9. Kutoa Rufaa katika Kipindi cha baada ya Kuzaa

Kipindi cha 9 Kutoa Rufaa katika Kipindi cha baada ya Kuzaa

Utangulizi

Kufikia mwisho wa Moduli hii, utafahamu jinsi jukumu lako la kutoa utunzaji baada ya kuzaa lilivyo muhimu. Wahudumu wa Afya Nyanjani kama wewe huhamasisha kuhusu afya ya kina mama na watoto wachanga katika jamii zenu hivyo huokoa maisha. Utunzaji wa baada ya mtoto kuzaliwa ni kitengo cha utunzaji wa afya endelevu kwa kina mama na watoto.

Utunzaji endelevu huanza hata kabla ya mwanamke kutunga mimba, kisha kuendelea kupitia utunzaji katika ujauzito na ujuzi na usaidizi wa wakati wa leba na kuzaa. Utunzaji huu huibuka katika jukumu lako katika kipindi cha baada ya kuzaa. Bila shaka utunzaji huu endelevu hauishii hapo. Baadaye utasoma Moduli kuhusu Udhibiti Unganifu wa Maradhi ya WatotoWachanga na ya Utotoni ambapo utajifunza jinsi ya kukuza na kulinda afya ya watoto wachanga na wakubwa. Hivyo unafahamu kuwa utunzaji huu ni utaratibu unaoendelea wa kutoa usaidizi katika awamu zote tangu kuzaliwa kupitia utotoni, ikiwemo usaidizi kwa mama zao.

Kidokezo cha mwisho cha mafundisho kimebaki kusomwa katika Moduli hii – kutayarisha kiungo cha rufaa. Kujua jinsi ya kuwahamisha kina mama na watoto wachanga ili wapate huduma bora ya kimatibabu ni jambo muhimu sana na kujua wakati wa Kutoa rufaa. Jambo hili hufanyika ili kufanikisha huduma ya Utunzaji wa baada ya Kuzaa. Kugundua mapema hali zinazohatarisha maisha ni jambo muhimu, ingawa kufuatilia utambuzi na ufanisi wa rufaa wa mama na mtoto hadi katika kituo cha afya kwa matibabu zaidi ni muhimu vile vile.

Malengo Somo la Kipindi cha 9