3.2.3 Mastitisi ya pupera

Mchoro 3.5 Uchungu wa matiti inaweza kuwa dalili ya mastitisi.

Mastitisi ni inflamesheni yenye uchungu wa matiti kutokana na maambukizi ya bakteria (Mchoro 3.5). Bakteria ambayo mara nyingi husababisha mastitisi, au jipu iliokali zaidi, huitwa Staphylococcus aureus. Chanzo kikuu cha bakteria hizi ni mtoto ambaye ananyonya. Mastitisi huweza kuwa wakati wa kunyonyesha kuliko wakati matiti hayatoi maziwa. Mara nyingi hutokea wakati maziwa hubaki kwa matiti kwa muda mrefu (kutokamua yote) kwa sababu mtoto hanyonyi vizuri, au kutoka kwa mipasuko ya chuchu.

  • Je, chuchu iliyopasuka inawezaje kuwa hatari kwa mastitisi?

  • Maumivu kutokana na chuchu iliyopasuka inaweza kumfanya mama asitishe unyonyeshaji, hivyo maziwa mengi hubaki kwa matiti yake. Zaidi ya hayo, bakteria kutoka kwa mdomo wa mtoto au kutoka kwa ngozi ya mama zinaweza kuingia ndani ya matiti kupitia mipasuko ya chuchu.

    Mwisho wa jibu

Maambukizi ya matiti yasiyotunzwa, yenye upinzani, au yaliyorejea huweza kusababisha ukuaji wa jipu, mkusanyiko wa usaha ndani ya matiti. Usaha ni kiowevu kilichoshikana cha rangi ya manjano-nyeupe katika tishu iliyoambukizwa na ina bakteria, seli nyeupe za damu, mabaki yaliyoundwa na seli, na tishu zinazokufa. Wanawake walio na mastitisi mara kwa mara hupata maumivu, joto jingi mwilini, kuhisi baridi, na maumivu ya misuli mwili mzima. Titi huonekana nyekundu, lenye joto, na lina uchungu mno likiguswa. Wakati uchunguzi unaonyesha mkusanyiko mgumu uliofunikwa na uwekundu, maumivu unapoguswa, kuna uwezekano kuwa titi lina jipu.

Iwapo utatekeleza utambuzi wa mastitisi au jipu la titi, dhibiti uchungu kwa kutumia paracetamol, ukishikilia matiti na sidilia au kitu chochote kinachoweza kufungwa kwa kifua. Pia rufaa mwanamke kwa kituo cha afya na/au hospitali iliyoko karibu kwa matibabu ya antibiotiki.

Rufaa mwanamke aliye na mastitisi au jipu kwa matiti.

Utakapomshauri mwanamke aliye na maambukizi kwa matiti, usimshauri KAMWE awache kumnyonyesha mtoto kwa matiti yaliyo ambukizwa. Kuruhusu mtoto kunyonya husaidia kupunguza tatizo na maumivu. Hivyo, mshawishi anyonyeshe ila tu usaha unatoka kutoka kwa chuchu. Hata hivyo, kunyonyesha hairuhusiwi ikiwa sababu ya maambukizi inashukiwa kuwa ni kifua kikuu, ambayo inahusishwa na ushahidi wa maradhi ya muda mrefu na kupona (kovu) na maambukizi mapya katika titi hilo.

3.2.2 Maambukizi kwa mfumo wa mkojo

3.2.4 Maambukizi kwa kidonda