4.4 Hatua kuu za kufuata unapomzuru mama nyumbani

Ili kuleta hali ya kumjali mama na kuifanya familia yake ikwamini, unapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:

  • Fahamu na udhiirishe kuwa unaheshimu imani, mila na desturi zao mnapozungumza.
  • Mwamkue kila mmoja ukitumia maneno yanayofahamika kwao.
  • Eleza sababu za ziara hiyo kwa mama na familia, ukitumia maneno ya lugha yao yanayoeleweka.
  • Tenga nafasi kubwa ya mazungumzo ya kijumla na kuleta imani baina yenu.
  • Onyesha ujasiri katika mazungumzo yako kwa kutumia sauti ya upole, na pia kuteleka wajibuwako kwa ujasiri.
  • Mheshimu kila mtu katika familia.

Ulizia kuhusu hali ya mama na mtoto na ukadirie kama kila mmoja wao ana tatizo lolote la kiafya, au kama kuna ugumu wa kukaribisha ‘mtoto mgeni’ katika familia. Tumia mtazamo wa kuchunguza uliokubalika: uliza, chunguza, orodhesha na uchukue hatua. Jambo muhimu zaidi ni kutumia kadi za uchunguzi ili kukusaidia kubaini hali yoyote inayohatarisha maisha au dalili zozote hatari kwa kina mama na watoto wachanga. Tayari umejifunza namna ya kufanya hivi katika Kipindi cha 1 na 3.

Ukitumia kadi za ushauri, mshauri mama kuhusu afya yake na hali na afya ya mtoto. Kila wakati, kadiria baadaye kama alielewa ushauri huo. (Rejelea kifungu Kifungu cha 4.5 hapa chini).

Jaza fomu ya ziara ya nyumbani na upangie siku ya ziara nyingine. Mshukuru kila mmoja kwa kukukaribisha nyumbani.

4.5 Kuwashauri kina mama katika kipindi cha baada ya kuzaa