5.2.4 Kuzuia upungufu wa vitamini A

Mshauri mama jinsi ya kuzuia upungufu wa vitamini A, ambayo si tishio tu kwa kuona kwake, lakini pia ni kisababishi kikubwa cha upofu utotoni mwa watoto walionyonyeswa na mama aliye na upungufu wa vitamini A. Vitamini A katika mlo huongezea kinga dhidi ya maambukizi na ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa maziwa ya mama yaliyo na virutubishi.

  • Mshauri mama jinsi ya kuzuia upungufu wa vitamini A, ambayo si tishio tu kwa kuona kwake, lakini pia ni kisababishi kikubwa cha upofu utotoni mwa watoto walionyonyeswa na mama aliye na upungufu wa vitamini A. Vitamini A katika mlo huongezea kinga dhidi ya maambukizi na ni muhimu hasa kwa utengenezaji wa maziwa ya mama yaliyo na virutubishi.

  • Mboga zilizo na rangi ya manjano kama karoti, matunda ya njano kama maembe, na mboga yenye rangi ya kijani kibichi kama vile mchicha na kabichi huwa na vitamini A nyingi. Vile vile ini, mafuta ya samaki, maziwa, mayai, na siagi.

    Mwisho wa jibu

Kumbuka kwamba kipimo cha upeo wa vitamini A kwa wajawazito ni IU 500,000; zaidi ya hapo ni sumu

Mojawapo ya huduma ya kawaida baada ya kuzaa ni kuchunguza kama mama amepata kapsuli ya vitamini A. Kipimo kilichopendekezwa kwa kina mama wanaonyonyesha ni kapsuli moja ya vitamini A, IU 200,000 mara moja baada ya kuzaa au ndani ya wiki sita baada ya kuzaa. Mweleze kwamba vitamini A humsaidia kupata nafuu vizuri na mtoto anapata kupitia maziwa yake. Mweleze iwapo anahisi kichefuchefu au ana maumivu ya kichwa baada ya kutumia kapsuli hii, itaacha baada ya siku kadhaa.

5.2.3 Kuzuia upungufu wa iodini

5.2.5 Kuzuia upungufu wa ioni na folate