Skip to main content
Printable page generated Saturday, 20 April 2024, 5:10 PM
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Saturday, 20 April 2024, 5:10 PM

1. Kupanga Utunzaji katika Ujauzito

Kipindi cha 1 Kupanga Utunzaji katika Ujauzito

Utangulizi

Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu hali ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga duniani kote, Afrika kwa jumla ili uweze kuelewa kiwango cha matatizo yanayohitaji kushughulikiwa kupitia huduma bora za afya kwa kina mama na wototo wachanga. Utunzaji katika ujauzito, ambao ni huduma ya kitaalamu ya afya ambayo mwanamke hupata kwa muda wote wa ujauzito ni muhimu kwa kusaidia kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wachanga wanaongoka katika ujauzito na kuzaliwa. Tunakuonyesha jinsi ya kupanga huduma za utunzaji katika ujauzito ambao jamii yako inahitaji ili kuimarisha na kulinda afya ya kina mama na watoto wachanga katika ujauzito, kuzaa na kipindi baada ya kuzaa. Utajifunza kinachomaanishwa na sifa za huduma zifaazo katika ujauzito katika jamii yako na jinsi ya kukokotoa idadi ya kina mama wajawazito kila mwaka katika eneo lako. Watahitaji utunzaji kwa muda wote wa ujauzito na usaidizi wako wa kistadi wakati wa uchungu wa kuzaa, kuzaa na katika kipindi baada ya kuzaa. Pia utakuwa ukikusanya na kuripoti data juu ya idadi ya awamu za huduma hizi anazopata kila mwanamke na sehemu ya waliozaa kwa kuhudumiwa na mtaalamu wa afya.

Malengo ya Kipindi cha 1

Baada ya kipindi hiki unafaa uweze;

1.1 Kufafanua na kutumia kwa usahihi maneno yote yaliyoandikwa kwa hefufi nzito (maswali ya kujitathmini 1.1, 1.2 na 1.4)

1.2 Kulinganisha kiwango cha vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga na matatizo barani Afrika na hali ilivyo ulimwenguni kote na Afrika kwa jumla (maswali ya kujitathmini 1.1)

1.3 Kujua jinsi ya kukadiria idadi ya wanawake wajawazito watakaohitaji utunzaji katika ujauzito katika jamii yako kwa mwaka mmoja (maswali ya kujitathmini 1.2)

1.4 Kujua jinsi ya kupanga mpango wa utunzaji katika ujauzito ulionuiwa wa mara nne kwa kila mwanamke mjamzito kwa muda maalum katika eneo lako (maswali ya kujitathmini 1.3)

1.5 Kujua jinsi ya kukokotoa kiwango cha matumizi ya huduma za utunzaji katika ujauzito na sehemu ya waliozaa kwa kuhudumiwa na mtaalamu wa afya katika eneo lako (maswali ya kujitathmini 1.2)

1.6 Kujua jinsi ya kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na wa vifo vya watoto wachanga katika eneo lako (maswali ya kujitathmini 1.4)

1.1 Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga

Tunaanza kipindi hiki kwa kueleza idadi ya kina mama na watoto wachanga wanaofariki kutokana na matatizo ya ujauzito na kuzaa duniani. Shirika la Afya Duniani liliweka malengo ya milenia ya maendeleo mwaka wa 2000 (1992 katika kalenda ya Afrika) ili kupunguza kwa robo tatu vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika kila nchi na kwa theluthi mbili vifo vya watoto walio chini ya miaka 5 kufikia mwaka 2015 (2007 katika kalenda ya Afrika). Afrika ni mojawapo ya bara chache duniani inayotarajiwa kutimiza malengo haya kwa kupunguza vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto. Jukumu lako kama mtalamu wa afya ni muhimu katika kutimiza malengo haya.

Tarehe zote zilizo katika moduli hii zinatumia mfumo wa kalenda ya Uropa na Amerika.

1.1.1 Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na matatizo

Kifo cha mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa hufafanuliwa kama kifo cha mwanamke akiwa mjamzito au katika muda wa siku 42 baada ya mwisho wa ujauzito, bila kuzingatia muda na mahali pa ujauzito, kutokana na visababishi vyovyote vinavyohusiana au kukuzwa na ujauzito au utunzaji wake, bali si kutokana na ajali au visababishi vinavyoambatana na matukio (yaani visababishi vya vifo visivyohusiana na ujauzito huo).

Visababishi vitano vikuu vya vifo vya kina mama kabla,katika na muda mfupi baada ya kuzaa ni:

  • Utoaji mimba usio salama
  • Eklampsia isababishwayo na shinikizo la damu hatari wakati wa ujauzito
  • Vizuizi wakati wa kuzaa
  • Kuvuja damu baada ya kuzaa
  • Maambukizi baada ya kuzaa

Utajifunza kuhusu kila aina ya visababishi hivi kwa kina katika vipindi vya baadaye katika moduli hii. Hapa tunaangazia jinsi data kuhusu vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa hukusanywa na kuripotiwa ili uweze kukadiria vifo hivi katika eneo lako.

Kila mwaka, Shirika la Afya Duniani hukadiria kuwa wanawake 536,000 ulimwenguni hufa kutokana na matatizo ya ujauzito na kuzaa na kuwa asilimia 99 yao wako katika nchi zinazoendelea. Angalau wanawake milioni 7 wanaoongoka katika kuzaa huathiriwa na matatizo mabaya ya kiafya kwa muda mrefu. Pia, wanawake milioni 50 zaidi huathirika kutokana na matokeo mabaya ya kiafya baada ya kuzaa. Mengi ya matatizo haya hutokea katika nchi zinazoendelea (Ripoti ya Shirika la Afya Duniani kuhusu Maendeleo ya kutimiza Malengo ya Milenia ya Maendeleo iliyochapishwa mwaka 2009).

Kila mwaka barani Afrika, wanawake milioni 30 hushika mimba na milioni 18 kati yao huzalia nyumbani bila kuhudumiwa na mtaalamu wa afya mwenye ujuzi. Kutokana na haya, wanawake waafrika zaidi ya 250,000 hufariki kila mwaka kutokana na matatizo yanayohusiana na ujauzito na kuzaa. Wanawake waafrika milioni 4 wana matatizo ya ujauzito yasiyo hatari (Okoa Watoto, USAID, UNFPA, UNICEF, WHO, Nafasi kwa Watoto Wachanga Waafrika; Data tendaji, Hati na utaratibu mwafaka wa kusaidia utunzaji wa watoto wachanga Afrika, mwaka 2006).

  • Ni sehemu gani ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa duniani hutokea barani Afrika?

  • Wanawake Waafrika wanachangia karibu nusu ya wanawake 536,000 wanaofariki kila mwaka duniani kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa.

    Mwisho wa jibu

Uwiano wa Vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa

Njia bora zaidi ya kulinganisha viwango vya vifo vya kina mama vitokanavyo na ujauzito katika maeneo tofauti ya dunia ni kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa ambao hukuonyesha idadi ya vifo vya kina mama kwa kila watoto 100,000 wazaliwao wakiwa hai. Uwiano huu umetambuliwa kimataifa kama mojawapo ya viashirio muhimu vya afya ya kina mama na ubora wa utunzaji katika ujauzito, kuzaa na baada ya kuzaa katika nchi fulani. Baadaye katika kipindi hiki, tutakuonyesha jinsi ya kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika eneo lako.

Ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa mwaka wa 2000 na 2005 umeonyeshamakadirio ya uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika nchini humo. Mwaka wa 2000, kina mama 871 walifariki kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai barani Afrika. Kufikia mwaka wa 2005, idadi hii ilikuwa imepungua hadi 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Hii ni chini ya 900 kwa kila watoto 100,000 wazaliwao wakiwa hai katika Afrika nzima. Hii bado ni mojawapo ya viwango vya juu sana duniani. Katika mwaka 2008, wastani wa dunia nzima wa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa ulikuwa vifo 400 vya kina mama kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Wastani wa Uropa ulikuwa 27 tu kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai.

Mchoro 1.1 Sehemu ya uzazi uliofanyika Nyumbani na Hospitalini katika mwaka wa 2005.

Barani Afrika mwaka wa 2005, takribani wanawake milioni 3,119,000 walizaa. Mchoro 1.1 unaonyesha kuwa asilimia 94 ya uzazi huu ulifanyika nyumbani - hasa katika jamii za vijijini kama yako (Ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa Barani Afrika mwaka wa 2005).

  • Kokotoa idadi ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika mwaka wa 2005 ukizingatia uwiano wa vifo vya kina mama kwa mwaka huo.

  • Uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika mwaka wa 2005 ni 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai na kulikuwa na wachanga 3,119,000 kwa jumla mwaka huo. 3,119,000 ikigawanywa na 100,000 ni 31.19. Kwa hivyo, nchini humo kwa jumla, 31.19 x 673 ni wanawake 20,991 waliofariki kutokana na matatizo ya ujauzito au kuzaa.

    Mwisho wa jibu

Ingawa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa huwapa wanaotengeneza sera za afya ya umma kipimo cha ukubwa wa tatizo la vifo hivi vya kina mama, hauwezi kutufahamisha kuhusu utatuzi unaohitajika kwa kuokoa maisha ya wanawake. Kusoma katika moduli hii yenye mchanganyiko wa mafunzo na mbili zifuatazo, ambazo zinahusu utunzaji katika leba, katika kuzaa na baada ya kuzaa pamoja na mafunzo tendaji husika kwa moduli hizi kutakuwezesha kupunguza vifo vya kina mama katika jamii yako.

1.1.2 Vifo vya watoto wachanga na matatizo

Kifo cha mtoto mchanga (ambacho pia hujulikana kama kifo cha mtoto mchanga) hufafanuliwa kama kifo cha mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa hai katika muda wa wiki 4 ya kwanza ya maisha. Ulimwenguni, takribani vifo milioni 3 vya watoto hutokea katika wiki 4 ya kwanza ya maisha na pia kuna watoto milioni 3 wanaozaliwa wakiwa mfu. Mtoto aliyezaliwa akiwa amefariki hufafanuliwa kama kuzaa mtoto baada ya wiki 24 ya ujauzito akiwa mfu. Kupoteza fetasi kabla ya wiki 24 kwa kawaida huitwa kuharibika kwa mimba.

Afrika huchangia asilimia 11 ya idadi ya watu duniani, lakini ina zaidi ya asilimia 25 ya vifo vya watoto wachanga duniani. Kati ya nchi 25 za dunia zilizo na hatari ya juu sana ya vifo vya watoto wachanga, 15 (asilimia 75) barani Afrika. Takribani watoto wachanga milioni 1 huzaliwa wakiwa mfu. Kati yao, angalau watoto 300,000 hufariki wakati wa kuzaliwa. Watoto waafrika milioni 1.16 zaidi hufariki katika wiki 4 ya kwanza ya maisha. Kati ya milioni 1.16 hawa, takribani hadi nusu yao hufariki katika siku ya kwanza ya kuzaliwa na wengine milioni 3.3 watafariki kabla ya miaka mitano. Watoto wachanga milioni 4 wanaozaliwa wakiwa na uzani wa chini na wengine walio na matatizo ya utotoni huongoka lakini huenda wasifikie uwezo wao kamili. (Okoa Watoto, USAID, UNFPA, UNICEF, WHO, Nafasi kwa Watoto Wachanga Waafrika; Data tendaji, Hati na utaratibu mwafaka wa kusaidia utunzaji wa watoto wachanga Afrika, mwaka 2006).

Viwango vya vifo vya watoto wachanga

Kiwango cha vifo vya watoto wachanga ni idadi ya vifo vya watoto katika wiki 4 ya kwanza (siku 28) ya maisha kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa wakiwa hai. Kiwango hiki kwa kawaida hujulikana kama vifo vya watoto wachanga kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai. Viwango vya vifo vya watoto wachanga pia vimeweza kukokotolewa na Ukaguzi wa Demografia na Afya wa Afrika. Katika mwaka wa 2005, kiwango hiki kilikuwa 39 kwa kila watoto 1000 wanaozaliwa wakiwa hai. Afrika ni mojawapo ya nchi tano zinazochangia nusu ya vifo vya watoto wachanga barani Afrika. Visababishi vya kimsingi vya vifo hivi ni maambikizi, asifiksia na watoto kuzaliwa kabla ya muda wao. Baadaye katika somo hili, tutakuonyesha jinsi ya kukokotoa kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika eneo lako.

1.1.3 Je, vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga vinawezaje kupunguzwa?

Kupunguza vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga vimetambuliwa kimataifa kama mojawapo ya malengo ya milenia ya maendeleo yaliowekwa mwaka wa 2000 na shirika la afya duniani. Inakadiriwa kuwa tunaweza kuzuia karibu asilimia 75 ya vifo vya watoto wachanga, zaidi ya asilimia 50 ya vifo katika mwaka wa kwanza wa maisha, na asilimia 99 ya vifo vya kina mama katika ujauzito kwa kuboresha afya na lishe ya mama mjamzito kupitia utunzaji katika huduma ya baada ya kuzaa moja kwa moja. Maendeleo haya yanaweza kutimizwa kupitia utatuzi unaofaa wa kijamii, ambao ni mawasiliano yanayofaa na elimu ya afya juu ya utunzaji kabla ya kuzaa (imeangaziwa katika kipindi cha 2). Kutambua na kudhibiti kwa mapema wa matatizo ya kiafya wakati wa ujauzito (kumeangaziwa katika vipindi vya baadaye katika moduli hii), na kuhusu huduma wakati wa uchungu wa kuzaa, wakati wa kuzaa, kipindi cha baada ya kuzaa, na kudhibiti maradhi ya watoto wachanga na yale ya utotoni (katika moduli tatu zifuatazo).

1.2 Kupangia mama mjamzito na mtoto mchanga utunzaji wa kiafya katika jamii yako

Wanawake wajawazito wanaweza kukabiliwa na matatizo mengi tofauti ya kiafya katika ujauzito. Baadhi ya haya ni kutokwa na damu, shinikizo la juu la damu mwilini, mitukutiko, kiwango cha juu cha joto, kiwaa, maumivu ya fumbatio, ugumu wa kupumua, maumivu makali ya kichwa, anemia, kisukari na maambukizi mengine. Utajifunza juu ya utambuzi na jinsi ya kudhibiti matatizo haya yote ya kiafya katika masomo ya baadaye ya moduli hii.

Ili kuhakikisha ufahamu kamili wa matatizo ambayo wanawake wajawazito wanaweza kukabiliwa nayo katika kipindi cha ujauzito na utatuzi unaoweza kutumika, mpango maalumu wa utunzaji unaofaa kabla ya kuzaa ni muhimu. Msingi wa maudhui ya mpango huo na utaratibu wa mtazamo unapaswa kuwa uwasilishaji wa jumbe wazi za kielimu (jinsi utakavyoona katika kipindi cha 2).

Kwa kupanga huduma bora ya afya kwa kina mama wajawazito na watoto wachanga, unahitaji kufanya makadirio ya jamii yako na kutambua mahitaji ya kiafya ya watu.

  • Unawezaje kufanya haya?

  • Unaweza kufanya makadirio haya kwa kuuliza maswali au kupitia majadiliano na waakilishi wa jamii na wazee wanaojua mwelekeo unaodumu wa tabia, mila, mitazamo na maadili katika jamii, ambayo hupokezwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.

    Mwisho wa jibu

Kisha unahitaji kutambua matatizo kwa mujibu wa hali ya kiafya ya kina mama wajawazito na watoto wachanga na kutathmini matumizi ya huduma. Katika kuendeleza huduma za afya kwa kina mama wajawazito na watoto, unapaswa kutambua wazi mitazamo na hali zozote zilizo na athari kwa matokeo. Kwa mfano, katika vijiji vidogo, mwanamke anapokuwa na tatizo wakati wa kuzaa ni vigumu sana kwenda katika kituo cha afya au hospitali. Ni wanakijiji wachache sana walio na magari, na hata mijini, madereva wengi wa teksi hukataa kumpeleka hospitalini mwanamke aliye katika uchungu wa kuzaa. Kwa hivyo ni muhimu sana kuwa na mpango wa huduma ya dharura, na kuwa na mipango ya kuwasafirisha wanawake wanaohitaji huduma za haraka za kutibu matatizo yanayohusiana na ujauzito au kuzaa. Utajifunza kuhusu mipango ya huduma za dharura katika kipindi cha 13.

Kuchunguza kinachowatatiza watu katika jamii yako ni hatua muhimu ya kwanza katika kutambua na kutafiti matatizo katika eneo lako. Hatua ifuatayo ni kuyapanga katika utaratibu wa kipaumbele.

1.2.1 Kupanga matatizo ya kushughulikia kwa msingi wa kipaumbele

Unapaswa kuyapanga matatizo yaliyoainishwa kwa msingi wa vigezo vifuatavyo:

  • Ukubwa wa tatizo (Je,tatizo hili ni kubwa kiasi gani?)
  • Uzito wa tatizo (Je, tatizo hili lina uzito upi kulingana na matokeo mabaya?)
  • Uwezekano wa kutatua (Je, ni njia ipi iliyo rahisi au ngumu kwa kukabiliana na tatizo hili?)
  • Tatizo kwa jamii (Je, tatizo hili lina umuhimu upi kwa jamii?)
  • Tatizo kwa serikali (Je, lina umuhimu upi kwa serikali?).

Kwa mfano, ikiwa kuna upungufu wa huduma kwa kina mama wajawazito na uchache wa vyoo katika eneo lako, unaweza kupanga kwa msingi wa kipaumbele matatizo haya mawili, kama inavyoonyeshwa katika Jedwali 1.1. Mfumo wa kutuza alama ni 1- 5, ambapo 1 ni ya chini zaidi na 5 ni ya juu zaidi. Unaamua juu ya tuzo katika kila sanduku katika jedwali kwa kuzingatia ufahamu wako wa jamii yako na mahitaji yake.

Jedwali 1.1 Mfano wa uchambuzi wa matatizo mawili yaliyotambuliwa kulingana na kipaumbele
Tatizo lililotambuliwaUkubwaUkubwa wa tatizoUwezekanoKinachotatiza jamiiKinachotatiza serikaliIdadi kamili kwa (kwa 25)
Upungufu wa kiwango cha hudumu za kabla ya kuzaa 5555525
Upungufu wa matumizi ya vyoo5444421

Unavyoona katika Jedwali 1.1, alama ya jumla ni 25 kwa upungufu wa kiwango cha huduma zifaazo katika ujauzito na 21 kwa upungufu wa matumizi ya vyoo. Kwa hivyo, katika mfano huu, ungeweka upungufu wa kiwango cha huduma kwa kina mama katika ujauzito kama tatizo litakalopewa kipaumbele. Baada ya kutambua tatizo litakalopewa kipaumbele katika jamii yako, hatua zifuatazo zimeorodheshwa katika kisanduku 1.1.

Kisanduku 1.1 Hatua katika kushughulikia tatizo.
  • Weka malengo (k.m kuongeza idadi ya wanawake wanaopata huduma ya utunzaji kabla ya kuzaa)
  • Tambua mikakati utakayotumia kufanikisha haya (k.m kwa kuandaa kampeni ya elimu ya kiafya ili kuendeleza faida za huduma ya kabla ya kuzaa - kama ilivyoelezwa katika somo la 2)
  • Tambua rasilimali zinazohitajika kwa utekelezaji wa mpango wako
  • Weka kipindi maalumu cha muda wa kutimiza malengo yako
  • Endelea kufuatilia na kutathmini jinsi unavyoendelea katika kutimiza malengo yako.

1.2.2 Kukokotoa idadi ya wanawake wanaohitaji huduma za kabla ya kuzaa

Hatua ya kwanza katika kutathmini haja ya huduma ya utunzaji katika ujauzito katika jamii yako ni kukokotoa idadi ya wanawake wanaoweza kushika mimba katika mwaka wa kawaida. Wakati mwingine wanawake hawa hujulikana kama wanaostahili utunzaji wa kabla ya kuzaa.

Wasifu wa jamii hueleza ukubwa na sifa bainifu za jamii na vipengele vikuu vya afya vinavyowaathiri watu. Takwimu za watu pamoja na ukweli na tarakimu juu ya afya ya kina mama wajawazito na ujauzito katika jamii na habari kuhusu jinsi shughuli za kijamii zinavyotekelezwa ni habari muhimu kwa kupanga na kuendeleza utunzaji kabla ya kuzaa. Lakini kumbuka kwamba kila jamii ni tofauti. Kwa hivyo, mifano tunayotoa katika sehemu hii inaweza kutofautiana na utakayopata katika jamii yako.

Kulingana na takwimu za watu barani Afrika, idadi ya wanawake wajawazito hukokotolewa kama asilimia 4 ya watu kwa jumla. Asilimia hii itabadilika kwa kiasi fulani kati ya jamii kulingana na idadi ya wanawake walio katika umri wa kuzaa miongoni mwa watu. Idadi ya wanawake wanaostahili utunzaji kabla ya kuzaa katika mwaka mmoja barani Afrika inaweza kukadiriwa kwa usahihi wa kutosha kwa kutumia tarakimu ya asilimia 4.

Zoezi 1.1 Kukokotoa idadi ya wanaostahili kupata huduma za utunzaji katika ujauzito katika jamii.

Dhania kuwa idadi kamili ya watu katika jamii moja ni 5,000. Kokotoa idadi ya wanawake wajawazito walio na uwezekano wa kustahili utunzaji katika ujauzito katika jamii hii kwa mwaka mmoja.

Answer

Idadi kamili ya wanawake wajawazito hukokotolewa kama asilimia 4 ya watu 5,000. Ili kukokotoa asilimia 4 ya 5,000, unazidisha 5000 mara 4 kisha ugawanye jawabu na 100. Njia nzuri ya kuandika haya ni kama ifuatavyo:

Kwa hivyo, jamii hii inatarajiwa kuwa na wanawake wajawazito 200 kwa mwaka mmoja wanaostahili utunzaji katika ujauzito, kuzaa na huduma baada ya kuzaa. Ikiwa unajua idadi ya watu katika jamii yako, tumia tarakimu ya asilimia 4 kukokotoa idadi ya wanawake wajawazito watakaohitaji huduma zako katika mwaka mmoja. Andika hesabu yako katika shajara yako ya masomo na umwonyeshe mkufunzi wako katika Kipindi kitakachofuata cha masomo cha kusaidiana.

Mwisho wa jibu

1.2.3 Kukokotoa idadi ya vipimo vilivyonuiwa vya utunzaji katika ujauzito

Wanawake walio na utunzaji katika ujauzito wanaweza kuzaa salama na kuwapata watoto wenye afya njema. Mbinu ifaayo zaidi kwa kutoa huduma kwa wajawazito imebuniwa katika miaka ya karibuni. Mbinu hii mpya huitwa utunzaji ulionuiwa wa kabla ya kuzaa. Ni ratiba ya awamu nne iliyopendekezwa kwa mwanamke mjamzito asiye na matatizo makubwa ya kiafya. Ratiba ya awamu hizi nne zilizonuiwa ni kama ifuatavyo:

Ziara Muda
Awamu ya kwanzaZaidi ya wiki 16 ya ujauzito
Awamu ya piliKati ya wiki 24 na 28
Awamu ya tatu Kati ya wiki 30 na 32
Awamu ya nneKati ya wiki 36 na 40

Utajifunza cha kufanya kwa undani katika kila kipimo kilichonuiwa kwa utunzaji katika ujauzito katika kipindi cha 13.

  • Tazama jibu la zoezi 1.1. Ni awamu ngapi za utunzaji katika ujauzito utakazokuwa nazo katika jamii hiyo kwa mwaka mmoja ikiwa ulitimiza utunzaji ulionuiwa kwa kila mwanamke mjamzito?

  • Ungekuwa na awamu 800 za utunzaji katika ujauzito (awamu 4 kwa kila mmoja wa wanawake wajawazito 200)

    Mwisho wa jibu

Jawabu hili hueleza jinsi utakavyohitaji kupanga huduma zako za ujauzitoni kwa umaakini, ikiwa utamtembelea kila mwanamke mjamzito mara nne! Kama huwezi kutimiza idadi hii, unapaswa kutembelea kila mwanamke mjamzito angalau mara moja, na unakili awamu kama ilivyoelezwa katika sehemu inayofuata.

1.2.4 Kukokotoa kiwango cha utumiaji wa huduma zifaazo katika ujauzito

Kiwango cha waliopata huduma zifaazo katika ujauzito ni sehemu ya idadi ya wanawake wajawazito waliohudumiwa angalau mara moja katika ujauzito wa wakati huo na mtaalamu wa afya kama vile mhudumu wa afya wa nje ya hospitali, kwa mujibu wa sababu zinazohusiana na ujauzito huo. Kukokotoa awamu za kwanza za huduma zifaazo kwa kina mama wajawazito hutoa habari juu ya asilimia ya wanawake wanaozitumia huduma zifaazo katika ujauzito.

Kiwango cha waliopata huduma zifaazo katika ujauzito hukokotolewa kama idadi kamili ya wanawake wajawazito waliohudumiwa angalau mara moja na mtaalamu wa afya kwa mujibu wa sababu zinazohusiana na ujauzito huo zikigawanywa na idadi kamili ya ujauzito unaotarajiwa kwa kipindi fulani cha muda (Kwa kawaida mwaka mmoja) katika eneo hilo. Jibu huwasilishwa kama asilimia kwa kuzidisha na 100.

Kwa mfano, ikiwa idadi kamili ya awamu za kwanza za kabla ya kuzaa ni 100, na idadi kamili ya ujauzito ni 200, basi kiwango cha waliopata huduma zifaazo katika ujauzito katika jamii yako itakuwa asilimia 50, kokotoa jinsi ilivyoandikwa hapa chini:

  • Je, ni kwa nini unafikiri ukokotozi wa kiwango cha huduma zifaazo katika ujauzito katika jamii yako ni muhimu?

  • Inakuwezesha wewe pamoja na msimamizi wako kuona ikiwa juhudi zenu za kuendeleza matumizi ya huduma zifaazo katika ujauzito zina mafanikio. Kwa mfano, kama kiwango cha huduma hizi ni asilimia 50 ya wanawake wajawazito kabla kuanza kampeni ya kuendeleza afya ili kuongeza matumizi ya huduma hizi, mnaweza kudai kuwa kampeni yenu ilikuwa na mafanikio ikiwa matumizi ya huduma hizi yaliongezeka kufikia asilimia 60 au zaidi.

    Mwisho wa jibu

1.2.5 Kukokotoa sehemu ya wanawake waliozaa kwa kuhudumiwa na` wataalamu wa afya

Vilevile, kufanikiwa katika kupanga huduma za kuzaa kunaweza kutathminiwa kwa kukokotoa asilimia ya wanawake wanaojifungua kwa kuhudumiwa na mtaalamu wa afya na kugawanywa na idadi kamili ya wanaotarajiwa kuzaa katika kipindi cha muda fulani (kwa kawaida mwaka mmoja) katika eneo hilo (mara 100).

Kulingana na ukaguzi wa demografia na Afya uliofanywa barani Afrika mwaka wa 2005, waliozaa kwa kuhudumiwa na mhudumu wa uzazi mwenye ujuzi ni asilimia 6 tu. Mhudumu huyu ni mtu ambaye huwa amepata mafunzo ya ujuzi wa ukunga kufikia kiwango cha ustadi muhimu wa kusimamia wanaozaa kwa kawaida na kuweza kutambua, kudhibiti au kupendekeza rufaa kwa matibabu mbadala kukiwa na matatizo ya ukunga. Ni lazima awe na uwezo wa kutambua mwanzo wa matatizo, kuingilia kati kwa kufanya shughuli fulani muhimu, kuanza matibabu, na kusimamia rufaa kwa matibabu mbadala ya mama na mtoto matatizo yakizidi uwezo wao au yakiwa hayawezekani katika mazingira hayo. Afrika ina kiwango cha chini zaidi duniani cha wanaozaa kwa kuhudumiwa na wenye ujuzi wa uzazi. Kukokotoa asilimia ya wanaojifungua kwa kuhudumiwa na mhudumu wa uzazi mwenye ujuzi ni ifuatavyo:

  • Kokotoa kiwango cha wanaozaa kwa kuhudumiwa na wahudumu wenye ujuzi ikiwa ulihudumia wanawake 150 kati ya 200 waliozaa katika eneo lako.

  • Itakuwa

    150/200 x 100 = 75%

    Mwisho wa jibu

Kutimiza kiwango cha juu cha wanaozaa kwa kuhudumiwa kutakusaidia kupunguza vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga na matatizo katika jamii yako. Katika sehemu mbili zijazo, tunakuonyesha jinsi ya kukokotoa viwango vya vifo hivi.

1.2.6 Kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa

Uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa hufafanuliwa kama idadi ya vifo vya kina mama hawa kakatika mwaka na eneo fulani (hii inaweza kuwa nchi nzima, eneo au jamii kama vile jamii yako), ikigawanywa na idadi ya watoto waliozaliwa wakiwa hai katika mwaka huo na eneo hilo. Jibu huzidishwa mara 100,000 ya watoto wanaozaliwa wakiwa hai ili iweze kulinganishwa na miaka mingine na maeneo mengine.

  • Katika eneo X mwaka wa 2002 kulikuwa na vifo 10 vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vifo vya watoto waliozaliwa wakiwa hai 10,000. Je kiwango cha vifo (katika asilimia) vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika eneo X kwa kila watoto 10,000 waliozaliwa wakiwa hai mwaka huo ni nini?

  • Mwisho wa jibu

  • Je, uwiano huu wa vifo vya kina mama kabla , katika na muda mfupi baada ya kuzaa unalinganaje na uwiano wa vifo hivi katika bara la Afrika mwaka wa 2005?

  • Ni mdogo mno ukilinganishwa na uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa wa Afrika ambao ni 673 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai kwa mwaka huo. Kama asilimia hii ingekuwa imetimizwa katika nchi nzima ya Afrika, Malengo ya Milenia ya maendeleo ya kupunguza vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa kwa robo tatu kufikia mwaka wa 2015 yangekuwa yametimizwa kwa kiwango kikubwa.

    Mwisho wa jibu

1.2.7. Kukokotoa kiwango cha vifo vya watoto wachanga

Kufikia sasa, unapaswa kuwa na uwezo wa kukokotoa kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika eneo lako. Kumbuka kwamba kiwango hiki huonyeshwa kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai.

Kwa kumalizia, somo hili limekuonyesha jinsi ya kupanga idadi ya awamu za huduma zako za ujauzitoni na jinsi utakavyokadiria mafanikio yako kila mwaka kwa kukokotoa ni kwa kiasi kipi umeongeza kiwango cha waliopata huduma hizi na cha waliozaa kwa kuhudumiwa. Pia litakusaidia kujua ni kwa kiwango kipi uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na wa vifo vya watoto wachanga katika eneo lako umepungua. Katika somo la 2, tunakuonyesha baadhi ya njia mwafaka za kudumisha huduma bora za kabla ya kuzaa katika jamii yako kupitia elimu ya kiafya,utetezi na uhamasishaji wa jamii.

Muhtasari wa kipindi 1

Katika kipindi hiki,umejifunza kuwa:

  1. Kila mwaka duniani kote, karibu wanawake nusu milioni hufariki kutokana na matatizo ya ujauzito na kuzaa, angalau million 7 hupatwa na matatizo makubwa ya kiafya kwa muda mrefu, na wengine milioni 50 hupatwa na athari mbaya sana. Vingi vya vifo hivi na matatizo hutokea katika nchi zinazoendelea, hasa Afrika.
  2. Ulimwenguni, karibu watoto wachanga millioni 3 hufariki katika majuma 4 ya kwanza baada ya kuzaliwa na pia kuna million 3 wanaozaliwa wakiwa wamefariki. Afrika huchangia asilimia 11 ya idadi ya watu duniani, lakini ina asilimia 25 ya vifo vyote vya watoto wachanga.
  3. Uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika mwaka wa 2005,ulikuwa 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Kiwango cha vifo vya watoto wachanga katika mwaka huo kilikuwa vifo 39 kwa kila watoto 1,000 waliozaliwa wakiwa hai.
  4. Malengo ya Milenia ya Maendeleo ya Shirika la Afya Duniani yaliyowekwa mwaka wa 2000 yana makusudio yaliyowekwa kwa kupunguza vifo vya watoto kwa thuluthi mbili na vifo vya kina mama wajawazito kwa robo tatu kufikia mwaka wa 2015.
  5. Upungufu mkubwa unaweza kutimizwa kupitia uhamasishaji mwafaka wa jamii, elimu ya kiafya, huduma za kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa zilizopangwa vizuri na uthibiti kamilifu wa maradhi ya watoto wachanga na ya utotoni.
  6. Ukadiriaji wa jamii yako na utambuzi wa mahitaji ya watu ya kiafya unaweza kufanywa kwa kuuliza maswali au majadiliano na wawakilishi wa jamii na wazee.
  7. Unaweza kukadiria idadi ya wanawake ambao wanastahili kupata huduma za kabla ya kuzaa kwa mwaka mmoja katika eneo lako ukiwa na usahihi wa kutosha kwa kukokotoa asilimia 4 ya watu wote kwa jumla katika eneo hilo.
  8. Unaweza kukokotoa kiwango cha wanaopata huduma za kabla ya kuzaa kutoka kwa idadi kamili ya kina mama wajawazito uliohudumia angalau mara moja kwa ajili ya sababu zinazohusiana na ujauzito wao na kugawanya na idadi kamili ya wanawake wajawazito wanaotarajiwa katika eneo lako kwa mwaka mmoja (× 100%).
  9. Unaweza kukadiria kiwango cha kuzaa kwa kupata huduma kwa kukokotoa uwiano wa uliohudumia wakizaa na kugawanya na idadi kamili ya wanaotarajiwa kuzaa katika mwaka mmoja (× 100%).
  10. Njia moja ya kukadiria ufaafu wa huduma zako za kabla na wakati wa kuzaa ni kukokotoa uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai na kiwango cha vifo vya watoto wachanga kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa wakiwa hai katika eneo lako ili kujua kama vinapungua kila mwaka.

Maswali ya kujitathmini kwa kipiondi cha 1

Kwa kuwa umemaliza somo hili, unaweza kukadiria ni kwa kiasi kipi umetimiza matokeo ya mafundisho haya kwa kujibu maswali haya. Andika majibu yako katika kitabu chako cha kumbukumbu za mafundisho na uyajadili na mkufunzi katika mkutano wa kusoma na kusaidiana utakaofuata. Unaweza kulinganisha majibu yako na muhtasari wa utokanao na maswali ya kujitathmini yaliyo mwisho wa moduli hii.

Maswali ya kujitathmini 1.1 (yanatathmini Malengo ya Somo 1.2)

Je , uwiano wa vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika mwaka wa 2005 unaweza kulinganishwa vipi na ule wa dunia nzima? Thibitisha chaguo lako kutoka kwa orodha ifuatayo.

  • A.Ni zaidi ya idadi ya wastani ya Afrika na zaidi ya idadi ya wastani ya dunia nzima.
  • B.Ni chini ya idadi ya wastani ya Afrika na chini ya idadi ya wastani ya dunia nzima.
  • C.Ni zaidi ya idadi ya wastani ya Afrika na chini ya idadi ya wastani ya dunia nzima.
  • D.Ni chini ya idadi ya wastani ya Afrika na zaidi ya idadi ya wastani ya dunia nzima.
Answer

D Ndilo jibu sahihi. Kufikia mwaka wa 2005, vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa barani Afrika vilikuwa 673 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Hii ni chini ya wastani wa 900 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai Afrika nzima. Hata hivyo, hii ingali mojawapo ya zilizo juu sana duniani. Katika mwaka wa 2008, idadi hii ya wastani ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa duniani ulikuwa 400 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai.

Mwisho wa jibu

Maswali ya kujitathmini 1.2 (yanatathmini Malengo ya Somo 1.1, 1.3 na 1.5)

Dhania kuwa idadi kamili ya watu katika eneo fulani ni 10,000 na idadi kamili ya huduma za utunzaji katika ujauzito alizofanya mhudumu wa afya ya nje ya kituo cha afya mwaka uliopita ni 150.

  • a.Kokotoa idadi ya wanawake wajawazito waliostahili kupata huduma za katika ujauzito katika eneo hili mwaka uliopita.
  • b.Je, ni nini kiwango cha huduma hizi kilichotimizwa na wahudumu hawa wa afya mwaka uliopita?
Answer
  • a.Idadi kamili ya wanawake wajawazito katika eneo hili hukokotolewa kama asilimia 4 ya watu 10,000. Kukokotoa asilimia 4 ya 10,000, unazidisha 10,000 na 4 kisha ugawanye jawabu kwa 100. Hii ni kama ifuatavyo:

Kwa hivyo, jamii hii inatarajiwa kuwa na wanawake wajawazito 400 kwa mwaka mmoja wanaostahili kupata huduma za utunzaji katika ujauzito, kuzaa na baada ya kuzaa.

  • b.Unakokotoa kiwango cha huduma kabla ya kuzaa kama idadi kamili ya wanawake wajawazito waliohudumiwa angalau mara moja wakati wa ujauzito wao na mhudumu wa afya kwa sababu zinazohusiana na ujauzito huo ikigawanywa na idadi kamili ya ujauzito unaotarajiwa katika mwaka huo. Jibu huonyeshwa kama asilimia kwa kuzidisha na 100. Unaweza kuikokotoa kama:

Ni asilimia 37.5 tu ya wanawake wajawazito katika eneo hili waliopata huduma za utunzaji katika ujauzito mara moja. Wahudumu hawa wa afya wa nje ya vituo vya afya wanapaswa kuboresha kiwango cha huduma hizi katika kebele zao.

Mwisho wa jibu

Maswali ya kujitathmini 1.3 (yanatathmini Malengo ya Somo 1.4)

Chukulia kwamba idadi ya watu katika jamii fulani ni 8,000. Je, wahudumu wa afya wa nje ya vituo vya afya watakuwa na awamu ngapi za huduma za utunzaji katika ujauzito kwa mwaka mmoja ikiwa walitimiza huduma zilizonuiwa kwa kila mwanamke mjamzito?

Answer

Kwanza kokotoa idadi kamili inayotarajiwa ya wanawake wajawazito kutoka kwa watu 8,000 katika jamii hiyo, kama inavyoonyeshwa hapa chini:

Kwa hivyo, jamii hii inatarajiwa kuwa na wanawake wajawazito 320 katika mwaka mmoja wanaostahili kupata huduma za utunzaji katika ujauzito. Kisha kokotoa idadi ya awamu za huduma watakazofanya wahudumu wa afya wa nje ya hospitali kwa mwaka mmoja ikiwa walitimiza kiwango kilichonuiwa cha awamu 4 kwa kila mwanamke mjamzito.

320 x 4 = idadi kamili ya awamu 1,280 za huduma za kabla ya kuzaa

Mwisho wa jibu

Maswali ya ukujitathmini 1.4 (yanatathmini Malengo ya Somo 1.1 na 1.6)

Chukulia kwamba kulikuwa na vifo 480 vya wanawake kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa, vifo 960 vya watoto wachanga na watoto 60,000 walizaliwa wakiwa hai katika eneo Y mwaka wa 2005.

  • a.Kokotoa uwiano wa vifo vya wanawake kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na wa vifo vya watoto wachanga katika eneo hili mwaka huo.
  • b.Je, eneo Y lilikuwa likiendelea vizuri au vibaya likilinganishwa na wastani wa kitaifa wa vifo vya wanawake kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga katika bara la Afrika mwaka wa 2005? Thibitisha uamuzi wako.
Answer
  • a.Kiwango cha vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa =
  • b.vifo vya wanawake kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa katika eneo Y vilikuwa 800 kwa kila watoto 100,000 waliozaliwa wakiwa hai. Hii ni mbaya sana ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa Afrika ambao ni 673 kwa kila watoto 100,000 wanaozaliwa wakiwa hai mwaka wa 2005. Ilikuwa ikiendelea vyema kuliko wastani wa kitaifa wa vifo vya watoto wachanga mwaka wa 2005 ambapo watoto wachanga 16 walikufa kwa kila watoto 1000 waliozaliwa wakiwa hai ikilinganishwa na 39 kwa kila 1000.

Mwisho wa jibu