5.1.4 Chunguza uvujaji wa damu nyingi (hemoreji)

Baada ya kuzalisha, ni kawaida kwa mwanamke kutokwa na damu kiasi sawa na ya hedhi. Damu lazima pia ionekane kama ile ya hedhi - utusitusi, au waridi. Mara ya kwanza, damu hutoka katika mbubujiko mdogo au kumwagika wakati uterasi inakazika, au wakati mama atakapokohoa, kusonga, au kusimama. Baada ya siku mbili hadi tatu, mtiririko unapaswa kupungua na kuwa mchozo mwekundu ulio majimaji zaidi inayojulikana kama lokia (Kipindi cha 2).

Kutokwa na damu nyingi sana ni hatari. Ili kuchunguza utokaji wa damu nyingi katika saa sita za kwanza baada ya kuzalisha, chunguza pedii ya mama mara kwa mara – milimita 500 (karibu vikombe viwili) ya kupoteza damu ni nyingi mno. Ikiwa atalowesha pedii moja kwa saa, inachukuliwa kama kutokwa na damu nyingi. Ikiwa mama anatokwa na damu nyingi, na hauwezi kuizuia, mpeleke hospitalini. Chunguza kwa ishara za mshtuko. Kumbuka kwamba kutokwa na damu baada ya kuzaa ni kisababishi kikubwa cha vifo vya wajawazito na kinaweza kutokea wakati wowote katika kipindi cha huduma baada ya kuzaa - ingawa ni ya kawaida katika siku saba za kwanza.

5.1.3 Safisha tumbo ya mama, viungo vya uzazi na miguu

5.1.5 Chunguza viungo vya uzazi vya mama iwapo kuna miraruko na matatizo mengine