Skip to main content
Printable page generated Saturday, 27 April 2024, 2:54 AM
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Saturday, 27 April 2024, 2:54 AM

7. Unyonyeshaji, kanuni ya mfululizo joto na kuwapa ushauri kina Mama walio na virusi vya ukimwi (VVU)

Kipindi cha 7 Unyonyeshaji, kanuni ya mfululizo joto na kuwapa ushauri kina Mama walio na virusi vya ukimwi (VVU)

Utangulizi

Katika kipindi, baada ya kuzaa ushauri kwa mama aliye na mtoto mchanga huangazia mambo mengi, pamoja na yale ambayo yamejadiliwa katika vikao vya somo vya awali. Mambo hayo ni pamoja na uzuiaji wa maambukizi, lishe kwa mama na upangaji uzazi. Katika Kipindi hiki cha somo, tunarejelea kwa undani mada mbili ambazo zimeguziwa hapo mbeleni: jinsi ya kuanza na kudumisha unyonyeshaji bora na jinsi ya kumpatia mtoto joto kwa kutumia kanuni ya mfululizo joto. Sehemu ya kwanza ya Kipindi hiki cha somo kinahusu ulishaji wa mtoto mwenye uzito wa kawaida, afya nzuri na mzima. Halafu tunaangalia ushauri maalum ambayo kina mama walio na VVU wanahitaji kuhusu ulishaji wa watoto walio wazima na wenye uzito wa kawaida. Kipindi cha 8 cha somo kinajadili huduma wa kijumla unaohitajika ili kulisha na kudumisha halijoto wa muda mwilini au uzito wa chini kwa watoto wachanga.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 7

Baada ya Kipindi hiki, unafaa kuweza;

7.1 Kufafanua na kutumia kwa ufasaha maneno yote muhimu yaliyochapishwa kwa herufi nzito. (Swali la Kujithamini 7.2)

7.2 Kueleza faida za maziwa ya mama kwa mtoto mchanga na umuhimu wa unyonyeshaji wa kipekee kwa mama na mtoto mchanga. (Swali la Kujitathmini 7.1)

7.3 Kuelezea hatua za kuanzisha unyonyeshaji bora kupitia njia nzuri ya mama kuketi na namna ya kumweka mtoto kwa matiti yake. (Swali la Kujitathmini 7.2)

7.4 Kuelezea jinsi ya kumshauri mama aliye na VVU kuhusu aina za ulishaji ili mtoto wake apunguze hatari ya kuambukizwa VVU kupitia maziwa ya mama. (Swali la Kujitathmini 7.1)

7.5 Kuelezea jinsi watoto wachanga hupoteza joto na jinsi ya kuzuia hipothemia kwa kutumia kanuni ya mfululizo joto

7.1 Kumpa ushauri mama kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga

Kila mara ni bora kupatiana ushauri kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga kabla ya kuzaliwa na pia kuendelea kusisitiza baada ya kipindi cha kuzaliwa. Mafunzo haya lazima yaangazie kuhusu uanzishaji na udumishaji wa unyonyeshaji bora. Utaratibu wa kupata haya yameandikwa kwa muhtasari katika Kisanduku 7.1

Kisanduku 7.1 Utaratibu wa unyonyeshaji bora

  • Anza kunyonyesha baada ya saa moja ya kuzaa (unyonyeshaji wa mapema)
  • Usimptie mtoto chochote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza (unyonyeshaji wa kipekee)
  • Usimwage maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaa, huwa na protini na kingamwili ambayo ni muhimu kwa mtoto mchanga. Unapaswa kumwambia mama amlishe nayo mtoto mchanga, kwa sababu ni ‘chanjo’ ya kwanza ambayo mtoto atapata.
  • Keti kwa hali nzuri wakati unanyonyesha
  • Hakikisha mtoto anapata vizuri matiti ya mama anaponyonya
  • Hakikisha mtoto ananyonya vizuri

Unapomtembelea baada ya kipindi cha kuzaa, mwambie mama amweke mtoto kwa matiti ili ukague namna anavyompatia matiti na anavyonyonya (tunaelezea jinsi ya kufanya hivyo katika sehemu inayofuata). Ikiwa mtoto alikuwa amelishwa hivi karibuni, ngojea angalau saa moja kabla ya kumpatia maziwa ya matiti tena. Hii itakupatia fursa ya kuchunguza jinsi mtoto anavyonyonya na kuweza kubaini iwapo kuna matatizo yoyote ya kunyonya, ambayo unaweza kumsaidia mama kutatua. Kabla ya kuondoka hakikisha kwamba mama anaelewa jinsi ya kunyonyesha mtoto wake kwa njia inayofaa.

7.1.1 Ishara nne nzuri za mama kukaa

Jambo la kwanza ni mama kuketi kwa utulivu (tazama Mchoro 7.1a) na kudumisha ishara nne nzuri za kuketi

  • Kichwa na mwili wa mtoto mchanga uwe laini
  • Mtoto mchanga atazame matiti yake na pua lake liwe kinyume cha chuchu
  • Mwili wa mtoto mchanga iwe karibu na ya mama
  • Mama anashikilia mwili wote wa mtoto bali sio shingo na mabega pekee yake.

Ikiwa mama amewahi kufanyiwa upasuaji wakati wa kuzaa au fumbatio lake ni uchungu kwa sababu nyinginezo, anaweza kuwa na starehe akimshikilia mtoto kama inavyoonyeshwa katika Mchoro 7.1(b). Inaweka uzito wa mtoto mbali na fumbatio lake. Anaweza kulisha mapacha hivi pia, kila mmoja na titi lake. Usiku au ikiwa amechoka na anahitaji kupumzika, anaweza kumlisha mtoto akiwa amelala chini (Mchoro 7.1c), lakini ikiwa atabaki macho tu.

Mchoro 7.1 (a) Mama huyu yuko katika hali nzuri ya unyonyeshaji bora (b)Hii ni hali nzuri ya kunyonyesha wakati mama amefanyiwa upasuaji wa fumbatio, au ikiwa analisha mapacha. (c) Mtoto anaweza kulishwa akilala chini, lakini ikiwa mama yuko macho.
  • Kunyonyeshaji ukiwa umelala chini (Mchoro 7.1c) sio nzuri isipokuwa tu mama akiwa macho tu. Unaweza kupendekeza ni kwa nini?

  • Ikiwa mama atalala, anaweza kumlalia mtoto mchanga ambaye anaweza kuwa hana uwezo wa kupumua na ukosefu wa hewa (kufa kutokana na oksijeni)

    Mwisho wa jibu

7.1.2 Ishara nne nzuri za uhusiano mzuri

Mara tu hali nzuri ya kuketi inapogunduliwa, mwonyeshe mama jinsi ya kumsaidia mtoto mchanga kufikia chuchu. Anapaswa

  • Kumguza kinywa cha mtoto mchanga na chuchu yake.
  • Ngojea hadi kinywa cha mtoto mchanga umefunguka wazi kabisa
  • Amshongeshe haraka mchanga wake kwa titi lake, akilenga kinywa cha chini, chini ya chuchu. Halafu tazama ishara za uhusiano mzuri (tazama Kielelezo 7.2)
Mchoro 7.2 (a) Mtoto huyu ameweka kinywa vizuri kwa titi; (b) Mtoto huyu hajaweka kinywa vizuri kwa titi.

Ishara nne za uhusiano mzuri ni:

  • Kinywa kifunguliwe wazi kabisa
  • Kinywa cha chini kiunuliwe juu
  • Kidevu kiguze titi
  • Areola (sehemu nyeusi inayozunguka chuchu) ionekane juu ya kinywa cha mtoto kuliko chini yake.

Mshauri mama atoe maziwa katika titi moja kabla ya kubadilisha kwa nyingine, ili mtoto apate maziwa ya nyuma yenye virutubishi tele, ambayo hutolewa wakati karibu maziwa yanaisha katika titi.

7.1.3 Unyonyeshaji unaofaa

Ishara nzuri za unyonyeshaji unazofaa ni kama ikiwa mchanga ananyonya kwa kawaida, polepole, na yenye nzito, wakati mwingine anapumzika kidogo. Mama anapaswa kukwambia yuko salama na hakuna maumivu yoyote.

Ikiwa utagundua kwamba uhusiano na unyonyeshaji sio nzuri kama inavyostahili, mweleze mama ajaribu tena na kukagua jinsi mtoto anavyokula. Ikiwa bado hawatatambua unyonyeshaji bora, hivyo utadhania mchanga ana shida ya kula au mama ana shida ya titi inayofanya uhusiano kuwa ngumu. Ikiwa hali ni hivyo, wapatie rufaa mama na mtoto kwa kituo cha afya kwa ushauri na utunzi zaidi.

7.2 Ni nini manufaa ya unyonyeshaji?

Unyonyeshaji huwa na manufaa mengi kwa mama na mtoto. Unapaswa kuwahimiza kina mama kunyonyesha kwa kipekee angalau kwa miezi sita za kwanza kwa kuwaelezea manufaa yake.

7.2.1 Manufaa ya unyonyeshaji kwa mtoto mchanga

Maziwa ya titi ni lishe kuu lililo bora kwa watoto kwa kuwa humpa virutubishi vyote kwa kiasi na ulinganisho sahihi kwa maendeleo na ukuaji wa kawaida hadi kufikia miezi sita. Hufyonzwa na kumeng’eywa kwa urahisi. Pia maziwa ya titi ni safi na yenye joto na huepekunane na hatari za kumlisha na maziwa yaliyotengezwa inayokuja kama poda na huchanganywa na maji kisha kutolewa kwa kutumia chupa.

  • Unaeza kupendekeza vyanzo vya hatari kwa mtoto mchanga kutokana na maziwa yaliyotengenzwa vibaya.

  • Kuna hatari ya kuambukizwa kutokana na utengenezaji wa maziwa kwa kutumia maji yaliyochafuliuwa, au ikiwa chupa na chuchu hazitasafishwa kabisa. Ikiwa mama atamlisha mara kwa wakati mmoja, na hawezi kuhifadhi katika sehemu baridi kwa sababu hakuna vifaa vya kuhifadhia katika sehemu baridi, bakteria inamea katika maziwa yenye joto. Vile vile, ikiwa ataweka poda nyingi au kidogo sana katika kila chupa, mtoto atashikwa na utapiamlo ikiwa kemikali ni hafifu sana au kupata kiwango kikubwa sana katika ogani zake kutokana na ukolezi mwingi wa kemikali.

    Mwisho wa jibu

Maziwa ya titi huwa na elemeti zinazopigana na maambukizi, kama vile kingamwili, seli hai na molekuli zinazosaidia mwili wa mtoto kupigana na maambukizi. Pia inahimiza ukuaji wa bakteria yenye faida katika utumbo wa mazwa. Vitu hivi vya maziwa ya titi husaidia kuzuia magonjwa ya kuhara, visababishi vikuu vya vifo vya wachanga kutoka jamii masikini.

Maziwa ya mama pia hupunguza hatari ya aleji kwa mtoto mchanga. Aleji ndio hupinga mabadiliko ya mwili dhidi ya elemeti za lishe, chavua kutoka kwa mimea, wanyama na vitu vingine visivyokuwa na athari vinavyoguza mwili au zinazoingia ndani kupitia pua, kinywa au macho. Watoto wako katika hatari zaidi ya aleji ikiwa kuna historia nzito ya aleji ya familia.

7.2.2 Manufaa ya unyonyeshaji kwa mama

Unyonyeshaji ni (karibu) bure – mama anahitaji chakula cha kuongezea wakati ananyonyesha, lakini bei ni angalau rahisi kuliko kunua lishe ya fomula/kemikali, chupa na chuchu. Kila wakati hupatikana mara moja, kwa hivyo mama hanashida ya kusafisha kabisa chupa na chuchcu, na kutengeneza lishe za kemilaki mara nyingi kila siku. Inatosheleza kihisia kwa mama kunyonyesha mtoto vizuri na uhusiano husaidia kuleta uelewano bora kati yao.

Homoni (oksitosini) ndiyo hufanya maziwa kububujika kutoka kwa matiti kwa kupunguza misuli ndogo zilizokaribu na chuchu vile vile zilizokaribu na uterasi. Kwa hivyo unyonyeshaji unasaidia uterasi kurudia hali yake ya kawaida.

  • Ni manufaa gani mengine ambayo unaweza kupendekeza yanayotokana na upunguaji wa miometriumu (safu ya msuli ulio katika uterasi)

  • Upunguaji husaidia kufunga mishipa ya damu iliyoraruka mahali plasenta umeshikana na ukuta wa uterasi na hii hupunguza kiasi cha uvujaji wa damu katika uke wakati wa kipindi cha kuzaa/puperiumu na kupunguza hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa.

    Mwisho wa jibu

Unyonyeshaji husaidia mama kupoteza uzani wa ziada alizoongeza wakati wa ujauzito. Ujauzito ndio hubadilisha maumbo ya matiti ya mwanamke bali sio unyonyeshaji.

7.2.3 Unyonyeshaji na kudhibiti muda wa kuzaliwa

Unyonyeshaji wa kipekee kwa watoto walio na umri wa chini ya miezi sita (kulisha mtoto kwa kutumia maziwa ya mama bila viowevu au vyakula vingine) hupunguza sana nafasi ya mama kuwa mjamzito tena iwapo itaanzishwa mwanzoni (katikati ya saa moja ya kuzaa), na kudumishwa kwa miezi sita ya kwanza iliyopendekezwa. Waeleze mama na mpenzi wake kwamba ikiwa mwanamke anajishirikisha na ngono na hafanyi unyonyeshaji wa kipekee kwa watoto walio na umri wa chini ya miezi sita, anaweza kuwa mjamzito haraka wiki nne baada ya kuzaa. Hivyo basi, taarifa juu ya wakati wa kuanza njia za kupanga uzazi zitatofautiana ikiwa mwanamke ana nyonyesha au la.

Katika Afrika inapendekezwa kwamba ujaribu kuwashawishi kina mama kuwapatia watoto unyonyeshaji wa kipekee kwa miezi sita kwa sababu nyingi, ikiwa ni pamoja na kukandamiza mzunguko wake wa hedhi, lakini tu ikiwa atatimiza vigezo vifuatavyo:

  1. Mtoto anapaswa kunyonyeshwa kwa kipekee akihitaji akiwa na umri wa chini ya miezi sita (wakati wowote mtoto anataka kulishwa) kati ya kiwango cha chini ya mara 8 hadi12 kwa siku, ikiwa ni pamoja na angalau lishe moja usiku.
  2. Muda baina ya lishe ya mchana haipaswi kuwa zaidi ya masaa manne na lishe ya usiku haipaswi kuwa zaidi ya masaa sita.
  3. Kama vipindi vyake vya hedhi vitarudi sawa wakati wa kunyonyesha kwa mtoto aliye na umri wa chini ya miezi sita, anaweza kupata mimba kwa urahisi!

Sisitiza kwamba baada ya miezi sita, hatakuwa salama kutokana na kuwa mjamzito kwa kunyonyesha pekee. Anapaswa kuchagua upangaji mwingine wa uzazi. Utajifunza yote kuhusu haya katika Moduli kuhusu upangaji wa uzazi katika mtaala huu. Jedwali 7.1 linatoa muhtasari wa manufaa ya unyonyeshaji wa kipekee kwa mama na mtoto mchanga.

Jedwali 7.1 Manufaa ya maziwa ya mama na unyonyeshaji.
MamaMtoto mchanga
Ni rahisi sana kuliko ile ya kutengenezwaIna lishe kamilifu
Inapatikana kila mara (tayari)Ina meng’enywa na kufyonzwa kwa urahisi
Huridhisha akiliNi safi na ina joto
Kupunguka kwa uvunjaji wa damu    Ina dutu za kupambana na maambukizi
Inaweza kutumika kama udhibiti wa uzaziHuzuia ugonjwa wa kuhara
Husaidia kupunguza uzito mwingi mwiliniHupunguza hatari ya aleji
Huongeza ari ya kuwaunganisha pamoja na mtoto mchangaHuongeza ari ya kuwaunganisha pamoja na mama

7.3 Kushauri mama aliye na VVU kuhusu kumlisha mtoto wake

Upimaji wa VVU, ushauri na uzuiaji wa maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto imejadiliwa kwa kina katika Moduli ya Magonjwa ambukizi, na pia katika Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito.

Kina mama ambao wana VVU na watoto wao wanahitaji huduma maalum kabla, baada ya leba na wa kuzaa. Hivyo basi, ikiwa mama ameshauriwa na kupimwa VVU kabla au wakati wa ujauzito, na anajua kwamba ana VVU, unapaswa kujaribu kumshawishi azae mtoto wake katika kituo cha afya. Kwa njia hiyo yeye na mtoto wake watapata huduma maalum kutoka kwa watalaamu wa afya na mafunzo maalum katika kuzaa watoto kutoka kwa mama aliye na VVU, na uzuiaji wa maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto.

Baada ya kuzaa anaweza hitajika kuchukua dawa za kupunguza makali ya VVU, dawa ambazo ameagizwa kwa kliniki ya VVU, na msaada wako ni muhimu kwa kumsaidia kuweka dawa kwa utaratibu. Idumishe siri kuhusu hali yake na ufanye ziara za mara kwa mara kwake kwa kuwa anaweza kuhitaji msaada mwingi wa kisaikolojia na wa kijamii mara tu baada ya kuzaa. Iwapo kuna kikundi cha jamii muunganishe naye kwa ajili ya msaada. Hakikisha kwamba mpenzi wake ameshauriwa na amepimwa kama ana VVU na pia ashiriki katika mchakato mzima wa huduma kwa.

7.3.1 Maziwa ya mama au ya pakiti?

Katika Kipindi hiki cha somo tunaangazia hatari ya VVU kuambukizwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto mchanga kupitia maziwa ya matiti yake, na jinsi unaweza kumsaidia na kumshauri kuhusu lishe nyingine. Iwapo kina mama 20 walio na VVU watanyonyesha kwa kipekee kwa miezi sita ya kwanza, kwa kawaida moja hadi watoto watatu wataambukizwa VVU kupitia maziwa ya mama. Hivyo mama anachaguo ngumu ya kufanya. Anapaswa kuangalia pande zote mbili za hatari ya mtoto kutokana na maambukizi ya VVU wakati wa kunyonyesha, dhidi ya hatari ya kukosa kunyonyesha na kupoteza manufaa yote kama yalivyoelezwa hapo juu. Lishe ya kutengenezwa pia huweka mtoto wazi kwa ongezeko la hatari ya maambukizi kwa kupitia chupa iliyochafu na utapiamlo kutokana na mlo usiotengenezwa vizuri.

7.3.2 Kubadilisha ulishaji na kigezo cha (IKGES) kinachokubalika, Kuaminika, Gharama nafuu, Endelevu na Salama

Unyonyeshaji wa kipekee kwa watoto walio na umri wa chini ya miezi sita HAIPENDEKEZWI kwa watoto wa wanawake walio na VVU, kwa kuwa njia pekee ya kulinda mtoto kabisa kutokana na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama yake ni kumlisha kwa kutumia maziwa ya pakiti. Hii inajulikana kama kubadilisha ulishaji. Hata hivyo, familia nyingi haziwezi kumudu kununua maziwa ya pakiti ya kulisha mtoto, na kulisha kwa chupa inaweza kuwa haikubaliki katika baadhi ya jamii. Pamoja na masuala haya yote akilini Shirika la Afya Duniani limeanzisha vigezo vifuatavyo (inayojulikana kama kigezo cha IKGES), ambayo inahitaji kufikiwa kabla ya kushauri mama aliyekuwa na VVU kutumia maziwa ya pakiti:

  • Inayokubalika: Kubadilisha ulishaji na maziwa ya mama inakubalika kwa mama, familia na jamaa.
  • Kuaminika: Mama anapata maji safi na yaliyosalama kutumia kuosha chupa za ulishaji, chuchu, kikombe cha kupima na kijiko, pia kuchanganya maziwa yaliyotengenezwa na maji ikiwa yameletwa kama poda.
  • Gharama nafuu: Familia wanaweza kumudu kununua maziwa yaliyotengenzwa ya kutosha au maziwa ya wanyama kulisha nayo mtoto vizuri.
  • Endelevu: Mama ana uwezo wa kuandaa vyakula kwa mtoto kila mara kama ilivyopendekezwa na mahitaji ya mtoto.
  • Salama: Maziwa ya kutengenezwa inapaswa kuwa salama na lishe bora kwa afya ya mtoto.

Kigezo cha IKGES imeelezwa kwa Mchoro 7.3. Wakati lishe ya kubadilisha inatimiza kigezo cha IKGES, kuepusha kwa kunyonyesha kwa kina mama wote wenye VVU inapendekezwa.

Mchoro 7.3 Kigezo cha IKGES hukusaidia kushauri kina mama walio na VVU kuhusu kulisha chaguzi kwa watoto wao wanaozaliwa. (Chanzo: WHO, 2010, Miongozo juu ya VVU na Ulishaji wa watoto wachanga)

7.3.3 Upunguzaji wa hatari ya virusi kutokana na unyonyeshaji

Iwapo ubadilishanaji wa lishe utakataliwa na mama aliye na virusi vya ukimwi, kwa sababu nyinginezo, kuna vitu anavyoweza kufanya ili kupunguza hatari ya usambazaji wa virusi wakati ananyonyesha. Mashauri:

  • Aweke nafasi baina ya unyonyeshaji iwe fupi iwezekanavyo (isiwe zaidi ya masaa tatu) ili kuepeukana na kukusanyika kwa virusi katika maziwa ya matiti.
  • Iwapo maambukizi ya bakteria (uvimbe wa matiti) ya matiti itaanza kukua, au ana chuchu ambayo imepasuka, asimlishe tena na titi lililo ambukizwa na utafute matibabu ya haraka.
  • Angalia kinywa cha mtoto mchanga ikiwa ana vidonda na utafute matibabu ikihitajika.
  • Andaa mabadiliko ya ubadilishanaji wa lishe iwapo hali ya mambo yake itabadilika na anaweza kupata kigezo cha IKGES (Inayokubalika, Uwezekano, Gharama nafuu, Endelevu na Salama).

Katika miezi sita, iwapo ubadilishanaji wa ulishaji ungali haujakubaliwa, hauwezekani, haupatikani, hauidhinishwi na sio salama, mshauri yeye anendelee kunyonyesha lakini akitumia ogezeko la chakula kinachokamilishana. Unyonyeshaji wote unafaa kusimamishwa mara tu lishe bora na inayotosha isiyokuwa na maziwa ya matiti inapotolewa.

7.4 Kumpatia mtoto mchanga joto

Watoto wachanga hushikwa na baridi au joto haraka kuliko watoto wengine au watu wazima kwa sababu hawawezi kudhibiti kwa urahisi halijoto mwilini mwao. Kwa hakika hupatwa na hipothemia, kwa hivyo inamaanisha baridi nyingi kwa mtoto, wakati halijoto katika kwapa au rektamu. Iwapo halijoto ya chini itaendelea kwa muda mfupi, itafanya mfumo wa mwili kukosa kufanya kazi vizuri na hii ni tishio kwa maisha. Hipothemia ni kisababishi kuu cha magonjwa na vifo katika watoto wachanga, haswa watoto wanaozaliwa mapema (Kuzaliwa kabla ya wiki 36 ya ujauzito) na wale wanaozaliwa na uzito wa chini (chini ya gramu 2,500). Kipindi cha 8 cha Somo itakufunza kuhusu matatizo na utunzi wa watoto hawa wadogo au wanaozaliwa mapema.

Kwa kawaida hipothemia husababishwa zaidi na mama kukosa maarifa bali sio nguo za kumpa mtoto joto. Kwa hivyo hakikisha umemwelezea mama umuhimu wa kumweka mtoto katika hali ya joto kila wakati ili kuhakikisha halijoto ya kawaida ya mwili imedhibitiwa, juu ya sentigredi 36.5 na chini ya 37.5.

7.4.1 Jinsi ya kupima halijoto ya mtoto mchanga.

Weka kipimajoto katikati ya kwapa (rektemu iwapo una kipamajoto ya kupima rektemu) kwa kati ya dakika mbili na tatu, kisha usome halijoto kwa kuzingatia aina ya kipimajoto unayotumia. (Ulijifunza jinsi ya kutumia aina mbalimbali za vipamajoto katika Kipindi cha 9 cha Somo cha Moduli ya Huduma Kabla ya Kuzaliwa.) Wakati vipimajoto havitumiwi vipaswa kuhifadhiwa kama vimekaushwa. Kabla na baada ya kupima halijoto ya mtu, kipimajoto kinapaswa kuoshwa na antiseptiki ili kuzuia maambukizi kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Ni muhimu kufahamu wakati halijoto iko chini ya kawaida, kabla ya kufika chini ya Sentigredi ya 35.5.

7.4.2 Je, ni wakati gani watoto wachanga wako katika hatari kubwa ya kupata hipothemia?

Watoto wachanga wanalio na matatizo hasa ya kutengeneza joto ya kutosha katika miili yao, au ambao hupoteza joto jingi kwa sababu ya matunzo mabaya kutoka kwa mama, wamo hatarini zaidi.

Watoto wachanga ambao wanaweza kukosa kutengeneza joto la kutosha ni pamoja na wale ambao:

  • Hawajatimiza umri wa kuzaliwa
  • Wana uzito wa chini wakati wa ukilinganisha na umri wa ujauzito.
  • dhoofika (konda)
  • Walioambukizwa
  • Hypoxic (upungufu wa oksijeni wakati wa uchungu wa kuzaa na wanapozaliwa).

Watoto wachanga wanaopoteza joto kupita kiasi ni pamoja na wale ambao:

  • Ulowa baada ya kuoshwa, au kuachwa na nguo zilizolowa
  • Hawajalishwa ya kutosha
  • Wameachwa kwa mazingira baridi, bila mavazi au mapambo ya kutosha, hasa wakati wanapolala
  • Huwa uchi wakati wana nyonyeshwa
  • Hulishwa karibu na dirisha baridi, katika upepo baridi.

7.4.3 Ni jinsi gani watoto wachanga hupoteza joto?

Utaratibu wa jinsi mtoto mchanga unapoteza joto imewekwa kwa muhtasari katika Kielelezo 7.4, na imeelezwa hapo chini.

Mchoro 7.4 Utaratibu wa upotezaji wa joto kutoka kwa ngozi ya mtoto mchanga. (Chanzo: Shirika la Afya Ulimwenguni, 1997, Safe Motherhood: Thermal Protection of the Newborn, Practical Guide, inapatikana kutoka http://whqlibdoc.who.int/ hq/ 1997/ WHO_RHT_MSM_97.2.pdf)

Myuko. Hii ni upotezaji wa joto kutoka ngozi ya mtoto mchanga kwa mazingira. Watoto wachanga hupoteza joto jingi kwa njia ya myuko wakati wameachwa kwa hewa baridi au upepo.

Upitishaji. Hii ni upotezaji wa joto wakati mtoto mchanga hulala juu ya pahali baridi. Watoto wachanga hupoteza joto kwa njia ya upitishaji wakiwekwa uchi juu ya meza baridi, kipima uzito au wamefunikwa na blanketi baridi au taulo.

Uvukizi. Hii ni upotezaji wa joto kutoka kwa ngozi ya mtoto mchanga ilio na maji kwa mazingira. Watoto wachanga hupoteza joto kwa njia ya uvukizi baada ya kuzaliwa au kuoga. Hata mtoto mchanga anaweza kupoteza joto kwa njia ya uvukizi akiwa na nepi iliyolowa.

Mnururisho. Hii ni upotezaji wa joto kutoka ngozi ya mtoto mchanga kwa vitu vilio mbali baridi, kama vile dirisha baridi au ukuta n.k.

Hatimaye, unapofahamu kwamba mtoto anaweza kupoteza joto kwa jinsi hizi nne zilizoelezwa hapo juu, lazima umshauri mama aepukane na hali ya kumwacha mtoto kwa upepo. Mshauri kwamba kabla ya kumvua mtoto nguo anapomwogesha, anapaswa kufunga milango na madirisha yote, amfunike mtoto aliyelowa na kumkausha haraka.

Wacha kusoma kwa muda na ufikirie uzoefu wako mwenyewe katika jamii yako. Umeona hali zenye kina mama walikuwanazo katika hatari ya kumwachilia mtoto wao kupoteza joto kwa njia yoyote imeelezwa hapo juu?

7.4.4 Kanuni ya mfululizo joto katika huduma baada ya kuzaa

Mama anapaswa kuelewa kwamba kumpatia mtoto joto si kazi ya mara moja. Ni kazi ya kuendelea ambayo ina maanisha kufuta ‘kanuni ya mfululizo joto’. Mfululizo joto ni mfumo wa kumpatia mtoto joto mara moja baada ya kuzaliwa, popote itokeapo (katika kituo cha afya au nyumbani kwa mama), wakati wa usafirishaji na wa kumlisha na kumtunza mtoto. Sehemu za kanuni ya mfululizo joto zimeorodheshwa katika kisanduku 7.2.

Kisanduku 7.2 Sehemu za mfululizo joto
  • Upanguzaji na ufunikaji wa mtoto mara tu anapozaliwa.
  • Kumpatia mtoto joto wakati wa utaratibu wowote, ikiwa ni pamoja na uhaisho.
  • Kumweka mtoto mchanga ngozi-kwa-ngozi na mama.
  • Unyonyeshaji wa mapema ndani ya saa moja ya kuzaliwa. Maziwa moto ya mama na uhusiano wa mwili husaidia kumpatia mtoto mchanga joto.
  • Kuhahirisha uoshaji wa mtoto kwa masaa 24 ya kwanza.
  • Kumweka mtoto joto wakati wa usafiriji.
  • Kuvalisha mtoto mavazi na matandiko sahihi wakati wote.

Kanuni ya mfululizo wa joto lazima idumishwe kwa watoto wote, lakini huduma maalum lazima ichukuliwe ili kuwapatia joto watoto wasiotimiza umri wa kuzaliwa na walio na uzito wa chini wakati wa kuzaliwa, kama utakavyoona katika Kipindi cha Somo kijacho.

Muhtasari wa Kipindi cha 7

Katika Kipindi cha 7 umejifunza kwamba:

  1. Unajukumu muhimu katika kipindi cha baada ya mama kuzaa, kumshauri juu ya kunyonyesha na jinsi ya kumpatia mtoto joto.
  2. Unapaswa kufunza mama kuhusu hali mbalimbali za kuketi kwa ajili ya unyonyeshaji bora na ishara za ushikiliaji wa titi vizuri.
  3. Kuna faida nyingi za maziwa ya mama na unyonyeshaji kwa mama na mtoto wake mchanga, ikilinganishwa na maziwa ya kutengenezwa, ikiwa ni pamoja na kupunguza hatari za maambukizi ya utumbo kwa mtoto, na kurudi haraka kwa uterasi kwa hali yake ya kawaida.
  4. Kina mama walio na VVU lazima wapewe ushauri ili waepukane na kunyonyesha kabisa kama wanaweza kulisha watoto na maziwa ya kutengenezwa ambayo hutimiza vigezo vya (AFASS): Kukubalika, Kuwezekana, Gharama Nafuu, Endelevu na Salama.
  5. Watoto wachanga wanaweza kupoteza joto haraka kupitia upotezaji wa joto, myuko, uvukizi, na mionzi. Kanuni ya mfululizo joto inakueleza jinsi ya kumweka mtoto joto wakati wote.

Maswali ya kujitathmini ya Kipindi cha 7

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki, jibu maswali haya kutathmini uliojifunza. 7.1 (Malengo ya Somo la 7.2 na 7.4)

Unashangaa utamwambia nini mama aliye na VVU ambaye anataka kunyonyesha. Je utamshauri vipi?

Answer

Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuwa umetengeneza nakala kuhusu hali hii ngumu. Utamhurumia mama kwa nia ya kutaka kunyonyesha na pengine faida za mtoto (kwa mfano, ukingaji dhidi ya maambukizi, virutubishi mwafaka, upunguzaji wa hatari ya aleji), na faida kwa mama (kunyonyesha ni nafuu, husaidia uterasi kurudi hali yake ya kawaida, ni muhimu kwa upangaji uzazi, na kadhalika). Lakini pia mwambie hatari ya kuambukiza VVU kwa mtoto kupitia unyonyeshaji.

Wakati utajadili kuhusu maziwa ya kutengenezwa kama njia mbadala, elezea umuhimu mkubwa wa maji safi na ufisha viini kwenye chupa na chuchu, vile vile haja ya kupima kila kitu kwa ufasaha ili mtoto apate lishe sahihi.

Kisha kupitia kigezo cha IKGES (Inayokukubalika, Kuwezekana, Gharama nafuu, Endelevu na Salama) na maswali katika mchoro 7.4. Kama atajibu 'ndiyo' kwa yote, mhimize atumie maziwa ya kutengenezwa au ya wanyama, na pia mshauri kuhusu upangaji wa uzazi. Kama atajibu 'la' na anataka kabisa kunyonyesha, mweleze jinsi anaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa kunyonyesha kwa vipindi vifupi (sio zaidi ya saa tatu), na awache kunyonyesha kutoka titi lina chuchu lenye mpasuko. Mkumbushe kuangalia kinywa cha mtoto kama kuna vidonda, na kutafuta matibabu ya haraka kwa ajili yake na mtoto wake iwapo mmoja wao atakuwa mgonjwa.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 7.2 (Malengo ya Somo la 7.2)

Kati ya fasili zifuatazo ni gani isio sahihi? Katika kila hali, toa fasili sahihi.

  • A.Unyonyeshaji wa kipekee ni kunyonyesha mtoto mmoja kwa wakati.
  • B.Kukaa vizuri unaponyonyesha ni wakati mama amekaa kwa ustarehe.
  • C.Ushikiliaji mzuri ina maanisha kuwa mtoto 'amejaza titi kinywani vizuri'.
  • D.Unyonyeshaji wa mapema inahitaji mama kuamka karibu alfajiri kwa ajili ya lishe ya kwanza.
  • E.Kanuni ya mfululizo joto inamaanisha kwamba unachopatia kipaumbele ni kumpatia mtoto joto wakati wote, ili aepukane na hipothemia.
Answer
  • A.Si kweli: Unyonyeshaji wa kipekee ni kutompea mtoto kitu kingine chochote bali maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza.
  • B.Kweli. Lakini angalia nyuma katika sehemu ya 7.1.1 na uangalie kuwa unafahamu jinsi ya kudumisha mama katika hali nzuri.
  • C.Kweli: Angalia nyuma katika sehemu ya 7.1.2 na uangalie kama unakumbuka ishara nne za ushikiliaji nzuri.
  • D.Si kweli: Unyonyeshaji wa mapema ni uanzaji wa unyonyeshaji katika saa moja baada ya kuzaliwa.
  • E.Kweli: Kanuni ya mfululizo joto inamaanisha kuchukua hatua za kumpatia mtoto joto wakati wote.

Mwisho wa jibu

Maswali ya kujitathmini 7.3 (Malengo ya Somo la 7.5)

Unapomtembelea mama aliyezaa kwa mara ya kwanza na ugunduwe kuwa mtoto anahisi baridi sana. Una wasiwasi kuhusu hipothemia. Utafanya nini?

Answer
  • Weka mtoto mchanga ngozi-kwa-ngozi na mama, wafunike wote wawili na mablanketi yaliyo na joto, weka kofia au kitambaa juu ya kichwa cha mtoto na mvalishe soksi au umfunike miguu.
  • Pima kiwango cha halijoto ya mtoto na kama iko chini ya sentigredi 37.5 pima tena baada ya nusu saa. Kama halijoto haitapanda kwa haraka, mpee mtoto rufaa haraka.
  • Wakati unasubiri kuona ikiwa mtoto anapata joto, Fanya uchunguzi wa kawaida ni kwa nini mtoto yuko baridi. Uliza mama kama mtoto alikuwa ameloa au hajalishwa hivi karibuni, au ikiwa anamlisha akiwa uchi. Angalia kama chumba kina madirisha wazi au ikiwa mtoto yuko kwa upepo.
  • Mwelezee mama jinsi watoto wachanga wanavyopoteza joto (njia muhimu imewekwa kwa muhtasari katika sehemu ya 7.4.3) na humweleza umuhimu wa kumpatia mtoto joto kila wakati.
  • Mwambie vipengele vya mfululizo joto. Ikiwa hutaka kumbuka angalia tena katika Jedwali 7.2.

Mwisho wa jibu