1. Kupanga Utunzaji katika Ujauzito

Kipindi cha 1 Kupanga Utunzaji katika Ujauzito

Utangulizi

Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu hali ya vifo vya kina mama kabla, katika na muda mfupi baada ya kuzaa na vya watoto wachanga duniani kote, Afrika kwa jumla ili uweze kuelewa kiwango cha matatizo yanayohitaji kushughulikiwa kupitia huduma bora za afya kwa kina mama na wototo wachanga. Utunzaji katika ujauzito, ambao ni huduma ya kitaalamu ya afya ambayo mwanamke hupata kwa muda wote wa ujauzito ni muhimu kwa kusaidia kuhakikisha kuwa wanawake na watoto wachanga wanaongoka katika ujauzito na kuzaliwa. Tunakuonyesha jinsi ya kupanga huduma za utunzaji katika ujauzito ambao jamii yako inahitaji ili kuimarisha na kulinda afya ya kina mama na watoto wachanga katika ujauzito, kuzaa na kipindi baada ya kuzaa. Utajifunza kinachomaanishwa na sifa za huduma zifaazo katika ujauzito katika jamii yako na jinsi ya kukokotoa idadi ya kina mama wajawazito kila mwaka katika eneo lako. Watahitaji utunzaji kwa muda wote wa ujauzito na usaidizi wako wa kistadi wakati wa uchungu wa kuzaa, kuzaa na katika kipindi baada ya kuzaa. Pia utakuwa ukikusanya na kuripoti data juu ya idadi ya awamu za huduma hizi anazopata kila mwanamke na sehemu ya waliozaa kwa kuhudumiwa na mtaalamu wa afya.

Malengo ya Kipindi cha 1