9.1 Huduma mwafaka ya rufaa

Uwezekano wa kumfikisha mama mgonjwa au mtoto mchanga katika kituo bora cha afya kwa wakati unaofaa unaweza kubaini iwapo watakufa au wataishi. Rufaa itasaidia ikiwa:

  • Umeimarisha uhusiano mzuri na vituo vya afya unavyovitumia (na wahudumu wa afya vituoni), hivyo rufaa inaweza kutekelezwa haraka na kwa njia mwafaka.
  • Umehamasisha jamii kutafuta usaidizi wa kisaikolojia, kifedha na wa kiutendaji katika visa ambapo kina mama na watoto wachanga walio mahututi ni sharti wafikishwe kituoni kwa dharura.
  • Umemshawishi mama na familia yake kuamini pendekezo lako kabla ya jambo la dharura kutokea, ili wawe tayari kufuata maagizo yako ikiwa jambo la dharura litatokea.
  • Unatia juhudi katika kufuatilia na kuhakikisha kuwa mama na mtoto wamefika katika kituo cha afya. Njia ya kidesturi ya kumwambia mama au watoa huduma waende kituoni au kuwaandikia barua ya rufaa tu bila usaidizi zaidi kamwe si suluhisho tosha.

Malengo Somo la Kipindi cha 9

9.2 Kiungo cha rufaa: maafikiano ya pande mbili