5.4 Kuhimiza mazoea utafutaji wa huduma

Mhimize mama, mwenzake, na wanafamilia wengine kupata huduma mara moja wakiona dalili yoyote hatari, ikiwa ni kwa hali yake ya kimwili au hisia. Ucheleweshaji ndio sababu kuu ya vifo vya kina mama na wachanga muda tu baada ya kuzaa na ni pamoja na:

  • Kuchelewa kutambua mapema na kufanya uamuzi wa kupata usaidizi, kutokana na imani potofu na miiko ya kitamaduni. Familia pia zinaweza kuwa na ogopa gharama kufuatia huduma za afya.
  • Kuchelewa kupata huduma ya usafiri hadi kituo cha afya, au kupata mhudumu wa afya wa kwenda naye nyumbani kwa mama.
  • Kuchelewa kupata huduma mwafaka anapofika katika kituo cha afya, kutokana na ukosefu wa wahudumu au vifaa.

Kuwapa motisha mama na familia juu ya kutafuta huduma mapema ndio msingi katika utoaji wa huduma mwafaka baada ya kuzaa. Unapaswa kujaribu kuweka uwezo kwa jamii wa kukabiliana na hali yoyote ya dharura ambayo inaweza kutokea wakati wa kipindi baada ya kuzaa. Hasa, lazima tahadhari itolewe katika kila kijiji kwa kubuni mfumo wa rufaa wa dharura kwa kina mama na wachanga walio kwa hali inayohatarisha maisha.

5.3.2 Wakati mama hana haja na mtoto wake

Muhtasari wa Kipindi cha 5