Maswali ya Kujitathmini ya Kipindi cha 5

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki cha somo, unaweza kutathmini mafanikio ya matokeo ya kujifunza kwa kujibu maswali yafuatayo. Andika majibu yako katika Shajara yako ya somo na uyajadili na na mkufunzi wako katika mkutano ujao wa Usaidizi kwa Somo. Unaweza kulinganisha majibu yako na Maelezo juu ya Maswali ya Kujitathmini yaliyo mwishoni wa Moduli hii.

Swali la Kujitathmini 5.1 (linatathmini Malengo ya Somo la 5.1 na 5.2)

Uliwasili kama umechelewa kuzalisha mtoto ambaye alizaliwa masaa mawili kabla ya wewe kufika huko. Utafanya nini?

Answer

  • Chunguza kama joto ya mama, kiwango cha mpigo kwa mshipa, na shinikizo la damu (ishara zake muhimu) ni za kawaida.
  • Papasa fumbatio lake ili kuchunguza kama uterasi ina mikazo. Fanya hili tena baada ya dakika 30 na kisha kila saa kwa masaa matatu yafuatayo.
  • Fuatilia kwa makini kiasi cha damu anayovuja - kama anajaza zaidi ya pedi moja kwa saa na huwezi kuisimamisha, mpeleke kwenye kituo cha afya kilichoko karibu. Hakikisha kwamba umechunguza ishara zozote za mshtuko na uanze utaratibu wa kiowevu kwa mshipa kabla ya rufaa kama shinikizo la damu yake ni ya chini na inaendelea kwenda chini na mpigo kwa mshipa ni ya kiwango cha haraka na yanaongezaka.
  • Kwa upole msaidie kujinyosha mwenyewe - tumbo, miguu, na viungo vya uzazi (kwa kutumia sabuni na maji safi sana). Chunguza viungo vya uzazi kama kuna upashukaji wowote, majeraha, au kuvunja damu ndani ya ngozi (hematoma), au kutoka kwa seviksi (sevikisi imeshuka hadi ukeni)
  • Msaidie kukojoa.
  • Hakikisha kwamba ameanza kunywa ilikurudisha maji mwilini, na kama inawezekana mshawishi ale chakula.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 5.2 (linatathmini Malengo ya Somo la 5.1, 5.3 na 5.4)

Lishe bora na usaidizi kwa mama baada ya kuzaa ni masuala muhimu ya huduma bora baada ya kuzaa. Kamilisha Jedwali 5.1 ilikuonyesha, kila tatizo katika safu ya kwanza:

  • Unayotumaini mama au familia yake watafanya.
  • Utakalofanya ili kuhakikisha kwamba mama ana kila anachohitaji.
Jedwali 5.1 Huduma na usaidizi kwa kina mama wapya.
Tatizo au uwezekano walo iwapo halitashugulikiwaHatua mama au familia yake inaweza kuchukua ili kumsaidiaMatibabu au hatua zingine unaweza kuchukua
Tezi (inayosababishwa na upungufu wa madini ya iodini)
Kutokula au kunywa katika masaa machache ya kwanza
Ukosefu wa nguvu(kudumisha nguvu wakati wa kunyonyesha)
Upungufu wa vitamini A
Anaemia
Utengwaji wa mama na mtoto
Kutokuwa na hamu na mtoto
Usaidizi kwa mama

Answer

Jedwali 5.1 Utunzaji na usaidizi kwa kina mama wapya (iliyokamilishwa).
Tatizo au uwezekano wa tatizoHatua mama au familia yake wanaweza kuchukua ili kumsaidiaMatibabu au hatua zingine unazoweza kuchukua
Tezi (inayosababishwa na upungufu wa madini ya iodini)Matumizi ya chumvi iliyowekwa iodini kwa kupikiaDozi ya mafuta iliyo wekwa iodini baada ya kuzaa, kama tezi inapatikana kwa urahisi.
Kutokula au kunywa katika masaa machache ya kwanzaMama anapaswa kujaribu na kukumbuka kwamba ni lazima anywe na ale kwa ajili ya afya yake na ya mtoto.Chunguza kama kuan utokaji wa damu, homa, au ishara zingine za ugonjwa ambazo zinaweza kuwa ndio kiini cha tatizo; mshawishi mama kuzungumza kuhusu vile anajihisi.
Ukosefu wa nguvu(kudumisha nguvu wakati wa kunyonyesha)Kula mara moja au mbili zaidi kwa siku vyakula vyenye protini vingi (nyama, maziwa, mafuta, karanga, na kadhalika) kama inawezekana.Chunguza kama kuna miiko kuhusu vyakula, zungumza na familia juu ya kuhakikisha mama anakula chakula cha kutosha na kuepukana na kazi ngumu.
Upungufu wa vitamini AOngezea ulaji wa vitamini A nyingi, mboga na matunda, kwa mfano, karoti, maembe, kabichi, mchicha; pia ule ini, mafuta ya ini ya samaki, maziwa, mayai, na siagi.Mpatie kapsuli moja ya vitamini A iliyo na IU 200,000 baada ya kuzaa au ndani ya wiki sita za kuzaa; elezea umuhimu wa vyakula vyenye vitamini A.
AnaemiaOngezea ulaji wa mboga na matunda yenye ioni na folate. Mpatie tembe za kutosha (miligramu 60 ioni na mikrogramu 400 folate) ameze moja kila siku kwa miezi mitatu
Utengwaji wa mama na mtoto.Wanafamilia kukaa na mama na mchanga kutoa ili kuwapa usaidizi, licha ya kanuni za kiutamaduni. Eleza ni kwa nini mama anahitaji mtu kukaa karibu naye, hasa katika siku saba ya kwanza, wakati kuna hatari kubwa; huduma ya haraka inahitajika iwapo chochote kibaya kitatokezea.
Kutokuwa na hamu na mtotoFamilia imtunze na imsaidie zaidi na kuwe na mtu wa kuhudumia mchanga kama kuna haja.Chunguza kuwepo kwa ugonjwa, kuvuja damu au maambukizi. Zungumza naye. Chunguza kama anasikia sauti, au ‘kuona vitu’. Kama ni hivyo mwelekeze kwa daktari wa akili kwa usaidizi.
Usaidizi kwa mama Mwenzake, nyanya na/au mama mkwe wachukue baadhi ya kazi za nyumbani za kawaida.Hakikisha kwamba mwenzake na familia wanajua dalili hatari na umuhimu wa kutochelewa kumpeleka mama kwenye kituo cha afya.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 5