Skip to main content
Printable page generated Friday, 29 March 2024, 6:15 AM
Use 'Print preview' to check the number of pages and printer settings.
Print functionality varies between browsers.
Unless otherwise stated, copyright © 2024 The Open University, all rights reserved.
Printable page generated Friday, 29 March 2024, 6:15 AM

9. Kutoa Rufaa katika Kipindi cha baada ya Kuzaa

Kipindi cha 9 Kutoa Rufaa katika Kipindi cha baada ya Kuzaa

Utangulizi

Kufikia mwisho wa Moduli hii, utafahamu jinsi jukumu lako la kutoa utunzaji baada ya kuzaa lilivyo muhimu. Wahudumu wa Afya Nyanjani kama wewe huhamasisha kuhusu afya ya kina mama na watoto wachanga katika jamii zenu hivyo huokoa maisha. Utunzaji wa baada ya mtoto kuzaliwa ni kitengo cha utunzaji wa afya endelevu kwa kina mama na watoto.

Utunzaji endelevu huanza hata kabla ya mwanamke kutunga mimba, kisha kuendelea kupitia utunzaji katika ujauzito na ujuzi na usaidizi wa wakati wa leba na kuzaa. Utunzaji huu huibuka katika jukumu lako katika kipindi cha baada ya kuzaa. Bila shaka utunzaji huu endelevu hauishii hapo. Baadaye utasoma Moduli kuhusu Udhibiti Unganifu wa Maradhi ya WatotoWachanga na ya Utotoni ambapo utajifunza jinsi ya kukuza na kulinda afya ya watoto wachanga na wakubwa. Hivyo unafahamu kuwa utunzaji huu ni utaratibu unaoendelea wa kutoa usaidizi katika awamu zote tangu kuzaliwa kupitia utotoni, ikiwemo usaidizi kwa mama zao.

Kidokezo cha mwisho cha mafundisho kimebaki kusomwa katika Moduli hii – kutayarisha kiungo cha rufaa. Kujua jinsi ya kuwahamisha kina mama na watoto wachanga ili wapate huduma bora ya kimatibabu ni jambo muhimu sana na kujua wakati wa Kutoa rufaa. Jambo hili hufanyika ili kufanikisha huduma ya Utunzaji wa baada ya Kuzaa. Kugundua mapema hali zinazohatarisha maisha ni jambo muhimu, ingawa kufuatilia utambuzi na ufanisi wa rufaa wa mama na mtoto hadi katika kituo cha afya kwa matibabu zaidi ni muhimu vile vile.

Malengo Somo la Kipindi cha 9

Baada ya kukamilisha Kipindi hiki unatarajiwa:

9.1 Kufasili na kutumia kisahihi maneno yote ya kina yaliyoandikwa kwa herufi nzito.

9.2 Kufafanua kwa nini mpango mwafaka wa rufaa unafaa kuwa umeafikiwa kwa pande zote mbili, kati ya kituo cha afya na mhudumu wa afya ugani, kisha utoe mifano ya njia utakazotumia kuimarisha mpango huu. (Swali la Kujitathmini 9.1)

9.3 Kuelezea jinsi utakavyohakikisha kuwa rufaa itatendeka vizuri unavyohamisha wagonjwa mahututi, pia utoe sababu ambazo zinaweza kufanya rufaa ikose kudhibitiwa inavyostahili. (Swali la Kujitathmini 9.2)

9.4 Orodhesha habari zinazopaswa kuwekwa katika daftari ya rufaa iliyojazwa. (Swali la Kujitathmini 9.2)

9.1 Huduma mwafaka ya rufaa

Uwezekano wa kumfikisha mama mgonjwa au mtoto mchanga katika kituo bora cha afya kwa wakati unaofaa unaweza kubaini iwapo watakufa au wataishi. Rufaa itasaidia ikiwa:

  • Umeimarisha uhusiano mzuri na vituo vya afya unavyovitumia (na wahudumu wa afya vituoni), hivyo rufaa inaweza kutekelezwa haraka na kwa njia mwafaka.
  • Umehamasisha jamii kutafuta usaidizi wa kisaikolojia, kifedha na wa kiutendaji katika visa ambapo kina mama na watoto wachanga walio mahututi ni sharti wafikishwe kituoni kwa dharura.
  • Umemshawishi mama na familia yake kuamini pendekezo lako kabla ya jambo la dharura kutokea, ili wawe tayari kufuata maagizo yako ikiwa jambo la dharura litatokea.
  • Unatia juhudi katika kufuatilia na kuhakikisha kuwa mama na mtoto wamefika katika kituo cha afya. Njia ya kidesturi ya kumwambia mama au watoa huduma waende kituoni au kuwaandikia barua ya rufaa tu bila usaidizi zaidi kamwe si suluhisho tosha.

9.2 Kiungo cha rufaa: maafikiano ya pande mbili

Kiungo cha rufaa kati ya kituo kuu cha afya na wewe kama mhudumu wa afya ugani, ni maafikiano ya pande mbili (Kielelzo 9.1). Ili mfumo huu ufaulu kikamilifu, unapaswa kujua wahudumu wa afya katika kituo au hospitali iliyo karibu. Pia unapaswa kuwafahamu wahudumu wote walio katika vituo vya eneo hilo.

Kielelezo 9.1 Kiungo cha rufaa: maafikiano ya pande mbili
  • Je, unafikiri kuwajua wafanyikazi wa afya katika vituo vya afya vya viwango vya juu una umuhimu gani?

  • Sababu moja ni kuwa ni rahisi sana kuiandika barua ya rufaa yenye ufanisi kwa watu unaowajua kuliko usiowajua. Sababu nyingine ni kuwa wakikujua, wataamini uamuzi wako na utakapomtuma mama au mtoto kwa rufaa atapata huduma ya haraka.

    Mwisho wa jibu.

9.2.1 Kupokea majibu

Bila shaka, hili si jambo tu la kumpa mama au mtoto rufaa kwenda katika kituo cha afya. Kwa mfano, ukimpa rufaa mama aliye mgonjwa, mfanyikazi wa afya katika kituo hicho anafaa kukuandikia arifa inayokufahamisha kuwa ameruhusiwa kurudi kijijini. Wanapaswa kukueleza walichokifanya alipokuwa chini ya utunzaji wao na kukueleza jinsi ya kutibu matatizo yake ya kiafya katika siku zijazo. Hivyo, utaweza kuendelea kumhudumia mama na mtoto mchanga kwa njia bora ipasavyo.

9.2.2 Kufahamu kuhusu vituo vya afya katika eneo lako

Ili kufanikiwa katika kutoa rufaa unahitaji orodha ya hospitali na vituo vyote vya afya katika eneo lako na huduma wanazozitoa. Hii ni ili, kwa mfano, ukizaa mtoto mwenye uzani wa chini sana mara moja utajua kituo cha afya chenye uwezo mwafaka, vifaa na wafanyakazi waliohitimu kutoa huduma ya dharura kwa watoto walio wadogo sana. Ukiwa na habari hii, unaweza kumpa mama na mtoto rufaa kwa haraka.

  • Je, ni nini kinachoweza kutokea ikiwa huna habari kuhusu huduma zinazotolewa katika vituo vya afya vya kiwango cha juu?

  • Hatari kubwa iliyoko ni kumtuma mama au mtoto kwenye safari ngumu na ghali kuenda katika kituo cha afya kisichokuwa na huduma inayofaa. Hii inaweza kuwa hatari kwa sababu inamaanisha utapoteza wakati mwingi barabarani.

    Mwisho wa jibu.

Kwa muhtasari, ili kuwa na nafasi ya kupata matokeo bora, wafanyakazi wote wa afya katika jamii wanahitaji kujua jinsi ya kuwapa wagonjwa wao rufaa na hususani kituo kipi cha rufaa ili waweze kupata huduma inayofaa kukidhi mahitaji yao.

9.3 Je, ni nini kinachozuia rufaa kutolewa kikamilifu?

Kuna sababu nyingi za kutopata rufaa au rufaa hiyo kutotolewa kwa wakati unaofaa, ikiwa ni pamoja na:

  • Kutompa mama, baba na walezi wengine ushauri wa kutosha, ili waelewe uzito wa tatizo.
  • Umbali wa kituo cha afya na ukosefu wa usafiri.
  • Familia kukosa akiba ya pesa za usafiri.
  • Vituo vya afya havivutii baadhi ya wagonjwa. Mara nyingi, vituo hivi havina dawa muhimu na vifaa sahihi au havina wafanyikazi wenye ujuzi wa huduma zinazohitajika. Kwa sababu hiyo, wazazi wanaweza kusita kwenda katika vituo vya afya vyenye sifa mbaya.
  • Je, kuna chochote unachoweza kufanya kupunguza uwezekano wa kutofaulu kwa rufaa?

  • Rejela Kipindi cha 13 katika Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito na majadiliano kuhusu Utunzaji Mahususi wakati wa Ujauzito. Kumbuka kuwa kupangia utunzaji wa dharura ni sehemu maalum ya ushauri ambao ungekuwa umetoa kwa kila mama mjamzito na familia yake kabla ya kuzaa. Familia inapaswa kuwa imeweka akiba ya pesa za safari na kupangia usafirishaji.

    Mwisho wa jibu

Pamoja na ushauri wa wakati wa ujauzito uliowafanyia kina mama wajawazito na familia zao, pia unahamasisha jamii kuhusika katika kuisaidia familia katika kipindi cha baada ya kuzaa. Kipindi cha 1 cha moduli hii kilijadili jinsi ya kutoa ushauri na uhamasisho ifaavyo. Kumbuka kuwa ni katika hali ya dharura unapoweza kuona kazi yako katika jamii ikizaa matunda.

  • Fikiria kuhusu mfano wa jinsi unavyoweza kurejelea jamii kwa usaidizi ukipata jambo la dharura baada ya mama kuzaa.

  • Pengine umefikiria mifano mingi tofauti. Ufuatao ni mfano mmoja tu. Familia haina pesa ya ziada na hawana mpango wa usafirishaji.Utamshawishi mtu wa aliye na gari kumpeleka mama na mtoto mchanga katika kituo cha afya kwa sababu wako katika hali ya kufa au kupona. Kwa msingi wa ulivyohusisha jamii hapo awali, unaweza kupata makubaliano ya mapema kutoka kwa viongozi wa kijiji kuwa pesa zitatolewa katika hazina ya jamii kulipia usafirishaji ikiwa familia haiwezi kuimudu. Unawashukuru viongozi wa jamii kwa usaidizi wao na utambuzi kuwa hali za dharura zinaweza kushughulikiwa vyema mara nyingi katika kituo cha afya cha ngazi ya juu ikiwa wagonjwa watafika katika muda unaofaa.

    Mwisho wa jibu

9.4 Jinsi ya kufanikisha rufaa

Kuandika arifa ya rufaa na kuwaambia watu kuenda katika kituo cha afya siyo hoja. Kama vile tulivyojadili, tatizo kuu ni kuwafikisha katika kituo cha afya kinachofaa na kupata utunzaji mwafaka. Je, ni jambo gani lingine linalosaidia kufanikisha rufaa?

9.4.1 Utaratibu mwafaka wa kuweka stakabadhi

Wakati wa ujauzito, kila mama anafaa kushauriwa kujitayarisha kuzaa, ikiwemo hatua za kuchukua ikiwa matatizo ya dharura yatamkumba yeye au mtoto. Unafaa kuwa na kadi ya kutoa ushauri kutoka katika eneo lako ili kukuwezesha kumshawishi mama huyu na wahudumu wengine kukubali kumpeleka rufaa ikilazimu. Kwa maneno mengine, ukiwaambia kuwa mama huyu au mtoto wake anahitaji usaidizi na tiba maalumu kutoka kwa kituo cha afya cha kiwango cha juu, wanafaa kuwa tayari kuamini uamuzi wako na waende.

Pia unafaa kuwa na muundo uliotayarishwa vyema wa kuandikia kituo cha afya arifa za rufaa. Ulisoma jinsi ya kufanya haya katika Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito, Kipindi cha 13.

  • Arifa ya rufaa inapaswa kuwa na habari gani?

  • Arifa inapaswa kuwa na yafuatayo:

    • Tarehe na wakati wa rufaa
    • Jina la kituo cha afya ulichomtuma mgonjwa
    • Jina, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya kitambulisho (ikiwa inajulikana) na anwani ya mteja
    • Historia husika ya kiafya ya mgonjwa
    • Matokeo ya uchunguzi na ukaguzi wa kimwili
    • Makisio yako ya utambuzi wa ugonjwa
    • Matibabu yoyote uliyompa mteja
    • Sababu yako ya kumpa mteja rufaa
    • Jina lako, tarehe na sahihi
    • Anwani yako ili kituo cha afya kiweze kuwasiliana nawe siku za usoni

    Mwisho wa jibu

9.4.2 Usafirishaji na mpango wa dharura wa uhamishaji

Kwa kawaida, kila kijiji au jamii ina mfumo wao wa mpango wa dharura wa kuhamisha wagonjwa, ambao utaanza kufanya kazi mara moja haja inapotokea, kuna uwezekano wa kuhakikisha kuwa kuna usafirishaji uliotayari ili kuwezesha kina mama au watoto walio katika hali mahututi kufika katika kituo cha afya wakati ufaao.

  • Andika kwa haraka hatua mbili unazoweza kuchukua ukiwa na mama au mtoto anayehitaji kufikishwa katika kituo cha afya kupokea huduma maalumu.

  • Unaweza kuandika arifa ya rufaa na uwasaidie watu wa familia hiyo kupata pesa za kumsafirisha mama na mtoto hadi katika kituo cha afya kilicho karibu.

    Mwisho wa jibu

Ukishahakikisha kuwa mama na mtoto wamepata namna ya kusafiri, bainisha kama kuna usaidizi wa kutosha kwa watoto au watu wengine wa familia waliobaki nyumbani wakati mama na wahudumu wengine wameondoka.

Ikiwezekana, panga kuandamana na mama au mtoto mgonjwa hadi katika kituo cha afya.

Usipoweza hakikisha kwamba ameandamana na mtu mzima atakayewashughulikia kwa niaba yako. Kumbuka kumweleza mtu huyu kuwasiliana nawe mara tu atakaporudi kijijini, ili kujua kwamba mgonjwa alifika kituoni salama. Anaweza pia kukufahamisha jinsi mama au mtoto anavyotibiwa. Kama hajawasiliana nawe kwa siku moja au mbili, nenda nyumbani udhibitishe iwapo walirudi kutoka kituoni, na jinsi wanavyoendelea.

9.4.3 Kuhakikisha kuwa watu kituoni wanafahamu jinsi ya kuwasiliana nawe

Wahudumu wa afya wa vituo vilivyo karibu wanahitaji kuangalia na kufahamu majina ya vijiji na maafisa wanaoendeleza elimu ya afya (au wahudumu wengine wa afya) walio katika vituo vidogo vilivyo karibu na kituo cha afya. Hakikisha kuwa wana habari yote wanayohitaji hasa kuhusu mahali wanapoweza kukupata, na njia bora zaidi ya kuwasiliana nawe. Iwapo utapata kuwa hawajakupatia habari yote unayohitaji wakati wanakutumia mgonjwa tena, wasiliana nao na uwaulize majibu yaliyoandikwa pamoja na utambuzi, kile tayari wamekifanya na unachohitajika kufanya. Wavutie kwa utaalumu wako na uhakikishe kuwa wanakutambua kama mmoja wa wahudumu wa afya wa thamani katika jamii.

Kwa njia nyingine, ili mfumo mzima wa afya uwe na ufanisi, wahudumu katika vituo vya afya vya ngazi ya juu na wale walio katika jamii wanahitajika kufanya kazi kwa pamoja. Ikiwa juhudi za kila mmoja zitaratibiwa, kuna nafasi nzuri ya kufikia lengo kuu - kuokoa maisha ya kina mama na watoto wachanga.

Kisha hatimaye, kila mtu angependa kuona maendeleo ya uboreshaji wa mfumo mzima kwa huduma ya afya. Njia moja ya kufikia lengo hili ni kupitia ukaguzi wa utendakazi mara kwa mara. Kuleta pamoja kila anayehusika ili kujadiliana jinsi unaweza kuboresha uratibu wa shughuli zako ili kufanya uendeleshaji wa huduma kuwa na mafanikio kwa wote wanaohusika.

Muhtasari wa Kipindi cha 9

Katika Kipindi cha 9, umejifunza ya kwamba:

  1. Rufaa huhusisha njia mbili. Rufaa hutoka kwa wahudumu wa afya katika jamii hadi kituo cha afya cha ngazi ya juu, na pia kutoka kituoni hadi kwenye wahidumu. Pande zote mbili hutegemeana na kuhusiana kwa usawa kwa mafanikio ya huduma ya kijumla baada ya kuzaa.
  2. Kiungo cha rufaa kinapaswa kushirikisha majibu kutoka pande zote mbili kuhusu kilichotokea kwa mgonjwa (utambuzi, matibabu na masuala mengine ya kudhibiti afya), vile vile jinsi ya kufuatilia mgonjwa na kumsaidia baadaye.
  3. Kuwaambia watu watembelee kituo cha afya tu au kuandika arifa ya rufaa ni sehemu ndogo tu ya mchakato wa rufaa, na hatua hii inaweza kukosa ufanisi iwapo hapatakuwa na ufuatilizi na matayarisho mapema ya kina.
  4. Cha muhimu ni ujuzi wako wa kushauri kwa kushawishi na kuwaridhisha familia kuhusu umuhimu wa rufaa, na jukumu lako la kufanya kazi katika jamii kuzuia vikwazo ambavyo vinaweza kuzuia kina mama na watoto wachanga kufika kituo cha afya wakati unapohitajika.
  5. Kutambua uhusiano bora na utaratibu ulio na ufanisi kati ya wanajumuiya wote wa huduma ya afya ya kina mama na watoto wachanga ni muhimu kwa kufikia lengo la kuendeleza huduma. Hii huanza kutoka kaya, inakuhusisha kufanya kazi katika jamii, na huunganisha hadi vituo vya afya vya ngazi ya juu na vituo vya matibabu vilivyoendelea, kabla ya wagonjwa kurudia huduma yako na familia zao katika jamii.

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 9

Swali la kujitathmnini 9.1 (linatathmini Lengo la 9.1 na 9.2)

Andika maelezo mafupi ya maneno yafuatayo na ueleze umuhimu wao kwa njia utakavyotoa huduma baada ya kuzaa:

  • Uendelevu wa huduma ya kina mama na afya ya mtoto
  • Uhusiano wa rufaa
Answer

Uendelevu wa huduma ya afya kwa kina mama na ya mtoto ni njia ya kufikiri inayotukumbusha kwamba huduma baada ya kuzaa ni moja tu ya awamu ya ndani ya muktadha wa huduma yako ya kijumla ya watu katika jamii unakofanyia kazi. Hivyo basi ni kumbusho kuwa ushauri na huduma utakayotoa kabla ya ujauzito inaweza kuwa muhimu kama vile hatua za kuingililia au rufaa unazo fanya baada ya kuzaa, na kwamba huduma yako kwa mtoto itaendelea wakati wa utotoni. Kila hatua na awamu ni muhimu kama vile katika kila mmoja wa mwendeleo.

Uhusiano wa rufaa huchukuliwa kama njia mbiliu tofauti baina yako na kituo cha afya cha ngazi ya juu na pia kutoka kituo cha ngazi ya juu hadi kwako. Inapendekeza kuwa huduma nzuri ni wakati nyinyi wote wawili mnagawana na kubadilishana habari. Hufanya kazi vizuri wakati unaposhughulika kufahamu wahudumu wa afya katika kituo kilichoko eneo lako (nao pia wa kufahamu), na pia ufahamu barabara ni vifaa gani vinavyotoa aina za huduma za kiafya.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 9.2 (linatathmini Malengo ya Somo 9.3 na 9.4)

Unatoa rufaa ya mtoto mchanga aliyezaliwa kabla ya wakati na mama yake, ambaye tayari yuko na watoto watatu. Ikiwa unahofia sana kuhusu mtoto, andika orodha ya vitu vyote ambavyo unahitaji kukumbuka ufanye.

Answer

Orodha yako angalau inakaa kama ile iliyoko hapa chini, lakini pia inaweza kuwa na nyongeza zingine zaidi:

  • Hakikisha kwamba mama na mtoto wamefunikwa vizuri (rejelea pia sehemu za 8.5 na 8.6 za Kipindi cha 8)
  • Mweleze mama (na familia) kwamba ni muhimu kuwa yeye na mtoto waendee kwa kituo cha afya. Iwapo hawataki kwenda, wakumbushe kuhusu hali ya hatari kwa mtoto bila huduma ya mtaalamu.
  • Angalia ni kituo kipi cha afya kinachotoa huduma maalum kwa watoto waliozaliwa kabla ya wakati na uamue ni kipi (ikiwa hakuna chaguo) rahisi na ya haraka kufikia.
  • Angalia ikiwa familia inaweza kupanga usafiri, ikiwa hawawezi, mtume mmoja wao kwa kiongozi wa kijiji kuchunguza iwapo jamii inaweza kuwasaidia, pamoja na usaidizi wa kifedha ikilazimu (tazama Sehemu ya 9.3.2).
  • Ukisubiri chombo cha usafiri, andika barua ya rufaa (usipoweza kukumbuka orodha, tazama sehemu ya 9.3.1)
  • Hakikisha kuwa kuna jamaa wa familia ambaye atawaangalia watoto wakubwa.
  • Hakikisha kuwa hakuna jambo la dharura na huduma inayohitajika, ikiwa hakuna, andamana na mama na mtoto kwa kituo cha afya, au mtume mtu mzima.
  • Iwapo hutaenda, kumbuka kumweleza yule atakaye andamana nao akujulishe namna wanavyoendelea wakirudi.

Mwisho wa jibu