4.5 Kuwashauri kina mama katika kipindi cha baada ya kuzaa

Ili kutimiza matarajio ya ushauri kwa mama kuhusu kipindi cha baada ya kuzaa kwa kuwazuru nyumbani, unapaswa kutumia kadi za ushauri zinazotolewa katika Shirika la Afya Mkoani. Unapowashauri kina mama, ni muhimu kutumia hatua za kiustadi zifuatazo:

  • Uliza na usikilize: Peleleza yale ambayo mama tayari anajifanyia mwenyewe, na mtoto wake kwa kumuuliza maswali yanayohusisha kufikiria, na uyasikilize kwa makini majibu yake. Hivyo, utafahamu yale mambo anayofanya kwa usahihi, na yale yanayohitaji kubadilishwa.
  • Msifu: Msifu mama kwa chochote cha dhamani alichokifanya. Kuna uwezekano kuwa kuna mambo ya dhamani kwake na kwa mtoto ambayo amefanya. Kwa mfano, anaweza kuwa anakula chakula bora, anamnyonyesha mtoto bila kumpa vyakula vya ziada, na kuzingatia usafi wake na wa mtoto. Hakikisha kuwa umemsifu bila unafiki, na kuwa umemsifu kwa mambo yatakayomfaidi yeye na mtoto wake kiafya.
  • Mshauri: Mshauri tu kuhusu mambo yaliyo muhimu kwake wakati huo pekee. Mawaidha mengi, au yanayotolewa wakati usiofaa yanaweza kumkanganya, hivyo anaweza kuyafutilia mbali. Tumia lugha anayoielewa. Ikiwezekana, tumia picha, kadi za uchunguzi, au vielelezo ili kumwelezea bayana yale anayohitajika kufanya, kufahamu au kuelewa.
Mchoro 4.4 Peleleza kwa umakini ili kubaini kama mama ameelewa ujumbe wako wa kiafya
  • Peleleza kama ameelewa: Ukimwelezea mama chochote, mwulize maswali ili kubaini anachoelewa na anachohitaji afafanuliwe zaidi (Mchoro 4.4). Usimwulize maswali elekezi (yaani, maswali yanayomwashiria jibu sahihi hata ikiwa haelewi). Pia usiulize maswali yanayojibiwa kwa ndio au la, kwa sababu hayasaidii kubaini kwa kina kile ambacho mama ameelewa.

Maswala muhimu ya kiafya unayopaswa kuzingatia unamposhauri mama baada ya kuzaa ukiwa katika ziara ya nyumbani yameonyeshwa katika Kisanduku 4.2.

Kisanduku 4.2 Maswala ya kiafya unayofaa kuzingatia unapomshauri mama

  • Kubaini dalili za kijumla za hatari
  • Usaidizi wa kihisia
  • Usaidizi wa lishe kwa mama
  • Kuimarisha kipeo cha kunyonyesha
  • Usafi na udhibiti maambukizi
  • Usaidizi wa upangaji uzazi
  • Huduma spesheli kwa kina mama walioambukizwa VVU
  • Mama na mtoto Kipindi kutafuta matibabu wakati unaofaa ikiwa matatizo yatatokea
  • Utunzaji wa kila mara kwa mtoto mwenye hali ya kawaida ya afya

Utajifunza zaidi kuhusu maswala haya katika vikao vijavyo vya moduli hii.

  • Ni mara ya pili umemtembelea mama aliyezalia nyumbani. Anakufahamisha kuwa mtoto wake analia sana, na alilala kwa muda mfupi na anajihisi kama ambaye amefura na mchovu sana. Je, utafanya nini?

  • Ni wazi kwamba unafaa umchunguze zaidi. Je, mama anaona shida kumlisha mtoto - anaweza kuwa na mastitisi? Je, mama na mtoto wanaweza kuwa na maambukizi fiche, kama vile matatizo kwenye kitovu cha mtoto ama maambukizi ya kindonda katika msamba wa mama? Je, mama anapata lishe bora analohitaji, na familia na jamii yake wanamasidia? Ikiwa maswali ya kwanza (na ikiwezekana uchunguzi) yanakuridhishia kwamba hakuna jambo la hatari kubwa, basi unaweza kumshauri ifaavyo. Ikiwa unafikiria ana matatizo, basi mpe rufaa.

    Mwisho wa jibu

4.4 Hatua kuu za kufuata unapomzuru mama nyumbani

Muhtasari wa Kipindi cha 4