara ikilinganishwa na mguu huo mwingine (wenye afya). Uvimbe unaweza kuwa kwa kafu au paja.
  • Ukamba unayohisika: unaweza kuhisi muundo-kama wa kamba ndani ya mguu uliovimba.
  • Mguu kubadilika rangi: mguu ulioathirika unaonekana kuwa nyekundu kidogo.
  • Maumivu kwenye kafu: anahisi uchungu wakati unajaribu kunyorosha kiungo cha kifundo cha mguu

3.5 Matatizo ya Akilini baada ya kuzaa

Matatizo ya akili ni jambo la kawaida baada ya kuzaa na ni pamoja na 'kununa' baada ya kuzaa, masumbuko baada ya kuzaa, na kichaa baada ya kuzaa.

3.5.1 Kununa na masumbuko baada ya kuzaa

Mchoro 3.7 Usaidizi unaweza kuwasaidia kina mama kupata nafuu kutokana na ‘kununa’ baada ya kuzaa.

Mabadiliko ya homoni hudhaniwa kuwa ndio hushababisha ‘kununa’ baada ya kuzaa, hali isiyo kali, ya muda, inayoisha yenyewe, ambayo kawaida hutokea siku chache baada ya kuzaa na huchukua hadi wiki mbili. Dalili zake kuu ni kuwepo kwa huzuni mara kwa mara, kulia, wasiwasi, kukasirika, kutotulia, kugeuza sununu mara kwa mara, maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, usahaulifu, na kukosa usingizi. Ni nadra kuathari vikubwa uwezo wa mama wa kufanya kazi au kuhudumia mtoto wake. Kutoa usaidizi wa upendo, huduma, na elimu imeonekana kuwa na mafanikio kwa uponaji wa mama (Picha 3.7).

Rufaa kina mama walio na masumbuko makali baada ya kuzaa.

Iwapo mama anapata masumbuko makali baada ya kuzaa (maendeleo ya huzuni, sununu iliyo chini, kukosa motisha ya kufanya chochote), itaathiri vikubwa uwezo wake wa kukamilisha shughuli za kawaida zinazohusiana na maisha ya kila siku. Hali za masumbuko huhitaji huduma muhimu na mama kutiwa moyo na wataalamu walio na mafunzo ya kiafya ya akili, hivyo rufaa mama haraka uwezavyo. Familia ya mama pia ni muhimu sana wakati wa matibabu. Kina mama wenye masumbuko makali wanaweza kukosa kunyonyesha mara tu baada ya kuzaa, na watoto wao wana uwezekano zaidi wa kuwa na matukio ya ugonjwa, kama vile kuhara.

  • Unaweza kueleza ni kwa nini mtoto anaweza kuathiriwa kwa njia hii?

  • Iwapo unyonyeshaji haitanzishwa, mama anaweza kumlisha mtoto na maziwa ya kutengeneza kwa kutumia chupa, ambayo huwa na hatari kubwa ya maambukizi kwa mtoto kutoka kwa chupa chafu. Mama aliye na masumbuko anaweza pia kukosa kuelewa maelezo ya ujumbe wa elimu ya afya juu ya namna ya kuzuia maambukizi kwa mtoto mchanga.

    Mwisho wa jibu

Rufaa mama, ikiwa dalili mbili au zaidi ya zifuatazo zitatokea katika wiki mbili za kwanza ya puperiamu:

  • Hali ya kujihisi mwenye hatia bila sababu au kujidharau
  • Kulia kwa urahisi
  • Kupungua kwa hamu au raha
  • Anahisi kuchoka, wasiwasi, na kukasirika wakati wote
  • Matatizo ya usingizi, kulala sana au kidogo sana
  • Kupungua kwa uwezo wa kufikiria au kumakinika kwa jambo
  • Kukosa hamu ya kula

Kunaweza pia kuwa na matukio ya kichaa baada ya kuzaa, inayoonekana kwa kudanganya au ndoto-kuona au kuamini mambo yasiyo kweli. Tutarejelea tatizo hili kali zaidi katika Kipindi cha 5 cha Somo. Utajifunza mengi zaidi kuhusu masuala ya afya ya akili, ikiwa ni pamoja na masumbuko na kichaa baada ya kuzaa, katika Moduli ya Magonjwa yasiyo ambukizi, Utunzaji wa Dharura, na Afya ya Akili.

Muhtasari wa Kipindi cha 3

Katika Kipindi cha 3, Umejifunza kuwa:

  1. Ingawa wakati muhimu zaidi wa kuvuja damu baada ya kuzaa ni katika kipindi cha tatu na nne cha leba, unapaswa kuendelea kuwa macho wakati wa puperiamu na kumshauri mama kuripoti utokaji wa damu yoyote kutoka ukeni.
  2. Sababu za kawaida za kuvuja damu baada ya kuzaa ni endometiritisi, mikazo duni, plasenta iliyobaka kwa uterasi, na kutoka kwa ngozi kavu katika makao ya plasenta.
  3. Kiasi chochote cha damu kutoka ukeni baada ya saa 24 ya kuzaa inafaa kuchukuliwa kama tatizo kuu na lazima mama apewe rufaa.
  4. Aina kuu za maambukizi baada ya kuzaa ni endometiritisi, mastitisi, maambukizi kwa mfumo wa mkojo, na kwa kidonda, ambazo zote kwa kawida uambatana na joto jingi mwilini.
  5. Hatari zinazochangia endometiritisis baada ya kuzaa ni leba ya muda mrefu, Kupasuka kwa Tando kabla ya Wakati inayochukuwa muda mrefu, uchunguzi wa ukeni kila mara, maambukizi kwa njia ya uzazi sehemu ya chini kabla ya ujauzito, plasenta iliyobaki kwa uterasi, uzaaji uliyo na matatizo ikiwa ni pamoja na upasuaji au kwa kutumia koleo.
  6. Mama ambaye amepata mastitisi baada ya kuzaa, anahimizwa kunyonyesha.
  7. Shinikizo la juu la damu baada ya kuzaa inayohusishwa na Shinikizo la juu la damu, odema, matatizo ya kuona, na mtukutiko (eklampsia), zinaweza kutokea kwa mama ambaye alikuwa na shinikizo la damu la kawaida na bila dalili wakati wa ujauzito, leba, na kuzaa.
  8. Mvilio ndani ya mshipa wa damu inahusishwa na maumivu na kuvimba kwa mguu, na kawaida zaidi hutokea katika kina mama ambao hukaa kitandani kwa siku kadhaa baada ya kuzaa.
  9. Baadhi ya kina mama wanaweza kupata matatizo ya kiafya akilini, ya kawaida na ni ya muda mfupi, ni kununa baada ya kuzaa ambayo si kali. Baadhi ya kina mama wanaweza kupata matatizo makali ya masumbuko, ambayo yanahitaji huduma na matibabu katika kituo cha afya cha ngazi ya juu.

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 3

Kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki, unaweza kutathmini mafanikio uliyopata katika Malengo ya somo kwa jibu maswali yafuatayo. Andika majibu yako katika shajara na uyajadili na Mkufunzi wako katika Mkutano ujao wa somo. Unaweza kulingasha majibu yako na nakala juu ya Maswali ya Kujitathmini mwisho wa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 3.1 (yanatathmini Malengo ya Somo 3.1, 3.2 na 3.5)

Unajadiliana na mmoja wa mhudumu wa afya mwenzawako kuhusu matatizo ambayo yanaweza kutokea wakati wa kipindi cha puperiamu. Ameanza tu mafunzo yake ya huduma ya afya na anataka kujua kuhusu maneno yafuatayo na dalili zao kuu. Utamwelezea nini kuhusu kila moja ya yafuatayo?

  • a.Kuchelewa kutokwa na damu baada ya kuzaa
  • b.Sepsisi baada ya kuzaa na joto njingi mwilini
  • c.Mastitisi
  • d.Shinikizo la juu la damu baada ya kuzaa
  • e.Masumbuko baada ya kuzaa
Answer
  • a.Kuchelewa kutokwa na damu, baada ya kuzaa ni uvujaji wa damu nyingi ukeni katika wiki ya kwanza na hadi wiki sita baada ya kuzaa. Kutokwa na damu baada ya kuzaa inaweza kuwa tishio kwa maisha na lazima mama apewe rufaa haraka. Visababishi vya kawaida ni pamoja na maambukizi (endometiritisi) ya ukuta wa ndani ya uterasi, mikazo duni ya uterasi, kutoka kwa ngozi kavu katika makao ya plasenta, au sehemu ya plasenta kubaki kwenye uterasi. Kisababishi cha hali hii kwa nafasi ndogo ni ujauzito isiyo kuwa ya kawaida.
  • b.Sepsisi baada ya kuzaa ni maambukizi ya bakteria kwa mfumo wa uzazi yaliyo kawaida sana baada ya kuzaa. Kawaida inaweza kuzuiwa kwa usafi wakati wa kuzaa. Joto jingi mwilini inaonyesha uwezekano wa sepsisi, lakini inaweza pia kuwa ni kutokana na maambukizi kwa mfumo wa mkojo au kidonda, VVU, malaria, homa ya matumbo, pepopunda, meningitisi, nimonia, na kadhalika.
  • c.Titi nyekundu lililo na maumivu huashiria mastitisi, inflamesheni kwa titi kutokana na maambukizi ya bakteria. Kina mama wanaonyonyesha wako katika hatari kubwa ya mastitisi baada ya kuzaa ikiwa mtoto hanyonyi vizuri na matiti hayaishi maziwa yote. Jipu ni hatari nyingine kutokana na maambukizi kwa titi, ambayo hutokea wakati usaha hukusanyika katika tishu iliyoambukizwa.
  • d.Shinikizo la juu la damu baada ya kuzaa ni shinikizo la juu la damu katika Utunzaji baada ya kuzaa. Dalili bainifu ni maumivu makali ya kichwa, mtukutiko (eklampsia), kufura, maumivu makali ya tumbo, na protini katika mkojo. Ni tisho kwa maisha na lazima mama apewe rufaa mara moja.
  • e.Masumbuko baada ya kuzaa ni kali kuliko kununa baada ya kuzaa. 'Kununa' ni hisia kali za wasiwasi na huzuni, au kuchanganyikiwa kwa akina mama wengi huwa nayo baada ya kuzaa na ambayo kwa kawaida huisha. Kina mama wanaopata masumbuko baada ya kuzaa (huzuni unayoendelea na sununu iliochini na motisha kidogo) lazima wapewe rufaa.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 3.2 (linatathmini Lengo la Somo 3.3)

Kamilisha mapengo yaliyowazi katika Jedwali 3.1, inayorejelea matatizo katika puperiamu.

Jedwali 3.1 Matatizo ya kawaida wakati wa puperiamu
DaliliIsharaUtambuzi unaoweza kuwepoHatua
Kutokwa na damu siku saba baada ya kuzaa
Maambukizi kwa mfumo wa mkojoMshawishi mama anywe kiowevu na umpatie rufaa
Uchungu kwa titi na joto jingi mwiliniTiti chungu inapogushwa, moto, na nyekundu
Uchungu kwa msambaKukatika kwa msamba na kutokwa na mchozo wa rangi ya manjano na uchungu ukigusa
Answer

Jedwali 3.1 lililokamilishwa linaonekana kama ifuatavyo:

Jedwali 3.1 Matatizo ya kawaida wakati wa puperiamu.
DaliliIsharaUtambuzi unaoweza kuwepoHatua
Kutokwa na damu siku saba baada ya kuzaa Uterusi ikiwa katikati ya kitovu na pelvisiEndometiritisisiAnza kumpatia kiowevu kwa mshipa
Kukojoa mara nyingi na kwa harakaUchungu kwenye pelvisi juu ya kibofuMaambukizi kwa mfumo wa mkojoMshawishi mama anywe kiowevu na umpatie rufaa
Uchungu kwa titi na joto njingi mwiliniTiti chungu linapoguswa, moto, na nyekunduMastitisi, labda jipu kwa titiMpatie dawa ya kupunguza uchungu na umpatie rufaa
Uchungu kwa msambaKukatika kwa msamba na kutokwa na mchozo wa rangi ya manjano na uchungu ukigushaMaambukizi kwa kidondaOsha na majimoto yaliyo na chumvi, finya usaha, mpatie, paracetamol ilikudhibiti uchungu, na labda umpatie rufaa ili apate antibiotiki

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 3.3 (linatathmini Lengo la Somo 3.4)

Umemtembelea mama aitwaye Lakesh ambaye alizaa siku saba zilizopita. Mara ya mwisho ulimwona alikuwa amelala kitandani. Wakati huu anaamka kukusalimia na unamwona kwamba anatembea kwa shinda. Unamuuliza kama ameumia. Anasema ana uchungu wa ghafla katika mmoja wa miguu wake. Unaweza kuthani ni nini na ungefanya nini kuhusu jambo hilo?

Answer

Unapaswa kukumbuka mara moja kwamba hatari ya mvilio ndani ya mshipa wa damu ni kubwa zaidi kama mama analala sana kwa muda mrefu baada ya kuzaa, kama vile Lakesh amekuwa akifanya. Ungechunguza kwa haraka kama ishara yoyote au zote za mvilio ndani ya mshipa wa damu kama ilivyowekwa katika Jedwali 3.2. Iwapo ishara zinakuelekeza kuwa Lakesh ana mvilio ndani ya mshipa wa damu, unafaa kumapatia rufaa kwa kituo cha afya cha ngazi ya juu haraka iwezekanavyo.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 3.4 (linatathmini Lengo la Somo 3.5)

Mama mwingine aitwaye Almaz yuko katika wiki ya kwanza baada ya kuzaa; anajihisi kila mara mwenye hatia na kujidharau, analia kwa urahisi na anahisi mchovu, wasiwasi, na kukasirika. Ni nini kinaweza kuwa kinamwathiri? Ni dalili gani hatia unaweza kumliza, ili kuthibitisha utambuzi wako?

Answer

Utambuzi unaoweza kuwa kwa hali ya Almaz ni masumbuko baada ya kuzaa. Ili kuthibitisha utambuzi wako, mwulize kuhusu dalili zifuatazo:

  • Kupungua kwa hamu ya chochote au furaha
  • Matatizo ya usingizi, kulala sana, au kidogo sana
  • Upungufu wa uwezo wa kufikiria au kumakinika kwa jambo
  • Ukosefu wa hamu ya kula

Mwisho wa jibu