5.2.5 Kuzuia upungufu wa ioni na folate

Upungufu wa damu kutoka mwanzo inaweza kuchochewa na madhara ya kuvuja damu kwa mama na ni moja ya kisababishi kikubwa cha vifo vya wajawazito katika kipindi baada ya kuzaa. Shawishi kina mama kula vyakula vilivyo na madini ya ioni (kwa mfano, mboga zilizo na rangi ya kijani kibichi, maharagwe, mbaazi na dengu, kuku na nyama nyekundu, nyama ya ogani kama vile ini na figo, na bidhaa za nafaka nzima), na vyakula ambavyo huongeza ufyonzaji wa ioni (matunda na mboga zilizo na vitamini C). Mshauri kukunywa tembe moja iliyo na miligramu 60 ya ioni na mikrogramu 400 cha folate (folic acid) kila siku kwa muda wa miezi mitatu baada ya kuzaa, na umpatie kiasi kinachotosha kwa miezi mitatu. (Baadhi ya maeneo yanaweza kuwa na tembe zilizo na ioni na folate zikiwa mbalimbali, lakini kipimo ni sawa.) Mshauri kuhifadhi tembe salama pahali ambapo watoto hawawezi kupata kwa urahisi.

  • Huduma bora ya kawaida baada ya kuzaa kwa mama ni pamoja na kumshauri kuhusu mahitaji yake ya lishe. Je, utamshauri kuhusu nini?

  • Kwamba lazima aanze kunywa na kula katika masaa machache ya kwanza baada ya kuzaa; kunyonyesha inamaanisha anahitaji kula zaidi (hasa vyakula vyenye protini nyingi); kama yuko katika eneo ambapo tezi yanapatikana, mshawishi yeye kutumia chumvi iliyo na iodini; ukimwelezea umuhimu wa mboga na vyakula vingine ambavyo viko na vitamini A, ioni, au folate.

    Mwisho wa jibu

5.2.4 Kuzuia upungufu wa vitamini A

5.3 Usaidizi wa kihisia kwa mama