7.1 Kumpa ushauri mama kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga

Kila mara ni bora kupatiana ushauri kuhusu ulishaji wa mtoto mchanga kabla ya kuzaliwa na pia kuendelea kusisitiza baada ya kipindi cha kuzaliwa. Mafunzo haya lazima yaangazie kuhusu uanzishaji na udumishaji wa unyonyeshaji bora. Utaratibu wa kupata haya yameandikwa kwa muhtasari katika Kisanduku 7.1

Kisanduku 7.1 Utaratibu wa unyonyeshaji bora

  • Anza kunyonyesha baada ya saa moja ya kuzaa (unyonyeshaji wa mapema)
  • Usimptie mtoto chochote isipokuwa maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza (unyonyeshaji wa kipekee)
  • Usimwage maziwa ya kwanza ya mama baada ya kuzaa, huwa na protini na kingamwili ambayo ni muhimu kwa mtoto mchanga. Unapaswa kumwambia mama amlishe nayo mtoto mchanga, kwa sababu ni ‘chanjo’ ya kwanza ambayo mtoto atapata.
  • Keti kwa hali nzuri wakati unanyonyesha
  • Hakikisha mtoto anapata vizuri matiti ya mama anaponyonya
  • Hakikisha mtoto ananyonya vizuri

Unapomtembelea baada ya kipindi cha kuzaa, mwambie mama amweke mtoto kwa matiti ili ukague namna anavyompatia matiti na anavyonyonya (tunaelezea jinsi ya kufanya hivyo katika sehemu inayofuata). Ikiwa mtoto alikuwa amelishwa hivi karibuni, ngojea angalau saa moja kabla ya kumpatia maziwa ya matiti tena. Hii itakupatia fursa ya kuchunguza jinsi mtoto anavyonyonya na kuweza kubaini iwapo kuna matatizo yoyote ya kunyonya, ambayo unaweza kumsaidia mama kutatua. Kabla ya kuondoka hakikisha kwamba mama anaelewa jinsi ya kunyonyesha mtoto wake kwa njia inayofaa.

Malengo ya Somo la Kipindi cha 7

7.1.1 Ishara nne nzuri za mama kukaa