4.2 Ratiba ya ziara za nyumbani kutekeleza utunzaji wa mtoto na mama baada ya kuzaa

Kwa sasa kuna ushahidi wa na maafikiano ya kutosha kuhusu vipengele vya kimsingi vya utunzaji wa baada ya kuzaa, ili kuimarisha afya na uhai wa kina mama na watoto wachanga. Hata hivyo, bado ni vigumu kupata mapendekezo yanayozingatia utafiti ambayo yanaweza kutumiwa kama kipimo kwa kiwango cha nyakati na marudio ya ziara za nyumbani. Mataifa mbali mbali ya Asia Kusini yameona nyakati tofauti za kufanya ziara, lakini yote yalitambua kuwa kina mama walitembelewa angalau mara 2 – 3 katika wiki ya kwanza baada ya kuzaa. Katika kauli zote, ziara ya kwanza ilikuwa katika saa 24 baada ya mtoto kuzaliwa.

Kama ulivyojifunza katika Kipindi cha 1 cha Moduli hii, saa 24 na siku saba za kwanza baada ya kuzaa ni muhimu ambapo kina mama na watoto wachanga mara nyingi hufa. Kulingana na habari zilizoko ambazo zinatokana na matukio ya nchi zingine, na uwezekano wa kutekeleza kila kauli katika bara Afrika, Shirika la Afya Duniani limependekeza ratiba ya ziara ya nyumbani ili kutoa huduma ya baada ya kuzaa. Kwa wanawake wasiokumbwa na matatizo, na walizaa mtoto aliyepevuka na mwenye uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa, ziara ya nyumbani imependekezwa ifanywe kama ifuatavyo:

  1. Ziara ya kwanza inapaswa kufanyika katika saa 24 za kwanza. Ikiwa inawezekana, mzuru mama haraka iwezekanavyo.
  2. Ziara ya pili iwe siku ya tatu baada ya mama kuzaa.
  3. Ziara ya tatu iwe siku ya saba baada ya mama kuzaa.
  4. Ziara ya nne ni katika wiki ya sita baada ya mama kuzaa.

Moduli inayohusu Udhibiti unaojumuisha Maradhi ya Utotoni na ya Watoto wachanga itakufunza kwa kina kuhusu ziara hizi za ziada za nyumbani.

Ziara nyongeza huitajika katika siku ya tano na ya kumi baada ya kuzaa, hasa katika hali spesheli kama vile katika:

  • Watoto waliozaliwa kabla ya wakati (wale waliozaliwa kabla ya wiki 37 ya ujauzito)
  • Watoto waliozaliwa na uzito wa chini (wenye uzani wa chini ya kilogramu 2.5)
  • Watoto na kina mama wote wagonjwa.
  • Kina mama wanaoishi na VVU.

Watu wa familia pia wanapaswa kuomba uende haraka ikiwa mtoto au mama ana tatizo wakati wowote baada ya kuzaa. Watu wa familia zingine wanaweza kusita kukuhusisha, hivyo basi, ni muhimu kwako kila wakati kumuhakikishia kila mmoja kuwa ni bora kukuarifu ikiwa wanatilia shaka afya ya mama au mtoto.

4.1.2 Ushahidi unaoonyesha kuwa ziara ya nyumbani huimarisha ubora wa utunzaji wa baada ya kuzaa

4.3 Maandalizi ya ziara ya nyumbani