3.5.1 Kununa na masumbuko baada ya kuzaa

Mchoro 3.7 Usaidizi unaweza kuwasaidia kina mama kupata nafuu kutokana na ‘kununa’ baada ya kuzaa.

Mabadiliko ya homoni hudhaniwa kuwa ndio hushababisha ‘kununa’ baada ya kuzaa, hali isiyo kali, ya muda, inayoisha yenyewe, ambayo kawaida hutokea siku chache baada ya kuzaa na huchukua hadi wiki mbili. Dalili zake kuu ni kuwepo kwa huzuni mara kwa mara, kulia, wasiwasi, kukasirika, kutotulia, kugeuza sununu mara kwa mara, maumivu ya kichwa, kuchanganyikiwa, usahaulifu, na kukosa usingizi. Ni nadra kuathari vikubwa uwezo wa mama wa kufanya kazi au kuhudumia mtoto wake. Kutoa usaidizi wa upendo, huduma, na elimu imeonekana kuwa na mafanikio kwa uponaji wa mama (Picha 3.7).

Rufaa kina mama walio na masumbuko makali baada ya kuzaa.

Iwapo mama anapata masumbuko makali baada ya kuzaa (maendeleo ya huzuni, sununu iliyo chini, kukosa motisha ya kufanya chochote), itaathiri vikubwa uwezo wake wa kukamilisha shughuli za kawaida zinazohusiana na maisha ya kila siku. Hali za masumbuko huhitaji huduma muhimu na mama kutiwa moyo na wataalamu walio na mafunzo ya kiafya ya akili, hivyo rufaa mama haraka uwezavyo. Familia ya mama pia ni muhimu sana wakati wa matibabu. Kina mama wenye masumbuko makali wanaweza kukosa kunyonyesha mara tu baada ya kuzaa, na watoto wao wana uwezekano zaidi wa kuwa na matukio ya ugonjwa, kama vile kuhara.

  • Unaweza kueleza ni kwa nini mtoto anaweza kuathiriwa kwa njia hii?

  • Iwapo unyonyeshaji haitanzishwa, mama anaweza kumlisha mtoto na maziwa ya kutengeneza kwa kutumia chupa, ambayo huwa na hatari kubwa ya maambukizi kwa mtoto kutoka kwa chupa chafu. Mama aliye na masumbuko anaweza pia kukosa kuelewa maelezo ya ujumbe wa elimu ya afya juu ya namna ya kuzuia maambukizi kwa mtoto mchanga.

    Mwisho wa jibu

Rufaa mama, ikiwa dalili mbili au zaidi ya zifuatazo zitatokea katika wiki mbili za kwanza ya puperiamu:

  • Hali ya kujihisi mwenye hatia bila sababu au kujidharau
  • Kulia kwa urahisi
  • Kupungua kwa hamu au raha
  • Anahisi kuchoka, wasiwasi, na kukasirika wakati wote
  • Matatizo ya usingizi, kulala sana au kidogo sana
  • Kupungua kwa uwezo wa kufikiria au kumakinika kwa jambo
  • Kukosa hamu ya kula

Kunaweza pia kuwa na matukio ya kichaa baada ya kuzaa, inayoonekana kwa kudanganya au ndoto-kuona au kuamini mambo yasiyo kweli. Tutarejelea tatizo hili kali zaidi katika Kipindi cha 5 cha Somo. Utajifunza mengi zaidi kuhusu masuala ya afya ya akili, ikiwa ni pamoja na masumbuko na kichaa baada ya kuzaa, katika Moduli ya Magonjwa yasiyo ambukizi, Utunzaji wa Dharura, na Afya ya Akili.

3.5 Matatizo ya Akilini baada ya kuzaa

Muhtasari wa Kipindi cha 3