Maswali ya kujitathmini ya Kipindi cha 7

Sasa kwa kuwa umekamilisha Kipindi hiki, jibu maswali haya kutathmini uliojifunza. 7.1 (Malengo ya Somo la 7.2 na 7.4)

Unashangaa utamwambia nini mama aliye na VVU ambaye anataka kunyonyesha. Je utamshauri vipi?

Answer

Kuna njia nyingi ambazo unaweza kuwa umetengeneza nakala kuhusu hali hii ngumu. Utamhurumia mama kwa nia ya kutaka kunyonyesha na pengine faida za mtoto (kwa mfano, ukingaji dhidi ya maambukizi, virutubishi mwafaka, upunguzaji wa hatari ya aleji), na faida kwa mama (kunyonyesha ni nafuu, husaidia uterasi kurudi hali yake ya kawaida, ni muhimu kwa upangaji uzazi, na kadhalika). Lakini pia mwambie hatari ya kuambukiza VVU kwa mtoto kupitia unyonyeshaji.

Wakati utajadili kuhusu maziwa ya kutengenezwa kama njia mbadala, elezea umuhimu mkubwa wa maji safi na ufisha viini kwenye chupa na chuchu, vile vile haja ya kupima kila kitu kwa ufasaha ili mtoto apate lishe sahihi.

Kisha kupitia kigezo cha IKGES (Inayokukubalika, Kuwezekana, Gharama nafuu, Endelevu na Salama) na maswali katika mchoro 7.4. Kama atajibu 'ndiyo' kwa yote, mhimize atumie maziwa ya kutengenezwa au ya wanyama, na pia mshauri kuhusu upangaji wa uzazi. Kama atajibu 'la' na anataka kabisa kunyonyesha, mweleze jinsi anaweza kupunguza hatari ya maambukizi ya VVU kwa kunyonyesha kwa vipindi vifupi (sio zaidi ya saa tatu), na awache kunyonyesha kutoka titi lina chuchu lenye mpasuko. Mkumbushe kuangalia kinywa cha mtoto kama kuna vidonda, na kutafuta matibabu ya haraka kwa ajili yake na mtoto wake iwapo mmoja wao atakuwa mgonjwa.

Mwisho wa jibu

Swali la Kujitathmini 7.2 (Malengo ya Somo la 7.2)

Kati ya fasili zifuatazo ni gani isio sahihi? Katika kila hali, toa fasili sahihi.

  • A.Unyonyeshaji wa kipekee ni kunyonyesha mtoto mmoja kwa wakati.
  • B.Kukaa vizuri unaponyonyesha ni wakati mama amekaa kwa ustarehe.
  • C.Ushikiliaji mzuri ina maanisha kuwa mtoto 'amejaza titi kinywani vizuri'.
  • D.Unyonyeshaji wa mapema inahitaji mama kuamka karibu alfajiri kwa ajili ya lishe ya kwanza.
  • E.Kanuni ya mfululizo joto inamaanisha kwamba unachopatia kipaumbele ni kumpatia mtoto joto wakati wote, ili aepukane na hipothemia.

Answer

  • A.Si kweli: Unyonyeshaji wa kipekee ni kutompea mtoto kitu kingine chochote bali maziwa ya mama kwa miezi sita ya kwanza.
  • B.Kweli. Lakini angalia nyuma katika sehemu ya 7.1.1 na uangalie kuwa unafahamu jinsi ya kudumisha mama katika hali nzuri.
  • C.Kweli: Angalia nyuma katika sehemu ya 7.1.2 na uangalie kama unakumbuka ishara nne za ushikiliaji nzuri.
  • D.Si kweli: Unyonyeshaji wa mapema ni uanzaji wa unyonyeshaji katika saa moja baada ya kuzaliwa.
  • E.Kweli: Kanuni ya mfululizo joto inamaanisha kuchukua hatua za kumpatia mtoto joto wakati wote.

Mwisho wa jibu

Maswali ya kujitathmini 7.3 (Malengo ya Somo la 7.5)

Unapomtembelea mama aliyezaa kwa mara ya kwanza na ugunduwe kuwa mtoto anahisi baridi sana. Una wasiwasi kuhusu hipothemia. Utafanya nini?

Answer

  • Weka mtoto mchanga ngozi-kwa-ngozi na mama, wafunike wote wawili na mablanketi yaliyo na joto, weka kofia au kitambaa juu ya kichwa cha mtoto na mvalishe soksi au umfunike miguu.
  • Pima kiwango cha halijoto ya mtoto na kama iko chini ya sentigredi 37.5 pima tena baada ya nusu saa. Kama halijoto haitapanda kwa haraka, mpee mtoto rufaa haraka.
  • Wakati unasubiri kuona ikiwa mtoto anapata joto, Fanya uchunguzi wa kawaida ni kwa nini mtoto yuko baridi. Uliza mama kama mtoto alikuwa ameloa au hajalishwa hivi karibuni, au ikiwa anamlisha akiwa uchi. Angalia kama chumba kina madirisha wazi au ikiwa mtoto yuko kwa upepo.
  • Mwelezee mama jinsi watoto wachanga wanavyopoteza joto (njia muhimu imewekwa kwa muhtasari katika sehemu ya 7.4.3) na humweleza umuhimu wa kumpatia mtoto joto kila wakati.
  • Mwambie vipengele vya mfululizo joto. Ikiwa hutaka kumbuka angalia tena katika Jedwali 7.2.

Mwisho wa jibu

Muhtasari wa Kipindi cha 7