Katika kipindi kilichopita, ulijifunza zaidi kuhusu kuvuja damu baada ya kuzaa. Hali hii ni mojawapo ya visababishi vikuu vya vifo vya kina mama vinavyo husiana na kuzaa. Kuvuja damu baada ya kuzaa husababisha 1/4 ya vifo vyote vya kina mama vinavyo husiana na kuzaa. Duniani kote, takriban wanawake 127,000 hufa kila mwaka kutokana na kuvuja damu baada ya kuzaa. Vingi vya visa hivi vya kuvuja damu kwa wingi hutokea katika saa 24 za kwanza baada ya kuzaa. Vifo hivi husababishwa na matatizo katika awamu ya tatu ya leba. Ili kupunguza hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa, wahudumu wote wa kuzalisha wanafaa kufuata mseto wa hatua maalum zilizowekwa. Hatua hizi hujulikana kama udhibiti tendeti la awamu ya tatu ya leba (UTATL). Utaratibu wa UTATL unapofanywa inavyofaa, hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa hupunguzwa kwa zaidi ya 60%.
Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu UTATL na mambo ya kufanya katika hatua zote 6. Maarifa haya yatakusaidia kutambua na kuyadhibiti kikamilifu matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba.
Baada ya kipindi hiki, unatarajiwa:
6.1 Kufasili na kutumia kwa usahihi maneno yote muhimu yaliyo andikwa kwa herufi nzito. (Swali la Kujitathmini 6.1 )
6.2 Kueleza utaratibu halisia wa kifisiolojia wa kutolewa kwa plasenta. (Swali la Kujitathmini 6.1 )
6.3 Kueleza hatua zote 6 za udhibiti tendeti wa awamu ya tatu ya leba (UTATL). (Swali la Kujitathmini 6.2 )
6.4 Kuandika kwa muhtasari taratibu zote za kila dawa ya uterasi inayotumiwa katika UTATL. (Swali la Kujitathmini 6.2 na 6.3)
6.5 Kueleza jinsi ya kuchunguza plasenta na membreni ili kubaini kama zimetoka zingali nzima. (Swali la Kujitathmini 6.3 )
6.6 Kueleza dalili hatari zinazoashiria matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba. (Swali la Kujitathmini 6.4 )
Awamu ya tatu ya leba huanza kwa kuzaliwa kwa mtoto na kuisha kwa kutolewa kwa plasenta na membreni za fetasi. Kwa kawaida, uatratibu huu unafaa kuchukua chini ya dakika 30.
Katika leba ya kawaida, awamu ya tatu ni wakati taratibu asilia za kifisiolojia huusababisha kutolewa kwa ghafla kwa plasenta na membreni za fetasi. Ni sharti seviksi ibakie wazi na uterasi kukazana vyema ili mama asikumbwe na matatizo. Katika kauli nyingi, taratibu hizi hutokea katika mfululizo ufuatao.
Utaratibu huu wa kutolewa kwa plasenta huashiria awamu ya tatu ya leba. Misuli ya uterasi huendelea kukazana kwa kishindo hivyo kuigandamiza mishipa ya damu iliyochibuka. Tuko hili pamoja na kuganda kwa damu husitisha kuvuja kwa damu baada ya kuzaa.
Kipindi cha 11 kinaelezea kwa kina kuhusu kuvuja kwa damu baada ya kuzaa na uterasi isiyo na mikazo. Istilahi zingine zilizo kwenye Kisanduku 6.1 zimeelezwa katika kipindi hiki.
Wanawake wanaozaa bila usaidizi wa mhudumu wa afya aliyehitimu wako katika hatari kuu zaidi ya kukumbwa na matatizo katika awamu zote za leba. Kisanduku 6.1 kinaorodhesha matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu. Matatizo yanaweza kutokea hata wakati plasenta imepandikika vyema katika sehemu ya 2/3 ya uterasi. Matatizo yanaweza kutokea wakati leba haijaendelea kwa muda mrefu na wakati utaratibu wa kuzaa ni wa kawaida. Katika leba ya kawaida, plasenta inatarajiwa kutolewa kwa utaratibu wa kawaida na unaojianzisha wenyewe katika awamu ya tatu ya leba. Hata hivyo, matatizo yanaweza kutokea. Jiweke tayari kwa jambo lolote la dharura lisilotarajiwa.
Matatizo yafuatayo yanaweza kutokea iwapo hutatumia utaratibu wa UTATL kudhibiti awamu ya tatu.
Plasenta inasalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30 baada ya mtoto kuzaliwa. Plasenta husalia kufuatia sababu zifuatazo:
Kuvuja damu baada ya kuzaa ni hali ambapo mama anavuja zaidi ya mililita 500 za damu baada ya kuzaa. Damu nyingi huvujia katika sehemu ambapo plasenta ilikuwa imeshikamana na uterasi. Damu ni ng’avu au nzito na yenye kunata. Damu nyingi huvuja iwapo uterasi haikazani ifaavyo, hasa kufuatia sababu hizi:
Sehemu ya ndani ya uterasi huvutika hadi kuja juu mtoto au plasenta inapotolewa. Sehemu ndogo ya uterasi hutokezea ukeni.
Mkunga anapotumia udhibiti tendeti katika hatua ya tatu ya leba (UTATL), hatari ya matatizo kama yalivyoorodheshwa katika Kisanduku 6.1 hupunguzwa. Neno ’’udhibiti tendeti’’ linaashiria kuwa hautasubiri hadi plasenta ijitoe yenyewe. Badala yake, unafaa kusaidia kwa namna iliyopangwa kwa utaratibu kama ifuatavyo:
Chunguza kama uterasi ina mtoto wa pili punde tu baada ya mtoto kuzaliwa. Papasa uterasi kupitia fumbatio la mama. Hakikisha kuwa uterasi haina mtoto wa pili. Kwa kutumia mikono, chunguza kama uterasi imerejea kimo kama cha umri wa wiki 24 za ujauzito. Baada ya kufanya hivi, nenda katika hatua ya 2. Chunguza kwa makini sana kwa sababu dawa unayompa mama kaatika hatua ya 2 hufanya uterasi ikazane kwa nguvu sana. Iwapo mtoto yuko ndani ya uterasi, anaweza kujeruhiwa. Iwapo kuna mtoto wa pili ndani ya uterasi, mpe mama dawa ya kukazisha uterasi baada ya mtoto huyu kuzaliwa.
Dawa hizi za kukazisha uterasi mara nyingi hutumika katika taaluma ya ukunga:
Dawa hizi huisaidia uterasi kukazana kwa nguvu na utaratibu maalum baada ya mtoto kuzaliwa. Dawa hizi husaidia katika kutolewa kwa plasenta na pia kuzuia damu kuvuja kwa wingi kutokana na uterasi isiyokazana. Dawa hizi tatu zinapatikana hata katika maeneo ya mapato ya chini, kama vile vijijini mwa Afrika. Hata hivyo, misoprostol inaweza kuwa dawa pekee unayoweza kutumia. Oxytocin ndiyo dawa iliyopendekezwa na Shirika la Afya Duniani, lakini haiwezi kutumika kwa sababu:
Vituo vya afya husambaziwa friji na sanduku la barafu ambazo hutumiwa kusafirishia dawa vijijini, kama ilivyoelezwa kwenye Moduli ya Chanjo
Ni sharti oxytocin na ergometrine zihifadhiwe katika kiwangojoto cha nyusi 2 -8. Dawa hizi haziwezi kutolewa katika nyumba zisizokuwa na friji au una sanduku la kubeba la barafu. Ni sharti pia dawa hizi zikingwe kutokana na mwangaza.
Chini ya dakika moja baada ya mtoto kuzaliwa na umefinya kamba kitovu kwa klempu kisha kukata kamba kitovu, mpe mama mojawapo ya dawa zifuatazo:
AU
AU
Uterasi huwa ngumu inapokazana ifaavyo. Mabadiliko haya hutokea dakika 2 -7 baada ya kundunga dawa hii. Dawa hizi hutenda kazi kwa muda tofauti.
Ergometrine haipendekezwi kutumiwa na Wahudumu wa Afya Ugani.
Misoprostol haina nguvu za kutenda kazi kama oxytocin. Misoprostol ina madhara zaidi ya ziada Hata hivyo, katika hali nyingi mle vijijini, ni sharti utumie misoprostol kwa sababu ni lazima oxytocin ihifadhiwe ndani ya friji au sanduku la barafu. Mshauri mama kuwa dawa hii huzuia kuvuja kwa damu, hata ingawa nafaa kutarajia madhara machache ya ziada. Dawa zote za kukazisha uterasi zina madhara ya ziada. Hata hivyo, misoprostol husababisha madhara kwa wanawake wengi zaidi. Yafuatayo ndiyo madhara ya misoprostol:
Je, manufaa makuu zaidi ya misoprostol ni yapi ikilinganishwa na dawa zingine za kukazisha uterasi.
Misoprotol ni tembe, hivyo hauhitaji sirinji na sindano. Misoprotol haihitaji kuhifadhiwa ndani ya friji, hivyo inaweza kutumika katika sehemu ambapo dawa zingine haziwezi kuhifadhika.
Mwisho wa jibu
Oxytocin ndiyo dawa ya kukazisha misuli iliyopendekezwa iwapo kuna friji. Oxytocin hutenda kazi zaidi kuliko dawa zingine, na ina madhara machache zaidi. Oxytocin ni homoni inayopatikana kiasilia katika mwili wa mwanamke. Oxytocin huhusishwa kuanzia mwanzo wa mikazo ya uteras wakati wa leba, na pindi inavyoendelea. Mpe mama oxytocin ya kutengenezewa viwandani akishazaa. Dawa hii huiwezesha uterasi kuendelea kukazana taratibu, kama katika njia ya kiasili. Hata hivyo, hali hii haidumu kwa muda mrefu, hivyo ni sharti oxytocin ihifadhiwe ndani ya friji na kukingwa dhidi ya mwangaza.
Ergometrine haitumiki mara nyingi kwa sababu hii ni dawa ya kukazisha misuli yenye nguvu zaidi. Dawa hii inaweza kusababisha kufungika kwa seviksi kabla ya plasenta kutolewa. Ergometrine huchukua muda mrefu zaidi kufanya kazi kuliko oxytocin. (Baada ya kudungwa ndani ya misuli, ergometrine huchukua dakika 6-7 kufanya kazi.) Ergometrine husababisha mishtuko ya uterasi ambayo hukazana upesi huku mikazo hii ikidumu kwa muda, kinyume na mikazo ya kiasili. Hata hivyo, athari ya ergometrine hudumu kwa muda mrefu, saa 2-4.
Usitumie ergometrine katika Huduma ya Afya Ugani.Usimpe mama mwenye prieklampsia, eklampsia au shinikizo la damu. Ergometrine hufinya mishipa ya damu huku ikisababisha ongezeko la shinikizo la damu.
Uterasi huwa ngumu inapokazana ifaavyo. Badiliko hili hufanyika dakika 2-3 baada ya kudunga dawa uterasini. Baada ya hatua hii, tumia njia ya kuvuta kitovu taratibu kwa msukumo pinzani ili kuitoa plasenta (Mchoro 6.2 na Kisanduku 6.3).
Unapotumia njia ya kuvuta kitovu taratibu, kumbuka KILA MARA kusuma fumbatio kwenda upande pinzani. Jambo hili hufanywa ili kuzuia kugeuka kwa uterasi. (Uterasi inapogeuka hupinduka hata sehemu yake ya ndani kuja juu kisha kutokezea ukeni.)
Plasenta inapotoka, ishike kwa mikono yote kwenye vulva. Hii ni ili kuzuia membreni kuraruka, jambo ambalo linaweza kupelekea sehemu za membreni kusalia ndani ya mwili wa mama. Ishike plasenta kwa mikono yote miwili kisha uigeuze taratibu hadi membreni zipindika (Mchoro 6.3). Ivute plasenta taratibu ili kuiondoa kabisa.
Kutolewa kwa plasenta huashiria mwisho wa awamu ya tatu ya leba. Sasa uterasi inafaa kuwa ngumu, ya duara na inayoweza kusonga uterasi inapopapaswa. Unafaa kuihisi ikiwa katikati mwa kitovu cha mama na mfupa wa kinena. Uke haufai kuwa ukivuja damu. Kibofu kinafaa kuwa kitupu.
Ipapase uterasi punde tu baada ya plasenta kutolewa ili kuikazisha na kusitisha damu kuvuja. Wanawake wengi huhitaji kupapaswa uterasi ili kuisaidia kukazana (Mchoro 6.4).
Ichunguze plasenta kwa makini kuhakikisha kuwa hakuna sehemu iliyosalia ndani.
Kumbuka anatomi ya plasenta kutoka Moduli ya Utunzaji wa kabla ya Kuzaa, Kipindi cha 5. Je, sehemu ya juu ya mama ni upande wa juu ambapo kambakitovu hutokezea, au ni upande wa chini wa plasenta?
Sehemu ya juu ya plasenta ni upande wa chini, iliyo mkabala na sehemu ambapo kambakitovu hutokeza.
Mwisho wa jibu
Kipande cha sehemu ya juu ya mama (Mchoro 6.5) kinaweza kuwa kinakosekana. Au unaweza kuona membreni ambazo zimeraruka zilizo na mishipa ya damu. Vipande hivyo vya plasenta husalia ndani ya uterasi. Mpendekezee mama rufaa ya dharura.
Eleza ni kwa nini unafaa kumpendekezea rufaa mwanamke aliye na plasenta ambayo ina vipande vilivyosalia ndani ya uterasi.
Vipande vya plasenta vilivyosalia ndani ya uterasi huongeza hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa.
Mwisho wa jibu
Sehemu za duara zisizo na umbo maalum zilizo chiniya plasenta huitwa ndewe. (Baadhi ya vitabu vya masomo huziitakotilidoni. )Kinyume na matarajio, sehemu ya juu ya plasenta ni nyororo na ng’avu. Kitovu hujipandikiza upande huu, kisha kusambaa kama mishipa ya rangi ya sanawati nzito mfano wa mizizi ya mti (Mchoro 6.6).
Iwapo vipande vya plasenta au membreni zimesalia ndani ya uterasi, mama huyu yuko hatarini.
Istilahi ya kimaumbile iliyo katika kifungu hiki ilielezwa na kufafanuliwa katika Kipindi cha 3 cha Moduli ya Utunzaji wa kabla ya Kuzaa, Sehemu ya 1 (Mchoro 3.2). Ili kuidhibti awamu ya tatu ya leba, fuata hatua zifuatazo:
Ni kwa nini ni muhimu kukamilisha hatua zote 6 za utaratibu wa UTATL? Utaratibu huu ni upi?
Ni muhimu kukamilisha hatua hizi katika utaratibu unaofaa. Utafiti unaonyesha kuwa iwapo UTATL inatumiwa vyema, inaweza kuounguza hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa kwa 60%. Kisanduku 6.2 kinaorodhesha hatua 6 kwa utaratibu maalum.
Mwisho wa jibu
Katika Kipindi cha 11, utajifunza fasili ya kuvuja damu kwa wingi na hatua unazofaa kuchukua iwapo mwanamme anavuja damu baada ya kuzaa. Kipindi cha 11 pia kinaeleza hatua za kuingilia kati ambazo zinafaa kuchukuliwa katika awamu ya tatu ya leba na baada ya awamu hii ili kupunguza hatari ya Kuvuja Damu baada ya Kuzaa. Vidokezo vilivyo muhimu vimeandikwa kwa muhtasari hapa.
Usizidishe vipimo 1,000 µg za misoprostol (tembe 5). Iwapo mwanamke atatumia vipimo 600 µg (tembe 3) baada ya kuzaa na anavuja damu kwa wingi, usimpe zaidi ya 400 µg (tembe 2) kupitia rektamu Kipimo sahihi hakisababishi madhara. Iwapo hakutumia vipimo 600 µg vya misoprostol kupitia mdomoni baada ya kuzaa na anavuja damu kwa wingi, mpe vipimo 1,000 µg vya misoprostol kupitia rektamu kwa kipimo kimoja.
Iwapo oxytocin ilitumika mwanzoni, usimpe misoprostol zaidi.
Iwapo mwanamke huyu atavuja damu kwa wingi, mpeleke kwenye kituo cha afya mara moja. Kipindi cha 11 kitakufunza hatua za kuchukua wakati wa safari.
Iwapo damu haikomi kuvuja upesi baada ya kipimo cha pili cha misoprostol, mpendekezee rufaa ya dharura kwenda katika kituo cha afya kilicho karibu. Wakati mwingine, damu huvuja kutoka kwenye uke uliojeruhiwa, seviksi iliyojeruhiwa au uterasi iliyojeruhiwa. Kwa kawaida, damu hii huvuja kwa mchiririko wa polepole na usiokoma. Damu hii kwa kawaida huwa nyembamba na ya rangi nyekundu ng’avu. Hatua za kuchukua unaposubiri uchukuzi:
Plasenta iliyosalia ni wakati plasenta imesalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30 baada ya mtoto kuzaliwa. Iwapo plasenta itasalia ndani ya uterasi kwa zaidi ya dakika 30, fanya mambo yafuatayo:
Katika Kipindi cha 6, ulijifunza yafuatayo:
Kwa kuwa sasa umekamilisha kipindi hiki, jibu maswali yafuatayo ili kubaini jinsi ulivyojifunza. Unaweza kulinganisha majibu yako na uliyoandika kwenye Maswali ya Kujitathmini mwishoni mwa Moduli hii.
Mwisho wa jibu
Alemitu ni Mhudumu wa Afya Ugani katika Kituo cha afya cha kijijini. Amemaliza kuzalisha katika kituo chake muda mfupi uliopita. Mama anayemhudumia yuko katika awamu ya tatu ya leba, na ameanza kunyonyesha. Alemitu amehitimu kutumia UTATL. Hatua 6 za UTATL, kwa kina, ni zipi?
Hatua 6 za UTATL ni kama ifuatavyo:
1: je, kuna mtoto wa pili?
2 Mpe mama dawa ya kukazisha uterasi ili kuiwezesha kukazana:
3 Itoe plasenta kwa kutumia njia ya kuvuta kitovu taratibu kwa msukumo pinzani (Kisanduku 6.3 kinaeleza kwa kina.)
4 Papasa uterasi
5 Ichunguze plasenta na membreni za fetasi kuhakikisha kuwa hakuna vipande vilivyosalia. Chunguza ndewe na sehemu ya juu ya mama. Tia mkono wako ndani ya membreni kuhakikisha kuwa membreni hizi ni nzima. Hakikisha kuwa hali ya kambakitovu ni ya kawaida.
6 Chunguza uke na sehemu ya nje ya uke wa mama ili kutambua kama kuna mchibuko au damu inayovuja.
Mwisho wa jibu
Husika kwa Utendeti katika Kudhibiti Awamu ya Tatu ya Leba Ulitumia UTATL ifaavyo, lakini mwanamke huyu ameendelea kuvuja damu.
Mwisho wa jibu
Je, dalili hatari zinazoashiria matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba ni zipi?
Dalili hizi hatari ni ishara ya matatizo katika awamu ya tatu ya leba:
Mwisho wa jibu