5.2.2 Ushauri juu ya lishe baada ya kuzaa

Baada ya kuzaa, ulaji wa mara kwa mara inapaswa kuongezwa ili kurudisha nguvu ya kunyonyesha pamoja na nguvu na afya yake. Anapaswa kula takriban 10% zaidi kuliko kabla awe mjamzito ikiwa hana shughuli nyingi au anafanya kazi yake ya kawaida na takriban 20% zaidi kama yuko na uwezo. Katika hali halisi, anashauriwa kuchukua angalau mlo mmoja au miwili zaidi kila siku. Ushauri wa lishe bora ni pamoja na:

Familia nyingi vijijini hawana uwezo wa kununua chakula cha ziada kwa kina mama ambao wamezaa kwa mara ya kwanza. Kipindi cha 14 katika Moduli ya Utunzaji katika ujauzito kinatoa ushauri kuhusu kula vizuri kwa kutumia pesa kidogo

  • Kushauri mama kula baadhi ya vyakula vilivyo na protini, nishati ya juu (kama vile familia inaweza kumudu), kama vile nyama, maziwa, samaki, mafuta, karanga, mbegu, nafaka, maharagwe na jibini, ili awe na afya pamoja na nguvu. Ushauri wako wa lishe bora itategemea na kile kilichoko nyumbani na kile wanakula kama chakula chao kikuu. Kile muhimu zaidi ni kuwaambia kwamba lazima ale zaidi kuliko kawaida.
  • Kuchunguza iwapo kuna miiko za kitamaduni ambazo ni muhimu kuhusu kula vyakula ambavyo ni lishe bora zaidi kiafya. Kwa mfano, katika baadhi ya tamaduni kula vyakula vilivyo na protini nyingi huchukuliwa vibaya, vyakula vilivyotiwa viungo, au vyakula baridi baada ya kuzaa. Mshauri kwa heshima dhidi ya miiko haya na hayapaswi kujizuia na chakula chochote chenye lishe bora.
  • Kuzungumza na wanafamilia, hasa mpenzi na/au mama mkwe, na kuwahimiza wasaidie kuhakikisha kwamba mwanamke anakula vyakula vya aina mbalimbali vya kutosha na kujiepusha na kazi ngumu ya kimwili.

Mshauri mama kuchukua virutubishi vidogo kuongeza lishe mara kwa mara ili kuzuia matatizo ya upungufu na anemia, kama tutakavyoeleza.

5.2 Lishe baada ya kuzaa

5.2.3 Kuzuia upungufu wa iodini