Ruka hadi kwa yaliyomo
Printable page generated Jumatano, 11 Des 2024, 22:15
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Jumatano, 11 Des 2024, 22:15

Namba ya moduli 3: Uhamasishaji wa mawasiliano katika lugha ya ziada

Sehemu ya 1: Kuandaa mazingira asilia kwa ajili ya mazoezi ya lugha

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya muundo wa lugha katika mazingira asilia?

Maneno muhimu: usimamizi wa darasa; michezo; mapishi; maelekezo; mchakato

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • Kutumia uongozi/utawala wa darasa kuwasaidia wanafunzi kujifunza lugha ya ziada;
  • Kutumia michezo na shughuli za kila siku kuimarisha wanafunzi kuhusu stadi za lugha na msamiati.

Utangulizi

Wanafunzi wako wana fursa gani kupitia –redio, vitabu, magazeti, wazungumzaji wa lugha na televisheni kwa lugha ya ziada ukilinganisha na ile inayotumika nyumbani?

Jawabu linaweza kuwa ni ‘fursa ndogo’. Wanaisikia na kuitumia kila siku darasani shuleni. Hii ina maana kuwa unawajibika kuwapa fursa ya kutumia lugha ambayo itawasaidia wanafunzi:

Kuitumia na kuwa wazungumzaji hodari katika matumizi ya msamiati mpya na muundo wa sarufi;

Kuwasiliana kwa kutumia lugha ya mazungumzo katika mazingira ya kijamii;

Kuimarisha na kuendeleza stadi zao za kusoma na kuandika.

Yote haya yanahitaji tafakuri ya hali ya juu, na upangaji na stadi makini. Sehemu hii itakupatia mikakati na mbinu za kukusaidia.

Somo la 1

Ukiwa mwalimu, utatoa maelekezo ya aina mbalimbali kwa wanafunzi wako.

Unaweza kutumia maelekezo ya kila siku kukuza msamiati mpya na stadi ya usikilizaji katika lugha ya ziada. Maelekezo hutumia muundo wa amri wa kitenzi. Wakiona muundo wa kuamuru katika kitenzi mara kwa mara katika mazingira yanayoleta maana, wanafunzi wataanza kuelewa na kujifunza muundo huo.

Wanafunzi wanapojifunza lugha mpya, usikilizaji huendelea haraka kuliko mazungumzo. Wanahitaji nafasi kubwa ya kusikiliza na kujibu katika lugha mpya. Katika hatua za mwanzo za ujifunzaji lugha (na baadaye pia), unaweza kutumia shughuli ambazo zinawahitaji kujibu kwa vitendo lakini haiwahitaji kujibu (kwa maneno) hadi wanapojisikia kuwa na uhakika zaidi. (Hii mara nyingi huitwa ‘mawazo ya mbinu jumuishi’- Angalia Nyenzo-rejea 1: Mawazo ya mbinu jumuishi .)

Uchunguzi kifani ya 1: Uongozaji wa darasa katika Kiingereza

Bibi Mujawayo anafundisha darasa la kwanza mjini Kigali, Rwanda. Anatumia Kiingereza katika uendeshaji wa darasa.

Asubuhi husalimiana na wanafunzi katika lugha zao za nyumbani, na huwauliza habari zao za nyumbani katika lugha zao.

Baada ya baraza, huanza kutumia Kiingereza darasani, ‘Pangeni mstari wanafunzi’ na huwaelekeza barazani, mahali ambapo wanapaswa kujipanga. ‘Ingia darasani’ husema huku akiwaonesha vitendo vya kuwaelekeza kuingia ndani. ‘Simameni karibu na madawati yenu.

Mwalimu na wanafunzi husalimiana kwa kutumia Kiingereza. Husema ‘Kaeni chini.

Hurejea tena katika lugha yao ya nyumbani ili kuanza kusimulia hadithi hadi anapowaweka katika vikundi, kwa ajili ya shughuli mbalimbali.

Kila kikundi kina alfabeti. Husema kwa Kiingereza kwa kunyoosha mikono A na B nyosheni mikono. Kwa kuonesha katika kisanduku huwaambia ‘Chukueni vitabu kutoka katika kisanduku.’ ‘Kaa chini, na msomee mwenzio.’ Kama wanaonekana kutoelewa, wanaigiza wanachopaswa kufanya.

Baadaye hutoa maelekezo zaidi kwa Kiingereza, bila kutafsiri. Vikundi viwili vinapaswa kuonesha hadithi yao na kikundi kingine watasoma pamoja naye katika lugha yao ya nyumbani kutoka katika kitabu kikubwa.

Bibi Mujawayo anagundua kuwa wanafunzi wake wanaanza kuelewa haraka maelekezo katika Kiingereza, na mara huanza kusema maneno.

Shughuli ya 1: Simple Simon husema

Katika mchezo huu unaojulikana sana, wanafunzi hufuata kwa vitendo maelekezo. Unaweza kutumia njia hii kuongeza msamiati na stadi ya usikilizaji katika maeneo mbalimbali ya masomo.

Kiongozi hutoa amri na kuonesha vitendo wakati huohuo. Wanafunzi wanapaswa kufuata amri hiyo kutoka kwa Simple Simon. (Unaweza kubadilisha jina hili kwa kutumia jina la mtu ambaye ni mashuhuri kijijini.) Mchezo huchezwa kama hivi:

Kiongozi: Simple Simon anasema , ‘Ruka!’ (Kiongozi anaruka.)

Wanafunzi wanaruka.

Kiongozi: Simple Simon husema, ‘Shika vidole vya miguu !’ (Kiongozi anashika vidole vya miguu)

Wanafunzi wanashika vidole vya miguu.

Kiongozi: ‘Kuna pua yako!’ (Kiongozi anakuna pua yake.)

Baadhi hukuna pua zao. Wengine hawafanyi hivyo. Wale ambao wamekuna pua zao wanatoka (kwa sababu amri haikutoka kwa Simple Simon Na kuendelea hivyo….. Tumia maelekezo rahisi kwa wanafunzi wanaojifunza lugha ngeni, maelekezo magumu kwa wale ambao ni wanaielewa lugha zaidi. Anza polepole, lakini endelea kwa kasi zaidi. Mshindi ni yule aliyebaki.

Somo la 2

Ni jambo muhimu kuwapa wanafunzi nafasi ya asilia ya kuendeleleza stadi zao katika lugha ya ziada. Hapa tunapendekeza njia ambazo unaweza kuzitumia kushirikisha jamii na kutumia stadi za asilia na busara kama njia ya Nyenzo-rejea ya shughuli za darasani.

Umeona, katika Uchunguzi-kifani 1 na shughuli 1, namna maelekezo ya kila siku yanavyoweza kuleta muktadha asilia wa ujifunzaji lugha. Wanafunzi walisikiliza na kuonesha uelewa kwa vitendo. Katika sehemu hii tunashauri utumie mapishi ya asilia na mchakato kama njia ya muktadha wa mafunzo, ukiwapa nafasi wanafunzi kuzungumza (na kuandika) na vilevile kusikiliza.

Shughuli zilizotumika hapa zitaendelezwa mbele katika sehemu ya 5, ambapo darasa lako litaanza kutayarisha kitabu cha mapishi.

Uchunguzi kifani ya 2: Wanafunzi watu wazima hujifunza kwa vitendo

Baadhi ya wanafunzi wa Kiswahili walitumia muda wa siku nzima mjini kama sehemu ya kozi yao. Kila mwanafunzi alikuwa akifuatana na msaidizi wa lugha ambaye alikuwa mzungumzaji wa Kiswahili. Wasaidizi waliwasaidia wanafunzi walipokuwa wakijaribu lugha waliojifunza; wakinunua mboga kutoka kwa wauzaji wa barabarani na kuzungumza na familia zilizokuwa zinawasaidia.

Sehemu muhimu ya siku hiyo ilitumika kupika chakula. Mwanafunzi alipaswa kupika chakula, akielekezwa na msaidizi wa lugha. Upikaji ulikuwa umefanyiwa mazoezi na kuigizwa, na mara nyingi kuandikwa au kurekodiwa katika kinasa sauti, wiki moja kabla darasani. Wanaume walipewa maelekezo ya kutayarisha moto, wakati wanawake walitakiwa kupika chakula kama ugali, ndizi na nyama na kabichi. Walizungumzia pia jinsi ya kubadilishana nafasi ili kuwasaidia kujifunza lugha.

Wakati chakula kilipokuwa tayari, nyimbo za Kiswahili ziliimbwa, na wanafunzi walijifunza michezo ya asili ya Kiswahili ya watoto. Baada ya vyombo kusafishwa, kundi la wanafunzi wenye furaha na uchovu walijipakia katika teksi na kurudi nyumbani.

Shughuli ya 2: Kujifunza kwa vitendo vya shughuli za kijamii

Waambie wanafunzi wako kwamba watakwenda kutafuta jinsi shughuli za nyumbani zinavyotekelezwa na kueleza njia za mchakato katika lugha ya ziada. Watake wanafunzi kuleta taarifa kutoka nyumbani au mkaribishe mwenyeji shuleni kutoka katika jamii ili kuonesha stadi.

Wagawane wanafunzi katika jozi au katika vikundi (vikundi hivi vinaweza kuwa vya mchanganyiko wa uwezo tofauti), kufanya kazi, na ikiwezekana kuandika hatua za moja ya mchakato katika lugha ya ziada. Zungukia darasa na kuwasaidia msamiati mpya ambao watuhitaji.

Vipe vikundi muda wa kukariri na kufanya mazoezi ya hatua zinazotumika, katika kujitayarisha kuwasaidia wengine. Wanaweza kukusanya toka nyumbani vitu vinavyohitaji katika mchakato huo.

Siku inayofuata, mpe nafasi mwanafunzi mmoja kutumia lugha ya ziada kuelekeza mjumbe wa kikundi kingine, wakati huohuo darasa likiangalia k.m. kusafisha nyumba.

Wanafunzi wamefanyaje katika shughuli hiyo?

Unaweza kuitumia njia hiyo katika mchakato mwingine ili kukuza msamiati wao?

Kama jibu ni ndiyo, vipi?

Somo la 3

Lugha hutumika kwa mawasiliano, na ni muhimu uwe na sababu za wanafunzi kuzungumza, kusikiliza, kusoma na kuandika katika lugha ya ziada. Hii si rahisi ukiwa katika mazingira ambapo lugha ya ziada haizungumzwi. Hata hivyo, lugha ya ziada inaweza kuwa lugha ya vitabu na ya mawasiliano ya maandishi.

Duniani kote watu hubadilishana mawazo kuhusu ‘jinsi ya kufanya shughuli’; kwa mfano wanapeana maelezo ya upishi au sulubu ya utengenezaji wa nguo. Umekwisha kulifanya hili kwa mazungumzo; sasa wanafunzi wanaweza kufanya kwa maandishi. Waoneshe wanafunzi wako muundo wa kawaida wa maandishi ya maelezo ya upishi, katika lugha ya ziada. Maelezo ya upishi huandikwa kama mfululizo wa maelekezo.

Tunapoandika maelezo ya upishi, au kuelezea mchakato wake, hatujali nani atatenda, bali tunajali kuwa tendo linatendeka.

Uchunguzi kifani ya 3: Kuchora na kuandika maelezo ya upishi

Katika shule iliyopo Njombe, kusini mwa Tanzania wanafunzi wamekuwa wakibadilishana maelezo ya upishi. Walitaka kuchora maelezo ya upishi katika michoro na kubadilishana na marafiki zao. Bibi Masawda, mwalimu wao, alifikiri kuwa itakuwa vizuri kwao kujua njia mbalimbali za kuwasilisha taarifa. Aliwaonesha jinsi ya kuchora michoro ya kuonesha mifumo. Mara wanapokuwa wamekwisha chora na kuweka maelezo katika mchoro wa mfumo, waliandika mchakato kama pia maelezo (angalia kwa mfano Nyenzo-rejea 2: maelezo ya upishi ).

Bibi Masawda alijadiliana na wanafunzi wake ni kipi walichokiona ni rahisi kufanya, na kwa nini. Zaidi ya theluthi mbili za darasa waliona kuwa chati ya mfumo ilikuwa inafurahisha na ilikuwa rahisi kutengeneza kwa sababu waliweza kubadilisha maelezo ya upishi katika hatua na mchoro uliwasaidia kukumbuka na kuelewa maneno.

Bibi Masawda alitumia wazo hili la chati za mifumo katika masomo mengine, kwa kuwa hili lilionekana kuwasaidia wanafunzi wake kukumbuka zaidi.

Kwa mfano, katika somo la jiografia, alitumia chati ya mfumo kuandika kuhusu maelekezo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, na wanafunzi walichora picha za alama za mipaka ili kuifanya iwe rahisi kukumbuka maneno.

Shughuli muhimu: Kuandika maelezo ya upishi na mchakato wa maelezo

Watake wanafunzi kutafuta jinsi ya kupika vyakula vyao wanavyovipenda sana kutoka nyumbani na shirikiana mawazo hayo na darasa.

Wajulishe wanafunzi wako muundo wa maandishi ya mapishi kabla hawajafanya mfano wao (Angalia Nyenzo-rejea 2)

Watake wanafunzi kuandika maelezo ya mapishi vizuri, kila mmoja akijiandikia maelezo, na mwingine akitumia maelekezo ya mapishi ya kitabu cha darasani. Maelezo ya pili yanaweza kutumia muundo tofauti na ule wa kwanza (angalia Nyenzo-rejea 2 kwa ajili ya mitindo).

Watake wanafunzi wako wabadilishane kazi zao na kujadili maelezo ya mapishi.

Nyenzo-rejea ya 1: Mjumuisho wa mwitikio wa vitendo

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Kwa toleo la mtandaoni:

http://www.tpr-world.com/

Webu inatoa taarifa kuhusu mjumuisho wa mwitikio wa vitendo kama njia ya kufanya kazi katika ujifunzaji lugha. Kuna maelezo mengine ambayo unaweza kufuatilia.

Kwa ajili ya kuhariri matini

Unaweza kuwajulisha wanafunzi wako muundo wa lugha mbalimbali kutokana na vitendo vya kimchezo ambavyo vinawahitaji kufuata maelekezo kwa vitendo (mjumuisho wa mwitiko wa vitendo). Hapa kuna mifano ya namna ya maelekezo ambayo unaweza kuwapa wanafunzi. Weka mkazo katika aina moja ya maelekezo kwa wakati mmoja, ili wanafunzi waelewe jinsi lugha inavyofanya kazi

Mtingishiko wa mwili

Simama.

Cheka.

Kohoa.

Lia.

Gonga meza.

Vitendo na vifaa

Onesha mlango.

Okota kalamu.

Funga dirisha.

Nusa ua.

Onesha mlima.

Onesha mwanamke anayetengeneza keki.

Vitendo, vifaa na watu

Chukua kalamu na umpe Nuru

Tafuta kitabu na unipe

Okota karatasi na mpe Thimba.

Ongeza vimilikishi

Mpe Aida kitabu cha Thimba.

Leta peni ya Nuru kwangu

Mpe Kito kitabu chake.

Mpe Eshe miwani yake.

Hiki na kile; hapa na pale

Mpe hiki Adia.

Tafuta kile kutoka kwake.

Tafuta kalamu na iweke hapa.

Tafuta kitabu na kiweke pale.

Kuhusisha nafasi

Weka kalamu katikati ya vitabu viwili.

Weka kalamu karibu na rula.

Weka kifutio ndani ya kisanduku.

Weka rula juu ya kisanduku.

Jumlisha namba, ziweke rangi na ukubwa

Weka kalamu mbili ndani ya kisanduku.

Chukua mawe matatu nje ya kisanduku.

Okota kalamu nyekundu na mpe Thimba.

Weka kitabu cha kijani mezani.

Chukua kitabu kidogo na mpe Nuru.

Weka kitabu kikubwa ndani ya kisanduku.

Maelekezo na maelezo, pamoja mazungumzo kiasi

Fanya na kusikiliza

Wanafunzi wanafanya tendo. Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) husema wanachofanya (k.m. ‘Umesimama.’)

Sikiliza na kufanya

Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) anamuelekeza mwanafunzi (k.m. Simama.’ Mwanafunzi anafuata amri, kwa kufanya tendo.

Sahihi au si sahihi

Mwanafunzi anajifunza kusema ‘sahihi’ na ‘si sahihi’. Mwalimu (au mwanafunzi mwingine) anatenda tendo, na kutoa tamko ‘lililo sahihi’ au ‘lisilo sahihi’ kuhusu anachofanya (k.m. ‘Nimekaa.’) Wanafunzi wanasema ‘kweli’ au ‘si kweli’

Sikiliza, igiza na tenda

Mwalimu (au mwanafunzi mwingine)anamuelekeza mwanafunzi. Mwanafunzi anarudia yaliyosemwa na halafu anatenda amri hiyo.

Eleza, sikiliza na igiza

Mwanafunzi hutenda na kueleza wanachofanya (k.m. ‘Nimesimama.’) Mwalimu ( au mwanafunzi mwingine) anaeleza kile kilichosemwa na mwanafunzi na anatekeleza kitendo.

Kwenda nje au kutumia picha ili kuongeza msamiati

Mwanzoni, unahitaji kutumia maneno yanayojulikana na maelekezo mapya. Baada ya msamiati wa darasa kujulikana, unaweza kutumia msamiati wa nje ya darasa, k.m.:

Gusa jani.

Onesha mbingu.

Unaweza pia kuongeza msamiati kwa kutengeneza kadi zenye maneno au picha, k.m. picha za aina ya chakula:

Chukua nyama na mpe Nuru.

Tafuta mkate wa Kapuki na unipe.

Zimetolewa kutoka: Total Phsyical Response Worldwide, Website

Nyenzo-rejea 2: Mapishi

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Hapa kuna njia tatu za kuonesha mapishi ya aina moja

Kutengeneza supu ya pilipili (mchoro mfumo)

Osha na kata nyama katika vipande vidovidogo

Pika/Chemsha nyama katika maji ya moto

Kata vitunguu, nyanya na pilipili

Weka vitunguu vilivyokatwa, nyanya na pilipili kwenye nyama na koroga

Tia maji mengi ya kutosha kiasi cha kufunika mchanganyiko na iache ichemke katika moto mdogo

Safisha, osha, katakata na kuongeza mboga nyinginezo

Iache ichemke polepole hadi nyama inapokuwa laini

Kula kwa wali

Kutengeneza supu ya pilipili (maelezo ya mchakato)

Wakati supu ya pilipili unapotayarishwa, 0.5 ya nyama inasafishwa na kukatwa katika vipande vidogo vidogo. Nyama inapikwa katika maji moto, na vitunguu, nyanya, mboga na pilipili zinaongezwa. Zinachemshwa hadi zinakuwa laini; halafu zinaliwa kwa wali.

Kutengeneza supu ya pilipili (viungo na mbinu)

Viungo:

0.5 kg ya nyama (iliyooshwa na kukatwa katika vipande vidogo)

Vitunguu 4

Nyanya 8

Pilipili zilizokaushwa 4 hadi 5

Mboga nyinginezo, zinazopatikana

Lita 1.5 ya maji

Mbinu: Weka maji katika sufuria na yachemshe Ongeza vipande vya nyama na chemsha Ongeza vitunguu vilivyokatwa, nyanya, pilipili na mboga nyinginezo, koroga na acha ichemke.

Sehemu ya 2: Njia zijengazo ufasaha na usahihi

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kujenga hali ya kujiamini katika utumiaji wa miundo ya lugha mahsusi?

Maneno muhimu: vitenzi; vielezi; urudiaji; mashairi; nyimbo; uhariri

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umewaongoza wanafunzi wako katika kuwapa ujuzi wa kudhibiti miundo ya lugha ya ziada;
  • umetumia urudiaji, nyimbo, mashairi na hadithi katika kufundisha miundo ya lugha;
  • umewasaidia wanafunzi wako kusimamia kazi yao wenyewe kadri wanavyotafuta maana na matumizi sahihi ya vitenzi.

Utangulizi

Ukiwa mwalimu wa lugha ya ziada, mara zote unatakiwa utafute mbinu mpya za kuwapa wanafunzi wako uzoefu wa lugha hiyo. Kama wanapewa fursa za kujizoeza lugha hiyo, matumizi yao ya lugha hiyo yatakuwa fasaha na sahihi zaidi.

Sehemu hii inakupatia mazoezi yanayofaa ambayo yanalenga katika kauli na miundo mahsusi.

Kumbuka kwamba vitendo utakavyovichagua ni lazima viwe vinafahamika kwa wanafunzi, ama kitendo chenyewe, au katika maisha yao (inapendelewa viwe vinavyohusu sehemu zote mbili).

Somo la 1

Kuwapatia wanafunzi wako fursa za kutumia miundo ya lugha mahsusi tena na tena ili waweze kuimudu, kunahitaji kuwa tendo la kufurahia.

Kuna nadharia isemayo kwamba watu hujifunza lugha kwa kuiga na urudiaji. Hapo zamani, kozi nyingi za lugha zilitumia sehemu kubwa ya urudiaji (mazoezi ya kurudiarudia). Siku hizi inadhaniwa kwamba vitendo vinavyowahusisha wanafunzi katika mawasiliano ‘halisi’ vinawasaidia zaidi kuliko urudiaji usiokuwa na maana. Hata hivyo, urudiaji bado unaweza kuwa wenye manufaa endapo wanafunzi watachomeka maana halisi katika sentensi. Inasaidia kama watawekewa urudiaji katika muziki.

Jaribu mawazo yaliyomo katika Uchunguzi-kifani 1 na Shughuli 1 kupima nadharia hizi.

Uchunguzi kifani ya 1: Urudiaji katika lugha unaohusu hadithi kutoka gazetini

Bwana Gasana anafundisha Kiingereza Darasa la 4 huko Butare, Rwanda. Mauaji yalitokea katika jiji lao, saa 2 usiku, siku mbili zilizopita. Aliwaonesha wanafunzi wake ripoti ya mauaji hayo kutoka kwenye gazeti. Alizungumza na wanafunzi wake (kwa lugha ya nyumbani) kuhusu jinsi askari wa upelelezi wanavyouliza watu wanapojaribu kutafuta mhalifu. Halafu akaweka sampuli ya swali na jibu ubaoni, kwa Kiingereza:

Q: Ulikuwa unafanya nini Jumanne saa 2 usiku, Kigeri?

A: Nilikuwa ninatazama runinga.

Aliwauliza wanafunzi wachache swali hilo hilo, ili kuhakikisha watatoa majibu yao wenyewe kwa utaratibu sahihi. Kisha, aliwaweka wanafunzi katika makundi ya wanafunzi sita sita. Kila mwanafunzi alitakiwa kuuliza swali kwa wanakikundi wake wengine watano, ambao kila mmoja atatoa jibu lake. Bwana Gasana aliwahimiza wanafunzi kusahihishana, na alitembea kuzunguka darasa, kusikiliza na kuongoza makundi.

Alimwambia kila mwanafunzi aandike ‘ripoti ya askari wa upelelezi’ kuhusu kundi lake. Kila moja kati ya sentensi sita zilionekana katika muundo ufuatao:

Saa 2 usiku Muteteli alikuwa anacheza na kaka yake.

Saa 2 usiku Erisa alikuwa anaandaa chakula.

Nyenzo-rejea 1: Miundo mbadala ya somo inatoa sampuli zilizotumiwa na Bwana Gasana akiwa na wanafunzi wake wakubwa wa Darasa la 5.

Shughuli ya 1: Urudiaji katika bei mbalimbali

Tafuta au tengeneza tangazo la mauzo au orodha ya bei za mbogamboga za mahali hapo, ukionesha mapunguzo ya bei (angalia Nyenzo-rejea 2: Tangazo la bei kwa mifano). Kabla ya somo, tengeneza nakala kubwa ya tangazo au orodha ya bei ubaoni, au tayarisha tangazo moja au orodha ya bei kwa kila kundi katika darasa lako.

Andika mfuatano ufuatao wa swali na jibu ubaoni.

Q: .…. ni bei gani ?

A. Kabla ilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu.

Q: Hizo …. ni bei gani?

A: Kabla zilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu.

Wakati wa somo, onesha baadhi ya bidhaa, huku ukiuliza swali kulingana na bidhaa, na kuwaambia wanafunzi wachache wajibu.

Kisha, waweke wanafunzi katika makundi, ili waulizane na kujibizana kwa utaratibu huo huo.

Waambie kila kundi watunge na kuigiza wimbo wenye mistari yenye muundo huu: Kabla, hiyo …. ilikuwa shilingi …., lakini sasa ni shilingi …. tu. 

Wanafunzi wako wamejifunza nini kutokana na shughuli hizi? Unajuaje? Je, utatumia aina hii ya zoezi tena?Kwa nini utalitumia tena, au kwa nini hutalitumia tena?

Somo la 2

Katika ufundishaji wa lugha ni muhimu kuzingatia maana ya lugha, kwa kukazia umuhimu wa mawasiliano, lakini wakati huohuo, kukazania ukuzaji wa uwezo wa kisarufi wa wanafunzi. Shughuli 2 inatoa mfano wa jinsi ya kutumia shairi la kusifu lililoandikwa kwa Kiingereza kufanyia kazi na wanafunzi kwa upande wa vitenzi na vielezi. Aina hii ya kazi inaweza kufanywa kwa kutumia matini za viwango mbalimbali, kwa kuzingatia viwango vya miundo mbalimbali. Vilevile, hakikisha kwamba unazingatia maana ya kipande cha maandishi, ingawa usitumie maana hiyo kwa urahisi tu kama nyenzo ya kufundishia sarufi. Ukiwa na wanafunzi wa umri mdogo, mkazo uwe kwenye maana na ufurahishaji.

Kwa kawaida hadithi hutumia njeo iliyopita, wakati maelezo aghalabu hutumia njeo iliyopo. Haya ni mazingira mazuri ya kuwapatia wanafunzi wako mazoezi ya njeo.

Kama hufundishi Kiingereza, fikiri kuhusu mada ya kisarufi ya lugha unayofundisha iliyo ngumu kwa wanafunzi, na utumie Shughuli 2 kulingana na lugha hiyo.

Uchunguzi kifani ya 2: Kujadili sarufi katika warsha ya walimu

Katika warsha iliyofanyika Tanga, walimu walikuwa na majadiliano changamfu kuhusu sarufi. Bwana Thomas Changae alishuhudia kuwa alisoma kwamba sarufi ni mifupa au kiunzi cha lugha na maneno mengine ni nyama. Vyote viwili mifupa na nyama vinachangia katika maana. Walimu walikubaliana kwamba wanafunzi wanahitaji kuendeleza welewa wao wa jinsi miundo ya lugha inavyofanya kazi, lakini pia walilalamika kuhusu wanafunzi kutopenda masomo ya sarufi.

Bi Susan Mkari alisema alijaribu kuhusisha shughuli ambazo zilikazia kwenye miundo ya lugha wakati wanafunzi wake wa Darasa la 6 wanaposoma hadithi na mashairi ya kuvutia. Kwa mfano, baada ya kufanya marudio ya njeo kuu za kitenzi cha Kiingereza, aliwaambia wanafunzi kutoa maoni yao kuhusu sababu za mwandishi wa hadithi au shairi kutumia njeo iliyopita, ya sasa au ya wakati ujao. Kisha, aliwaambia wanafunzi kuamua njeo ipi ya kitenzi au njeo zipi wanazihitaji katika kuandika hadithi au shairi lao wenyewe ili kuleta mvuto zaidi kwa wasomaji wao.

Kwa kuwa Kiingereza ni lugha ya ziada kwa wanafunzi, Bi Mkari hutengeneza chati kubwa nyuma ya kalenda za zamani. Hii huwapa wanafunzi taarifa kuhusu njeo mbalimbali za vitenzi kuhusu wakati uliopo, uliopita na ujao. (Angalia Nyenzo-rejea 3: Chati za njeo za kitenzi kwa mfano rahisi ambao unaweza kutumia na wanafunzi wako.) Anawahimiza wanafunzi wake kusoma chati hizi wanapoandika.

Shughuli ya 2: Mchezo wa ugunduzi wa kitenzi na kielezi

Toa nakala za Nyenzo-rejea 4: Shairi la kusifu . Mahali ambapo mashine za kutolea nakala hazipo, nakili shairi ubaoni au sehemu ya nyuma ya kalenda.

Mara wanafunzi watakaposoma shairi na kulielewa, waache wafanye kazi kwenye makundi kwa kutafuta vitenzi vyote vilivyomo katika shairi. Wakumbushe wanafunzi kwamba vitenzi vingi ni maneno ‘yanayoonesha kutenda’. Waambie kila kundi kuripoti mbele ya darasa kuhusu vitenzi katika ubeti mmoja (angalia Nyenzo-rejea 5: Vitenzi na vielezi katika shairi ).

Waulize wanafunzi vitenzi viko katika njeo gani. Katika ubeti wa 1 na 2, vitenzi viko katika njeo iliyopo; baadhi ya vitenzi katika ubeti wa 3 viko katika njeo ijayo na vingine katika ubeti wa 4 viko katika njeo iliyopita. Kwa wanafunzi wa kiwango cha juu zaidi, jadili kwa nini njeo hizi zilitumika.

Waulize kuna tofauti gani kwenye maana inayosababishwa na utumiaji wa njeo tofauti na athari yake kwa shairi?

Unaweza kutumia mashairi na hadithi nyingine kwa njia zinazofanana na hizi.

Somo la 3

Yumkini utakuwa umegundua kwamba ni vigumu, wakati mwingine, kusahihisha kazi zilizoandikwa na wanafunzi, kwa sababu kuna makosa mengi sana ya lugha ndani yake. Hutakiwi kuwavunja moyo wanafunzi wako kwa kufanya masahihisho mengi kupita kiasi. Lakini pia hutakiwi kuwaacha waendelee na tabia mbaya. Tutatatuaje tatizo hili?

Njia mojawapo ni kuunganisha maana na miundo ya lugha. Andaa zoezi la kuandika ambalo lina maana kwa wanafunzi. Wahimize wahariri kazi zao kabla hawajazikusanya. Unaweza kuwaambia, wawili wawili, waandike ili waweze kusaidiana. Kisha wanaweza kurudishiwa kazi zao bila kuwa na maoni mengi ya kiusahihishaji.

Unaposahihisha kazi zao, zingatia kwenye maana na jambo linalopendelewa. Uzingativu wa pili, kazia kwenye kipengele kimoja cha muundo wa lugha –tahajia au pengine njeo za kitenzi au viunganishi. Kwa njia hii, maoni ya kiusahihishaji huwa si mengi na huelekeza sehemu maalum, na wanafunzi wana uwezekano mkubwa wa kuyaona na kuyazingatia.

Uchunguzi kifani ya 3: Kubadilishana uzoefu katika ‘Gurudumu la Waandishi’

Kozi ya kundi la walimu waliomo kwenye mafunzo kazini mjini Tabora walikuwa wakijaribu kuboresha uandikaji wao wenyewe. Wakufunzi waliwahimiza kuunda ‘Gurudumu la Waandishi’, ambako watasomeana kazi zao na kupeana maoni. Waliandika kuhusu uzoefu wao –kumbukumbu za utotoni, watu na mahali pa ajabu wanapopakumbuka, mambo ambayo hawatayasahau.

Wakufunzi waliwaongoza katika utoaji wa maoni, kwa kutumia vigezo mbalimbali kutegemeana na kitu kilichokuwa kimeandikwa. Hii hapa ni mifano:

Je, mwandishi anakisema akitakacho kwa ufasaha? Je, kuna sehemu ambazo zinahitaji kufafanuliwa?

Sehemu zipi zinavutia? Kitu gani kinazifanya zivutie? Sehemu gani zinachusha? Zinawezaje kuboreshwa?

Je, kila aya ina wazo kuu? Je, kuna baadhi ya mawazo makuu yanayohitaji kuendelezwa zaidi? Je, aya zinahitaji kupangwa tena?

Je, sentensi ni kamilifu? Je, ni ndefu sana au fupi sana? Je, zimewekewa alama za uandishi kwa usahihi? Je, tahajia za maneno ni sahihi?

Kazi hiyo imeandikwa kwa kutumia njeo ipi? Kagua ili kuhakikisha kwamba kila kitenzi kiko katika njeo stahili au kama kuna sababu ya msingi ya kutumia njeo nyingine.

Kitabu kiliwekwa pamoja kwa kujumuisha maandiko ya walimu hawa ambacho kilshirikishwa kwa familia na rafiki. Walimu waliamua kwamba baadhi ya mawazo haya yanaweza kutumika darasani, vikabadilishwa kulingana na umri na uwezo wa wanafunzi wao.

Shughuli muhimu: Uhariri wa kujifanyia mwenyewe na wa kubadilishana na wanadarasa kwa lengo la kuboresha uandishi

Waambie wanafunzi wako waandike kuhusu jambo linalotokana na uzoefu wao wenyewe. Jadili mawazo yatakayojitokeza ili kusisimua ubunifu wao. Kwa mfano, wanaweza kueleza kitu ambacho ni mali yao au mtu wa kuvutia wanayemfahamu. (Kwa kuwa uandishi huu ni wa kutoa maelezo, ni yumkini wakatumia njeo iliyopo.) Wanaweza kusimulia hadithi ya kutisha au tukio la kusisimua, au jambo la kijumuiya. (Kwa vile uandishi huu unajumuisha hadithi au masimulizi, ni yumkini wakatumia njeo iliyopita.) Wanafunzi wengine wanaweza kuona inasaidia zaidi kufanya kazi hii wawili wawili.

Kisha, waambie wafanye kazi katika makundi madogo madogo, kwa kusomeana maandishi yao. Watake watumie mojawapo au zote mbili kati ya seti za maswali zifuatazo ili kutoa maoni kwa kila kundi:

  • A.Sehemu zipi zinavutia? Kitu gani kinazifanya zivutie? Sehemu zipi zinachusha? Hizi zinawezaje kuboreshwa?
  • B.Uandishi huu umetumia njeo gani? Kagua ili kuhakikisha kwamba kila kitenzi kiko katika njeo stahili AU hakikisha kuwa kuna sababu ya msingi ya kutumia njeo nyingine.

Baada ya kupata maoni kutoka kwenye makundi, kila kundi liandike tena kazi yao. Kusanya kazi hizo, na tumia vigezo sawa kusahihisha kazi zote.

Utaratibu huu ulifanikiwa kwa kiasi gani? Je, utaurudia tena?

Je, hali ya uandishi wa wanafunzi wako ilipata ubora? Unajuaje?

Nyenzo-rejea ya 1: Miundo mbadala ya somo – iliyotumiwa na Bwana Gasana 

Usuli/taarifa ya mwanzo/uelewa wa mwalimu

Mfuatano wa swali na jibu

S:     Je, Bibi Yuhi, ulisikia mlio wa bunduki?

J:      Ndiyo, wakati huo tulikuwa tunakula cha jioni.

au

S:     Je, Bwana Mulifi, ulisikia mlio wa bundukit?

J:      Hapana, wakati huo nilikuwa ninasafiri kwenda Nyanza.

Miundo ya ripoti ya askari wa upelelezi

Bibi Yuhi alisikia mlio wa bunduki wakati walipokuwa wakila chakula cha jioni.

au

Bwana Mulifi hakusikia mlio wa bunduki kwa sababu alikuwa safarini kwenda Nyanza.

Nyenzo-rejea  2: Tangazo la mauzo

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Kwa wanafunzi wenye umri mkubwa, unaweza kutumia mfuatano wa kiwango cha juu zaidi, kama vile:

S: Tazama shati ile! Hiyo ni bei rahisi.

J: Ndiyo, walikuwa wanaliuza kwa ShzT …. wiki iliyopita!

au

S: Ninakuonea huruma ulinunua hizo jeans wiki iliyopita!

J: Ndiyo, natamani ningesubiri punguzo la bei. Nimepoteza ShzT ….

Orodha ya bei za mboga mboga

Onesho hili linaweza kuwa lenye manufaa kama uko eneo la vijijini ili kuunda mazingira kwa ajili ya Shughuli 1.

Chanzo: Decade Volcano Photograph, Website.

BEI POA KABISA ZA LEO –NJOO UNUNUE!

MUHOGO siyo ShzT 2500 SASA ShzT 2000!

NYANYA siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1200!

VITUNGUU siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1100!

NDIZI siyo ShzT 1500 SASA ShzT 1000!

Nyenzo-rejea 3: Chati za njeo za kitenzi

Nyenzo ya Mwalimu ya kutumia na wanafunzi kwa ajili ya kupanga/kurekebisha

Njeo iliyopoNjeo iliyopitaNjeo ijayo
NatembeaNilitembeaNitatembea
Nang’ataNiling’ataNitang’ata
NachaguaNilichaguaNitachagua
NalimaNililimaNitalima
NachoraNilichoraNitachora
NakulaNilikulaNitakula
NasahauNilisahauNitasahau
NafahamuNilifahamuNitafahamu
NaonaNilionaNitaona
NalalaNililalaNitalala
NaogeleaNiliogeleaNitaogelea
NaandikaNiliandikaNitaandika

Nyenzo-rejea 4: Shairi la kusifu

Kwa matumizi ya wanafunzi

Ngoma Yangu na Francis Faller

Inapiga

kwa uvumilivu

kama maji

yadondokayo

toka kwenye

bomba la

mfereji

au kwa majivuno

kama sauti ya mapigo ya maji ya bahari.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inaita upendo.

Inatwanga hasira.

Inahubiri uhuru.

Haisimami kamwe

Hata wakati hakuna mtu

anayesikia ngoma yangu

isipokuwa mimi.

Ngoma yangu inasalimia

kila kitu

kipitacho njia:

jua linalochomoza

mvua inayogongagonga

upepo unaovuma

familia ya korongo

makazi pote angani.

Inamsalimia chenene

Anayelia mlio mwembamba kwa sababu ya raha yake.

Inawasalimia wafanyakazi

ambao vifaa vyao vya kutobolea na kupasulia

vinachimba mashimo

kwa kuchosha.

Ninaifuatilia

katika kicheko

Ninaiongoza kuvuka

maumivu yanayopwita.

Ni shorewanda anayedonoa mbegu

ni ufito kando ya ukingo

ni risasi iendayo kasi.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inapiga kwa kiherehere

makaribisho

kwa ajili yako.

Je, utaisikia

kwa furaha?

Je, utakimbia kwa hofu?

Ngoma ni

ngozi na mbao tu

kwa hiyo utakuja?

Ni lazima uje.

Ni lazima uje.

Ngoma yangu kipenzi

ilikuwa jana dhaifu sana.

Leo inapiga.

Kwa nguvu.

Hakika haikutumika zaidi

duniani kote

kupiga bure.

Ingawa kamwe

haipati jibu

Nafikiri

sitaweza kuishi

kama wimbo

wa ngoma yangu

utakufa.

Chanzo asilia: My Drum – Meyerowitz, B., Copans, J. & Welch, T. (watunzi)

Nyenzo-rejea 5: Vitenzi na vielezi katika shairi – Ngoma Yangu na Francis Faller

Taarifa za msingi / welewa wa somo wa mwalimu

Katika tafsiri hii ya shairi vitenzi vimepigiwa mstari na vielezi vimewekewa wino uliokolezwa.

Inapiga

kwa uvumilivu

kama maji

yadondokayo

Dokezo 1: patiently ni kielezi cha namna, ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyopiga/lia: kwa utulivu, kwa kurudiarudia pasipo kuudhika au kuwa na hasira.

toka kwenye

bomba la

mfereji

Dokezo 2: dripping ni sehemu ya kitenzi kamili ‘is dripping’: kama maji [that is/ambayo] inadondoka – mshairi ameamua kutotumia ‘that is’.

au kwa majivuno

kama sauti ya mapigo ya maji ya bahari.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Inaita upendo.

Inatwanga hasira.

Dokezo 3: proudly vilevile ni kielezi ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia: kwa kujipenda, kama kwamba inajifurahia sana.

Inahubiri uhuru.

Haisimami kamwe

Hata wakati hakuna mtu

anayesikia ngoma yangu

isipokuwa mimi.

Dokezo 4: never ni kielezi cha wakati ambacho kinaongezea taarifa kwenye kitenzi ‘stops’: ngoma haiwezi kusimama hata mara.

Ngoma yangu inasalimia

kila kitu

kinachopita njia: jua

Dokezo 5: battering ni sehemu ya kitenzi kamili ‘is battering’: mvua [that is/ambayo] inagongagonga.

linalochomoza mvua

igongayo upepo

unaovuma familia ya

korongo makazi

Dokezo 6: monotonously ni kielezi cha namna ambacho kinaeleza jinsi kazi ya kuchimba inavyoendelea kwa namna inayochosha na ya kurudiarudia

pote angani.

Inamsalimia chenene

Anayelia mlio mwembamba kwa sababu ya raha yake.

Dokezo 7: It’s ni kifupi cha It is na ‘is’ ni kitenzi, ingawa si kitenzi kinachoonesha tendo.

Inawasalimia wafanyakazi

ambao vifaa vyao vya kutobolea na kupasulia

vinachimba mashimo

Dokezo 8: Nervously ni kielezi cha namna ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia: kama kwamba ngoma ina hamu au ina woga kidogo.

kwa kuchosha.

Dokezo 9: ‘will come’ ni iko katika njeo ijayo lakini iko katika muundo wa swali, ‘will you come?’

Ninaifuatilia katika

kicheko Ninaiongoza

kuvuka maumivu

yanayopwita.

Ni shorewanda anayedonoa mbegu

You should ni muundo uliofupishwa wa You should come – vilevile ni tendo katika njeo ijayo.

ni ufito kando ya ukingo

Dokezo 10: was ni njeo iliyopita ya ‘is’.

ni risasi iendayo kasi.

Ngoma yangu. Ngoma yangu.

Dokezo 11: Strong kwa kawaida ilitakiwa iandikwe ‘strongly’: hiki ni kielezi ambacho kinaeleza jinsi ngoma inavyolia.

Inapiga kwa kiherehere

makaribisho

kwa ajili yako.

Dokezo 12: wasn’t stretched ini kitenzi kilicho katika njeo iliyopita.

Je, utaisikia

kwa furaha?

Je, utakimbia kwa hofu?

Dokezo 13: never ni kielezi cha wakati (tazama Dokezo 4).

Ngoma ni

ngozi na mbao tu

kwa hiyo utakuja?

Ni lazima uje.

Ni lazima uje.

Dokezo 14: could not live na should die ni vitenzi ambavyo vinarejelea katika wakati ujao kwa sababu vinaashiria kwamba mshairi hataweza kuishi hapo baadaye bila ngoma.

Ngoma yangu kipenzi ilikuwa jana dhaifu sana. Leo inapiga.

Kwa nguvu.

Hakika haikutumika zaidi

duniani kote

kupiga bure.

Ingawa kamwe

Dokezo 15: Wanafunzi wanaweza kukanganywa na maneno yanayoishia na ‘ing’. Wakati mwingine maneno haya ni sehemu ya kitenzi, mfano: ‘I am singing. Pengine maneno haya ni nomino, mfano: ‘The singing’ of the choir was excellent. Pengine, ni vivumishi ambavyo vinafafanua nomino, mfano: ‘The singing canaries’ flew to the top of their cage. Katika shairi hili dripping, battering, chirping, digging, pecking, beating ni sehemu za vitenzi. The pounding ni nomino. Throbbing ni kivumishi kinachofafanua pain.

haipati jibu

Ninafikiri

sitaweza kuishi

kama wimbo

wa ngoma yangu

utakufa.

Everything ni kiwakilishi ambacho kinasimama mahali pa nomino ambazo zinakifuatia katika ubeti wa 2. For nothing ni msemo ambao unamaanisha ‘without payment/bila malipo’ au ‘for no reason/bila sababu’.

Sehemu ya 3: Kuunda Fursa za Mawasiliano

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuunda shughuli za kukuza mawasiliano katika lugha ya ziada?

Maneno muhimu: tofauti katika taarifa; maingiliano ya kimawasiliano; umaanifu; kuunda shughuli; makundi     

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • umeunda shughuli za mawasiliano halisi katika darasa lako la lugha ya ziada;
  • umeendeleza ‘maktaba’ ya nyenzo za kuchochea mazungumzo asilia;
  • umetumia kazi za vikundi na za wanafunzi wawili wawili ili kukuza mawasiliano ya lugha ya ziada.

Utangulizi

Ukiwa mwalimu, unapaswa kutumia matokeo ya tafiti kuhusiana na kitu unachokifanya. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kwamba watu hujifunza lugha kutokana na kushiriki katika mawasiliano yenye maana ya lugha husika, katika mazingira asilia. Hoja hii inamaanisha nini?

‘Kushiriki’: Kila mwanafunzi lazima ashiriki –au ahusishwe kikamilifu.

‘Umaanifu’: Shughuli lazima iwe inalandana na mazingira halisi na ilete maana kwa wanafunzi.

‘Maingiliano’: Mawasiliano lazima yahusishe njia-mbili (au njia tatu au nne).

‘Mazingira asilia’: Lugha inayotumiwa lazima iwe lugha ya kawaida ya mawasiliano ya kila siku.

Katika sehemu hii, tunaangalia jinsi ya kuchochea maingiliano ya kimawasiliano ya aina hii darasani kwako, hususan kwa kutumia picha. Tunashauri kwamba uunde uteuzi wa zana.

Kwa kawaida, darasa lenye kazi za maingiliano ya kimawasiliano hufanywa katika makundi madogo madogo. Itasaidia kusoma Nyenzo-rejea Muhimu: Kutumia kazi za vikundi katika darasa lako .

Somo la 1

Kuwatia hamasa wanafunzi ili wawasiliane miongoni mwao kunahusu uandaaji wa shughuli wanazoweza kuzifanya pamoja, na ambazo ni ‘halisi’. Makundi yanasaidia kutiana moyo na yanawawezesha wanafunzi kujaribu lugha mpya.

Mawasiliano ‘halisi’ huhusisha ‘tofauti za taarifa’; kwa maneno mengine, wanafunzi hugundua kitu ambacho hawakukifahamu awali kutoka kwa wenzao. Zamani, wanafunzi wangeweza kuagizwa kumwuliza mwanadarasa mwenzao, ambaye jina lake wanalifahamu vizuri, ‘Jina lako nani?’ Hapa hakuna tofauti ya taarifa, kwa hiyo mawasiliano haya si ‘halisi’.

Uchunguzi-kifani 1 na Shughuli 1 zinaonesha jinsi utafutaji wa taarifa zinazokosekana unavyoweza kutumika kwa lengo la kuunda makundi au kazi za watu wawili wawili. Vile vile, angalia Nyenzo-rejea 1: Mifano zaidi kuhusu Shughuli za tofauti za taarifa .

Uchunguzi kifani ya 1: Shughuli za tofauti za taarifa katika kuunda makundi

Liz Botha wa East London, Afrika ya Kusini, alitaka kugawanya kundi la walimu 40 katika makundi manne, kwa namna ambayo ingewasaidia kuwasiliana miongoni mwao.

Alitafuta jumla ya picha 16 zote katika ukurasa mmoja wa kitabu (angalia Nyenzo-rejea 2: Mawazo katika picha ). Alitengeneza nakala nne za ukurasa huo na kukata picha kumi kutoka katika kila ukurasa ili apate makundi kumi yenye picha nne nne: viatu; bendera, nk. Kisha alizichanganya picha.

Walimu walipofika, alimpatia kila mmoja picha moja, na kuwaambia wasiioneshe kwa mtu yeyote. Kisha akawaagiza watembee kuzunguka darasa, wakiuliza maswali ya aina hii:

Swali: Una picha ya (n) …. ?

Jibu: Hapana, sina./Ndiyo, ninacho.

Waliendelea namna hii mpaka wakaunda kundi la watu wanne wenye picha zinazofanana.

Baada ya makundi kuundwa, wanavikundi wakaanza kusemezana, na wakagundua, kwa njia ya majadiliano, kwamba wana kitu kimoja kilicho sawa kwa wote: labda wote wanne wana dada wadogo, au wanapenda au hawapendi aina fulani ya chakula au muziki, nk.

Walifurahia mno shughuli hii, na waliikamilisha kwa kufahamiana zaidi miongoni mwao.

Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya shughuli kama hii katika darasa lako?

Shughuli ya 1: Tafuta mwenzi wako

Andika orodha ya maneno yanayohusiana na somo la hivi karibuni (angalia Nyenzo-rejea 3: Maneno na maana ili kuona baadhi ya maneno).

Wape kila wanafunzi wawili wawili neno moja kutoka kwenye orodha na vipande vidogo viwili vya karatasi. Waambie waligawe neno lao katika sehemu mbili/nusu, na waandike nusu moja katika kila kipande miongoni mwa vipande hivyo vidogo vya karatasi.

Kusanya na changanya vipande vyote vya karatasi. Sasa mpe kila mwanafunzi nusu-neno.

Waambie wanafunzi wamtafute mwanafunzi ambaye ana nusu nyingine ya neno lao, na kisha wasimame naye.

Kundi la wanafunzi wawili wawili lisome maneno yao mbele ya darasa.

Kisha, kila kundi la wanafunzi wawili wawili liandike maana ya neno lao katika kipande kingine cha karatasi. Kusanya maana hizo na maneno yaliyo nusu.

Wape tena maneno yaliyo nusu na rudia mchakato wa kuoanisha.

Baadaye, taja kila maana kwa zamu na liambie kundi la wanafunzi wawili wawili likae chini litakaposikia maana ya neno lao. Mtu yeyote asiseme kama wamekaa chini kwa kukosea au kwa usahihi. Mwishoni maana zitafafanuliwa.

Jaribu mchezo huu tena na angalia kama wanaweza kuucheza kwa haraka na kwa usahihi zaidi.

Je, shughuli hii iliwasaidia wanafunzi wako kuelewa maana za maneno? Unajuaje?

Somo la 2

Ukiwa mwalimu, mara zote unapawa kutafuta shughuli ambazo zinakuza ujuzi wa kusikiliza kwa kuelewa.

Hapa, Shughuli 2 inahusisha kusikiliza na kuchora, au kubadili lugha ya taarifa kwenda katika kielelezo cha taarifa. Ina faida inayofanana na mwitikio wa mwili wote (total physical response); kwa sababu wanafunzi hawalazimiki kutumia lugha katika kuonesha welewa wao. Hata hivyo, inatakiwa yule anayeelezea awe fasaha na sahihi sana –vinginevyo, athari zinaweza kuonekana kwenye picha ya mwanafunzi mwenza.

Uchunguzi kifani ya 2: Kueleza na kupanga mawasiliano yasiyofahamika kwa njia ya posta

Aghalabu, Lulu alikuwa akipata ‘mawasiliano asiyoyafahamu’ yaliyowekwa kwenye sanduku lake la barua: matangazo kutoka kwenye maduka mbalimbali yanayoonesha picha za bidhaa zao. Siku moja aliamua kuyaweka, badala ya kuyatupa kwenye pipa la taka.

Alikata sehemu tofauti tofauti za bidhaa za nyumbani: pakiti za vyakula, sukari na unga; maboksi ya sabuni za unga na nafaka, nk. Alikuwa na nakala nyingi.

Alichora picha sita za vinafasi vya kabati la jikoni, na kuchomeka bidhaa za nyumbani katika vijinafasi vitatu ( Nyenzo-rejea 4: Eleza na panga sinaonesha mifano). Kila moja kati ya picha hizo tatu ilikuwa tofauti na nyingine. Kisha alikata nakala za bidhaa zote kwenye vijinafasi vya kabati la jikoni. Bado alibakiwa na vijinafasi titatu visivyo na kitu.

Siku iliyofuata, kwenye Darasa lake la 4, makundi matatu ya wanafunzi sita sita au saba saba yalipewa picha za vijinafasi vya kabati vilivyojaa vitu. Vile

vilivyokuwa vitupu, viligawiwa kwa makundi mengine matatu, na wanafunzi tofauti katika makundi haya walipata nakala za bidhaa.

Aligawa makundi hayo katika sehemu mbili, na kulifanya sehemu ya 1 (ililo na picha zilizokamilika) kukaa karibu na sehemu ya 2 (yenye vijinafasi visivyo na kitu na bidhaa tofauti). Wanakundi la sehemu 1 walieleza jinsi bidhaa zilivyopangwa kwenye vijinafasi, na wanakundi la sehemu 2 walizipanga katika vijinafasi vilivyokuwa vitupu. Waliuliza maswali pale ambako hawakuwa na uhakika. Mchezo huu uliwapa zoezi la kutumia maneno kuhusu nafasi mbalimbali katika mazingira ‘halisi’.

Somo lilikwenda vizuri. Lulu aliamua kwamba wakati mwingine atakuza msamiati wa wanafunzi wake kwa kuwaambia wachambue na kueleza taswira za –au, kama itawezekana, ngoma-halisi na vitu vilivyobuniwa kutoka katika jumuiya ya mahali hapo.

Shughuli ya 2: Eleza na chora

Shughuli hii hufanywa katika makundi au na watu wawili wawili. Mtu mmoja anaeleza na mwingine/wengine anachora/wanachora. Darasa lenye wanafunzi wa viwango mbalimbali, wanafunzi wakubwa wanaweza kutoa maelezo, na wadogo wachore.

Tafuta picha au michoro rahisi sana au chora ya kwako, m.f. mchoro wa vistari wa picha ya nyumba au mti. Utahitaji picha moja kwa kila jozi au kundi la wanafunzi. Picha zinaweza kuwa sawasawa au tofauti.

Anza kuwafundisha wanafunzi msamiati na aina za sentensi ambazo watahitaji kuzitumia, mfano, ‘Chora mraba katikati ya ukurasa’. ‘Chora kuku wawili kando ya nyumba.’

Toa picha moja kwa kila jozi (au kundi) la wanafunzi, huku ukiwaambia ‘watoa maelezo’ kutowaonesha wenzao picha hizo. Mwanafunzi aliyeshika picha anaielezea picha hiyo kwa wanafunzi wengine/mwanafunzi mwingine, ambaye anajaribu kuchora kitu kinachotolewa maelezo. Hawatakiwi kusema picha hiyo ni nini.

Mwishoni, mtoa maelezo na mchoraji wanalinganisha picha zao. Anza mjadala wa darasa zima: Duara la ‘Asanda’ ni dogo kuliko lililoko katika picha’. Kuku wa Amina wana vichwa vikubwa, lakini kuku walioko katika picha wana vichwa vidogo.’ Wakiwa wanafanya mazoezi, wataifanya vizuri zaidi shughuli ya aina hii.

Nyenzo-rejea Muhimu: Kufanya kazi katika madarasa makubwa/madarasa ya mchanganyiko kunatoa mawazo zaidi kuhusu mbinu za kufanya kazi.

Somo la 3

Ukiwa mwalimu, unapaswa kukumbuka kwamba aghalabu, binadamu (pamoja na wanafunzi) hutaka kujua maana ya kitu wanachokifanya. Kila shughuli unayowapa wanafunzi lazima iwape fursa ya kutafuta maana.

Uchunguzi-kifani 3 na Shughuli Muhimu vinatalii njia za kutafuta maana katika aya au matini. Wanafunzi wafanye mazoezi ya baadhi ya maarifa muhimu yaliyomo katika maandishi hayo: utabiri na utazamiaji (kukisia kitu gani kitatokea baadaye). Walitakiwa pia kuwasiliana miongoni mwao ili kutatua tatizo. Kila mmoja alikuwa na nafasi ya kuchangia ili kutatua ‘fumbo’ na kutafuta maana.

Uchunguzi kifani ya 3: Hadithi: kutoka vyanzo tofauti na kuwekwa pamoja

Darasa la 6 la Bibi Ndaba lilileta hadithi kutoka majumbani na kuzieleza kwa ufafazi. Katika kila ukurasa, waliandika sentensi na kuchora picha inayoona na sentensi husika. Kurasa hizo zilipachikwa kwenye magamba ya plastiki ya kurekodia na kuunda jarida ambalo ili kutengeneza kitabu.

Mfanyakazi mwenzie, Bibi Mapande, ambaye anafundisha darasa la 3 aliziona hadithi zilizofafanuliwa, na akaomba kuziazima kwa ajili ya shughuli ya kusoma katika darasa lake. Bibi Ndaba alifika kuangalia darasa la mwenzie.

Bibi Mapande aliligawa darasa lake katika makundi matano. Alilipa kila kundi hadithi lakini alizitoa kurasa kutoka kwenye jarida na kuliweka jarida hilo katikati ya meza. Alimpa kila mwanafunzi katika kundi ukurasa mmoja wa hadithi, huku akihakikisha kwamba amechanganya mpangilio wa kurasa hizo. Kila mwanafunzi alitakiwa kusoma sentensi iliyo kwenye ukurasa wake mbele ya kundi lake. Kwa njia ya majadiliano, kundi liliamua sentensi ipi ikae mwanzo wa hadithi, na kuweka sentensi nyingine zote katika mpangilio unaostahili; na kurudishia kurasa katika jarida kwa mpangilio sahihi.

Bibi Mapande alimwambia mwanafunzi mmoja kutoka katika kila kundi, asome hadithi ya kundi lake mbele ya darasa; na wanadarasa walitoa maoni kuhusu mpangilio wa sentensi. Wakiwa katika darasa, walichagua hadithi waliyoipendelea zaidi, na igizo la dakika tano likaandaliwa kuonesha hadithi hiyo.

Shughuli muhimu: Sehemu za kitu kizima

Unaweza kutumia shughuli ya aina hii kwa darasa la kiwango chochote

Chagua hadithi fupi, iliyoandikwa vizuri, au aya ambayo wanafunzi wako wanaweza kuielewa na kuihusisha na ukweli. Unaweza kutumia hadithi, hadithi au aya za/ya picha kama zile zilizoko katika Nyenzo-rejea: Kuunda maana , au aya ambayo ni changamano zaidi ya lugha au mada yoyote. Kila kundi linaweza kuwa na hadithi hiyo hiyo au tofauti ya kushughulikia.

Ikate hadithi katika vipande sita au saba. Vipande vyaweza kuwa aya, sentensi au kundi la sentensi, kulingana na umri na uwezo wa wanafunzi wako. Pachika kila kipande kwenye kadi.

Lipe kila kundi seti ya sehemu za aya zilizokatwa.

Kila mwanakikundi ana kipande cha aya, na anawasomea wengine kipande chake. Wakiwa kama kundi, wanaziweka aya zao pamoja katika mpangilio wake sahihi.

Kwa wanafunzi ambao wana uwezo au uzoefu zaidi, waambie waeleze jinsi walivyofanya mpaka kupata mpangilio sahihi.

Soma aya au hadithi hizo mbele ya darasa.

Nyenzo-rejea ya 1: Shughuli zaidi zihusuzo tofauti za taarifa

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Kufanana ni nini?

Chagua seti za picha sita au nane. Kila seti ya picha lazima iwe na kitu kinachofanana kwa picha zote. Kwa mfano, unaweza kuwa na picha sita ambazo zote zina kitu kimoja ambacho kimetengenezwa kwa kioo, au seti ya picha sita ambazo katika kila picha kuna mtu anakula. Pengine una picha sita ambazo zinaonesha mtoto, au zinaonesha umaskini, au ukarimu.

Gawa darasa lako katika makundi ili kila kundi linaweza kuwa na seti ya picha kadhaa. Hakikisha kwamba una baadhi ya picha za akiba, kwa ajili ya kundi lolote litakalomaliza kazi haraka. Mara kundi linapomaliza, unaweza kukusanya seti za picha zao na kuzigawa kwa kundi lingine ambalo limemaliza.

Wanakikundi wasioneshane picha zao. Wanatakiwa kuulizana na watu wengine katika kundi aina ifuatayo ya maswali:

Je, kuna (kitu)…. katika picha yako?

Je, kuna (vitu)…. katika picha yako?

Je, picha yako inaonesha …. ?

Wanakikundi wengine wanajibu:

Hapana, hakuna. Au, Ndiyo, ipo/zipo.

Hapana, haioneshi. Au, Ndiyo, inaonesha.

Mtu ambaye anabainisha sifa ya ufanano ndiye mshindi.

Mchezo huu ni rahisi au mgumu zaidi kutegemeana na kiwango cha udhahania kilichomo kwenye sifa ya ufanano.

Unafanya nini ili kujipatia kipato?

Andika orodha ya kazi ubaoni, kama hii iliyopo hapa chini.

DaktariDaktari wa MenoMwalimu
Muuza dukaMuuguziMeneja
KaraniRubaniMhandisi
Mtunza BustaniMkutubiAskari polisi
MkulimaMchuuzi wa samakiFundi wa ngamizi
Mhudumu katika ndegeMfamasiaMama Ntilie/Lishe
Mtaalam wa mauaMwanasayansiMwanamuziki
Mtaalam wa ngamiziMhudumu wa dukaniFundi gereji

Waambie wanafunzi waseme wangependa kufanya nini watakapomaliza masomo yao. Wanaweza kuongeza kazi nyingine katika hizo zilizoorodheshwa.

Toa kadi kwa jozi za wanafunzi na waambie waandike jina la kazi kwenye kadi hiyo. Kwenye kadi nyingine, wanatakiwa waandike fasili ya kazi hiyo.

Mwambie mwanafunzi mmoja kutoka katika kila jozi kutoa ripoti mbele ya darasa kuhusu kazi waliyonayo, na fasili yake. Wanafunzi wengine lazima watoe maoni kama wanadhani fasili ni sahihi.

Kusanya kadi za kazi na maana zake, zisambaze kwa wanafunzi bila kufuata utaratibu wowote. Waambie wanafunzi wazunguke darasani na kutafuta mwenza ambaye ana fasili au neno sahihi.

Wenza wanapopatana, wanatakiwa wasimame pamoja mpaka kila mmoja hapo darasani amalize shughuli hiyo.

Kisha waambie waunde sentensi kwa kutumia kazi walizozifasili.

Nyenzo-rejea 2: Madokezo kwa ajili ya picha

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Chanzo asilia: Books on display: New Day-by-Day English Course

Line drawings: Modern English Teacher, 10

Nyenzo-rejea 3: Maneno na maana – mifupa katika mwili

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

NenoMaana
Muungabega/Hu merusAina ya mfupa iliyopo sehemu ya juu ya mkono
Fuu la kichwa/CraniumFuvu, ambalo huhifadhi ubongo
Fibula/gokoMfupa mdogo kati ya mifupa miwili iliyopo sehemu ya chini ya mguu
Radias/RadiusMmoja kati ya mifupa ya kwenye kiwiko ambao huzunguka kadri unavyouzungusha mkono wako
Fema/FemurMfupa mmoja uliopo juu ya mguu na ulio mrefu kuliko yote mwilini
Pingilimgongo/Ve rtebraeMifupa ambayo huunda uti wa mgongo na inayoshikilia neva zipitazo sehemu hiyo
Kifupakono/Meta carpalsMifupa iliyopo kwenye mkono
Kifupakidari/Ster numMfupa wa kwenye kidari, ambao unahifadhi moyo
Skapula/ScapulaMfupa ambao unajulikana kama bapa la bega sehemu ya nyuma
Muundi goko/TibiaMifupa mikubwa miwili iliyopo sehemu ya chini ya mguu
Tarisas/TarsusMkusanyiko wa mifupa inayounda sehemu ya juu ya kiwiko na goti

Nyenzo-rejea 4:

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Unaweza kuandaa michezo kama hii kwa kutumia mpangilio wa nyumbani na picha za samani. Viweke katika sanduku lako la zana kwa matumizi ya baadaye, au ili wanafunzi watumie wakati watakapokuwa na nafasi kwa ajili ya shughuli za kujisomea na ujifunzaji binafsi, na kufanya mazoezi ya msamiati. Unaweza kuhitaji kutumia vitu na bei za mahali hapo.

Nyenzo-rejea 5: Kuunda maana

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Aya kwa ajili wanafunzi wa madarasa ya juu: Wafalme wa Zulu

Wafalme wa Zulu walianzisha utawala wa kinasaba wenye nguvu kuliko tawala zote za watu weusi katika Afrika. Mkuu Shaka, ambaye alianzisha utawala wa kinasaba mwanzoni mwa karne ya 19, aliunganisha taifa la Wazulu na kuunda kikosi cha kijeshi kilichokuwa cha kuogopesha. Kufuatia kujulikana kwake kama ‘Napoleon Mweusi’, mfalme huyu wa kwanza wa Wazulu alikuwa katili, ingawa pia alikuwa kiongozi mwerevu sana. Kutokana na sifa yake ya kuwa mshindi na asiye na huruma katika vita, aliongoza watu wake kujipatia umashuhuri na aliwatawala kwa nidhamu ya ukali. Mauaji aliyomtendea nduguye aliyechangia naye mzazi mmoja ambaye alimsaliti, Dingane, hayakusaidia kupunguza utawala wa kigaidi. Lakini Dingane, aliyejiingiza matatani, ijapokuwa alikuwa katili na dikteta, hakuwa mwanajeshi, na utawala wake uliishia katika maafa. Baada ya kuzidiwa nguvu na Makaburu katika vita ya Mto wa Damu, hatimaye Dingane alilazimika kuikimbia nchi ya Zulu, na alifia uhamishoni. Baada ya kifo chake eneo la jirani la Natal likawa makazi ya wazungu, na mkondo wa historia ya Zulu ukabadilika.

Vyanzo asilia:

Matini iliyoandikwa – imetoholewa kutoka ‘The Zulu Kings’, na Brian Roberts, Hamish Hamilton, 1974. imekaririwa katika Rodseth, V. na wengine. 1992. Think Write: A writing skills course for students, teachers and business people. Randburg: Hodder and Stoughton Educational. ISBN 0 947054 87 1

Hadithi ya picha – Standard 2 Language Book, Maskew Miller Longman

Sehemu ya 4: Namna ya kujenga juu ya ujuzi wa lugha ya nyumbani

Swali Lengwa muhimu: Utawezaje kukuza umilisi katika lugha ya ziada kwa kutumia ujuzi wa lugha ya nyumbani?

Maneno muhimu: kujenga; msamiati; dhana; uwili-lugha nyongeza

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • kutumia lugha ya nyumbani kupeusha ubunifu, welewa na ukuzaji wa mawazo;
  • kuelewa umuhimu wa mwingiliano baina ya lugh aya nyumbani na lugha ya ziada.

Utangulizi

Ukiwa mwalimu, unahitaji kupeusha ujifunzaji na stadi katika lugha ya ziada na kwa hiyo unahitaji kufanya maamuzi kuhusu lini na jinsi ya kutumia lugha ya nyumbani. Uchaguzi wako wa lugha unapaswa kutegemea jinsi lugha hiyo itakavyowasaidia wanafunzi katika kujifunza, na sio urahisi wa lugha wa lugha kwa mwalimu.

Katika shule nyingi, lugha za nyumbani za wanafunzi zinatumika nyumbani, na tena katika miaka michache ya mwanzoni ya shule tu. Hali hii husababisha watu wawe na fikira kwamba lugha ya nyumbani haina thamani kubwa. Walimu na wazazi husahau kwamba ni muhimu kutumia ujuzi na stadi za lugha ya nyumbani ya wanafunzi na kutumia lugha zote mbili.

Sehemu hii inaonesha jinsi kutumia lugha ya nyumbani inavyoweza kupeusha ubunifu, welewa na ukuzaji wa mawazo, kadhalika ukuaji wa lugha ya ziada.

Somo la 1

Wanafunzi wako huja shuleni wakiwa tayari na usuli tajiri wa mitagusano ya kibinadamu na tajiriba za ulimwengu. Wanayo pia lugha ya kuelezea ulimwengu wao. Wanapotumia lugha yao ya nyumbani wanaweza kutumia tajiriba yao kusheheneza uneni na uandishi wao kwa maelezo makini na jazanda. Ukiwa mwalimu, unahitaji kuwahimiza wafanye hivi, na kuwafanya watumie maarifa waliyo nayo.

Kuhusu kusema au kuandika katika lugha ya ziada, wanafunzi mara nyingi hawatang’amua kuwa wanaweza kutumia maarifa hayo. Walimu, pia, wanaweza kusahau kwamba kazi yao ni kuwasaidia wanafunzi wahamishe maarifa yao katika/kwa lugha yao ya nyumbani ili yawe katika lugha ya ziada, na sio kuanza na bure.

Katika kisehemu hiki, tunapendekeza kuwa uwasaidie wanafunzi kueleza wanayofahamu na kubuni/kufikiria kwa lugha yao wenyewe, na kisha kufikiria njia za kuhamishia maana hiyo kwenye lugha ya ziada.

Uchunguzi kifani ya 1: Kuandika katika isiZulu kutajirisha Kiingereza

Bi Nonhlanhla Dlamini anafundisha Kiingereza kwa wanafunzi 64 wa darasa la 6 wanaosema isiZulu katika wilaya ya Nongoma katika KwaZulu-Natal, Afrika ya Kusini.

Siku moja, alisoma na kujadili mifano ya mashairi ya sifa na hadithi na wanafunzi wake na kupendekeza kuwa nao waandike yao. Walifurahi sana, lakini jitihadi zao katika Kiingereza hazikuridhisha; kwa hiyo aliamua kuchukua mkabala tofauti.

Bi. Dlamini aliwataka wanafunzi wake kufanya kazi wawiliwawili waelezane kitu wanachotaka kukiandika na kusaidiana waandike hadithi na shairi kwa isiZulu.Kisha wakafanya kazi wawiliwawili kuandika nakala za Kiingereza.

Aliwakumbusha wasifanye tafsiri za neno kwa neon kwa sababu sarufi na msamiati wa lugha mbili hizi vimejengwa kwa namna tofauti.

Jitihadi zilizofuata katika uandishi katika Kiingereza zilivutia zaidi, ingawa hazikusheheni maelezo yenye undani na mvuto kama nakala za Kizulu.

Bi. Dlamini alifanya kazi ya kukuza msamiati na wanafunzi kupanua masafa yao ya vitenzi na vielezi katika lugha ya ziada, kwa kuwa aliona kuwa eneo hili lilikuwa na upungufu. Kisha, akawataka wanafunzi warekebishe uandishi wao, kwa kutumia vitenzi na vielezi vingi zaidi.

Baada ya kuandika majina kwenye kazi zao, wanafunzi waliweka mashairi na hadithi zao kwenye meza nyuma ya darasa. Walifurahia kusomeana kazi zao.

Bi. Dlamini aliona jinsi vitenzi na vielezi vingi zaidi vilivyokuwa sehemu ya msamiati wa kawaida wa wanafunzi kutokana na zoezi hili.

Shughuli ya 1: Picha za maneno katika lugha mbili

Andika ubaoni shairi la matusi ‘Wewe’. Andika ubaoni shairi la ‘matusi’ ‘Wewe’, lililo katika Nyenzo-rejea 1: Shairi .

Lisome na wanafunzi na mjadiliane kila ulinganishi, k.m. ‘kichwa ni kama ngoma tupu’ humfanya mtu afikiri kuwa ni kikubwa na kitupu, n.k.

Watake waandike shairi la sifa, kama darasa, juu ya mtu anayefahamika sana wanayemheshimu.

Amua kwa kushirikiana nao sifa au vipengele ambavyo wataeleza. Kama mtu ni mwanariadha, wanaweza kuchagua sifa za kimwili, miguu, umbo, jinsi anavyotembea, n.k.

Sasa vigawie sifa hizi vikundi au mtu mmojammoja, na watake wafikirie vilinganishi katika lughaya nyumbani.

Watakapotaja vilinganishi vyao, amua, kama darasa, kuhusu kilinganishi bora kwa kila sifa, na viandike katika lughaya nyumbani.

Sasa jadili jinsi wanavyoweza kusema hayo katika lugha ya ziada. Tafsiri ya moja kwa moja (tafsiri sisisi) haifai, lakini jaribu kujenga taswira inayolingana na iliyo katika lugha ya nyumbani.

Kwa njia hii, lijenge shairi lako na darasa lako katika lugha ya ziada.

Watake watunge shairi lao wenyewe –‘matusi’ au ‘sifa’. Wanafunzi wahahakikishe wasisababishe chuki ya kweli. Je, mkabala huu umefaulu kuwasaidia wanafunzi kukuza msamiati katika lugha ya ziada?

Somo la 2

Mara nyingi watu huwaza kwamba mwalimu lazima atumie lugha ya ziada tu darasani ili wanafunzi waweze kuwa na ufasaha katika lugha hiyo. Hili si wazo baya na linatekelezeka vizuri katika hali fulani. Hata hivyo, hali halisi katika madarasa mengi hapa Afrika ni kwamba:

hakuna wasemaji wazawa au wasemaji wajuzi (walimu au walimu) wa lugha ya ziada shuleni;

wanafunzi wana nafasi finyu sana kutumia lugha ya ziada nje ya darasa;

walimu wengi zaidi hubadilisha msimbo kwa kiasi kingi (hutumia lugha hizi kwa kuzichanganya wanapozungumza);

iwapo lugha ya ziada tu ikitumika wanafunzi hawaelewi wakati mwingi, hasa katika miaka ya mwanzo ya kujifunza lugha mpya.

Wanafunzi wanapojifunza lugha ya ziada kwa miaka michache tu, na kama hawana nafasi ya kuitumia nje ya darasa, wanaweza tu kuelewa na kutunga sentensi zinazohusiana na mambo ya kawaida ya kila siku. Aghalabu hawajawa tayari kuitumia kujadili fikira na dhana. Ili kupanua ujifunzaji ujumuishe kujadili fikira, inafaa kutumia mkabala wa utumizi wa lugha mbili.

Uchunguzi kifani ya 2: Kujadili mawazo katika lugha ya nyumbani

Huko Kibaha, Zawadi Nyangasa aliongoza darasa la 7,kipindi cha Kiingereza, katika somo lililojikita kwenye hadithi juu ya mfalme na mshona-viatu. Alitaka wafikiri juu ya hulka ya busara ya kweli na ujanja, na madhumuni ya elimu.

Alisoma hadithi kwa sauti kwa wanafunzi, akisita mara kwa mara kuuliza maswali kuona kama wameelewa.

Maswali na majibu mengi yalikuwa katika Kiingereza, lakini kulikuwa na nyakati ambapo alitumia lugha ya kwanza kuelezea dhana au kuhusisha na maisha ya wanafunzi (taz. Nyenzo-rejea 2: Mfano wa somo .)

Baada ya kusoma hadithi, aliwataka wanafunzi kujadili maswali yafuatayo, katika vikundi vidogo vya watu wanne hadi sita. Aliwahimiza kutumia lugha yao ya mama.

Unafikiri mshona-viatu alikuwa mtu mwenye elimu? Alikuwa mwenye busara? Mjanja? Mwenye furaha? Ni sababu zipi zimekufanya useme hivyo?

Ni mambo yapi muhimu tunayojifunza shuleni? Kwa nini ni muhimu?

Walitoa taarifa baadaye katika lugha yao ya mama, na walikuwa na mjadala wa kijumla juu ya maswali. Aliandika madondoo ubaoni, pia katika lugha ya mama.

Shughuli ya 2: Watu wazima ninaoheshimu

Soma Nyenzo-rejea 3: Usalama na fikiria juu ya vipengele vya usomaji ambavyo vinaweza kusababisha matatizo kwa darasa lako.

Soma kara na wanafunzi wako, huku ukijadili maneno au dhana zisizo za kawaida.

Waulize juu ya mienendo ya watu wazima.

Je, wanatenda kama wale walioelezwa katika aya tatu za kwanza za kara, au kama wale walioelezwa katika aya ya nne?

Mienendo ya watu wazima inawasaidia kama vijana? Kama inawasaidia au haiwasaidii kwa nini?

Fanya majadiliano haya katika lugha ya nyumbani/lugha mama. Kama itahimiza mjadala mzito zaidi, waruhusu wanafunzi wafanye majadiliano katika vikundi vidogo na kisha watoe taarifa baada ya kama dakika 15.

Watake wachague mtu mzima wanayemfahamu na kumheshimu na kuandika maelezo ya mtu huyu, kwa kutumia lugha watakayoiteua. (Taz. Nyenzo-rejea 4: Baba yangu ni nani ?) Wanaweza kufanya kazi wawiliwawili au vikundi vya watu watatu ay wanne.

Kusanya kazi zao na uwape mrejesho. Wanaweza kuwa na hisia-bia zilizo nzito, kwa hiyo uwajibu kwa uungawana kuhusiana na maudhui, badala ya kulenga makosa ya kisarufi, n.k. (Taz. Nyenzo-rejea muhimu: Kutathmini kujifunza.)

Somo la 3

Baada ya stadi na welewa kuimarishwa katika lugha inayofahamika vizuri, ni rahisi zaidi kuvihamishia kwenye lugh aya ziada. Wataalamu wengi huamini pia kuwa kama mtu ataliangalia somo kutumia mitazamo ya lugha mbili, stadi zao za kufikiri huwa bora. Ni muhimu uhakikishe wanafunzi wako wanajiona kuwa tajiri –badala ya fukara –kwa kuwa na lugha mbili au zaidi.

Wanafunzi wako wanapojadili mawazo katika lugha ya nyumbani au lugha ya mawasiliano mapana, inafaa kutafuta and kujifunza njia za kueleza mawazo haya katika lugha ya ziada. Unapaswa daima kufikiria njia kuwasaidia kufanikisha hili. Kisehemu hiki kinakupatia mawazo kadhaa.

Uchunguzi kifani ya 3: Kueleza mawazo kwa Kiingereza

Zawadi alihakikisha kuwa tini katika Kiswahili juu ya somo la mfalme namshona-viatu hazikufutwa ubaoni.

Katika somo lililofuata la darasa la 7, alianza kujadiliana na wanafunzi jinsi ya kujibu, kwa Kiingereza, maswali aliyokuwa ameuliza.

Walizungumzia baadhi ya maneno au mafungu muhimu waliyokuwa wametumia, mathalani tabia, maumbile. Ni mtu au sifa ya namna gani iliyorejelewa na kila neno? Walifahamu watu wenye sifa hizo?

Walijadili pia, kwa njia hiyo hiyo, baadhi ya maneno muhimu ya Kiingereza katika maswali: educated (mwenye elimu); wise (mwenye busara); clever (mjanja); happy (mwenye furaha); learned (msomi). Aliwakumbusha kuwa hakuna tafsiri sisisi wakati wote kutoka Kiingereza kwenda Kiswahili au kutoka Kiswahili kwenda Kiingereza. Hata hivyo walipata njia za kueleza mawazo yaliyokuwa ubaoni kwa Kiingereza. Katika kufanya hivyo, walijifunza miundo mipya ya lugha na msamiati mpya.

Zawadi aliyaandika haya ubaoni, na akawataka wafanye kazi katika vikundi na kuandika majibu ya maswali yake mawili kwa Kiingereza. Kikundi kingeweza kuandaa majibu pamoja, lakini kila mwanafunzi alipaswa kuandika majibu yake mwenyewe.

Zawadi aligundua kuwa mbinu ya kubadili msimbo iliwasaidia wanafunzi wake kukuza Kiingereza chao zaidi.

Shughuli muhimu: Mtu mzima ambaye ningetaka niwe: Kauli ya Dira

Watake baadhi ya wanafunzi wako kuwasilisha maelezo ya watu wazima wanaowaheshimu darasani. Litake darasa kubainisha watu wazima wawili wanaowaheshimu katika jumuiya yao, na panga ili watu wazima hawa wazungumze na wanafunzi.

Amua kuhusu maswali ya kuuliza, k.m.:

Ni jambo lipi ni muhimu kabisa katika maisha?

Ni tajiriba zipi za maisha zilizokufanya uwe imara zaidi?

Nani aliyekuwa na athari kubwa kabisa kwako katika makuzi yako?

Kubalianeni nani atauliza maswali, na jinsi ya kurekodi yanayosemwa. Wanafunzi na watu wazima yumkini watatumia lugh aya nyumbani.

Baada ya ugeni, jadilianeni wanafunzi walichojifunza.

Waulize wanafunzi: Ni sifa na maadili yapi ungependa kuyajenga ili uwe nayo ukiwa mtu mzima?

Tafuta maneno ya lugha ya nyumbani na lugha ziada yanayotaja sifa na maadili haya, na uyaandike.

Watake waandike kauli za dira na/au malengo yao katika lugha ya ziada. ( Nyenzo-rejea 5: Kauli za dira na lengo inatoa mifano.)

Nyenzo-rejea ya 1: Shairi

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Wewe!

Kichwa chako ni kama ngoma tupu.

Wewe!

Macho yako ni kama mabonge ya moto.

Wewe!

Masikio yako ni kama pepeo za kuchochea moto.

Wewe!

Tundu la pua yako ni kama shimo la panya.

Wewe!

Mdomo wako ni kama bonge la tope.

Wewe!

Mikono yako ni kama mikwiro.

Wewe!

Tumbo lako ni kama chungu cha maji machafu.

Wewe!

Miguu yako ni kama nguzo za miti.

Wewe!

Mgongo wako ni kama kilele cha mlima.

Ibo

Tini za Mwalimu

Shairi hili limeundwa kwa mfuatano wa tashibiha. (Katika mfano huu, mfuatano wa tashibiha ni mfuatano wa matusi pia!). Tashibiha ni ulinganishi, unaotumika kusisitiza sifa fulani alizo nazo mtu au kitu kinachoelezwa. Unaposoma au unaposikia tahsibiha unapiga taswira ya ‘shimo la panya’ (kwa mfano), nah ii inakusaidia kujua jambo fulani kuhusu tundu la pua. Katika kuchambua tashibiha hii zaidi, unajiuliza: ‘tundu la panya li vipi? Ni kubwa kabisa (kulinganisha na tundu la pua). Kuna giza ndani. Kumejaa viota vilivyokaa ovyoovyo na ni kuchafu. Hapo tutaweza kuona waziwazi zaidi mshairi anavyofikiri kuhusu pua ya mtu aliyelengwa.

Tashibiha ni ulinganishi wa wazi. Kwa maneno mengine, mwandishi au msemaji yuko wazi kuhusu ukweli kwamba huu ni ulinganishi. Baadhi ya maneno yanayoashiria tashibiha ni ‘kama’, mathalani: ‘Tundu la pua yako ni kama shimo la panya’ au ‘ Katika shimo la chini kwa chini, kulikuwa ni kweusi kama usiku’.

Kama mshairi angeandika ‘Tundu la pua yako ni shimo la panya’, hii ingekuwa na athari inayofanana nayo, lakini ulinganishi wa namna hii unaitwa sitiari. Hapa ulinganishi ni wa mdokezo. Hatuambiwi kuwa ulinganishi unafanyika. Tundu la pua linaelezwa kama kwamba ni tundu la panya.

Chanzo cha awali: Machin, N. African Poetry for Schools: Book 1

Nyenzo-rejea 2: Mfano wa somo

Taarifa ya usuli / maarifa ya somo kwa mwalimu

Mwalimu (M) anawafundisha wanafunzi (W) wa darasa la 7 Kiingereza (somo la kusoma) (Mwanafunzi = Mw)

M:     Ninalotaka kufanya sasa ni kwamba nitasoma kwanza, na nitawaomba mnifuate. Sawa?

W:    Ndiyo.

M:     Hapo zamani za kale, Mfalme wa Misri alitaka kufahamu jinsi watu wake walivyoishi. Misri iko wapi?

Mw:  Kaskazini mwa Afrika.

M:        Mnakubali? Mnakubali?

W:Ndiyo (Kwa pamoja).

M:     Sawa. Usiku mmoja alivaa kama mtu fukara na kuenda jijini. Jiji ni nini?

Mw: Mji…

M:     Aliwasikiliza watu wake wakilalamika. Watu wake walikuwa wakilalamika. Unapolalamika … ni kwamba huwa hujaridhika na hali ilivyo…

Mw:  Kutoridhika…

M:     Ndiyo, kutoridhika…niendelee na hadithi?

W:Ndiyo.

M:     Basi watu walisema kuwa walikuwa masikini na chakula kilikuwa ghali…Walilalamika…Hakuna aliyecheka katika jiji hili. Hakuna aliyeimba nyimbo, na hakuna aliyekuwa na furaha. Kila mtu alikuwa na huzuni… Mfalme alipokuwa akirejea kwenye ikulu yake… Ikulu ni nini?

Mw:       Ikulu ni mahali anapokaa mfalme.

M:     Vyema. Hadithi inaendelea…

Alipita karibu na kijiduka. Akasikia mtu akiimba. Ndani ya kijiduka. Aliingia ndani. Kijana mwanamme alikuwa amekaa sakafuni, akishona viatu, huku akiimba.

Mshona-viatu alipoona kwamba kuna mgeni, alisimama na kumsalimu. Kisha akampa mfalme mkate na maji. Alimpa nini?

W:    Mkate na maji.

M:     Je, mshona-viatu alifahamu kuwa huyu alikuwa mfalme? Kwa hakika, hakufahamu. Kwa nini hakufahamu?

Mw: Alivaa kama mtu fukara.

M:     Turudi kwenye hadithi. Hebu fikiria picha ya Madiba akiwa amevaa nguo kuukuu.…Unapata picha ya jambo ninalozungumzia?

W:    Ndiyo.

M:     Je, utamfahamu Madiba akitokea mlangoni hapo?

W:        La.

M:     La, hakuna anayeweza kumjua?

Mwalimu aliendelea kusoma hadithi na wanafunzi, akiwauliza maswali kuhusu hadithi hiyo. Maswali mengi yalikuwa yanafanana na hayo ya juu. Wanafunzi waliyajibu kwa ufupi, kwa Kiingereza. Kisha somo liliendelea kama lilivyoelezwa katika Uchunguzi-kifani 2.

Imetoholewa kutoka: Umthamo 3, Mradi wa Elimu-Masafa wa Chuo Kikuu cha Fort Hare

Nyenzo-rejea 3: Usalama

Nyenzo za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Kaka yangu

Kaka yangu ni Ipyana Mwakipesile. Ana umri wa miaka 18, na ni kama baba kwangu. Baba yangu alikufa zamani sana. Ana nafasi muhimu sana katika maish ayetu, ingawa bado ni kijana anayesoma kidato cha tano Shule ya Sekondari Azania. Ni muwajibikaji. Anatutunza. Anapika chakula na kusafisha nyumba. Anamlea mtoto mchanga kwa sababu mama yetu aliaga dunia miezi michache iliyopita. Kila adhuhuri hufunga lango la ua ili tuwe salama ndani. Anatusaidia kwa kila njia. Hatujihisi kuwa mama yetu pia hayupo nasi. Kaka yetu hutupatia upendo ambao tulizoea kuupata kutoka kwa wazazi wetu. Kila Jumamosi, anaoka keki, anafanya manunuzi kama mama alivyokuwa akifanya. Kaka yangu ni kama baba kwetu. Tunamwamini, tunampenda.

Baba yangu

Baba yangu alizaliwa na kukulia Mbeya; baadaye akahamia Dar. Alisomea Shule ya Sekondari ya Minaki; mama yake alikufa baada yamiaka miwili. Baba yake alimwacha na wadogo zake wawili wa kike. Aliishi na babu na bibi, kisha akaishi na shangazi yake, kabla kuhamishiwa kwenye kituo cha watoto yatima.

Wakati akiwa katika kituo cha watoto yatima, alikabiliwa na shida nyingi na alijifunza mengi. Alipambana na watu wajeuri na mara nyingi ilimpasa kuwalinda dada zake. Ingawa alionekana kuwa na muda mgumu, alithamini yote aliyopata kituoni. Jambo gumu kuliko yote lilikuwa kutokuwa na familia yake.

Kutokana na malezi katika kituo cha mayatima, alijifunza kujikimu.

Akiwa ngazi ya juu ya Shule ya Sekondari, alifanywa kuwa kiranja mkuu. Alikuwa maarufu pia, na alishiriki katika shughuli mbalimbali za kitamaduni na riadha pia.

Alipomaliza shule, alijiunga na jeshi la kujenga taifa, na kuona sehemu nyingi za Tanzania. Mara nyingi husimulia hadithi na matukio aliyoshiriki wakati akiwa jeshini. Tajiriba zake katika kituo cha mayatima zilimsaidia kuyamudu maisha ya jeshini, na alikuwa kwenye kundi la viongozi, na akawa mkufunzi. Baba yangu daima amekuwa na marafiki wema na maalumu, na daima amekuwa katika nafasi fulani ya uongozi. Baada ya kumaliza mafunzo na huduma ya kijeshi, alikwenda kuchukua mafunzo ya ualimu.

Akiwa chuoni, alikutana na msichana ambaye baadaye alikuwa mtu muhimu sana katika maisha yake. Baada ya kumaliza masomo, alimposa. Uhusiano huu haukuendelea. Ni wakati huu ambapo mama alikuja kufanya kazi shule moja na baba. Walishikana urafiki na baadaye akamwoa.

Mwaka 1990 nilizaliwa, na tangu hapo nimekuwa karibu naye sana.

Baba yangu amekuwa na nafasi muhimu katika maisha yangu, na ninataka siku moja kurithisha tuzo aliyonipa. Amekuwa mwalimu wangu, kocha wangu wa michezo ya riadha, mshauri wangu, na juu ya yote, rafiki yangu wa karibu.

Imetoholewa kutoka ‘Children First’ Nov/Dec 2004/ Vol 8 No 58, ukurasa wa 5, 6, na 7

Nyenzo-rejea 4: Kauli za Dira na Malengo - mifano

Taarifa ya usuli / maarifa ya somo kwa mwalimu

Kauli ya dira kwa kawaida in fupi. Inalenga siku za usoni na unachotaka kuwa siku za usoni.

Kauli ya lengo kwa kawaida ni ndefu zaidi, na inatoa maelezo zaidi kuhusu mambo ya kufanya ili kutimiza dira.

Hapa kuna mifano miwili:

Kauli ya dira ya shule ya Mtakatifu Jude, Kaskazini mwa Tanzania 

Kuwa asasi ya kisasa, ya mfano na yenye kujiendeleza yenyewe, inayoibua badiliko la kimwelekeo katika mfumo wa elimu wa Tanzania kwa kuwawezesha Watanzania kuendesha shule zenye mafanikio na maadili, na kwa hiyo kupunguza umaskini na kuvunja mzunguko wa utegemezi kwenye misaada ya nje.

Chanzo cha awali: School of St. Jude, Website

Kauli ya lengo la maisha la mtu asiyefahamika

Kuwa mtu ambaye watoto wangu watajivunia wanaposema, ‘Huyu ni babangu”.

Kuwa mtu ambaye watoto wangu watakuja kupata upendo, faraja na welewa.

Kuwa rafiki wanayemfahamu kwa kujali na daima kuwa tayari kusikiliza matatizo yao kwa makini.

Kuwa mtu asiye tayari kushinda kwa gharama ya kuumiza wengine kiroho.

Kuwa mtu anayeweza kusikia maumivu na asiyetaka kuumiza wengine.

To be the person that speaks for the one that cannot, to listen for the one that cannot hear, see for the one without sight, and have the ability to say, ‘You did that, not I.’

Kuhakikisha vitendo vyangu vinalandana daima na maneno yangu kwa neema ya Mungu.

Chanzo cha awali: Covey, S. et al. First Things First

Sehemu ya 5: Kusaidia ujifunzaji wa lugha ya ziada

Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kujenga mahusiano ya kusaidiana katika lugha ya ziada?

Maneno muhimu: mawasiliano ya mtu binafsi; marafiki wa kalamu; kupeana taarifa za ndani.

Matokeo ya ujifunzaji

Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:

  • kuanza kukuza mahusiano baina ya wanafunzi ambayo yatasaidia ujifunzaji wao wa lugha ya ziada na kuwasaidia katika kutafakari juu ya ujifunzaji wao wenyewe;
  • kutoa nafasi kwa wanafunzi kuwasiliana kwa kutumia maarifa ama wazungumzaji wa lugha ya ziada amabao kwao hiyo ni lugha mama kuweka nafasi kwa ajili ya mawasiliano na wanafunzi nje ya shule yako.

Utangulizi

Wanafunzi wengi Afrika wana nafasi chache za kushirikiana na wazungumzaji wa lugha yao ya ziada ambao kwao hiyo ni lugha mama.

Mara nyingi welewa kwenye lugha unapatikana kwa njia za kusoma, kusikiliza redio na kutazama televisheni.

Hata hivyo, zipo njia zitakazowasaidia wanafunzi wako kuzungumza na kuandika kwa watu wenye ufasaha katika lugha ya ziada. Unaweza pia ukawasaidia wanafunzi wako kuwasiliana kwa kutumia lugha ya ziada na wanafunzi wa shule nyingine

Sehemu hii inaangalia njia zitazotumika kufanikisha jambo hili.

Somo la 1

Kwa watu ambao hujifunza lugha katika mfumo wa kawaida wa darasani, misemo ambayo watu hutumia kila siku katika maingiliano yao mara nyingi huwa ni kitu cha mwisho kujifunza.

Zipo njia ambazo zinaweza zikatumika kuwasaidia wanafunzi wako kupata ustadi katika misemo na sentensi ambazo wanaweza kuzitumia pindi wanapokutana na watumiaji stadi wa lugha ya ziada. Kila seti ya misemo au sentensi zinatakiwa:

ziwe fupi na rahisi kujifunza;

ziseme kitu ambacho wanafunzi wanataka;

ziwe zinatumiwa na watu wengi;

ziwaruhusu wanafunzi kuanza majibizano na kujenga mahusiano;

ziwaruhusu wanafunzi kujifunza zaidi kuhusu lugha kutoka kwa watu wanaozungumza nao;

zisichochee majibu marefu toka kwa watu wengine.

Uchunguzi kifani ya 1: Kujifunza kiZulu kupitia katika mahusiano

Liz Botha aliyepo Mashariki mwa London, Afrika Kusini, alijifunza kiZulu kama lugha ya ziada kupitia mradi wa lugha za ndani uitwao TALK. Kauli-mbiu ya mradi wa TALK ilikuwa, ‘Jifunze kidogo, na utumie SANA!’

Alianza kwa kujifunza namna ya kusalimia kwa kiZulu, na kuwaeleza watu kuwa alikuwa anajifunza kiZulu. Alijifunza pia kuwataka wao wamsemeshe kwa kiZulu na kumsaidia katika zoezi lake la kujifunza lugha hiyo.

Aliwatafuta watu ambao anaweza kuzungumza nao kiZulu, na kubaini kuwa kuna idadi kubwa ya wazungumzaji wa kiZulu wanaofanya biashara ya kutembeza matunda na mbogamboga katika mtaa wa karibu na nyumbani kwake. Alifanya mazoezi ya sentensi zake kwao na kuanza kuwaelewa.

Alikuwa na rafiki aliyekuwa anamfundisha misemo mipya, na kujifunza kutoka kwake namna ya kuuliza bei ya kitu fulani na kukinunua. Hizi ndizo sentensi alizozitumia wakati uliofuata alipowaona rafiki zake wanaotembeza biashara.

Kadiri muda ulivyozidi kwenda, alijifunza kujieleza kwao kuhusu yeye mwenyewe na familia yake. Baadaye aliwasimulia hadithi fupi kuhusu nini kilichotokea kwake siku moja kabla, au mwisho wa wiki. Mmoja wa watembeza biashara aliyeitwa Jabu, akawa rafiki yake wa karibu sana na kumfundisha maneno na sentensi nyingi. Mwishowe akawa anawasaidia watu wengine kujifunza kiZulu katika mradi wa TALK.

Shughuli ya 1: Kujenga mahusiano ya kujifunza lugha

Waulize wanafunzi wako ni wapi wamesikia lugha ya ziada ikizungumzwa. Ni watu gani pia wanaowafahamu kuwa wanaitumia vizuri? Ni nani wanaweza kuzungumza naye lugha ya ziada? Zingatia watu waliopo nje na ndani ya shule na pia watu ambao unaweza ukawaalika katika darasa lako. Fikiria ushirikiano na shule ya karibu kama unaweza kukuza mtagusano katika lugha ya ziada.

Sasa wanafunzi wako wanafahamu ni akina nani wanataka kuzungumza nao, pangilia mambo wanayotaka kusema nao.

Kwa utaratibu maalum, wasaidie kujifunza msamiati kama mradi wa muda mrefu. Weka uzito katika sauti na matamshi bayana.

Waache wafanye mazoezi wawiliwawili.

Mawazo juu ya vitu vya msingi vya kujifunza yanajumuisha:

salamu na kuagana;

kutaja na kuuliza majina na taarifa binafsi na za familia;

kueleza kuwa wao ni watu wanaojifunza lugha na kuwa wanahitaji msaada wa kujifunza;

kununua vitu;

kuzungumzia kuhusu hali ya hewa;

kuelezea mambo yalitokea jana;

kuomba radhi, kuomba kitu au jambo, kusifu, n.k

Wahimize wafanye mazoezi na watu waliowapendekeza (hapo juu).

Tenga muda fulani kila wiki ili kufuatilia maendeleo yao.

Je kuna mafanikio na matatizo gani wamekumbana nayo? Ni lugha ipi mpya wamejifunza?

Nini kingine walichojifunza?

Somo la 2

Katika sehemu hii,tunapendekeza kuwa uwahamasishe wanafunzi waandike barua kwa kutumia lugha ya ziada. Hii inaweza kuwa na maana ya kuweka mhusiano ya mbali na wazungumzaji wa lugha ya ziada, ama wanaweza kuwaandikia rafiki zao wa karibu.

Unaweza kuanzisha utaratibu wa rafiki wa kalamu na darasa lingine (tazama Nyenzo-rejea 1: Marafiki wa kalamu ). Hili linaweza kuwa darasa katika nchi yako au nchi nyingine.

Kama wanafunzi watakuwa waandishi na wasomaji wanaojiamini wakingali shule ya msingi, kuna uwezekano mkubwa kuwa waandishi wa barua wenye mafanikio hapo baadaye katika maisha yao. Kadiri wanavyoandika barua binafsi kwa marafiki zao, unaweza pia ukafundisha mtindo mwingine wa uandishi wa barua. Hili litawaandaa kwa ajili ya mahitaji ya baadaye, kama vile, kuomba kazi, barua kwenda magazetini, barua za pongezi au rambirambi.

Uchunguzi kifani ya 2: Kuandika kwa ajili ya kufariji au kulalamika

Wanafunzi wa darasa la 5 la Bibi Linda Shigeka walikuwa katika mfadhaiko na hawakuweza kushiriki vema katika kazi zao za shule. Mwanafunzi mwenzao mmoja, Mandisa, alifariki katika ajali ya basi. Walimkumbuka sana rafiki yao.Walikuwa pia na hasira kwa sababu walisikia kuwa basi halikuwa na breki.

Bibi Shigeka aliwahimiza wanafunzi kueleza namna wanavyojisikia. Alibaini kuwa wanataka kufanya jambo fulani, akawauliza kama wanataka kuiandikia familia ya Mandisa barua. Akapendekeza kuwa waandike barua mbili, moja kwa Kiswahili kwa ajili ya wazazi na wazee (babu na bibi) na nyingine kwa Kiingereza kwa ajili ya kaka na dada ambao wamekulia London wakati wazazi wao walipokuwa uhamishoni. Wanafunzi walisema kuwa wanataka kuieleza familia ya Mandisa kuwa wapo pamoja nao na pia wanataka kuwaeleza mambo mazuri kuhusu Mandisa.

Bibi Shigeka aliwasaidia kwa kuwapa dondoo za maandishi yao. Wanafunzi waliandika barua binafsi kwa Kiswahili. Katika somo lililofuata, Bibi Shigeka aliwasaidia kuandika barua moja kwa Kiingereza kwa ajili ya darasa zima na kisha kila mwanafunzi aliweka saini yake

Kwa msaada wa Bibi Shigeka, waliandika pia barua kwa Kiingereza kwenda kwenye kampuni ya basi wakiomba kuwa mabasi yakaguliwe vema kuhakikisha kuwa ni salama na yanafaa kutembea barabarani.

Wanafunzi walipata majibu ya barua zote mbili walizoandika. Bibi Shigeka akazibandika barua hizi kwenye ubao wa matangazo uliopo darasani.

Bibi Shigeka alibaini ni kwa namna gani suala hili limewahamasisha wanafunzi na kuwapa stadi muhimu ya kijamii. Imewasaidia pia kuona lengo la kujifunza lugha ya ziada.

Shughuli ya 2: Barua ya kwenda kwa rafiki au rafiki wa kalamu

Soma Nyenzo-rejea 1 kwanza, na anzisha uwenza na shule jirani.

Mpe kila mwanafunzi darasani mwako jina la rafiki wa kalamu ambaye wanaweza kuanzisha uhusiano. (Kama haitawezekana, jaribu kumfanya kila mwanafunzi kumtambulisha mwanafunzi wa darasa lingine au jamaa au rafiki wa mbali na nyumbani ambao wangependa kuandikiana barua). Kama una shule nyenza tayari au ndiyo unaiasisi ( angalia Nyenzo-rejea 1 kwa namna ya kulitekeleza hili ), dumisha mawasiliano ya karibu na mwalimu mwenza wako, kujadili matatizo nyeti na kuyatafutia suluhisho kwa pamoja.

Jadili na darasa lako juu ya vitu ambavyo wangependa kuzungumzia katika barua yao ya kwanza. Wakati huo huo wanaweza kubadilishana habari juu ya maisha yao, familia zao, rafiki zao, mambo wayapendayo na matarajio yao.

Ridhia muundo wa barua (angalia Nyenzo-rejea 2: Kuandika barua ), na waache waanze kuandika. Zungukazunguka ukiwasaidia maneno na virai wanayohitaji.

Waache wapitie na kuhariri barua zao katika jozi. (angalia Nyenzo-rejea 3: Kupima ubora wa barua za marafiki wa kalamu ). Zichukue barua, na toa mrejesho saidizi na wenye kujenga.

Waache wanafunzi waandike toleo la mwisho la barua yao, andika anuani juu ya bahasha na uitume (kwa njia ya posta).

Kwa wanafunzi wadogo, hii yaweza kuwa shughuli ya darasa zima na andika wanayotaka kusema. Wanaweza kuwaandikia darasa jingine hapo shuleni.

Je, unawezaje kusaidia maendeleo ya huu uhusiano wa kuandikiana barua?

Je, unawezaje kusaidia pale unapohitajika, wakati wa kutoa nafasi kwa mahusiano kukua?

Somo la 3

Kuzalisha vitabu ambavyo wanafunzi wameandika na kuvitengeneza, sio tu kunawaongezea kujisifu, lakini pia kunakupatia Nyenzo-rejea nzuri darasani.

Sehemu hii hujengwa na mawazo ya Kitabu Kikubwa katika Moduli 1, Sehemu 5. Inapendekeza kuwa uwape moyo wanafunzi wako kuyaleta maandishi na michoro yao katika hatua ya mwisho kwa kutengeneza kitabu. Hii wanaweza kushirikiana darasani, au na watu, kikundi au shule nyingine.

Unatakiwa ufikirie ni kwa jinsi gani unaweza kupanga na kuendesha zoezi kama hili. Utatakiwa kufikirikiria juu ya aina ya kitabu cha kutengeneza (mfano kitabu cha kukunja), vielelezo na mpangilio wa kitabu, na aina ya kitabu (k.m kitabu cha nyimbo, kitabu cha hadithi au kitabu cha hadithi isiyo ya kubuni).

Utapaswa kufikiria juu ya nyeno rejea zitakiwazo na wapi pa kuzipata. Uanweza kuwashirikisha wanafunzi katika kukusanya baadhi yake kabla hujaanza kabisa kazi darasani. Aina hii ya upangaji na uandalizi ni muhimu kama darasa lako ni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kujifunza (angalia Nyenzo-rejea muhimu: Kuwa mwalimu mwerevu katika mazingira (hali) yenye changamoto .)

Uchunguzi kifani ya 3: Kutengeneza kitabu cha darasa

Bibi Ndekule, ambaye anafundisha wanafunzi 44 wa darasa la 5 huko Zanzibar, alitaka kuwatia moyo kama waandishi na wasomaji na aliamua kutengeneza nao kitabu kwa kutumia lugha yao ya ziada ya Kiingereza.

Aliwambia kuwa alitamani kuanzisha hifadhi ya vitabu kwa ajili ya darasa, na ingestawi tu kama wangezalisha baadhi ya vitabu vyao wenyewe. Walijadili aina gani ya vitabu walipenda kusoma na aliviorodhesha ubaoni. Orodha ilijumuisha, riwaya, mashairi na vitabu juu ya michezo na mavazi. Halafu aliwambia wanafunzi waunde makundi madogo yasiyozidi watu sita wenye kupenda aina fulani ya kitabu.

Bibi Ndekule ailjadiliana na kila kundi juu ya aina ya kitabu watakachoandika. Kundi moja liliamua kujigawa katika makundi mawili ya watu watatu kutengeneza vitabu viwili vya michezo, kimoja cha mpira wa miguu na kingine cha riaadha. Kundi jingine lilitaka kuandika kitabu cha hadithi juu ya hadthi za mapokeo. Bibi Ndekule aliyapa makundi muda kupanga dondoo zao kabla hajawaambia wajadiliane na wengine. Darasa lilitoa mwitikio kwa kila kundi. Katika wiki iliyofuata, aliwapa muda wa darasani na wa kazi za nyumbani kuadika kazi zao.

Walipomaliza rasimu zao za mwanzo, Bibi Ndekule alizipitia na kutoa mwitikio juu ya njia za kuboresha vitabu vyao. Rasimu zao za mwisho zilikuwa ziameisha katika wiki iliyofuata na ziliwekwa kwenye maonesho kwa ajli ya darasa zima kuvisoma.

Shughuli muhimu: Kutengeneza kitabu cha ubia

Pendekeza kwa darasa lako watengeneze kitabu kwa ajili ya shule nyenza (au kwa lengo jingine) kikiwa na nyimbo, mapishi na habari nyingine za nyumbani. Kama una kitabu cha mapishi, waoneshe. Baadhi ya vitabu vya mapishi huwa na picha , habari na hadithi juu ya mahali na watu wanaohusiana na mapishi.

Amua ni nyimbo zipi au mapishi yapi yatajumuishwa na jinsi yatakavyo wasilishwa. (angalia Sehemu 1).

Amua kwa pamoja ni mambo gani zaidi yatakuwemo ndani ya kitabu. Angalia Nyenzo-rejea 4: Nyimbo na hadithi kuhusu michakato –nyimbo hizo hizo na hadithi zinaweza kujumuishwa. Mashairi na maelezo kutoka kwenye shughuli zilizopo katika Sehemu 2 na 4 zinaweza kuhusishwa. Fikiria kuhusu vielelezo(michoro), picha, maelekezo ya michezo ya asili, riwaya au mashairi.

Panga na wanafunzi wako ambao watafanya kila sehemu ya kazi, nani atahariri kazi na lini kila sehemu ya kazi itakuwa iimekamilika. (Moduli 1, Sehemu 5, Nyenzo-rejea 1: Jinsi hadithi zinavyotengenezwa kitabu. Huonesha jinsi kitabu kinavyoandaliwa na watu tofauti.)

Andaa mpango. Kama inawezekana, toa nakala ya kitabu ili kimoja ubaki nacho na kingine ukipeleke katika shule nyenza. Waombe pia shule nyenza kama wanaweza kukutumia kitabu walichotengeneza.

Pale nyenzo zinapokuwa chache, karatasi zilizotumika, kalenda za zamani, magazeti ni vifaa ambavyo unaweza kuvikusanya kirahisi kutengenezea kitabu. Kwa mawazo zaidi, angalia Rejea muhimu: Kuwa mwalimu mwerevu katika mazingira yenye changamoto.

Nyenzo-rejea ya 1: Marafiki wa kalamu

Taarifa ya usuli / maarifa ya somo kwa mwalimu Wewe!

Kama unapenda kuwa na mawasiliano na shule katika nchi yako au nchi nyingine ambayo pia hutumia vifaa vya TESSA , tafadhali wasiliana na Jane Devereux wa Open University, kwa kutumia j.b.devereux@open.ac.uk au tumia anuani ifuatayo: The Open University, P O Box 77, Walton Hall, Milton Keynes MK7 6BT, UK.

Pia unaweza kuasisi uhusiano kati ya darasa lako na darasa la rika sawa kutoka shule nyingine na panga kila mmoja wa wanafunzi wako kuwa na rafiki wa kalamu. Hii itawapa wanafunzi wako faida ya kuwa na rafiki wa kumwandikia na kupokea majibu kutoka kwake, juu ya maswala yanayowapendeza, kutumia lugha ya ziada au lugha ya biashara/maasiliano. Watapata mazoezi katika kusoma na kuandika kwa lengo maalum, na kujifunza zaidi juu ya watu wengine, familia zao, shule, nchi na mtindo wa maisha.

Kabla hujawaingiza wanafunzi wanafunzi wako kwenye mpango/mradi, hakikisha umeshachanganua vizuri mambo kama ville mgawo na malipo ya bahasha na stampu. Unaweza ukaweka barua zote kwenye bahasha kubwa na kuituma kwa mwalimu.

Nyenzo-rejea 2: Uandishi wa barua

Taarifa ya usuli / maarifa ya somo kwa mwalimu

Wanafunzi wana mwelekeo wa kufurahia zaidi uandishi wa barua (katika ama lugha ya mama au lugha ya ziada) kama wanahisi kuna sababu halisi ya kuandika na kwamba watu wengine watavutiwa kuzisoma. Kutakuwa na hali kadhaa ambapo utumizi wa lugha ya ziada utakuwa ni mwafaka zaidi. Kwa kila hali, unapaswa kujadili lugha ipi ya kutumia.

Unaweza kupanga na walimu katika shule nyingine ili wanafunzi wa shule moja wawaandikie barua wanafunzi wa shule nyingine (taz. Nyenzo- rejea 1). Unaweza pia kuwasaidia wanafunzi kuandika barua kwenye kampuni kuomba mchango wa fedha, vitu au huduma kwa ajili ya shule. Kama umewapeleka kwenye ziara katika jumuiya yako kwa mfano kliniki, mradi wa kilimo au kiwanda, unaweza kuwasaidia kuandika barua ya shukurani. Kunaweza kuwepo matukio ya furaha au huzuni ambapo ingekuwa vyema kwao kumwandikia mtu barua ya pongezi/hongera au rambirambi.

Kwa aina yoyote ya barua utakayotaka kushughulikia, kwanza jadiliana na wanafunzi kwa nini watu huandika barua na mambo wanayotaka kusema katika aina hiyo ya barua. Andika mawazo yao ubaoni, na uwasaidie kuyapanga katika aya. Ukitaka unaweza kutumia vidokezo vilivyo hapa chini.

Pindi wanafunzi wamalizapo barua zao, zitume kwa mtu au shirika lililolengwa. Unaweza kukusanya barua zote na kuziweka kwenye bahasha moja kubwa ikiwa na anwani husika. Kama wewe na wanafunzi mna bahati, mtapata jibu!

Vidokezo vya barua kwa ‘rafiki wa kalamu’ katika shule nyingine (au nchi nyingine).

Mpendwa ……………….

Nimefurahi sana kwamba tutakuwa marafiki wa kalamu. Katika barua hii lengo langu ni kujitambulisha kwako.

Jina langu kamili ni ………………………………. Nina umri wa miaka …... Kwa kuwa sina picha ya kukutumia sasa hivi, nitaeleza ninavyoonekana. [ikifuatwa na sentensi zenye maelezo haya]

Ningependa kukuambia juu ya familia yangu [ikifuatwa na sentensi kuhusu familia]

Tunaishi ………………… [ikifuatwa na sentensi juu ya mahali ]

Haya ni baadhi ya mambo ninayopenda. Chakula ninachokipenda ni….muziki ninaoupenda ni ……………. Somo ninalolipenda zaidi shuleni ni ……..

Wakati wa wikendi mimi hupendelea……….

Nitakapomaliza shule ninatarajia ……………….

Ninatarajia kupata jibu kutoka kwako hivi karibuni……………

Ninakutakia kila la heri,

Wako,

[Jina na saini]

Vidokezo vya barua ya shukurani baada ya ziara ya shule

Mpendwa ……………….

Kwa hakika nilifurahia ziara yetu hapo.……………….

Kilichonivutia kuliko vyote kilikuwa …………………………….

Nilifikiri hili lilikuwa na mvuto kwangu kuliko vitu vingine kwa sababu……………………

Kama shule yetu itapata nafasi ya kufanya ziara nyingine, ningependa ……………….

Ninakushukuru sana kwa ……………………………………………….

Wako mwaminifu,

[Jina na saini]

Vidokezo vya barua kwa kampuni kuomba mchango

Bw./Bi ……… [jina la mtu]

Ninaandika barua kuomba msaada wako. Shule yetu inahitaji …………………

Tunahitaji hili kwa sababu ……………………………………………………….

Ninakuandikia kwa sababu …………………. [sababu kwa nini kampuni hii inaweza kusaidia]. Ninatumaini utaweza kutusaidia. Wako mwaminifu

[Jina na saini]

Nyenzo-rejea 3: Kutathmini barua za urafiki wa kalamu

Kwa matumizi ya mwanafunzi

Je, barua inaunda picha hai na ya kuvutia ya mwandishi? Taarifa gani zinatakiwa kuongezwa ili kuifanya ivutie zaidi?

Je, maelezo yametolewa kwa ufasaha? Je, barua inasomeka kwa urahisi?

Je, mada tofauti zimeshughulikiwa katika aya tofauti?

Je, barua iko katika njeo sahihi? (Maelezo yanaweza kuwa katika njeo iliyopo.) Je, kila kitenzi kiko katika njeo iliyopo au, kama si hivyo, kuna sababu ya msingi ya kutumia njeo tofauti? (Unaweza kuamua kuhusu aina za miundo unayotaka kukazia katika shughuli hii.)

Je, barua inaonekana ni nzuri? (Safi, imepangiliwa vizuri.)

Nyenzo-rejea 4: Nyimbo na hadithi kuhusu michakato

Nyenzo-rejea za mwalimu kwa ajili ya kupanga na kutumia na wanafunzi

Hapa kuna wimbo wa kijadi wa Kiswahili unaofafanua michakato mbalimbali ambamo nafaka hupitia kabla ya kuliwa. Uliambatishwa katika kijitabu cha ‘Michakato na Uchakataji’. Wimbo huo unaweza kuingizwa kwenye kitabu cha mapishi. Hadithi zinafuatia, ambazo nazo zinatoka kwenye chanzo hicho hicho, zinaweza pia kujumuishwa kwenye kitabu hicho cha mapishi au cha mchakato.

Ninakipenda chakula

Chakula cha asubuhi,

Makande, uji na viazi

Ugunduzi wa mtama

Hapo zamani za kale palikuwa na mwanaume aliyekuwa na wake wawili. (Katika baadhi ya sehemu za Afrika, wanasema, ‘Mke mmoja – tatizo moja. Wake kumi na mbili – matatizo kumi na mbili!’) Mke mkubwa hakuweza kuwa na watoto, kwa hiyo alipogundua kuwa mke mdogo alikuwa mjamzito, aliona wivu sana. Lakini hakuwa na la kufanya.

Mume na mke mdogo wakapendana sana. Na hili likamfanya mke mkubwa aone wivu zaidi. Kwa hiyo mke mkubwa aliamua kusubiri mpaka baada ya mke mdogo kujifungua.

Lakini mtoto alipozaliwa, alikuwa ni mtoto wa kiume. Kwa mujibu wa mila, mke mkubwa alitakiwa kuwatunza mtoto mchanga na amariya (mke mdogo) kwa miezi michache. Mke mkubwa aliamua kwenda msituni kutafuta kitu cha kumpikia mke mdogo ambacho kingemdhuru. Alitarajia kwamba mke mdogo angekufa, na hapo angeweza kumlea mtoto mchanga kama mtoto wake mwenyewe.

Kule msituni, mke mkubwa aliona mmea ambao ulikuwa na vichwa vyenye punje zikuazo juu yake. Hajawahi kuona kitu kama hiki hapo awali. ‘Hii itamfanya alale, usingizi mzito hasa, kiasi kwamba hataweza kuamka siku itakayofuata. Kisha nitaandaa mazishi mazuri sana.’

Alipika mtama na kumlisha amariya. Alipata mshangao, amariya hakulala usingizi mzito wala kufa. Badala yake, alinenepa na kuonekana mwenye afya na kupendeza kila uchao. Vilevile, mtoto mchanga alinawiri.

Mke mkubwa alipoona matokeo ya kitu alichokuwa anakipika na kumlisha mke mdogo, aliamua kukionja yeye mwenyewe. Aliipenda ladha yake, na aliendelea kukipika na kukila kitu hicho kipya. Yeye pia, alianza kunenepa na kuwa na afya zaidi.

Sawa, mume alishindwa kujizuia kuona kuwa wake zake wawili walipendeza sana, na mtoto alikuwa na afya. Alitaka kukionja, kwa vyovyote kilivyo kitu hicho, ambacho wakeze walikuwa wanakula. Kwa hiyo, wote wakawa wanene na wenye afya.

Na, kwa hakika, katika kijiji, neno husambaa kwa haraka sana, Kabla muda haujapita, wanakijiji wote waliobaki walitaka kujua kitu ambacho familia hii ilikuwa inakula. Na ndivyo ikawa kwamba mtama ukagunduliwa.

Ugunduzi wa jibini

Hapo kale palikuwa na wanandoa vijana waliokuwa na kundi kubwa la ng’ombe na kundi kubwa la kondoo. Mume aliilisha familia yake kwa kukamua ng’ombe. Nyakati hizo, walihifadhi maziwa kwenye vibuyu.

Wanandoa hao wakati mwingine waligombana; na mke alionekana akikimbilia kwa mama yake, huku mumewe akikimbia kumfuata, kwa kufoka na kupiga ngumi hewani.

Siku moja wakati walipokuwa wakigombana, mume alikuwa ameshika kimojawapo kati ya vibuyu vyenye maziwa mazito yenye malai. Wakati mke wake alipokimbia, mume alimkimbiza, kama kawaida. Lakini safari hii alisahau kuweka chini kibuyu cha maziwa mazito yenye malai. Kadri alivyokuwa akikimbia na kumfokea mkewe, alikunja ngumi yake huku akiwa amekishika kibuyu hewani. Kwa hakika, mume alikimbia upesi sana kiasi kwamba kibuyu cha maziwa kilitikisika kwa nguvu hasa.

Aliposhindwa kumkamata mkewe, hali ya kuwa ameishiwa na pumzi, mwanaume alikaa chini. Alikuwa anasikia joto na kiu baada ya kumkimbiza mke wake na kumfokea. Kwa hiyo aliweka kibuyu mdomoni ili anywe kinywaji cha maziwa mazito yenye malai. Lakini hayakuwa maziwa yaliyomwagika toka kwenye kibuyu. Yalikuwa vitu kama maji! Haya yote yalikuwa ni makosa ya mke wake!

Mume alipigwa na butwaa. Alikaa chini na kuangalia ndani ya kibuyu. Kitu gani kimetokea kwenye maziwa mazito yenye malai? Kwa nini yamegeuka kuwa kitu cha majimaji? Akajaribu kuweka funda lingine mdomoni. Ikawa hivyo hivyo. Akaweka mkono wake ndani ya kibuyu na kugundua kwamba kulikuwa na bonge fulani. Nina hakika unaweza kukisia kitu alichokiona. Ndiyo, ni sawa, ilikuwa ni bonge la jibini laini yenye mafuta. Wakati mume aliporamba vidole vyake, aliona kwamba bonge la kitu hicho lilikuwa na ladha nzuri. Ilikuwa kama mafuta.

Alirudi nyumbani kwake haraka, akatafuta mkate wa mahindi, na kuupaka kiasi cha mafuta toka kwenye kibuyu kwenda kwenye kibonge cha mkate. Mkate ulikuwa na ladha nzuri zaidi kuliko kawaida. Hasira yake ikayeyuka. Wakati mkewe aliporudi baada ya kitambo kidogo, alimwonesha kilichotokea, na alimpa kiasi cha mafuta ili ajaribu kukionja kwenye mkate.

Kwa muda mrefu baada ya hapo, kila jibini inapokuwa imemalizika, mume alianzisha ugomvi na mkewe ili aweze kuchukua kibuyu cha maziwa mazito yenye malai anapomkimbiza. Alielewa kwamba kwa namna hiyo, maziwa mazito yenye malai yatatengeneza jibini.

Siku moja wakati jibini kidogo sana ilikuwa imebakia, mke alichukua kibuyu cha maziwa mazito yenye malai na kukitikisa kwa nguvu kadri alivyoweza. Alikitikisa, na kukitikisa. Alipoacha kukitikisa zaidi, alikiweka chini. Unaweza kukisia alichokiona ndani ya kibuyu, huwezi? Aliona jibini, na kiasi cha majimaji ya maziwa.

Jioni hiyo mume aliporudi nyumbani, mkewe alimgeukia na kusema, ‘Labda kama tutatingisha kibuyu kilichojaa maziwa mazito yenye malai kwa nguvu, tutatengeneza jibini nyingi zaidi. Hivyo hatutalazimika kugombana tena.’

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa, kwamba waliishi kwa raha mustarehe, na kuwa familia yenye afya kwa kupiga maziwa mazito yenye malai kutoka kwenye mifugo yao, na jibini, ambayo wamejifunza kuitengeneza.

Imetoholewa kutoka: Ngtetu, C. & Lehlakane, N., Inqolowa, The Discovery of Amazimba and The Discovery of Butter, Umthamo 3, University of Fort Hare