VVU (Virusi Vya Ukimwi) huharibu kingamwili na kusababisha kifo mtu asipotibiwa ipasavyo na dawa za kupunguza makali ya VVU. Virusi hubebwa kwa damu ya mtu aliyeambukizwa na pia hupatikana katika njia ya uzazi ya wanaume na wanawake walioambukizwa. Vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono bila kinga (ngono bila kondomu) au uhamishaji wa damu ulioambukizwa. Mama anaweza pia kumwambukiza mtoto virusi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na pia unyonyeshaji.
Ni muhimu kuwashauri wajawazito kuhusu uzuiaji wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto na kuchunguza VVU ni shughuli ya kawaida ya utunzaji katika ujauzito. Kipindi hiki kinaeleza unachohitaji kujua kuhusu Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto hivyo unaweza kuijadili kwa njia inayofaa na wajawazito utakapowatembelea. Pia tunakuelimisha jinsi ya kuchunguza VVU katika damu, kule vijijini au katika Kituo chako cha Afya. Utakaposoma Moduli mbili zinazofuata, Utunzaji wa leba na kuzaa na Utunzaji baada ya kuzaa, utajifunza kuhusu sera na utendaji wa Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto katika muda huo. Moduli ya Magonjwa Ambukizi, inashughulikia uchunguzi wa VVU, uzuiaji na matibabu katika jamii nzima. Hapa tunazingatia wanawake wajawazito kabla ya kuzaa.
Ukimaliza kipindi hiki, unapaswa kuwa na uwezo wa:
16.1 Kufafanua na kutumia kwa usahihi maneno yote muhimu yaliyochapishwa kwa herufi nzito. (Swali la Kujitahmini 16.1)
16.2 Kueleza mambo yanayozidisha maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto wakati wa utunzaji katika ujauzito. (Swali la Kujitahmini 16.2)
16.3 Kutoa huduma muhimu na ushauri bora kuhusu VVU kwa wajawazito. (Swali la Kujitahmini 16.3)
16.4 Fahamu jinsi ya kutumia mbinu ya uchunguzi wa VVU ya kutoshirikisha na utaje tofauti kati ya mbinu ya kushirikisha na kutoshirikisha. (Swali la Kujitahmini 16.4).
Kwa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto tunamaanisha hatua zilizoundwa ili kupunguza maambukizi ya VVU kutoka kwa wajawazito walio na VVU hadi kwa watoto. Ingawa uchunguzi wa VVU na ushauri kabla ya ujauzito ni muhimu, unapaswa kukumbuka kwamba utunzaji katika ujauzito inaweza kukupa nafasi ya kuchunguza na kuwashauri wanawake katika jamii kuhusu VVU. Unapaswa kuangalia Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kama swala muhimu ya utunzaji katika ujauzito kabla ya kuzaa, kama ulivyojifunza katika Kipindi cha 13. Ni njia ya kuwasaidia na kuwatunza wajawazito walio na maambukizi ya VVU, pia kwa wapenzi na watoto wao. Hii itachangia kufanikisha lengo la nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Afrika kuondoa VVU ifikapo mwaka 2020’.
Bara la Afrika linalenga kuchunguza wanawake wote wajawazito waliotayari kutoa maelezo. Inamaanisha taarifa yoyote inayotolewa na mtu yeyote anayefanyiwa uchunguzi au kutibiwa, na anayefahamu hatari au umuhimu wa taratibu zinazotolewa. Hata ikiwa vifaa na mafunzo ya kufikia lengo la 100% ya kuchunguza wanawake wote katika Kituo cha Afya cha ngazi ya juu hazijapatikana, unapaswa kufahamu kuhusu uchunguzi wa VVU na utawapatia matibabu ya aina gani wanawake walioambukizwa VVU. Kwa hivyo, wakikubali kuchunguzwa unaweza kuwaelezea kitakachofanyika. Tunapaswa kusisitiza umuhimu wa kutoa taarifa yote.
Ingawa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto inaweza kutokea wakati wa ujauzito, hatari kubwa ya maambukizi ni wakati wa leba na kuzaa. Hatari ya maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto (MKMM) wakati wa kunyonyesha, hutegemea namna na muda wa kunyonyesha.
Kabla ya kushughulikia, inakadiriwa kuwa kati ya watoto wachanga 40 kutoka 100 (40%) waliozaliwa na kina mama walio na VVU wataambukizwa. Jedwali 16.1 linaonyesha hatari ya maambukizi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na wakati wa kunyonyesha. Asilimia sitini ya watoto wa kina mama walio na VVU hawatapata virusi hivi kamwe. Hata hivyo, sio rahisi kutabiri ni mama yupi atakayesambaza virusi kwa mtoto, hivyo ni lazima utoe huduma ya uzuiaji wa maambukizi kutoka kwa mama hadi kwa mtoto kwa wajawazito wote walio na VVU
Muda wa maambukizi | Hatari ya maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto (MKMM) bila suluhisho lolote |
---|---|
Wakati wa ujauzito (katika uterasi) | 5–10% |
Wakati wa leba na kuzaa | 10–15% |
Wakati wa kunyonyesha baada ya kuzaa | 5–10% |
Hatari ya kijumla bila kunyonyesha | 15–25% |
Hatari ya kijumla na kunyonyesha hadi miezi 6 | 20–35% |
Hatari ya kijumla na kunyonyesha hadi miezi 18-24 | 30–45% |
Jumla ya hatari ya MKMM | 20–40% |
Kwa kuangalia data katika Jedwali 16.1, Kipindi cha unyonyeshaji huathiri vipi hatari ya MKMM?
Mtoto huwa katika hatari ya kuambukizwa VVU, akinyonyeshwa kwa muda mrefu. Ikiwa mtoto atanyonyeshwa hadi miezi 6 hatari ya kupata maambukizi ni 20-35%. Hatari huongezeka hadi 30-45% ikiwa mtoto atanyonyeshwa hadi umri wa miezi 18-24. Hii ni kupanda kwa 10% kwa hatari ya MKMM
Mwisho wa jibu
Ikiwa maambukizi ya VVU inaweza kutambuliwa na kutibiwa kwa njia inayofaa katika kipindi cha utunzaji katika ujauzito, basi itapunguza uwezekano wa MKMM wakati wa leba na kuzaa au unyonyeshaji. Baada ya hapo, tutaangalia mambo ambayo huongeza hatari ya MKMM wakati wa ujauzito.
Virusi hupatikana kwa wingi katika njia ya uzazi (seviksi na ukeni) na kwa damu ya mama, kwa wajawazito walio na VVU. Kwa hivyo, ikiwa mtoto atakuwa wazi kwa viowevu vya ukeni au damu ya mama wakati wa leba na wa kuzaa, kuna chanzo kikubwa cha kutokea kwa MKMM.
Kawaida, hakuna mchanganyiko wa moja kwa moja kati ya damu ya mama na ya fetasi kwa uterasi, kulingana na Kipindi cha 5. Hata hivyo, chochote kitakachovunja kizuizi kati ya plasenta na ukuta wa uterasi kitazidisha hatari ya MKMM. Kisanduku 16.1 kinaorodhesha baadhi ya mambo ambayo wakati wa ujauzito yanaweza kudhuru kizuizi cha usambazaji wa damu kati ya mama na fetasi katika plasenta, na kuzidisha hatari ya MKMM. Utajifunza mengi kuhusu mambo ya hatari yanayoongeza chanzo cha Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto wakati wa leba na kuzaa, na wakati wa kunyonyesha, katika Moduli mbili zifuatazo za Utunzaji wa Leba na Kuzaa na Utunzaji baada ya kuzaa.
Mambo ya kawaida ambayo huharibu kizuizi kati ya fetasi na mishipa ya mama katika plasenta na kuweka wazi fetasi kwa damu ya mama ni pamoja na:
Swali unaloweza kuuliza ni je, mimba huathiri maendeleo ya ugonjwa wa VVU, au maendeleo ya ugonjwa wa VVU huathiri ujauzito. Hadi sasa, kuna ithibati kwamba mimba haizidishi VVU. Vile vile, hakuna ithibati kwamba maambukizi ya VVU husababisha matokeo mabaya ya mimba.
Unapaswa kuwashawishi wajawazito wote wajitolee kuchunguzwa kwa VVU. Unaweza kutekeleza uchunguzi wewe mwenyewe (tazama Sehemu 16.5.1 hapa chini), lakini kama huwezi kutekeleza uchunguzi, uchunguzi huo hupatikana katika vituo vyote vya afya na hospitali. Mweleze mjamzito kwamba ikiwa atapatikana na VVU, anaweza kupata huduma bora ya kuzuia mtoto wake kutokana na VVU kabla au baada ya kuzaa. Pia mwambie kwamba kuna matibabu yake na mpenzi wake (ikiwa mpenzi wake atapatikana na VVU). Maswala muhimu ya UMKMM zilizozingatiwa zimetajwa katika Jedwali 16.2.
Profilaksisi (inatamkwa kama ‘proff-ill-aksisi’) inamaanisha ‘tiba linalolenga kuzuia’. Dawa za kupunguza makali ya VVU hutumiwa ili kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama aliye na VVU hadi kwa mtoto.
Dawa za kupunguza makali ya virusi ya kukinga maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto zinahusisha kumpatia mama dawa za kurefusha maisha kwanzia wiki 28 za ujauzito, pia kwa mama wakati wa leba na kuzaa, na kwa mtoto wake mara tu baada ya kuzaliwa. Dawa hizi hupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa mtoto. Ni tofauti na tiba ya kupunguza makali ya virusi anayopewa mama ili kutibu maambukizi ya VVU, kulingana na uhakiki wa vigezo vyake.
Ikiwa mama aliye na VVU anapendelea na asisitize kuzaa nyumbani, dawa za kupunguza makali ya virusi za kisasa ambazo zinaweza kupatikana zinaitwa Nevirapine. Wakati utajua kwamba mama aliye na VVU yuko karibu kuzaa nyumbani, ikiwa umepewa mamlaka na umehitimu kufanya hivyo, unapaswa kumpa dozi moja ya Nevirapine (miligramu 200) ameze leba inapoanza. Ni bora ikiwa utatekeleza utambuzi wa leba na umpatie dawa wewe mwenyewe. Pia, mtoto anapaswa kupokea dozi moja ya Nevirapine baada ya siku 3 za kuzaliwa. Unapaswa kuwapa dawa hii moja kwa moja kulingana na uzito wa mtoto. Utajifunza kufanya hivi katika Moduli ya Magonjwa Ambukizi katika mtaala huu.
Kwa wale wanaozaa katika kituo cha afya au hospitalini, aina tatu ya dawa za kurefusha maisha zinapaswa kumezwa na kina mama walio katika leba kama profilaksisi (AZT + Neverapine + Lamuvudine). Mke na mumeo wanapaswa kujua kwamba aina hizo tatu za dawa zimezwapo wakati wa leba humkinga mtoto.
Aidha, mtoto atapewa dawa mbili (AZT + Lamuvudine) kwa wiki 1-4. Hivyo basi, unapaswa kuwashawishi kina mama walio na VVU kuzalisha katika vituo vya afya au hospitalini.
Dawa hizi za kupunguza makali ya virusi hupunguza hatari ya Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto, lakini hazitibu maambukizi ya VVU kwa mama wala haziboreshi afya yake. Wakati mwingine, mjamzito anaweza kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU ili kutibu VVU kabla ya kuzaa (iwapo anastahiki). Kwa hivyo, unapaswa kuwahimiza wajawazito wote walioambukizwa VVU kwenda kwenye kituo cha afya kilicho karibu kuangalia kama wanaweza kuanza kunywa dawa za kupunguza makali ya VVU ambazo zitalinda watoto wao.
Ni bora kufanya uchunguzi wa VVU kwa wajawazito wote. Huu ni uchunguzi wa hiari, baada ya kuelimishwa kabla ya uchunguzi, mjamzito ana haki ya kukataa kuchunguzwa (kama ilivyoelezwa hapo mbeleni, katika Sehemu ya 16.5.2). Barani Afrika fomu iliyotiwa sahihi haihitajiki ili uchunguzi wa VVU ufanywe – lakini maelezo ya wazi ni muhimu.
Shirika la Afya Duniani na huduma za afya katika nchi nyingi Afrika, linahamasisha swala la kutoa ushauri na uchunguzi wa VVU. Hii inamaanisha kwamba utakapofunzwa kufanya hivyo, unapaswa kutoa uchunguzi na ushauri wa VVU mara kwa mara kama sehemu ya huduma ya wajawazito na afya ya watoto. Hupaswi kusubiri hadi mama aitishe (ushauri na uchunguzi wa VVU). Iwapo hujapata mafunzo katika swali hili, unapaswa kutoa elimu kabla ya uchunguzi na umpatie mama rufaa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu, au umjulishe siku ya uchunguzi wa kijumla.
Maambukizi ya VVU yanaweza kutambuliwa katika damu kwa aina tatu za uchunguzi. Hii ni pamoja na Uchunguzi wa VVU wa Haraka, ambayo ni uchunguzi unaoweza kutekelezwa tu nyumbani au katika Kituo cha Afya. Uchunguzi mwingine wa pili (the Western blot test and enzyme immunoassay test), zinaweza kufanyika katika kituo cha afya cha ngazi ya juu. Kulingana na urahisi wa kutumia, Uchunguzi wa VVU wa haraka hutumika kwa kawaida barani Afrika. Inahusu kuchukua kiasi kidogo cha sampuli ya damu kutoka kwenye kidole kwa kutumia chombo safi, na uchukue tone la damu ili uiweke kwenye kifaa cha kuchunguzia (Jedwali 16.1). Utajifunza jinsi ya kutekeleza uchunguzi na kusoma matokeo katika Moduli ya Magonjwa ya Ambukizi.
Kanuni mbalimbali ya vifaa vya kufanyia uchugnuzi wa VVU ambazo zimeendelezwa za kuchunguza damu ni sawa. Uchunguzi huu ni wa kina katika utambuzi wa maambukizi ya VVU. Zinafanya kazi kwa kugundua kingamwili (protini zinazotengenezwa na mwili ili kupambana na maambukizi) ambazo hutokea kwa damu baada ya kipindi cha utambulizi wa maambukizi ya VVU. Kipindi tambulizi ni kipindi cha muda (hadi wiki 12 au miezi 3) kati ya virusi kuingia mwilini mwa mtu na kuonekana kwa ugunduzi wa kingamwili katika damu ya mtu. Katika baadhi ya hali, mtu asiyekuwa na maambukizi ya VVU anaweza kuwa na virusi, lakini visionekane kwa sababu bado yuko katika kipindi virusi visivyotambulika. Kumchunguza mtu huyu tena baada ya miezi 3 kutoka siku ya maambukizi ya VVU matokeo yataonyesha kuwepo kwa maambukizi.
Sampuli kiasi cha damu ya mtu inapitishwa kwa Uchunguzi wa VVU wa Haraka kwa kutumia vifaa viwili kutoka kwa watengenezaji tofauti. Je, unaweza kueleza ni kwa nini damu hiyo imechunguzwa mara mbili kwa kutumia vifaa viwili tofauti?
Matokeo yataaminika zaidi ikiwa mikakati yote miwili itabainisha. Ikiwa matokeo yote mawili ni tofauti, inaonyesha kwamba uchunguzi unaweza kuwa haujafanywa vizuri na wa tatu unapaswa kufanywa kama ‘kihakikishi’
Mwisho wa jibu
Kuna mbinu mbili tofauti za kushauri wajawazito kuhusu umuhimu wa kuchunguzwa kwa VVU: zinajulikana kama ‘kushiriki’ na ‘kutoshiriki.’ Mbinu ya kushiriki inahusisha kushauri mwanamke kwa muda wa dakika 40 katika chumba cha kibinafsi, umjulishe kila kitu anapaswa kujua, ili akubali kuchunguzwa kwa hiari (yaani, kushiriki, au kuaminiwa na mwanamke). Hata hivyo, mwishoni mwa kipindi cha ushauri, anaweza kukataa kuchunguzwa. Mbinu ya kushiriki ulifanywa hadi mwaka wa 2006 Afrika na bado ndio inayotumiwa.
Mbinu ya kutoshiriki, kwa upande mwingine, inahusisha kumfahamisha mwanamke kwamba yuko karibu kufanyiwa uchunguzi wa VVU. Lengo kuu la mbinu ya kutoshiriki ni kuhakikisha kuwa wanawake wengi (na wanaume) wamefanyiwa uchunguzi wa maambukizi ya VVU. Tofauti kati ya kushiriki na kutoshiriki imeelezewa kwa muhtasari katika Jedwali 16.2. Hasa unavyoweza kuiona, mbinu za kutoshiriki imefaulu zaidi katika kufikia uchunguzi wa juu kuliko ilivyo kuwa kwa kushirki.
Hali | Kushiriki | Kutoshiriki |
---|---|---|
Mwongozo wa Kitaifa ya Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto | 2001 | 2007 |
Kushauri | Kushauri kabla na baada ya uchunguzi (kabla na baada; kabla ya uchunguzi inaweza kuchukua muda mrefu hadi mteja akubali uchunguzi) | Baada ya uchunguzi (baada ya matokeo ya uchunguzi isipokuwa mteja akatae kuchunguzwa au kutoshiriki) |
Kiwango cha ukweli wa uchunguzi (idadi ya watu waliochunguzwa) | Chini sana | Juu sana |
Husaidia watu kuona uchunguzi wa VVU kama ya kawaida | La | Ndio |
Manufaa mengine ya mbinu ya kutoshiriki kwa uchunguzi wa VVU ni utaratibu wa kawaida kwa kila mtu. Kutekeleza uchunguzi wa VVU kwa kawaida husaidia kuondoa uoga wa kufanyiwa uchunguzi, kwa hivyo siku za mbeleni itakuwa kama uchunguzi wa ugonjwa mwingine wa kawaida. Taarifa kuhusu uchunguzi wa VVU unaweza kutolewa katika vikao vya vikundi, ambavyo pia husaidia; kwa mfano, unaweza kupanga mkutano wa kikundi cha wajawazito katika jamii kuyajadili masuala ya huduma inayolenga wajawazito, na utaje uchunguzi wa VVU kama sehemu ya huduma ya kawaida kwa wajawazito. Mwisho, haichukui muda mwingi wa mhudumu wa afya, kwa sababu haichukui muda mrefu kushauri kila mwanamke.
Kuna baadhi ya mambo muhimu juu ya mbinu ya kutoshirki ambazo unahitaji kuelewa. Kwanza, mama anaweza kukataa kufanyiwa uchunguzi - yeye anaweza-kukataa. Pili, iwapo atapatikana na VVU, atapewa ushauri baada ya kuchunguzwa, mama atapewa ushauri baada ya uchunguzi. Tatu, kina mama wasioshiriki (waliokataa) watatengewa kipindi kirefu zaidi cha ushauri, ambacho huanza kwa kuwapa nafasi ya kueleza wasiwasi wao na sababu za kukataa kufanyiwa uchunguzi, kwa hivyo unaweza kushughulikia maswali yao maalum na wasiwasi.
Ili ufanikiwe kushauri kina mama waliokataa kuchunguzwa, washawishi ili wakuamini. Sisitiza kuwa utambuzi wa mapema na matibabu au tiba ya kuzuia maradhi linaboresha sana nafasi ya kuishi kwa kina mama wanalio na VVU na watoto wao. Mama akijua hali yake ya VVU haimaanishi mume wake au mwenzake ana haki ya kujua pia - ni hiari yake kuarifu hali yake ya VVU au iwe siri. Hata hivyo, akifichua hali yake, atakuwa na manufaa makubwa maana familia yake inaweza kumsaidia. Mhakikishie mama kuwa VVU si ugonjwa unaohitaji kuwa siri tena au ya aibu. Pia, si ugonjwa unaosababisha kifo, ikiwa itatambuliwa mapema na kutibiwa.
Iwapo mama ataendelea kukataa kuchunguzwa kwa VVU, ushauri zaidi unapaswa kutolewa atakapozuru kituo cha afya kwa huduma ya utunzaji katika ujauzito. Anapaswa kuhakikishiwa kuwa kukataa kwake kuchunguzwa haiathiri huduma yake ya utunzaji katika ujauzito, leba na kuzaa, baada ya kuzaa, au huduma zinazohusiana. Mshawishi achunguzwe. Usimlazimishe, lakini mjulishe kwamba ikiwa atabadili wazo lake, uchunguzi wa VVU na ushauri unaweza kutolewa katika ziara ya baadaye. Andika sababu zake za kukataa iwe kumbusho la kutoa ushauri na uchunguzi wakati ujao. Kisanduku 16.3 kinatoa muhtasari wa baadhi ya sababu za kawaida za kina mama kukataa kuchunguzwa kwa VVU.
Algorithm ni seti ya miongozo inayo kuwezesha kufuata hatua kwa mipangilio ya vitendo, ikiwa na maelezo katika kila hatua kulingana na matokeo. Kielelezo 16.2 inaonyesha miongozo iliyopitishwa kwa Uchunguzi wa Haraka wa VVU Afrika.
Kama unavyoona kutoka Kielelezo 16.2, ikiwa uchunguzi wa kwanza unaonyesha kuwepo kwa VVU, ili kuhakikisha mteja anayo VVU, kuna haja ya kufanya uchunguzi wa pili ili kuthibitisha matokeo ya uchunguzi wa kwanza.
Je, mwongozo katika Kielelezo 16.2 unaonyesha ni nini kinapaswa kufanyiwa ikiwa uchunguzi wa pili hauonyeshi kuwepo kwa VVU (ni kinyume na matokeo ya uchunguzi wa kwanza)?
Mwongozo unahitaji uchunguzi wa tatu ufanywe ili kuamua - uchunguzi huu utathibitisha matokeo ya kuwepo kwa VVU katika uchunguzi wa kwanza, au kutokuwepo katika uchunguzi wa pili.
Mwisho wa jibu
Kufuatia hatua katika mwongozo inahakikisha kuwepo kwa VVU kumethibitishwa na vipimo viwili tofauti kabla ya matokeo kutolewa kwa mteja.
Ikiwa mama amekubali, na amechunguzwa kwa VVU, unahitaji kujua jinsi ya kujadili matokeo (pamoja na mume wake) wakati wa ushauri baada ya kuchunguzwa. Kwa watu wazima, matokeo ya kuwepo kwa VVU kunamaanisha kwamba kwa hakika mtu ana maambukizi ya VVU. Kama utakavyojufunza katika Moduli za baadaye, matokeo ya kuwepo kwa VVU kwa mtoto mchanga hakumaanishi kwamba mtoto ana maambukizi. Antibodi za mama zinazokinga VVU zinaweza kuingia kwenye damu ya mtoto wakati wa leba na wa kuzaa, na ni vigumu kutambua kutokana na Uchunguzi wa Haraka wa VVU kama inatambua antibodi zake au za mtoto. Matokeo ya kutokuwepo kwa VVU kwa kawaida inamaanisha mama au mtoto hana maambukizi ya VVU.
Mama anaweza kuwa katika hatari kubwa ya maambukizi ya VVU iwapo alifanya ngono bila kinga na mtu ambaye hali yake ya VVU haijulikani, au anayejulikana kuwa na VVU, au iwapo mumewe ana mke mwingine au wenzi wengine, au mume wake anajidunga dawa za kulevya. Ikiwa matokeo ya uchunguzi wa mara ya kwanza kwa mama kama huyu yanaonyesha kutokuwepo kwa VVU, anapaswa kuchunguzwa tena baada ya miezi 3 ili kuthibitisha matokeo ya awali.
Unapozungumza na mama aliyepatikana na VVU, unapaswa kuwa makini sana kwa hisia zake, ambazo ni pamoja na mshtuko, hasira au kutoamini. Akiwa na uwezo wa kukusikiza, hakikisha kuwa:
Magonjwa nyemelezi ni maambukizi yanayosababishwa na bakteria au virusi kwa watu ambao mifumo ya kingamwili yao ni dhaifu, kwa mfano kwa sababu ya VVU. Mtu aliye na afya kwa kawaida huwa na uwezo wa kupambana na maambukizi ya bakteria au virusi hivi.
Hata ingawa mama atakuwa na utulivu kuwa hana VVU, unapaswa kuhakikisha kuwa anaelewa:
Jedwali16.3 hapo chini linatoa muhtasari wa hatua zinazofuatwa katika uchunguzi na ushauri wa VVU katika kipindi cha ujauzito, wakati wanapotembelea kliniki mara ya kwanza na kila mara. Ni matumaini yetu kuwa ni ya manufaa kwako. Kumbuka pia hutapata mafunzo ya utendaji katika funzo la Kuzuia Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto, jambo ambalo pia litahusisha sera na taratibu wakati wa kipindi cha leba na baada ya kuzaa.
Uliza, Chunguza | Matokeo | Matibabu na ushauri |
---|---|---|
|
|
|
|
| |
|
|
Hatimaye, utafiti wa hivi karibuni barani Afrika ulionyesha kwamba wengi wa washiriki wa utafiti huo waliamini kuwa ikiwa kina mama wanaoishi na VVU wanapata mimba, afya zao kwa ujumla uzorota kwa sababu ujauzito uchochea uendelezaji wa VVU. Kama ilivyoelezwa hapo juu, kuwa mjamzito haimaanishi kwamba hali ya afya ya mama itazorota. Hata hivyo, afya ya mama inaweza kuzorota wakati wa ujauzito kwa sababu ya hatua ya VVU. Mama akipata mimba akiwa katika hali kali ya VVU, bila shaka atapata matatizo mengi ya kiafya, ikiwa ni pamoja na magonjwa nyemelezi. Kwa hivyo si kuwa na VVU yenyewe yenye itaongoza wahudumu wa afya kutoa huduma ya ziada - ni hatua ya ugonjwa huo.
Katika Kipindi cha 16, umejifunza kwamba:
Kwa kuwa umekamilisha kipindi hiki, unaweza kutathmini jinsi ulivyofanikisha Malengo ya Somo kwa kujibu maswali haya. Andika majibu yako katika shajara yako ya somo na uyajadili na Mkufunzi wako katika Mkutano ujao wa somo la usaidizi. Unaweza kulinganisha majibu yako na Maelezo juu ya Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.
Mama anafanya ngono na mtu aliye na VVU. Baada ya wiki mbili anafanyiwa uchunguzi wa maambukizi ya VVU. Matokeo yanaonyesha kutokuwepo VVU.
Mwisho wa jibu
Hali nyingi huongeza hatari ya MKMM katika kipindi cha ujauzito. Nini hufanana kwa hali hizi mbili? Toa mifano miwili.
Hali mbili ni ufutaji wa sigara, na jeraha katika fumbatio, kwa mfano kutoka chombo kilichochongoka. (Kumbuka: Unaweza kuwa umechagua hali zingine kutoka zile zilizoorodheshwa katika Kisanduku 16.1.) Hali hizi hufanana kwa sababu zinaweza kuharibu kizuizi kati ya usambazaji wa damu kwa plasenta na fetasi na hivyo damu ya mama kuchanganyika na ya fetasi. Hii inaongeza hatari ya Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto.
Mwisho wa jibu
Mama mjamzito amekataa kuchunguzwa kwa VVU. Je, unaweza kufanya lolote?
Ikiwa mama mjamzito amekataa kuchunguzwa kwa VVU, unaweza:
Mwisho wa jibu
Je, ni manufaa gani kuu ya kutumia mbinu ya kutoshirikisha badala ya kushirikisha katika uchunguzi wa VVU?
Kwanza, kina mama wajawazito wengi wanaweza kukubali uchunguzi wa VVU ikiwa mbinu ya kutoshirikisha itatumika. Pili, kina mama wengi wakichunguzwa, uchunguzi wa VVU itaonekana kama jambo la kawaida na kukubali kama sehemu ya kawaida ya utunzaji katika ujauzito. Tatu, haichukui muda mwingi wa wahudumu wa afya, kwa sababu haihusishi muda mrefu wa ushauri kabla ya uchunguzi kwa kila mwanamke.
Mwisho wa jibu