5.1.6 Msaidie mama kukojoa

Mchoro 5.6 Mama anaweza kuchuchumaa kwa bakuli ili akojoe ikiwa ni rahisi kwake.

Kibofu cha mkojo kiliojaa kinaweza kusababisha uvujaji wa damu na matatizo mengine. Kibofu cha mkojo kinaweza kuwa kimejaa baada ya kuzaa, lakini anaweza kuwa hana hamu ya kukojoa. Mwambie akojoe katika saa mbili au tatu za kwanza. Ikiwa amechoka sana kwa kuamka na kutembea, anaweza kuchuchumaa kwa bakuli kitandani au sakafuni (Mchoro 5.6). Anaweza pia kukojoa kwa taulo au kitambaa nene wakati amelala chini. Ikiwa hawezi kukojoa, unaweza kumsaidia kwa kumwagia maji safi, iliyo na joto kwa viungo vya uzazi wakati anapojaribu kukojoa.

Ikiwa mama hawezi kukojoa baada ya saa nne, na kibofu chake cha mkojo hakijajaa, anaweza kuwa na upungufu wa maji mwilini. Msaidie anywe viowevu. Ikiwa kibofu chake kimejaa na bado hawezi kukojoa, lazima aingizwe katheta ili kutoa mkojo ulio kwa kibofu cha mkojo wake. Ikiwa umepata mafunzo ya kufanya hivi, tumia katheta kama ilivyoonyeshwa katika Kipindi cha 22 cha Moduli ya Utunzaji katika Ujauzito na masomo yako ya ujuzi tendaji. Kisha mpatie rufaa kwa kituo cha afya au hospitali kilicho karibu.

  • Je, ni jambo gani muhimu unapaswa kufanya kabla ya kumpima mama ambaye amezaa wakati huo?

  • Nawa mikono yako vizuri kila wakati ili kupunguza uwezekano wa kupitisha bakteria zinazoweza kuwa kwa mikono. Ikiwa unapima sehemu yake ya viungo vya uzazi, kisha baada ya kunawa mikono, vaa glavu.

    Mwisho wa jibu

5.1.5 Chunguza viungo vya uzazi vya mama iwapo kuna miraruko na matatizo mengine

5.2 Lishe baada ya kuzaa