Ruka hadi kwa yaliyomo
Printable page generated Alhamisi, 2 Mei 2024, 19:39
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Alhamisi, 2 Mei 2024, 19:39

Namba ya moduli 2: Kutumia Sauti za Kijumuia Darasani Kwako

Sehemu ya 1: Kuchunguza hadithi

Swali Lengwa muhimu: Je, unawezaje kutumia uchunguzi kuendeleza mawazo juu ya hadithi?

Maneno muhimu: utafiti; hadithi; lengo; maswali; kuchunguza; jumuia

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • kutumia njia za utafiti na uchunguzi katika kuendeleza mazoezi ya darasani mwako;
  • kuchunguza welewa wa wanafunzi juu ya hadithi;
  • kuchunguza njia za kutunga hadithi mpya.

Utangulizi

Usimuliaji wa hadithi ni sehemu muhimu ya maisha na utamaduni wa jamii nyingi. Moduli hii inachunguza jinsi ya kuimarisha uhusiano baina ya shule na jamii kwa kutumia jamii na hadithi zake kama rasilimali ya kujifunza.

Sehemu hii inakufahamisha juu ya umuhimu wa utafiti katika kufundisha na kujifunza. Kwa kuandaa shughuli za utafiti, utaweza kupata majibu kwa maswali yako, kujaribu mawazo mapya na kisha kuyatumia katika kuunda kazi mpya halisi.

Somo la 1

Sote husimulia hadithi, kuhusu maisha yetu ya kila siku au yaliyopita.We all tell stories, about our daily lives or about the past. Kuna desturi nyingi katika usimuliaji hadithi na mafundisho mengi kutoka kwenye hadithi. Shughuli 1 talii kutafiti ni nini, unafanywaje, na matokeo yanaweza kuchanganuliwa. As you work alongside the class on the task, utajifunza ni nini wanafunzi wako wanakiweza.

Tunashauri usome Nyenzo-rejea muhimu: Kuchunguza darasani kabla ya kuanza. Kama ungependa kusoma tafiti za watu wengine, Nyenzo-rejea 1: Ngano za kimapokeo pia ni nzuri, inatoa taarifa juu ya warsha iliyofanyika Qunu mashariki ya rasi ya Afrika-kusini, ambapo wazazi, walimu na wanafunzi walijadili maswali unayotafiti.

Uchunguzi kifani ya 1: Kutafiti ni kwa nini watu husimulia hadithi

Bibi Rashe na wanafunzi wake wa darasa la 3 katika shule ya Nqamakwe, mashariki mwa rasi ya Afrika kusini husimulia hadithi kila siku.

Siku moja aliandika swali ubaoni ‘Kwa nini watu husimulia hadithi?’ na kuorodhesha majibu ya wanafunzi:

Kufurahisha

Kuogopesha watu

Kunifundisha nisifanye jambo fulani.

Alimuomba kila mwanafunzi aende nyumbani na kumuuliza mtu mzima swali hilo hilo na kuleta majibu. Alihakikisha kwamba amewakumbusha wanafunzi kuwa wanatakiwa kuwakabili watu kwa unyenyekevu pindi wanapouliza maswali. Pia aliwakumbusha kuelezea vipi taarifa zingetumika.

Siku iliyofuata aliongezea majibu yao kwenye orodha. Pale ambapo watu zaidi ya mmoja walitoa jibu sawa aliongeza alama (√) (angalia Nyenzo-rejea 2: Kwa nini watu husimulia hadithi ).

Aliwaomba wanafunzi kuongeza tiki kwa kila sababu. Walijadili maswali yafuatayo:

Sababu zipi ni maarufu sana? Umejuaje? Unakubaliana na mawazo ya wakubwa? Kwa nini ndio/hapana? Baada ya majadiliano, Bibi Rashe aliwaomba wanafunzi wake waandike wamepata nini kutokana na utafiti wao.Siku iliyofuata, aliwaomba wanafunzi wachahe wenye mawazo tofauti kusoma ripoti zao. Alikuwa akishangazwa na kufurahishwa na mawazo tofauti ambayo wanafunzi walikuja nayo.

Shughuli ya 1: Kuchunguza usimuliaji hadithi

Waeleze wanafunzi kuhusu utafiti, tumia Nyenzo-rejea muhimu: Kuchunguza darasaniikusaidie kupanga unachotaka kusema. Waeleze kuwa watakusaidia katika kuchunguza usimuliaji wa hadithi (angali Nyenzo-rejea muhimu: Kuelezea na kuonesha darasani)

Andika maswali ubaoni kutoka katika Nyenzo-rejea 3: Maswali kuhusu hadithi .

Eleza kuwa kila mwanafunzi ataenda kuuliza maswali haya kwa mtu mzima mmoja miongoni mwa jamii. Wakumbushe pia kuwakabili watu wazima kwa heshima na kurekodi majibu watakayopewa.

Siku kadhaa baadaye, wagawe wanafunzi katika makundi ya watu sita mpaka nane na waache waorodheshe (kwa kila swali) majibu waliyoyapata; ongeza alama ya tiki kwa jibu lililotolewa na mtu zaidi ya mmoja.

Sasa kila kundi liripoti, na wewe kumalizia seti ya data (taarifa zilizokusanywa na darasa) ubaoni.

Jadili mawzo yaliozoeleka sana. Je, wanafunzi wanakubaliana nayo?

Wasaidie wanafunzi kuandika ripoti rahisi kuhusiana na walichokipata (angalia Nyenzo-rejea 2 kwa mpango wa ripoti ya utafiti).

Somo la 2

Unapokuwa na matokeo ya utafiti, yanatakiwa yatafsiriwe ili uweze kutumia taarifa. Katika mfano wetu, hii ina maana kuwasaidia wanafunzi wako kutumia taarifa iliyopatikana kuelewa hadithi zaidi. Shughuli 2 inakusaidia kutalii maana katika hadithi kama ufuatiliaji baada ya uchunguzi.

Uchunguzi-kifani 2 inatambulisha wazo muhimu la kuwasaidia wanafunzi kutunga maswali yao wenyewe na kujaribu kuyatafutia majibu. Kuweza kuuliza maswali yao wenyewe katika makundi madogo huwajengea fikra huru na hukuza uwezo wa wanafunzi wa kufikiri kiubunifu na kwa makini.

Uchunguzi kifani ya 2: Kumalizia hadithi

Bibi Mwenda kutoka Dodoma alifanya utafiti makini katika vipengele vya hadithi nzuri ambayo haifahamiki sana (angalia Nyenzo-rejea 4: Namna Bibi Mwenda alivyopata hadithi yake ).

Siku moja aliwakusanya wanafunzi wake wa darasa la 2 kumzunguka, na aliwasimulia sehemu ya kwanza ya hadithi (aya tatu za mwanzo za Nyenzo-rejea 5: Mto ambao ulifagilia mbali waongo ). Baadaye, aliwaomba kila mmoja afikirie swali juu ya kingetokea nini katika sehemu iliyobaki ya hadithi. Baada ya dakika mbili walimpa maswali yao, na aliyaandika ubaoni.

Aliomba darasa kufikiria majibu ya maswali, kuchukua swali baada ya swali. Wanafunzi walitoa sababu za majibu yao.

Baada ya kuyapitia maswali na majibu yote, aliwaomba kumsaidia kuandika mwisho wa hadithi. Wallipendekeza nini kingeweza kutokea baadaye na aliyaandika maoni yao ubaoni. Hakukurupua mchakato, au kulazimisha mawazo yake kwa wanafunzi.

Pale hadithi ilipokuwa imekamilika, waliisoma kwa pamoja.

Wanafunzi walipenda kushughulika pamoja kwenye hadithi. Siku iliyofuata, katika watu wawili wawili, walichora picha za sehemu mbalimbali za hadithi. Hizi ziliwekwa pamoja katika kitabu.

Mwisho, Bibi Mwenda aliwasomea hadithi yenyewe. Wanafunzi walifurahishwa na mwisho wa hadithi zao ikilinganishwa na mwisho wa hadithi halisi na walizungumza mengi juu ya matatizo ya kusema uongo.

Shughuli ya 2: Kujadili kwa nini hadithi maalumu husimuliwa

Chagua hadithi nzuri kutokana na unazozijua. Hakikisha una masimulizi kamili ya hadithi.

Andaa nakala moja kwa kila kikundi katika darasa lako, au uandike hadithi ubaoni, mahali ambapo wanaweza kuiona wote.

Pia andika sababu za kusimulia hadithi zilizotokana na utafiti wa darasa.

Wambie wanafunzi wako kujadili katika makundi kwanini wanafikiri watu wangewasimulia hii hadithi (k.v lengo lake).

Kadri makundi yatoavyo ripoti, waambie waeleze sababu zao. Kasha, jadili wahusika wa hadithi na tabia zao.

Waulize wanafunzi ni jinsi gain wangeweza kutumia hadithi hii katika maisha yao wenyewe.

Waambie, katika makundi, kujadili lengo la hadithi nyingine, labda moja kutoka nyumbani na kasha kuandika aya juu ya lengo la hadithi.

Je, wote walielewa malengo ya hadithi zao? Umelijuaje hili?

Hii shughuli haihitaji kumalizwa kwa muda wa somo wa dakika 30. inaweza ikaendelea katika vipindi vya somo jingine kama wanafunzi wako wana mambo mengi ya kujadili.

Somo la 3

Utafiti unaonesha kuwa watu hujifunza vizuri pale ambapo kile kilichokuwa kikifundishwa ni muhimu kwao. Ukiwa kama mwalimu daima unatakiwa kuhakikisha kuwa wanafunzi wako wanapata maarifa ambayo yatawasaidia kuuelewa ulimwengu wao.

Wewe na darasa lako mmetafiti ni kwa nini watu husimulia hadithi na mmeangalia maana ya hadithi maalum. Sasa tunaangalia ni jinsi gain unaweza kuwasaidia wanafunzi wako kutumia usimuliaji wa hadithi katika hali ya maisha halisi na kwenye matatizo.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuandika hadithi

Bibi Kaniki alitaka kuwasidia wanafunzi wake wa darasa la 6 pale Arusha kuandika hadithi zao wenyewe katika vikundi vya watu wawili wawili. Aliandika orodha ya sifa yamkini za hadithi (angalia chini) ubaoni na alizijadili na wanafunzi wake jinsi sifa hizo zinaweza kuabiri aina ya hadithi inaandikwa.

Wanyama wanawakilisha binadamu

Matukio ya ajabu, viumbe visivyo vya kawaida

Mtu kupata matatizo na kutafuta njia ya kuyatatua

Mwema na muovu

Maelezo ya jinsi vitu vilivyo

Pia aliwapa orodha ya matukio, mazuri na mabaya, yaliyotokea mjini hivi karibuni na alipendekeza watumie moja ya matukio haya kama muktadha wa hadithi zao. Baadaye , aliwaambia wachague ikiwa wahusika wa hadithi zao wangekuwa ni watu au wanyama. Mwisho, aliwauliza dhamira wangechagua, kama vile vita kati ya wema na uovu. Walipokuwa wamshaamua dhamira, aliwapa moyo kila kikundi cha watu wali kuanza kuandika.

Baada ya wiki moja au mbili, Bibi Kaniki aliliambia kila kikundi kuchangia (mawazo) ya hadithi na darasa zima, halafu walijadili lengo la hadithi lilikuwa lipi. Aliridhishwa na aina anuai za hadithi.

Shughuli muhimu: Kutunga hadithi mpya (halisi)

Waambie wanafunzi wafikirie matatizo katika familia zao, shule na jamii ambayo hutokana na jinsi wanavyotendeana. Matatizo yangeweza kuanzia yale ya kila siku, kama uvivu hadi mambo mazito, kama vile virusi vya UKIMWI na UKIMWI. Ungeweza kuwachochea kwa kueleza hali za kawaida zinazohusisha baadhi ya aina za tabia, lakini kuwa makini na hali binafsi za wanafunzi katika darasa lako. Ungeweza kutumia magazeti kusaidia kupata mawazo ya hadithi.

Kila kundi lichague tatizo moja na kulitungia hadithi ambayo inaonesha athari za aina hii ya tabia na kutoa busara juu ya tabia hiyo.

Jadili baadhi ya sifa za hadithi kabla hawajaandika hadthi zao au panga jinsi gain wataisimulia (angalia Uchunguzi-kifani 3 ).

Waambie kila kundi kusimulia hadithi zao darasani. Jadili lengo la kila hadithi, yaorodheshe, na yalinganishe na matokeo ya utafiti wao kutoka Shughuli 1.

Waache wanavikundi wajiamulie kama hadithi yao ilifanikiwa na kwa nini (Angalia maswali katika Nyenzo-rejea 6: Kuikadiria hadithi yako .)

Kwa kiasi gani walifanikiwa kujikadiria?

Je, unakubaliana na makadirio yao?

Kama una wanafunzi wadogo, ungeweza kufanya zoezi hili kama shughuli ya darasa zima ambapo unaandika mawzo yao ubaoni au kwenye karatasi.

Nyenzo-rejea ya 1: Ngano za kimapokeo

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Usuli

Warsha iliendeshwa kama sehemu ya kazi za kitengo cha maendeleo na kisomo vijijini cha mfuko wa Nelson Mandela na shule tano kutoka eneo la Qunu mashariki mwa rasi zilishiriki. Kutoka kila shule kulikuwa na walimu wawili na mwanafunzi mmoja na mzazi mmoja na mjumbe mmoja wa kamati ya shule.

Lengo la warsha lilikuwa ni kuakisi pamoja juu ya thamani ya ngano za kimapokeo katika elimu ya watoto na jamii, na kupanga njia za kutumia hadithi hizi ndani na nje ya shule.

Kifuatacho ni ripoti ya majadala uliokuwa ukiendeshwa katika makundi katika siku ya kwanza ya warsha. Washiriki walitoa mawazo yao.

Je, unakubaliana na mwazo na maoni yao?

Ngano ni nini?

Ngano ni hadithi fupi zenye lengo maalum, zina baadhi ya mafundisho, ucheshi, maonyo. Husifu, hukosoa na hurekebisha. Hunoa ubongo kuufanya ufikiri kwa makini na hujenga ufikiriaji wa kina. Baadhi ni matukio halisi ambayo baadaye hubadilishwa kuwa ngano; baadhi zimekuwa zikitungwa maalum kwa dhamira ya kuchoma au kuumiza ili kuachana na matukio yaliopita na kufundisha staha.

Ni watu gain husimulia au husimuliwa ngano?

Kwa kauli moja walisema ni watu wazima- bibi na babu, pia watoto wenyewe kwa wenyewe, kipindi cha mafunzo ya jando na unyago. Pia walimu, watangazaji wa redio na luninga husimulia hadithi.

Waliwasimulia/huwasimulia nani?

Zilisimuliwa kwa watoto, vijana na watu wazima.

Lini na wapi ngano zinasimuliwa/zilisimuliwa?

Chumba cha kupumzikia mara nyingi hutumika, wakati mwingine chumba cha kulala na mara nyingine hadithi zilisimuliwa wakati wakiota jua karibu na maboma ya ng’ombe. Seheme nyingine zilikuwa kingo za mito, malishoni, viwanja vya nyumba na kwenye kumbi za jando na unyago.

Kwa nini walisimuliwa/ wanasimuliwa hadithi?

Zilikuwa kwa ajili ya kufurahisha, kunoa ubongo, kama kikumbushi, kama katazo au onyo, kuchochea uzalendo kupitia tabia fulani, kutupa msamiati na vitatanishi vyake (kama tamathali za usemi, nahau, methali na maneno mapya ambayo huingia kwenye kamusi).

Wanasimuliwaje/ walisimuliwaje hadithi? (mtindo wa usimulizi)

Kulikuwa na mashindano katika usimuliaji wa hadithi. Ilikuwa sanaa, iliyohusisha muziki, ucheshi na kubadili sauti. Ngano za kimapokeo zina mwanzo na mwisho wa pekee.

Hadithi mpya husimuliwa kama zinavyosimuliwa hadithi za zamani? Kwa sababu zipi hadithi mpya hutungwa ?

Ngano za zamani na mpya zimekuwa zikitumika, na hufanya kazi moja.

Kwa kawida, hadithi mpya hujumuisha maeneo yote mpya za maisha.

Je, una masimulizi ya ngano yalioandikwa? Yataje.

Kuna ngano za zamani chache zilizo katika maandishi ( Baadhi zimetajwa)

Kilichokuwa kimeonekana ni kwamba ngano chache sana zilikumbukwa na kundi na haikuwa kazi rahisi kufanya hivyo.Mtu mmoja pekee alikumbuka tatu, baadhi hawakuweza kukumbuka yoyote. Kutokana na washiriki 23, ngano 19 tu zilitolewa. Hii inamaanisha nini?

Wapi na kwa namna gain ngano zilizoandikwa hutumika?

Ngano husomwa kutoka vitabuni mara kwa mara. Ndicho kinachotokea nyumbani ambapo ngano zile zile hurudiwa kusimuliwa kwa kujifurahisha. Shuleni husomewa watoto. Zina mchango kwa msamiati wa watoto. Ni chache. Kuna baadhi katika maktaba na wakati mwingine huigizwa jukwaani.

Lugha inayotumika

Lugha iliyozoeleka ni lahaja, lugha za kitoto pia hutumika, vile vile maneno yalioundwa kuonesha staha

Dondoo limendondolewa kutoka ripoti ya warsha juu ya ngano za kimapokeo iliyofanyika Qunu, Rasi ya Mashiriki.

Nyenzo-rejea ya 2: Kwa nini watu husimulia hadithi

Mfano wa kazi za wanafunzi

Ubao wa Bibi Rashe

Ni kwa nini watu husimulia hadithi?

kufurahisha √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ 35

kuogopesha watu √√√√√ √√ 7

kunifundisha kutofanya jambo fulani √√√√√ √√√√√ 10

kufundisha busara juu ya maisha √√√√√ √√√√√ √√√√ 14

kuonesha tabia sahihi, √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√√√√ √√ 32

kukuza lugha yetu, √√√√√ √√ 7

mpango wa ripoti ya utafiti

Swali la utafiti

Tulifanya nini

Tunachambuaje data

Tulipata nini

Ripoti juu utafiti wa hadithi

Wanafunzi wa darasa la 3 waliwauliza watu wazima: ‘Kwa nini watu husimulia hadithi?’

Watu wazima wapatao 35 walilijibu swali hilo.

Wanafunzi waliandaa orodha ya majibu, na walihesabu watu wangapi walijibu kila swali.

Kifani cha ripoti

Watu 34 walidhani kuwa hadithi husimuliwa kwa ajili ya kuwafurahisha wasikilizaji.

Watu 32 walidhani kuwa hadithi husimuliwa ili kuonesha tabia nzuri/sahihi.

Watu 14 walidhani kuwa hadithi husimuliwa ili kufundisha busara katika maisha.

Watu 10 walidhani kuwa hadithi husimuliwa ili kufundisha watu kutofanya jambo fulani.

Watu 7 wao walidhani hadithi husimuliwa ili kukuza lugha.

Watu 7 walidhani kuwa hadithim husimuliwa ili kuogofya watu.

Nyenzo-rejea ya 3: Maswali kuhusu hadithi

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

  1. Ni watu gani ambao kwa kawaida husimulia hadithi?
  2. Wanawasimulia nani?
  3. Wapi na lini hadithi husimuliwa?
  4. Kwa nini watu husimulia hadithi?
  5. Husimuliaje hadithi? (mtindo wa usimulizi)
  6. Je, hadithi mpya pia husimuliwa kama zinavyosimuliwa za zamani ? Ni sababu zipi zinazopelekea kutungwa kwa hadithi mpya?

Nyenzo-rejea hii ni nzuri kwa matumizi ya wanafunzi wakubwa. Kwa wanafunzi wadogo ungeweza kuwa na hiyari ya kuchagua swali moja au mawili kati ya haya kwa ajili wanafunzi wako kuchunguza.

Nyenzo-rejea ya 4: Namna Bibi Mwenda alivyopata hadithi yake

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Patricia Mwenda alijaribu kutafakari juu ya hadithi ambayo haikutambulika sana. Aliikumbuka nahau iliyorandana na hadithi yake. Nahau yenyewe ilisema: ‘Hakuna mbweha aliye mkubwa kuliko mwingine, mbweha wote wana umbo sawa.’ Alikumbuka kuwa hadithi ilikuwa juu ya Bwana na mtumishi wake waliokuwa wakisafiri juu ya farasi, na yule mtumishi alimsimulia Bwana wake juu ya hadithi ya mbweha aliyekuwa na umbo la ndama au maksai. Bibi Mwenda alikumbuka pia kulikuwa na mito ipitayo, na mmoja wapo uliitwa ‘mto unao somba waongo wote’. 

Alipokuwa hana uhakika na nini haswa kilijiri, alimuuliza wifi yake aitwaye Amina juu ya hadithi. Amina alimwambia kuwa, mtumishi yule alikuwa muongo sana. Hapo zamani alijaribu pia kusimulia hadithi ya kunguni kumfananisha na kitu kikubwa sana, hadithi ambayo haiwezi kuwa kweli. Bado walikuwa na tondoti chache, hivyo walikwenda kwa Bwana Majengo ambaye aliyewahi kuwa mwalimu wa Kiswahili, kwa sasa ni mkaguzi wa shule. Hakuweza kukumbuka hadithi, lakini alikumbuka kuwa tafsiri yake ipo kwa msomaji maalum.

Siku moja, Patricia alikuwa akiongea na Bi. Kolisa Ngodwana, mwalimu wa hisabati, aligundua kuwa alifamu ujumbe uliopo kwenye hadithi. Alisema kwamba yule Bwana alitumia mbinu fulani kumsimamisha yule mtumishi kudanganya. Hakutaka kumshutumu moja kwa moja kwa uongo. Bi. Ngodwana alisema kuwa mbinu zile zilifanikiwa, kwani mtumishi alitubu na kuzungumza kabla ya kufika mtoni. Lakini Bw. Ngodwana pia hakuweza kukumbuka tondoti za hadithi yote.

Kisha Patricia alikwenda kwa Bw. Mr Hintsa Siwisa, mwanasheria. Alijua nahau na ujumbe wa hadithi. Alifikiri ilitokana na jamii kuchoshwa na uongo wa mtu yule. Waliamua kumuweka kwenye jaribio la nguvu na kumpa somo. Masimulizi ya hadithi ya Bw. Siwisa ipo kwenye Nyenzo- rejea 5: Mto uliofyagilia mbali wa waongo.

Imenakiliwa kutoka: Umthamo 2, University of Fort Hare Distance Education Project

Nyenzo-rejea 5: Mto uliofagilia mbali waongo

Nyenzo ya mwalimu kwa ajili ya mpango au utohozi utakaotumiwa na wanafunzi

Bwana mmoja alikuwa safarini na mtumishi wake. Ilikuwa ni safari ndefu juu ya farasi. Kadri walivyokuwa wakisafiri, yule Bwana aliona mbweha akikatiza kwenye njia.Yule Bwana alisema: ‘Mbweha yule ni mkubwa sana.’ Yule mtumishi akajibu, ‘Oh, Bwana huyu si chochote ukilinganisha na niliyemuona jana.’ ‘Ndivyo hivyo?’ alidakia yule Bwana. ‘Oh! Ndiyo, Alikuwa mkubwa sana sana. Kwa hakika alikuwa mkubwa kama maksai!’ ‘Mkubwa kama maksai?’ Bwana aliuliza. ‘Ndiyo mkubwa kama maksai,’ alijibu mtumishi. Bwana akasema tena, ‘Umesema “ni mkubwa kama maksai”?’ ‘Ndiyo haswa, mkubwa kama maksai,’ alisema mtumishi. Yule Bwana hakusema neno waliendelea na safari yao, bila kusemezana takribani kwa muda wa saa moja.

Mtumishi alibaini kuwa Bwana wake hakuwa na raha na hukujua ni nini kilimsumbua. Kwa hiyo alimuuliza alikuwa na jambo gani. Yule bwana alimwambia kwamba wangevuka mito minne kabla ya kufika mwisho wa safari yao. Mto wa mwisho ni mkubwa na hatari zaidi kuliko yote. Mto huu ulikuwa na mzio na waongo na hakuna mwongo angeweza kuepuka hasira yake. Iliwazoa waongo huku na huko hadi kwenye kina kirefu cha bahari ya bluu. Haikuwahi kumkosa mwongo hata kama wakimuomba ‘Ifa’ awaletee bahati (watu humuomba Ifa awaletee bahati, na kuwapa nguvu ya kuwashinda pepo waovu).

Mtumishi aliposika hivi, alitishika sana kwa sababu alijua uwezo aliokuwa nao Ifa. Kama mto huu usingeshindwa na Ifa, basi alijua wazi kuwa ni lazima utakuwa ni mto wenye nguvu SANA. Kwa kadri walivyokuwa wakiendelea na safari ndivyo alivyoendelea kukosa utulivu. Bwana wake naye aliendelea kukasirika sana. Na jinsi anavyoendelea kukasirika ndivyo mtumishi wake alivyoendelea kushikwa na hofu na hofu kubwa.

Wakati walipokwa wanaukaribia mto mmoja baada mwingine, ndivyo umbo la mbweha nalo lilivyokuwa likipungua. Walipoukaribia mto wa kwanza, mtumishi alisema, ‘Bwana wangu, mbweha si mkubwa kabisa kama maksai, ni mdogo kidogo kuliko maksai.’ Bwana hakusema kitu chochote.

Walipoufikia mto wa pili, mtumishi alisema , ‘Mbweha hata hakaribiani kwa umbo na maksai. Ni mkubwa kama ndama.’ Lakini yule Bwana, akaendelea kukaa kimya. Walipovuka mto wa pili yule Bwana alieleza jinsi anavyojisikia kuhusiana na ule mto hatari wa mwisho na hakusema kitu tena.

Walivyoukaribia mto wa tatu, mtumishi alimwambia Bwana wake, ‘Mbweha sio mkubwa kama ndama. Ni mkubwa kama mbuzi.’

Kabla tu hawajakaribia mto wa mwisho, mbweha alikuwa na umbo sawa na mbweha wengine, ambao hupatikana kila sehemu.

Imenakiliwa kutoka: Umthamo 2, University of Fort Hare Distance Education Project

Nyenzo-rejea 6: Kukadiria hadithi yako

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Maswali

  1. Darasa lilifurahia hadithi yako?
  2. Umejuaje ?
  3. Darasa limejifunza kitu kutokana na hadithi yako?
  4. Hadithi yako inatoa ujumbe wake vizuri?
  5. Umejuaje?

Sehemu ya 2: Njia za kukusanya na kutenda hadithi

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia utendaji katika kukuza stadi za lugha za wanafunzi wako?

Maneno muhimu: hadithi; kusanya; kuigiza; kujiamini; uhodari; heshima; urithi wa utamaduni

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kufanya kazi na jumuia yako katika kukuza /kujenga stadi za lugha na heshima katika urithi wa utamaduni;
  • Kupanga na kusimamia nafasi za utendaji mbele ya hadhira.

Utangulizi

Matumizi ya mazoezi mbalimbali ya mdomo yanaweza kukuza kujiamini kwa wanafunzi katika kuzungumza na kusikiliza na kuwajengea heshima katika lugha zao za nyumbani. Jambo hili litakuwa na athari chanya katika kujistahi. Wanafunzi wanaojiamini na kujitambua wataweza kujifunza kwa wepesi zaidi.

Uigizaji katika sehemu hii unatoa nafasi kwa wanafunzi wako katika kukusanya, kukariri na kusimulia hadithi mbele ya hadhira. Inapendekezwa kwamba, ufanye kazi na wanajumuia wenye umri mkubwa kwa kuomba msaada wao katika kusimulia hadithi na kubadilishana ujuzi katika kusimulia hadithi. Shughuli hizi zitajenga umahiri katika lugha za nyumbani, ambapo baadaye unaweza ukajenga stadi za kujifunza lugha nyingine.

Somo la 1

Ujuzi wa hadithi kwa wanajumuia ni nyenzo muhimu katika mazoezi ya kusikiliza na kuzungumza nje na ndani ya darasa. Ni muhimu wanafunzi wajifunze kuheshimu na kupenda busara na urithi wa lugha zao za nyumbani na tamaduni zao. Kwa kuimarisha stadi zao za kuzungumza na kusikiliza lugha za nyumbani kwa njia inayofurahisha, wanafunzi watakua katika hali ya kujiamini pia.

Kwa kuwa sanaa ya kusimulia hadithi haipewi thamani katika baadhi ya jumuia, watu wanaweza kuwa wamesahau baadhi ya tondoti na thamani za hadithi. Njia ya kujenga Nyenzo-rejea lugha kwa wanafunzi wako ni kuweka wazi matoleo ya zamani na halisi ya hadithi. Unaweza kufanikisha jambo hili kwa kuzungumza na watu wengine katika jumuia.

Uchunguzi kifani ya 1: Matumizi ya lugha nyingi za wanafunzi wako darasani

Bwana Kimaryo hufundisha darasa la 4 katika shule ya msingi Makanya iliyopo nchini Tanzania. Shule ipo karibu na shamba la mkonge, ambapo wafanyakazi huzungumza lugha nyingi mbalimbali. Katika darasa lake lenye wanafunzi 70, wanafunzi 10 wanazungumza Kichaga, wanafunzi 6 wanazungumza Kirundi, wanafunzi 3wanazungumza Kinamwanga na waliobakia wanazungumza Kipare. Kwa kawaida yeye huzungumza Kiswahili anapowafundisha

Bwana Kimaryo aliwataka wanafunzi wake kukusanya hadithi toka majumbani mwao na kuwajengea hali ya kujiamini katika kuzungumza kwa kusimulia hadithi kwa kutumia lugha zao za nyumbani. Alianza somo lake kwa kuwaonesha wanafunzi picha ya mtu wa makamo na baadhi ya wanafamilia waliokuwa wamekaa pembezoni mwa moto. Kisha akawataka wanafunzi wawili wawili kujadili watu hawa wanafanya nini. Vikundi viliwasilisha majibu yao darasani. Kisha akawauliza wanafunzi kama na wao hukaa pembezoni mwa moto na kusikiliza hadithi, wengi waowalisema hawafanyi hivyo. Aliwataka wanafunzi waende nyumbani na kumuomba mtu mmoja wa makamo awasimulie hadithi.

Katika somo lililofuata, aliwaganya wanafunzi katika vikundi. Aliunda vikundi viwili vya wazungumzaji wa Kichaga, kikundi kimoja cha wazungumzaji wa Kirundi, na kikundi kimoja cha wazungumzaji wa Kinamwanga. Aliwagawanya wazungumzaji wa Kipare katika vikundi kumi. Akamtaka kila mwanafunzi asimulie hadithi yake kwa wanakikundi wenzake kwa kutumia lugha ya nyumbani.

Bwana Kimaryo alizunguka katika vikundi na kusikiliza namna wanafunzi walivyokuwa wakisimulia hadithi. Alifurahia sana namna walivyokuwa wakisimulia hadithi, hususani namna walivyokuwa wakitumia sauti zao kuongeza mvuto.

Shughuli ya 1: Kusimuliana hadithi kwa kutumia lugha za nyumbani

Katika sehemu ya 1,wanafunzi wako wameshabaini mbinu muafaka ya kusimulia hadithi toka kwa wazee wao. Huu sasa ni wakati muafaka kwa wao kukusanya hadithi toka kwao.

Zungumza na wanafunzi wako kuhusiana na uzoefu wao katika kusikiliza hadithi na kubaini ni aina gani ya hadithi wanazozifurahia. Waulize kama wanasikiliza hadithi nyumbani na akina nani husimulia hadithi katika jumuia zao.

Waagize wamtafute mtu mmoja toka katika jumuia zao za nyumbani ili awasimulie hadithi. Watatakiwa kuwa na kumbukumbu za hadithi hizi, kwa sababu watahitajika kuwasimulia wenzao darasani. Njia nzuri ya kujifunza hadithi ni kwa wao kuwasimulia watu mbalimbali nyumbani. Kadiri watakavyokuwa wanafanya hivi, watatakiwa kuzingatia kuwa wana taarifa zote muhimu za hadithi.

Katika somo lijalo, waweke pamoja wanafunzi wenye lugha za nyumbani zinazofana (tazama Nyenzo-rejea muhimu: Tumia kazi ya kikundi katika darasa lako). Waagize wasimuliane hadithi walizokusanya kwa kutumia lugha zao za asili.

Je wanafunzi wako wamepokea vipi shughuli hii?

Je unaweza vipi kujenga utashi katika hadithi hizi?

Somo la 2

Kuwaalika wanajumuia darasani kutasaidia katika kuwahamasisha wanafunzi na kuwajengea ustadi katika kusimulia hadithi kwa kutumia lugha zao za asili. Unaweza pia ukawataka wageni wako kutumia ujuzi wao wa hadithi ili kuhakikisha kwamba hadithi zinazosimuliwa na wanafunzi ni za kweli na zenye kujitosheleza kadiri iwezekanavyo. Hii itamaanisha kwamba hadithi zitakuwa nyenzo za msingi ya kujifunzia.

Kama una darasa kubwa, aina hii ya uungwaji mkono na jumuia inasaidia sa Kuomba kuungwa mkono na mkuu wako wa shule na walimu wenzio kutalifanya jambo hili kuwa katika msingi unaoeleweka.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuwaalika wanajumuia katika siku wanajumuiya

Walimu wanne wa shule ya msingi ya Mtakatifu Maria iliyopo Dar es Salaam wameandikishwa katika programu ya kuwaendeleza walimu. Moja ya moduli katika programu hii, inawataka kuchunguza ni kwa namna gani Nyenzo-rejea zinazowazunguka zinaweza kutumika darasani. Walifanya kazi ya kukusanya maboksi, chupa, mimea na nyenzo nyingine na kuzitumia katika mazoezi ya sayansi, hesabu na lugha.Hata hivyo, moduli ziliwakumbusha kuwa watu ni nzenzo muhimu kwa ajili ya kujifunzia.

Ilipendekezwa kuwa wapange siku ya kuwakutanisha pamoja wanafunzi na wanajumuia wanye umri mkubwa kwa lengo la kubadilishana maarifa na ujuzi.

Siku ambayo walimu hawa wanne waliipanga, ilikuwa na mafanikio makubwa. Bibi Rwakatare, mwenyekiti anayeongoza bodi ya shule, alielezea historia ya shule. Baadhi ya wanajumuia walioshiriki walionesha kwa vitendo stadi mbalimbali kama vile,ususi wa vikapu,ukaushaji wa tumbaku, na kutengeneza shanga,.wanawake walisifika kwa kutoa maelezo kuhusu mapishi ya vyakula vya asili. Wazee mbalimbali, wanaume kwa wanawake walisimulia ngano.

Kisha ikafuata zamu ya wanafunzi kuonesha kwa vitendo mambo waliyojifunza shuleni. Siku ilimalizika kwa kuimbwa nyimbo na dansi toka katika vikundi mbalimbali.

Kutokana na shughuli za siku hii, wanajumuia mbalimbali wakawa wanatembelea shule mara kwa mara. Walitoa ujuzi wao katika stadi mbalimbali na pia walisimulia hadithi ambazo baadaye zilitumiwa darasani.

Shughuli ya 2: Mafunzo toka wanajumuia ‘mahiri’

Utatakiwa kupangilia vema shughuli hii mapema na kutenga muda wote wa asubuhi au mchana kwa ajili ya shughuli hii.

Wapange wanafunzi wako katika vikundi kulingana na lugha zao za nyumbani. Waagize kila kikundi kualika mtu mmoja toka katika jumuia zao kuja darasani ili kuwasaidia wanafunzi katika ustadi wao wa kusimulia hadithi. Wape kila kikundi barua ya mwaliko waendenayo nyumbani. (tazama Nyenzo-rejea 1: Mfano wa barua ya mwaliko ).

Waagize wanajumuia wajiunge na kikundi na kusikiliza wanafunzi wakiwa wanasimulia hadithi siku hiyo. Waombe wageni waalikwa wawape wanafunzi muongozo na ushauri juu ya namna ya kuboresha hadithi na masimulizi yao.

Kipindi cha mafunzo kikimalizika, vikundi vinaweza kukaa pamoja na kusikiliza hadithi kutoka kwa wageni waliowaalika. Nyimbo, mashairi na vitendawili vinaweza vikatolewa siku hiyo.

Je, ushirikishwaji wa wanajumuia umeongeza nini katika ujifunzaji darasani mwako?

Je umefurahia namna ulivyopangilia shughuli zako?

Je utafanya nini cha tofauti wakati ujao?

Somo la 3

Ni muhimu kila mwanafunzi awe na uwezo wa kuwasiliana vema na kuwa kuwa anapewa nafasi ya kuwa mbunifu.Uwasilishaji wa hadithi katika vikundi unatoa nafasi hata kwa wanafunzi wakimya kuzungumza, kuimba, kutenda,kucheza n.k bila ya shinikizo. Kila mwanafunzi katika uigizaji wa hadithi anaweza kupata nafasi ya kuwa muhusika katika hadithi, msimuliaji ama kuwa sehemu ya kiitio. Wanafunzi wenye vipaji maalum wanaweza wakaandaa ‘vifaa’ na ‘mavazi’ wakiwa na vitu kama vipande vya nguo ama karatasi ama matawi ya mti.

Katika madarasa ambapo wanafunzi wote hawazungumzi lugha moja ya nyumbani, kufanya kazi na wazungumzaji wa lugha inayofanana kwa lengo la kuandaa uigizaji katika lugha hii kunaweza kuwa na matokeo bora.

Sehemu inayofuata inakupa njia ya kukuza kujiamini na stadi kwa wanafunzi katika lugha zao za nyumbani. Njia hizi pia zinaweza zikatumika katika kuimarisha stadi katika lugha ya mawasiliano ama lugha ya ziada.

Uchunguzi kifani ya 3: Siku ya kuigiza hadithi katika darasa kubwa

Bibi Rebecca Kassam hufundisha darasa la tano lenye wanafunzi 100, katika kijiji kilichopo karibu na Tanga Kaskazini mwa Tanzania. Aliamua kuwa na siku ya kuigiza hadithi mwisho wa muhula. Aliwapanga wanafunzi wake katika vikundi vya watu watanowatano na kisha kuwahimiza sio tu wasimulie hadithi bali pia waigize, hivyo, waigizaji na hadhira kwa pamoja wataweza kufurahia. Aliwaeleza wanafunzi kwamba kama watataka kuigiza katika lugha ambayo si kila mtu anaifahamu, hawana budi kuamua kuisaidia hadhira kuelewa maana inayokusudiwa kwa kutumia vitendo, ishara na vitu mbalimbali.

Bibi Kassam huwapa wanafunzi wake muda wa kuandaa na kukariri hadithi zao. Wanapokuwa wanafanya kazi hii husimamia maendeleo yao na wakati mwingine huweza kufupisha ama kurefusha muda wa maandalizi. Alibaini kuwa wanafunzi wanapendelea kuandaa na kuigizia kazi zao nje.

Kwa wanafunzi 80, itachukua muda mrefu kama makundi yote yataigiza darasani. Katika siku ya kuigiza hadithi, Bibi Kassan huwaagiza wanafunzi waunde maduara manne ambapo kila duara linakuwa na makundi manne. Huyapa namba makundi katika kila duara kuanzia 1-4. Kikundi cha 1 huigiza katikati ya duara kwa ajili ya kikundi cha 2,3 na 4, kisha kikundi cha 2 huigiza kwa ajili ya kikundi cha 1,3,na 4 na kuendelea hadi makundi yote yamalize mzunguko

Baada ya uigizaji, Bibi Kassam, hukitaka kila kikundi kujadili juu ya kile walichojifunza. Hufikiri juu ya kile ambacho mwanafunzi mkimya darasani mwake alichoonesha kuhusu uelewa wake wa siku ile na namna anavyoweza kutumia taarifa hizi kuandaa hatua nyingine ya kujifunzia.

Nyenzo-rejea muhimu: Kufanyakazi na madarasa makubwa na/au madarasa ya viwango mbalimbali inatoa mawazo ya ziada kwa ajili ya kufundishia madarasa makubwa.

Shughuli muhimu: Kuigiza hadithi kwa ajili ya hadhira

Waagize wanafunzi kujigawa katika vikundi vya watu sita sita. Waagize wanafunzi ::

Kukumbuka kuhusu hadithi walizosimulia na kusikiliza

Kuamua ni hadithi ipi wanadhani itakuwa bora kuigizwa kwa ajili ya darasa ambapo kila mmoja ataweza kuelewa na kuifurahia. Kikundi zaidi ya kimoja kinaweza kuchagua hadithi ileile.

Wateue wahusika wote na kuamua kila nafasi itachukuliwa na nani. Watahitaji pia kuwa na msimuliaji.

Toa maamuzi juu ya lugha (z)itakayotumika, athari za sauti, matumizi ya ishara,mavazi, na vitu vitakavyosaidia kuipa hadithi uhai na nani ataleta Nyenzo-rejea zipi.

Wape muda wa kukariri na kuweka muda maalum kwa ajili ya uigizaji. Simamia kila kikundi na kuwasaidia kadiri inavyowezekana kwa kutoa mawazo na mapendekezo juu ya njia ya kufanya kazia.

Itake hadhira kutoa kuleta mwitikio kwa kila kikundi. ( Tazama Nyenzo-rejea 2: Tathmini uigizaji wa hadithi katika vikundi ).

Kama utaweza, rekodi hadithi zitakazoigizwa.Vinginevyo chukua dondoo kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Hadithi zinaweza kuigizwa mbele ya wazazi na viongozi wa jumuia katika eneo lako kwa lengo la kukusanya michango kwa ajili ya kununulia nyenzo za darasa lako.

Nyenzo-rejeaya1: Mfano wa barua ya mwaliko

Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kutohoa na kutumia na wanafunzi.

Mpendwa …………………

Darasa letu la …… linajifunza kuhusu hadithi za asili na stadi za kusimulia hadithi. Tumesikia kuhusu ubingwa wako na tunapenda kukukaribisha kuja na kutusaidia kujifunza ni namna gani tunaweza kukuza stadi zetu za kusimulia na kujifunza hadithi pia.

Tungependa uje …………………………………. Tafadhali tujulishe kama muda huu ni mwafaka kwako. ………………………………… kutoka katika darasa letu atakusubiri geti la shule saa 4.00 asubuhi.

Tunashukuru sana

Darasa la 5

Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maria

Nyenzo-rejea ya 2: Tathmini uigizaji wa hadithi za vikundi

Matumizi ya mwanafunzi

Sifa ya uigizajiVizuri sanaVizuriWastaniDhaifu
Hadithi ya kufurahisha na rahisi kufuatilia.
Matumizi ya sauti mbalimbali
Matumizi ya athari za sauti
Matumizi ya miondoko
Matumizi ya mavazi na/au vifaa

Watu wa Afrika Mashariki wakiigiza hadithi

Vyanzo vya asili: Two Help; Website.

Sehemu ya 3: Kutumia michezo ya jadi katika kujifunza

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia michezo ya jadi ili kusaidia ujifunzaji wa lugha?

Maneno muhimu: kutafakari; utafiti; michezo ya jadi; mapokeo; mashairi; nyimbo; kuchunguza

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia michezo ya jadi na ya mahali husika katika kusaidia shughuli za ujifunzaji;
  • umewahamasisha wanafunzi na kuongeza ujasiri wao wa kutumia lugha kwa njia ya michezo, nyimbo na mashairi;
  • umepanua stadi zako mwenyewe katika kutafakari wajibu na uwezo wako kwa kuchunguza thamani ya michezo katika ujifunzaji.

Utangulizi

Baadhi ya walimu ambao wamefundisha kwa miaka 20 ni kama tu wanakuwa na uzoevu wa mwaka mmoja tu, ambao unarudiarudia. Hii ni kwa sababu hawajifunzi tena kwa bidii au hawajiendelezi ili waweze kuwa walimu bora zaidi.

Walimu wazuri ni wale ambao wanapanga kile wanachotaka kukifanya, na mara wanapokifanya, wanarekodi kilichotokea, na kujiuliza wenyewe mafanikio ni yapi na ni wapi panahitaji kuboreshwa. Wanatafakari endapo wanafunzi wamejifunza chochote, na kama wamejifunza, wamejifunza nini? Kwa msingi huu wa ‘tafakari’, wanapanga tena kwa ajili ya shughuli inayofuata. Nyenzo rejea 1: duara la tenda-tafakari huonesha mchakato huu katika muundo wa kielelezo.

Somo la 1

Watoto hawajifunzi tu wakiwa darasani, wanajifunza pia wakiwa wanacheza. Wanajifunza kutoka kwa wengine, kwa kuangalia kile wanachokifanya wengine. Hujifunza kwa kuzungumza, kuimba, kwa kukariri na kwa kushirikishana katika mazungumzo. Unaweza kutumia mchezo ili kufanya ujifunzaji katika darasa lako uwe wa mafanikio na kuziba uwazi kati ya kinachotokea darasani na nje ya darasa.

Katika Shughuli 1, wanafunzi wako wanakuwa kama watafiti, na wanakwenda kwenye uwanja wa michezo (au mahali pengine) ili kurekodi kile wanachofikiri kuwa wataweza kujifunza pale. Wanaporudi darasani wanazungumzia kile ambacho wamekigundua: Unaweza kusikiliza mazungumzo yao ili kuona kile ambacho unafikiri wanafunzi wako wamejifunza uwanjani hapo.

Uchunguzi kifani ya 1: Mwanafunzi wa miaka sita ajifunza na kufundishaKiswahili

Maria ambaye ana umri wa miaka sita anasoma katika shule ambayo

Kiswahili ni lugha inayotumika darasani, ingawa si lugha yake ya kuzaliwa.

Kila siku kwa muda wa wiki nzima, Maria aliweza kuonekana wakati wa mapumziko akiwaangalia watoto wengine wakiruka kamba. Hakujiunga, lakini alisimama karibu ili kuweza kuona na ‘kusikiliza’ wimbo ambao wanafunzi walikuwa wakiuimba. Siku ya kwanza ya wiki ya pili, Maria alikuwa kwenye ile sehemu yake ya kawaida hatua chache kutoka eneo la kuchezea, lakini sasa aliweza kusikika ‘akitoa sauti’ za maneno ya kwenye wimbo.

‘Ruu-ka, ruuu-kia ndani na seeema

Moja-aa mbili-iii, tatuuu,

Ruuu-kia na-a mimi.’

Alirudia maneno haya tena na tena, akijitahidi kuyasema kwa sauti kubwa, kwa wororo na kwa kutumia mkazo tofauti tofauti kwenye sehemu za neno. Alirudia wimbo huu mara kadhaa na kisha kuwasikiliza tena wanafunzi wengine. Alitabasamu, na kuimba tena ule wimbo.Mwishoni alitafuta kamba na kwenda kwa rafiki yake, Migueli. Aliimba ule wimbo, mstari kwa mstari, akimfundisha rafikiye huu wimbo. Alitafsiri yale maneno ya Kiswahili ili rafiki yake aweze kuelewa alichokuwa akijifunza. Kwa muda mfupi Migueli aliweza kuimba wimbo ule pamoja na Maria.

Shughuli ya 1: Kuchunguza ujifunzaji wa asili

Kabla ya kuanza shughuli hii, soma Nyenzo Rejea 2: Utafiti juu michezo ya jadi katika mtalaa . Nyenzo rejea hii inaeleza kazi moja ya utafiti na micezo miwili ambayo walimu waliibuni kama matokeo ya utafiti huo. Kusoma pia Nyenzo Rejea Muhimu: Kufanya utafiti darasani kutasaidia sana. Zungumza na wanafunzi wako kuhusu ujifunzaji. Je, wanajua kwamba daima hujifunzia: nyumbani, shuleni, wakati wanapocheza?

Liambie darasa lifanye uchunguzi katika ujifunzaji wa ‘asili’. Swali lao ni: Ujifunzaji gani unaotokea wakati watoto wanapocheza? Wanafunzi lazima waandike na kuchora kuhusu ujifunzaji wanaouona kwenye uwanja wa michezo na baada ya kutoka shule, wakati wanafunzi wengine wanapocheza, na wanapocheza wao wenyewe.

Wwaambie wanafunzi darasani washirikishane matokeo yao, kwenye vikundi. Kiambie kila kikundi kioneshe jinsi ya kucheza mchezo mmoja. Rekodi nyimbo au mikarara/viitikio wanavyoimba wakati wa mchezo, kwenye tepu, au kwa kuandika.

Waambie wanafunzi kwenye kila kikundi wajadili kile ambacho wanaweza kujifunza kutokana na michezo hii. Andika mawazo yao.

Umejifunza nini kutokana na shughuli hii inayohusu namna michezo inavyoweza kusaidia katika ujifunzaji?

Somo la 2

Aina zote za michezo zinaweza kutumika kwa kujifunzia na unahitaji kufikiri kiubunifu jinsi ya kuitumia michezo darasani (angalia Shughuli 2). Inasaidia kama unaweza kushirikiana na wenzako pamoja na rafiki zako, na pia kushirikiana na wanafunzi wako, katika kubuni mawazo mapya ambayo yanaweza kufanya ujifunzaji darasani kwako uwe wa kufurahisha na wenye mafanikio.

Katika sehemu hii, wewe na darasa lako panueni utafiti wenu kwa kuwauliza wanajumuiya kuhusu michezo waliyokuwa wanaicheza walipokuwa wadogo.

Uchunguzi kifani ya 2: Michezo na mikarara/viitikio katika kadi za kusoma

Kuna ongezeko la kupenda lugha nyingi za nyongeza katika mitalaa kote Afrika. Hii ina maana kuna ujifunzaji wa awali unaotumia lugha mama, na lugha nyingine za nyongeza (bila kuchukua nafasi ya ile lugha mama). Mtalaa unalenga kuingiza lugha zote ambazo watoto wanazijua wakati wa masomo yao.

Bwana Maleke mkoani Lindi hutumia shughuli ifuatayo, ambayo hujumuisha lugha nyingi za nyongeza, pamoja na wanafunzi wake wa darasa la 5. Humpatia kila mwanafunzi kipande cha kadi. Wanafunzi huchora picha katika upande mmoja wa kadi. Kwa upande mwingine, huandika nyimbo, michezo, mikarara/viitikio au mashairi, ambayo wanayapata nyumbani.

Kila siku, wana kipindi cha kusoma ambapo wanafunzi wanasoma (au wanaimba!) kile kilichoandikwa kwenye zile kadi. Wakati mwingine, msomaji bora husoma kadi na msomaji anayesoma polepole zaidi. Wakati mwingine, mzungumzaji wa lugha moja, humsaidia mwanafunzi mwingine kusoma lugha yake na kuingiza sauti. Wakati mwingine, wanaigiza hayo mashairi au wanacheza michezo hiyo. Bwana Maleke amegundua jinsi darasa lake linavyokuwa na furaha na jinsi wanafunzi wanavyoshirikiana vizuri katika mazungumzo na wanavyochanganyika vizuri zaidi tangu waanze kufanya hivi.

Shughuli ya 2: Michezo na nyimbo kutoka kwa wanajumuiya ambao ni watu wazima

Waambie wanafunzi wako wamwombe mtu mzima (mzazi, babu/bibi, jirani n.k.) awafundishe mchezo, wimbo au mkarara ambao walikuwa wakiufurahia wakati wa utotoni. Wanatakiwa wajue kanuni za maneno na nyenzo zozote ambazo zinahitajika.

Siku inayofuata, orodhesha michezo na nyimbo ambazo wanafunzi wamezileta toka nyumbani.

Waweke pamoja wanafunzi wanaojifunza mchezo au wimbo wa aina moja. Waambie wajiandae kufundisha darasa mchezo au wimbo huo.

Waambie waandike huo wimbo au huo mkarara au wacheze mchezo wa kwenye kadi.

Darasa litakapomaliza kujifunza mchezo au wimbo huo, jadilianeni kitu ambacho wanaweza kujifunza kutokana na mchezo au wimbo huo. Andika tini kama ulivyofanya hapo awali.

Kwa masomo yatakayofuata, wahamasishe wanafunzi wasome magazeti ili kutafuta nyimbo, michezo, vitendawili na mizaha kama msingi wa kuandika vitu vyo wenyewe.

Somo la 3

‘Kuakisi’ ni kutafakari juu ya kile kilichotokea na kuona jinsi ya kufanya vizuri zaidi wakati mwingine. Baada ya kuwa umejaribu shughuli mpya, inasaidia sana kuakisi/kutafakari juu ya mafanikio na kitu gani kinahitaji maboresho. Fanya mchakato wa ‘Panga-Tenda-Rekodi-Tafakari’ kuwa sehemu ya mazoea yako ya kila siku (angalia Nyenzo Rejea 1 ).

Sasa una mkusanyiko mzuri wa michezo, unaweza kuitumia michezo hii kama msingi wa shughuli za ujifunzaji, na kama msingi wa kuakisi/kutafakari na uboreshaji. (kazi hii pia inaweza kufanywa kwa kutumia hadithi.)

Nyenzo Rejea 3: Michezo ya maneno ina michezo kadhaa ambayo unaweza kuijaribu pamoja na wanafunzi wako.

Uchunguzi kifani ya 3: Vitenzi vya Kiswahili katika wimbo wa kurukaruka maneno

Bi Alison aliimba wimbo wa kurukaruka maneno wakati alipokuwa mtoto pale Mazimbu, Morogoro. Aliamua kuutumia wimbo huo kufundishia wanafunzi wake wa darasa la 2 maneno kadhaa na virai vya wakati uliopo vya Kiswahili.

Kwanza wanafunzi waliuimba kwa Kiswahili na kisha aliwasaidia kuuimba kwa Kiingereza.

Alimpatia kila mwanafunzi kipande cha karatasi chenye kitenzi (m.f. la, nywa, cheka, kohoa, ruka, kimbia, rukaruka) kilichoandikwa kwenye karatasi hiyo. Alihakikisha kuwa kila mtoto anafahamu maana ya neno hilo na jinsi ya kufanya vitendo vinavohusiana na neno hilo.

Alimwambia kila mwanafunzi mmoja mmoja afanye vitendo bila maneno, na darasa liliimba ubeti mpya: ‘Antoni, msichana huyu anafanya nini? Antoni, msichana anacheka,’ n.k.

Baada ya somo, alitafakari kuhusu:

Kile kilichokwenda vema;

Kile ambacho hakikwenda vema sana;

Kile kilichomshangaza;

Kile ambacho angekibadili kama angerudia lile somo.

Bi Alison alishangazwa na jinsi wanafunzi walivyoutumia muda katika kujifunza toleo la Kiswahili lakini pia jinsi wanafunzi waliufurahia muda. Aliona kuwa alihitaji kutumia muda zaidi katika shughuli hii, na pia kufundisha maneno machache zaidi.

Wiki iliyofuata, alitumia toleo la aina nyingine la Kiswahili lililokuwa na wimbo wa kurukaruka maneno kwa jinsi ile ile, ya kutunga beti zenye aina mbalimbali za vyakula.

(Angalia Nyenzo Rejea 4: Wimbo wa kurukaruka maneno kutoka katika wimbo wa kurukaruka maneno wa Igbo.)

Shughuli muhimu: Kujifunza kutokana na mkarara, wimbo au mchezo

Je, kuna mkarara kwenye makusanyo ya darasa lako ambao lugha yake inaweza kubadilishwa na kuwa kama lugha ya nyongeza na kuweza kutumiwa katika kuhamasisha ujifunzaji wa lugha?

Bainisha sentensi katika mkarara ambayo neno (au maneno) yangeweza kubadilishana nafasi kwa zamu. Kwa mfano, ‘Anacheka’ lingeweza kubadilishana nafasi na (Anaruka, anarukaruka, anakimbia’ n.k.). Kila mwanafunzi, au kikundi, kinaweza baadaye kuimba ubeti mpya, wenye neno jipya katika sentensi ya mwanzo.

Ingeweza hata kufurahisha zaidi kama maneno au sentensi yataweza kuambatana na vitendo.

Panga jinsi utakavyopanga darasa lako kwa ajili ya kuimba/ kukariri na kuigiza (zoezi hili ni mbadala’. (Huu ni mfululizo wa sentensi, ambazo zinafanana isipokuwa kwa neno au kishazi kimoja. Sentensi hizi zinatumika kufanya mazoezi ya mitindo ya lugha.)

Kama hutafanikiwa, utatakiwa kujaribu wimbo mwingine, au njia nyingine ya kuendesha shughuli hii.

Nyenzo-rejea ya 1: Duara la tenda - tafakari

Nyenzo-rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kutohoa na kutumia na wanafunzi.

Mpendwa …………………

Darasa letu la …… linajifunza kuhusu hadithi za asili na stadi za kusimulia hadithi. Tumesikia kuhusu ubingwa wako na tunapenda kukukaribisha kuja na kutusaidia kujifunza ni namna gani tunaweza kukuza stadi zetu za kusimulia na kujifunza hadithi pia.

Tungependa uje …………………………………. Tafadhali tujulishe kama muda huu ni mwafaka kwako. ………………………………… kutoka katika darasa letu atakusubiri geti la shule saa 4.00 asubuhi.

Tunashukuru sana

Darasa la 5

Shule ya Msingi ya Mtakatifu Maria

Nyenzo-rejea ya 2: Tathmini uigizaji wa hadithi za vikundi

Usuli/welewa wa somo wa mwalimu

Kielelezo kinaonesha hatua zifuatazo katika mduara wa tenda- Akisi/Tafakari:

Panga shughuli. 

Tenda kwa kuweka mpango katika vitendo, na chunguza unavyoendelea.

Rekodi kile unachokiona.

Akisi/Tafakari juu ya kilichotokea. 

Pitia tena mpango wako, au andaa mpango mpya.

Weka mpango uliopitiwa tena au mpango mpya katika vitendo, na angalia tena.

Rekodi na tafakari tena.

Na kadhalika, na kadhalika …

Kila kitu unachokifanya kama mwalimu kinaweza kuwa sehemu ya mduara wa

Tenda -Tafakari.

(Angalia pia Nyenzo Rejea Muhimu: Kufanya utafiti darasani)

Nyenzo rejea 3: Utafiti juu ya michezo ya jadi katika mtalaa

Usuli/welewa wa somo wa mwalimu

Nonhlanhla Shange alifanya utafiti katika Shahada yake ya Uzamili katika Kitengo cha Usomeshaji wa Vijijini cha Nelson Mandela katika Chuo Kikuu cha Fort Hare nchini Afrika Kusini. Alitafiti kuhusu utumizi wa michezo ya jadi darasani, utafiti ambao aliufanya katika shule nne za vijijini.

Wanafunzi na walimu wao walifanya utafiti wa vitendo katika michezo ya jadi.

Walimu walisikiliza kwa makini na waliandika tini za michezo ambayo wanafunzi waliileta darasani. Walijaribu kutayarisha masomo yanayohusu michezo hii. Wanatunza juzuu, ambamo huwekwa kumbukumbu za masomo haya, na kujaribu kufanya maboresho kwa ajili ya matumizi ya baadaye.

Maelezo ya michezo miwili ambayo ilichezwa kama sehemu ya utafiti huu ni haya yafuatayo hapa chini.

1. Mchezo wa duara

Matayarisho ya mchezo huu yanajumuisha uchoraji wa kielelezo kama hiki hapa chini ambacho huchorwa ardhini.

Mchezo unachezwaje?

Mchezo huu unachezwa kwa vikundi vidogo vya wanafunzi watano watano au sita sita. Mwanafunzi mmoja anarukia ndani ya nafasi za duara, akigeuka upande hadi upande, wakati wanafunzi wengine wakiimba wimbo mfupi au shairi fupi, kwanza kwa lugha ya asili, na kisha kwa Kiswahili.

Shughuli gani za ujifunzaji zilizohusiana na mchezo huu?

Mchezo ulibuniwa ili kuonesha ni jinsi gani kurudia rudia kwa kutumia lugha ya wanafunzi wenyewe na lugha ya Kiswahili kunavyoweza kusaidia katika kujifunza. Kwa kutumia wimbo mfupi au shairi, mchezo huu pia uliweza kutumika katika kuwafundisha wanafunzi kuhesabu.

2. Mcezo wa mawe

Matayarisho kwa ajili ya mchezo hujumuisha uchoraji wa duara chini ardhini na kuweka idadi fulanii ya mawe kwenye duara hilo. (duara lisizidi kipenyo cha mita moja.)

Mchezo unachezwaje?

Wanafunzi wanagawanywa katika vikundi vya watano watano au sita sita. Kila kikundi kinakuwa na duara lake lililochorwa ardhini na kuwekwa mawe ndani yake.

Mchezaji anarusha jiwe moja juu; kabla halijatua ardhini, lazima wajaribu kuokota mawe mengine ndani ya duara.

Kila mwanafunzi katika kikundi lazima ajipe namba mwenyewe (chini ya 10). Namba hii ni idadi ya mawe ambayo mchezaji atajaribu kucheza na kuokota.

Mchezaji mmoja anaingia kwanza. Kama mchezaji huyu ataokota idadi ya mawe inayotakiwa kutoka kwenye duara, wanasema orodha ya kuzidisha ya namba hii (kwa mfano, orodha ya 3 ya kuzidisha, wanakomea kwenye 30 – hii inaweza kuwa ni ya chini kwa wanafunzi wadogo zaidi).

Kama mchezaji atashindwa kuokota idadi inayotakiwa ya mawe kutoka kwenye duara, watapaswa kuzidisha idadi ya mawe waliyookota kwa idadi ya mawe ambayo walipaswa kuokota, na kupata jibu sahihi. Kwa mfano, kama walitakiwa kuokota mawe hadi 5, lakini wakaokota mawe 3 tu, watatoa jibu sahihi la 5 x 3.

Wachezaji wengine watapima/watajaji endapo wametoa jibu sahihi au jibu ambalo si sahihi.

Shughuli gani za ujifunzaji ambazo zinahusishwa na mchezo huu?

Mchezo huu ulitumiwa ili kuwafanyia wanafunzi mazoezi ya ’ stadi’ za kuzidisha.

Chanzo cha Asilia: Shange, N., Kitengo cha Mfuko wa Nelson Mandela wa Usomeshaji na Maendeleo ya Vijijini [ utafiti haujachapishwa ] Nelson Mandela Foundation’s Unit for Rural Schooling and Development [unpublished research]

Nyenzo rejea 4: Michezo ya maneno

Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Michezo hii inaweza kuchezwa kwa kutumia lugha yoyote na kwa umri wowote, ilimradi tu wanafunzi wanajua vizuri stadi za kusoma na kuandika.

Mchezo 1: Bingo

Wasomee wanafunzi hadithi wanayoipenda na waambie wachague maneno mawili wanayoyataka.

Mwulize kila mwanafunzi maneno yao na andika maneno muhimu ubaoni ambapo kila mmoja ataweza kuona.

Ligawe darasa katika vikundi vya wanafunzi sita sita na kiambie kila kikundi kichague maneno 12 kwa ajili ya kikundi chao. Haya yanaweza kutofautiana kwa kila kikundi.

Kila mwanafunzi atengeneze karatasi ya bingo kwa kuchora mraba mkubwa uliogawanyika katika miraba midogo tisa (angalia mfano hapa chini).

Mwambie kila mwanafunzi achague maneno yoyote tisa kutoka kwenye orodha yao ya maneno 12 na kuyanakili katika karatasi yao ya bingo, neno moja kwa kila mraba. Makaratasi ya wanafunzi yatakuwa tofauti, kwa sababu wataweza tu kuchagua maneno tisa kati ya maneno 12.

Mwanafunzi mmoja atakuwa na karatasi kuu yenye maneno 12. Watatoa maneno bila mpangilio maalum. Neno linavyotajwa kila mwanafunzi ambaye atakuwa na neno hilo katika karatasi ya bingo atatakiwa kulikata. Wa kwanza kukata maneno yake yote atapiga kelele ‘Bingo’ na atakuwa ameshinda.

Kiache kila kikundi kicheze tena na kila mwanafunzi apate zamu ya kutaja maneno.

Kama unataka kutumia karatasi ya bingo zaidi ya mara moja, waambie wanafunzi wazibe maneno hayo kwa mawe au vihesabio wakati wa kutaja maneno.

Je, wanafunzi walijifunza maneno mapya? Unajuaje?

Orodha ya Sampuli ya maneno kwa ajili ya Bingo:

Ndizi

Maharage

Kabeji

Mihogo

Nazi

Punje za mahindi

Maembe

Mahindi

Machungwa

Mapapai

Mapeasi

Spinachi

Viazi vitamu

Mifano miwili ya kadi za bingo:

Mchezo 2: Maneno yanayohusu supu

Tengeneza orodha ya maneno tisa, mf. sehemu za mwili, vyumba vya nyumba, au mboga za majani. Weka orodha hii ubaoni (pembeni mwa picha toa maelekezo ya maneno kama unaweza).

Mpatie kila mwanafunzi kipande cha karatasi cha mraba, herufi moja kwa kila mraba. Waambie waingize maneno muhimu katika karatasi hiyo kwenye miraba hiyo, herufi moja kila mraba mmoja. Waambie kuwa maneno yanaweza kutoka kushoto kwenda kulia, au juu mpaka chini. Waambie wanafunzi wajaze miraba ya ziada kwa herufi zozote zile za alfabeti. (Angalia mfano hapa chini).

Kila mwanafunzi akishafanya hivi, kusanya makaratasi yote na yachanganye. Sasa wagawie wanafunzi makaratasi hayo bila mpangilio maalum, na waambie wanafunzi wazungushie maneno yote wanayoweza kuyapata. Kila mwanafunzi anajua lazima maneno yawe tisa. Wa kwanza kumaliza ndiye mshindi.

Wanafunzi wanaweza baadaye kuchagua somo lao wenyewe au eneo lao wenyewe na maneno yanayohusu supu kutoka kwenye orodha hii na kumpatia rafiki acheze.   

Mfano wa maneno yanayohusu supu

Maneno ya kutafuta kwenye maneno ya supu

Mbuzi Ngamia
Simba Twiga
NyokaNyani
Chui Farasi

Unaweza kufanya shughuli hii iwe ya kusisimua zaidi kwa kuwauliza ‘Neno gani ambalo LINALOHUSIKA katika supu?’ Unaweza kutumia mchezo huu kwa maneno mengi mbalimbali na kwa masomo mbalimbali.

Kiolezo wazi kwa ajili ya maneno ya supu ni hiki hapa chini. Unaweza kuongeza miraba zaidi au kuifanya iwe midogo zaidi ili kufanya mchezo uwe mgumu zaidi au mrahisi zaidi kutegemeana na umri na uwezo wa wanafunzi wako.

Nyenzo Rejea 5: Wimbo wa kurukaruka maneno

Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Wimbo wa Kiigbo wa kurukaruka maneno

Ikuku buru gi

Zamiriza

Buru gi buru nwa nnegi

Zamiriza

Nwa nnegi idobere na ukwu osisi kporonku

Chọ ya ịhuyi ya (2x)

Tafsiri ya Kiswahili

Acha upepo ukupeperushe

Zamiriza

Ukupeperushe wewe na mdogo wako wa kike

Zamiriza

Yule mdogo wako wa kike yupo chini ya mti wenye matawi yote yenye kivuli

Unamtafuta mdogo wako huyo, huwezi kumpata (x2)

Sehemu ya 4: Utumizi wa hadithi na ushairi

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kutumia ushairi na hadithi kuhamasisha wanafunzi ili waandike?

Maneno muhimu: jina; sifa; mashairi; hadithi; wasifu, uandishi

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umetumia mashairi au hadithi za majina au za kusifu ili kuchochea mawazo ya wanafunzi ya uandishi;
  • umetumia Nyenzo-rejea kama vile makala za kwenye magazeti ili kuchochea mawazo ya uandishi wa hadithi za maisha (wasifu);
  • umetalii ‘uandishi wa rasimu ’ na ‘uandishi wa kisanaa’ wakati wa kuandika.

Utangulizi

Afrika nzima, tuna utajiri wa fasihi simulizi na fasihi andishi kuhusu watu ambao bado ni muhimu au hapo zamani walikuwa muhimu kwa familia zao, jumuiya zao na nchi zao. Watu hawa hushangiliwa kupitia nyimbo na mashairi ya kuwasifu na hadithi zinazohusu maisha yao (wasifu). Kwa kutumia utajiri huu wa historia ya kitamaduni katika ufundishaji wako kunaweza kukusaidia ili kujua vitu vya kusoma kwa ajili ya lugha itakayotumika darasani na kuamsha mvuto wa wanafunzi katika uandishi.

Somo la 1

Kama wanafunzi wanasikiliza na kusoma mashairi na hadithi wanazozifurahia, ni rahisi sana wakapenda kuendeleza stadi zao za usomaji na uandishi kwa kutumia lugha zao za asili au lugha wanayoitumia darasani.

Ili kuwa waandishi wenye mafanikio, wanafunzi wanahitaji ‘zana’ mbalimbali. Kwanza, wanahitaji mada ya kuandikia. Katika Shughuli ya 1, utatumia mifano ya mashairi ya majina au ya kusifu au hadithi ili kuwapatia wanafunzi mawazo. Kisha utawaongoza katika kuandika rasimu ya kwanza ya shairi la majina au la kusifu au hadithi. Hii ina maana kwamba itabidi kuandika matoleo kadhaa ya rasimu, ambayo yatazidi kuboreshwa, mpaka watakaporidhika kuwa shairi au hadithi zao ni nzuri na wanaweza kutoa toleo la mwisho.

Uchunguzi kifani ya 1: Kusoma na kuandika mashairi ya majina na hadithi katika warsha ya mwalimu

Katika warsha ya siku nne mjini Johannesburg nchini Afrika Kusini, baadhi ya walimu wa Kiingereza/Kiswahili walisoma mashairi na hadithi kuhusu majina. Katika warsha hii, waandishi walieleza jinsi walivyopata hayo majina yao, kitu walichokipenda au ambacho hawakukipenda kuhusiana na majina yao na maneno ambayo yalihusiana na majina hayo. Kwa kweli walimu walifurahia kile walichokisoma na kuomba iwapo wangeweza kupatiwa nafasi ya kuweza kuandika mashairi au hadithi zinazohusu majina yao wenyewe wakati wa warsha.

Siku ya pili, kila mwalimu alimsomea mwenzake rasimu yake ya kwanza. Walipeana majibu ya kile walichokipenda na kile ambacho walifikiri kinafaa kiboreshwe, kwa mfano kwa kuongeza maelezo na kuchagua msamiati tofauti au alama za uakifishi.

Siku ya nne, wakiwa wameshafanyia kazi rasimu zao siku moja kabla, kila mmoja alikisomea kikundi kizima shairi au hadithi ambayo ilikuwa imekamilika. Kulikuwa na kicheko, kulikuwa na machozi na kulikuwa na makofi mengi.

Walipoambiwa waakisi uzoefu wao, walisema:

  • hakuna mtu aliyekuwa ‘amekwama’ kuhusiana na kitu/mada ya kuandikia;

  • wakati wengi wao waliandika kwa Kiingereza, walifurahia mara kadhaa kutumia maneno au virai vya Lugha ya Kiafrika ili kueleza wazo fulani;

  • walinufaika na matokeo ya rasimu zao za kwanza; walijisifu sana kutokana na toleo la mwisho; walifurahia kusikiliza hadithi/mashairi ya wengine;

  • mengi ya mashairi yalikuwa yanafanana na yale mashairi na zile nyimbo za jadi za kusifu.

Walimu waliamua kuwasomea wanafunzi mashairi na hadithi zao pamoja na mashairi na hadithi nyinginezo za majina katika kuwasaidia ili waweze kuandika kuhusu majina yao.

Shughuli ya 1: Kuandika rasimu ya mashairi au hadithi za majina

Ili kupata mawazo jinsi ya kuandaa shughuli hii, tumia Nyenzo-rejea 1: Kuandaa masomo juu ya mashairi ya majina au ya kusifu na Nyenzo-rejea 2: Mashairi na hadithi za majina au Nyenzo-rejea 3: Mashairi na hadithi za kusifu. Chagua ama mashairi/hadithi za majina au mashairi/hadithi za kusifu.

Waambie wanafunzi wapendekeze shairi/hadithi ya majina au shairi/hadithi ya kusifu itahusu nini.

Waambie wasikilize wakati wewe ukiwa unasoma shairi (ma)/hadithi uliyoandaa kwa sauti.

Waulize maswali kuhusu kile ulichowasomea.

Waambie wanafunzi wajadiliane na wenzao ama kuhusu kile wanachokijua kuhusu jina hili ulilowasomea, au kile wanachokijua kuhusu mtu, mnyama au kitu wanachotaka kukisifia.

Baadaye, waambie baadhi ya wanafunzi watoe ripoti ya mjadala wao darasani.

Waambie wanafunzi waandike rasimu ya kwanza ya shairi au hadithi kuhusu wao wenyewe au wanafamilia au kumsifu mtu, mnyama au kitu watakachokichagua.

Kusanya rasimu ili kutayarisha Shughuli Muhimu.

Je, kuandika mashairi/ hadithi za majina au za kusifu kunawapa wanafunzi mawazo ya kuandika?

Uliridhika na jinsi ulivyoendesha somo? Utafanya marekebisha gani wakati ujao?

Ukiwa na watoto wadogo zaidi, unaweza kuandika mashairi ya majina kwa pamoja, mkishirikishana mawazo na kutumia maneno yaliyozoeleka katika lugha inayotumika darasani.

Somo la 2

Baadhi ya hadithi za kwanza wanazozisikia watoto ni zile ambazo zinahusu uzoefu wa maisha ya familia au wanajumuiya. Hadithi za maisha ya watu mashuhuri (wasifu wao) mara nyingi huchapishwa katika magazeti na hata katika muundo wa vichekesho, hivyo, kama wanazisikia au wanazisoma, wanafunzi wengi watakuwa wana fununu juu ya hadithi kuhusu maisha. Huu ni mwanzo mzuri ili kuamsha hamasa ya kusoma na kuandika.

Darasani, wanafunzi wanahitaji msaada kutoka kwa mwalimu wao na kutoka kwa wenzao wakati wanapojifunza kuzungumza, kusoma na kuandika –hasa kama lugha hii ni ya nyongeza. Uchunguzi Kifani 2 na Shughuli 2 zinaonesha jinsi unavyoweza kuwapatia wanafunzi fursa ya kusoma, kuzungumza, kufanya kazi pamoja katika vikundi vidogo na kuandika rasimu za kwanza za hadithi za maisha ya watu wanaowapenda.

Wanafunzi wanahitaji mifano ili kuwaendeleza kama waandishi. Makala wanazozisoma zinaweza kuwasaidia katika kupangilia uandishi wao na kuwasaidia katika miundo ya sentensi na msamiati. Wanafunzi wadogo watakuhitaji wewe ili ufanye nao kazi, uwaongoze katika uandishi wao na polepole wapanue msamiati wao.

Uchunguzi kifani ya 2: Kutumia mambo yanayowavutia wanafunzi ili kuendeleza stadi za usomaji na uandishi

Bw. Simoni Raphaeli aligundua kuwa, katika uwanja wa mpira, baadhi ya wavulana wa darasa la 6 –ambao hawakuonesha kuvutiwa na usomaji na uandishi wakati wa masomo ya Kiingereza –mara kwa mara walikaa pamoja ili kusoma gazeti la soka, Mwanaspoti. Walimwambia Bw. Simon kuwa wanafurahia kutafuta taarifa zinazohusu maisha ya wachezaji wanaowapenda.

Hali hii ilimpa Simoni wazo. Aliwauliza wanafunzi wa darasa lake kama wameshawahi kusoma magazeti na, kama wameshawahi kuyasoma, walifurahia kusoma kitu gani. Wengi walisema kuwa walijaribu kusoma hadithi kuhusu watu ambao waliwavutia, hata kama hawakuweza kuelewa maneno yote. Simon aliandaa mkusanyiko wa magazeti kwa ajili ya darasa. Kisha aliwauliza wanafunzi kuhusu mambo waliovutiwa nayo na kuwafanya wasome magazeti hayo. Nyota wa michezo ndio waliopendwa zaidi (hasa wachezaji wa soka, pia mpira wa kikapu, mbio na ndondi), wanamuziki, nyota wa filamu na TV, wakifuatiwa na wanamitindo, wanasiasa, viongozi wa jumuiya na wafanyabiashara maarufu.

Simoni aliwapanga wanafunzi kufuatana na yale mambo yaliyowavutia. Kulikuwa na vikundi kadhaa vya nyota wa michezo na wanamuziki! Alikipatia kila kikundi magazeti na kuviambia vikundi vitafute makala/picha kuhusu mtu mmoja aliyewavutia wanakikundi. Kisha, kama kikundi, walisaidiana kuandika sentensi fupi moja au mbili kuhusu maisha ya mtu huyo. Walitumia maneno yao wenyewe na pia msamiati kutoka kwenye makala. Waliandika kichwa cha habari chao wenyewe.

Simoni aliridhika kuona kuwa wanafunzi wengi walishiriki katika usomaji na, wengine wakiandika sana kuliko wengine, wote walishiriki. Kila kikundi kilifurahia kusoma na kukisomea kikundi kingine wasifu wa kikundi.

Shughuli ya 2: Usomaji na uandishi wa hadithi za maisha

Ili kuandaa shughuli hii tumia Nyenzo-rejea 4: Kuandaa msomo ya hadithi za maisha.

Waambie wanafunzi wasome kwa pamoja hadithi uliyoinakili ubaoni au kwenye karatasi. Au wasomee hadithi hiyo na eleza inahusu nini.

Jadilini sifa za hadithi za maisha (wasifu). Waulize wanafunzi wakuambie ni kategoria gani za watu (m.f. wachezaji wa taifa wa mpira wa miguu, wanamuziki wa jadi) ambao wanawapenda, na kwa nini.

Kipatie kila kikundi chenye mwelekeo wa aina moja magazeti mbalimbali ambayo yana makala kuhusu kategoria ambayo wanakikundi wanaipenda/wanaifurahia.

Waambie watafute makala kuhusu mtu kutoka katika kwenye kategoria waliyoichagua na watumie taarifa ili kuandika mambo mawili yanayomhusu mtu huyu (angalia Nyenzo-rejea 4 kwa mwongozo katika kuwasaidia wanafunzi wako kuweza kufanya kazi hii).

Kusanya rasimu hizi ili kuzitumia katika Shughuli Muhimu.

Kama darasa lako ni kubwa sana, ungeweza kufanya shughuli hii kwa kuhusisha nusu ya darasa au vikundi vidogo kwa zamu. Ungeweza pia kuwaweka wanafunzi katika vikundi kulingana na uwezo wao –ukichanganya wenye uwezo zaidi na wale wenye uwezo mdogo ili wasaidiane. Ukiwa na wanafunzi wadogo, unaweza kufanya kazi hii kama zoezi la darasa zima ambapo unawasaidia kunukuu mawazo yao na kushirikishana maneno yao.

Somo la 3

Tunapoandika kitu, ni muhimu tuweke wazi kile tunachotaka kukisema. Tunatakiwa tupange. Baadaye, tunaanza kuandika na kusoma kile tulichokwisha andika. Tunaweza kuamua kubadili mpangilio wa baadhi ya maneno, kuongeza, kupunguza baadhi ya maneno na kuongeza au kubadili baadhi ya taarifa. Mwishoni, tunakagua uandisha ambao si sahihi, alama za kiuakifishi/uandishi au sarufi. Kazi ya mwisho inaweza kuwa tofauti kabisa na ile rasimu yetu ya mwanzo. Tunakuwa tumefanya uandishi wetu uwe wa kisanaa.

Katika darasa, kazi moja ingeweza kukamilika (yaani iwe imeandikwa kisanaa) kabla ya kuanza kazi nyingine. Uchunguzi Kifani 3 na Shughuli Muhimu hukuonesha jinsi ya kuandaa masomo ambapo wanafunzi wanatakiwa wafanye uandishi wao uwe wa kisanaa.

Uchunguzi kifani ya 3: Kushirikiana na mwenzako ili kuwasaidia wanafunzi katika uandishi

Bibi Dorcas Mabula na Bibi Beatrice Mntambo wanafundisha wanafunzi wa darasa la 6 katika Wilaya ya Kinondoni somo la Kiingereza. Huwapatia wanafunzi maoni ya kina kuhusiana na uandishi wao, hivyo wakati mwingine walimu hawa hubaki shuleni baada ya saa za shule na kushirikiana katika kusahihisha.

Siku moja mchana, kabla ya kuanza kusahihisha wakiwa wanakunywa Maltina, wote wawili walielezana kuwa walikuwa wanajisikia kuchanganyikiwa kutokana na baadhi ya wanafunzi kupuuzia maoni na masahihisho katika madaftari yao. Marafiki hawa waliona kuwa hali hii ilikuwa inatisha, kwa sababu waligundua kuwa maoni waliyowapatia katika rasimu ya kwanza katika kazi zilizotangulia yaliwasaidia kuboresha matoleo yao ya mwisho ya kazi kwa ajili ya kuendeleza kozi zao za kitaalamu. Baadaye Dorcas aligundua kitu muhimu! Wanafunzi wake hawakupata nafasi ya kufanya kazi nyingi zinazohusiana na kazi hii ya uandishi. Badala yake, kulikuwa na mada mpya katika kila somo la uandishi.

Alipomwambia Beatrice jambo hili, rafiki yake alikubali kuwa jambo hili pia lilitokea katika darasa lake. Hivyo ndivyo walivyofundishwa walivyokuwa shuleni!

Waliamua kujaribu mkabala mpya. Wakaamua kutumia masomo kadhaa kuandika rasimu na kuandika kisanaa andiko hilohilo. Wakawapatia wanafunzi mawazo ya kuwaongoza katika uandishi wao na katika marudio ya andiko hilo. Mwanzoni, wanafunzi hawakupenda kurudia kuandika andiko hilohilo, lakini walipoona jinsi kazi zao zilivyokuwa bora, walianza kulipenda zoezi hili.

Shughuli muhimu: Kutoka kwenye uandishi wa rasimu wa mashairi/hadithi mpaka uandishi wa kisanaa

Kabla ya somo, soma rasimu za kwanza za wanafunzi na amua juu ya maswali ya jumla ya kuwauliza ili kuboresha kazi zao (angalia Nyenzo-rejea 5: Maswali kwa ajili ya wanafunzi ). Yaandike maswali haya ubaoni.

Warudishie wanafunzi rasimu zao, zikiwa na maoni ya jumla juu ya kile unachotaka kuhusu uandishi wa wanafunzi. Eleza kuwa sasa uandishi wao utakuwa wa kisanaa.  

Waambie wasome tena rasimu zao za kwanza na watumie maswali yaliyoko ubaoni katika kuandika na kuboresha rasimu za pili. 

Waambie wabadilishane na wenzao rasimu zao za pili na wapeane mapendekezo kwa ajili ya maboresho.

Waambie watumie mapendekezo haya kuandika toleo la mwisho. Zungukia darasa na toa msaada inapobidi. Wahimize watumie michoro katika uandishi wao.

Kama hakuna muda ili kumalizia shughuli hii katika muda wa kipindi darasani, waambie wanafunzi wamalizie shughuli hii nyumbani na watoe ripoti siku inayofuata.

Waulize jinsi mchakato huu wa kuandika rasimu ulivyowasaidia. Kulikuwa na maboresho yoyote katika uandishi wa wanafunzi kama matokeo ya mchakato wa wanafunzi wa uandishi wa rasimu na uandishi wa kisanaa? Unaweza kujenga mambo haya?

Ukiwa na wanafunzi wadogo au ambao hawajui sana lugha inayotumiwa darasani, ungeweza kufanya nao kazi ya kuandika rasimu na kuandika tena rasimu ya kazi rahisi kwa vipindi viwili – ukiwapatia muda katika somo ambao wataweza kutafakari kile ambacho walitaka hasa kukisema.

Nyenzo-rejea ya 1: Kuandaa masomo juu ya mashairi ya majina au ya kusifu

Usuli/welewa wa somo wa mwalimu

Amua kama unataka kuchagua mashairi/hadithi za majina au za kusifu ili kuzifanyia kazi na wanafunzi wako.

  1. Chagua mfano mmoja au zaidi kutoka Nyenzo-rejea 2 au 3 AU kutoka katika Nyenzo-rejea nyingine ulizonazo AU andika shairi au hadithi yako mwenyewe.
  2. Andika shairi (ma)/ hadithi hiyo au hadithi hizo kwenye karatasi kubwa au ubaoni ili unapozitumia darasani wanafunzi waweze kusoma chapa kubwa pamoja na wewe na baadaye waweze kurejelea mashairi na hadithi hizo wanapoandika mashairi au hadithi zao wenyewe. Kama huna karatasi kubwa, andika kwenye ubao wako.

Andaa maswali ya kuwauliza wanafunzi kuhusu shairi (ma)/hadithi. Kwa hakika, aina ya swali itategemea kile ulichokichagua.

Kwa mfano, kama utachagua shairi la Thabo, ungeweza kuanza na:

‘Unagundua nini kuhusu jinsi shairi hili lilivyoandikwa?’ (Jibu: Kila mstari umeanza kwa herufi moja ya jina la Thabo).

Ukichagua hadithi ya kusifu ya Hugh Lewin kuhusu mama yake Jafta, ungeweza kuuliza: ‘Ungependa kuwa na mama kama mama yake Jafta? Nipatie sababu ya jibu lako.’

Ukishamaliza maandalizi haya, uko tayari kufundisha masomo kuhusu mashairi na hadithi za majina na za kusifu. Wanafunzi wanapoanza kuandika, zungukia darasa ili kumsaidia yeyote ambaye atapata shida katika kuanza. Wengine watahitaji msaada wa mawazo, wengine shida ya msamiati.

Nyenzo-rejea 2 na 3 zote ni mashairi, nyimbo na hadithi za kusifu lakini lugha ni ngumu kwa baadhi yazo kuliko nyingine.

Nyenzo-rejea ya 2: Mashairi na hadithi za majina

Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Shairi la majina lililoandikwa na mwalimu nchini Tanzania:

Hanna – Jina langu la Sifa lililoandikwa na Hanna Simpassa

Fahari ya moyo wangu –

Nani alileta jina hili?

Nililipataje?

Hakuna hata mmoja katika familia aliyeliota – ila mimi!

Jina langu la Kikristo.

Wazazi wangu hawakulichagua – Nililiunda,

Zamani kabla sijawa Muislamu.

Hasina – jina linalomaanisha uzuri.

Hasina – jina langu maalumu.

Roho ziliniambia katika ndoto

Umebadilishwa dini kuwa Mkristo

Hanna ni jina lako.

Hanna – jina linalomaanisha ‘Neema, huruma na sala’.

Yeye ni wa thamani kama almasi,

Hujua thamani ya kujitoa,

Kamwe hakati tamaa,

Anapata marafiki kwa urahisi,

Furaha ni nguvu yake,

Kicheko chake ni dawa nzuri;

Mtu ambaye asili yake ni maarifa thabiti.

Yeye ni mtoto wa ulimwengu.

Hivyo nilibadilishwa dini

Hasina kuwa Hanna

Na ninajivunia jina langu

Shairi la jina lililoandikwa na mwalimu nchini Afrika Kusini

Mawazo kuhusu herufi za jina langu na Thabo X

T inasimama badala ya thabiti – Mimi ni mtu imara

H kwa ajili ya hafukasti – baba na mama yangu wana asili tofauti

A ni aminifu…

Bora

Ona nilivyo–ni mimi hasa!

Hadithi ya jina iliyoandikwa na mwalimu nchini Tanzania:

Hadithi ya kupewa jina niliyohadithiwa na Nyalupala Mtavangu

Zamani, katikati ya kiangazi, babu yangu, wakati huo alikuwa anaitwa Nyalukolo, alikwenda mtoni ili kukamilisha sherehe za matambiko. Pale mtoni alitokea simba mkubwa ambaye alikwenda kunywa maji. Mnyama huyu alimshambulia, na Nyalukolo alipambana naye. Aliwaua wanyama wengi wa mwituni na haraka alikimbilia nyumbani kumwambia baba yake kuhusu kitendo hiki cha ushujaa cha kushangaza.

Baba yake, Mungai, alituma ujumbe kijiji kizima na watu walikimbilia mtoni. Ilikuwa kweli – simba aliyekufa alikuwa amelala pale chini!

Tangu siku ile, Nyalukolo alipata heshima kutoka kwa kila mtu ambaye alijua alichokifanya. Wanaume na wanawake, vijana na wazee, walimheshimu. Katika sehemu nyingine walimtania kichinichini ‘Nyalupala’. Jina hilo la minong’ono lilimfikia baba yake, Mungai, ambaye aliamua kuita watu wa kabila lile pamoja kwa ajili ya sherehe ya kubadili jina. Nyalukolo aliitwa Nyalupala rasmi, kwa maana ya ‘simba’ katika lugha ya Kihehe.

Wakati nilipozaliwa, katikati ya karne ya 20, nilipewa jina la babu yangu. Ni jina ninalolihusisha na ushujaa na ushupavu wa mzimu wangu na ninajivunia jina hili.

Nyenzo-rejea 3: Mashairi na hadithi za kusifu

Nyenzo rejea ya mwalimu kwa ajili ya kupanga au kurekebisha ili kutumia na wanafunzi

Shairi la Kiyoruba la kusifia chatu

Baadhi ya ushairi wa kusifu husifia wanyama au vitu kuliko watu. Hapa pana shairi kutoka kwa Wayoruba wa Naijeria. Maelezo kwa baadhi ya lugha iliyotumika yametolewa baada ya shairi hili.

Chatu

Mwana wa mfalme mwenye mikogo [Mstari 1]

Mkubwa miongoni mwa nyoka.

Wanasema chatu hana nyumba.

Nilisikia maneno haya zamani

Na nilicheka nikacheka na kucheka.

Kwani ni nani anamiliki ardhi chini ya nyasi za mlimao? [Mstari 6]

Nani anamiliki ardhi chini ya nyasi za tembo?

Nani anamiliki kinamasi – baba wa mito?

Nani anamiliki dimbwi lililosimama – baba wa maji?

Kwa sababu hawatembei kwa kuongozana [Mstari 10]

Watu wanasema kuwa nyoka hutembea tu pekee pekee.

Lakini hebu fikiria

Chukulia kipiribao atembee mbele ya wote

Hongo afuatie

Na chatu atambae akinguruma nyuma yao [Mstari 15]

Nani atakuwa jasiri

Kuwasubiri?

Tini

  1. Kutembea kwa mikogo ni kutembea kwa kujivuna – ukidhani kuwa wewe ni bora kuliko wote, kujidai. Katika mstari 1, shairi linamweleza chatu kama mtoto wa mfalme mwenye mikogo.
  2. Maswali yaliyopo kwenye mstari wa 6 hadi wa 9 inaonesha kuwa chatu ana nyumba nyingi – sehemu zote mbili; katika ardhi na kwenye maji. 
  3. Katika ubeti wa pili, shairi linaonesha kuwa wanyama na watu wengine wangeogopa sana kutembea karibu na nyoka – ndio maana nyoka ‘hutembea’ pwekepweke.

Hadithi ya kumsifu mama

Mama na Hugh Lewin

Ningependa wewe, alisema Jafta, ukutane na mama yangu. Hakuna yeyote kati ya watu ninaowafahamu ambaye ni kama mama yangu. Mama yangu ni kama ardhi – amejaa mambo mazuri, mwenye joto na nguvu, na wa rangi ya kahawia. Mama yangu ni kama jua linalochomoza alfajiri, likiangaza sehemu zenye giza na kutuamsha likitubembeleza taratibu.

Huchochea moto ili uwake na baada ya muda kila mahali panajaa harufu ya chakula, ambayo hulifanya tumbo langu lingurume na kunifanya nitake kuamka.

Jinsi jua linavyoaanza siku yake na maua yakichanua na kurusha maua hayo angani ninamkumbuka mama yangu. Kama lilivyo anga, daima yeye yuko pale. Daima unaweza kumwangalia na kumwona.

Mchana jua linapokuwa kali, hutupatia kivuli na kutuburudisha, kama mti ulioko kwenye mto. Au wakati hali ya hewa inapokuwa na joto sana na vurugu, anatupoza kama mvua ifanyavyo inapoondoa vumbi kwa njia ya mawimbi, na kunyeshea nyasi na kuzifanya tena za kijani.

Halalamiki mara kwa mara, hata katika saa mbaya. Lakini kuwa makini! Akikukamata unafanya mchezo wa kudang’anya, au kuwachokoza wadogo zako wa kike, anaweza kutoa sauti kama ya radi ya mchana na macho yake yakatoa mwanga kwenye mawingu meusi.

Mama yangu hakasiriki mara kwa mara, alisema Jafta, ila ni vema zaidi anapoimba. Anatuimbia anapopika mlo wa jioni. Kama umeshawahi kusikia hopoe akiita kwenye mahindi, basi utakuwa umeshasikia mama yangu akiimba.

Baada ya mlo wa jioni, unafuata muda wa hadithi. Kwa kiasi fulani, alisema Jafta, takriban ninampenda mama wakati huo kuliko wakati wowote – baada ya kula chakula, na pilikapilika za hapo, pindi jua linapokuchwa na kila kitu ni kitulivu na kimepoa. Hapo mama hutukumbatia na kuondoa masikitiko yetu. Tunazungumzia ya leo, ya kesho, na hasa ya kesho.

Kisha blanketi la usiku linapofunika dunia, na mwezi ukiwa juu yake, mama yangu hutufunika kwa uangalifu na kutubusu na kututakia usiku mwema; hutulaza.

Vyanzo vya asili:

Chatu imechukuliwa kutoka English Matters, Grade 7 Anthology, iliyokusanywa na Lloyd, G. & Montgomery, K.

Mama na Hugh Lewin imechukuliwa kutoka New Successful English, Reading Book, Grade 6

Nyenzo-rejea 4: Kuandaa masomo juu ya hadithi za maisha

Usuli/welewa wa somo wa mwalimu

  1. Kusanya Nyenzo-rejea utakazozihitaji. Kazi hii inaweza kuchukua muda, lakini magazeti na vichekesho unavyokusanya vinaweza kutumika kwa masomo ya lugha nyingi mbalimbali pamoja na zile za usomaji na uandishi wa hadithi za maisha. Baadhi ya wanafunzi wanaweza kuleta magazeti kutoka nyumbani, hivyo waambie waziombe familia zao ruhusa ya kuchukua magazeti hayo. Waombe wenzako na rafiki zako wakukusanyie magazeti ambayo wameshamaliza kuyasoma. Katika baadhi ya nchi, wachapishaji wa magazeti huweza kutoa msaada wa nakala za magazeti kwa shule yako. Baadhi ya AZAKI pia zina machapisho mazuri sana. Kwa mfano, makala kuhusu maisha ya Julius Nyerere yanapatikana kutoka magazeti mbalimbali ya Kitanzania na nchini Afrika Kusini ucheshi kuhusu maisha ya Nelson Mandela unapatikana katika Mfuko wa Nelson Mandela.
  2. Kabla ya kuanza masomo haya lazima uwe na vitu vya kutosha vya kusoma kuhusu aina mbalimbali za watu maarufu kwa ajili ya kufanyiwa kazi na kila kikundi cha wanafunzi.
  3. Nakili katika karatasi kubwa au ubaoni, hadithi ya maisha ya Freddy Macha (wasifu ufuatao hapa chini) AU hadithi nyingine utakayoichagua ambayo imeandikwa kwa kutumia lugha rahisi.
  4. Tengeneza orodha ya vipengele vinavyofanana vya hadithi hizi za maisha ili kuvijadili pamoja na wanafunzi wako. Hivi hujumuisha:
    • i.kwa kawaida usimulizi wa hadithi huzingatia mfuatano wa wakati toka miaka ya awali mpaka ya baadaye ya maisha ya mtu;
    • ii.hudokeza mafanikio ya maisha ya mtu;
    • iii.hutoa maelezo ya kina ya kitu fulani kinachovutia au cha kushangaza kuhusu maisha ya mtu.

Sasa uko tayari kuanza somo!

Waongoze wanafunzi wakati wanapoandika hadithi kuhusu maisha

Wakati wanafunzi wanafanya kazi katika vikundi vyao, zungukia darasa ili kukagua kama wameelewa kazi hiyo na wanaweza kupata makala za kutumia. Ungeweza kuandika ‘orodha-kaguzi’ ubaoni ili kuwaongoza wanafunzi katika uandishi wao. Kwa mfano:

jina(ma) ya mtu huyo;

sehemu aliyozaliwa;

maelezo ya familia;

‘historia’ – siku za shule, mafanikio ya awali, mafanikio ya baadaye;

Vitu vya kuvutia/vya kuhuzunisha/vya kushangaza ambavyo vimetokea katika maisha ya mtu huyo.

Wahimize wanafunzi wafikirie kuhusu utaratibu watakaoutumia ili kuandika habari za mtu huyo na kutumia maneno yao wenyewe. Wasinakili tu kutoka kwenye makala.

Hadithi ya maisha ya Freddy Macha (wasifu)

Freddy Macha alizaliwa katika miteremko ya mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Yeye ni mwandishi wa nathari, ushairi, tamthiliya na nyimbo, na pia ni mpiga-ala mbalimbali, mwimbaji na mwigizaji.

Akiwa na umri wa miaka 13, Freddy alianza kuimba na kuigiza jukwaani. Katika miaka ya 1970 na 1980, alikuwa anaishi na kufanya kazi kama mwandishi wa habari jijini Dar es Salaam na alikuwa na vitabu vyake alivyochapisha vikiwemo Twenzetu Ulaya (mkusanyiko wa hadithi za Kiswahili ), wasifu wa mwana muziki maarufu Remi Ongala na mkusanyiko wa mashairi yanayoitwa Papers! Papers! Papers! Freddy alishinda tuzo ya BBC ya ushairi mwaka 1981 na mashairi hayo yalitokea katika mkusanyiko Summer Fires.

Mwaka1984, Freddy alifanya ziara iliyokuwa ya mafanikio katika nchi za Skandinavia ikiwa ni pamoja na Tamasha la Kimataifa la Thieta la Oslo pamoja na kikundi chake cka Kitanzania cha Sayari. Baadaye, kwa kipindi cha miaka mine tangu 1988, Freddy alikuwa anaongoza kikundi cha bendi cha rege kilichoitwa ‘reggae-afro-funk band Os Galas’, cha Brazili.

Freddy alikwenda Uingereza mwaka 1996 na alifanya miradi mingi ikiwa ni pamoja na warsha, drama na muziki. Kwa kutembelea sehemu nyingi, Freddy huzungumza na kuigiza kwa kutumia lugha mbalimbali. Tangu 1998 mpaka 2001, katika miji ya Stoke Newington na Brixton, Freddy amefanya tamasha maarufu katika Baa ya Lorca lililoitwa Usiku wa Muziki wa Dunia ambapo wanamuziki waliweza kukutana na kujaribu vifaa vipya. Hili lilijulikana kama 'the local WOMAD' na gazeti la ‘The Hackney Gazette’ na ndiyo sababu muhimu kwa Freddy kuwa Mwakilishi wa Umoja wa Wanamuziki wa Dunia kwa upande wa sehemu ya muziki wa Jadi na wa Kimapokeo mwaka 1999–2001.

Hivi sasa, Freddy anaweza kuendesha warsha na matamasha mbalimbali mashuleni na katika kumbi za Uingereza. Alitunga kichekesho cha kitashtiti kinachoitwa ‘News No News’, ambacho wakati mwingine anakiigiza peke yake au na bendi yake ya Kitoto. Bendi ya Kitoto imeundwa na wanamuziki sita kutoka sehemu mbalimbali za Afrika, Karibiani, nchi za Uingereza na Amerika Kusini.

Nchini Uingereza, Freddy ametoa rekodi mbili: albamu inayoitwa Constipation (2000) yenye miziki 11 na wimbo mmoja unaoitwa Kilimanjaro. Constipation ina muziki, nathari na ushairi na inatumia lugha mbalimbali, ambayo imetengenezwa kutokana na utaalamu wa Freddy. Kwa mfano, kuna aina mbalimbali za nyimbo nzuri za Kiswahili na nyimbo za Kiingereza ambazo zinatoa mafunzo mazito kuhusiana na jamii. Freddy anafanya kazi sana za kutoa albamu mpya kwa ajili ya watoto wa shule. Matarajio ni kwamba albamu hiyo itakuwa bora kama Constipation.

Sehemu ya 5: Kubadilisha hadithi simulizi, mashairi na michezo kuwa vitabu

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kusaidia ujifunzaji wa lugha kwa kutunga na kusanifu vitabu?

Maneno muhimu: uandikaji; uchoraji wa vielelezo; usanifu; kitabu; gamba la kitabu (jalada la kitabu)     

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutumia njia ya majadiliano kwasaidia wanafunzi kuelewa uhusiano na tofauti zilizopo kati ya matini simulizi na matini andishi;
  • Kukuza njia ambazo wanafunzi wanaweza kuzitumia kubadilisha hadithi simulizi, mashairi, nyimbo au michezo kuwa katika maandiko na vielelezo;
  • Kutalii jinsi ya kutoa vitabu vya hadithi, mashairi, michezo na nyimbo kwa ajili ya maktaba ya darasa.

Utangulizi

Kipengele kimojawapo cha kufundisha ni kwa wanafunzi kuona lengo halisi la kazi unazowapa. Kwa kuwasaidia wanafunzi kutengeneza vitabu kwa ajili ya maktaba ya darasa, utakuwa umewapa sababu ya kuwa waangalifu katika maandishi na michoro yao. Hali hii itawasaidia kuthamini lugha zao za nyumbani na lugha ya mawasiliano darasani au lugha ya ziada. Vitabu vinaweza kuandikwa katika lugha yao ya nyumbani, lugha ya mawasiliano darasani au lugha ya ziada. Zaidi ya lugha moja inaweza kutumika katika kitabu kile kile. Vitabu wanavyoandika wanafunzi, kwa msaada wako, vitakupa matini zaidi kwa ajili ya shughuli za kusoma.

Somo la 1

Wanafunzi wanaozungumza lugha ya nyumbani ambayo ni tofauti na wanayotumia darasani wanahitaji kujua kama unaithamini lugha yao ya nyumbani. Hii ni muhimu kwa kuwa lugha ya nyumbani ni sehemu ya mtu alivyo. Njia mojawapo ya kueleza hili ni kuwahimiza wanafunzi wako kutoa hadithi na vitendawili, kughani mashairi, kuimba nyimbo na kueleza michezo katika lugha za nyumbani na kisha kuziandika, ama kwa lugha zao za nyumbani au lugha nyinginezo.

Katika Shughuli 1, uwasaidie wanafunzi wako kugundua tofauti kati ya matini simulizi na andishi. Utawahimiza kufikiri kuhusu yaliyo na thamani katika utamaduni simulizi, kwa nini watu huandika na lugha zipi hutumika katika mazungumzo na katika maandishi.

Uchunguzi kifani ya 1: Kusimulia hadithi katika lugha za nyumbani; kuziandika katika lugha ya mawasiliano darasani

Hivi karibuni Bwana Okitikpi, mwalimu mzungumzaji wa lugha ya Kiyoruba, amehamishiwa Kaskazini mwa Nijeria katika jamii izungumzayo lugha ya Kihausa ikiwa lugha kuu, lakini baadhi ya wanafunzi wanazungumza lugha tatu za Kinijeria. Wazazi wachache na vijana watu wazima wamekubali kuwa walimu ‘wasaidizi’. Wanafahamu Kihausa na Kiingereza kidogo na wanamsaidia Bwana Okitikpi kujifunza Kihausa ili aweze kwasiliana na wanafunzi vyema. Kwa kuwa baadhi ya wanafunzi wake wanaweza kuzungumza lugha tatu za Kinijeria, Bwana Okitikpi amewahusisha wasaidizi hawa katika shughuli za utambaji wa hadithi ili kujenga kujiamini kwa wanafunzi katika uzungumzaji na kuwaonesha kuwa lugha zao za nyumbani zinathaminiwa.

Anataka wanafunzi kuandika hadithi, hususan katika lugha zao za nyumbani. Hata hivyo baadhi ya lugha hizo hazina mfumo wa maandishi, kwa hiyo ameamua waandike hadithi zao kwa kutumia lugha ya Kihausa.

Mmoja wa wasaidizi wake amejadiliana na wanafunzi kuhusu sababu za watu kuandika hadithi. Kisha, wanaandika hadithi wanayoipenda sana, kwa kutumia lugha ya Kihausa, ili waiweke katika kitabu kwa ajili ya maktaba ya darasa.

Bwana Okitikpi aliwaweka wanafunzi wake katika vikundi kwa ajili ya shughuli hii, akihakikisha kuwa angalau mwana-kikundi mmoja ni mzungumzaji mzuri wa lugha ya Kihausa na anaweza kuwasaidia wengine. Pia alimtaka msaidizi wake amsaidie kuangalia mchakato wa uandishi.

Shughuli ya 1: Uandishi wa fasihi simulizi na michezo

Kwanza, soma Nyenzo-rejea 1: Jinsi hadithi zinavyoandikwa katika vitabu, na fikiria juu ya majibu ya maswali matano kwa ajili ya wanafunzi.

Watake wanafunzi wakueleze vichwa vya habari vya hadithi, mashairi, nyimbo na michezo katika lugha za nyumbani. Viandike ubaoni.

Jadili maswali haya na wanafunzi:

Je, matini hizi za lugha ya nyumbani zimeandikwa katika vitabu? Kwa nini watu huandika hadithi, mashairi, nyimbo na michezo katika vitabu?

Ungependa hadithi, mashairi, nyimbo na michezo ya lugha yako ya nyumbani kuandikwa katika vitabu? Kwa nini iandikwe au kwa nini isiandikwe?

Ni katika lugha ipi au zipi ambazo ungeandika mashairi, hadithi na michezo katika kitabu?

Vitabu vinaandikwaje na vinatolewaje? Waambie wanafunzi watakuwa wanaandika vitabu kwa ajili ya maktaba yao ya darasa.

Watake wanafunzi kila mmoja kuchagua hadithi aipendayo na kuandika mswada wa jaribio la kwanza katika lugha aipendayo.

Umefurahia majadiliano?

Wanafunzi wamefanyaje katika shughuli hii?

Somo la 2

Baadhi ya ujifunzaji, kama kujifunza kucheza ala za muziki, kutumia kompyuta au kuendesha gari, huhitaji mazoezi mengi. Kama mwalimu, unahitaji kuwapa wanafunzi nafasi ya kurudia na kufanya mazoezi ya kile walichokwishafanya kabla ili waweze kufanya maendeleo katika juhudi zao za mwanzo. Wakati ambapo Shughuli 2 katika sehemu hii inafanana na Shughuli muhimu katika Sehemu 4, marudio haya ni muhimu. Wanafunzi watajifunza kuwa uandishi ni mchakato, na kuwa hadithi, mashairi na maelekezo yao ya michezo yaliyoandikwa yatawapa wengine furaha zaidi kama zitaandikwa kwa makini.

Kuandika, kuchora vielelezo na kusoma vitabu hivi yanaweza kuchukua masomo mengi, lakini kwa kuwa shughuli hizi huwezesha nafasi nyingi za kazi za lugha , muda utatumika vizuri. Unaweza kutumia Nyenzo-rejea 2: Orodha ya kupimia ya wanafunzi ili kuwasaidia kutathmini kazi zao. Uchunguzi-kifani unaelekeza jinsi walimu wanavyoweza kuandika vitabu pamoja na wanafunzi ambao hawajapata ujuzi wa kutosha wa uandishi.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuwasaidia wasomaji na waandishi chipukizi jinsi ya kuandika kitabu cha hadithi

Mwalimu Goodluck Nkini anawafundisha kwa pamoja wanafunzi 60 wa darasa la 1 na la 2, katika shule mojawapo karibu na mji wa Kigoma. Mwalimu mwenzake anafundisha wanafunzi 48 wa darasa la 3 na la 4. Mara kwa mara walimu hawa wawili huwakaribisha wazazi shuleni kusimulia hadithi kwa lugha ya Kiha.

Mwalimu Goodluck Nkini aliwataka wanafunzi kumsaidia kugeuza hadithi wanayoipenda, ambayo wamesaidia kuitunga, ili iwe kitabu.

Kwanza alitengeneza daftari kubwa lisiloandikwa chochote (Angalia Nyenzo-rejea 3: Kubadilisha hadithi za wanafunzi kuwa ‘kitabu kikubwa’ ).

Aliandika hadithi kwa kutumia vifungu na sentensi fupifupi. Halafu aliamua mahali ambapo kila kifungu au sentensi iwekwe wapi katika lile daftari kubwa. Alitumia rangi nyeusi pamoja na nta kuandika hadithi kwa herufi kubwa nzuri, akiacha nafasi kwa ajili ya picha.

Aliwaonesha wanafunzi kitabu darasani, na kusoma nao hadithi. Alijadiliana nao aina ya picha zilizotakiwa katika kila ukurasa. Aliwapa kila wanafunzi katika jozi vipande vya karatasi, na jozi mbili za wanafunzi walichora picha katika kila karatasi kati ya karatasi 15.

Aliwataka wanafunzi kutafuta ukurasa unaofaa kwa kila picha, na kuwasaidia kugundisha picha hizo katika kitabu.

Shughuli ya 2: Ustadi wa kuandika rasimu ya kwanza na kusanifu vitabu

Watake wanafunzi katika vikundi vya watu wanewane kusoma rasimu ya kwanza ya hadithi zao (kutoka Shughuli 1). Watake wachague rasimu mbili (kutoka katika zile nne) za kufanyia kazi katika jozi ili kuziboresha. Wanatakiwa kutumia orodha ya kupimia ya wanafunzi katika Nyenzo-rejea 2 ili kuwaelekeza jinsi ya kufanya kazi zao.

Hatua nyingine ni kuwataka waioneshe katika kundi la jozi nyingine ya wanafunzi kwa ajili ya kuiboresha. 

Sasa kusanya kazi zao na sahihisha makosa ya tahijia, sarufi na vituo vya uandishi.

Halafu vipe vikundi kitabu chao kisichoandikwa kitu chochote (Angalia Nyenzo-rejea 3) na watake wafanye yafuatayo:

  • wapange ni sentensi zipi ziwe katika kila ukurasa na michoro iwe wapi;

  • waamue jinsi ya kugawa kazi za maandishi na michoro, ili kila mwana-kundi anashiriki.

Watake waoneshe mpango wao; jadiliana nao na watake watekeleze mpango wao.

Kwa wanafunzi wadogo, mnaweza kuandika hadithi pamoja katika kitabu kikubwa na baadaye wanafunzi wanaweza kuchora kwa kila ukurasa.

Somo la 3

Mawasiliano sio kuhusu maneno tu. Siku hizi magazeti mengi yana picha nyingi kuliko zamani na vitabu vya siku hizi vina vielelezo vingi zaidi kuliko vitabu vya zamani. Watoa matangazo hutumia picha katika mabango, katika majarida na katika televisheni (luninga) ili kuuza bidhaa zao. Skrini za kompyuta huchanganya maneno na picha katika hali ya kusisimua. Wanafunzi wanahitaji kuandika na kusoma matini ambazo zinachanganya maelezo ya mazungumzo (maneno) na michoro (picha). Ukiwa mwalimu majukumu yako ni:

Kuwa na habari za sasa za mambo yanayowafurahisha wanafunzi;

Ukijumlisha na shughuli za michoro ya ubunifu (kwa mfano, ubunifu wa michoro ya vifurushi vya kuchukulia bidhaa za madukani, mabango ya matangazo, matangazo ya biashara) katika lugha na masomo ya kusoma na kuandika.

Sehemu hii inazingatia uchoraji wa gamba la vitabu vya watoto vinavyohusu hadithi, mashairi, nyimbo na michezo.

Uchunguzi kifani ya 3: Kujadili na kutengeneza magamba ya vitabu

Mwalimu Malaitji anawahimiza wanafunzi wake wa somo la Kiingereza wa darasa la 6 kuuliza maswali wakati wa somo lao la kusoma kuhusu maneno na misemo ambayo wanaisikia au kuisoma lakini hawaielewi. Siku moja asubuhi, mwanafunzi aliliambia darasa kuwa amesikia mhusika mmoja wa mchezo wa kuigiza katika televisheni akimwambia mwenzie kuwa ‘Usihukumu kitabu kwa kuangalia gamba lake.’ Mwalimu Malaitji aliwauliza wanafunzi wake mawazo kuhusu msemo huo una maana gani na kwa nini ulitumika katika mchezo huo wa kuigiza. Baada ya muda mfupi wa majadiliano, wanafunzi walielewa kuwa uchoraji wa gamba la kitabu unaweza au usiweze kutoa wazo zuri kuhusu yaliyomo katika kitabu. Kwa mtazamo huo, mtu aonekanavyo au asemavyo inaweza isiwe kielelezo cha jinsi mtu huyo alivyo ‘ndani mwake’.

Mwalimu Malaitji aliamua kuendeleza majadiliano. Aliwataka wanafunzi darasani kufikiri kuhusu shabaha za gamba la vitabu, halafu waangalie gamba la kitabu cha hadithi ambacho alileta darasani. Wanaweza kueleza kuhusu hadithi inahusu nini kwa kuangalia gamba la kitabu? Wamependa nini au ni kitu gani ambacho hawakukipenda kuhusu gamba hilo la kitabu? Gamba hilo linaweza kuboreshwa, na kama jibu ni ndiyo, linaweza kuboreshwaje? Baada ya mjadala hai na kusoma hadithi kwa wanafunzi, aliwataka wafanye kazi katika vikundi vya wanafunzi wanewane kutengeneza gamba jipya kwa ajili ya kitabu hiki na aliwapa makaratasi ya kufanyia kazi. Walipomaliza, mwanafunzi mmoja kutoka kila kikundi alitoa maelezo darasani kwa nini wamechora gamba la kitabu katika namna waliyochagua. Mwalimu Malaitji aliyabandika magamba ya vitabu katika ukuta wa darasa.

Shughuli muhimu: Kuandika vitabu na kutayarisha gamba la vitabu

Baada ya kumaliza kuandika na kuchora kwa ajili ya vitabu vya hadithi, wanafunzi sasa wako tayari kutayarisha gamba la kitabu. Unaweza kutumia migongo ya mabango, karatasi za maboksi na vifaa vingine ‘vilivyotupwa’, hasa kama vifaa havitoshi shuleni kwenu. Tazama Nyenzo-rejea muhimu: Kuwa mwalimu mwenye msaada katika hali zenye changamoto kwa mawazo zaidi.

Waoneshe watoto magamba ya vitabu na waulize sifa nzuri za gamba hilo (Tazama Nyenzo-rejea: Sifa za matayarisho ya gamba la vitabu).

Watake kila kikundi kutayarisha gamba la kitabu chao. Wanapaswa kukubali kuhusu maneno watakayotumia, michoro na sehemu watakapoiweka na kuamua waamue nani ataandika au kuchora kila sehemu ya gamba.

Zungukia vikundi kujadiliana matayarisho yao na wasaidie na kuwaongoza wanapotengeneza gamba lao la kitabu

Vipe muda vikundi kukamilisha vitabu vyao.

Mtake mwanafunzi mmoja wa kila kikundi kuonesha kitabu chao na wahimize wanafunzi wengine katika vikundi kukisoma.

Viweke vitabu katika maktaba ya darasa.

Unafikiri wanafunzi wako wamejifunza nini katika shughuli hii?

Je, vitabu hivyo vilisomwa na wanafunzi wengine vilipowekwa katika maktaba ya darasa?

Kwa watoto wadogo, soma hadithi au mashairi na watake wachore picha kwa ajili ya gamba la kitabu au ndani ya kitabu.

Nyenzo-rejea 1: Jinsi hadithi zinavyoandikwa kuwa vitabu

Usuli wa welewa kwa ajili ya mwalimu

Uandishi wa kitabu kwa ajili ya darasa lako sambamba na shughuli zao za kawaida ili za usomaji na uandishi huwapa wanafunzi welewa wa umuhimu wa kuweza kusoma kupata taarifa na hadithi mpya. Mchakato huu unaweza kuwahimiza wanafunzi wako kutaka kusoma zaidi kwa kuandika kitabu kwa ajili ya darasa kwa kutumia michoro/picha zao na maneno yao wenyewe kadiri wanavyokuwa waandishi hodari.

Hatua ya 1: Vitabu huanza na wazo kuu

Mwandishi huandika hadithi. Huenda mwandishi ataandika rasimu kadhaa za hadithi, akijaribu kuiboresha kila mara. Mara nyingi waandishi hufanya uchunguzi kwa ajili ya hadithi zao kuhakikisha kuwa wanaandika maneno kwa tahijia sahihi na uhakika wa mambo wanayoyaandika. Wakati mwingine inamchukua mwandishi majuma kadhaa kabla ya kupata njia sahihi ya kuandika hadithi yake. Mwandishi anaporidhika, ataandika maneno yake katika muswada, ambayo ataituma kwa mhariri wake katika jumba la uchapishaji

Hatua ya 2:Wahariri wana majukumu mengi, na wanapaswa kusoma SANA.

Miswada hupokelewa kila siku kutoka sehemu mbalimbali za dunia. Wahariri wanapaswa kuichambua na kuamua ni hadithi zipi wanazofikiria kuchapisha. Wahariri hufurahia kuwaambia waandishi kuwa wanataka kuchapisha hadithi zao. Na bila shaka mwandishi husisimka! Mhariri huamua pia nani atachora michoro ya muswada. Si kawaida kufikiri kuwa kwa baadhi ya vitabu mhariri na mchoraji hawakubaliani! Wakati mwingine mhariri husaidia mawasiliano.

Hatua ya 3: Kuanza kazi kwa msanii.

Kabla ya mwandishi kuanza kuandika hadithi, hufikiria ukubwa wa kitabu utakuwaje, halafu hupanga karatasi. Hutengeneza mfano wa kitabu, kikiwa na vielelezo vya awali, ili kumuonesha mhariri na msanii wa kitabu. Katika hatua hii, mhariri anaweza kufanya mabadiliko katika matini ya hadithi. Wahariri ni wazuri katika kuwasaidia waandishi kupata namna bora ya kujieleza.

Hatua ya 4: Kuhusika kwa msanifu wa kitabu.

Msanifu huangalia kitabu cha mfano, na hutoa mapendekezo kwa ya michoro. Hutafuta pia aina za maandishi za kutumia katika kitabu. Mtindo na ukubwa wa herufi unaweza kuleta tofauti kubwa katika muonekano wa kitabu. Msanii anaweza pia kumsaidia mchoraji kuamua jinsi maneno ya hadithi yatakavyofaa katika muono wa kitabu. Halafu hadithi inapelekwa kwa mhariri ili ahakiki tahjia, sarufi, na uandishi wa vituo. Mwandishi anapewa nafasi nyingine ya kubadilisha sehemu yoyote ya hadithi.

Wakati huohuo…..

Hatua ya 5: Msanii anashughulika sana kutunga kazi za mwisho

Hutumia kitabu chake cha mfano kama kiongozi. Lazima karatasi zipimwe kwa usahihi ili achore michoro katika sehemu husika. Huchora alama katika mchirizi ambapo karatasi zitakaposhonwa na kubanwa, na huweka alama katika mikunjo ambapo karatasi zitakatwa.

Sio rahisi! Anahitaji kutengeneza usanii kwa namna itakavyoonekana katika kitabu kilichochapishwa. Inahitajika kuwa kazi nzuri. Mistari inahitajika kuwa nyoofu, na panahitajika kuwepo na nafasi kwa ajili ya maneno ya hadithi.

Wakati kazi hii inapomalizika, anaipeleka kwa mhariri katika shirika la uchapishaji.

Kule, kazi inakaguliwa ili kuhakikisha kuwa hamna makosa, na mkurugenzi wa uzalishaji anafanya makadirio ya gharama itakayotumika kutengeneza kitabu. Anaamua muda wa uchapishaji wa kitabu na kuagiza karatasi.

Hatua ya 6: Kitabu kinapelekwa uzalishaji!

Msanii anaonesha jinsi maneno na michoro itakavyowekwa. Prufu za rangi zinatengenezwa, na kila mmoja anakagua kuhakikisha kuwa rangi zilizochapishwa zinaoana na michoro ya msanii. Hii ndicho kitu wanachokiangalia katika picha hii.

Kila mmoja akisharidhika na jinsi michoro inavyoonekana katika kurasa, visahani vya maandishi ya kuchapisha vinatengenezwa. Visahani hivyo vitatumika katika usindikaji wa uchapishaji kuchapisha kurasa.

Hatua ya 7: Mwisho! Ni wakati wa kuchapisha kitabu

Baada ya miezi ya matayarisho uchapishaji huchukua siku moja tu.

Vijisahani vyembamba (vyenye chapa ya kitabu) vinafungwa kuzunguka silinda kubwa ambayo hupelekwa kwenye mathaa. Kila silinda inachapisha rangi mojawapo kati ya rangi nne za kitabu - ya kwanza ni ya njano, halafu bluu, halafu nyekundu, halafu nyeusi. Rangi nyingine zinatengenezwa kutokana na mchanganyiko wa rangi hizo nne.

kikamatiyo maalum na mikanda wa kuchukulia husaidia kusogeza karatasi kupitia katika mtambo wa kusindika.

Hatua ya 8: Hongera! Dakika ambayo kila mmoja alikuwa akiisubiri imefika

Kitabu kimechapishwa na kimetoka vizuri sana!

Ulijua kuwa karatasi zote za kitabu zimechapishwa katika karatasi moja KUBWA! Nusu ya kurasa zimechapishwa katika sehemu moja ya kurasa za kusindika na nusu nyingine imechapishwa katika kurasa iliyopo kinyume chake. Baada ya karatasi hizi kuchapishwa, zinakunjwa, kukatwa na kufungamanishwa katika kitabu.

Hatua ya 9: Vitabu vipya vinasambazwa!

Vitabu vilivyofungamanishwa vinachukuliwa ghalani, ambapo hutunzwa hadi vinapouzwa katika maktaba na maduka ya vitabu.

Wakutubi na wauzaji wa vitabu wanajuaje kuwa vitabu vizuri vipya vimechapishwa? Watu wengine katika ofisi za uchapishaji huuza na kutangaza vitabu. Wakati mwingine mabango na maonesho maalum hufanywa. Wachapishaji hupeleka nakala za mapitio ya vitabu kwa watu waandishi wa habari. Waandishi mara nyingi husailiwa na waandishi wa habari magazetini na katika televisheni.

Watu wengi hufanya kazi kwa bidii wakijua kuwa siku moja...

Hatua ya 10: …umesoma kitabu!

Watu wote uliokutana nao wanakufikiria na kama utakipenda au hutakipenda kitabu. Mwandishi na wasanii wanakufikiria wakati wanabuni hadithi na michoro. Mhariri na mchoraji vielelezo wanakufiria, pia, wakati wanapotayarisha kitabu. Na WEWE ndiye sababu mtambo wenye kelele wa kusindika vitabu unachapa vitabu kwa ajili yako ili uvisome.

Usomaji mwema!

Imerekebishwa kutoka: How a book is made: Harper Childrens; Website. ThinkQuest, Website. Fact Monster, Website.

Nyenzo-rejea 2: Orodha ya kuhakiki kwa ajili ya wanafunzi - ili kutumika wakati wanapohariri kazi zao kwa ajili ya kitabu

Kwa ajili ya matumizi ya mwanafunzi

Orodha ya kuhakiki hadithi
Hadithi ina kichwa cha habari?
Je, Kichwa cha habari hicho kitawafurahisha wasomaji wa hadithi?
Je, wasomaji wataweza kufuata mtiririko wa matukio katika hadithi (ilitokea nini kwanza halafu kilichofuata ni nini)?
Je, Wahusika na mandhari katika hadithi vimeelezwa vizuri ili wasomaji waweze kupata taswira yavyo?
Je, hadithi inafikia upeo/mwisho?
Orodha ya kuhakiki mashairi
Shairi au wimbo una kichwa cha habari?
Je, kichwa cha habari hicho kitawafurahisha wasomaji wa mashairi au wimbo?

Je, shairi au wimbo una wizani au vina (au vyote viwili)

ambavyo vinawafanya wasomaji wafurahie?

Maneno yameteuliwa vyema kuelezea watu, wanyama, vitu, matendo au hisia?
Orodha ya kuhakiki michezo
Je, mchezo una jina?
Je, maelekezo yana mtiririko sahihi? (kwanza fanya hili ……)
Je maelekezo yako wazi?
Iwapo vitu (kama changarawe au karatasi) vinahitajika katika mchezo, je, vimeorodheshwa?

Nyenzo-rejea 3: Kubadilisha hadithi za wanafunzi kuwa ‘kitabu kikubwa’

Nyenzo ya Mwalimu kwa ajili ya kupanga/kurekebisha na kutumia na wanafunzi

Utakavyohitaji

Makaratasi makubwa ya ‘kuchapia habari’ (karibu 60 sm x 85 sm)

Penseli kubwa ya nta

Penseli

Peni kubwa zenye ncha kali

Sindano kubwa ya kushonea

Kamba nyembamba

Gundi

Vipande vidogo vya karatasi zisizo na maandishi

Karatasi kubwa ya bango au chati

Mwanzo wa hadithi uliowaambia wanafunzi wako

Sehemu iliyobaki ya hadithi, ambayo wanafunzi wamekusomea

Jinsi ya kutengeneza kitabu kikubwa

Kuandika vitabu kunaweza kuwahamasisha watoto kutaka kusoma na kujiandikia zaidi. Kwa watoto wadogo, unahitaji kufanya matayarisho kabla, ukifupisha kazi wanazohusika nazo kwa kuzingatia vipengele maalum (angalia hapa chini). Kwa watoto wakubwa na kwa kuzingatia ujuzi wao, wanaweza kujifanyia kazi zaidi (kama katika Shughuli 2).

  1. Kwanza soma hadithi yote kwa makini na hakikisha ni kamili na vituo vya uandishi vimewekwa kikamilifu.
  2. Amua ni urefu wa matini kiasi gani unaotaka kuandika katika kila ukurasa wenye sehemu mbili. Kama una madarasa ya darasa la kwanza na ni mwanzo wa mwaka wa masomo, utapenda kuhakikisha kuwa hakuna zaidi ya sentensi mbili au tatu kwa kila ukurasa wenye sehemu mbili. Katika baadhi ya sehemu za hadithi huenda ukapenda kuandika aya moja. Kama unafanya kazi na wanafunzi wakubwa, unaweza kuandika zaidi.
  3. Fikiria michoro au vielelezo ambavyo unataka viambatane na matini. Hii itakusaidia kuamua ukubwa wa kitabu, na kitakuwa na kurasa ngapi. 
  4. Chukua kadi yako nyembamba, na ikunje katikati. Hili litakuwa gamba la kitabu chako. Kama kitabu kilichotengenezwa na karatasi za uchapishaji kina gamba gumu, kinadumu kwa muda mrefu.
  5. Andika hadithi yote katika karatasi zenye mistari za ukubwa wa A4 na weka matini kwa kila kurasa yenye sehemu mbili katika mstari mpya.
  6. Kunja kila karatasi mara mbili. Ziweke karatasi pamoja na hakikisha kuwa ni safi, na zinabana vizuri. Usizifungamanishe karatasi pamoja kwanza. 
  7. Sasa amua utakapotaka kuweka matini. Utaiweka kushoto kwa kila ukurasa wenye sehemu mbili zilizotandazwa? Au utaiandika kulia mwa ukurasa? Utaiandika juu ya ukurasa? Au utaiandika chini ya ukurasa? Kila ukurasa wa sehemu mbili utaonekana tofauti? Labda utaamua kuandika toka upande mmoja hadi mwingine katika ukurasa wenye sehemu mbili? Unapaswa kuamua kuhusu hili.
  8. Sasa chukua karatasi zilizokunjwa. Fanyia kazi katika meza kubwa. Tumia kalamu ya nta ya rangi nene na andika kwa unadhifu kipande cha hadithi sehemu ya nje ya karatasi ya kwanza. Andika sehemu ndogo kwa jinsi itakavyoonekana katika ukurasa wa kwanza katika kitabu ambacho ungenunua dukani. Unahitaji kitabu chako kuonekana kimeandikwa na bingwa.
  9. Chini, kwa herufi ndogo andika majina ya wanafunzi wote ambao walishiriki kuandika hadithi, au darasa lako. (Kama ni darasa zima, itakuwa vigumu kuandika majina ya wanafunzi 50 au zaidi, kwa hiyo taja darasa kama majina yote hayawezi kuenea!)
  10. Halafu, fungua ukurasa wa kwanza wa karatasi za magazeti. Huu utakuwa ukurasa wako wa kwanza ulioandikwa sehemu zote mbili. Andika sentensi au aya ya kwanza katika ukurasa huu ulioandikwa sehemu zote mbili, ukitumia kalamu ya rangi nene yenye nta. Unapaswa kuacha nafasi ya kutosha kwa ajili ya vielelezo au michoro.
  11. Unapokuwa umekwisha andika matini katika ukurasa ulioandikwa sehemu mbili, geuza ukurasa mwingine ulioandikwa sehemu mbili, na andika sentensi au virai kwa kalamu y nta ya rangi nyeusi. Endelea hivyo hadi kumalizia kuandika hadithi yote.
  12. Chukua ‘gamba’ la kitabu chako. Unahitaji kuamua ni mahali gani pa kuandika kichwa cha habari. Ni wazo zuri kuacha nafasi kwa ajili ya vielelezo. Utaandika kichwa cha habari juu, au chini? Ukifurahia jinsi kazi ilivyo, rudishia tena maandishi yaliyoandikwa kwa penseli.
  13. Ingiza vizuri karatasi za magazeti ndani ya ‘gamba’.
  14. Sasa shona karatasi pamoja na gamba la kitabu pamoja. Kuna njia tofauti ambazo unaweza kutumia kufanya jambo hili, lakini njia zifuatazo ni bora zaidi:
  15. Fungua kitabu chako ili gamba la kitabu liwe liko chini, na katikati ya kurasa zilizoandikwa sehemu mbili ziko juu. Kwa kitabu kikubwa, ni wazo zuri kuweka alama katika nafasi mbili kwenye mkunjo katikati, ambapo unaweza kushona
  16. Weka alama juu katika nusu ya mkunjo, na weka alama ya pili katika nusu ya chini. Katika kila sehemu, tengeneza alama tatu. Alama hizi ziwe na nafasi ya sentimita 4.
  17. Tunga uzi mwembamba katika sindano wenye urefu wa sentimita 50. Ingiza ncha ya sindano katikati ya seti ya alama zile tatu, katika kurasa zote pamoja na gamba lake. Vuta uzi , lakini acha kipande cha uzi chenye urefu wa kama sentimita 7 kikining’inia na fuata chati. Kata uzi ulioshikizwa katika sindano, karibu sentimita 7 kutoka mahali ulipopenyeza kwenye karatasi. Sasa funga kwa uthabiti nyuzi za sehemu zote mbili za urefu wa sentimita 7.
  18. Rudia mchakato huu nyuma ya mkunjo.
  19. Tengeneza orodha ya vielelezo unavyotaka. Amua kama unawataka wanafunzi fulani kutengeneza vielelezo, au unataka darasa lako zima kuhusishwa. Wanafunzi wanaweza kufanya vizuri wakiwa wawiliwawili kutengeneza picha. Panga jinsi ya kutengeneza michoro.
  20. Uchaguzi wa picha. Soma , pamoja na wanafunzi wako matini yote. Fungua kurasa na soma hadithi kwa sauti. Isome hadithi kwa namna ambayo itafurahisha.
  21. Waeleze wanafunzi wako kuwa unawataka kuchora picha. Usomapo hadithi kwa mara ya pili, sita kwa muda kwa kila kurasa zenye sehemu mbili na jadili kuhusu picha inayotakiwa. Wewe na darasa lako mnapofanya uamuzi kuhusu picha inayotakiwa kwa kila ukurasa, gawia kila kielelezo kwa mwanafunzi fulani, au wanafunzi wawiliwawili.

Wape muda kutengeneza picha vizuri. Wahusishe wanafunzi kushughulikia yaliyomo kwenye kitabu. Hata wanaoanza kusoma wanaweza kukariri hadithi, na wana taarifa ya kila picha inapopaswa kuwekwa. Chini ya picha hiyo, andika majina ya wanafunzi walioichora. Endelea kwa njia hii hadi picha zote zigandishwe na kuwekewa jina.

Wakati ambapo vielelezo vyote vimekwishagundishwa, soma kitabu pamoja na wanafunzi wako. Tuna hakika kuwa wewe na wanafunzi wako mtajivunia juhudi zenu.

Imerekebishwa kutoka: Umthamo 2, University of Fort Hare Distance Education Project

Nyenzo-rejea 4: Sifa za usanifishaji wa gamba la kitabu

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Imetolewa kutoka: Nancy Keane, Website.

Kinachovutia machoni – msomaji huvutiwa na ‘sura’ ya gamba la kitabu

Kichwa cha habari kinawekwa mahali pazuri na kinaonekana waziwazi

Kichwa cha habari kinawahimiza wasomaji kukifungua

Maneno ya kichwa cha habari na majina ya waandishi ni rahisi kusomeka.

Matumizi ya rangi yanamvutia msomaji.

Matumizi na sehemu za kurasa zilipowekwa sanamu (michoro au picha) zinavutia msomaji na sanamu hizi ‘zinahusishwa’ na kitabu.

Kuna nafasi wazi katika gamba la kitabu ili michoro isiwe imejazana.

Chanzo: Two Bookmark; Website.