Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 4

Sasa kwa kuwa umemaliza Kipindi hiki, jibu maswali haya ili kukadiria uliyojifunza. Swali la Kujitathmini 4.1(litathmini Malengo ya Somo la 4.1 na 4.3)

Unapangia utunzaji baada ya kuzaa kwa mama aliyezaa kabla ya wakati, na mtoto yuko na uzito wa chini ya kawaida. Eleza uainishaji huu, kisha uweke ratiba yako ya utunzaji ukieleza jinsi gani (na kwa nini) ratiba hii ya utunzaji inatofautiana na ile ya mtoto mwenye uzito wa kawaida, aliyezaliwa wakati ufaao.

Answer

Mtoto aliyezaliwa kabla ya wakati ni -aliyezaliwa kabla ya wiki ya 37 ya ujauzito. Mtoto mwenye uzito wa chini ya kawaida ni aliye na uzito wa chini ya gramu 2500. Kwa kawaida, tukichukulia kuwa huyu mtoto alizaliwa kabla ya wakati, unatumai kuwa jamii ingekuharifu mapema ili uwepo mtoto anapozaliwa. La si hivyo, basi unafaa kufika hapo haraka iwezekanavyo katika saa 24 za kwanza baada ya mtoto kuzaliwa. Baadaye, utahitaji kupanga jinsi utawatembelea siku ya tatu, tano, saba na ya kumi, halafu katika wiki ya sita baada ya kuzaa. Ziara za siku ya sita na ya kumi ni za ziada ukilinganisha na ratiba unayoweza kumpangia mtoto aliyezaliwa wakati ufaao. Hii ni ishara ya hatari kubwa ya vipindi vya mwanzo vya utotoni (siku saba za kwanza) ikiwa mtoto amezaliwa kabla ya wakati ama yuko na uzito mdogo.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 4.2 (linatathmini Malengo ya Somo la 4.2)

Ingetarajiwa kuwa kina mama wote barani Afrika wangepata huduma za hali ya juu katika vituo vya afya. Ni sababu gani kuu zinazopelekea hali hii isitimilike kwa sasa, na ni kwa nini ziara za nyumbani ni muhimu sana?

Answer

Changamoto kuu za huduma ya baada ya kuzaa katika vituo vya afya zimeorodheshwa katika Kifungu cha 4.1.1. Linganisha majibu yako na vidokezo vilivyoorodheshwa hapo. Je, ulifikiri kuhusu changamoto zingine, labda kutokana na matukio uliyoshuhudia mwenyewe? Ikiwa ni hivyo, basi ni vyema.

Kuwazuru kina mama nyumbani katika kipindi cha baada ya kuzaa ni muhimu kwa sababu ziara hizi huchangia pakubwa katika kuendelea kuishi kwa watoto wachanga kwa kijumla. Utafiti wa ule mfano wa Asia Kusini unaonyesha upungufu wa visa vya vifo vya kina mama kwa kati ya 30% na 61% kwa sababu ya ziara za nyumbani. Hatua mbali mbali zimeorodheshwa katika Kifungu cha 4.1.2.

Mwisho wa jibu

Maswali ya Kujitathmini 4.3 (yanathmini Malengo ya Somo la 4.4, 4.5 na 4.6)

Unapangia kumtembelea Naomi. Yeye ni mama aliyezaa kifungua mimba chake siku kumi zilizopita. Umemtembelea hapo awali, lakini ana haya sana hivyo inakuchukua muda mrefu kumfahamu yeye na familia yake. Unajitayarisha kuondoka kwenda kwake, na unashangaa jinsi utakavyowafanya wakuamini.

  • a.Unapoendelea kufunga virago vyako, unafikiria kuhusu kupeleleza iwapo una vyote unavyohitaji katika ziara ya baada ya kuzaa, kisha unaandika kumbusho la kutumia wakati ujao. Umeandika nini?
  • b.Baadaye, unaandika vidokezo zaidi kuhusu mambo muhimu ya kukumbuka utakapokutana na Naomi wakati mwingine umeandika nini?

Answer

Yafuatayo ni baadhi ambayo huenda umeyaandika:

Mfuko wa vifaa

Ninahitaji kudhibitisha kuwa vifaa vifuatavyo havijaisha – kapsuli za Vitamini A, vidonge vya iron, lihamu ya tetracycline nk., na sabuni!

Taulo safi? Saa ya mkono? Kadi za ushauri na uchunguzi za kutosha? Kitabu cha kurekodi, kalamu, na fomu za rufaa?

Vifaa vyote vya kawaida vinavyobakia mfukoni: mizani, stethoskopu, vifaa vya kupima shinikizo la damu, kipimajoto nk.

Kisha nitahitaji kujiangalia kama niko safi na mnadhifu!

Lakini nitachukua hatua gani ili kumpunguzia hofu Naomi? Haya ni baadi tu ya maswali machache ninayoweza kujiuliza:

‘Labda situmii istilahi mwafaka kikamilifu, kwa hivyo familia yake pengine inafikiria kuwa siheshimu desturi zao. Sijui kama ushauri wangu unasikika kama wenye ufidhuli au ukali- inanilazimu kukumbuka kuwa mpole na kumpa muda wa kutosha kwa mazungumzo ya kijumla ili kumtuliza. Utaratibu huu ni mgumu sana kwa sababu kuna mengi ya kufanya, hivyo inanibidi kujiharakisha kila mara. Najua yeye hunisikiza lakini pengine ninampa ushauri mwingi. Nitajaribu zaidi kumsifu na kumsikiza wakati huu na labda hatua hizi zitasaidia’.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 4