Skip to main content
Printable page generated Thursday, 8 Dec 2022, 23:18
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2022 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Thursday, 8 Dec 2022, 23:18

9. Leba Iliyozuiliwa

Kipindi cha 9 Leba Iliyozuiliwa

Utangulizi

Leba iliyozuiliwa inaweza kukingwa. Moja wapo ya majukumu yako makuu kama mhudumu wa kuzalisha mwenye ujuzi ni kukinga leba iliyozuiliwa kwa wanawake katika jamii yako. Leba iliyozuiliwa hutokea zaidi katika maeneo ya vijiji vya Afrika, hasa miongoni mwa wanawake wanaokaa na leba nyumbani kwa muda mrefu.

Leba iliyozuiliwa inahusishwa na vifo wakati wa kuzaa na magonjwa. (Vifo wakati wa kuzaa ni vifo vya fetasi au mtoto mchanga. Ugojwa ni hali ya kuugua na ulemavu unaotokea wakati huo wa kuzaliwa. Leba iliyozuiliwa inachangia kati ya asilimia 10- 25 ya vifo vya kina mama Sahara ya Afrika. Kwa kweli, takwimu hii inayoshangaza ni kupuuza ya tatizo. Vifo vinavyosababishwa na leba iliyozuiliwa mara nyingi vinaainishwa chini ya matatizo mengine (kama vile sepsisi, kuvuja damu baada ya kuzaa, au uterasi iliyopasuka).

Katika Kipindi hiki, utajifunza kutambua dalili za kawaida za leba za muda mrefu na zilizozuiliwa. Utajifunza kutambua njia bora zaidi ya udhibitishaji. Udhibitishaji uliochelewa wa leba iliyozuiliwa mara nyingi husababisha nasuri kwa wanawake wanaoishi. Ikiwa fistula haitatibiwa, kina mama wanaweza kutengwa na jamii.

Malengo ya Kipindi cha 9

Baada ya Kipindi hiki cha, utaweza:

9.1 Kufafanua na kutumia kwa ufasaha maneno yote muhimu yaliyochapishwa kwa herufi nzito. (Maswali ya Kujitathmini 9.2 na 9.3)

9.2 Kuorodhesha visababishi vikuu vya leba iliyozuiliwa. Kuelezea jinsi kila hali inachangia kwa ukuwaji wa leba iliyozuiliwa. (Swali la Kujitathmini 9.1)

9.3 Kuelezea dalili za kawaida za leba iliyozuiliwa. Kuelezea matatizo ya kawaida kwa mama na fetasi yanayotokana na leba iliyozuiliwa. (Swali la Kujitathmini 9.3)

9.4 Kuelezea udhibitishaji wa leba iliyozuiliwa. Kuelezea njia za kukinga leba iliyozuiliwa. (Swali la Kujitathmini 9.3)

9.5 Kueleza jinsi mabadiliko ya kijamii katika jamii inaweza kupunguza nafasi ya kuwa na leba iliyozuiliwa inaweza kutokea (Swali la Kujitathmini 9.4)

9.1 Ufafanuzi wa leba iliyozuiliwa

Leba iliyozuiliwa ni kushindwa kwa fetasi kuteremka kupitia njia ya uzazi kwa sababu kizuizi kinazuia kuteremka. Leba iliyozuiliwa hutokea hata na mikazo mikali ya uterasi. Kwa kawaida uzuiliaji hutokea ukingoni mwa pelvisi. Inaweza kutokea katika tundu au mlangoni mwa pelvisi. Wakati leba inapokaa kwa muda mrefu kwa sababu ya kukosa kuendelea kukua, kuna hatari kubwa hivi kwamba ushukaji wa fetasi itazuiliwa. Leba iliyokaa kwa muda mrefu haina ufafanuzi mmoja. Inayobainishwa kama “muda mrefu” inatofautiana kulingana na hatua ya leba (Jedwali 9.1).

Jedwali 9.1 Ni wakati upi leba itasemekana kuwa imedumu muda mrefu katika hatua tofauti za leba?

 • Awamu fiche ya leba tendi iliyorefushwa: wakati leba ya ukweli inapoendelea zaidi ya masaa kama 8 lakini haiingii katika hatua ya kwanza.
 • Awamu ya leba tendi iliyorefushwa: wakati leba ya ukweli inapochukua zaidi ya saa kama 12 lakini haiingii kwa hatua ya pili.
 • Hatua ya pili ya leba iliyorefushwa:
  • Mama Multigravida: wakati leba hukaa zaidi saa 1.
  • MamaPrimigravida: wakati leba hukaa zaidi masaa 2.

Leba inaweza kuainishwa kuwa “iliyorefushwa” katika hatua yoyote. Hata hivyo, kumbuka kuwa leba iliyozuiliwa kawaida hutokea baada ya leba kuingia hatua ya pili.

9.2 Visababishi vya leba iliyozuiliwa

Kwa kawaida, leba iliyozuiliwa hutokea katika hatua ya pili ya leba kwa wanawake ambao leba yao hurefushwa. Kwa nini leba huwa ya muda mrefu au iliyozuiliwa, hii inaweza kuwa ni sababu ya “nguvu”, “abiria”, na “njia”.

 • Nguvu:Upungufu wa nguvu ni sababu kuu ya leba iliyorefushwa. Upungufu wa nguvu husababishwa na mikazo ya uterasi iliyoduni au isiyokuwa na mpangilio. Wakati mwingine mikazo ya uterasi haina nguvu ya kutosha ya kuvuta na kupanua seviksi katika hatua ya kwanza ya leba. Wakati mwingine nguvu ya mikazo ya uterasi haitoshi kusukuma mtoto chini kwa njia ya uzazi katika hatua ya pili.
 • Abiria:Fetasi ndio “abiria” ambaye hupita kwa njia ya uzazi. Ikiwa kichwa cha fetasi ni kubwa sana kupita kwa pelvisi ya mama, leba iliyorefushwa inaweza kutokea. Ikiwa kitangulizi sio cha kawaida, leba iliyorefushwa inaweza kutokea.
 • Njia: Njia ya uzazi ndipo pahali mtoto hupitia. Ikiwa kichwa cha fetasi ni kubwa sana kupita kwa pelvisi ya mama, leba iliyorefushwa inaweza kutokea. Ikiwa pelvisi inaumbo isiyo ya kawaida, au ikiwa uvimbe au kizuizi chochote kile katika pelvisi, leba inaweza kurefushwa.

Jedwali 9.1 Inatoa muhtasari wa visababishi vya ukosefu wa “abiria” and “njia”.

Jedwali 9.1 Visababishi vya abiria na ukosefu wa njia ya uzazi zinazosababisha leba ya muda mrefu na zilizozuiliwa.
Abiria Njia

Kichwa:

● Kichwa cha fetasi kikubwa (kikubwa kwa hicho fetasi)

● Hidrosefalasi (kukusanyika kwa maji ndani ya kichwa, inayosababisha uvimbe wa fuvu)

Kitangulizi na mkao:

● Paji la uso, uso, bega

● Uendelefu wa kukaa vibaya kwa fetasi

Mimba ya mapacha:

● Mapacha waliofungiana (kufungiana kwa shingo)

● Mapacha walioshikana (walioshikana na kutumia baadhi ya viungo pamoja)

Mifupa ya pelvisi:

●   Upungufu (kwa sababu ya utapia mlo)

●   Iliyoumbuka (kwa sababu ya jeraha au polio)

Tishu nyororo:

●   Uvimbe kwenye pelvisi

●   Maambukizi ya virusi kwenye uterasi au fumbatio

●   Kovu (kutokana na ukeketaji)

Vizuizi vinavyosababisha leba ya muda mrefu na leba iliyozuiliwa katika jedwali 9.1 vinaweza kuwekwa kwa vikundi: kichwa kisicholingana na pelvisi; kitangulizi na mtoto kukaa vibaya; au fetasi ambaye si wa kawaida au mama ambaye analeba iliyozuiliwa kwa njia ya uzazi. Kila aina imeelezwa kwa undani.

9.2.1 Kutolingana kwa kichwana pelvisi

Kutolingana kinakueleza kwamba ukubwa wa kichwa cha fetasi ni tofauti na ukubwa wa ukingo wa pelvisi ya mama.

Kutolingana kwa kichwa na pelvisi inamaanisha kuwa fetasi haiwezi kupita kwa usalama pelvisi ya mama. Aidha pelvisi ni nyembamba sana kwa kichwa cha fetasi au kichwa ni kubwa mno ukilinganisha na pelvisi. (Mchoro 9.1) Kumbuka anatomi ya pelvisi ya wajawazito na fuvu ya fetasi ambayo ulijifunza katika Kipindi cha 6 cha Somo la Moduli ya Huduma ya wajawazito). Wanawake katika nchi zinazoendelea wanaweza kuwa na pelvisi ndogo au imepunguka. Hali hii inasababishwa na utapia mlo utotoni unaoendelea hadi kufikia utu uzima. Kutolingana kwa kichwa na pelvisi kwa kawaida haiwezi kutambulika kabla wiki ya 37 ya ujauzito. Kabla ya wakati huo, kichwa cha mtoto hakijapata ukubwa wa kuzaliwa.

9.2.2 Kitangulizi kisicho cha kawaida na mimba nyingi

Mchoro 9.1 Kutolingana kwa kichwa na pelvisi: pelvisi ya mama huyu ni ndogo sana kwa kichwa cha mtoto wake.

Ukaaji wa kitangulizi au kukaa vibaya ni sababu zingine kuu za leba iliyozuiliwa.

 • Je, unaweza kutofautisha kati ya maneno haya mawili na kukumbuka baadhi ya vitangulizi vya fetasi visivyokuwa vya kawaida na kutokuwa katika mkao wa kawaida katika uterasi kutoka Kipindi cha 8 cha Somo?

 • Kitangulizi kisicho cha kawaida ni kitangulizi chochote bali sio kipeo, ambayo ni wakati fuvu la kichwa cha mtoto hutangulia kwanza. Kawaida vitangulizi visivyokuwa vya kawaida huwa makalio na bega itakapotoka “bega kwanza”. (Kitanguliza cha makalio ni wakati makalio ya mtoto na/au miguu hutoka kwanza.) Mkao mbaya in wakati mtoto huwa “kichwa chake kiko chini” (kichwa ndio–kitangulizi) lakini kipeo kiko pahali hapafai ikilinganishwa na pelvisi ya mama. Aina mbili za kawaida zaidi za mkao wa fetasi usiofaa husababisha utangulishi wa uso na paji la uso.

  Mwisho wa jibu

Pia ulijifunza kuhusu kupata mimba nyingi katika Kipindi cha 8 cha Somo. Leba inaweza kuzuiliwa na mapacha waliofungiana au mapacha walioshikana. Mapacha waliofungiana ni watoto wawili “waliofungana” pamoja kwa shingo wakati pacha wa kwanza akiwa katika kutanguliza tako na wa pili yuko katika kutanguliza kichwa mwanzo. Mapacha walioshikana huwa wameungana kwa kifua, kichwa, au eneo lingine lolote lile.

9.2.3 Ulemavu wa fetasi

Baadhi ya ulemavu wa fetasi usiokuwa wa kawaida husababishwa na fetasi ambaye ana kichwa mkubwa ambayo usiokuwa wa kawaida. Mfano mmoja ni hidrosefalasi, ambayo inasababishwa na viowevu kukusanyika katika ubongo wa mtoto.

9.2.4 Njia ya uzazi isiyokuwa ya kawaida

Leba iliyozuiliwa inaweza kusababishwa na njia ya uzazi ya mama isiyokuwa ya kawaida. Mama anaweza kuwa na tyuma (ukuwaji au uvimbe wa tishu) katika kaviti ya pelvisi. Au mama anaweza kuwa na kovu katika njia ya uzazi sababu ya njia kali ya ukeketaji. Au anaweza kuwa na msamba ambayo imebana, usio panuka ili kupitisha mtoto. (Msamba ni ngozi iliyo katikati ya ufa wa uke na mkundu.)

Ukeketaji ndio lengo la Kipindi cha 5 Somo katika moduli ya Balehe na afya ya uzazi ya vijana.

9.3 Dalili za leba iliyozuiliwa

Ishara ya uhakika wa leba iliyozuiliwa ni wakati kipenyo pana ya fuvu ya fetasi hubaki bila kusonga juu ya ukingo wa pelvisi sababu haiwezi kushuka. Ili kutambua kizuizi hiki, papasa fumbatio ya mama kwa makini kama uterasi inatulia na kuwa nyororo kati ya mikazo. Hata hivyo, uterasi inaweza kuwa na mikazo toni (inaendelea kuwa ngumu) na inakaa na inafinyilia fetasi. Ni vigumu kuhisi kama fetasi inateremka kwa njia ya uzazi. Kupapasa uterasi pia inamfanya mama kuhisi maumivu makali. Katika hali hii, tegemea dalili zingine kwa utambuzi wako.

9.3.1 Utathmini wa dalili za kliniki ya hali iliyozuiliwa

Kuna uwezekano zaidi ya leba iliyozuiliwa kutokea iwapo taarifa hizi ni za kweli:

 • Leba ikiwa ni ya muda mrefu (kukaa zaidi ya saa 12).
 • Mama anaonekana kuwa amechoka, anawasiwasi, na amedhoofika.
 • Membreni ya fetasi imepasuka na amnii kutoka saa kadhaa kabla ya leba kuanza.
 • Mama ana dalili muhimu zisizo za kawaida: mpigo wa mshipa wa damu ulio wa kasi, zaidi ya mipigo 100 kwa dakika; kiwango cha chini cha shinikizo la damu; kiwango cha kupumua zaidi ya 30 kwa dakika; pengine kiwango cha joto mwilini kilicho juu.

Tathmini mwanamke aliye na historia hii ya leba kwa kupima uke wake. Yoyote kati ya dalili hizi inaonyesha kuwa kuna leba iliyozuiliwa:

 • Mekoniamu iliyo na harufu mbaya inayotoka ukeni.
 • Mkojo uliomumunyika, ambayo unaweza kuwa na mekoniamu au damu.
 • Edema ya valva, hasa ikiwa mwanamke amekuwa akisukuma kwa muda mrefu. Unahisi uke kuwa moto na kavu kwa kidole chako kilicho na glavu kwa sababu ya upungufu wa maji mwilini. (Edema ni uvimbe kwa sababu ya mkusanyiko wa viowevu wa tishu. Valva ni sehemu siri ya nje ya mwanamke, ikiwa ni pamoja na midomo.)
 • Edema ya seviksi.
 • Unaweza kuhisi uvimbe mkubwa juu ya fuvu ya fetasi (Kaputii, Kipindi cha 4).
 • Kitangulizi au mlalo usiokuwa wa kawaida wa fetasi.
 • Uambatanano duni wa seviksi na kitangulizi (angalia nyuma katika Mchoro 1.1 katika Kipindi cha kwanza somo); kama matokeo seviksi inahisi kama “mkono tupu wa vazi”.
 • Bandl’s ring (Mchoro 9.2).

9.3.2 Bandl’s ring

Bandl’s ring ni jina linalopewa mbonyeo katikati ya uterasi ya juu na chini, karibu na kitovu. Haufai kuona au kuhisi Bandl's ring ukipima fumbatio ya mama katika leba ya kawaida (Mchoro 9.2a). Unapoona au kuhisi Bandl's ring (Mchoro 9.2b), ni ishara ya mwisho ya leba iliyozuiliwa. Juu ya mbonyeo hiuu kuna sehemu ya juu ya uterasi ambayo ni nene mno. Sehemu hii ya juu imevutwa kwa upande wa juu (kurudi ndani) kuelekea kwenye mbavu za mama. Chini ya Bandi's ring ni uvimbe (uliofura), mkonde hatari, sehemu ya chini ya uterasi. Sehemu ya chini ya fumbatio inaweza zaidi kuvimbishwa na kibovu kilichojaa na gesi ndani ya matumbo.

Mchoro 9.2 (a) Umbo la kawaida la fumbatio iliyo na mimba wakati wa leba, kwa mwanamke aliye lala chali; (b) Bandi's ring kwa fumbatio ya mama aliye kwa leba iliyozuiliwa.

9.3.3 Ushahidi kutoka kwa patografu

Kumbuka kutoka Kipindi 4 cha Somo kwamba patografu ni chombo muhimu cha kutambua leba usiokuwa wa kawaida au ya muda mrefu. Leba iliyozuiliwa inaonyeshwa na rekodi ya patografu ya kiwango cha utanuzi wa seviksi na kiwango cha kuteremka kwa kichwa cha fetasi. (Kumbuka kwamba seviksi inapaswa kutanuka angalau sentimita 1 kwa saa) Mchoro 9.3 (a) kinaonyesha rekodi ya patoghraph ya kawaida na utanuzi unaoendelea kuteremka kwa kichwa cha fetasi. Hata hivyo katika Mchoro 9.3 (b) unaweza kuona ushahidi wa leba ya muda mrefu katika hatua ya leba ya kwanza au ya pili. Kipimo cha utanuzi wa seviksi kimepita “Mstari wa Tahadhari”. Iwapo hatua haitachukuliwa, itapita mstari wa Hatua. Licha ya mikazo mikali ya uterasi, kichwa cha fetasi haki shuki.

Mchoro 9.3 (a) Utanuzi wa seviksi wa kawaida na kuteremka kwa kichwa cha fetasi iliyorekodiwa katika patografu. (b) Utanuzi wa seviksi umekoma na mstari wa kurekodi umepita mstari wa Hatua.

Rekodi ya utanuzi wa seviksi kwenye patografu haipaswi kupita mstari wa Tahadhari na/au wa Hatua. Iwapo aidha ya mstari itapitwa, leba hii ni ya muda mrefu na pengine iliyozuiliwa. Fanya rufaa wa haraka.

 • Katika Mchoro 9.3 (b), ni masaa ngapi baada ya kuanza kurekodi patografu ndipo maendeleo ya utanuzi wa seviksi ulipokoma?

 • Seviksi ilikoma kutanuka masaa 4 baada ya kuanza kurekodi patografu.

  Mwisho wa jibu

 • Katika patografu inayoonyeshwa katika Mchoro 9.3(b), ni saa ngapi imepita tangu kuwe na ishara yoyote ya utanuzi wa seviksi?

 • Patografu inaonyesha kwamba kipenyo cha seviksi hakijaongezeka kwa masaa mawili na nusu yaliyopita.

  Mwisho wa jibu

9.4 Udhibiti wa leba iliyozuiliwa

Iwapo rekondi ya utanuzi wa servikisi imefika mstari wa Tahadhari kwa patografu, jaribu kuondoa kizuizi kabla haijafikia mstari wa hatua. Ulijifunza taratibu hizi katika Moduli ya huduma za ujauzito (Kipindi cha 22 cha Somo) na ujuzi wako kwa mafunzo ya vitendo. Zimeelezewa hapa kwa ufupi:

 • Ikiwa mwanamke ana dalili za mshtuko, mpe kiowevu aina ya Normal Saline au Ringer’s Lactate ili kuregeshea kiowevu mwilini. (Dalili za mshtuko ni mpigo wa mshipa wa haraka na shinikizo la damu ilio chini.) Tumia kanula kubwa (Nambari. 18 au 20) Mpe lita 1 ya viowevu, haraka iwezekanavyo. Rudia lita 1 kila baada ya dakika 20 mpaka kiwango cha mpigo wa mshipa upungue chini ya 90 kwa kila dakika, na shinikizo la damu diastoli ifikie 90 mmHg au zaidi (Diastoli ya shinikizo la damu ni wakati roho inatulia baada ya piga.)
 • Kama unafikiri kizuizi ni kutokana na kibofu cha mkojo kilio jaa sana, toa na catheta. Safisha msamba na weka katheta kwa kibofu cha mama. Weka mkojo katika chombo kilicho funikwa. Kutoa kizuizi hiki inawezesha mtoto kuzaliwa. Kumbuka kwa kawaida ni vigumu sana kuweka katheta kwenye kibofu kwa mwanamke aliye na leba iliyozuiliwa. Urethra pia huwa imefungwa na kichwa cha mtoto, ambacho kiko ndani kabisa.

Mpeleke mama haraka kwa kituo cha afya ambapo huduma ya upasuaji inapatikana (Mchoro 9.4). Anaweza kuhitaji uzalishaji wa dharura kwa operesheni ya upasuaji ilikutoa mtoto akiwa hai na kuokoa maisha yake. (Operesheni ya siza ni wakati fumbatio yake na uterasi hufunguliwa kwa kukatwa ili kutoa mtoto.)

Mchoro 9.4 Usichelewe kurufaa mwanamke ambaye leba yake ina kizuizi.

9.5 Matatizo yanayotokana na leba iliyozuiliwa

Matatizo ya uterasi iliyozuiliwa kwa mama na fetasi au mtoto mchanga yanaweza kuwa hatari sana. Kumbuka kwamba vizuizi vya uterasi hutokea hasa kwa sababu ya leba ya muda mrefu nyumbani ambayo haijafuatiliwa vizuri na rufaa haikupeanwa kwa haraka. Matatizo ya kawaida zaidi ambayo huathiri mama ni ukuaji wa fistula.

9.5.1 Fistula

Fistula ni ufunguzi usiokuwa wa kawaida (kwa kawaida hutokea kwa sababu ya tishu kukatika) kati ya:

 • Uke na kibofu cha mkojo
 • Uke na rektamu
 • Uke na urethra (neli ambayo huleta mkojo kutoka kwa kibofu hadi ufunguzikatika valva)
 • Uke na ureta(mshipa ambayo huleta mkojo kutoka kila figo kwa kibofu cha mkojo)
Mchoro 9.5 Fistula ni tatizo la leba iliyozuiliwa inayosababisha matatizo zaidi.

Fistula inapitisha mkojo au kinyesi ndani ya uke na kisha hutokea kwa njia isiyozuilika. Mwanamke aliye na fistula anaweza kutoa mkojo au kinyesi wakati anapotembea au kufanya shughuli yoyote ya kila siku. Uchafu huu uchafua nguo zake na huleta harufu mbaya (Mchoro 9.5). Kwa sababu ya athari hizi, mume wake na familia wanaweza kumshutumu au kumtenga. Unaweza kufikiria kuendelea kuvuja kwa mkojo au kinyesi ina maana gani kwa mtu binafsi. Matokeo mengine ya fistula ni pamoja na mfadhaiko kila mara, magonjwa ya mwili na maambukizi ya njia ya uzazi, kibofu na figo. Wakati mwingine mwanamke hujiua.

Leba iliyozuiliwa husababisha karibu 20% ya kesi zote za ukuaji wa fistula (Mchoro 9.6).

Matukio = 0.20 x 0.25 x 0.20 = 0.001, au 1 kwa kila 1,000 wanaozaa Mchoro 9.6 Ukadiriaji wa majaribio ya kitaalamkwa maendeleo ya leba ya muda mrefu kwa uzazimfu na utokezaji wa fistula katika nchi zilizo na hatari-kubwa katika nchi za Afrika jangwani mwa Sahara (Chanzo:Amy Tsui and others, The Gates Institute, Johns Hopkins Bloomberg School of Public Health, July 30, 2005).

Katika hali chache, mambo haya yanaweza kusababisha fistula:

 • matatizo ya kuzaliwa: mawasiliano yasiyokuwa ya kawaida kati ya rektamu na uke, inayopatikanawakati wa kuzaliwa
 • maambukizi: hasa kifua kikuu
 • jeraha
 • ngono ya lazima: ubakaji
 • ngono katika umri mdogo

9.5.2 Matatizo mengine ya kawaida ya leba iliyozuiliwa

Ikiwa leba iliyozuliwa haitadhibitiwa vizuri, inaweza kusababisha matatizo haya mengine kwa mama:

 • Kuvuja damu baada ya kuzaa (utajifunza kuhusu tatizo hili katika Kipindi cha 11)
 • Kurudi polepole kwa uterasi kwa hali iliyokuwa kabla ya ujauzito
 • Mshtuko (shinikizo la damu la chini na moyo kupiga kwa haraka)
 • Utumbo mdogo inapooza na inaacha kusonga(ileus iliyopooza)
 • Sepsisi (kuenea kwa maambukizi mwili mzima)
 • Kifo

Leba iliyozuiliwa inaweza kusababisha matatizo haya kwa mtoto mchanga:

Unaweza kujifunza kuhusu matatizo yanayowaathiri watoto wachanga katika Moduli ya Utunzaaji baada ya kuzaa na Moduli ya Huduma Sawa kwa watoto wachanga na Magonjwa ya watoto

 • Sepsisi kwa mtoto mdogo
 • Degedege
 • Jeraha usoni
 • Ukosefu mkali wa oksijeni (ukosefu wa oksijeni unaotishia maisha)
 • Kifo

9.6 Kukinga leba iliyozuiliwa

Mkunga mwenye ujuzi anaweza kufanya mambo kadhaa ili kuzuia leba ya muda mrefu. Zaidi ya hayo, baadhi ya mabadiliko ya kitamaduni huleta tofauti kubwa kwa hali zinazoongezea hatari ya leba iliyozuliwa. Sasa tuangalie kwa kifupi hali hizi.

9.6.1 Mkunga aliye na ujuzi

Leba iliyozuliwa ni sababu kubwa ya vifo vya kina mama kote duniani na hasa katika nchi zinazoendelea barani Afrika. Hatua muhimu zaidi inayoweza kuzuia vifo hivi na ulemavu ni kuwa na huduma ya mkunga mwenye ujuzi wakati wa kuzaa. Jukumu lako muhimu kama mfanyakazi wa afya vijijini ni kuwafundisha watu katika jamii yako umuhimu wa kupata huduma yenye bora wakati wa kuzaa kila wakati. Hamasisha wanawake kuja kwenu kwa ushauri. Dumisha uhusiano wa karibu na vituo vya afya au hospitali (kama ipo) katika eneo lako. Unahitaji rufaa kwa haraka na inayofaa wakati wa hali za dharura.

9.6.2 Tumia Patografu

Chombo bora zaidi kwa utambuzi wa leba ya muda mrefu ni kuandika hatua za leba kwenye patografu. Wakati huo huo, mara kwa mara tathmini hali ya fetasi na ya mama (Kipindi cha 4). Rekodi iliyo kwa patografu inakupa onyo mapema kuwa leba inaweza kuwa ya muda mrefu kwa hakika ambapo uwezekano wa uzuizi wa uterasi inaonekana kuwa na rufaa ni muhimu. Daima tumia patografu wakati unapotoa huduma ya kuzaa.

 • Ni mambo gani mawili lazima uyafanye kuzuia mwanamke ambaye yuko katika leba kupata fistula?

 • Fanya mambo haya mawili:

  • Fuatilia kwa makini maendeleo ya leba kwa kutumia patografu. Hakisha kwamba rekodi ya upanuzi wa seviksi unakaa juu au kwa kushoto wa mstari wa tahadhari.
  • Kwa haraka mtume mama kwenye kituo cha afya iwapo yuko na leba iliyozuiliwa. (Rufaa iwapo rekodi ya utanuzi wa seviksi inakaribia mstari wa hatua kwa patografu.) Kama inafaa, weka kiowevu kwa mshipa au katheta kwa kibofu cha mama kabla ya kurufaa.

  Mwisho wa jibu

9.6.3 Maandalizi ya kuzaa na kujitayarisha kwa matatizo

Kama ulivyojifunza katika Moduli ya huduma za ujauzito (Kipindi cha 13), maandalizi ya kuzaa na kuwa tayari kwa matatizo ni muhimu kwa ajili ya leba na kuzaa kwa usalama. Hivyo saidia jamii yako kujipanga katika vikundi vya maandalizi ya kuzaa. Vikundi hivi lazima viwe na uongozi, elimu, fedha, na namna ya usafiri. Iwapo hali ya dharura kama vile leba iliyozuiliwa inatokea, vikundi hivi lazima vipeleke mama kwenye kituo cha afya kilicho karibu.

9.6.4 Mafunzo ya lishe bora

Ni muhimu kuwaelezea hali zinazoongeza hatari za leba iliyozuiliwa. Sababu kuu ya leba iliyozuiliwa ni pelvisi iliyo ndogo. Mara nyingi, pelvisi ndogo ni matokeo ya lishe duni katika utotoni inayoendelea katika utu uzima. Boresha lishe utotoni kwa njia ya elimu ya afya, hasa kwa wasichana. Lishe bora kwa wasichana hupunguza hatari ya leba ya muda mrefu na leba iliyozuliwa katika maisha ya baadaye.

9.6.5 Zuia ndoa ya mapema

Ndoa ya mapema ndio suala la Kipindi cha somo katika Moduli juu ya Vijana Waliobaleghe na Afya ya Uzaaji wa Vijana.

Suala lingine ni ndoa ya mapema. Utafiti katika Sahara ya Afrika imeonyesha kuwa 50% ya wanawake, hasa wale wa vijijini, huolewa katika wastani ya miaka karibu 16. Wengi wa wanawake wadogo hupata mimba haraka. Kikuundi hiki cha kina mama wadogo sana kiko katika hatari hasa ya leba iliyozuiliwa. Pelvisi ya mama wa umri mdogo haijakomaa vilivyo ili kutoshea kichwa cha mtoto. Katika mazungumzo yako na wanawake, wenzio, na viongozi wa jamii, sisitiza hatari za ndoa ya mapema. Jaribu kuwashawishi kuchelewesha kuzaa mtoto wa kwanza mpaka baada ya mwanamke kufikia miaka 18. Kuza njia za kupanga uzazi ili kuchelewesha mimba ya kwanza miongoni mwa wanawake hawa wadogo sana. Ikiwa mimba isiyotarajiwa itatokea, ni muhimu pia kuwashauri kuhusu huduma salama ya utoaji wa mimba (Moduli ya Utunjazi katika Ujauzito, Sehemu ya 2, Kipindi cha 20).

Muhtasari wa Kipindi cha 9

Katika Kipindi cha 9, umejifunza mambo haya:

 1. Leba iliyozuiliwa ni kushindwa kwa fetasi kuteremka kupitia njia ya uzazi (pelvisi). Kizuizi huzuia fetasi kushuka licha ya mikazo ya uterasi yenye nguvu.
 2. Sababu za leba iliyozuiliwa ni kutolingana kati ya kichwa na pelvisi, kitangulizi kisichokuwa cha kawaida, fetasi iliyo na kasoro za kimaumbile, na matatizo kwa njia ya uzazi ya mama.
 3. Sababu za leba ya muda mrefu ni matatizo katika mmoja au zaidi ya hizi tatu: nguvu, fetasi, na njia.
 4. Chombo bora kwa kutambua leba ya muda mrefu ni patografu.
 5. Ishara za leba iliyozuiliwa ni pamoja na: mama kuwa kwa leba kwa zaidi ya saa 12, upungufu wa maji mwilini, uchovu na kushindwa kujisimamisha mwenyewe, ishara muhimu zisizokuwa za kawaida, huwepo wa Bandl’s ring kwa fumbatio, kibofu kilichojaa juu ya pubis symphysis, kaputi na ufinyazi mkubwa, ufunguzi wa uke unaweza kuwa na edema.
 6. Matatizo ya kawaida kwa mama ya leba iliyozuiliwa ni pamoja na sepsisi, utumbo uliopooza, kuvuja damu baada ya kuzaa na ukuaji wa fistula.
 7. Matatizo ya kawaida kwa fetasi ya leba iliyozuiliwa ni ukosefu mkali wa oksijeni, sepsisi kwa mchanga, na kifo.
 8. Rufaa ya mapema inaweza kuokoa maisha ya mwanamke na mtoto wakati leba iliyozuiliwa inapotokea

Maswali ya Kujitathmini kwa Kipindi cha 9

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, jibu maswali haya ilikutathmini uliyojifunza. Linganisha majibu yako na Vidokezo juu ya maswali ya kujitathmini mwishoni wa moduli hii.

Maswali ya Kujitathmini 9.1 ( Maswali ya Kujitathmini Malengo ya Somo la 9.2)

Andika maana ya hali tatu na jinsi zinasababisha leba iliyozuiliwa.

Answer

Hizi hali tatu (nguvu, msafiri, na njia) ni njia fupi ya kuelezea sababu kuu za leba iliyozuiliwa. Baada ya kukagua majibu yako ukilinganisha na haya, soma sehemu ya 9.2 tena ili kupata mengi zaidi kuhusu sababu hizi.

 • Nguvu inahusisha nguvu ya mikazo ya uterasi: mikazo duni mno au isiyo na ratiba na mtoto hasukumwi kwenye njia ya uzazi.
 • Msafiri anahusisha mtoto: kama kichwa ni kikubwa mno au kinakasoro, au kuna makosa kwa hali ile kichwa kinakaa au kitangulizi, mtoto hawezi kuteremka chini kwa njia ya uzazi
 • Njia inahusisha njia ya uzazi: ikiwa ni ndogo mno au kuna kasoro, au imefungana kutokana an uvimbe au makovu, mtoto hawezi kushuka vizuri.

Mwisho wa jibu

Maswali ya Kujitathmini 9.2 ( Maswali ya Kujitathmini ya Malengo ya Somo la 9.1)

Andika maana ya maneno haya:

 1. Vifo na magonjwa wakati wa kuzaliwa
 2. Muda mrefu wa awamu fiche ya leba
 3. Muda mrefu wa hatua ya pili ya leba
 4. Kukaa vibaya
 5. Kaputi
 6. Fistula
Answer
 1. Vifo na magonjwa wakati wa kuzaliwa: vifo kwa fetasi na watoto wachanga, ugonjwa na ulemavu unaotokea wakati wa kuzaa.
 2. Muda mrefu wa awamu fiche ya leba: wakati leba ya kweli inaendelea kwa zaidi ya saa 8 na haiingie katika hatua ya kwanza ya leba
 3. Muda mrefu wa hatua ya pili ya leba: wakati leba itaendelea kwa zaidi ya saa 1 (kwa mama multigravida) na zaidi ya saa 2 (mama primigravida).
 4. Kuka vibaya kwa: wakati mtoto "kichwa chini" lakini veteksi iko katika pahali pabaya ikilinganishwa na pelvisi ya mama. (Veteksi sehemu ya juu ya fuvu la mtoto.)
 5. Kaputi: Uvimbe mkubwa katikati ya fuvu ya fetasi.
 6. Fistula: ufunguzi usiokuwa wa kawaida kati ya uke na kibofu cha mkojo. Ufunguzi huu kawaida ni matokeo ya kupasuka. Ufunguzi pia unaweza kuwa kati ya rektamu au mkojo au ureta.

Mwisho wa jibu

Soma Uchunguzi Kifani 9.1 kisha ujibu maswali ambayo yanayofuatia.

Uchunguzi Kifani 9.1 Kisa cha Tadelech

Tadelech anaishi MekitWoreda. Safari kutoka kijijini hadi mjini inaweza kuchukua siku nyingi, na anaishi mbali na hata kituo ndogo cha afya. Tadelech ana umri wa miaka 25 na tayari amezaa watoto wawili salama kijiji. Ujauzito huu wake ni wa tatu. Mikazo ilianza katika wiki ya 40 ya ujauzito. Baada ya siku mbili za leba, Tadelech anabebwa kwenye machela hadi kwa kituo chako ndogo cha afya. Wakati unamchunguza Tadelech, unapata uvimbembili juu ya fumbatio na mbonyeo kati yao karibu na kitovu (kifungo kwa fumbatio). Pia unapata kuwa kichwa cha mtoto hakijaingia kwenye pelvisi. (Iko tu juu ya ukingo wa pelvisi). Uchunguzi wa uke, unakadiria kuwa seviksi ya Tadelech ina upanuzi wa sentimeta 8 na kituo cha kichwa cha fetasi ni -3. Uke wa Tadelech una moto na mkavu na ana edema kwa valva.

Maswali ya Kujitathmini 9.3 (Maswali ya Kujitathmini ya Malengo ya Somo la 9.1, 9.3 na 9.4)

 1. Ni dalili gani katika uchunguzi huu maalum zinazoonyesha leba ya muda mrefu au iliyozuiliwa?
 2. Jinsi gani unaweza kudhibiti hali ya Tadelech?
Answer
 1. Dalili hizi katika uchunguzi maalum kuhusu Tadelech zinaonyesha leba ya muda mrefu na iliyozuiliwa:
  • Tadelech amekuwa katika hatua ya kwanza ya leba kwa muda (upanuzi wa seviksi wa sentimita 8). Hata hivyo, anaweza kuwa katika hali ya muda mrefu ya awamu ya leba dhahiri. (Muda mrefu wa awamu ya kwanza ya leba ni wakati leba dhahiri inaendelea kwa zaidi ya saa 8 lakini haingii hatua ya pili.) Huja kuwa ukifuatilia leba yake hadi sasa. Hivyo huwezi kuwa na uhakika kama seviksi yake inapanuka polepole, au kama upanuzi umekoma kabisa na leba haijaendelea kabisa.
  • Uvimbe miwili juu na chini ya mbonyeo katika fumbatio yake huhitwa Bandl’s ring . Bandl’s ring inaonyesha leba iliyozuiliwa.
  • Kichwa cha mtoto kiko katika -3, haijaingia kwa pelvisi, na inabakia juu ya ukingo wa pelvisi. Hali hii inaonyesha kwamba hakishuki inavyotarajiwa kwa sababu Tadelech amekuwa kwa leba kwa siku mbili.

   Uke una moto na mkavu na edema ya valva ni ishara zaidi ya uwezekano wa iliyozuiliwa. (Edema ni uvimbe kutokana na ukusanyikaji wa maji katika tishu.)

 2. Ni wazi kwamba Tadelech anahitaji rufaa wa haraka kwenye kituo cha afya. Hatua zako ni:
  • Kuleza kwa upole yeye na familia yake kwamba ni lazima atumwe hospitali nyingine.
  • Anzisha maandalizi ya matayarisho ya kumrufaa kwenye kituo cha afya haraka iwezekanavyo. Mwenziwe wa kuzaa aende naye.
  • Dalili muhimu za Tadelech zinaonyesha kwamba yuko katika hali ya mshtuko: ana mpigo wa moyo wa kiwango cha juu na shinikizo la damu liko chini. Uke ulio na moto na mkavu inaonyesha upungufu wa maji mwilini. Mtibu mshtuko na upungufu wa maji mwilini na kumpa viowevu kwa njia ya mshipa (sehemu 9.4). Endelea kumpa viowevu katika safari ya kuelekea kituo cha juu cha afya.
  • Iliyozuiliwa inaweza kusababishwa na kibofu cha mkojo chenye kujaa zaidi na mwanamke hawezi kukojoa kwa njia ya kawaida. Tumia katheta kutoa mkojo.

Mwisho wa jibu

Maswali ya Kujitathmini 9.4 ( Maswali ya Kujitathmini Malengo ya Somo la 9.5)

Jinsi gani unavyoweza kupunguza hatari ya leba ya muda mrefu na iliyozuliwa kwa wanawake ambao wanazalia nyumbani?

Answer

Ili kupunguza hatari za leba iliyozuiliwa, fanya haya:

 • Fundisha umuhimu wa lishe bora utotoni. Lishe bora husaidia mifupa ya pelvisi ya wasichana kukua kwa kiwango cha kawaida kwa uzaaji ulio salama.
 • Kuza upangaji wa uzazi na kukatisha tamaa ya ndoa ya mapema na hasa mimba katika umri wa chini ya miaka 18.
 • Elezea kwamba lazima kuwe na huduma kutoka kwa mhudumu aliye na ujuzi wakati wote wa kuzaa kwa usalama wa mama na mtoto.
 • Saidia jamii yako kuandaa vikundi vya maandalizi ya kuzaa. Wakati wa dharura, wanaweza kusafirisha mama haraka kwenda kituo cha afya kilicho karibu.
 • Daima tumia patografu kwa kufuatilia maendeleo ya leba.

Mwisho wa jibu