1.6.2 Je, Kwa nini kushiriki kwa jamii ni muhimu sana?
Watu huwajibika wanapohusika na kushiriki katika shughuli fulani. Hii husaidia kwa kudumisha ari, shughuli na mipango. Pia ina manufaa haya:
- Kuongezeka kwa upatikanaji wa raslimali wanajamii wanapotoa kwa hiari wakati na raslimali zao kwa yale wanayoyachukulia kuwa ari na shughuli zao.
- Kuleta dhana ya umoja kati ya wanajamii.
- Kuongezeka kwa matumaini mafanikio ya matoleo yao yanapoonekana.
- Watu Kuwezeshwa kutumia ujuzi na talanta zao na kukuza uwezo wao.
- Mbadiliko wa mienendo kuwa haraka na rahisi.
- Urahisishaji wa uzuiaji wa asasi za kijamii zenye madhara.
Back to previous pagePrevious
1.6.1 Mbinu za kuhamasisha utendaji wa jamii