9. Leba Iliyozuiliwa

Kipindi cha 9 Leba Iliyozuiliwa

Utangulizi

Leba iliyozuiliwa inaweza kukingwa. Moja wapo ya majukumu yako makuu kama mhudumu wa kuzalisha mwenye ujuzi ni kukinga leba iliyozuiliwa kwa wanawake katika jamii yako. Leba iliyozuiliwa hutokea zaidi katika maeneo ya vijiji vya Afrika, hasa miongoni mwa wanawake wanaokaa na leba nyumbani kwa muda mrefu.

Leba iliyozuiliwa inahusishwa na vifo wakati wa kuzaa na magonjwa. (Vifo wakati wa kuzaa ni vifo vya fetasi au mtoto mchanga. Ugojwa ni hali ya kuugua na ulemavu unaotokea wakati huo wa kuzaliwa. Leba iliyozuiliwa inachangia kati ya asilimia 10- 25 ya vifo vya kina mama Sahara ya Afrika. Kwa kweli, takwimu hii inayoshangaza ni kupuuza ya tatizo. Vifo vinavyosababishwa na leba iliyozuiliwa mara nyingi vinaainishwa chini ya matatizo mengine (kama vile sepsisi, kuvuja damu baada ya kuzaa, au uterasi iliyopasuka).

Katika Kipindi hiki, utajifunza kutambua dalili za kawaida za leba za muda mrefu na zilizozuiliwa. Utajifunza kutambua njia bora zaidi ya udhibitishaji. Udhibitishaji uliochelewa wa leba iliyozuiliwa mara nyingi husababisha nasuri kwa wanawake wanaoishi. Ikiwa fistula haitatibiwa, kina mama wanaweza kutengwa na jamii.

Malengo ya Kipindi cha 9