6. Husika kwa Utendeti katika Kudhibiti Awamu ya Tatu ya Leba

Kipindi cha 6 cha Somo Husika kwa Utendeti katika Kudhibiti Awamu ya Tatu ya Leba

Utangulizi

Katika kipindi kilichopita, ulijifunza zaidi kuhusu kuvuja damu baada ya kuzaa. Hali hii ni mojawapo ya visababishi vikuu vya vifo vya kina mama vinavyo husiana na kuzaa. Kuvuja damu baada ya kuzaa husababisha 1/4 ya vifo vyote vya kina mama vinavyo husiana na kuzaa. Duniani kote, takriban wanawake 127,000 hufa kila mwaka kutokana na kuvuja damu baada ya kuzaa. Vingi vya visa hivi vya kuvuja damu kwa wingi hutokea katika saa 24 za kwanza baada ya kuzaa. Vifo hivi husababishwa na matatizo katika awamu ya tatu ya leba. Ili kupunguza hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa, wahudumu wote wa kuzalisha wanafaa kufuata mseto wa hatua maalum zilizowekwa. Hatua hizi hujulikana kama udhibiti tendeti la awamu ya tatu ya leba (UTATL). Utaratibu wa UTATL unapofanywa inavyofaa, hatari ya kuvuja damu baada ya kuzaa hupunguzwa kwa zaidi ya 60%.

Katika kipindi hiki, utajifunza kuhusu UTATL na mambo ya kufanya katika hatua zote 6. Maarifa haya yatakusaidia kutambua na kuyadhibiti kikamilifu matatizo yanayoweza kutokea katika awamu ya tatu ya leba.

Matokeo ya Masomo ya Kipindi cha 6