4. Maandalizi ya Utunzaji wa baada ya Kuzaa

Kipindi cha 4 Maandalizi ya Utunzaji wa baada ya Kuzaa

Utangulizi

Unafahamu kuhusu mambo haya kutoka kwenye moduli ya Utunzaji wa Wajawazito na Utunzaji katika Leba na Kuzaa

Mara nyingi, utaanza kujadiliana na mama na familia yake kabla hajazaa kuhusu jinsi atakavyojitunza baada ya kuzaa. Ni katika kuwazuru wajawazito ambapo utakusanya habari kuhusu mama, familia na hali zao za kijamii. Pia unaweza kuwapa anwani yako na uwaarifu kuhusu namna ya kukufikia wanapohitaji usaidizi wako. Wakati wa ujauzito, pia unawahimiza kina mama wote wazalie katika kituo kikuu cha afya, kama itawezekana, ingawa zaidi ya 94% ya wanawake wa mashinani mwa Afrika huzalia nyumbani. Katika kauli kama hizo, ishauri familia yake kukufahamisha punde leba inapoanza.

Ikiwa utakuwepo mwanamke akizaa, tayari unafahamu kwamba unapaswa kukaa naye kwa angalau saa 6 za kwanza baada ya kuzaa. Hata hivyo, ikiwa alizaa wakati hukuwepo, mtembelee haraka iwezekanavyo, hususan katika saa chache baada ya kuzaa, wala usichelewe hata kwa siku moja.

Kabla ya kumzuru mama kwa mara ya kwanza baada ya kuzaa, andaa vifaa na dawa unazohitaji ili kumpa huduma bora. Katika Kipindi hiki, utajifunza kuhusu vifaa, ratiba na malengo ya kumzuru mama baada ya kuzaa. Pia utajifunza kuhusu hatua za maandalizi muhimu yanayofanywa kabla ya kuondoka, na yale utakayofanya ukiwa nyumbani mwa mama.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 4