4.1.2 Ushahidi unaoonyesha kuwa ziara ya nyumbani huimarisha ubora wa utunzaji wa baada ya kuzaa
Kinachosikitisha ni kuwa hakuna utafiti wa kutosha kuhusu ziara ya nyumbani katika bara la Afrika ili kuwa kielelezo kinachoweza kuigwa katika kila eneo. Hata hivyo, kuna ushahidi na mifano kutoka Asia Kusini inayoonyesha matokeo muhimu katika kuimarisha utunzaji baada ya kuzaa na kupunguza kima cha vifo vya kina mama na watoto wachanga kwa kipindi kifupi kupitia mtazamo wa ziara ya nyumbani. Bila shaka, kuna tofauti za kimila katika nchi mbalimbali, ingawa matokeo yanatia moyo. Kwa mfano, utafiti uliofanywa nchini India, Bangladesh na Pakistan umeonyesha kuwa ziara za nyumbani zinaweza kupunguza vifo vya watoto wachanga kwa 30-61% katika nchi zinazostawi, ambapo vifo vingi hutokea. Ziara za nyumbani hasa huimarisha utimizaji wa maswala ya watoto wachanga yenye umuhimu mkuu na yenye gharama ya chini.
Maswala haya ni kama:
- Kuanza kumnyonyesha mtoto mapema.
- Kuguzana kwa ngozi ya mama na ya mtoto (Mchoro 4.2).
- Kuchelewesha kumuosha mtoto Kipindi hadi angalau saa 24 baada ya kuzaliwa.
- Kusisitiza kanuni za usafi, kama vile kunawa mikono kwa sabuni na maji safi.
- Kuzingatia usafi wa kitovu cha mtoto.

Tutarejelea maswala hayo baadaye katika Kipindi hiki, au baadaye katika moduli hii. Ingawa hatuna utafiti unaotoka Afrika ili kulinganisha, utafiti huu kutoka Asia Kusini unaonyesha vipengele vikuu vinavyohitajika ili kutoa huduma mwafaka ya utunzaji wa mtoto na mama nyumbani.
4.1.1 Changamoto za utunzaji wa baada ya kuzaa unaofanyiwa kituoni
