3.2 Sepsisi inayosababishwa na uzazi na joto jingi mwilini

Sepsisi inayosababishwa na uzazi inahusu maambukizi yoyote ya bakteria ambayo huenea katika mfumo wa uzazi wa mwanamke baada ya kuzaa. Baadhi ya wanawake wako hatarini zaidi dhidi ya sepsisi inayosababishwa na uzazi, kwa mfano wanawake ambao wana anemia na/au wana utapiamlo. Joto jingi (joto lililo juu mwilini) kwa mama wakati wa kipindi cha baada ya kuzaa ni dalili hatari ya kijumla. Anahisi baridi kwa ghafla na kutetemeka, kufuatia kuhisi joto na kutokwa na jasho. Joto jingi mwilini baada ya kuzaa inaweza kuwa imesababishwa na sepsisi inayosababishwa na uzazi, lakini pia inaweza kusababishwa na:

Maambukizi haya yote yaliyoelezwa katika Moduli ya Magonjwa ya Kuambukizana.

  • Maambukizi kwa mfumo wa mkojo
  • Maambukizi kwa jeraha
  • Mastitisi au jipu kwa matiti
  • Maambukizi zisizohusiana na mimba au kuzaa, kama vile VVU, malaria, homa ya matumbo, pepopunda, meninjitisi, nimonia, na kadhalika

Katika hali nyingi, ili kuzuia maambukizi kwa mama baada ya kuzaa tekeleza uzalishaji kwa njia safi na iliyo salama, kuchanja wajawazito dhidi ya pepopunda, na kutoa matibabu kabla ya maambukizi. Katika maeneo ya endemiki ya malaria, usisahau kutoa vyandarua vilivyotibiwa na dawa ya kudumu ya kuua wadudu (Vyandarua vilivyotibiwa kukinga wadudu, Picha 3.3) wakati wa ziara yako ya nyumbani, ikiwa hawakupewa hapo awali. Pia washauri kina mama jinsi ya kuzitumia mara kwa mara kila wakati. Hakikisha kwamba mama na mtoto wake wanalala chini ya chandarua kila wakati.

Picha 3.3 Mama huyu amepewa chandarua kilichotibiwa watumie na mtoto wake wanapolala. (Picha: Hazina ya Dharura ya Watoto ya Umoja wa Mataifa)

3.1.2 Rufaa kabla ya kudhibiti uvujaji damu baada ya kuzaa

3.2.1 Endometritisi