5.3.2 Wakati mama hana haja na mtoto wake

Baadhi ya kina mama hawahisi vizuri kuhusu watoto wachanga (Mchoro 5.10). Kunaweza kuwa na sababu nyingi kwa hii. Mama anaweza kuwa amechoka sana, au ni mgonjwa au anatokwa na damu. Anaweza kuwa hakutaka mtoto, au kuwa na wasiwasi kwamba hawezi kumtunza. Kama ulivyojifunza katika Kipindi cha 3 cha Somo, anaweza kuwa anafadhaika sana: ishara kama hizi ni kama mama anaonekana kuwa na huzuni, utulivu, na hana hamu ya kitu chochote. Pia chunguza ishara zingine za tabia isiyo kuwa ya kawaida ambayo ni tofauti na ile yake ya kawaida.

Mchoro 5.10 Mama ambaye anakataa mtoto wake anaweza kuwa na masumbuko baada ya kuzaa.

La kufanya iwapo unajishughulisha na mama kukosa haja na mtoto wake:

  • Mchunguze kwa makini kwa ishara za uvujaji wa damu au maambukizi, au ugonjwa wa shinikisho la damu. Anaweza kuwa mgonjwa, badala ya kufadhaika au wasiwasi.
  • Unaweza kuzungumza na mama kuhusu hisia zake, au huhisi kuwa ni bora kuangalia na kusubiri.
  • Ikiwa unajua kwamba alikuwa amefadhaika sana baada ya kuzaa hapo awali, washauri wanafamilia kumtunza na kumsaidia zaidi kwa wiki chache zijazo. Kawaida mfadhaiko huu huisha, lakini wakati mwingine inachukua muda wa wiki chache au hata miezi, na inaweza kuhitaji rufaa kwa utathmini na matibabu zaidi. Kama anaonyesha dalili zozote za kichaa baada ya kuzaa (Kisanduku 5.1), mpee rufaa haraka.
  • Hakikisha kwamba mtu katika familia anamtunza mchanga iwapo mama hawezi au hataweza.

Kichaa baada ya kuzaa kinaweza kutisha maisha, hivyo ichukue kama hali ya dharura. Utajifunza zaidi kuhusu kichaa katika Moduli juu ya Magonjwa yasiyo kuwa ya Kuambukiza, Huduma za Dharura, na Afya ya Akili.

Kisanduku 5.1 Dalili za kichaa baada ya kuzaa

Hali hii ni nadra (inayoathiri takribani mmoja kati ya wanawake 1,000), lakini ni kali sana na mama lazima apewe rufaa kwa haraka kwa matibabu maalamu kama anaonyesha dalili yoyote kati ya zifuatazo:

  • Kusikia sauti au mlio wakati hakuna mtu pale
  • Kuona mambo ambayo si ya kweli
  • Kuhisi kama mawazo yake si yake mwenyewe
  • Kuhisi uoga kuwa anaweza kujidhuru au mtoto wake
  • Kupoteza uzito kwa ghafula na kukataa kula
  • Kukosa usingizi kwa masaa 48 au zaidi.

5.3.1 Kina baba na wanafamilia wengine wanaweza kumsaidia

5.4 Kuhimiza mazoea utafutaji wa huduma