3.1 Kuvuja damu baada ya kuzaa

Vipindi vya 3 na 11 vya somo la Moduli ya Utunzaji wa Leba na Kuzaa vilielezea kwamba kutokwa na damu baada ya kuzaa inayohatarisha maisha hutokana na upotezaji wa angalau mililita 500 ya damu kutoka uterasi au ukeni. Kipindi hatari cha kupata uvujaji wa damu baada ya kuzaa ni katika vipindi vya tatu na nne vya leba.

  • Je, vipindi vya tatu na nne vya leba ni nini?

  • Kipindi cha tatu ni utoaji wa plasenta na tando za fetasi; kipindi cha nne ni masaa manne yanayofuatilia.

    Mwisho wa jibu

Mchoro 3.1 Uterasi inapaswa kujikaza vyema masaa 4-6 baada ya kuzaa.

Karibu vifo 90% inayosababishwa na utokaji wa damu hutokea kati ya masaa manne baada ya kuzaa. Katika masaa manne hadi sita ya kwanza, hakikisha kwamba uterasi imekazwa vyema (Mchoro 3.1) na hakuna upotezaji wa damu nyingi. Hata hivyo, mwanamke anaweza kutokwa na damu wakati wowote wa puperiamu, kwa kijumla katika wiki ya kwanza, lakini hata hadi wiki sita baada ya kuzaa. Aina hii ya kuvuja damu inajulikana kama hatua ya mwisho ya kutokwa na damu iliyochelewa baada ya kuzaa.

Kuwepo kwa anemia au hali ya moyo inaweza kuhatarisha maisha ya mama hata kama upungufu wa damu ni chini ya mililita 500. Kwa kawaida mwanamke ambaye ana utapiamlo hana uwezo wa kukabiliana na upotezaji wa damu kuliko mwanamke ambaye analishe bora.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 3

3.1.1 Visababishi vya kuvuja damu iliyochelewa baada ya kuzaa