Namba ya moduli 3: Uhamasishaji wa mawasiliano katika lugha ya ziada
Sehemu ya 1: Kuandaa mazingira asilia kwa ajili ya mazoezi ya lugha
Swali Lengwa muhimu: Unawezaje kuwasaidia wanafunzi kufanya mazoezi ya muundo wa lugha katika mazingira asilia?
Maneno muhimu: usimamizi wa darasa; michezo; mapishi; maelekezo; mchakato
Matokeo ya ujifunzaji
Mwishoni mwa sehemu hii, utakuwa umeweza:
- Kutumia uongozi/utawala wa darasa kuwasaidia wanafunzi kujifunza lugha ya ziada;
- Kutumia michezo na shughuli za kila siku kuimarisha wanafunzi kuhusu stadi za lugha na msamiati.
Utangulizi
Wanafunzi wako wana fursa gani kupitia –redio, vitabu, magazeti, wazungumzaji wa lugha na televisheni kwa lugha ya ziada ukilinganisha na ile inayotumika nyumbani?
Jawabu linaweza kuwa ni ‘fursa ndogo’. Wanaisikia na kuitumia kila siku darasani shuleni. Hii ina maana kuwa unawajibika kuwapa fursa ya kutumia lugha ambayo itawasaidia wanafunzi:
Kuitumia na kuwa wazungumzaji hodari katika matumizi ya msamiati mpya na muundo wa sarufi;
Kuwasiliana kwa kutumia lugha ya mazungumzo katika mazingira ya kijamii;
Kuimarisha na kuendeleza stadi zao za kusoma na kuandika.
Yote haya yanahitaji tafakuri ya hali ya juu, na upangaji na stadi makini. Sehemu hii itakupatia mikakati na mbinu za kukusaidia.