7.4.3 Ni jinsi gani watoto wachanga hupoteza joto?

Utaratibu wa jinsi mtoto mchanga unapoteza joto imewekwa kwa muhtasari katika Kielelezo 7.4, na imeelezwa hapo chini.

Mchoro 7.4 Utaratibu wa upotezaji wa joto kutoka kwa ngozi ya mtoto mchanga. (Chanzo: Shirika la Afya Ulimwenguni, 1997, Safe Motherhood: Thermal Protection of the Newborn, Practical Guide, inapatikana kutoka http://whqlibdoc.who.int/ hq/ 1997/ WHO_RHT_MSM_97.2.pdf [Tip: hold Ctrl and click a link to open it in a new tab. (Hide tip)] )

Myuko. Hii ni upotezaji wa joto kutoka ngozi ya mtoto mchanga kwa mazingira. Watoto wachanga hupoteza joto jingi kwa njia ya myuko wakati wameachwa kwa hewa baridi au upepo.

Upitishaji. Hii ni upotezaji wa joto wakati mtoto mchanga hulala juu ya pahali baridi. Watoto wachanga hupoteza joto kwa njia ya upitishaji wakiwekwa uchi juu ya meza baridi, kipima uzito au wamefunikwa na blanketi baridi au taulo.

Uvukizi. Hii ni upotezaji wa joto kutoka kwa ngozi ya mtoto mchanga ilio na maji kwa mazingira. Watoto wachanga hupoteza joto kwa njia ya uvukizi baada ya kuzaliwa au kuoga. Hata mtoto mchanga anaweza kupoteza joto kwa njia ya uvukizi akiwa na nepi iliyolowa.

Mnururisho. Hii ni upotezaji wa joto kutoka ngozi ya mtoto mchanga kwa vitu vilio mbali baridi, kama vile dirisha baridi au ukuta n.k.

Hatimaye, unapofahamu kwamba mtoto anaweza kupoteza joto kwa jinsi hizi nne zilizoelezwa hapo juu, lazima umshauri mama aepukane na hali ya kumwacha mtoto kwa upepo. Mshauri kwamba kabla ya kumvua mtoto nguo anapomwogesha, anapaswa kufunga milango na madirisha yote, amfunike mtoto aliyelowa na kumkausha haraka.

Wacha kusoma kwa muda na ufikirie uzoefu wako mwenyewe katika jamii yako. Umeona hali zenye kina mama walikuwanazo katika hatari ya kumwachilia mtoto wao kupoteza joto kwa njia yoyote imeelezwa hapo juu?

7.4.2 Je, ni wakati gani watoto wachanga wako katika hatari kubwa ya kupata hipothemia?

7.4.4 Kanuni ya mfululizo joto katika huduma baada ya kuzaa