Muhtasari wa Kipindi cha 4

  1. Changamoto kuu katika utoaji huduma za Utunzaji wa baada ya Kuzaa katika vituo vya afya ni changamoto za kijamii, kitamaduni, kimaumbile, kijografia, kidhamani na kifedha. Mtazamo wa kuwatembelea wateja nyumbani ndio unaotumika kushughulikia matatizo haya ifaavyo katika jamii za mashinani.
  2. Utaratibu wa kutoa huduma za Utunzaji wa baada ya Kuzaa za kuwatembelea nyumbani wanawake wasio na matatizo na watoto wachanga ni: ziara ya kwanza katika saa za 24 kwanza baada ya kujifungua, kisha umtembelee tena siku ya tatu, ya saba na wiki ya sita.
  3. Ni sharti pia uwatembelee siku ya tano na ya kumi kina mama wote wagonjwa na watoto wachanga, kina mama walioambukizwa virusi vya UKIMWI, watoto wenye uzito wa chini na waliozaliwa kabla ya wakati.
  4. Unapomtembelea mteja nyumbani kwa huduma za Utunzaji wa baada ya Kuzaa, hakikisha kuwa umevaa mavasi ya kadri lakini yaliyo safi, nawe uzingatie usafi mwenyewe.
  5. Usisahau kubeba vifaa na dawa muhimu zinazohitajika wakati wa kutoa huduma za Utunzaji wa baada ya Kuzaa.
  6. Waheshimu watu wote nyumbani. Kuwa na ujasiri na uwasiliane vyema kwa lugha na istilahi zinazoeleweka.
  7. Tumia kadi na fomu zilizoko ili kuhakikisha umeshughulikia vipengee vyote vya uchunguzi na ushauri, hasa kutambua dalili hatari kwa mama na mtoto Kipindi.
  8. Unapomshauri mama unafaa kumuuliza na kumsikiliza, uzisifu hatua bora alizochukua, umpe ushauri anaohitaji kujua kwa wakati huo pekee, na upeleleze kama ameelewa ushauri huo.

4.5 Kuwashauri kina mama katika kipindi cha baada ya kuzaa

Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 4