4.1 Ziara za nyumbani: fursa nzuri ya kutoa utunzaji wa baada ya kuzaa

Njia bora ya kutoa huduma ya mama na mtoto ni inapotolewa katika kituo cha afya na mhudumu wa afya aliyehitimu. Hata hivyo, barani Afrika mna changamoto nyingi zinazozuia kulitimiza lengo hili, kama vile uhaba wa vituo, wahudumu wa afya waliohitimu, na pia ugumu wa kufikia vituo vya afya kwa watu wa vijijini.

Inaweza kuchukua miaka mingi kutatua changamoto hizi. Kwa hivyo, unapoendelea kufanya juhudi ili kuboresha mfumo wa afya na ufikikaji katika vituo vya afya humo mashinani, jukumu lako sasa kama Mhudhumu wa Afya Ugani ni kulenga ziara za nyumbani ili kutoa huduma ya utunzaji wa baada ya kuzaa.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 4

4.1.1 Changamoto za utunzaji wa baada ya kuzaa unaofanyiwa kituoni