4.3 Maandalizi ya ziara ya nyumbani

4.3.1 Usafi wa kibinafsi

Mchoro 4.3 Wajihi wako unafaa kumhimiza mama akuamini katika usatadi wako.

Kabla ya kuanza ziara, hakikisha umeshughulikia usafi wako binafsi, hususan kwa kuzingatia nywele, kucha na nguo zako. Maagizo haya yanaweza kuwa rahisi na ya kimsingi, lakini wajihi na usafi duni unaweza kuathiri vibaya uusiano wako na jamii na familia, na pia kuaminika kwa kazi yako. Vaa nguo za kawaida. Lakini zilizo safi unapokuwa ziarani kupeana huduma ya utunzaji baada ya kuzaa. (Mchoro 4.3)

  • Ni sababu gani nyengine inayofanya iwe muhimu kusisitiza usafi? Rejelea uliyojifunza katika baadhi ya vikao vya mbeleni katika moduli hii.

  • Kutilia maanani usafi na unadhifu wakati mama anapozaa na katika ziara za kutoa huduma ya utunzaji wa baada ya kuzaa husadia kuzuia maambukizi baada ya mtoto kuzaliwa. Ukizingatia usafi wako binafsi, itakuwa rahisi kumshawishi mama na familia yake kuhusu umuhimu wa usafi iwapo atazalia nyumbani katika siku zijazo.

4.2 Ratiba ya ziara za nyumbani kutekeleza utunzaji wa mtoto na mama baada ya kuzaa