4.1.1 Changamoto za utunzaji wa baada ya kuzaa unaofanyiwa kituoni

Kabla ya kuanzisha huduma ya utunzaji wa baada ya kuzaa katika jamii yako, kwanza unapaswa kufahamu kuhusu changamoto zake. Pia unapaswa kuelewa kwa kina sababu zinazofanya ziara za nyumbani kubakia kama njia kuu za kutoa huduma ya utunzaji mle mashinani. Changamoto kuu zinazozuia utunzaji wa baada ya kuzaa unaofanyiwa kituoni ni:

Mchoro 4.1: Umbali wa kituo ni changamoto kuu kwa wanawake wanaotaka utunzaji wa baada ya kuzaa.
  • Changamoto za kijamii na kimila: tambiko na tamaduni za jamii kama vile kumfungia mama na Kipindi nyumbani kwa siku chache baada ya kuzaa, katika kipindi cha kutengwa huwazuia kina mama kutembelea kituo kupata huduma. Unapaswa kuchunguza changamoto hizi pole pole katika eneo lako ukishirikiana na viongozi wa jamii ili kubadilisha desturi hizi.
  • Changamoto za kijiografia: kupanda milima, kuvuka mito isiyo na madaraja katika msimu wa mvua na ukosefu wa barabara ni baadhi ya changomoto za kijiografia zinazowazuia wanawake kukifika kituo ili kuhudumiwa. (Mchoro 4.1).
  • Umbali wa kituo: Hata ingawa baadhi ya wanawake wangependelea kwenda kituoni au hospitalini, kituo kilicho karibu hakifikiki kwa mguu au kwa kutumia chombo cha usafiri kilichoko.
  • Changamoto za kifedha. Katika sehemu fulani za afrika, watu huamini kuwa huduma za afya zinazohusu leba, uzazi na utunzaji baada ya kuzaa hutolewa bila malipo. Ukweli ni kwamba ni sharti familia igharamie nauli ili mama afike kituoni, na pia ilipie vifaa vinavyotumika kama vile dawa na glavu. Gharama hii ya ziada ni changamoto kuu kwa huduma ya baada ya kuzaa inaayotolewa kituoni.
  • Changamoto za ubora wa huduma: Wanapofika kituoni, mama na mtoto Kipindi wanaweza kukosa huduma bora walizotarajia kwa sababu za ukosefu wa wahudumu wa afya waliohitimu vyema au upungufu wa vifaa au dawa. Huduma duni hupunguza imani ya baadhi ya wanawake, hivyo wanaweza kupunguza juhudi zao za kufikia kituoni.
  • Lengo la pili muhimu la ziara ya nyumbani ili kutoa huduma za utunzaji baada ya kuzaa ni kutafiti baadhi ya changamoto za kijamii na kimila zilizotajwa hapo juu, kisha uungane na viongozi wa jamii kujaribu kuzibadilisha. Kipindi cha 1 cha moduli hii kilieleza njia nyingi unazoweza kutumia ili kufanya hivi. Kwa kurejelea maswala hayo, andika ratiba fupi ya hatua utakazojaribu kufanya.

  • Kuna hatua nyingi ambazo huenda ulijumuisha. Rejelea Kipindi cha 1, Kifungu cha 1.6, na ulinganishe majibu yako na maoni yaliyoko.

4.1 Ziara za nyumbani: fursa nzuri ya kutoa utunzaji wa baada ya kuzaa

4.1.2 Ushahidi unaoonyesha kuwa ziara ya nyumbani huimarisha ubora wa utunzaji wa baada ya kuzaa