16. Mikakati ya Kupunguza Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto kabla ya Kuzaliwa

Kipindi cha 16 Mikakati ya Kupunguza Maambukizi ya VVU kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto kabla ya Kuzaliwa

Utangulizi

VVU (Virusi Vya Ukimwi) huharibu kingamwili na kusababisha kifo mtu asipotibiwa ipasavyo na dawa za kupunguza makali ya VVU. Virusi hubebwa kwa damu ya mtu aliyeambukizwa na pia hupatikana katika njia ya uzazi ya wanaume na wanawake walioambukizwa. Vinaweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa kufanya ngono bila kinga (ngono bila kondomu) au uhamishaji wa damu ulioambukizwa. Mama anaweza pia kumwambukiza mtoto virusi wakati wa ujauzito, leba na kuzaa, na pia unyonyeshaji.

Ni muhimu kuwashauri wajawazito kuhusu uzuiaji wa maambukizi ya VVU kutoka kwa mama hadi kwa mtoto na kuchunguza VVU ni shughuli ya kawaida ya utunzaji katika ujauzito. Kipindi hiki kinaeleza unachohitaji kujua kuhusu Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto hivyo unaweza kuijadili kwa njia inayofaa na wajawazito utakapowatembelea. Pia tunakuelimisha jinsi ya kuchunguza VVU katika damu, kule vijijini au katika Kituo chako cha Afya. Utakaposoma Moduli mbili zinazofuata, Utunzaji wa leba na kuzaa na Utunzaji baada ya kuzaa, utajifunza kuhusu sera na utendaji wa Uzuiaji wa Maambukizi kutoka kwa Mama hadi kwa Mtoto katika muda huo. Moduli ya Magonjwa Ambukizi, inashughulikia uchunguzi wa VVU, uzuiaji na matibabu katika jamii nzima. Hapa tunazingatia wanawake wajawazito kabla ya kuzaa.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 16