9.2.2 Kufahamu kuhusu vituo vya afya katika eneo lako

Ili kufanikiwa katika kutoa rufaa unahitaji orodha ya hospitali na vituo vyote vya afya katika eneo lako na huduma wanazozitoa. Hii ni ili, kwa mfano, ukizaa mtoto mwenye uzani wa chini sana mara moja utajua kituo cha afya chenye uwezo mwafaka, vifaa na wafanyakazi waliohitimu kutoa huduma ya dharura kwa watoto walio wadogo sana. Ukiwa na habari hii, unaweza kumpa mama na mtoto rufaa kwa haraka.

  • Je, ni nini kinachoweza kutokea ikiwa huna habari kuhusu huduma zinazotolewa katika vituo vya afya vya kiwango cha juu?

  • Hatari kubwa iliyoko ni kumtuma mama au mtoto kwenye safari ngumu na ghali kuenda katika kituo cha afya kisichokuwa na huduma inayofaa. Hii inaweza kuwa hatari kwa sababu inamaanisha utapoteza wakati mwingi barabarani.

    Mwisho wa jibu.

Kwa muhtasari, ili kuwa na nafasi ya kupata matokeo bora, wafanyakazi wote wa afya katika jamii wanahitaji kujua jinsi ya kuwapa wagonjwa wao rufaa na hususani kituo kipi cha rufaa ili waweze kupata huduma inayofaa kukidhi mahitaji yao.

9.2.1 Kupokea majibu

9.3 Je, ni nini kinachozuia rufaa kutolewa kikamilifu?