3.2.4 Maambukizi kwa kidonda

Maambukizi kwa kidonda wakati wa puperiamu kwa kawaida uathiri tishu ya msamba iliyokatika, maambukizi kwa episiotomi (mkato wenyewe hutekelezwa ili kuongeza uwazi wa uke ili mtoto aweze kupitia), au kidonda kufuatia upasuaji kwa fumbatio baada ya kuzaa kwa njia upasuaji inayotekelezwa kwa kituo cha afya.

Kwa ujumla, maambukizi kwa kidonda huwa wazi katika siku ya tatu au ya nne baada ya kuzaa na utambuliwa kwa erithema (wekundu katika eneo lililoambukizwa), na ugumu wa tishu iliyo juu ya eneo lililoathirika, ambayo hupata joto na huwa chungu inapoguswa. Usaha wa rangi ya manjano unaweza kutiririka kutoka kwa kidonda, na mama anaweza pia kuwa na joto jingi mwilini.

Mchoro 3.6 Kidonda kilichoambukizwa kwa msamba kinaweza kutibiwa kwa kuosha na maji vuguvugu yaliyo na chumvi, au kufinywa ili kutoa usaha.

Matibabu ya kidonda kwa msamba kilicho na maambukizi ni pamoja na kuondoa maumivu na paracetamol na kuosha eneo hilo na maji vuguvugu ambayo yametiwa chumvi kijiko kimoja katika kila lita ya maji. Kama kuna usaha kutoka kwa kidonda kwenye msamba, utoe kwa kufinya eneo hilo na kitambaa kilichowekwa katika maji vuguvugu yenye chumvi (Mchoro 3.6).

Ikiwa mama pia ana joto jingi mwilini na anahisi baridi, na unadhani kuna usaha ambayo haitoki nje ya kidonda, rufaa kwa kituo cha afya cha gazi ya juu ili aweze kutibiwa na antibiotiki. Ikiwa ana jipu, inaweza kutolewa kwa njia ya upasuaji. Wengi hupona haraka wakati usaha inatolewa kwa njia ya upasuaji na kutumia antibiotiki. Kwa kijumla antibiotiki hutumika hadi wakati mama hana joto jingi mwilini kwa masaa 24-48. Maambukizi ya kidonda kwenye fumbatio kwa kijumla hutibiwa katika hospitali, hivyo rufaa kina mama kwenye kituo cha afya cha gazi ya juu.

3.2.3 Mastitisi ya pupera

3.3 Uchunguzi wa shinikizo la juu la damu baada ya kuzaa