5.1.1 Chunguza ishara muhimu kwa mama

Ulijifunza jinsi ya kuchunguza ishara muhimu katika Kipindi cha 9 cha Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito.

Chunguza ishara muhimu kwa mama, yaani, joto lake, kiwango cha mpigo kwa mshipa, na shinikizo la damu, na kuhakikisha kwamba ziko katika kiwango cha kawaida. Mara tu baada ya kuzaliwa, chunguza mipigo yake kwa mshipa na shinikizo la damu angalau mara moja kila saa, na joto lake angalau mara moja katika saa sita za kwanza.

  • Je, ishara muhimu za kawaida zinapaswa kuwa aje ikiwa mama anaendelea kupata nafuu vizuri tangu wakati wa kuzalisha?

  • Joto lake linapaswa kuwa karibu na Sentigredi 37; kiwango chake cha mpigo wa mshipa inapaswa kuwa kati ya midundo 60 - 80 kwa dakika moja wakati ametulia; systoli yake ya shinikizo la damu (nambari ya juu, ambayo hupima shinikizo wakati moyo wake unakazika) inapaswa kuwa mmHg 90 - 135, wakati diastoli ya shinikizo la damu yake (nambari ya chini, ambayo hupima shinikizo wakati moyo wake imetulia) inapaswa kuwa 60-85 mmHg.

    Mwisho wa jibu

Mpatie mama rufaa ya haraka ambaye anaonyesha dalili ya mshtuko na/au kutokwa na damu baada ya mtoto kuzaliwa.

Ikiwa shinikizo la damu yake iko chini mno na inashuka, na mipigo ya mshipa yake inaenda haraka na inaongezeka, anaelekea kuwa na mshtuko. Huenda kinasababishwa na utokaji wa damu wa kuhatarisha maisha. Kama hakuna dalili ya kutokwa na damu kutoka ukeni, anaweza kuwa anapoteza damu ndani ya mwili.

5.1 Kiini cha utaratibu wa huduma kwa mama baada ya kuzaa

5.1.2 Chunguza kama uterasi yake ina mikazo ya kawaida